Nikiwa uwanja wa ndege wa Nairobi, huku nikiwa nimetawaliwa na
mawazo mengi, maana niliyoyasikia kwa mama docta yalinichanganya. Nilihitaji
muda wakuyafanyia kazi,na niseingeliweza kufiki uamuzi wowote kichwani, mpaka
nikutane nao, au nipate maelezo ya ziada, mimi huwa simini kitu, mpaka
nikifanyie kazi.
Kwahiyo katika utaratibu wangu wa kikazi nikapanga kukutana
na mke wa wakili wetu wa kitengo ili kujirizisha na hayo niliyosikia ,najua inaweza ikaleta sintofahamu, lakini huyu mtu ni muhimu sana kwangu, kukutana nayena rahisi, lakini kuna huyu
mwanadada,binti wa kijijini kama tulivyozoea kumuita, kwanza sina mazoea naye, na
sijakutana naye kwa karibu, tukaongea kiundani, mengi kuhusu yeye nimeyasikia
toka kwa watu wengine,nilihitaji sana, nioenane na yeye, nisikie yake ya moyoni.
Nakumbuka siku zilizopita, nijaribu kufanya hivyo,lakini sikufanikiwa,maana kila nilipopata huo mwanya, yeye akawa hana
nafasi. Sasa sina ujanja lazima nikakutane naye....nikajiwekea azima hiyo na kuiweka kwenye kitabu changu cha kumbukumbu.
Nilipoweka ratiba yangu vyema, nikakirudisha kitabu changu cha kumbukumbu kwenye mkoba wangu. Niliangalai saa nikaona imebakia dakika thelathini na mbili tuwezekuondoka hapo,nikachukua gazeti la nyumbani na kuanza kusoma mambo mbali mbali, nilijaribu kutafuta kama kunalolote kuhusu kesi nilizoziacha,sikuona lolote linalohusu hizo kesi,....
Nilishituka pale niliposhikwa bega,ingekuwa bongo,
ningejihami maana kuna ule wizi wa kibongo , mtu anakushika bega, ukigeuka
upande ule mkono ulipotokea, upande mwingine wanakuchomolea, kile kichopo
kwenye mfuko wa shati. Wizi huo wanauita `mdudu’…
‘Nimekuwahi, maana kama ungeliondoka kabla sijaongea na wewe
ningejisikia vibaya sana,…na sio kujisikia vibaya tu, kesho ningelifunga safari
nije huko Dar…lakini nimekuwahi,najua mambo yataishia hapa….’ilikuwa sauti ya mama Docta, nilishangaa
kufika hapo uwanjani, maana wale watu niliowaacha pale ofisini wakitaka kumuona yeye, isingelikuwa rahisi kuwamaliza kwa muda huo, labda katoa uzuru, na kuchomokakuja huku uwanja wa ndege.
Nakumbuka nilipofika pale asubuhi, nilimkuta ana wateja, yeye akaniona, na akanipungia mkono kuwa nisubiri kidogo, akawa
anawapanag wale wateja, waende kumuoa msaidizi wake na binti yake,….lakini kama
unavyojua binadamu, akiwa kakamia jambo, itachukau muda kumshawishi, wengi
wakawa hawamsikilizi wanataka kumuona yeye, angalau kidogo.
‘Wewe mlinzi nilikuambia nini….na wewe mratibu nini hiki
unafanya, mbona mambo yanakwenda kinyume cha ratiba….?’ Akawa anafoka.
‘Bosi hawa wameamua kuingia kwa nguvu tu….’akajitetea na mlinzi
akawa na kazi ya ziada, na ili kuleta picha nzuri,ikabidi huyo mama atumie
hekima na kuwasikiliza angalau kidogo….nahapo muda
ukawaumekimbia,nilipoaangalai saa yangu nikaoan sina muda tena wakuonana na
huyo mama, nikainuka na kuanza kuondoka.
Mara akaja binti yake na kusalimiana na mimi,akaniambai kuwa
mama kashindwa kuonana na mimi, lakini atajitahidi muwasiliane naye,
‘Hamna shida,nimeiona hiyo hali,siwezikabisa kumlaumu….’nikamwambia
nakumwangalia huyo binti,na kila nikimwangalia niliona kama namwangalia,mke wa
wakili wetu wa kitengo, nikamuuliza.
‘Mume wako hajambo….?’ Nilisema huku nikiangalai pete yake
inayoonyesha kuwa kaolewa.
‘Hajambo hana wasiwasi,…..nashukuru mungu kuwa nimepata mume
tunayeshibana, na hata yeye kila siku anashukuru kwa hilo, …..’akasema.
‘Hongera sana,maana wewe ni mwalimu wa ndoa,docta….mke
mwema,…..kama mimi ningekuwa mume ningeshukuru sana…’nikasema.
‘Nimesikitikasana sikupta muda wakuongea na wewe,na nilitaka
kujua mengi kuhusu ndugu yangu, …unajua alichukua maamuzi ya haraka kuolewana na huyo mume wake…..nilimshauri sana. Huyu mume wake mwanzoni alikuwa namchumba wake….akambwaga
huyo mchumba wake wa awali nakumchukua ndugu yangu…’akasema.
‘Ooh, mbona nimekosa mengi, sikuyasikia hayo toka kwa mama
yako…!’nikasema.
‘Hayo yalikuwa ya awali na hayakuwa na nguvu sana,mimi
nayajua zaidi,…maana hata mama mengine tulimficha, siunajau tena ukiwa mwingi
wa wasichana unaweza ukachumbua wasichana zaidi ya mmoja, maana ni tamaa na
hata mwishoni utaoa,huku nafsi haijatulia,….huyo mume wake anaonekana alikuwa
na tama...
‘Kwahiyo tusema, ndugu yako alikuwa akijua hilo….?’nikauliza.
‘Alikua akijua, na alishampenda huyo shemeji,…na akaahidi
kuwa atawabwaga wengine wote…unajua nafsi ikipenda haitizami mbali,…ukipenda,ukiona
chongo unaita kengeza..na usichana,damu inachemka,basi tena, ..lakini nahisi hivi
sasa anajuta…’akasema.
‘Ulishawahi kuwaslina naye kweney simu?’ nikamuuliza.
‘Mara nyingi sana,siunajau tena sisi ni mapacha, ananimbia baadhi ya mambo yake kuhusu yeye na mume wake, kwa ujumla ndoa yao sio nzuri, lakini kwa vile
keshaolewa, inabidi afunge mkanda, mimi nilimshauri aivunje tu ajue moja, lakini hakukubali…ana.mpenda
sana mume wake, ila mumewe hapendiki..ndio tatizo hapo’akasema.
‘Lakini nyie mumefundwa mnajau jinsi gani ya kumweka mume
sawa, kwanini yeye ashindwe…?’ nikauliza.
‘Hilo linatokana na mume mwenyewe, na tatizo jingine ni wewe
mwanamke ukiwa na mjukmu ya ziada ukashindwa kujipanga unaweza ukajisahau, na
hasa pale unapojaribu kumweka mume wako sawa, akawa mgumu kupita kiasi,…wapo
wanaume sugu, utajaribu kila mbinu, lakini haeleweki, na kama ujuavyo kazi za
udakitari ni wito, zinachosha kweli, …sehemu nyingine unafanya kazi kupita kiasi, ..unachoka…’akasema.
‘Ndugu yako aliwahi kukulamikai kuwa anachoka kiasi kwamba
anakosa muda wa kutimiza majukumu yake kama mke….?’ Nikauliza.
‘Sana, hilo analalamika sana,anasema hapo anapofanya kazi,
kuna waginjwa wengi, na wengi wa wafanyakazi hapo waantega kaz, sio watendaji
wazuri, sasa yeye anaipenda sana hiyo kazi, anapenda saan kuwasaidia wagonjwa,
na mwisho wa siku anajikuta anabeba majukumu mengi zaidi ya uwezo wake….anasema
wagonjwa wengi wanapenda kumuona yeye tu….’akasema.
‘Kwahiyo ulimshauri nini ….weweni mtaalamu wa ndoa, ni
mtaalamu,dakitari…?’ nikamuuliza.
‘Kwanza ajaribu kuwa na ratiba, ahakikishe anaifuata, na
majukumu yasiivuruge hiyo ratiba, pili ajue kuwa yeye ni mke wa mtu, ahakikishe
kuwa anakuwa karibu na mume wake….asimpe muda mume wake kupaat visingizio….na
ni limlaumu sana pale alipochukua mfanyakazi wa nyumbani, wa nini…..bado hawana
watoto….’akasema.
‘Ilisaidia huoushauru wako…?’ nikamuuliza.
‘Aaah,yeye mwenyewe aandai anafanya hivyo, lakini mume wake hashibi…..nikajua kuna tatizo hapo,kama
wangelikubali wakaja yeye na mume wake,tungelijua jinsi gani ya kulitatua hilo,
maana mara nyingi dakitari hawezi kujiganga….maana ni vyema ukasikilizwa na
mwenzako,….anaweza akajua nini ambacho wewe hujakijua….’akasema.
‘Je kuna mengina alikuambia,hajakuambia kuwa anataak uanzisha
kliniki kama hii hapa?’ nikamuuliza.
‘Hilo tulimshauri sisi awali, alisema kazi zenyewe alizo
nazo ni nyingi, atakuwa na mudagani wakuanzsiha hiyo kliniki…ila alitaka kama
ianawezekana aanzishe kidogo kwa ajili ya kuwasaidia akina dada wasiotulia,
unajau ukiwa an kitu kama hicho ukawapa ushauri akina dada,….inaweza
aiaksaidia, lakini sijamuulizia hilo limefikia wapi,…maaan kila tukiaonge naye
tuna kuwa na mengi ya kuongea, hata mengine unayasahau.
‘Hakuna tatizo lolote jingine aliwahi kukuambia…maana
umesema nyie siri zenu mnajauna….?’ Nikamuuliza.
‘Hakuna….hana tatizo jingine zaidi ya hilo la ndoa…na
ukisema siri…hakuna cha siri sana,tunaonega mambo ya kawaida, yeye ana ndoa
yake na mimi yangu, maswala ay ndoa ya ndani sana, ni siri ya mweney ndoa,
sizani kama ana tatizo kubwa…kuna siku aliongea kwasauti ya unyonge, niamuuliza
kuwa kuna tatizo gani….hakusema, alisema ni kawaida tu na yataisha….’akatulia
na mimi nilipoangalia saa nikaona niondoke
‘Nashukuru sana,nin ahamu sana ya kuongea na wewe na mama
yako…lakini muda hautoshi…ipo siku tutakuatana tutaongea sana….’nikamwambia.
‘Nisalimie sana ndugu yangu,na mume wake, waambie tupo
pamoja….’akasema huku akikimbilia ofisini kwake,na mimi nikapanda taksi
nakuondoka….
*********
‘Kazi zimekuwa nyingi sana, nimejaribu kuajiri wasaidizi wengi,
lakini cha ajabu, wengi wanataka kuniona mimi mwenyewe, nilikuona pale
ulipofika,lakini nilishindwa jinsi gani ya kukutana na wewe , …na nikamtuma
binti yangu akuage kwa niaba yangu, natumai mlione akidogo. Pale nahitaji
mpangilioa mwingine, na kama nitampata Yule binti niliyekuambia, akija huku
nitakuwa na ahueni sana,Yule akiwa apmoja na binti yangu, kazi zitapungua sana,
ukimuonamwambia namuhitaji sana…’akasema.
‘Nitamtafuta,….sijawahi kuongea naye kwa karibu,unajua yeye
ni docta na madocta kama hawo wana kazi nyingi sana,ukimuhitaji labda muda wake
wakupunmzika,….’nikasema.
Ndivyo ilivyo,hizi kazi za kusaidia jamii, kwa maswala ya
kiafya, maswala nya ndani ,yanayogusa nafsi, afya na utashi wa binadamu ni
magumu sana, yanhitaji muda,kukaa pamoja kuelezana, kiundani, na wengine hawawi
wawazi, sasa mpaka ujeumgundue inachukua muda sana…na muda hautoshi…’akasema.
‘Nilipopata upenyo tu, nikaoana nikuwahi …nashukuru sana nimekukuta,
naona kuna nusu saa ya kuongea na wewe, sijui kama itatosha, ….’akasema.
‘Hamna shida, mimi mwenyewe nilishapanga niondoke
kwanza,kwasababu nahitajika huko Dar, kuna kesi naisimamia,na niliondoka mara
moja kwa vile pia nilikuwa na yangu
ambayo ni muhimu,ya kuonanana na wewe ….’nikamwambia.
‘Na hilo ndilo limenifanya nije haraka,maana mimi nikianza
kuongea, nasahau mengine nakumbuka nilikuulizia kuhusu binti yangu, maana moyo
una wasiwasi sana kuhusu maisha yake na mumewe, kuna tatizo lolote juu yake…maana
kuja kwako huku,sizani kuwa ni kuhusu mambo yako tu…nahisi kuna jambo jingine,
hukutaka kuniambia?’ akauliza.
‘Kwani binti yako aliwahi kukuambia kuwa ana tatizojingine….la
kisheria, au ni yale ya yeye na mume wake,ambayo najua ni ya akwaida tu….?’ Nikamuuliza.
‘Hajaniambia lolote zaidi ya hilo la yeye na mume
wake,lakini moyo wangu unaingiwa na wasiwasi …….unajau kama mzazi, ukishakuwa
na watoto, hata wawe wakubwa vipi, kama kuna jambo utalihisi mwilini, nahisi
hivyo, nanimejaribu kuwasiliana naye, lakini simu yake siku mbili tatu hizi haipatikani,
nikaona nikuwahi, ….’akasema huku akiweka mguu mmoja juu ya mwingine.
‘Mimi sijui kama ana tatizo jingine, hajawahi kuniambia KUWA kuwa….lakini
hata kama ana tatizo lolote, mume wake ni mwanasheria, kama kuna tatizo mume
wake yupo hilo lisikutie shaka….’nikamwambia.
‘Mume wake yupo, lakini kama nihisivyo, mume wake anaweza
asimsaidie lolote, kama ni mambo hayo ya
kusigishana yeye na mume wake, hajaniambia kuwa hiyo hali imekuwa mbaya kiasi
gani….ila tu nakuomba sana,tena sana, hilo liwe juu yagu mimi na wewe, kama kuna
tatizo, nakuomba sana…mwanangu, unajau jinsi gani mzazi anavyojisikia kwa mwanae,
na mabinti zangu ni mapacha, ….mwenzake keshaniambia anataka aende huku akamsaidie
ndugu yake ,kama kuna tatizo….’akasema.
‘Mimi sizani kama kuna tatizo, kama lipo angelisha kuambia,….na
kama nilivyosema yeye yupo jikoni ,yupo kwenye wasimamizi wa sheria, kwahiyo
kama kuna tatizo atasaidiwa kisheria, ….mimi sioni tatizo hapo…na sijui kama
kuna tatizo lolote’nikamwambia.
‘Mimi ninachokuomba ni kuwa kama kuna tatizo, nakutegemea
wewe, ….sana sana, simtegemai sana mume wake, nilipokuona wewe nilishukuru
sana,…..tena sana, wewe sasa ndio tegemeo langu…’akaniangalia na mara akatoa
karatasi, ilikuwa imeandikwa mkataba…..akauangalia kwanza, alafu akasaini chini
yake, na kunikabidhi.
‘Huu ni mkataba ambao nautumia sana katika shughuli zangu,
wewe nimekuchagua kuwa wakili wa mtoto wangu, kama kuna lolote,….wewe
utamsimamia kiusauri hasa kisheria,….’akatulia na kuniangalia huku akiwa
ananikabidhi ile karatasi,mimi mkono ukawa mnzito kuipokea, nikatulia kwanza
akasema;
‘Kama kuna lolote wewe utakuwa mshauri wake, hasa mambo ya
kisheria….nakutegemea wewe….so zaidi na kwa vile wewe mwenyewe umesema hakuna
tatizo, mimi sioni shida kuwa naye kama
litatokea,..hatuombei hivyo…’akanikabidhi ile karati , zilikuwa nakala mbili,
ina maana moja niweke saini ya makubaliano na nakala anabakia nayo.
Hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi, na akili ikaanza kufanya
kazi, nikajiuliza kwanini huyu mama akimbilie huko, anahisi kuna nini, au
anajua jambo, nahataki kuniambia, nikasita kuichukua ile karatasi, nikamuuliza.
‘Nakumbuka uliniambia kuwa unapenda sana mtu mkweli…na mimi
hivyo hivyo, hebu niambie ukweli, kuna jambo gani unalihishi auu umelisikia, au…..?’
na kabla sijaulimaliz akuulizia sauti ikasikika kuwa sisi abiria tunaokwenda
Dar, tuingie kwenye ndege.
‘Hakuna ninalolijua, ….nahisia tu, huo ndio ukweli wenyewe,
labda kama wewe unajua lolote hutaki kuniambia,na kama hutasaini huu mkataba,itadhirikakuwa
kuna jambo unalijua ambalo unaogopa kuwa litakukwaza, ….hata hivyo ni mkataba
wa kawaida tu, kuwa umekubali kuwa wakili wa binti yangu, kwa mswala yake,….ila,
…hili ni kati yangu mimi na wewe…..tafadhali,’ akasema huku akiniangali
machoni.
‘Na kamaunajua kuwa hana tatizo basi wewe uwe msimamizi wake
tu, mshauri, maana sisi ni binadamu
huwezi jua, kwani hujafa hujaumbika,..tafadhali….’akanikabidhi kalamu na
ile karatasi.
Hapo akanitega, lakini hata kama ningelikubali na kuasaini
ule mkataba, haungeliweza kunifunga mimi kutimiza wajibu wangu. Nikaona
nijaribu karata yangu ya mwisho, nikasema;
‘Mimi ni wakili wa serikali,….sijawa wakili wa kujitegemea, ….kwahiyo
hilo litakuwa gumu, ila nitakubali kuwa karibu naye kiushauri ukihitajika hadi
hapo nitakapo kuwa wakili wa kujitegeemea..kwa hivi sasa nitfanya hivyo kuwa
mshauri tu,…., kama sehemu yangu ya ziada na hapa nandika hivyo kuwa itakuwa
mshauri wake tu kwa maswala ya kisheria,…nikasema na kusaini ule mkataka, na
kuandika maelezo hayo ya ziada chini yake.
‘Hata hivyo nashukuru sana,….sasa moyo wangu utatulia maana
najua binti yangu ana ndugu wakumsaidia, huko yupo ugenini, hana ndugu…mmh,….’akatulia
kidogo, kama vile kakumbukajambo, akasema kwa harakaharaka.
‘Yupo binamu yake mmoja, …huyo ndiye naweza kusema ni ndugu
yake wa karibu aliye naye huko, lakini tangu utotoni hawaivani, sijui kwanini, alikubali
kumtafutia kazi huko,….baada ya yeye kukorofishana na mumewe,… sikupenda kabisa
wakae karibu naye,.. huyu binamu yake ni nesi…wanafanana ukimuona…’akasema na
mimi sikuwa na muda tena, nikamshika mkono na kuagana naye,nikambilia ndani
huku, tukipungiana mkono.
‘Wanafanana ukimuona…ni nesi,ni nani huyu, mbona sijawahi
kumsikia, au…..?.’nikawa najiuliza kichwani na mawazo haya yakawa yakijirudia
mara kwa mara kichwani,…. lakini sikutaka kuumiza kichwa changu tena,
nikatuliza akili yangu na kufikiria safari yangu.
NB Nimeona niweke kipande hiki kidogo, kilichokuwa kimebakia katika
sehemu iliyopita, maana mambo manzito, lakini tutafika tu,..Insha-Allah.
WAZO LA LEO:
Udugu ,ujirani ni kitu muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Usivunje
udugu, ukajitenga, hasa pale unapijiona umefanikiwa, na mtendee mema jirani
yako,maana hujui katika maisha haya nani atakusaidia katika dhiki.
Naju kweli wapo wandugu hawabebeki, ni mzigo,na wanaweza
wakawa sumu katika maisha yako, lakini ni ndugu yako, ni vyema, ukajitahidi
iwezekanavyo kutokuwa wa kwanza kuuvunja udugu. Timiza wajibu wako,….Kwasababu zambi
ya kuvunja udugu, zambi ya ubinafsi haiishii hapo hapo, inaambukiza,inasambaa….
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Kazi nzuri mkuu, japamimi niseme kidogo!
Post a Comment