Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 15, 2012

Hujafa hujaumbika-53 hitimisho-11Sokoti alifunua macho,harufu ya madawa ikamtawala…, aliwaza na kujiuliz ayupo wapi, mbona, hajafa au ndio yupo ahera, …hapana, mbona kuna harufu ya madawa, ina maana sijafa, ….Akaanza kuogopa na ile hali ya mateso ikamjia kichwani, akakumbuka ile mikasi iliyokuwa ikimkata sikioni, akajaribu kuinua amkono kushika sikio mara akasikia maumivu, kwenye mkono.

Alipoinua mkono kuuangalia na kukuta umefungwa bandeji,kumbukumbu za tukio zikaanza kumjia, alijihisi yupo sehemu ile aliyokuwa kajificha, akakumbuka jinsi gani alivyokuwa akiwaogopa watu, alianza kuwaogopa watu baada ya kusikia kuwa watu wengi wameshamgundua kuwa yeye ndiye aliyekuwa na mitambo ya kutengenezea hiyo mikanda ya mambo yaliyokuwa yakifanyika   kwa wanandoa walihini ndoa zao.

Akapata taarifa kuwa polisi wanamtafuta, na akipatikana anaweza akapelekwa Segerea au Keko, na huko anaweza akakutana na mahasimu wake aliowahi kuwatendea ubaya, na huenda wakataka kulipiza kisasi, akakumbuka jinsi alivyosimuliwa mabaya ya jela, alipokumbuka hilo mwili mzima ukazizima.

‘Ni heri kufa kuliiko kupelewa jela…’akajikuta akijisemea,

‘Wewe wakati unafanya hayo hukujua kuwa ni ubaya, hukujua kuwa wenzako nao wanaumia au ilikuwa mkuki kwa nguruwe….’akasikia sauti ikimwambia, akaguka na kumwangalia huyo  mwanadada ambaye ndiye aliyebakia akimsaidia. Huyu binti alijuana naye kwasababu ya mambo yake ya ushauri, na mbinu za kumfanya mume aogope kufanya mabaya na alishamtumia kwenye kazi zake na hapo alikuwa akidao pesa zake alizoahidiwa.

‘Mimi nakusaidia tu, kwa vile ulinisadia kipindi kile, vinginevyo ningekuitia polisi, na ujue wakili mkuu ni rafiki yangu mpenzi, akijua ninakuficha wewe hapa ….maana jana tu kaniuliza kuwa sijasikia lolote kuhusu wewe, anakufuta kama nini sijui, na akijua kuwa mimi najua ulipo na sijamwambia, ataniua….ila ninachotaka kutoka kwako ni pesa zangu…ukinipa hizo,aaah, mdomo naufunga kabisa….’akasema.

‘Pesa zako nimeshakuambia nitakulipa, lakini siwezi kwenda benki,…nitafikaje huko,unaju kila sehemu jina langu limeshafika, na hasa benki, wanajua nitaishiwa, na nitakwenda benki, ….naomba unipe muda, nitajua la kifanya….’akasema.

‘Mimi hayo sijui,..unakumbuka ulivyonitumia, na mapicha mbaya uliyochukua kwangu, na ukapata pesa nyingi, na kunihadaa na Yule Malaya wako…..ole wake ningelimwahi mimi Yule ningemtafuna nayma yake,lakini nilikuta watu wameshamuwahi….’akasema.

‘Ina maana hukumuua wewe….?’ Akauliza.

‘Ina maana huniamini, nimeshakuambi kuwa, nilipofika pale, nikakuta keshauliwa….kama unavyojua alikuwa na maadui wengi,….sijui ni nani, kama ningelimjua ningempa zawadi….’akasema.

‘Kweli ulikuwa ukimchukia kiasi hicho, mimi mbona niliwaona kuwa ni mrafiki mlioshibana,maana kila mara mpo naye,….na nilimpenda sana Yule binti, ni mjuzi na mtaalamu mzuri kwenye mambo Fulani, kweli kizuri hakidumu,i,…kumkosa Yule ilikuwa ni pigo kubwa….’akasema.

‘Alikuwa mjuzi gani Yule Malaya mkubwa yule, ana nini cha zaidi kuliko sisi, haya kamfukue awafanyie hayo uliyokuwa ukitaka,….’akasema kwa hasira.

‘Sikiliza tuyaache hayo, nenda kwa mkuu, ujue nini wamepanga, maana njua ananitafuta mimi,na kama kapanga mbinu gani uje uniambie, na polisi wana mipago gani na mimi…halafu nilikuwa natakaunitafutie mteja,…nataka niisukumeile mashine yangu,…’akasema.

‘Mimi siendi popote, ninachohitaji ni pesa zangu, ujue hapa ulipo nimekuwa nikikulisha mimi, unafikiri nitapata wapi pesa za kukulisha kila siku,….mimi natoka nikirudi nikute pesa zangu, vinginevyo, …kesho tu polisi watakuwa wamekunasa, ukacheze segerea….’akasema na huku akiondoka.

'Nikiuza hiyo mashine,tutapata pesa…hizo za benki siburi kwanza….’akasema.

‘Hiyo mashine ipo wapi?’ akauliza mwanadada kwa hamasa

‘Ilipo ni siri kubwa sana kwangu, wewe nitafutie mteja, ....nimekumbuka wewe nenda kwa Yule muhindi wangu…yule niliyekuelekeza siku ile, Yule atainunua tu,ilemashine inahitajika sana, na thamani yake ni kubwa…’akasema.

‘Mimi naona hapa unaniletea zongozongo,huna lolote umeshafulia, kwanza hatuaminiani,….sasa ngoja niondoke,……’akasema huku akichukua mkoba wake.

‘Sasa unaondoka,…mimi nitakuala nini….?’ Akauliza.
‘Kula mawe, sina pesa za kupoteza zaidi, nimekuchoka, maana unanifanya niishi maisha ya dhiki ,kama vile nina familia,lakini huenda hata huko moyoni mwako, huna nafasi na mimi, ni kwa vile unahitaji kunitumia kwa maslahi yako, nawajau sana nyie wanaume,….’akasema na kufunga mlango.

‘Nenda bwana,usinibabaishe,….nitaibuka kinamna yangu, na ole wako ukiwaambia hawo mabwana zako,nitahakikisha unamfuata Kimwana hukoalipo, ….unanijua nilivyo, ….

‘Ni mpaka,kwanza usinitisha kabisa, zako zinahesabika, wewe subiri kidogo tu, utaona nini kitafuata, hata kama sitapata hizo pesa, lakini najua utakipata cha mtema kuni,…na utanikumbuka ukiwa jela….’akasema huku akihakikisha amefunga mlango wake kwa nje.

‘Tutaona….ukija hapa hunikuti…..’akasema huku akiwaza la kifanya,alijua kabisa hapo sasa hakuna usalama, ni lazima afanye mpango wa kuondoka hapo haraka iwezekanavyo, lakini atakwenda wapi, akaichukua simu yake,

Alipopiga simu akasikia salio halitoshi, akashangaa, mbona jana aliweka pesa ya kutosha, nani kaitumia simu yake….na tangu huyo mwanadada afike, hakumuona kabisa akitumia simu yake, akataka kuangalia majina yaliyopigwa, simu ikazimika, haina chaji,akatafuta kifaa cha kujachia akakuta hakipo, akasonya, akahangaika kuwasha lakini ikawa haiwaki,….

‘Sasa nifanyeje, akafikiri kwa muda,akaangalia kabatini na kutafuta nguo zake, anazoona zinafaa akaziweka kwenye begi, akaangalia sehemu yake anapoweka pesa, hakuna kitu, alijua kabisa hana pesa, …akaenda chumba anapolala. Alipohakikisha kuwa hakuna pesa yoyote, akaamua kuondoka hivyo hivyo, akaufikia mlango, ukaukuta umefungwa, haufungiki.

‘Ina maana huyu mwanamke kanifungia, ..’akasema kwa hasira, huku akitafuta ufunguo,….hakuna ufunguo,….akaanza kuhaha,jasho likaanza kumtoka, akijua sasa huyo mwanamke kadhamiria ubaya, akaangalia dirishani, akakuta madirisha yoye yamezungushiwa nondo huwezi kabisa kupenya, akaishiwa nguvu.

‘Mungu wangu, Segerea hiyooo, inaniita, mungu wangu, sasa nimeumbuka, lakini sikubali, siwezi kwenda Segerea, au Keko, au …..wapi kule, ….hapana nikifika huko hawo jamaa watanirukia kama mpira wa kona,nitageuzwa ….hapaan sikubali, sasa nifanyeje…’akawa anaongea peke yake.

Wazo likamjia haraka, alishangaa kwanini wazo kama hilo limemjia, nahakuwazia katika maisha yake kuwa atafikiria hivyo, maisha kwakwe ni kitu cha muhimu sana, sasa kwanini anawazia hivyo, kujiua…

‘Nijiue mimi….hapana hilo wazo silitaki….hapana,siwezi kujiua….’akasema huku akianza kutetemeka, lakini cha ajabu akili ikawa inamshinikiza hivyo,kuwa ajiue,mbona yeye alikuwa akiwashauri wale waliotaka kusaliti kundi, kuwa wajiue, na kweli kuna waliojiua kwa shinikizo lake, kutokana na mambo yake, je yeye kwanini ishindikane.

Akaona kisu kwenye kabati, akakifuata na kukiangalia..’jiue, jiue, bwana, utakwenda kuuwawa kinyama Segerea, watakutesa na baadaye utakufa kwa aibu, bora ufe kabla hujakamatwa….’akasikia sauti ikisema

‘Kweli ngoja nijimaliza, nikijimaliza, nikijimaliza basi tena,sitakuwa na deni na mtu, watakuta maiti yangu tu, na mambo yamekwisha,….ooh, mungu wangu nisaidie,…ooh, nisameheeni nyie niliowafanyia mabaya, ….najua nimekosa sana,kwa tamaa zangu za pesa,…..najua kwa hayo niliyofanya nastahili adhabu kubwa, lakini nikutafuta maisha..ooh, nimekwisha….’akajikuta akilia .

Alianza kuwakumbuka wazazi wake,ambao kwakweli anawapenda sana pamoja na mengine pamoja na tabia yake hiyo, lakini wazazi wake alikuwa akiwajali, akamkumbuka mama yake, akawa anamuwaza jinsi gani atakavyolia akisikia kuwa amekufa,….na baya zaidi amekufa hata hana mjukuu wake, akakumbuka mama yake alivyokuwa akimshaurii aoe, ili angalau apate mjukuu…

‘Nitaoa tu mama, lakini nikioa sitaki mke wangu apate shida,..nataka ni kwanza na nyumba ya kifahari, gari la maana…yote ya kifahari…usije kupata taabu. …’anakumbuka alivyomwambia mama yake kwamara ya mwisho.

Akachukua kisu,akaona njia njema ni kukata mshpa wa mkono, hapo akitoa damu nyingi atakufa haraka,…akachukua kisu akajaribu kidogo,maumivu aliyoyapata akakitupa kile kisu chini, akaangalia damu kidogo iliyotoka, akasema hapana lazima nijiue, sikubali kwenda Segerea,….akachukua kile kisu akafumba macho, kwa kasi akakata mkono….alipiga ukulele. Nadamu ukaanza kutoka kwa kasi, na mara mlango ukafunguliwa…

Alipoaangali mlangoni,akamuona mbaya wake, ….wakili mkuu, …akajua sasa anakamatwa,kumbe Yule mwanadada keshamsaliti,kumbe keshamuambia huyu jamaa kuwa yupo hapo,….akamwangalia na kuanza kucheka,akijua kachelewa, hizo damu zinavyotoka hataweza kufanya lolote……

NB: Kidogo kidogo tunamalizia

WAZO LA LEO: Maisha ni kupambana,na kila hatua ni maendeleo, na kila jambo lina vikwazo vyeka. Tusikate tamaa pale tunapojikuta tupo kwenye mitihani. Mitihani na majukumu,ndio changamoto ya kuboresha kile ulichodhamiria kukifanikisha,…kaza buti, na nyosha mguu, utafika…kwani mungu hamtupi mja wake.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Mambo safi kama movie vile...hongera sana

Anonymous said...

Sasa jamaa analia nini?