Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 29, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-7



Rose muda wake wa kuondoka ulipofika alijikuta akiwa kachoka sana, na alichofanya ni kuhakikisha kuwa katoa maagizo yote kwa mwenzake anayeingia na hakuishia hapo alikutana na mlizi wa siku hiyo kumpa maagizo yote, na baadaye akakutana na manesi wanaoingia siku hiyo kuwapa taarifa kuhusu huyo mgonjwa maalumu. Na alipohakikisha kuwa kila kitu kipo sawa akarejea pale alipolala yule mgonjwa na kumpima vipimo vyote, na alipofika kumwangalia usoni akajikuta akisisimukwa mwili mzima, …akadharau hiyo hisia kwani hakutaka kabisa hisia kama hizo zimjia akilini, hataki hataki, hawataki kabisa waanaume tena!

Akairudisha hali yake ya kawaida na moyoni akisema, `mmmh, sura kama ya …oh,….shiti…’ akajilaumu kwanini kajikumbusha mbali. Akainama tena wanaume…akainama kutaka kumsikilizia mapigo ya moyo kifuani kwani hakukiamini kipimo chake,…akasimama ghafla na kusema `at last’….hatimaye….wuwuuuu..’ akaangalia vifaaa vya kuangalia mapigo ya moyo na kutabasamu alikuwa anaona mabadiliko makubwa, kuoneysha kuna maendeleo mazuri na huenda mgonjwa huyo akaamuaka wakati wowote…

‘Lakini mabadiliko hayo nimeyaona muda mrefu lakini hakuna dalili yoyote…, cha muhimu ni kuwa anatupa matumaini maana ilifikia hatua tukajua huyu sio wa kuishi tena,…..’ akasema Rose akimkabidhi mwenzake.

‘Anaonekana bonge la `handsome’…hivi atakuwa katokea wapi nan i kitu gani kilimsibu, au ni mmojawapo wa wavuvi wageni waliopotea…au..hapana sidhani kama ni gaidi huyu haonyeshi hiyo dalili’ akasema Dakitari mwenzake akimkagua kagua…
‘Lakini shosti kuwa makini…Mhh, kuwa makini…usijali uhandsome wa hawa watu wote tabia zao ni moja…I hate them, unajua kuwachukuia hawa watu, basi mimi nawachukia ile basi….!..’ Akasema Rose, na mwenzake alimuelewa, ingawaje yeye alishukuru kwani ana mume wake sasa na..wanataraji mtoto..alimuonea sana huruma Rose, hata inapofikia hatu ahiyo ya kuhadithia maisha yake yaliyopita…!

‘Unajua Docta… , majangiri wote wapo hivyo, wakiwa katika mishemishe zao, hakikisha huchezi mbali naye, na humpi nafasi ya kutoka nje…akizindukana tu, simu polisi….’ Rose akamwambia , na kurudi kumwangalia tena usoni, na akajikuta akitabasamu tena, huku moyoni akisema, `whatever… all are the same…’ alijikutwa hana mawazo siku hiyo kwani alikuwa na kibarua kikubwa, kuhudumia wagonjwa na kila mara kuja kumwangalia huyo mgonjwa ana maendeleao gani, …na kila alipojiwa na mwazo alijaribu kutafut aakzi ya kufanya ambayo ilimsahaulisha hayo anayowaza. Hata hivyo alijiuliza sana, kwanini tangu amuone huyoo mgonjwa, akili yake imekuwa kiwaza maisha yake yaliyopita!

Tangu alipofika asubuhi alitaraji atapata muda wa kupumzika kidogo kabla hajaanza majukumu, lakini kilichomshangaza ni kukutana na bosi wake ambaye aliomba sana kwa mungu wake kuwa sikutane naye kwa siku hiyo ya kwanza ya kurejea kazini, lakini hakukuwa na jinsi kwani alitakiwa kujua kazi ipo au la…halafu hata baada ya kuwa na uhakika kuwa kazi ipo akajikuta akibambikwa kazi moja kubwa, ambayo ilihitaji muda wake mwingi kuwa karibu na huyo mgonjwa, kama dakitari na bado kama mlinzi.

`Eti wananipa na kazi ya ulinzi tena, huyu dakitarii kweli hanitakii mema, mimi nitatimiza wajibu wangu kama dakitari na hiyoo ya ulinzi nimewapa maaskari, of-course nitafuatlia kuona hawafanyi makosa ,lakini asitarajie eti nitashinda hapo na hata kulala hapo hospitalini….hiyo haipo kwenye mkataba wetu wa aira, kama hanitaki aseme, nisepe kimbele, nikauze vitumbua…’ akawa anaongea na rafiki yake wakati wanaondoka kwenda nyumbani.

‘Lakini nafikiri umemuelewa vibaya kwani nionavyo hivyo ndivyo ilivyo sizani kwamba kwa vile kakwambia eti uhakikishe unamlinda huyo mgonjwa asitoroke, ina maana ugeuke kuwa mlinzi wake…lakini unamuonaje huyo mgonjwa anafanana kweli na hawo wanaowaita majingiri sijui..au nasikia wana jina lao siku hizi…wanaitwaje vile…ma…magaidi..?’ akauliza mwenzake.

‘Kwani hawo magaidi wanaandikwa usoni, ni watu kama sisi… , lakini wana nyendo zao wana yao wanayopigania. Na watu hawa ni werevu sana wanachofanya ni kuzisoma tabia za mahali na watu wake halafu wanajifanya kama wao ni raia wema kabisa…kiasi kwamba mnakuwa hamna shaka nao tena, na wakiona kuna nafasi ya kufanya hujuma, wanaitumia, unasikia bomu limelipuka mahala usipotarajia kabisa….kwahiyo ndivyo ilivyo…, lakini nilivyomwangalia huyo mgonjwa kwa ujumla na hisia zangu hafanani na watu kama hao, anaonekana mpole, mrembo…yaani wewe hata akiwa kafumba macho unavutia kwelikweli…….’ Akasema Rose huku akiangali hewani kama anajenga hisia fulani.

‘Umeanza,…duh, mungu mkubwa, kukusikia leo ukisema hayo maneno, ama kweli kila jambo lina mwanzo na mwisho wake…naona kabisa akili ya kibinadamu ya kutamani wanaume imekurudia maana tangu yule nduli akutelekeze wewe na wanaume mumekuwa maadui utafikiri jamaa huyo alikaa kikao na wanaume wote duniani kupanga wakufanyie hivyo, …rafiki yangu huwa kila jambo hutokea kwa sababu fulani huwezi jua kwanini ilitokea hivyo, bahati yako haikuwa kwake, wewe angalia ,mbele kama utampata mwingine endelea naye, sasa wewe miaka mingapi unawagomea wanaume wote, hutaki urafiki au uchumba, ina maana umegeuka `mtawa’ shauri lako uzazi utaganda na….’ wakawa wanaongea na rafiki yake na basi walilopanda lilikuwa limeshafika sehemu yao ya kuteremka, lilikuwa basi lao la kazini na wakiteremka hapo huwa wanatembea kidogo kwa miguu kuingia eneo la nyumba yao waliyopangishiwa.

Rose alikuwa katoneshwa kidonda na rafiki yake , hakutaka kabisa kukumbushwa maisha yake yaliyopita, alikuwa keshafikia hatua kuwa yaliyopita yamepita agange yajayo, lakini kila alipokutana na mwanaume akamtamkia kuwa `anampenda’ ile taswira ya maisha yake ya nyuma humjia anakumbuka lile tukio kama vile limewekwa mbele yake na kufunikwa na kitambaa laini ambacho ukija upepo kinafunuka na kuyaona maisha yake yaliyopita….alifumba macho na kumbukumbu za maisha yake ya nyuma zilimrejea tena.

********

Ilikuwa siku ya sherehe ya kumaliza chuo cha Makerere, akiwa kashika shahada yake yakumaliza elimu yake hiyo ya udakitari na ilikuwa nia yake kuendelea zaidi na kufikia hatua ya juu, hasa akiwa kabobea katika maswala ya akili (Neurologist) na nyanja hii aliipenda sana na hata lilipotokea hilo tatizo lililomharaibia mpangilio wake wa kimaisha hakukata tama akawa anajiendeleza hadi akafikia kiwango hicho cha dakitari kamili, lakini lengo lake hasa ni kufikia kiwango cha kuitwa dakitari bingwa `specilist’

Alikumbuka siku ile wakati wakiwa na furaha na kila mmoja akiota ndoto zake kuwa sasa hatua muhimu wameimaliza kilichabakia ni kuingia kwenye jamii na kujichanganya kwa kutoa huduma na matumaini ni kupata marejesho mazuri ambayo yatawafanya maisha yao yawe mazuri. Kinyume na matarajio hayo wengi wao walijikuta wakipambana na mitihani mingi, ukizingatia kipato na kazii hiyo ngumu, na wengi walitupwa kwenye hospitali za serikali zilizopo mbali na mji, na kwenye mazingira magumu…na matokea yake wengine wakakata tamaa kabisa na kazi hiyo na hata kuamua kubadili muelekeo lakini hakuwa kwa Rose, kazi hii ilimkaa kwenye damu.

‘Rose kuna barua yako hii, nimeiona tangu jana, ina maana hukuangalia sehemu ya barua ,maana naiona kama imekua siku nyingi, au hukutarajia barua yoyote karibu!’ Rafiki yake akawa anaingalia ile barua kabla hajamkabidhi rafiki yake na kuendelea kusema ,`…. maana najua baada ya sherehe hii kila mmoja anachukua begi lake anaishia kivyake, huenda imetoka kijijini, hapana hii imetoka Marekani…sio ya inatoka kwa mchumba wako hii…au ndio ajira zinakujia mapema…’ akamwambia rafiki yake waliyekuwa wakichangia chumba.

‘Barua ya nini tena, …unajua meti, hapa akilini mwangu sihisi kitu, akili yangu haipo hapa, hata hiii sherehe ya kumaliza chuo hapa kwangu haipo akilini, mimi ninawaza ndoa yangu tu, maana huyu mchumba wangu alitaka kuwa anashuka uwanja wa ndege anaingia kwenye kufunga ndoa, …na imebakia wiki moja tu, na nilivyosikia kuwa kila kitu karibu kipo sawa, familia yangu wameshapanga kila kitu, nasikia huko nyumbani vigelegele vimeshaanza kusikika…sasa hapa nipo kama sipo’ akasema Rose

Rose akaipokea ile barua na kuiangalia akashangaa mbona mwandiko ni wa mchumba wake, na barua hiyo inaonekana ilifika wiki mbili zilizopita, kwa tarehe ile inaonyesha ilifika kipindi wakiwa katika mitihani migumu, …labda walimu waliamua kutotoa barua yoyote wakati kama ule, wakiwa katika mitihani hiyo, ili isije ikawaharibia mazingatio yao…labda…lakini tangu afike hapo itakuwa mara ya kwanza…na akashukuru kuwa ni barua toka kwa mchumba wake,…ambayo hatarajii kuharibiwa mazingatio yake… labda ilikuwa na maneno ya kumtakia maandalizi mema ya mtihani na ndoa inayokuja…akaishika na hakuwa na haraka nayo kuifungua, akasema moyoni barua kama hii inatakiwa unaisoma wakati upo kitandani umejipumzisha, haihitaji haraka, …kwani maneno mengi yatakuwa ya kimapenzi…na anamjua mpenzi wake anavyojua kuandika hayo maneno, unasoma huku unasisimukwa na mwili mzima…utafikiri mpo naye karibu …mnaonngea naye mmmh, akaguna huku akiiangalia ile barua….

‘Nitaisoma baadaye ,… wakati huu ni wa kupumzisha kichwa, kidogo, mtu uoge ujiande na huko mnakokuita kujirusha, mimi sina hata hamu ya kwenda huko ukumbini, lakini kwa vile ni siku ya moja muhimu ya kumbukumbu itabidi niende tu…maana nitawahadithia nini wazazi wangu ikizingatiwa kuwa wapo mbali na hakuna hata jamaa yangu aliyebahatisha kuja hapa kushuhudia sherehe hii, kwahiyo nahitaji kila hatua niiweke kwenye kumbukumbu zangu…na ni vyema nipate kumbukumbu sahihi kwa ajili ya kwahadithia wazazi wangu na hasa mchumba wangu…’ akasema Rose

‘Mhhh, mchumba wangu, mchumba wangu, unanikifu na hiyo kauli, utazania wewe tu ndio …lakini nakuonea wivu sana, maana siku hizi kupata mchumba nako kazi kweli…. , halafu ndio umpate na mfikie hatua ya ndoa ni jambo la kushukuru sana, wengi huishia kuzalilishwa na kupata watoto bila kuwepo kwenye ndoa, …hilo kwangu nalipinga sana, nataka mtoto anafaidi ndoa ya wazazi wake, anazaliwa anakuta wazazi wake wapo kwenye ndoa, na sio anakuja kukutana nayo….sijui unanielewa maana ukisema hivi watu wengine wanakuelewa vibaya, …lakini mimi ndio msimamo wangu….’akasema rafiki yake.

‘Sio msimamo wako, ni msimamo wa kila msichana, kila mwanamke, kuwa anaolewa, halafu wanapata watoto, sio wanapata watoto ndio wanaoana…lakini wengine inatokea kinyume chake, kwasababu sijui ni wanaume wadanganyifu au ni kujisahau au ndio huko kupimana kizazi…hata sielewei, lakini yote ni mtu na kili yake…hilo nakuunga mkono, hata mimi nilishamwambia mchumba wangu yote yatafanyika baada ya ndoa, na hili lilikuwa likimuumiza sana,…akija likizo anakuja akiwa na mambo ya kizungu-zungu, siunajua tena wenzetu hawo waliosomea nje, wanataka kila kitu kizungukizungu…mimi nilimwambia `no way’ hapa kwangu ni `ubantu’ kwa kwenda mbele, …’ akasema Rose huku wanaingia kwenye mabweni yao ya kulala...

‘Naona tuapte nusu saa ya kulala kidogo, halafu tuoge, baada ya hapo…nina wazo usivae kwanza, wewe lete nguo zako chumbani kwangu, tusivae kwanza tuchague nguo gani inafaa kwa siku ya leo,…nitakusubiri kwangu…’ wakakubaliana na wao walipata bahati sehemu wanayokaa ina vyumba viwili na varanda katikati, na bahati njema hakukuwa na wanafunzi wengi kwahiyo kila mmoja alilala kwenye chumba chake na kuchangia varanda…

Ilishapita saa moja na rafiki wa Rose hakuona dalili ya kutoka nje kwa rafiki yake, na hakumbuki kumsikia akioga, yeye alipopata usingizi kidogo na baadaye aliamuka na kuimwagia maji ,alipomaliza kuoga, aliingia chumbani kwake akawa anatafuta nguo za kumuonyesha mwenzake, na alipomaliza kwa vile waliahidiana kuwa Rose ndiye atakuja kwake, akawa anamsubiri…huku akitizama kitabu chake cha picha, akasubiri wee kimiya, akapanga vitu vyake na kuona ngoja yeye achukua baadhi ya nguo zake amwendee mwenzake chumbani kwake….

‘Rose vipi wewe , ndio maandalizi gani hayo, nimekumbia uje huku kwangu kwanza tukaguane wewe kimiya…aaah, tabia hiyo mimi siitaki…haya mimi nakuja huko kwako…’akawa anasema kwa sauti, lakini hakusikia mwenzake akijibu. Akashikwa na mshangao akaita kwa sauti `Rose, Rose…..’ kimiya, akafunga mlango wa chumba chake na kuelekea chumba cha rafiki yakke huku akiwa kaingiwa na wasiwasi, sio kawaida ya rafiki yake kuwa hivyo, wakiahidiana jambo yeye huwa wa kwanza kuhakikisha kuwa kalitekeleza, sasa imekuwaje, au ndio kapitiwa na usingizi…haiwezekani!.
Akafungua mlango wa rafiki yake bila hodi akiwa na hasira na wasiwasi…`wewe mwanamke mbona….’ Alishikwa na mshangao, na nguo alizokuwa kazishika mkononi zote zikamdondoka chini na kushika mdomo kuzua sauti,…lakini haikuwezekana, alijikuta akipaza sauti kwa guvu akisema akisema `heeelp..jamani help…..’

NB: Imekuwaje jaje…mmmh, nashindwa kuenedleza zaidi maana leo ni Ijumaa, natakiwa kumalizia kazi za siku, na sehemu hii nimeiandika harakaharaka leo , ili angalau kusiishe siku bila kuandika chochote, nahisi kuna makosa mengi mnisamehe kidogo….TUPO PAMOJA

Thursday, July 28, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-6



Docta Adamu alichukua kipimo chake na kukiweka kifuani kwa yule mgonjwa, aliskiliza kwa makini halafu akakiondoa, alipeleka kidole kwenye jicho la yule mgonjwa , akabenua mboni za macho yake akatizama halafu akamfunua shuka alilofunikwa na kumkagua maungoni, …akachukua kadi na kuandika maelezo halafu akamwambia nesi kuwa ampeleka huyu mgonjwa kwenye chumba cha uchunguzi na uwaite madakitari wengine tukutane huko…
Mgonjwa alipofikishwa kwenye chumba cha uchunguzi, madakitari wengine walishafika na kumsubiri docta Adamu ambey alitoa maelezo mafupi ya huyo mgonjwa na kila mmoja akapewa kazi ya kumfanyia uchunguzi kutokana Nyanja yake, na hiyo imekuwa kawaida yaoo hasa kwa madaktari waliofika hapo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
‘Kila mmoja alileta uchunguzi wake kwa dakitari Adamu , ambaye alitikisa kichwa na kusema kuwa ndivyo hivyohivyo alivyokuwa akizania, kuwa huyu mgonjwa ana `Naimonia’(pneinomia), na malaria nyingi,….kwahiyo inabidi aanze matibabu haraka….’ Akasema dakitari Adamu, na kaundika maelezo ya ni dawa gani apatiwe na maelezo mengine…
‘Lakini docta huyu mgonjwa kaletwa tu hapa, hana ndugu, na  hatujui hata jina lake, hilo kwenye kadi tumeamua kuandika tu, na waliomleta hapa wameshaondoka, sasa hatujui gharama yake atalipa nani…….’ Akasema dakitari mmojawapo
‘Kwasababu tumeshaanza kumfanyia matibabu hilo tutalijadili baadaye cha muhimu tufanye juhudi za kupambana na matatizo aliyo nayo, na je taratibu za kisualama zimechukuliwa, yaani polisi wanalijua hili, kwani kama kaokotwa …umesema wapi?’ akauliza docta Adamu.
‘Walimkuta ufukweni mwa ziwa Victoria, hawa na wavuvi na haraka wakajaribu kumzindua lakini hakuzindukana na wao walijua keshakufa, na juhudi za kumjua ni nani zilishindikana , wakatoa taarifa polisi, na polisi na hawo raia wakamleta hapa wakiwa na nia tukauhifadhi mwili wake wakijua keshakufa, hata sisi tulijua hivyo, na wakati tunataka kumchoma sindano ya…’ akasimama kidogo yule Dakitari akimwangalia yue mgonjwa kwa mashaka kwani yeye bado hakuamini kuwa bado yupo hai
Tuliona mabadiliko fulani mwilini kuonyesha kuwa bado yupo hai , nilipompima tena nikaona ni mzima, kwahiyo ndiyo tukakuletea taarifa…kwa ujumla hana ndugu… na polisi walisema kuwa waliona karatasi iliyokuwa na namba za simu, na namba hizo sio za hapa nchini…huenda ni za nchi za jirani, na hilo polisi wanalifanyia kazi…’ akasema yule dakitarialiyempokea huyo mgonjwa.
‘Sawa kabisa sisi kama tulivyosema tunatimiza wajibu wetu, na kazi kama hizi wakati mwingine unacheza pata potea, unaweza ukamtibua baadaye ukapata gharama zako na zaidi au ukakosa kabisa, kwasababu huyu ni binadamu hatuwezi tukasema tumwache tu mapaka kijulikane …kwahiyo tuendelee na akzi yetu kama kawaida, ila nawaombeni tena msipende kupokea wagonjwa kama hawa, wakiletwa waambieni polisi wampeleke hospitali za setrikali, tutampokea kama dharura, baada ya hapo inabidi tuwaarifu serikalini kwasababu gharama zake kama hazitapata mlipaji inabidi tuzipeleke serikalini ili watulipe, na unajua ufuatiliaji wake …tutamaliz amwaka hatujalipwa….’ Akasema Docta Adamu.
‘Sasa mgonjwa huyu inabidi tumakabidhi nani ambaye atahakikisha kuwa kila kitu kinaenda salama na uslama wake, asije akapona akatoroka, nani ambaye hana majukumu kwa sasa…’a akuliza docta Adamu.
‘Rose, hana majukumu kwa sasa, naona tumkabidhi huyu mgonjwa…’ akasema yule dakitari mwingine
‘Rose mwenyewe yupo wapi?’ akauliza Docta Adamu
‘Ametoka kidogo kupata chochote..’ akaavyo alivyombiwa,
‘Basi muiteni nimpe maelekezo yote …..’ akatoa  amri docta Adamu
Docta Rose, alikuwa ndio karudi toka likizo na siku ya kwanza ya kazini ukiwa umetoka likizo inakuwa ya kutegatega, kwani unakuwa hujakabidhiwa majukumu, na mwenzako, huwa naye anamalizia kazi zake alizokuwa kaanza nazo, na hapo nawe unapata nafasi kusalimiana na wenzako hapa na pale, ndivyo alivyokuwa kafanya Maua na kuwaaga wenzake kuwa anapata chochote kumbe yupo kwa shoga yake anapata yaliyotokea wakati hayupo naye kuelezea kuhsu likizo yake.
‘Nasikia kuna mgonjwa mahututi kaletwa hapa hospitalini na madakitari wote wapo huko wanamhudumia vipi wewe, mbona upo nje, umemsahau docta Adamu, hajabadilika, ujue ukiafanya maksoa kazi hauna na ukiitwa na yeye kuna mawili, kupandishwa cheo au kufukuzwa kazi, …hizo bado ndizo tabia yake , nikukumbushe kama umemsahau….’ Akamwambia shoga yake.
‘Nimsahau Bosi,, hata nikiwa likizo nilikuwa namuwaza yeye , hata nikisikia mtu ananiita jina langu nabakia kujiuliza isije katumwa na Bosi, ….’ Akasema Maua na kabla hajawacheka mara mlango ukafunguliwa.
‘Maua unaitwa na Bosi….’ Akasema nesi akiwa kashika sinia la madawa.
‘Mungu wangu nini tena, ndio nimefika leo, Bosi kajuaje,…” akasema Rose akiinuka haraka haraka kutoka nje.
 Rose ni miongoni mwa madakitari walioajiriwa karibuni, baada ya kumaliza masomo yake udakitari na kufanya kazi kidogo hospitali za serikalini na baadaye akapata nafasi hapo kama dakitari, na amekuwa mchapakazi mzuri, lakini mbele ya docta Adamu, huwezi kukosa kukosolewa, hana simile katika aina yoyote ya uzembe, hutaamini hata licha ya kuwa dakitari mkuu wa hiyo hospitali, lakini anaweza akaingia muda wowote hata usiku kufanya kazi na madakitari wengine.
Rose alipofika hapo alipenda sana uchapakazi wa dakiatri huyu na akaahidi moyoni kuwa atajituma kaam yeye kwani alikuwa na mipango ya mbeleni ya kuanzisha zahanati yake. Lakini kila alivyojaribu aliikuta kama kasimama wakati mwenzake anakimbia, kwahiyo anakijuta aanacwa mbali ajabu.
‘Huyu dakitari ana mapafu ya mbwa ina maana hachoki na kila kitu anakijua, ….mmh, kweli sidhani kama nitamuweza huyu na kweli anastahili kuitwa dakitari mkuu..’akasema Rose siku moja
‘Rose ukitaka ufanikiwe katika hii kazi yetu uhakikishe unajitolea, kwani kazi hii ni wito, na ili ujue vyema, inabidi uwe mwepesi kujifunza kitu kipya, uwe karibu sana na wagonjwa, uweze kuwajua vyema, usichoke, na usionyeshe dharau, yoyote kwako ni mgonjwa wako….na uwe mwepesi kusoma, kubukua kila kitu kinachohusu fani yako…tafuta kwanini,….hiyo ndiyo siri ya mafanikio…’ akakumbuka siku moja alivyoambiwa na dakitari huyu. Na akajitahisi mara kwa mara kufanya hivyo, lakini alijikuta akichoka kwani kila akimaliza zamu yake,  hujikuta keshachoka na sasa eti ajitolee kufanya kazi nyingine au ajitolee kufanya hili na lile…..oh, alijikuta anataka kuzimia, akasema kwanini nijitese, wakati mshahara ni ule ule….hapana, nitakuwa nafanya kadiri ya uwezo wangu..
Alikumbuka kuwa likizo hii alipewa kama `onyo’ ingawaje alistahili kupewa likizo yake ya mwaka, lakini kulitokea uzembe fulani yeye akiwa dakitari wa zamu, na adhabu yake ikawa ni kwenda likizo huku uchunguzi unafanyika na akirudi atakuta taarifa kuwa anaendelea na kazi au basi….na aliporudi likizo hii bado alikuwa hajiamini kuwa kazi ipo au ndio basi tena, na kurudi tena serikalini aliona hatapata maslahi kama hapo, na je hata hivyoo watampokea wakati aliondoka kienyeji….hata hivyo hakukata tamaa akijua kuwa yeye au wenzake hakuna aliyefanya makosa ni uzembe wa mngonjwa mwenyewe tu….sasa sijui ndiyo hivyo anaitwa kwa dakitari mkuu ili kupewa barua ya kusimamishwa au kuendelea na kazi..
 Rose alifika chumba cha dakitari mkuu, na kabla hajagonga mlango akasikia mtu akija kwa nyuma yake, na alipogeuka akajikuta ana kwa ana na Docta Mkuu, Docta Adamu, alimuona akiwa bado kweney vazi la kikazi…balaa …..anaonekana kakunja uso hii ni ishara mbaya , ngoja nimsikilize kwanza
‘Shikamooo bosi….’ Akasema Rose akiwa kashikwa na kigugumizi..
‘Usiniambie umerudi toka likizo na hutaki kuja kutoa taarifa…na ulikuwa wapi wakati wenzako tunahangaika kwenye chumba cha uchunguzi, unafikiri kwa namna hiyo utafikia malengo yako, kazi ya udakitari ni wito, kujituma, umeenda likizo umeshalemaa, sema kama unataka nikuongezee siku …na ujue zikiisha na kazi imekweisha..njoo ndani kuna kazi maalumu kwako ’ akasem Docta Adam, huku akimkaribia Docta Rose, akashngaa Bosi wake ananyosha mkono wa kusalimiana naye. Naye kwa wasiwasi akaonyosha mkono wake laini..
‘Bosi ndio nilikuwa ..nilitoka kidogo kupata chochote…siunajua tena nilishazoea kula…sasa kupoteza muda wa kula ..’ akasema Rose huku akijiumauma, na wakati huo akitikiswa mkono kwa ile salamu ya kiume, ya kutikisana mikono…aliposhikwa na ule mkono wenye nguvu na kutikiswa alisikia kama bega linataka kutoka…
‘Sikiliza kwa makini , kuna mgonjwa kaletwa hapa, na huu ndio mtihani wako wa kuendelea na kazi hapa, vinginevyo utarejea huko ulikoharibu na sizani kama utapokelewa, ….najua unalijua hilo…na ukiacha hapa hata cheti chao kitaharibika siunajua hilo sasa kazi kwako. Sikiliza kwa makini…huyu mgonjwa hajulikani ni nani…kuna habari toka vyombo vya usalama, kuwa kuna watu ambao wanatafutwa…usiniulize kwanini, kama ujuavyo nchi yetu bado inaandamwa na vita!
 Docta Adamu akawa anafungua mlango wa ofisini kwake huku anaongea na kusema `Sasa hatujui huyu kama ni mmojawapo wa hao wanaotafutwa au ni mtu baki, ila kaokotwa ufukweni, kwa taarifa za siri na iwe siri yako, huyu anaweza akawa mmoja ya watu wanaotafutwa, sasa, kazi kwako kuhakikisha anakuwa katika mikono yako, ujue ni nani, ujue anataka nini, ujue kilitokea kitu gani mpaka akafika hapa, na ole wako akitoroka…ukumbuke huo ndio mtihani wako wa kuamua kuwa unaendelea na  udakitari au unataka kwenda kula-kula nyumbani…hata hivyo nina barua yako toka huko ulikochafua, sijui kama…inasemaje, huenda unatafutwa, sijui…hilo huko halihusu sana,…lakini hata hivyo…ok wewe soma hiyo barua halafu utaniambia inasemaje nisije nikawa nakupa kazi kumbe huhitajiki tena hapa…
Rose alijikuta akiishiwa na nguvu, barua toka serikalini, wizara ya afya… ina maana wameshajua kuwa nipo hapa na huyu dakitari wangu keshanijua kuliko alivyopanga kuwa atafanya kazii huku anatafuta mwanya wa kwenda nje kuongeza elimu yake, ina maana …hapana haiwezekani, kama ni hivyo hatakuwa na maisha mazuri hapa kazini, ni bora arudi serikalini akawapigie magoti,….lakini hapana kwanini nirudi serikalini , ….siwezi kuogopa, lazima nipambane kijasiri, na siri ya kazii kama hizi ni ujasiri…akapiga moyo konde na kumfuata docta mkuu ndani ili pate maelezo ya huyo mgonjwa au na kupewa hiyo barua , na ili ajue moja kuwa ni hitimisho la kazi aui…….



NB. Haya haya, hapa ni uwanja wa madakitari, hawa ni watu muhimu sana katika kisa hiki, ...kutana na Dakitari Rose, mtaona makali yake kwenye kisa hiki. Tuendelee kuwepo
Ni mimi: emu-three

Wednesday, July 27, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-5



                                                         **********
Ilikuwa ni ndani ya basi la `Luxury Coach’ linaloelekea Arusha, Maua alikuwa kashikwa na usingizi na pembeniyake alikaa Maneno, na muda mwingi walikuwa hawaongei, ikiwa moja ya masharti yake, waliongea pale palipokuwa na kitu cha muhimu cha kuongea, kiasi kwamba hata Maneno alijisikia ovyo, kwani mtu aliyezoea kuongea ukimwambia akae kimiya, ni macho uyaambie yasione wakati yanaona na yamefunguka….lakini ilibidi afuate masharti, akijua masharti hayo yatayeyuka yenyewe moja baada ya jingine, akajifnya kaishiwa cha kuongea. Alichokuwa akikwepa ni kuongea jambo litakalo muuzi Maua, kwahiyoo kila hatua alijaribu kuwa makini. Alichoshukuru ni kuwa hatua ya kwanza ya mikakati yake imekubalika ya kumshawishi shemejii yake akubali wakabadilishe mazingira, hakuamini pale alimomba hivyo na baada ya kufikiri sana alisema sawa amekubali.
Maneno aligeuka kumwangalia shemeji yake na kumkuta akiwa kasinzia, kinyume na mwanzoni ambapo alionekana kuwa na mawazo na wakati mwingine machoni kulionekana dalili ya machozi, na hapa Manenoo alifikiria mbali, kuwa ina maana kweli mke na mume wanapendana kiasi hiki, mapaka mmoja akiondoka mwingine anatamani naye afe ili wakakutane huko ahera, aliona ajabu sana, akatamani naye ampate mke ambaye atampenda kama Maua alivyompenda Mhuja. `Nikipata mke kama huyu mbona nitashukuru sana, kwani hawa walionakana kupendana tangu mwanzo na sizani kama mapenzi yao yangefika mahali yachujuke, sidhani….’ Akajikuta akisema kwa sauti ndogo, kumbe Maua alihis kitu akafumbua macho na kumwangalia Maneno, na Maneno akatabasamu
‘Umechoka sana, lala tu, unajua tena hii ni safari ya siku nzima, na ukifika kule utakuwa na shauku ya kuangalia wanyama, na huenda usipate muda wa kulala….lala shemeji yangu usijali nipo karibu yako kuhakikisha upo salama…’ akasema Maneno na kweli Maua akafumba macho kurudia kwenye usingizi, na hapo Maneno akamwangalia Maua sura yake na hata vile alivyokonda , lakini urembo wake ulikuwa haufichiki, alitamani angemsogelee na kumbusu shavuni,lakini kwa wakati mwingine alikuwa amemuogopa hata kumgusa, akikumbuka pale alipomkuta jikoni kalala anatoa mapofu mdomoni,…
 Maneno hakuamini kuwa mrembo kama huyu angefikia hatua ya kutaka kujiua, eti kwasababu mume wake kafa, mbona waume wapo wengi wanaomtamani, wanaompenda….`siamini kuwa mrembo kama huyu aliamua kujiua , kuna kitu kimejificha hapa na nitakigundua tu, na nikigundua kuwa kipo kitu kama hicho, ole wao wale mawifi , urafiki utakwisha ...alishukuru sana jinsi madakiatari walivyofanya juhudi kubwa hadii kumuokoa maisha yake, alikumbuka pale yule dakitari alipokuja na kumuita pembeni.
‘Natumai huyu ni mgonjwa wako na mpo karibu sana, je wewe ni mume wa huyu mgonjwa…?’ Docta aliuliza, na kuanza kumfanya Maneno ashikwe na kimuhemuhe, maana ile kauli ilikuwa kauli tata, na haikuashiria mema, akashikwa na kigugumizi cha kujibu….
‘Mmmh, ni shemeji yangu, …vipi atapona do-docta, …eti docta natumai yupo hai….mume wake ni miongoni mwa wahanga wa Mv Bukoba, kwahiyo mimi nasimama kwa niaba yake..je kuna matumaini yoyote…naomba sana docta niambie ukweli …na fanya kila njia apone..’ akasema Maneno akiwa na wasiwasi
‘Siwezi kusema lolote mpaka sasa, imebidi tumfanyie upasuaji wa haraka, na …bado hali yeka ni tete, ndio maaana nilitaka kukujulisha hilo, kuwa tumechukua hatua hiyo bila kukuarifu, hatua na jinsi, kwani kulikuwa hakuna muda wa kukutana na wewe…tunachomba mtuelewe hivyo, ila kwasasa mnatakiwa mvute subira,… lakini matumaini yapo kwani ile sumu haijaasiri kitu ndani…hilo ndilo la kutia matumaini, mengine bado tunajaribu kufanya kila iwezekanavyo kuokoa maisha yake na….mengine yote yanategemea uwezo wa muumba..’ akasema Docta na kuondoka
 Maneo alibaki kaduwaa, ina maana docta kasemaje pale, kuwa yupo hai, au ndio bado wanataka kumfanyia upasuaji,…au …mbaona sijaelewa… akawa anajiuliza kwani wakati docta anaongea, yeye alikwua mbali , alikuwa akisubiritu kauli ya mwisho ya docta kuwa kafa au kapona, lakini hakusikia lolote kati ya hayo maneno mawili, alipoona docta kaondoka, akakurupuka mbio kumfua nyuma, lakini kabla hajamfikia akawa keshafunga ule mlango wa chumba maalumu…akajikuta anajilaumu kwa kutokuwa makini kumsikiliza docta…
‘Aaah , sasa nitawaambiaje jamaa zake…’ akafikiria halafu moja kwa moja akelekea kwenye chumba chenye simu na kumpigia shangazi yake, ambaye baada ya kupata taarifa hiyo tu, alikuja haraka hospitalini, kwani alishasikia kuwa Maua hayupo nyumbani, na haijulikani katowekaje, taarifa hii aliipata toka kwa wifi wa Maua ambeya alikuwa na zamu siku hiyo. Na shangazi alipofika tu wakawa wansubiria pamoja na baadaye jamaa wengine wakawa wanafika mmoja mmoja kwani walikuwa wameshapata taarifa , na ilipofika jioni taarifa ikaja kuwa Maua yupo hai na keshazindukana baada ya kufanyiwa huo upasuaji kwahiyo baadaye atapelekwa wodini.
                                                                     *******
  `Mimi sijanywa sumu….  Sikumbukikabisa kufanya hivyo….’ Hiyo ilikuwa kauli ya Maua wakati anahojiwa                                                           
‘Maua kwanini uliamua kufanya hivyo, wewe unashindana na mungu, kujiua ili iweje,,,mbona unaniabisha shangazi yako, mimi sijakufundisha tabia kama hiyo, nilikufundisha ucha mungu, ujasiri na subira wakati wa matatizo..sasa umefanya nini mwanagu…’ shangazi akawa kakaa pembani yake akimhojii kwa uangalifu, alikuwa akitaka kujua ukweli mapema.
‘Shangazi mbona mimi siwaelewi, mnasemaje…?,’ Maua aliinua kichwa na kumwangalia shangazi yake huku akiwa na macho ya kushangaa, akaenedelea kusema `…eti nimekunywa sumu…haiwezekani kabisa, mimi sijanywa sumu kabisa….nilitamanai kujiua mwanzoni, lakini siku zilivyokuwa zikienda, hilo wazo lilikuwa limeondoka, ninachokumbuka mimi ni kuwa nilikunywa kahawa ….na pale nilipomaliza  kuinywa ile kahawa mara nikaanza kusikia tumbo likikata sana, …nikapiga ukulele kumuita wifi, ….lakini sikuweza kupaza sauti sana, nikaita weee…kimiya…na tumbo lilipokata mara ya pili nikajikuta mwili mzima ukikosa nguvu, mara nikaona kizunguzungu na ….sikumbuki tena kilichofuatia kwani tumbo lilikuwa na maumivu sana…sikumbuki shangazi, na mimi sikunywa sumu kabisa….hilo nakataaa…’akasema Maua na kuwaacha shangazi yake midomo wazi…
Pembeni yake alisimama wifi mkubwa, ni mmoa wa dada zake Mhuja, na mdogo wake ndiye aliyekuwa na zamu siku hiyo lilipotokea hilo kasheshe, aliposikia kauli hiyo ya Maua akahamaki na kusema kwa sauti
‘Wewe umechanganyikwia tu, …sasa mbona dakitari kasema kuwa imegundulika kuwa umekunywa sumu,…. Sumu… , lakini bado haijagundulika ni sumu ya aina gani…tuambie ukweli tu ulitaka kujiua kwasababu ya akili yako ndogo….’ Akasema yule wifi…….
Maneno aliposikia hivyo huyo wifi akiongea kwa sauti akasogea karibu kusiliza nini kinaendelea
‘Hivi wifi yake yule aliyekuwa naye yupo wapi, mbona aliondoka na kumuacha mgonjwa peke yake, ….na …mimi nataka kuongea naye kwa makini ilikuwaje akaondoka, maana tulikubaliana kuwa mtu asiondoke..mnaona kilichotokea…’ akasema Maneno kwa hasira.
‘Hivi huyu ni mtoto mdogo, nani asiyekuwa na uchungu, sisi Mhuja ni kaka yetu, keshaondoka hatuwezi kabisa kumpata kaka mwingine kama yeye, yeye kama mke itafika sehemu atasahau hatimaye atapata mume mwingine, hivi ina maana sisi hatuna uchungu….kaka , damu moja, lakini tumekubali ukweli na tumemuachia mungu…sasa yeye anazidi mpaka, hatukatai kwasababu walikua naye karibu na tunasema watu wakioana wanakuwa mwili mmoja, lakini lazima tukubali ukweli, kuwa hata iweje , ipo siku mmoja ataondoak duniani, ama itokee bahatii muondoke wote au atangulie mmoja, ni swala la muda, hakuna mwenye maamuzi na mungu…kwahiyo mimi nasema toka leo, kama utaendelea na tabia yako hiyo, sisi hatutavumilia…cha muhimu ni kukubali ukweli, na kumuombea kaka yetu huyo apumzike mahala pema peponi, lakini sio kutufanya sisi tutaabike bure…’akasema yule wifi yao mkubwa.
Maneno alikuwa mbali akiwaza kwanini Maua kakataa kuwa hakunywa sumu, ina maana basi kama hakunywa sumu kuna jambo limejificha hapo,…au kuna mdudu mtu kaingilia katu…haiwezekani, …lakini labda inaweza kwa  kweli kuwa Maua alikunywa hiyo sumu akiwa kuchanganyikiwa na kasahau kuwa alifanya hivyo…akakuna kichwa kwa mawazo, kwani alikuwa akiwaza jambo ambalo hakulitaka kabisa liingie kichwani mwake na hakutaka kuweka wazo hisia zake, kwani kama ataongea hivyo anaweza akaanzisha uhasama usiofaa, na huenda kweli Maua alikunywa sumu bila kujijua kwa kuchanganyikiwa.
‘Jamani imeshaeleweka naona tumuache mgonjwa apumuzike, na hili swala liishie hapa hapa kwenye familia , lakini inabidi baadaye tukae kama familia tuongee vyema, mimi kama shangazi yake nahitaji maelezo ya kina kwani tulikubaliana sote siku ile kuwa tuwekeane zamu, …ndio yeye sio mtoto mdogo, lakini hali ilivyokuwa muliiona wenyewe, na nyie ndio mliokuwa wa kwanza kutoa wazo hilo,..na hii sio yeye tu inaweza kumtokea yoyote…kufiwa na mume sio mchezo kama mnavyofikiria, na inatokea watu kuzidiana katika kuweza kuhimili hiki kishindo, ni mtihani mkubwa…lakini kwanini huyu wifi aliondoka kwa kipindii chote hicho, je kama asingekuaj Maneno ingekuwaje?’ akasema Shangazi mtu.
‘Hiyo ilipangwa iwe hivyo, hata asingekuja Maneno kuja hapo na kumkuta katika hiyo hali bado angekuja mtu mwingine akamuokoa… siku yake ilikuwa haijapangwa na tusitake kutafuatana uchawi , wakati mwenye kosa tunamjua, ni yeye mwenyewe huyu wifi…mimi sitaki kuongea sana, lakini lawama zote ni zake mwenyewe na asijifanya hajanywa hiyo sumu, na kutaka kuanzisha mambo mengine ambayo hayapo, kabisa….tumuache apumzike na akili ikimrudia vyema anaweza akatuambia ukweli kama ni lazima, na sidhani kama polisi wana umhimu sana na hili jambo, kama mgonjwa wetu kapona, mimi naona yaishie hapa…
‘Hilo halina uhakika, lakini kiutaratibu lazima polisi wafanue uchunguzi wao ili wajue nini kilitokea na hatuwezi kuwazua kwa hilo…na kama hakuna ubaya , mimi sioni kwanini watu wawaogope polisi…’ akasema Maneno.
‘Kwanini hatuwezi kuwazuia kwa hilo , hamuwajui polisi wataanza kasheshe yao na kwuasumbua watu wasio na hatia…kwa sababu ya…aah, bwana mimi mtaniona nina roho mbaya lakini pale penye ukweli siwezi kuvumilia…najua hisia zitajitokeza kwa vile mdogo wangu ndiye alikuwepo siku ile na akafnya uzembe wa kuondoka, na yeye anaweza kufikiriwa vibaya…na kusababisha hilo, ….lakini mimi nitamtetea mdogo wangu kwa nguvu zote, mimi ninamjau sana mdogo wangu, katika watu wanaompenda wifi yao huyo ni namba moja…sasa mkianza kuchokonoa chokonoa mtaazua mambo yasiyo na ukweli, …hakuna mchawi hapa, mchawi ni wifi mwenyewe, aache hiyo tabia, sisi tuna uchungu kama yeye na huendazaidi yake yeye…’ akasema yule wifi mkubwa.
 Maneno hakutaka kuingilia sana hilo swala, lakini baadaye polisi waifuatilia kiundani na walipombana sana Maua , Maua sijui kwa kutokutaka matatizo zaidi alisema kuwa `inawezekana ilitokea hivyo kuwa alikunywa sumu bila kujijua lakini hakumbuki kabisa kufanya hivyo…’.na polisi walipoona hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kumbana yoyote, wakahitimisha uchunguzi wao na baadaye mambo yakanyamazishwa kiaina, lakini kichwani kwa Maneno hakuliacha hilo jambo liishe hivyo hivyo, aliliweka kichwani kuwa ni lazima atamuulizia shemeji yake vyema kuwa ni kweli alitaka kujiua na je ile kauli yake ya kukataa kuwa hakunywa sumu aliitunga baadaye au kuna kitu kinaendelea kati ya Maua na wifi zake, kwani kama hivyo kuna haja ya kuokoa jahazi haraka iwezekanavyo…
Siku moja baada ya Maua kuruhusiwa kutoka hospitalini , Maneno alimtembela kama kawaida yake, akawa anatumia ujanja wake wakuongea na kuchekesha mpaka Maua akatabasamu, na kweli kazi hiyo ya kuongea anaijulia, na kama hutacheka basi utafurahi na kama hutafurahi, utaongea na wewe…huyo alikuwa Maneno, mwenye maneno kweli.
‘Shameji unajua wewe ni jasiri sana, na tena urembo wanko huo ndio unakusaidia …na nina jambo moja kubwa nataka kukuomba, naomba sana unikubalie ombo langu…unajua ili akili itulie ili uondokane na mawazo na kama dakitari alivyopendekeza , inabidi …akili ione kitu tofauti..na mimi nimewaza sana na wazo kubwa likanjia akilini, niakongea na wenzangu ofisini, na kweli wakakubaliana na wazo langu, sasa ikabidi nifanye juhudu zote na kweli kila kitu kimewekwa sana, kinachotakiwa na kauli yako tu….sasa nakuomba unikubalie ombi langu hilo…unajua shemeji kuna wimbo mmoja unaimbwa hivi;
‘Nikubalie mama we, taratata…kauli yako nisikie taratata, taratata
‘Usipate taabu kwa ajili yangu eeee….taratataa…
 Akawa Maneno anaimba huku anacheza, na kwa jinsi alivyokuwa akicheza alimuacha shemeji yake hoii na kuanza kucheka…na kicheko hiki ni cha mara ya kwanza tangu msiba utokee, na hapo Maneno akakatiza na kubakia kushangaa, bila kuamini, hivi kweli naota au kweli Maua kacheka…akashukuru sana kimoyomoyo…na kuendelea kusema kimoyomoyo kuwa sasa mambo yanaanza kurejea katika hali yake,…halafu akatabasamu na kumsogelea shemeji yake halafu akachukua mikono yake na kumshika viganja vyake, alitamani kuvibusu, lakini akavishikilia kwa muda…
‘Tafadhali sana shemeji nakuomba sana unikubalie ombi langu hili…’ akamwangalia usoni,halafu akatikisa kichwa, alipoona shemeji yake kamwangalia machoni mara moja halafu akaangalia chini, yeye akaendelea kuongea kwa kusema ` hili ni ombi letu, kwani sikulipitisha mimi mwenyewe, na tumeona hii huenda itakuwa heri kwetu na kwako na huenda ikasaidia kukutuliza moyo wako. Tunakuomba sana, …hasa mimi ninakuomba kuwa ili uondokane na mawazo yako, ambayo yamefikia hadi hatua ya kunywa sumu,…unajua shemeji hiyi ni hatua ya …lakini natumaini hilo limekwisha , sisi tumeonelea kuwa inabidi usafiri kidogo, ubadili hali ya hewa, ubadili mazingira kidogo…na kusafiri huku tumeonelea kuwa twende ukaone mbuga za wanyama, Ngorongoro…
Maua  akapanua mdogo kwa kushangaa, kama kuna kitu ambacho alikitamani katika maisha yake mojawapo ni kutembelea mbuga za wanyama na hili waliwahi kuongea na mume wake, …alifika hapo lile tabasamu la mdomoni likayeyuka,..lakini baadaye akawaza na kusema, ilimradi kaamua kuondoa mawazo na kujaribu kukubali ukweli atakubali ombo hilo , akasema
‘Sawa, kama mumeshapanga kila kitu, hutegemei mimi nikate , ..au mlitarajia nini kama mliamua bila kunishirikisha, sawa nitashukuru sana kuwemo kwenye hiyo safari,… sawa nimekubali…’ akasema na kutabasamu, na Maneno akaruka juu na kusema `yessss’ …akamsogelea shemaji yake na kumkumbatia, ingawaje shemeji yake hakunyosha mikonoo alikuwa katulia tuliii, mikono yake kaionyosha chini, huku anamshangaa shemeji yake…na hapo Maneno akamwachia haraka kama vile kagutiliwa na kitu na kusema `samahani sana shemeji, …ni raha ndiyo imenifanya niwe kama mwehu, raha kukuona umerudi katika hali yako…

‘Nimekubali kwa masharti…..’ akasema Maua, huku machozi yakimtoka, na kumfanya Maneno aingiwe na wasiwasi na kuwaza hayo masharti ni ya nini na atayaweza kweli......

NB, Jamani mniwie radhi, kwani umeme, foleni na uwajibikaji ofisini vinanikwaza kushindwa kutimiza wajibu wangu...natamani sana kuipeleka hiki kisa haraka , ikibidi kila siku, lakini wapiii...Nawaomba msichoke kusubiri, nitajitahidi iwezekanavyo...TUPO PAMOJA DAIMA


Ni mimi: emu-three

Monday, July 25, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-4



 Maneno akiwa ofisini kwake akili yake ikawa inakwazwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, alishindwa hata ashike lipi aache lipi, hata kazi yake ilikuwa nzito! Akakumbuka kuwa jana hakupata muda wa kumuona shemei yake kwasababu haikuwa zamu yake, na pale mezani alikuwa na kazi nyingi za kiofisi ambazo alitakiwa kuzimaliza, lakini kila akijaribu kutuliza mawazo alishindwa kufanikiwa, pamoja na kumuwaza rafiki yake kuwa ndio basi tena, mwezi na siku kumi na tano imeshapita tangu lile tukio, lakini bado akili zao zilikuwa hazikubali.  
Maneno alijitahidi sana kufanya kazi za watu za ofisini ili angalau azipunguze, lakini moyo wake ukawa unaambaa-ambaa kwenye ndoto ya jana, ndoto ambayo ilimkubusha mengi, ndoto ambayo ilimkutanisha yeye na rafiki yake, hutaamini hilo lakini wakati mwingine marahemu anaweza akakutokea akakumbusha umsaidie kulipa deni aliloacha, kwani huko anateseka na ukilipa anakutokea na kukushukuru … na Maneno alitokewa na rafiki yake alikimkumbushia asisahau urafiki wao, na kumuongezea kauli ambayo ilimkaa sna moyoni, na Maneno akawa anaikumbuka mara kwa mara, kuwa hata kama kasafiri mbali, isiwe ndio sababu ya kumsahau mkewe, kwani akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli.
Alipoisikia kauli toka kwa rafiki yake kwenye hiyo ndoto, akataka kumuulizia, kwanini anasema hivyo wakati yeye na familia nzima wapo pamoja na mkewe? Lakini kabla hajaweza akumuulizia hivyo na kupata `la kwanini’ mara akazinduka toka usingizini, …. Kwa hali hii akawa anajaribu kuangalia wapi kafanya vibaya, au ni ndoto tu. Akawaza sana tangu rafiki yake aondokea kuwa alifanya vibaya kinyume na urafiki wao, lakini hakuona kosa alilofanya, hivyo akaichukulia kama ni ndoto tu ya kawaida na labda ni  kwa vile alikuwa akimuwaza sana rafiki yake  huyo inawezekana ndio maana akamuota.
 Hakutaka kumhadathia mtu  yoyote ile ndoto, hasa alipoaina haina ujumbe muhimu kwake, kwani kila kitu alikitimiza…`hiyo ni ndoto tu ya kawaida ….’, ila aliona kuwa bado ana kazi kubwa ya kumhudumia mke wa rafiki yake  na huenda huo ujumbe ulikuwa ukilenga huko, na kama ni hivyo aliahidi moyoni kuwa atajitahidi sana kuhakikisha hilo linafanyika ili roho yay a rafiki yake huko ulipo, ipate kustarehe …huko mbele ya haki kwani huo ndio urafiki wa kweli…..
Ilishapita mwezi na kitu sasa tangu lile tukio kubwa litokee, watu wengi walikuwa bado hawajaamini kuwa ndio imekuwa hivyo…hasa wale ambao jamaa zao hawakuonekana kabisa, kila mara wanadhania huenda jamaa zao wakatokea, labda walinusurika, , labda siku hiyo ya safari hawakuwepo humo ndani…ni mawazo ya kibinadamu kwasababu binadamu hana uwezo wa kuona ghaibu lakini kwa kipindi chote hiki kama alikuwa hai angeonekana au hata kutoa taarifa. Maneno akaguna alipowaza hivyo akikumbuka ile hali aliyoiona siku ile alipoenda kuhakikisha kwa macho ayke mwenyewe, kwa hali kama ila alikuwa na uhakika kuwa rafiki yake keshapotea, hayupo tena duniani.
Kila alipojaribu kushika kazi akili yake ilikuwa haitulii, na mara akamkubuka shemeji yake , jana hakuweza kupitia nyumbani kwake kwasababu alikuwa kabanwa na kazi nyingi za ofisini, na kwahiyo leo kwa vovyote inabidi apitie kidogo, kwani itakuwa anakiuka masharti aliyowekewa na rafiki yake kuwa kila siku ahakikishe anampitia shemeji yake na hata chakula ahakikishe ana kula hapo nyumbani, na alijitahidi kufanya hivyo, ila kwasababu ya hilo tatizo na kuwa shemeji yake ailikuwa hawezi hata kupika kwa jinsi alivyiathirika na huo msiba, ikawa siku moja moja hafiki, ila aliahidi moyoni kuwa atajitahidi  kwa siku zote kwa kadri yauwezo wake awe anamhudumia shemeji yake hadi hapo kitakapojulikana.
`Hadi hapo kitakapojulikana, sitaki kulianza hili mapema, lakini moyo wangu unatamani iwe hivyo, mmmh, wakati bado huenda rafiki yangu ..hapana haiwezekani katika ile hali haiwezekani, atakuwa keshatangulia mbele ya haki..’ akajikuta akisema kwa sauti.  Na hapo kumbukumbu za hali aliyoikuta kule Mwanza siku ile zilimjia kichwani, jinsi alivyoiona ile hali na kwa yoyote angejua tu kuwa kama jamaa yako hakuwepo miongoni mwa yale maiti basi keshaliwa na samaki, na hata kama ungebahatisha kuuona mwili wake, angeukuta haupo kamilifu, angelikuwa kaharibika sana na baadhi ya viungo vitakuwa havipo….hapo tukio zima la siku ile likaanza kumrudia tena akilini jinsi siku ile ilivyokuwa.
                                      ****
Baada ya lile tukio kikao cha wanafamilia kilikutana na Maneno alialikwa kwa vile ni rafiki wa karibu, na yeye aliwakilisha taarifa ya kutoka kazini kwao kuwa wao kazini wamewatumia wafanyaakzi wao wa kule kufuatilia kwa karibu, lakini hawakugundua lolote, kwahiyo wanatka kusikia wanafamilia wanasemaje. Taarifa hiyo alipoifikisha kwa wanafamilia hawakuipokea kwa mikono miwili wakataka mtu atoek hapa Dar, akaone kwa macho yake, na kutokana nah li ilivyo, walimkatalia kabisa mke wa Mhuja kwenda huko, hasa kwa taarifa zilizopokelewa kuwa watu wamejaa, na hali ilivyo hapo inataka mtu mwenye moyo wa ujasiri kuihimili.
Wanafamilia walijadiliana wakaona wamtoe mtu wa familia aende huko, bsi Maneno akasema ili kuondoa shaka yeye ataondoka kwenda huko haraka iwezekanavyo, ingawaje kule wana ofisi na wana wafanyakazi kama yeye, na wanamjua sana Mhuja na wamefuatilia kwa karibu na wengine walihusika hata kuwepo kwenye kikosi cha uokoaji, alkini hawakuweza kumgundua au kuona dalili yoyote ya kuwepo kwake, kwahiyo wana imanai huenda ni miongoni mwa wale walioshindwa kabisa kutoka ndani ya kile chombo na kama alitoka basi huenda kakumbwa na ajali nyingine.
Kesho yake Maneno akafunga safari akiwa kapata baraka za ofisini na bahati nzuri alipata nafasi katika ndege ya ejshi ambyo ailikuwa inaeleeka huko kwahiyo alifika haraka pale Mwanza na alipofika tu hakupoteza muda, moja kwa moja akaelekea eneo ambapo maitizilizobahatika kuopolewa zilikuwa zimehifadhiwa, na hata akaonana na wafanyakazi wenzao ambao walimhakikishia kuwa wao wamepitia kila maiti na wamepitia kila eneo na wao walibahatika kuwepo kwenye kundi la waokoaji , lakini hakuna kilichopatikana
Maneno hakutosheka na hizo taarifa akaanza kukagua maiti zote, akatoka hapo akaelekea sehemu ya kumbukumbu za majina kuhakiki kuwa kweli aliwahi kusafiri siku hiyo, na kweli aliliona jina lake kwenye yeye ni miongoni mwa watu waliopata tiketi mapema kabisa, akaangali amajina ya watu waliotambulikana na wale waliotoka hai hakuona jina la rafiki yake huyo, akaanza kukata tama, akajadilian na marafiki zake na hatimaye walifikia muafaka kuwa huenda mfanyakazi mwenzao huyo ni miongoni mwa hawo waliopotea ndani ya maji.
Kwakweli kila hali ilivyokuwa hakukuwa na dalili yoyote ya kupatkana mwili mwingine ukiwa na hali nzuri, kwani kila mwili uliopatika kwa siku ile ulikuwa umeharibika vibaya, umeshanyofolewa na samaki…na haushikiki, na hata serikali ilikuwa imeshasitisha lile zoezi la uokoaji kwa kupitia kwa raisi mwenyewe, na raisi kipindi hicho alikuwa Mkapa. Basi Maneno akawa hana jinsi alijitayarisha kurudi nyumbani kutoa hiyo taarifa…
Siku niliporudi wanafamilia wote walikusanyika uwanja wa ndege waliwa wanajua huenda karudi angalau na mwili wake, lakini lipoonekan mwenyewe, kila mmoja alijikuta akibibijikwa na machozi, akakutana na na wanafamilia na kutoa hiyo taarifa aliyoiona huko, na ikawa haina jinsi ni kutangaza msiba, na kila mmoja akawa anatafuta jinsi ya kumfahamisha mke wa Mhuja, na kazi hiyo ikamuendea Maneno ambay ndiye aliyekuwa karibu sana na shamaji yake.
‘Niambie ukweli shemeji , …umeshindwa kuibeba maiti ya rafiki yako …kwasababu imeharibika au unataka kuniambia nini…au mimi najua kabisa mume wangu hajafa nina uhakika huo, msiniambie kitu…’ akaanza kusema Maua hata pale alipofahamishwa jinsi ilivyo huko Mwanza hakuamini hilo, alichofanya nai kumrukia Maneno na kuanza kumpiga mingumi akisema huyo aliyeenda hakufanya juhudi za maana, na huenda kaiona maiti yake imeharibika akaogopa kusema., …na akwa anaongea maneno mengi…lakini wote walijua ni kihoro cha kufiwa, itachukua muda kitaisha. Basi msiba ukatangazwa na wanafamilia wakakutana na ikabidi mke wake aambiwe akae eda kwa mujibu wa taratibu, lakini hakukubali kabisa, ila aliposhurutishwa na wazee ikawa hana jinsi akakaa shingo upande…..na kila mara ilikuwa ikimjia sura ya mume wake, na alipopata usingizi akawa anamuota yupo naye.
`Maua maisha haya ya kupanga nyumba sio mazuri, tukianza kupata watoto, itatuwia shida , naona tuanze kujenga kwanza kabla ya kufikiria watoto, au unasemaje..’akaulizwa na mume wake.
‘Kwani wewe Mungu, unasema hivyo, unajuaje utapata watoto wakati gani ni bora tuzae mapema, ili hata mmojawapo akiondoka duniani aache mbegu’ akasema Maua, na hapo ukaanza ubishi kila mmoja akidai lake, na mara Mhuja akakasirika na kutaka kuondoka, na Maua akawa anambembeleza mume wake asiondoke, lakini haikusaidia kitu, hata akawa aanajiuliza ina maana ubishi huo mdogo tu ndio unaomfanya mume wake azire na kuondoka, akaamua kutoa nje kumfuatilia, alipofika nje akamuona mume wake anaondoka kwa kasi na huku kuna gari linakuja kwa kasi, lakini ilivyoonekana mume wake alikuwa halioni.
‘Mume wangu hatari, angalia gri hilolinakuja, utagongwa…’ akawa anasema kwa sauti, lakini ilionekana mume wake hamsikii akawa anakwedna tu na lile gari likamfikia mume wake na hapo Maaua hakutaka kuangalia hilo gari likimgonga mume wake akageuza kichwa huku akisema `jamani mume wangu anagongwa na …akiwa amegeuza kichwa kutokumwangalia mume wake na huko alipogeuzia kichwa alikuwa kasimama shemeji yake Maneno ambaye alikuwa akimcheka kwa dhihaka na kusema
‘Unaona mume wako alivyo mbishi,, nilikuwambia mimi ndiye nakufaa kukuoa sasa angalia kagongwa na gari, humuoni tena ng’ooo’ alisema Maneno.
‘Hapana hajagongwa, hapana wewe una roho mbaya, ….wakati anayasema haya akawa anageuza kichwa taratibu ili ahakikishe kuwa kweli mume wake ahajagongwa, na alipogeuza kichwa vizuri, ….ooh, kumbe ilikuwa ni ndoto, akajizoa zoa na kutoka nje akiwa na nia ya kumuona mume wake…akakuta kweupe, watu wanapitapita mabarabarani, wengine wakiwa wameshikana na waume zao , wengine..na wapenzi wao, yeye hakuamini kuwa ndiyo aliyempenda keshaondoka, hatamuona tena duniani, hakuamini hilo, akaingia ndani akavaa nguo, nia anataka asafirihadi huko Mwanza, akahakikishe mwenyewe kuwa kweli mume wake kafa!
‘Hapana lazima yupo mahali, sikubali mume wangu hajafa…
                                ***************
Maneno baada ya kuona akili yake haitulii vyema na kwa kiasi kikubwa alikuwa akimwaza shemeji yake ambaye kila siku hali yake inazidi kuwa mbaya, anakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, anazidi kukonda…na bado akili yake hataki kukubali kuwa mume wake keshatangulia mbele za haki! Aliamua atoke akamuone mara moja, ingawaje ilikuwa sio zamu yake ya kukaa naye, kwani ilikuwa imefikia mahali wafanye hivyo kupangiana zamu ya kumlinda,…amechanganyikiwa kabisa, na akibaki peke yake lolote linaweza kutokea, kwa kufikia vile akaona akimbie akamuone mara moja na kuona kama kuna kitu kinahitajika, halafu arudi kazini, akaaga na kuondoka,…
 Aliingia ndani ya gari ambalo alikuwa akiiendesha Mhuja, na kila akiingia ndani ya gari hilo huwa anamua rafiki yake kaka pembeni kimawazo, gari hilo lilikuwa limenunuliwa kikazi na Mhuja ndiye alikabidhiwa, na kwa kuondoka kwake ikabidi Maneno apewe yeye! Maneno aliwaza sana kuhus maisha , kuwa maisha kweli ni safari, leo upo hapa duniani kesho haupo, …kama mchezo tu, na huwezi hata kuamini, …aaah, kweli inatakiwa kujiandaa wakati wote, huwezi amini rafiki yangu keshaondoka, na kaacha mke mzuri, hawajazaa, hawajafaidi maisha ya ndoa, na walikuwa na mikakati mingi ya kimaisha, lakini yote imesimama, na sasa inategemea mke wake atakavyojipanga….
‘Mke wake..’ sio mke tena, …kaondoka na huenda akapata mume mweingine, ukishakufa kila kilichobaki duniani sio chako tena…hivi ndivyo ilivyo, naogopa hata kuoa, maana nikioa nitakufa wenzangu watamchukua mke wangu, mali yangu…mmh, haya maisha jamani…kwakweli shemeji ni mzuri hatakawia kupata mume mwingine, na …inibidi nimlinde sana kuhakikisha kuwa nimelinda urafiki wangu na rafiki yangu, hata kama ataamua kuolewa na mtu mwingine, nitahakikisha atakayemuoa hawezi kumpa shida, na ikibidi …na ikibidi…siwezi kumlazimisha,…mmh, kwelinampenda sana tangu siku nilipitambuslishwa na rafiki yangu, nilitamani sana kuwa angelikuwa wangu, lakini kila ninpofikiria namuoa sasa kama dada yangu….
 Mawazo na mwendo wa gari na kwasababu kulikuwa hakuna foleni alijikuta keshafika nyumbani kwa Mhuja kwa muda mfupi tu na hata bila kujitambua…alipofika akaangza huku na kule kama atamuaona yule ambaye ni zamu yake kukaa na huyo ambaye sasa anaitwa `mgonjwa’ anakitwa `mjane’ akasogea kwenye mlango na kupiga hodi akashngaa kuona kimiya, huyu anayemhudumia `mgonjwa ‘ kaenda wapi na shemeji yake, ina maana leo kaweza kutoka kidogo, kama ni hivyo mbona tutashukuru sana, aua kazidiwa kapelekwa hospitalini, lakini wasingefanya hivyo bila kumtaarifu…akajaribu kufungua mlango akaona umefungwa kwa ndani labda, akajipapasa mfukoni, kwani alikuwa na ufunguo wa akiba aliokuwa kakabidhiwa na rafiki yake.
‘Ufungu huu ni akiba, kaa nao shemeji yako anaweza akapoteza funguo zake mkapata shida au unaweza ukafika shemeji yako hayupo unaweza ukaingia ndani au likatokea tatizo na unahitaika kumsaidia shemeji yako, na huna ufunguo,…huu unaweza ukakusaidia..’ aliwaza jinsi gani rafiki yake alivyokuwa akiotea mambo, kwani kila alichoongea hutokea na kusaidia katika hali usiyoitegemea.
‘Shemeji upo wapi, …wifi wa sheemji upo wapi!?’ akaanza kuita lakini kulikuwa kimiya…na hapo nywele za Maneno zikawa zinasisimuka na moyo kwenda mbio, hii ikionyesha ishara ya kitu ambacho sio kawaida, hali amijenga mwilini mwake, akihisi hivyo kuna jambo… na alipotizama pale varandani akaona begi la safari, limebagwa chini, …akalifuata na kulingalia kwa makini , alilikumbuka kuwa ni la shemaji yake, alinunuliwa kipindi fulani alipokuwa akisafairi kwenda kwao kusalimia…alilichagua mwenyewe wakiwa watatu, yeye Maneno , Mhuja na mkewe…akatabasamu alipokumbuka siku ile, maana alipolichagua ili bidi wamcheke, kuwa anachagua begi la kijijini…lakini yeye aliling’ang’ania na ikabidi anunuliwe hilo hilo…akaliinua na kuliweka juu ya kochi, hakutaka hata kulifungua kutizama kuna nini cha zaidi… , akajiuliza ina maana shemeji yake alishajiandaa kuondoka , na kama ni kuondoka alikuwa na safari ya wapi, na wifi yake yupo wapi, ambaye ndiye mwenye zamu ya kuwa na huyo mgonjwa, mbona hayupo ndani…watakuwa wametoka pamoja nini…
Akaita mara nyingi lakini hakuona dalili yoyote, mwishowe akaamua kukagua nyumba nzima, alianzia chumbani kwa shemaji yake akakuta kitanda kimetandikwa vyema kabisa, akatoka mle akaingia bafuni akakuta hakuna mtu chooni , akaingia chumba cha wageni ambapo alitegemea kumkuta wifi wa shemeji yake, hakuna mtu, hakuna mtu…. akarudi varandani akatulia kuwaza hawa watu lazima wametoka…kama simu yangu ingekuwa nzima ningewapigia, akalaani kutokulishughulikia kupata simu za mkononi,….lakini haiwezekani, kama amjuavyo huyo shemeji yake amekuwa hataki kabisa kwenda kokote, hatiki nje kabisa..labda kawa na hamu ya kutoka nje, lakini hili begi je, ni la nini…akaona muda unakwenda, akasema ngoja niingie jikoni nipate chochote kama kipo…..akatembea hukuanatizam huku na kule akafungua mlango wa jikoni…mamamamamama… akapata mshituko wa moyo..
Alijikuta akipiga kelelele za `mamamamam….’ Halafu akaingia ndani na kuinama pale skafuni
‘Wewe shemeji vipi mbona upo hivyo…’ alimkuta shemeji yake yupo sakafuni kalala na mapofu yanamtoka mdomoni…Mara moja akili yake ilikwenda haraka kuwaza hivyo kuwa kanywa sumu , na alichofanya ni kukimbia kwenye jokofu na hapo akakuta maziwa akamimina kwenye kikombe, akarudi haraka na kuanza kazi ya kumnywesha, ilikuwa kazi kubwa, kwani meno yalikuwa hayafunguki , ikabidi achukue kijiko na kupanua yale meno kwa nguvu, na baada ya kazi nzito akafanikiwa…alipohakikisha yamepita maziwa ya kutosha, akatulia kuwaza afanyaje nini tena, alipogeuka kuangalia pale juu ya meza linapowekwa jiko ndipo akaona kikombe cha chai, au kahawa…akainusa, haikuwa na dalili yoyote ya harufu ya sumu…lakini alijua kabisa huenda sumu hiyo ilikuwa imechanganywa na ile chai, …auakameza vidonge na kwanini kafikia hatua ya kujiua….
Alijaribu kwamwangalia mapigo ya moyo, …duh, hakuona dlili yoyote ya uhai, mungu wangu, ina maana tumempoteza mtu mwingine tena, haiwezekani, akamwiinamia na kuweka sikio karibu na mapigo ya moyo, kulikuwa kimiya…keshakufa masikini ya mungi…Oh Maneno akasimama na kuanza kupiga kurukaruka, halafu akasimama mwili mzima ukaanza kumwishia nguvu..halafu baadaye akapiga moyo konde na kusema sio muda wa kukata tamaa, hata kama keshafariki afadhali wakajulie huko huko hospitalini..wazo la kuwa keshakufa hakulitaka kabisa liingie akilini mwake …hapana usife shemeji, kwanini ukimbilie kujiua , hujui tupo wengi tunaokupenda…wazazi wako wanakuhitaji sana, jamaa zako, na mimi mwenyewe nipo kwa ajili yako..oh, usife Maua ….akajikuta akilia kama mtoto mdogo
 Aliona ni heri ampigie simu dakitari wao wa kazini aje haraka, lakini alipowaza zaidi na kujiuliza zaidi kuhusiana na swala la sumu akaona ni vyema amkimbize hospitalini,huenda hajafa kapoteza fahamu tu, na kama kanywa sumu ambayo ni mbaya sana, huko hospitalini wanaweza wakafnya juhudi hata za kumfanyia upasuaji na huenda wakamuokoa maisha yake,…akaanza kazi ya kumbeba, ilikuwa kazi nzito kweli na hata alipomfikisha kwenye gari alikuwa yupo hoi kwani ulikuwa mzito na hali ile ilimfanya Maneno ahisi mbali kuwa huenda alikuwa kabeba mwili usio na uhai….akaondoa gari haraka hadi hospitaini na huko akapokelewa na kuingizwa chumba maalumu cha uangalizi maalumu…na hapo akapumua kidogo, kwani kule kupokelewa na dakitari …halafu wamkimbize moja kwa moja kwenye humba maalumu, akaona ni bahati, siunajua tena…
Sasa ikawa kazi ya kutafuta mawasiliano, ukumbuke kipndi cha 1996-7, simu za mikononi hazikuwa nyingi sana, na waliokuwa wakitumia ni wachache , kwahiyo hata ukiwa nayo unaweza uakapata shida ya mawasiliano, zilikuwepo lakini watumiaji waliobahatika kuwa nazo ni wachache, na alijua kabisa familia ya akina Maua wanatumia simu ya mezani, kwahiyo akawa anatafuta kibanda cha simu awapigie…lakini wazo likamjia kuwa ni vyema akasubiri kwanza asikia taarifa ya dakiatari kuwa huyo mtu yupo hai au ndio….hapana sitaki kuwaza hivyo hajafa….Maua hajafa….ngoja asogee karibu na kile chumba cha waginjwa mahututi  amsubiri docta ili ajue atasema nini kwa wahusika…Na baada kama ya nusu saa mara docta akatoka kutoka kwenye chumba maalumu na akamsogelea yule dakiatari…

Nisingependa kumalizi  hapa kwa leo, lakini umeme umekatika….balaaa...Maoni yaje!

Ni mimi: emu-three

Friday, July 22, 2011

Attention ; Dangerous Drugs in Circulation


 Hapa Tanzania kumekuwa ni jalala la vitu vibovu, na baya zaidi sio vifaa tu hata dawa. Hii ni hatari kwasababu Watanzania tulio wengi hatuna tabia ya kudadisi dawa, zimetengezwa wapi, zimeisha muda wake nk. Na tunajali tu unafuu wa bei.
 Hili tangazo nimeliona mara nyingi, lakini hutaamini watu wanalichukulia kimzahamzaha, nami leo nimeona niliweke hapa kijiweni kwetu baada ya kutumiwa na mdau wetu Emmy. Habu tulipitie tena hili Tangazo na kama unaweza toa nakala nyingi wapelekeeni majumbani kwa kumbukumbu, na kama ukiandikiwa dawa kama hii , toa taarifa kwa viongozi au polisi ili watu kama hawa wanaotaka kumaliza maisha ya watu kwa madawa yasiyofaa washungulikiwe!



Please take this seriously and if possible keep a copy at HOME....!!!
 Make a checklist, check whether 
this medicine is in your home or 
whether it has been recommended 
by your doctor.... please DO NOT
 use it...

Please Read Very Carefully
 
INFORM ALL YOUR FRIENDS & 
FAMILY MEMBERS

Asia and Africa has become a dumping ground for banned drugs; 
also the business for production of banned drugs is booming. 
Plz make sure that u buy drugs ! only if prescribed by a 
doctor(Also, ask which  company manufactures it, this would
 help to ensure that u get what is prescribed at the Drug Store)
 and that also from a reputed drug store. 
Not many people know about these banned drugs and consume them 
causing a lot of damage to themselves. We forward Jokes and other
 junk all the time. This is far more important.

Please make sure u forward it everyone u know.


DANGEROUS DRUGS HAVE BEEN GLOBALLY DISCARDED BUT 

ARE AVAILABLE IN INDIA and can be exported / smuggled or produced 
in other countries by Indian Pharmaceuticals. The most common ones are Action 
500 & Nimulid!!!!!!

1. PHENYLPROPANOLAMINE : 
cold and cough. Reason for ban : stroke.
Brand name : Vicks Action-500
2. MIST EXPECTORANT SEDATIVE : cold and cough. Reason for ban : cancer.
Brand name : MES


3. ANALGIN: 
This is a pain-killer. Reason for ban: Bone marrow depression.
Brand name: ! Novalgin


4. CISAPRIDE: 
Acidity, constipation. Reason for ban : irregular heartbeat
Brand name : Ciza, Syspride

5. DROPERIDOL: 
Anti-depressant. Reason for ban : Irregular heartbeat.
Brand name : Droperol

6. FURAZOLIDONE: 
Antidiarrhoeal. Reason for ban : Cancer.
Brand name : Furoxone, Lomofen


7. NIMESULIDE: 
Painkiller, fever. Reason for ban : Liver failure.
Brand name : Nise, Nimulid

8. NITROFURAZONE: 
Antibacterial cream. Reason for ban : Cancer.
Brand name : Furacin

9. PHENOLPHTHALEIN: 
Laxative.... Reason for ban : Cancer.
Brand name : Agarol

10. OXYPHENBUTAZONE: 
Non-steroidal anti-inflammatory drug.
Reason for ban : Bone marrow depression.
Brand name : Sioril

11. PIPERAZI! NE: 
Anti-worms. Reason for ban : Nerve damage.
Brand name : Piperazine


12. QUINIODOCHLOR:
 Anti-diarrhoeal. Reason for ban : Damage to sight.
Brand name: Enteroquinol

PLZ SPREAD THE INFO....YOU 
MAY JUST SAVE SOMEONE'S LIFE.  
In Happy Moments Praise GodIn Difficult Moments Seek God,
In Quiet Moments Worship GodIn Painful Moments Trust God,
Always Tell the Truth and Every Moment Thank God
#####################################################################################
Hamisi Masanja Malebo, Dip. Ed (Sc), B.Sc (Hons), M.Sc, PhD
Area of Specialization:  Medicinal Phytochemistry
Principal Research Scientist and Head, Department of Traditional Medicine Research,
National Institute for Medical Research,
P.O. Box 9653, Dar es Salaam, Tanzania.
Mobile:



         +255 7623773 07 begin_of_the_skype_highlighting            +255 7623773 07      end_of_the_skype_highlighting
         Email:Malebo@hotmail.comhmalebo@nimr.or.tz


Ni mimi: emu-three