Sokoti alifunua macho,harufu ya madawa ikamtawala…, aliwaza
na kujiuliz ayupo wapi, mbona, hajafa au ndio yupo ahera, …hapana, mbona kuna
harufu ya madawa, ina maana sijafa, ….Akaanza kuogopa na ile hali ya mateso
ikamjia kichwani, akakumbuka ile mikasi iliyokuwa ikimkata sikioni, akajaribu
kuinua amkono kushika sikio mara akasikia maumivu, kwenye mkono.
Alipoinua mkono kuuangalia na kukuta umefungwa bandeji,kumbukumbu
za tukio zikaanza kumjia, alijihisi yupo sehemu ile aliyokuwa kajificha,
akakumbuka jinsi gani alivyokuwa akiwaogopa watu, alianza kuwaogopa watu baada
ya kusikia kuwa watu wengi wameshamgundua kuwa yeye ndiye aliyekuwa na mitambo
ya kutengenezea hiyo mikanda ya mambo yaliyokuwa yakifanyika kwa wanandoa walihini ndoa zao.
Akapata taarifa kuwa polisi wanamtafuta, na akipatikana
anaweza akapelekwa Segerea au Keko, na huko anaweza akakutana na mahasimu wake
aliowahi kuwatendea ubaya, na huenda wakataka kulipiza kisasi, akakumbuka jinsi
alivyosimuliwa mabaya ya jela, alipokumbuka hilo mwili mzima ukazizima.
‘Ni heri kufa kuliiko kupelewa jela…’akajikuta akijisemea,
‘Wewe wakati unafanya hayo hukujua kuwa ni ubaya, hukujua
kuwa wenzako nao wanaumia au ilikuwa mkuki kwa nguruwe….’akasikia sauti
ikimwambia, akaguka na kumwangalia huyo mwanadada ambaye ndiye aliyebakia akimsaidia. Huyu
binti alijuana naye kwasababu ya mambo yake ya ushauri, na mbinu za kumfanya
mume aogope kufanya mabaya na alishamtumia kwenye kazi zake na hapo alikuwa
akidao pesa zake alizoahidiwa.
‘Mimi nakusaidia tu, kwa vile ulinisadia kipindi kile,
vinginevyo ningekuitia polisi, na ujue wakili mkuu ni rafiki yangu mpenzi,
akijua ninakuficha wewe hapa ….maana jana tu kaniuliza kuwa sijasikia lolote
kuhusu wewe, anakufuta kama nini sijui, na akijua kuwa mimi najua ulipo na
sijamwambia, ataniua….ila ninachotaka kutoka kwako ni pesa zangu…ukinipa
hizo,aaah, mdomo naufunga kabisa….’akasema.
‘Pesa zako nimeshakuambia nitakulipa, lakini siwezi kwenda
benki,…nitafikaje huko,unaju kila sehemu jina langu limeshafika, na hasa benki,
wanajua nitaishiwa, na nitakwenda benki, ….naomba unipe muda, nitajua la
kifanya….’akasema.
‘Mimi hayo sijui,..unakumbuka ulivyonitumia, na mapicha
mbaya uliyochukua kwangu, na ukapata pesa nyingi, na kunihadaa na Yule Malaya
wako…..ole wake ningelimwahi mimi Yule ningemtafuna nayma yake,lakini nilikuta
watu wameshamuwahi….’akasema.
‘Ina maana hukumuua wewe….?’ Akauliza.
‘Ina maana huniamini, nimeshakuambi kuwa, nilipofika pale,
nikakuta keshauliwa….kama unavyojua alikuwa na maadui wengi,….sijui ni nani,
kama ningelimjua ningempa zawadi….’akasema.
‘Kweli ulikuwa ukimchukia kiasi hicho, mimi mbona niliwaona
kuwa ni mrafiki mlioshibana,maana kila mara mpo naye,….na nilimpenda sana Yule
binti, ni mjuzi na mtaalamu mzuri kwenye mambo Fulani, kweli kizuri hakidumu,i,…kumkosa
Yule ilikuwa ni pigo kubwa….’akasema.
‘Alikuwa mjuzi gani Yule Malaya mkubwa yule, ana nini cha
zaidi kuliko sisi, haya kamfukue awafanyie hayo uliyokuwa ukitaka,….’akasema
kwa hasira.
‘Sikiliza tuyaache hayo, nenda kwa mkuu, ujue nini
wamepanga, maana njua ananitafuta mimi,na kama kapanga mbinu gani uje uniambie,
na polisi wana mipago gani na mimi…halafu nilikuwa natakaunitafutie
mteja,…nataka niisukumeile mashine yangu,…’akasema.
‘Mimi siendi popote, ninachohitaji ni pesa zangu, ujue hapa
ulipo nimekuwa nikikulisha mimi, unafikiri nitapata wapi pesa za kukulisha kila
siku,….mimi natoka nikirudi nikute pesa zangu, vinginevyo, …kesho tu polisi
watakuwa wamekunasa, ukacheze segerea….’akasema na huku akiondoka.
'Nikiuza hiyo mashine,tutapata pesa…hizo za benki siburi
kwanza….’akasema.
‘Hiyo mashine ipo wapi?’ akauliza mwanadada kwa hamasa
‘Ilipo ni siri kubwa sana kwangu, wewe nitafutie mteja, ....nimekumbuka wewe nenda kwa
Yule muhindi wangu…yule niliyekuelekeza siku ile, Yule atainunua tu,ilemashine inahitajika sana, na thamani yake ni kubwa…’akasema.
‘Mimi naona hapa unaniletea zongozongo,huna lolote
umeshafulia, kwanza hatuaminiani,….sasa ngoja niondoke,……’akasema huku
akichukua mkoba wake.
‘Sasa unaondoka,…mimi nitakuala nini….?’ Akauliza.
‘Kula mawe, sina pesa za kupoteza zaidi, nimekuchoka, maana
unanifanya niishi maisha ya dhiki ,kama vile nina familia,lakini huenda hata
huko moyoni mwako, huna nafasi na mimi, ni kwa vile unahitaji kunitumia kwa maslahi
yako, nawajau sana nyie wanaume,….’akasema na kufunga mlango.
‘Nenda bwana,usinibabaishe,….nitaibuka kinamna yangu, na ole
wako ukiwaambia hawo mabwana zako,nitahakikisha unamfuata Kimwana hukoalipo,
….unanijua nilivyo, ….
‘Ni mpaka,kwanza usinitisha kabisa, zako zinahesabika, wewe
subiri kidogo tu, utaona nini kitafuata, hata kama sitapata hizo pesa, lakini
najua utakipata cha mtema kuni,…na utanikumbuka ukiwa jela….’akasema huku
akihakikisha amefunga mlango wake kwa nje.
‘Tutaona….ukija hapa hunikuti…..’akasema huku akiwaza la
kifanya,alijua kabisa hapo sasa hakuna usalama, ni lazima afanye mpango wa
kuondoka hapo haraka iwezekanavyo, lakini atakwenda wapi, akaichukua simu yake,
Alipopiga simu akasikia salio halitoshi, akashangaa, mbona
jana aliweka pesa ya kutosha, nani kaitumia simu yake….na tangu huyo mwanadada
afike, hakumuona kabisa akitumia simu yake, akataka kuangalia majina
yaliyopigwa, simu ikazimika, haina chaji,akatafuta kifaa cha kujachia akakuta
hakipo, akasonya, akahangaika kuwasha lakini ikawa haiwaki,….
‘Sasa nifanyeje, akafikiri kwa muda,akaangalia kabatini na
kutafuta nguo zake, anazoona zinafaa akaziweka kwenye begi, akaangalia sehemu
yake anapoweka pesa, hakuna kitu, alijua kabisa hana pesa, …akaenda chumba
anapolala. Alipohakikisha kuwa hakuna pesa yoyote, akaamua kuondoka hivyo
hivyo, akaufikia mlango, ukaukuta umefungwa, haufungiki.
‘Ina maana huyu mwanamke kanifungia, ..’akasema kwa hasira,
huku akitafuta ufunguo,….hakuna ufunguo,….akaanza kuhaha,jasho likaanza
kumtoka, akijua sasa huyo mwanamke kadhamiria ubaya, akaangalia dirishani,
akakuta madirisha yoye yamezungushiwa nondo huwezi kabisa kupenya, akaishiwa
nguvu.
‘Mungu wangu, Segerea hiyooo, inaniita, mungu wangu, sasa
nimeumbuka, lakini sikubali, siwezi kwenda Segerea, au Keko, au …..wapi kule,
….hapana nikifika huko hawo jamaa watanirukia kama mpira wa kona,nitageuzwa
….hapaan sikubali, sasa nifanyeje…’akawa anaongea peke yake.
Wazo likamjia haraka, alishangaa kwanini wazo kama hilo
limemjia, nahakuwazia katika maisha yake kuwa atafikiria hivyo, maisha kwakwe
ni kitu cha muhimu sana, sasa kwanini anawazia hivyo, kujiua…
‘Nijiue mimi….hapana hilo wazo silitaki….hapana,siwezi
kujiua….’akasema huku akianza kutetemeka, lakini cha ajabu akili ikawa
inamshinikiza hivyo,kuwa ajiue,mbona yeye alikuwa akiwashauri wale waliotaka
kusaliti kundi, kuwa wajiue, na kweli kuna waliojiua kwa shinikizo lake,
kutokana na mambo yake, je yeye kwanini ishindikane.
Akaona kisu kwenye kabati, akakifuata na kukiangalia..’jiue,
jiue, bwana, utakwenda kuuwawa kinyama Segerea, watakutesa na baadaye utakufa
kwa aibu, bora ufe kabla hujakamatwa….’akasikia sauti ikisema
‘Kweli ngoja nijimaliza, nikijimaliza, nikijimaliza basi
tena,sitakuwa na deni na mtu, watakuta maiti yangu tu, na mambo
yamekwisha,….ooh, mungu wangu nisaidie,…ooh, nisameheeni nyie niliowafanyia
mabaya, ….najua nimekosa sana,kwa tamaa zangu za pesa,…..najua kwa hayo
niliyofanya nastahili adhabu kubwa, lakini nikutafuta maisha..ooh, nimekwisha….’akajikuta
akilia .
Alianza kuwakumbuka wazazi wake,ambao kwakweli anawapenda sana
pamoja na mengine pamoja na tabia yake hiyo, lakini wazazi wake alikuwa
akiwajali, akamkumbuka mama yake, akawa anamuwaza jinsi gani atakavyolia
akisikia kuwa amekufa,….na baya zaidi amekufa hata hana mjukuu wake, akakumbuka
mama yake alivyokuwa akimshaurii aoe, ili angalau apate mjukuu…
‘Nitaoa tu mama, lakini nikioa sitaki mke wangu apate
shida,..nataka ni kwanza na nyumba ya kifahari, gari la maana…yote ya
kifahari…usije kupata taabu. …’anakumbuka alivyomwambia mama yake kwamara ya
mwisho.
Akachukua kisu,akaona njia njema ni kukata mshpa wa mkono,
hapo akitoa damu nyingi atakufa haraka,…akachukua kisu akajaribu kidogo,maumivu
aliyoyapata akakitupa kile kisu chini, akaangalia damu kidogo iliyotoka,
akasema hapana lazima nijiue, sikubali kwenda Segerea,….akachukua kile kisu
akafumba macho, kwa kasi akakata mkono….alipiga ukulele. Nadamu ukaanza kutoka
kwa kasi, na mara mlango ukafunguliwa…
Alipoaangali mlangoni,akamuona mbaya wake, ….wakili mkuu, …akajua
sasa anakamatwa,kumbe Yule mwanadada keshamsaliti,kumbe keshamuambia huyu jamaa
kuwa yupo hapo,….akamwangalia na kuanza kucheka,akijua kachelewa, hizo damu
zinavyotoka hataweza kufanya lolote……
NB: Kidogo kidogo tunamalizia
WAZO LA LEO: Maisha
ni kupambana,na kila hatua ni maendeleo, na kila jambo lina vikwazo vyeka.
Tusikate tamaa pale tunapojikuta tupo kwenye mitihani. Mitihani na
majukumu,ndio changamoto ya kuboresha kile ulichodhamiria kukifanikisha,…kaza
buti, na nyosha mguu, utafika…kwani mungu hamtupi mja wake.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Mambo safi kama movie vile...hongera sana
Sasa jamaa analia nini?
Post a Comment