Tukiwa katika maongezi yetu, tukiwaa tumemgeukia muongeaji mkuu ambaye alikuwa wakili
mwanadada,mara mlango ukagongwa, na wote tukageuka kuangalia ni nani
aliyegonga, maana mimi mwenyewe nilimsikia mkuu akitoa amri kuwa asisumbuliwe na
mtu yoyote, kwasababu yupo kwenye maongezi muhimu. Akageukia kule mlangoni na
kusema kwahasira;
‘Nani wewe, ….?’ Akauliza mkuu kwa sauti.
‘Mkuu kuna dharura,….’sauti ya askari ikasema, na hapo mkuu,
akajua kuna jambo, akainuka haraka nakufungua mlango, na tukasikia sauti ya
mkuu ikiguna, kukawa na mazungumzo huko nje,ambayo hatukuweza kuyasikia na mara
mlango ukafunguliwa, akaingia mkuu, na
kusema;
‘Haya yule mtu wetu muhimu tuliyekuwa tukimtafuta kajileta
mwenyewe,…ingawaje hali aliyo nayo, intisha tuvumilie hivyo hivyo…’ akageuka
mlangoni nakuangalia ,na sisi macho yetu yakawa yanaangalia kwa hamu kumuona
huyo aliyetambulikana kama `mtu muhimu’
Harufu ya pombe kali ilianza kusikika, na ….mara akaingia
jamaa akiwa kachafuka kweli, anatoa harufu ya pombe, kama vile alimwagiwa mwili
mzima, akasogea, huku anayumba yumba, na kukaa kwenye kiti kilichokuwa wazi, na
hata kukaa kwake alikaa upande upande ,ilionyesha kabisa kuwa hana nguvu, ..ama
kutokana na ulevi aliokuwa nao,au hajala,au anaumwa…au vyote.
‘Mkuu kwanza naomba maji baridiiii….’akasema huyo jamaa huku
akiwa kama kafumba macho, macho yalionekana mazito kuyafumbua,…akawa kama
anayalazimisha.
‘Maji yatapita kwei hapo, maana inaoena kama hujala
,…kwanini unajitesa hivyo, ..kwanza angalai ulivyo, huoni hali kamahiyo
nikutazalilisha sisi…na kitengo kizima cha sheria…’akalalamika mkuu.
‘Kula sitaki, chakula changu sasa ni pombe….nitakunywa hadi
kieleweke, maana sioni umuhimu wa kuishi tena, kuwaabisha, sijaabisha mtu,
tatizo lenu hamjui nini kinachoendelea....kuna watu hawanitakii mema,lakini
kaba sijafa nimeamua kuwamalizawote waionifanya hivi….’akajiangalia huku
akiyumba kwenye kiti
‘Hivi…hivi wewe mkuu
unanionaje, unafikiri napenda hii hali, ukiona hivi ujue, maji yamezidi
unga,…mwanaume, tena mkwe kaingia choo cha kike na kumkukuta mama mkwe wake…..’akasema
huku akijaribu kukaa vyema kwenye kiti.
‘Mwanaume mzima naonekana hivi,zalili….nazalilika mwenzenu,
eti… kwasababu ya...eti kwasababu ya kijike,…mwanamke…hapana, tutafikishana
mbali…mmmh, sasa mkuu maji utanipa au hunipi mkuu au ndio nimeshaanza
kifungo,….bado, hafungwi mtu hapa….kesi itasimama, na waliofanya haya yote, ama
wawe hai au mfu, watasimama kizimbani, mimi ni mwanaume bwana,wazazi wangu
wanajua kuwa walizaa dume….’akasema huku akipiga kifuani.
‘Mmmmh, ngoja nimalizie hii,…haya maji ya uhai….hii ndio
chai kule kwetu, lakini ndio hivyo, kule inaitwa gongo, lakini wenzetu,
wameifnaya hivi, …na kuuita wiski…hii ni chpa ya mwisho, basii….’mara akatoa
chupa ya pombe, aliyokuwa kaweka mfukoni na kunywa.
Kila mmoja alikuwa kaduwaa, na hakuna hata mmoja ambaye moyo
wake hakuingiwa na simanzi, huwezi amini. Mtu ambaye siku kazaa nyuma, alikuwa
na afya yake, mtanashati, na mwenye hadhi, leo hii anaonekana kama mtu
aliyetindikiwa na ubongo,…kweli hujafa hujaumbika.
Mkuu aliinuka na kuchukua gilasi ya maji na kumpa huyoo
jamaa, akaipokea huku mikono ikitetemeka, akaiangalia kwanza na halafu akainua
kichwa, akatuangalia mmoja baadaya mwingine, akatikisa kichwa, hakusema kitu,
akainua ile gilasi akawa kama anaongea kitu, au kuomba, akainua kichwa tena na
kutuangalia kwa muda,…machozi yakaanza kumtoka.
‘Mungu wangu nisamehe…..najua jinsi gani
nilivyokukosea,….sijui nini kiliiningia hadi yakanifikahaya yote, sijui….naomba
kwa nguvuu ya haya maji, unipe ujasiri niweze kuitenda haki, niweze kuwafikisha
wote walionifanyia hivi mbele ya mahakama,….ndugu muheshimiwa, nataka
kukutambulisha jambo…kuwa mhusika mkuu wa haya yote, nimeshammaliza, ….’akainua
maji na kuanza kunywa.
‘Tulimwangalia kwa makini, akiyanywa yale maji, na mara
mlango ukagongwa tena, na mkuu hakusemaneno akainuka na kuufungua mlango,
akaingia dada mmoja,……wote tukageuka kumwangalia na Yule dada akatuangalia kwa
mashaka huku akiwa kashika kichwa kwa aibu, alipomuona yule jamaa alivyo. Ilionekana wanajuana, lakini hakupenda ile hali aliyomuona huyo jamaa, lakini akajifanya hajali, akamsogelea yule jamaa na kukaa karibu yake. Yule jamaa aliinua
uso na kumwangalia, akasema;
‘Umefika mpenzi,…ahsante sana kwa kutimiza ahadi yako, na mimi
nimetimiza ahadi yangu kama tulivyopanga, nakuomba unyoshe mikono juu, maana
hapa upo chini ya usalama, upo chini ya nini, ya usalama, kwa utambulisho
tu,mmh, ngoja nikutambulishe wahusika humu ndani….’akajaribu kuinuka, lakini
hakuweza, akarudi kukaa,na kaunza
kucheka…alicheka hadi akadondoka kwenye kile kiti.
Yule mwanadada akamfuta pale chini na kumsaidia kumuinua,…na
Yule mwanadada akasema kwa uchungu;
‘Yeye tangu afike kwangu ndio hivii hivi, kunywa pombe tu,
hataki kula, hajijali, namimi sina muda wa kumuogesha kama mtoto mdogo,hataki
hata kubadili nguo, nimembeleza sana, ajitoe kwa polisi hataki,….lakini ikafika
muda nikasema basi liwalo naliwe,ikabidi nivunje ahadi yangu, kuwa nitamlinda hadii
mwisho nikamwambia kama hataki kujitoa, mimi nitakwenda kuwaita polis waje
wenyewe….’akasema Yule mwanadada.
‘Tulia, usianze kuongea wewe,..mimi ndiye wakili wako
nitaongea, mwenyewe…usijitie matatani kwa jambo ambalo nimelisababisha mimi
mwenyewe, kwasababu ya huyo jamaa anayejiona ana akii sana....sasa wewe tulia…’akawa
anaongea huyo jamaa kilevi levi.
‘Lakini kwa hali kama hiyo naona sio wakati muafaka ,ngoja
tuangalie afuya yako kwanza….’akasema mkuu.
‘Wewe unajau nini kuhusu afya yangu, usicheze na muda, hapa
naweza kukata kamba, nikafa, mtajua wapi ukweli wa haya yote, simtabakia kuwafunga
watu wasiohusika, mimi najua kila kitu, mimi nilijua yote yaliyokuwa yanakuja
juu yangu, na aliyesabibisha haya yote….lakini kila jambo lina mwisho
wake,…niliyempenda naye hanipendi..sasa ningelifanyaje, na Yule, …..aliyeninisaliti
awali, akapata jaza yake,hatunaye tena….nitamfuata huko huko…..’akataka kuanguka
kwenye kiti.
‘Mimi nashauri kwanza tumfikishe huyu mtu hospitalini
akapate, matababu, hali aliyo nayo sio nzuri, alipoteza fahamu masaa mengi,
nikahangaika naye sana, na alipozindukana akaja na wazo hilo la kuja hapa,
akidai kuwa anataka kuwafahamisha ukweli,kwani anaona kifoo kinamjia….’akasema
Yule mwanadada.
‘Tatizo lako unajitia kimbelembele…wewe hujui sheri,utajiweka
kitanzi mwenyewe….shauri lako ngoja mimi niongee mwenyewe, sitakufa mpaka
nimalize kazi yangu, kwanza mkuu waambie
vijana wako wakamchukue huyo jamaa ndani ya gari, asije akafa kabla hamjajua
nini …unasikia mkuu, haraka, sio swala lakufikiria…’akasema namkuu kweli
akaamrisha vijana wake wakaangalie kwenye gari kuna nini.
‘Mkuu, kuna jamaa, sijui kamayupo hai, kafungwa pingu, na
kamba kwenye gari, anavuja damu….’akasema huyo askari.
‘Waite watu wa huduma , wamshughulike, kwani ni nani
huyo….?’akauliza mkuu huku akimwangalia Yule jamaa.
‘Mhusika mkuu wa hii kesi,..huyo ndiye chanzo cha haya
yote….aje mbele yenu akiri mwenyewe…maana keshakubali, hana ujanja tena,…hana
mbele wala nyuma, wenzake wamemkimbia, hana pesa, hana nini…..’akasema.
‘Mbona wanasema hali yake ni mbaya..’akasema mkuu.
‘Hali yake ni mbaya ndio, ni njaa….lakini hata hivyo haijawa
mbaya bado, nione mimi hapa, nina hali nzuri…mimi ni kama yeye tu, na alijifanya
kichwa maji ndio maana akawa vile, angekuwa mtiifu, yasingelimfika hayo
yaliyomfika,sikuwa na jinsi, nikamfinya kidogo,akaropoka yote…hii hapa kanda
niliyomrekodi kama mnataka kuiskiliza, na kama hataki kuongea ,au..kama kafa,
lakini ushahidi huu hapa….’akatoa CD’S
nakumkabidhi mkuu.
‘Ila nataka mke wangu, na rafiki yake mpendwa wafike
hapa,…nataka hili swala liishe leo hii hii,
na ukweli uwe wazi, na….hata nikifa nijue naenda kutulia,sio kwenda
kuteseka,….unaweza kufanya hilo mkuu, au nikalifanye mwenyewe….?’akaninuka huku
akipepesuka.
‘Hebu tulio hapo kwanza, tulia hapo kwenye kiti, hali uliyo
nayo sio nzuri…’akasema Yule mwanadada.
‘Unajua hali nzuri wewe,tatizo lako unanipenda sana,lakini
mimi kuna mtu nampenda zaidi, kwanza mke wangu, lakini….mapenzi
yaipungua,..macho yakaona mwingine…mmh….lakini nitafanyaje, nafsi imeumbwa kupenda
vizuri, baadaye…., nimependa …mwingine, mmh,kweli huyo, hata kama ni kuoa mke
mwingine nitamuoa yeye, na wewe pia, nataka wake hawa…’akaonyesha kwa vidole
vitatu huku akimshika yue mwanadada.
‘Sawa, lakini hayo yote yanahitaji afya yako kwanza…’akasema
huyo mwanadada.
‘Umekubali sio, …basi kwanza aje mke wangu wa
kwanza,…akikubali, na akikubali huyo rafiki yake, tukafunga ndoa, aaah, mimi
tena, nitatulia nyumbani kimiya, nataka nini tena,…lakini huyo rafiki yake,
hanitaki,….anasema ana mtu wake,…mtu wake gani huyo, nikimuuliza ni nani hamtaji….’akainama
kama vila kichwa kimekuwa kizito, akainua kichwa na kumwangalia mkuu.
‘Mkuu, nimekuambia nawataka hapa, mke wangu, narafiki
yake,waje hapa tuyamalize…na huyo mfu keshapona…?’akageuza kichwa kuangalia
nje.
‘Mfu gani huyo….?’akauliza mkuu.
‘Huyo muhusika mkuu,huyo ndiye aliyejifanya anajua sana, eti
ana akili …akawapagawisha hawa akina dada, na…na kutaka kutuzalilisha, ..mkuu
unakumbuka ile kanda ya Cd,uliyoichukua kipindi kileee…huyo ndiye muhusika,
mleteni hapa….hata kama ni maiti yake, nataka iongee…hajafa huyo, nimemfinya kidogo
tu, tatizo ni kuwa hajala,ana njaa…mpeni chakula.’akasema huku akiinuka kwenye
kiti.
Safarii hii alisimama vyema kabisa, na kugeuka kutuangalia
mmoja mmoja, aliponigeukia mimii akaniangalai kwa muda, akasema.
‘Na wewe umefuata nini hapa…mkuu huyu hahusiki hapa, nataka
hili swala tuliongelee kikazi, wahusika ni mimi, wewe, mke wangu, rafiki yake,
huyu mwanadada, nataka awepo hapa, ili athibitishe, ni shahidi yangu muhimu….hata
wewe wakili, msaidizi wangu,…wewe utakuwa wakili wangu mtetezi, au sio…hata
kama hutaki sijali….lakini huyu jamaa, sijui anahitaji au vipi, lakini mmmmh,labda
awe kama shahidi tu, sijui,mnamjau nyie….’akanisogelea na kunishika begani.
‘Huyu ni mtu wetu….’akasema mkuu
‘Kwani wewe ni nani….aaah, nimeshakukumbuka,ndio wewe eeh,
tumeshakufunga mara mbili, samahani sana,sasa nimekukumbuka usiondoke,nataka
uyasikie mwenyewe, utaona ni nani mbaya wako…’akasogea pale aliposimama wakili
mwanadada.
‘Sasa unasemaje unakubali kuwa wakili wangu..nitetee rafiki
yako….aah, hata kama hutaki sio mbaya, …mkuu watume vijana wako wawalete hawo
watu hapa haraka tumalize haya mambo, hakuna muda wa kupoteza tena, kesi
imefika penyewe, na ikibidi muite na hakimu, …na wazee wa baraza, au…nina wazo,
sote twendeni mahakamani tukayamazie huko huko…’akasema huku akiyumba.
‘Mimi natoa wazo, kama unataka haya yote yafanyike, wote
hawo uliowataka watachukuliwa na kusimama mbele ya mahakama, na kama unavyotaka
kila kitu kitafanyika hivyo, kwanza tuhakikisha kuwa umekula, una
afya,hujalewa….utasimama je mbee ya hkimu ukiwa na hai kama hiyo,….hebu fikiria
kwanza….kila kitu kitafanyika kama unavyotaka, tena kisheria unasemaje…?’
akasema Yule mwanadada.
Yule jamaa alitulia kwa muda kama anawaza jambo,halafu
akamwangali Yule mwanadada, akatabasamu, halafu akamgeukia mkuu akasema;
‘Mkuu unasemaje ,maana hapa nakuheshimu wewe tu….utakalosema
nitalisikiliza,lakini je hiyo kesho itafika, maana nimeshamuona izraili
akinichungulia,anasubiri muda, aichukue roho yangu, sasa nyie mnamwekea
kiwingu,….ongeeni naye, kamatakubai kuahirisha kazi yake, sawa…..maana kaja
kasema nina kesi huko mbele, Kimwana ananisubiri…’akapepesuka hadi kwenye kiti
chake na kabla hajakifikia akayumba, na mara akadondoka chini ….
Yule mwanadada akamsogelea nakujaribu kumuinua,lakini
haikuwa kazi rahisii akatugeukia na kusema;
‘Keshapoteza fahamu, naona huu ndio wakati muafaka tumpeleke
hospitalini,maana akizindukana hapa tunaweza tukashindwa kumsadia,ni kweli ana
mengi ya kuwaambia, ….lakini afya yake kwanza, amekuwa kama kachanganyikiwa….’akasema
huyo mwanadada.
‘Na huyo jamaa huko nje ni nani maana sijawauliza watu wangu
vyema namlimpatia wapi…?’akauliza mkuu.
‘Jamaa gani huyo?’ Yule mwanadada akauliza kwa mshangao huku
akihagaika kutoa hudum ya kwanza kwa huyo jamaa aliyedondoka chini.
‘Huyo aliyekuwa kwenye gari…ambaye wanasema kazimia kwa kupoteza
damu nyingi…?’ akauliza mkuu.
‘Yupi huyo mbona sielewi, unajua mimi nimekuja kivyangu,…huyu
…aliondoka mapema hapo ninapokaa,…ooh,au ndioo huyo Sokoti…..mmh, …kwakweli sin auhakika kuwa ni nani, labda akizindukana
atawaambia mwenyewe, …maana alisema anakwenda kumkamata mbaya wake….’akasema
huyo mwanadada huku akimweka sawa huyo jamaa aliyedondoka chini bado akiwa
kapoteza fahamu.
‘Unasema ni huyu Sokoti tunayemtafuta….!?...hebu niwauize
vijana wangu,…..’Mkuu akauliza huku akiwa kashangaa akapiga simu kwa vijana
wake kuulizia.
NB: Nimeona siku isipite bure, japo kwa shida, nimewaletea sehemu hiyo. Tutakuja kuhitimisha kisa hiki,inabidi kwanza nikipitie
kidogo,….na kama kuna kitu nimekisahau naomba mnifahamishe,…tuweni
pamoja,….shukurani kwa wale mnaokuwa pamoja nami,hata kama ni kwakimiya kimiya,
sio mbaya, Tupo pamoja.
WAZO LA LEO: Zarau sio jambo jema, hata kama unacho, hata
kama unajua sana, hata kama umesoma sana,...hata kama,....lakini usipende kuwazarau wenzako, kwani pamoja na
hayo mpaji ni mungu, huwezi jua kuna leo na kesho, leo kwako kesho anajua mwenyewe Muumba.. Hapa nikaumbuka usemi
usemao; aliyekupa wewe kiti, ndiye aliyenipa mimi kumbi, na pia mzarau mwiba guu huota tende.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Tupo pamoja,mara nyingi tupo kimiya kimiya!
Post a Comment