Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 27, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-5



                                                         **********
Ilikuwa ni ndani ya basi la `Luxury Coach’ linaloelekea Arusha, Maua alikuwa kashikwa na usingizi na pembeniyake alikaa Maneno, na muda mwingi walikuwa hawaongei, ikiwa moja ya masharti yake, waliongea pale palipokuwa na kitu cha muhimu cha kuongea, kiasi kwamba hata Maneno alijisikia ovyo, kwani mtu aliyezoea kuongea ukimwambia akae kimiya, ni macho uyaambie yasione wakati yanaona na yamefunguka….lakini ilibidi afuate masharti, akijua masharti hayo yatayeyuka yenyewe moja baada ya jingine, akajifnya kaishiwa cha kuongea. Alichokuwa akikwepa ni kuongea jambo litakalo muuzi Maua, kwahiyoo kila hatua alijaribu kuwa makini. Alichoshukuru ni kuwa hatua ya kwanza ya mikakati yake imekubalika ya kumshawishi shemejii yake akubali wakabadilishe mazingira, hakuamini pale alimomba hivyo na baada ya kufikiri sana alisema sawa amekubali.
Maneno aligeuka kumwangalia shemeji yake na kumkuta akiwa kasinzia, kinyume na mwanzoni ambapo alionekana kuwa na mawazo na wakati mwingine machoni kulionekana dalili ya machozi, na hapa Manenoo alifikiria mbali, kuwa ina maana kweli mke na mume wanapendana kiasi hiki, mapaka mmoja akiondoka mwingine anatamani naye afe ili wakakutane huko ahera, aliona ajabu sana, akatamani naye ampate mke ambaye atampenda kama Maua alivyompenda Mhuja. `Nikipata mke kama huyu mbona nitashukuru sana, kwani hawa walionakana kupendana tangu mwanzo na sizani kama mapenzi yao yangefika mahali yachujuke, sidhani….’ Akajikuta akisema kwa sauti ndogo, kumbe Maua alihis kitu akafumbua macho na kumwangalia Maneno, na Maneno akatabasamu
‘Umechoka sana, lala tu, unajua tena hii ni safari ya siku nzima, na ukifika kule utakuwa na shauku ya kuangalia wanyama, na huenda usipate muda wa kulala….lala shemeji yangu usijali nipo karibu yako kuhakikisha upo salama…’ akasema Maneno na kweli Maua akafumba macho kurudia kwenye usingizi, na hapo Maneno akamwangalia Maua sura yake na hata vile alivyokonda , lakini urembo wake ulikuwa haufichiki, alitamani angemsogelee na kumbusu shavuni,lakini kwa wakati mwingine alikuwa amemuogopa hata kumgusa, akikumbuka pale alipomkuta jikoni kalala anatoa mapofu mdomoni,…
 Maneno hakuamini kuwa mrembo kama huyu angefikia hatua ya kutaka kujiua, eti kwasababu mume wake kafa, mbona waume wapo wengi wanaomtamani, wanaompenda….`siamini kuwa mrembo kama huyu aliamua kujiua , kuna kitu kimejificha hapa na nitakigundua tu, na nikigundua kuwa kipo kitu kama hicho, ole wao wale mawifi , urafiki utakwisha ...alishukuru sana jinsi madakiatari walivyofanya juhudi kubwa hadii kumuokoa maisha yake, alikumbuka pale yule dakitari alipokuja na kumuita pembeni.
‘Natumai huyu ni mgonjwa wako na mpo karibu sana, je wewe ni mume wa huyu mgonjwa…?’ Docta aliuliza, na kuanza kumfanya Maneno ashikwe na kimuhemuhe, maana ile kauli ilikuwa kauli tata, na haikuashiria mema, akashikwa na kigugumizi cha kujibu….
‘Mmmh, ni shemeji yangu, …vipi atapona do-docta, …eti docta natumai yupo hai….mume wake ni miongoni mwa wahanga wa Mv Bukoba, kwahiyo mimi nasimama kwa niaba yake..je kuna matumaini yoyote…naomba sana docta niambie ukweli …na fanya kila njia apone..’ akasema Maneno akiwa na wasiwasi
‘Siwezi kusema lolote mpaka sasa, imebidi tumfanyie upasuaji wa haraka, na …bado hali yeka ni tete, ndio maaana nilitaka kukujulisha hilo, kuwa tumechukua hatua hiyo bila kukuarifu, hatua na jinsi, kwani kulikuwa hakuna muda wa kukutana na wewe…tunachomba mtuelewe hivyo, ila kwasasa mnatakiwa mvute subira,… lakini matumaini yapo kwani ile sumu haijaasiri kitu ndani…hilo ndilo la kutia matumaini, mengine bado tunajaribu kufanya kila iwezekanavyo kuokoa maisha yake na….mengine yote yanategemea uwezo wa muumba..’ akasema Docta na kuondoka
 Maneo alibaki kaduwaa, ina maana docta kasemaje pale, kuwa yupo hai, au ndio bado wanataka kumfanyia upasuaji,…au …mbaona sijaelewa… akawa anajiuliza kwani wakati docta anaongea, yeye alikwua mbali , alikuwa akisubiritu kauli ya mwisho ya docta kuwa kafa au kapona, lakini hakusikia lolote kati ya hayo maneno mawili, alipoona docta kaondoka, akakurupuka mbio kumfua nyuma, lakini kabla hajamfikia akawa keshafunga ule mlango wa chumba maalumu…akajikuta anajilaumu kwa kutokuwa makini kumsikiliza docta…
‘Aaah , sasa nitawaambiaje jamaa zake…’ akafikiria halafu moja kwa moja akelekea kwenye chumba chenye simu na kumpigia shangazi yake, ambaye baada ya kupata taarifa hiyo tu, alikuja haraka hospitalini, kwani alishasikia kuwa Maua hayupo nyumbani, na haijulikani katowekaje, taarifa hii aliipata toka kwa wifi wa Maua ambeya alikuwa na zamu siku hiyo. Na shangazi alipofika tu wakawa wansubiria pamoja na baadaye jamaa wengine wakawa wanafika mmoja mmoja kwani walikuwa wameshapata taarifa , na ilipofika jioni taarifa ikaja kuwa Maua yupo hai na keshazindukana baada ya kufanyiwa huo upasuaji kwahiyo baadaye atapelekwa wodini.
                                                                     *******
  `Mimi sijanywa sumu….  Sikumbukikabisa kufanya hivyo….’ Hiyo ilikuwa kauli ya Maua wakati anahojiwa                                                           
‘Maua kwanini uliamua kufanya hivyo, wewe unashindana na mungu, kujiua ili iweje,,,mbona unaniabisha shangazi yako, mimi sijakufundisha tabia kama hiyo, nilikufundisha ucha mungu, ujasiri na subira wakati wa matatizo..sasa umefanya nini mwanagu…’ shangazi akawa kakaa pembani yake akimhojii kwa uangalifu, alikuwa akitaka kujua ukweli mapema.
‘Shangazi mbona mimi siwaelewi, mnasemaje…?,’ Maua aliinua kichwa na kumwangalia shangazi yake huku akiwa na macho ya kushangaa, akaenedelea kusema `…eti nimekunywa sumu…haiwezekani kabisa, mimi sijanywa sumu kabisa….nilitamanai kujiua mwanzoni, lakini siku zilivyokuwa zikienda, hilo wazo lilikuwa limeondoka, ninachokumbuka mimi ni kuwa nilikunywa kahawa ….na pale nilipomaliza  kuinywa ile kahawa mara nikaanza kusikia tumbo likikata sana, …nikapiga ukulele kumuita wifi, ….lakini sikuweza kupaza sauti sana, nikaita weee…kimiya…na tumbo lilipokata mara ya pili nikajikuta mwili mzima ukikosa nguvu, mara nikaona kizunguzungu na ….sikumbuki tena kilichofuatia kwani tumbo lilikuwa na maumivu sana…sikumbuki shangazi, na mimi sikunywa sumu kabisa….hilo nakataaa…’akasema Maua na kuwaacha shangazi yake midomo wazi…
Pembeni yake alisimama wifi mkubwa, ni mmoa wa dada zake Mhuja, na mdogo wake ndiye aliyekuwa na zamu siku hiyo lilipotokea hilo kasheshe, aliposikia kauli hiyo ya Maua akahamaki na kusema kwa sauti
‘Wewe umechanganyikwia tu, …sasa mbona dakitari kasema kuwa imegundulika kuwa umekunywa sumu,…. Sumu… , lakini bado haijagundulika ni sumu ya aina gani…tuambie ukweli tu ulitaka kujiua kwasababu ya akili yako ndogo….’ Akasema yule wifi…….
Maneno aliposikia hivyo huyo wifi akiongea kwa sauti akasogea karibu kusiliza nini kinaendelea
‘Hivi wifi yake yule aliyekuwa naye yupo wapi, mbona aliondoka na kumuacha mgonjwa peke yake, ….na …mimi nataka kuongea naye kwa makini ilikuwaje akaondoka, maana tulikubaliana kuwa mtu asiondoke..mnaona kilichotokea…’ akasema Maneno kwa hasira.
‘Hivi huyu ni mtoto mdogo, nani asiyekuwa na uchungu, sisi Mhuja ni kaka yetu, keshaondoka hatuwezi kabisa kumpata kaka mwingine kama yeye, yeye kama mke itafika sehemu atasahau hatimaye atapata mume mwingine, hivi ina maana sisi hatuna uchungu….kaka , damu moja, lakini tumekubali ukweli na tumemuachia mungu…sasa yeye anazidi mpaka, hatukatai kwasababu walikua naye karibu na tunasema watu wakioana wanakuwa mwili mmoja, lakini lazima tukubali ukweli, kuwa hata iweje , ipo siku mmoja ataondoak duniani, ama itokee bahatii muondoke wote au atangulie mmoja, ni swala la muda, hakuna mwenye maamuzi na mungu…kwahiyo mimi nasema toka leo, kama utaendelea na tabia yako hiyo, sisi hatutavumilia…cha muhimu ni kukubali ukweli, na kumuombea kaka yetu huyo apumzike mahala pema peponi, lakini sio kutufanya sisi tutaabike bure…’akasema yule wifi yao mkubwa.
Maneno alikuwa mbali akiwaza kwanini Maua kakataa kuwa hakunywa sumu, ina maana basi kama hakunywa sumu kuna jambo limejificha hapo,…au kuna mdudu mtu kaingilia katu…haiwezekani, …lakini labda inaweza kwa  kweli kuwa Maua alikunywa hiyo sumu akiwa kuchanganyikiwa na kasahau kuwa alifanya hivyo…akakuna kichwa kwa mawazo, kwani alikuwa akiwaza jambo ambalo hakulitaka kabisa liingie kichwani mwake na hakutaka kuweka wazo hisia zake, kwani kama ataongea hivyo anaweza akaanzisha uhasama usiofaa, na huenda kweli Maua alikunywa sumu bila kujijua kwa kuchanganyikiwa.
‘Jamani imeshaeleweka naona tumuache mgonjwa apumuzike, na hili swala liishie hapa hapa kwenye familia , lakini inabidi baadaye tukae kama familia tuongee vyema, mimi kama shangazi yake nahitaji maelezo ya kina kwani tulikubaliana sote siku ile kuwa tuwekeane zamu, …ndio yeye sio mtoto mdogo, lakini hali ilivyokuwa muliiona wenyewe, na nyie ndio mliokuwa wa kwanza kutoa wazo hilo,..na hii sio yeye tu inaweza kumtokea yoyote…kufiwa na mume sio mchezo kama mnavyofikiria, na inatokea watu kuzidiana katika kuweza kuhimili hiki kishindo, ni mtihani mkubwa…lakini kwanini huyu wifi aliondoka kwa kipindii chote hicho, je kama asingekuaj Maneno ingekuwaje?’ akasema Shangazi mtu.
‘Hiyo ilipangwa iwe hivyo, hata asingekuja Maneno kuja hapo na kumkuta katika hiyo hali bado angekuja mtu mwingine akamuokoa… siku yake ilikuwa haijapangwa na tusitake kutafuatana uchawi , wakati mwenye kosa tunamjua, ni yeye mwenyewe huyu wifi…mimi sitaki kuongea sana, lakini lawama zote ni zake mwenyewe na asijifanya hajanywa hiyo sumu, na kutaka kuanzisha mambo mengine ambayo hayapo, kabisa….tumuache apumzike na akili ikimrudia vyema anaweza akatuambia ukweli kama ni lazima, na sidhani kama polisi wana umhimu sana na hili jambo, kama mgonjwa wetu kapona, mimi naona yaishie hapa…
‘Hilo halina uhakika, lakini kiutaratibu lazima polisi wafanue uchunguzi wao ili wajue nini kilitokea na hatuwezi kuwazua kwa hilo…na kama hakuna ubaya , mimi sioni kwanini watu wawaogope polisi…’ akasema Maneno.
‘Kwanini hatuwezi kuwazuia kwa hilo , hamuwajui polisi wataanza kasheshe yao na kwuasumbua watu wasio na hatia…kwa sababu ya…aah, bwana mimi mtaniona nina roho mbaya lakini pale penye ukweli siwezi kuvumilia…najua hisia zitajitokeza kwa vile mdogo wangu ndiye alikuwepo siku ile na akafnya uzembe wa kuondoka, na yeye anaweza kufikiriwa vibaya…na kusababisha hilo, ….lakini mimi nitamtetea mdogo wangu kwa nguvu zote, mimi ninamjau sana mdogo wangu, katika watu wanaompenda wifi yao huyo ni namba moja…sasa mkianza kuchokonoa chokonoa mtaazua mambo yasiyo na ukweli, …hakuna mchawi hapa, mchawi ni wifi mwenyewe, aache hiyo tabia, sisi tuna uchungu kama yeye na huendazaidi yake yeye…’ akasema yule wifi mkubwa.
 Maneno hakutaka kuingilia sana hilo swala, lakini baadaye polisi waifuatilia kiundani na walipombana sana Maua , Maua sijui kwa kutokutaka matatizo zaidi alisema kuwa `inawezekana ilitokea hivyo kuwa alikunywa sumu bila kujijua lakini hakumbuki kabisa kufanya hivyo…’.na polisi walipoona hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kumbana yoyote, wakahitimisha uchunguzi wao na baadaye mambo yakanyamazishwa kiaina, lakini kichwani kwa Maneno hakuliacha hilo jambo liishe hivyo hivyo, aliliweka kichwani kuwa ni lazima atamuulizia shemeji yake vyema kuwa ni kweli alitaka kujiua na je ile kauli yake ya kukataa kuwa hakunywa sumu aliitunga baadaye au kuna kitu kinaendelea kati ya Maua na wifi zake, kwani kama hivyo kuna haja ya kuokoa jahazi haraka iwezekanavyo…
Siku moja baada ya Maua kuruhusiwa kutoka hospitalini , Maneno alimtembela kama kawaida yake, akawa anatumia ujanja wake wakuongea na kuchekesha mpaka Maua akatabasamu, na kweli kazi hiyo ya kuongea anaijulia, na kama hutacheka basi utafurahi na kama hutafurahi, utaongea na wewe…huyo alikuwa Maneno, mwenye maneno kweli.
‘Shameji unajua wewe ni jasiri sana, na tena urembo wanko huo ndio unakusaidia …na nina jambo moja kubwa nataka kukuomba, naomba sana unikubalie ombo langu…unajua ili akili itulie ili uondokane na mawazo na kama dakitari alivyopendekeza , inabidi …akili ione kitu tofauti..na mimi nimewaza sana na wazo kubwa likanjia akilini, niakongea na wenzangu ofisini, na kweli wakakubaliana na wazo langu, sasa ikabidi nifanye juhudu zote na kweli kila kitu kimewekwa sana, kinachotakiwa na kauli yako tu….sasa nakuomba unikubalie ombi langu hilo…unajua shemeji kuna wimbo mmoja unaimbwa hivi;
‘Nikubalie mama we, taratata…kauli yako nisikie taratata, taratata
‘Usipate taabu kwa ajili yangu eeee….taratataa…
 Akawa Maneno anaimba huku anacheza, na kwa jinsi alivyokuwa akicheza alimuacha shemeji yake hoii na kuanza kucheka…na kicheko hiki ni cha mara ya kwanza tangu msiba utokee, na hapo Maneno akakatiza na kubakia kushangaa, bila kuamini, hivi kweli naota au kweli Maua kacheka…akashukuru sana kimoyomoyo…na kuendelea kusema kimoyomoyo kuwa sasa mambo yanaanza kurejea katika hali yake,…halafu akatabasamu na kumsogelea shemeji yake halafu akachukua mikono yake na kumshika viganja vyake, alitamani kuvibusu, lakini akavishikilia kwa muda…
‘Tafadhali sana shemeji nakuomba sana unikubalie ombi langu hili…’ akamwangalia usoni,halafu akatikisa kichwa, alipoona shemeji yake kamwangalia machoni mara moja halafu akaangalia chini, yeye akaendelea kuongea kwa kusema ` hili ni ombi letu, kwani sikulipitisha mimi mwenyewe, na tumeona hii huenda itakuwa heri kwetu na kwako na huenda ikasaidia kukutuliza moyo wako. Tunakuomba sana, …hasa mimi ninakuomba kuwa ili uondokane na mawazo yako, ambayo yamefikia hadi hatua ya kunywa sumu,…unajua shemeji hiyi ni hatua ya …lakini natumaini hilo limekwisha , sisi tumeonelea kuwa inabidi usafiri kidogo, ubadili hali ya hewa, ubadili mazingira kidogo…na kusafiri huku tumeonelea kuwa twende ukaone mbuga za wanyama, Ngorongoro…
Maua  akapanua mdogo kwa kushangaa, kama kuna kitu ambacho alikitamani katika maisha yake mojawapo ni kutembelea mbuga za wanyama na hili waliwahi kuongea na mume wake, …alifika hapo lile tabasamu la mdomoni likayeyuka,..lakini baadaye akawaza na kusema, ilimradi kaamua kuondoa mawazo na kujaribu kukubali ukweli atakubali ombo hilo , akasema
‘Sawa, kama mumeshapanga kila kitu, hutegemei mimi nikate , ..au mlitarajia nini kama mliamua bila kunishirikisha, sawa nitashukuru sana kuwemo kwenye hiyo safari,… sawa nimekubali…’ akasema na kutabasamu, na Maneno akaruka juu na kusema `yessss’ …akamsogelea shemaji yake na kumkumbatia, ingawaje shemeji yake hakunyosha mikonoo alikuwa katulia tuliii, mikono yake kaionyosha chini, huku anamshangaa shemeji yake…na hapo Maneno akamwachia haraka kama vile kagutiliwa na kitu na kusema `samahani sana shemeji, …ni raha ndiyo imenifanya niwe kama mwehu, raha kukuona umerudi katika hali yako…

‘Nimekubali kwa masharti…..’ akasema Maua, huku machozi yakimtoka, na kumfanya Maneno aingiwe na wasiwasi na kuwaza hayo masharti ni ya nini na atayaweza kweli......

NB, Jamani mniwie radhi, kwani umeme, foleni na uwajibikaji ofisini vinanikwaza kushindwa kutimiza wajibu wangu...natamani sana kuipeleka hiki kisa haraka , ikibidi kila siku, lakini wapiii...Nawaomba msichoke kusubiri, nitajitahidi iwezekanavyo...TUPO PAMOJA DAIMA


Ni mimi: emu-three

3 comments :

samira said...

mume anauma asikwambie mtu m3 mambo mazuri cant wait unajitahidi

Iryn said...

Aiseee mambo yanazid kunoga m3 bt huyo wif nae ana mdomo hatari.. Kaza buti upo juuuuuu

Pam said...

bwana hapo penye sumu suspect number moja ni wifi no doubt walishachoka zamu za kumuangalia wifi yao na kaka yao hayupo... too sad.
Maneno maneno mmmh wampenda shemejio jamani haya take care.