Maneno akiwa ofisini kwake akili yake ikawa inakwazwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, alishindwa hata ashike lipi aache lipi, hata kazi yake ilikuwa nzito! Akakumbuka kuwa jana hakupata muda wa kumuona shemei yake kwasababu haikuwa zamu yake, na pale mezani alikuwa na kazi nyingi za kiofisi ambazo alitakiwa kuzimaliza, lakini kila akijaribu kutuliza mawazo alishindwa kufanikiwa, pamoja na kumuwaza rafiki yake kuwa ndio basi tena, mwezi na siku kumi na tano imeshapita tangu lile tukio, lakini bado akili zao zilikuwa hazikubali.
Maneno alijitahidi sana kufanya kazi za watu za ofisini ili angalau azipunguze, lakini moyo wake ukawa unaambaa-ambaa kwenye ndoto ya jana, ndoto ambayo ilimkubusha mengi, ndoto ambayo ilimkutanisha yeye na rafiki yake, hutaamini hilo lakini wakati mwingine marahemu anaweza akakutokea akakumbusha umsaidie kulipa deni aliloacha, kwani huko anateseka na ukilipa anakutokea na kukushukuru … na Maneno alitokewa na rafiki yake alikimkumbushia asisahau urafiki wao, na kumuongezea kauli ambayo ilimkaa sna moyoni, na Maneno akawa anaikumbuka mara kwa mara, kuwa hata kama kasafiri mbali, isiwe ndio sababu ya kumsahau mkewe, kwani akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli.
Alipoisikia kauli toka kwa rafiki yake kwenye hiyo ndoto, akataka kumuulizia, kwanini anasema hivyo wakati yeye na familia nzima wapo pamoja na mkewe? Lakini kabla hajaweza akumuulizia hivyo na kupata `la kwanini’ mara akazinduka toka usingizini, …. Kwa hali hii akawa anajaribu kuangalia wapi kafanya vibaya, au ni ndoto tu. Akawaza sana tangu rafiki yake aondokea kuwa alifanya vibaya kinyume na urafiki wao, lakini hakuona kosa alilofanya, hivyo akaichukulia kama ni ndoto tu ya kawaida na labda ni kwa vile alikuwa akimuwaza sana rafiki yake huyo inawezekana ndio maana akamuota.
Hakutaka kumhadathia mtu yoyote ile ndoto, hasa alipoaina haina ujumbe muhimu kwake, kwani kila kitu alikitimiza…`hiyo ni ndoto tu ya kawaida ….’, ila aliona kuwa bado ana kazi kubwa ya kumhudumia mke wa rafiki yake na huenda huo ujumbe ulikuwa ukilenga huko, na kama ni hivyo aliahidi moyoni kuwa atajitahidi sana kuhakikisha hilo linafanyika ili roho yay a rafiki yake huko ulipo, ipate kustarehe …huko mbele ya haki kwani huo ndio urafiki wa kweli…..
Ilishapita mwezi na kitu sasa tangu lile tukio kubwa litokee, watu wengi walikuwa bado hawajaamini kuwa ndio imekuwa hivyo…hasa wale ambao jamaa zao hawakuonekana kabisa, kila mara wanadhania huenda jamaa zao wakatokea, labda walinusurika, , labda siku hiyo ya safari hawakuwepo humo ndani…ni mawazo ya kibinadamu kwasababu binadamu hana uwezo wa kuona ghaibu lakini kwa kipindi chote hiki kama alikuwa hai angeonekana au hata kutoa taarifa. Maneno akaguna alipowaza hivyo akikumbuka ile hali aliyoiona siku ile alipoenda kuhakikisha kwa macho ayke mwenyewe, kwa hali kama ila alikuwa na uhakika kuwa rafiki yake keshapotea, hayupo tena duniani.
Kila alipojaribu kushika kazi akili yake ilikuwa haitulii, na mara akamkubuka shemeji yake , jana hakuweza kupitia nyumbani kwake kwasababu alikuwa kabanwa na kazi nyingi za ofisini, na kwahiyo leo kwa vovyote inabidi apitie kidogo, kwani itakuwa anakiuka masharti aliyowekewa na rafiki yake kuwa kila siku ahakikishe anampitia shemeji yake na hata chakula ahakikishe ana kula hapo nyumbani, na alijitahidi kufanya hivyo, ila kwasababu ya hilo tatizo na kuwa shemeji yake ailikuwa hawezi hata kupika kwa jinsi alivyiathirika na huo msiba, ikawa siku moja moja hafiki, ila aliahidi moyoni kuwa atajitahidi kwa siku zote kwa kadri yauwezo wake awe anamhudumia shemeji yake hadi hapo kitakapojulikana.
`Hadi hapo kitakapojulikana, sitaki kulianza hili mapema, lakini moyo wangu unatamani iwe hivyo, mmmh, wakati bado huenda rafiki yangu ..hapana haiwezekani katika ile hali haiwezekani, atakuwa keshatangulia mbele ya haki..’ akajikuta akisema kwa sauti. Na hapo kumbukumbu za hali aliyoikuta kule Mwanza siku ile zilimjia kichwani, jinsi alivyoiona ile hali na kwa yoyote angejua tu kuwa kama jamaa yako hakuwepo miongoni mwa yale maiti basi keshaliwa na samaki, na hata kama ungebahatisha kuuona mwili wake, angeukuta haupo kamilifu, angelikuwa kaharibika sana na baadhi ya viungo vitakuwa havipo….hapo tukio zima la siku ile likaanza kumrudia tena akilini jinsi siku ile ilivyokuwa.
****
Baada ya lile tukio kikao cha wanafamilia kilikutana na Maneno alialikwa kwa vile ni rafiki wa karibu, na yeye aliwakilisha taarifa ya kutoka kazini kwao kuwa wao kazini wamewatumia wafanyaakzi wao wa kule kufuatilia kwa karibu, lakini hawakugundua lolote, kwahiyo wanatka kusikia wanafamilia wanasemaje. Taarifa hiyo alipoifikisha kwa wanafamilia hawakuipokea kwa mikono miwili wakataka mtu atoek hapa Dar, akaone kwa macho yake, na kutokana nah li ilivyo, walimkatalia kabisa mke wa Mhuja kwenda huko, hasa kwa taarifa zilizopokelewa kuwa watu wamejaa, na hali ilivyo hapo inataka mtu mwenye moyo wa ujasiri kuihimili.
Wanafamilia walijadiliana wakaona wamtoe mtu wa familia aende huko, bsi Maneno akasema ili kuondoa shaka yeye ataondoka kwenda huko haraka iwezekanavyo, ingawaje kule wana ofisi na wana wafanyakazi kama yeye, na wanamjua sana Mhuja na wamefuatilia kwa karibu na wengine walihusika hata kuwepo kwenye kikosi cha uokoaji, alkini hawakuweza kumgundua au kuona dalili yoyote ya kuwepo kwake, kwahiyo wana imanai huenda ni miongoni mwa wale walioshindwa kabisa kutoka ndani ya kile chombo na kama alitoka basi huenda kakumbwa na ajali nyingine.
Kesho yake Maneno akafunga safari akiwa kapata baraka za ofisini na bahati nzuri alipata nafasi katika ndege ya ejshi ambyo ailikuwa inaeleeka huko kwahiyo alifika haraka pale Mwanza na alipofika tu hakupoteza muda, moja kwa moja akaelekea eneo ambapo maitizilizobahatika kuopolewa zilikuwa zimehifadhiwa, na hata akaonana na wafanyakazi wenzao ambao walimhakikishia kuwa wao wamepitia kila maiti na wamepitia kila eneo na wao walibahatika kuwepo kwenye kundi la waokoaji , lakini hakuna kilichopatikana
Maneno hakutosheka na hizo taarifa akaanza kukagua maiti zote, akatoka hapo akaelekea sehemu ya kumbukumbu za majina kuhakiki kuwa kweli aliwahi kusafiri siku hiyo, na kweli aliliona jina lake kwenye yeye ni miongoni mwa watu waliopata tiketi mapema kabisa, akaangali amajina ya watu waliotambulikana na wale waliotoka hai hakuona jina la rafiki yake huyo, akaanza kukata tama, akajadilian na marafiki zake na hatimaye walifikia muafaka kuwa huenda mfanyakazi mwenzao huyo ni miongoni mwa hawo waliopotea ndani ya maji.
Kwakweli kila hali ilivyokuwa hakukuwa na dalili yoyote ya kupatkana mwili mwingine ukiwa na hali nzuri, kwani kila mwili uliopatika kwa siku ile ulikuwa umeharibika vibaya, umeshanyofolewa na samaki…na haushikiki, na hata serikali ilikuwa imeshasitisha lile zoezi la uokoaji kwa kupitia kwa raisi mwenyewe, na raisi kipindi hicho alikuwa Mkapa. Basi Maneno akawa hana jinsi alijitayarisha kurudi nyumbani kutoa hiyo taarifa…
Siku niliporudi wanafamilia wote walikusanyika uwanja wa ndege waliwa wanajua huenda karudi angalau na mwili wake, lakini lipoonekan mwenyewe, kila mmoja alijikuta akibibijikwa na machozi, akakutana na na wanafamilia na kutoa hiyo taarifa aliyoiona huko, na ikawa haina jinsi ni kutangaza msiba, na kila mmoja akawa anatafuta jinsi ya kumfahamisha mke wa Mhuja, na kazi hiyo ikamuendea Maneno ambay ndiye aliyekuwa karibu sana na shamaji yake.
‘Niambie ukweli shemeji , …umeshindwa kuibeba maiti ya rafiki yako …kwasababu imeharibika au unataka kuniambia nini…au mimi najua kabisa mume wangu hajafa nina uhakika huo, msiniambie kitu…’ akaanza kusema Maua hata pale alipofahamishwa jinsi ilivyo huko Mwanza hakuamini hilo, alichofanya nai kumrukia Maneno na kuanza kumpiga mingumi akisema huyo aliyeenda hakufanya juhudi za maana, na huenda kaiona maiti yake imeharibika akaogopa kusema., …na akwa anaongea maneno mengi…lakini wote walijua ni kihoro cha kufiwa, itachukua muda kitaisha. Basi msiba ukatangazwa na wanafamilia wakakutana na ikabidi mke wake aambiwe akae eda kwa mujibu wa taratibu, lakini hakukubali kabisa, ila aliposhurutishwa na wazee ikawa hana jinsi akakaa shingo upande…..na kila mara ilikuwa ikimjia sura ya mume wake, na alipopata usingizi akawa anamuota yupo naye.
`Maua maisha haya ya kupanga nyumba sio mazuri, tukianza kupata watoto, itatuwia shida , naona tuanze kujenga kwanza kabla ya kufikiria watoto, au unasemaje..’akaulizwa na mume wake.
‘Kwani wewe Mungu, unasema hivyo, unajuaje utapata watoto wakati gani ni bora tuzae mapema, ili hata mmojawapo akiondoka duniani aache mbegu’ akasema Maua, na hapo ukaanza ubishi kila mmoja akidai lake, na mara Mhuja akakasirika na kutaka kuondoka, na Maua akawa anambembeleza mume wake asiondoke, lakini haikusaidia kitu, hata akawa aanajiuliza ina maana ubishi huo mdogo tu ndio unaomfanya mume wake azire na kuondoka, akaamua kutoa nje kumfuatilia, alipofika nje akamuona mume wake anaondoka kwa kasi na huku kuna gari linakuja kwa kasi, lakini ilivyoonekana mume wake alikuwa halioni.
‘Mume wangu hatari, angalia gri hilolinakuja, utagongwa…’ akawa anasema kwa sauti, lakini ilionekana mume wake hamsikii akawa anakwedna tu na lile gari likamfikia mume wake na hapo Maaua hakutaka kuangalia hilo gari likimgonga mume wake akageuza kichwa huku akisema `jamani mume wangu anagongwa na …akiwa amegeuza kichwa kutokumwangalia mume wake na huko alipogeuzia kichwa alikuwa kasimama shemeji yake Maneno ambaye alikuwa akimcheka kwa dhihaka na kusema
‘Unaona mume wako alivyo mbishi,, nilikuwambia mimi ndiye nakufaa kukuoa sasa angalia kagongwa na gari, humuoni tena ng’ooo’ alisema Maneno.
‘Hapana hajagongwa, hapana wewe una roho mbaya, ….wakati anayasema haya akawa anageuza kichwa taratibu ili ahakikishe kuwa kweli mume wake ahajagongwa, na alipogeuza kichwa vizuri, ….ooh, kumbe ilikuwa ni ndoto, akajizoa zoa na kutoka nje akiwa na nia ya kumuona mume wake…akakuta kweupe, watu wanapitapita mabarabarani, wengine wakiwa wameshikana na waume zao , wengine..na wapenzi wao, yeye hakuamini kuwa ndiyo aliyempenda keshaondoka, hatamuona tena duniani, hakuamini hilo, akaingia ndani akavaa nguo, nia anataka asafirihadi huko Mwanza, akahakikishe mwenyewe kuwa kweli mume wake kafa!
‘Hapana lazima yupo mahali, sikubali mume wangu hajafa…
***************
Maneno baada ya kuona akili yake haitulii vyema na kwa kiasi kikubwa alikuwa akimwaza shemeji yake ambaye kila siku hali yake inazidi kuwa mbaya, anakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, anazidi kukonda…na bado akili yake hataki kukubali kuwa mume wake keshatangulia mbele za haki! Aliamua atoke akamuone mara moja, ingawaje ilikuwa sio zamu yake ya kukaa naye, kwani ilikuwa imefikia mahali wafanye hivyo kupangiana zamu ya kumlinda,…amechanganyikiwa kabisa, na akibaki peke yake lolote linaweza kutokea, kwa kufikia vile akaona akimbie akamuone mara moja na kuona kama kuna kitu kinahitajika, halafu arudi kazini, akaaga na kuondoka,…
Aliingia ndani ya gari ambalo alikuwa akiiendesha Mhuja, na kila akiingia ndani ya gari hilo huwa anamua rafiki yake kaka pembeni kimawazo, gari hilo lilikuwa limenunuliwa kikazi na Mhuja ndiye alikabidhiwa, na kwa kuondoka kwake ikabidi Maneno apewe yeye! Maneno aliwaza sana kuhus maisha , kuwa maisha kweli ni safari, leo upo hapa duniani kesho haupo, …kama mchezo tu, na huwezi hata kuamini, …aaah, kweli inatakiwa kujiandaa wakati wote, huwezi amini rafiki yangu keshaondoka, na kaacha mke mzuri, hawajazaa, hawajafaidi maisha ya ndoa, na walikuwa na mikakati mingi ya kimaisha, lakini yote imesimama, na sasa inategemea mke wake atakavyojipanga….
‘Mke wake..’ sio mke tena, …kaondoka na huenda akapata mume mweingine, ukishakufa kila kilichobaki duniani sio chako tena…hivi ndivyo ilivyo, naogopa hata kuoa, maana nikioa nitakufa wenzangu watamchukua mke wangu, mali yangu…mmh, haya maisha jamani…kwakweli shemeji ni mzuri hatakawia kupata mume mwingine, na …inibidi nimlinde sana kuhakikisha kuwa nimelinda urafiki wangu na rafiki yangu, hata kama ataamua kuolewa na mtu mwingine, nitahakikisha atakayemuoa hawezi kumpa shida, na ikibidi …na ikibidi…siwezi kumlazimisha,…mmh, kwelinampenda sana tangu siku nilipitambuslishwa na rafiki yangu, nilitamani sana kuwa angelikuwa wangu, lakini kila ninpofikiria namuoa sasa kama dada yangu….
Mawazo na mwendo wa gari na kwasababu kulikuwa hakuna foleni alijikuta keshafika nyumbani kwa Mhuja kwa muda mfupi tu na hata bila kujitambua…alipofika akaangza huku na kule kama atamuaona yule ambaye ni zamu yake kukaa na huyo ambaye sasa anaitwa `mgonjwa’ anakitwa `mjane’ akasogea kwenye mlango na kupiga hodi akashngaa kuona kimiya, huyu anayemhudumia `mgonjwa ‘ kaenda wapi na shemeji yake, ina maana leo kaweza kutoka kidogo, kama ni hivyo mbona tutashukuru sana, aua kazidiwa kapelekwa hospitalini, lakini wasingefanya hivyo bila kumtaarifu…akajaribu kufungua mlango akaona umefungwa kwa ndani labda, akajipapasa mfukoni, kwani alikuwa na ufunguo wa akiba aliokuwa kakabidhiwa na rafiki yake.
‘Ufungu huu ni akiba, kaa nao shemeji yako anaweza akapoteza funguo zake mkapata shida au unaweza ukafika shemeji yako hayupo unaweza ukaingia ndani au likatokea tatizo na unahitaika kumsaidia shemeji yako, na huna ufunguo,…huu unaweza ukakusaidia..’ aliwaza jinsi gani rafiki yake alivyokuwa akiotea mambo, kwani kila alichoongea hutokea na kusaidia katika hali usiyoitegemea.
‘Shemeji upo wapi, …wifi wa sheemji upo wapi!?’ akaanza kuita lakini kulikuwa kimiya…na hapo nywele za Maneno zikawa zinasisimuka na moyo kwenda mbio, hii ikionyesha ishara ya kitu ambacho sio kawaida, hali amijenga mwilini mwake, akihisi hivyo kuna jambo… na alipotizama pale varandani akaona begi la safari, limebagwa chini, …akalifuata na kulingalia kwa makini , alilikumbuka kuwa ni la shemaji yake, alinunuliwa kipindi fulani alipokuwa akisafairi kwenda kwao kusalimia…alilichagua mwenyewe wakiwa watatu, yeye Maneno , Mhuja na mkewe…akatabasamu alipokumbuka siku ile, maana alipolichagua ili bidi wamcheke, kuwa anachagua begi la kijijini…lakini yeye aliling’ang’ania na ikabidi anunuliwe hilo hilo…akaliinua na kuliweka juu ya kochi, hakutaka hata kulifungua kutizama kuna nini cha zaidi… , akajiuliza ina maana shemeji yake alishajiandaa kuondoka , na kama ni kuondoka alikuwa na safari ya wapi, na wifi yake yupo wapi, ambaye ndiye mwenye zamu ya kuwa na huyo mgonjwa, mbona hayupo ndani…watakuwa wametoka pamoja nini…
Akaita mara nyingi lakini hakuona dalili yoyote, mwishowe akaamua kukagua nyumba nzima, alianzia chumbani kwa shemaji yake akakuta kitanda kimetandikwa vyema kabisa, akatoka mle akaingia bafuni akakuta hakuna mtu chooni , akaingia chumba cha wageni ambapo alitegemea kumkuta wifi wa shemeji yake, hakuna mtu, hakuna mtu…. akarudi varandani akatulia kuwaza hawa watu lazima wametoka…kama simu yangu ingekuwa nzima ningewapigia, akalaani kutokulishughulikia kupata simu za mkononi,….lakini haiwezekani, kama amjuavyo huyo shemeji yake amekuwa hataki kabisa kwenda kokote, hatiki nje kabisa..labda kawa na hamu ya kutoka nje, lakini hili begi je, ni la nini…akaona muda unakwenda, akasema ngoja niingie jikoni nipate chochote kama kipo…..akatembea hukuanatizam huku na kule akafungua mlango wa jikoni…mamamamamama… akapata mshituko wa moyo..
Alijikuta akipiga kelelele za `mamamamam….’ Halafu akaingia ndani na kuinama pale skafuni
‘Wewe shemeji vipi mbona upo hivyo…’ alimkuta shemeji yake yupo sakafuni kalala na mapofu yanamtoka mdomoni…Mara moja akili yake ilikwenda haraka kuwaza hivyo kuwa kanywa sumu , na alichofanya ni kukimbia kwenye jokofu na hapo akakuta maziwa akamimina kwenye kikombe, akarudi haraka na kuanza kazi ya kumnywesha, ilikuwa kazi kubwa, kwani meno yalikuwa hayafunguki , ikabidi achukue kijiko na kupanua yale meno kwa nguvu, na baada ya kazi nzito akafanikiwa…alipohakikisha yamepita maziwa ya kutosha, akatulia kuwaza afanyaje nini tena, alipogeuka kuangalia pale juu ya meza linapowekwa jiko ndipo akaona kikombe cha chai, au kahawa…akainusa, haikuwa na dalili yoyote ya harufu ya sumu…lakini alijua kabisa huenda sumu hiyo ilikuwa imechanganywa na ile chai, …auakameza vidonge na kwanini kafikia hatua ya kujiua….
Alijaribu kwamwangalia mapigo ya moyo, …duh, hakuona dlili yoyote ya uhai, mungu wangu, ina maana tumempoteza mtu mwingine tena, haiwezekani, akamwiinamia na kuweka sikio karibu na mapigo ya moyo, kulikuwa kimiya…keshakufa masikini ya mungi…Oh Maneno akasimama na kuanza kupiga kurukaruka, halafu akasimama mwili mzima ukaanza kumwishia nguvu..halafu baadaye akapiga moyo konde na kusema sio muda wa kukata tamaa, hata kama keshafariki afadhali wakajulie huko huko hospitalini..wazo la kuwa keshakufa hakulitaka kabisa liingie akilini mwake …hapana usife shemeji, kwanini ukimbilie kujiua , hujui tupo wengi tunaokupenda…wazazi wako wanakuhitaji sana, jamaa zako, na mimi mwenyewe nipo kwa ajili yako..oh, usife Maua ….akajikuta akilia kama mtoto mdogo
Aliona ni heri ampigie simu dakitari wao wa kazini aje haraka, lakini alipowaza zaidi na kujiuliza zaidi kuhusiana na swala la sumu akaona ni vyema amkimbize hospitalini,huenda hajafa kapoteza fahamu tu, na kama kanywa sumu ambayo ni mbaya sana, huko hospitalini wanaweza wakafnya juhudi hata za kumfanyia upasuaji na huenda wakamuokoa maisha yake,…akaanza kazi ya kumbeba, ilikuwa kazi nzito kweli na hata alipomfikisha kwenye gari alikuwa yupo hoi kwani ulikuwa mzito na hali ile ilimfanya Maneno ahisi mbali kuwa huenda alikuwa kabeba mwili usio na uhai….akaondoa gari haraka hadi hospitaini na huko akapokelewa na kuingizwa chumba maalumu cha uangalizi maalumu…na hapo akapumua kidogo, kwani kule kupokelewa na dakitari …halafu wamkimbize moja kwa moja kwenye humba maalumu, akaona ni bahati, siunajua tena…
Sasa ikawa kazi ya kutafuta mawasiliano, ukumbuke kipndi cha 1996-7, simu za mikononi hazikuwa nyingi sana, na waliokuwa wakitumia ni wachache , kwahiyo hata ukiwa nayo unaweza uakapata shida ya mawasiliano, zilikuwepo lakini watumiaji waliobahatika kuwa nazo ni wachache, na alijua kabisa familia ya akina Maua wanatumia simu ya mezani, kwahiyo akawa anatafuta kibanda cha simu awapigie…lakini wazo likamjia kuwa ni vyema akasubiri kwanza asikia taarifa ya dakiatari kuwa huyo mtu yupo hai au ndio….hapana sitaki kuwaza hivyo hajafa….Maua hajafa….ngoja asogee karibu na kile chumba cha waginjwa mahututi amsubiri docta ili ajue atasema nini kwa wahusika…Na baada kama ya nusu saa mara docta akatoka kutoka kwenye chumba maalumu na akamsogelea yule dakiatari…
Nisingependa kumalizi hapa kwa leo, lakini umeme umekatika….balaaa...Maoni yaje!
Ni mimi: emu-three
9 comments :
kama kawaida yangu sichoki kuzuru humu.... kila nimalizapo kusoma lazima nishushe pumzi kwa nguvu sana.
ahsante sana kwa simulizi zenye kusisimua.
Fadhy Mtanga nashukuru sana kuwa wakati wote tupo pamoja, KARIBU SANA, NA SHUKURANI ZA ZATI ZIENDE KWAKO
Simulizi nzuru usipofanya yale niliyokushauri wajanja watatajirika mikononi mwako. Kusanya zile za mwanzo tafuta publisher wa kitabu, hata kama paperwork kwa njia hiyo utalinda kazi zako. Utakapopata uwezo utapublish toleo la pili kwa publisher mzuri ndivyo wanavyofanya hivyo.
Subira
mambo mazuri m3 ni nakuamini sana yaani inasikitisha natamani isiishe
duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh. umeme noma
Ni kweli Subira, hilo naliona, ...najaribu sana kufanya hivyo, ila ndio sijui nifanyeje, maana unategemea computa ya mwajiri, nafasi yake ya kazi ujiibe, ....ni kazi kweli kweli....lakini ndivyo ilivyo, juhudi na dhamira vinaleta mafanikio, na nawaomba hawo wenye nia hiyo ya kuchukua jasho la mtu , wafikiri mara mbili, kwani asho la mtu haliliwi, ....cha mhimu ni kuchukua print-out kama unataka kusoma, hiyo haikatazwi, ila kuchuku kazi hapa na kutunga kitabu , au kuigizia tamithilya ni vyema tuwasiliane kwanza!
Tupo pamoja wapenzi wa blog hii, endeleeni kutoa maoni ili mori upande..lol
Hebu nunua kitabu au hivyo vitabu vinavyouzwa kwenye meza za magazeti vya elfu moja moja au elfu mbili mbili, kama vya aina mbili tofauti, kisha angalia nyuma yake nani amepublish. Kisha pitia duka la vitabu angalia publishers vya vitabu vya hadithi kama zako ni nani. Njoo na list ya publishers niandikie kwa email yangu nitakushauri cha kufanya.
Subira
Mpendwa subira, nimejitahidikutafuta e-mail yako sijaipata naomba unitumie kwa e-mail, kama hutojali!
Wow that's awesome news about your insha keep it up
Post a Comment