Docta Adamu alichukua kipimo chake na kukiweka kifuani kwa yule mgonjwa, aliskiliza kwa makini halafu akakiondoa, alipeleka kidole kwenye jicho la yule mgonjwa , akabenua mboni za macho yake akatizama halafu akamfunua shuka alilofunikwa na kumkagua maungoni, …akachukua kadi na kuandika maelezo halafu akamwambia nesi kuwa ampeleka huyu mgonjwa kwenye chumba cha uchunguzi na uwaite madakitari wengine tukutane huko…
Mgonjwa alipofikishwa kwenye chumba cha uchunguzi, madakitari wengine walishafika na kumsubiri docta Adamu ambey alitoa maelezo mafupi ya huyo mgonjwa na kila mmoja akapewa kazi ya kumfanyia uchunguzi kutokana Nyanja yake, na hiyo imekuwa kawaida yaoo hasa kwa madaktari waliofika hapo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
‘Kila mmoja alileta uchunguzi wake kwa dakitari Adamu , ambaye alitikisa kichwa na kusema kuwa ndivyo hivyohivyo alivyokuwa akizania, kuwa huyu mgonjwa ana `Naimonia’(pneinomia), na malaria nyingi,….kwahiyo inabidi aanze matibabu haraka….’ Akasema dakitari Adamu, na kaundika maelezo ya ni dawa gani apatiwe na maelezo mengine…
‘Lakini docta huyu mgonjwa kaletwa tu hapa, hana ndugu, na hatujui hata jina lake, hilo kwenye kadi tumeamua kuandika tu, na waliomleta hapa wameshaondoka, sasa hatujui gharama yake atalipa nani…….’ Akasema dakitari mmojawapo
‘Kwasababu tumeshaanza kumfanyia matibabu hilo tutalijadili baadaye cha muhimu tufanye juhudi za kupambana na matatizo aliyo nayo, na je taratibu za kisualama zimechukuliwa, yaani polisi wanalijua hili, kwani kama kaokotwa …umesema wapi?’ akauliza docta Adamu.
‘Walimkuta ufukweni mwa ziwa Victoria, hawa na wavuvi na haraka wakajaribu kumzindua lakini hakuzindukana na wao walijua keshakufa, na juhudi za kumjua ni nani zilishindikana , wakatoa taarifa polisi, na polisi na hawo raia wakamleta hapa wakiwa na nia tukauhifadhi mwili wake wakijua keshakufa, hata sisi tulijua hivyo, na wakati tunataka kumchoma sindano ya…’ akasimama kidogo yule Dakitari akimwangalia yue mgonjwa kwa mashaka kwani yeye bado hakuamini kuwa bado yupo hai
Tuliona mabadiliko fulani mwilini kuonyesha kuwa bado yupo hai , nilipompima tena nikaona ni mzima, kwahiyo ndiyo tukakuletea taarifa…kwa ujumla hana ndugu… na polisi walisema kuwa waliona karatasi iliyokuwa na namba za simu, na namba hizo sio za hapa nchini…huenda ni za nchi za jirani, na hilo polisi wanalifanyia kazi…’ akasema yule dakitarialiyempokea huyo mgonjwa.
‘Sawa kabisa sisi kama tulivyosema tunatimiza wajibu wetu, na kazi kama hizi wakati mwingine unacheza pata potea, unaweza ukamtibua baadaye ukapata gharama zako na zaidi au ukakosa kabisa, kwasababu huyu ni binadamu hatuwezi tukasema tumwache tu mapaka kijulikane …kwahiyo tuendelee na akzi yetu kama kawaida, ila nawaombeni tena msipende kupokea wagonjwa kama hawa, wakiletwa waambieni polisi wampeleke hospitali za setrikali, tutampokea kama dharura, baada ya hapo inabidi tuwaarifu serikalini kwasababu gharama zake kama hazitapata mlipaji inabidi tuzipeleke serikalini ili watulipe, na unajua ufuatiliaji wake …tutamaliz amwaka hatujalipwa….’ Akasema Docta Adamu.
‘Sasa mgonjwa huyu inabidi tumakabidhi nani ambaye atahakikisha kuwa kila kitu kinaenda salama na uslama wake, asije akapona akatoroka, nani ambaye hana majukumu kwa sasa…’a akuliza docta Adamu.
‘Rose, hana majukumu kwa sasa, naona tumkabidhi huyu mgonjwa…’ akasema yule dakitari mwingine
‘Rose mwenyewe yupo wapi?’ akauliza Docta Adamu
‘Ametoka kidogo kupata chochote..’ akaavyo alivyombiwa,
‘Basi muiteni nimpe maelekezo yote …..’ akatoa amri docta Adamu
Docta Rose, alikuwa ndio karudi toka likizo na siku ya kwanza ya kazini ukiwa umetoka likizo inakuwa ya kutegatega, kwani unakuwa hujakabidhiwa majukumu, na mwenzako, huwa naye anamalizia kazi zake alizokuwa kaanza nazo, na hapo nawe unapata nafasi kusalimiana na wenzako hapa na pale, ndivyo alivyokuwa kafanya Maua na kuwaaga wenzake kuwa anapata chochote kumbe yupo kwa shoga yake anapata yaliyotokea wakati hayupo naye kuelezea kuhsu likizo yake.
‘Nasikia kuna mgonjwa mahututi kaletwa hapa hospitalini na madakitari wote wapo huko wanamhudumia vipi wewe, mbona upo nje, umemsahau docta Adamu, hajabadilika, ujue ukiafanya maksoa kazi hauna na ukiitwa na yeye kuna mawili, kupandishwa cheo au kufukuzwa kazi, …hizo bado ndizo tabia yake , nikukumbushe kama umemsahau….’ Akamwambia shoga yake.
‘Nimsahau Bosi,, hata nikiwa likizo nilikuwa namuwaza yeye , hata nikisikia mtu ananiita jina langu nabakia kujiuliza isije katumwa na Bosi, ….’ Akasema Maua na kabla hajawacheka mara mlango ukafunguliwa.
‘Maua unaitwa na Bosi….’ Akasema nesi akiwa kashika sinia la madawa.
‘Mungu wangu nini tena, ndio nimefika leo, Bosi kajuaje,…” akasema Rose akiinuka haraka haraka kutoka nje.
Rose ni miongoni mwa madakitari walioajiriwa karibuni, baada ya kumaliza masomo yake udakitari na kufanya kazi kidogo hospitali za serikalini na baadaye akapata nafasi hapo kama dakitari, na amekuwa mchapakazi mzuri, lakini mbele ya docta Adamu, huwezi kukosa kukosolewa, hana simile katika aina yoyote ya uzembe, hutaamini hata licha ya kuwa dakitari mkuu wa hiyo hospitali, lakini anaweza akaingia muda wowote hata usiku kufanya kazi na madakitari wengine.
Rose alipofika hapo alipenda sana uchapakazi wa dakiatri huyu na akaahidi moyoni kuwa atajituma kaam yeye kwani alikuwa na mipango ya mbeleni ya kuanzisha zahanati yake. Lakini kila alivyojaribu aliikuta kama kasimama wakati mwenzake anakimbia, kwahiyo anakijuta aanacwa mbali ajabu.
‘Huyu dakitari ana mapafu ya mbwa ina maana hachoki na kila kitu anakijua, ….mmh, kweli sidhani kama nitamuweza huyu na kweli anastahili kuitwa dakitari mkuu..’akasema Rose siku moja
‘Rose ukitaka ufanikiwe katika hii kazi yetu uhakikishe unajitolea, kwani kazi hii ni wito, na ili ujue vyema, inabidi uwe mwepesi kujifunza kitu kipya, uwe karibu sana na wagonjwa, uweze kuwajua vyema, usichoke, na usionyeshe dharau, yoyote kwako ni mgonjwa wako….na uwe mwepesi kusoma, kubukua kila kitu kinachohusu fani yako…tafuta kwanini,….hiyo ndiyo siri ya mafanikio…’ akakumbuka siku moja alivyoambiwa na dakitari huyu. Na akajitahisi mara kwa mara kufanya hivyo, lakini alijikuta akichoka kwani kila akimaliza zamu yake, hujikuta keshachoka na sasa eti ajitolee kufanya kazi nyingine au ajitolee kufanya hili na lile…..oh, alijikuta anataka kuzimia, akasema kwanini nijitese, wakati mshahara ni ule ule….hapana, nitakuwa nafanya kadiri ya uwezo wangu..
Alikumbuka kuwa likizo hii alipewa kama `onyo’ ingawaje alistahili kupewa likizo yake ya mwaka, lakini kulitokea uzembe fulani yeye akiwa dakitari wa zamu, na adhabu yake ikawa ni kwenda likizo huku uchunguzi unafanyika na akirudi atakuta taarifa kuwa anaendelea na kazi au basi….na aliporudi likizo hii bado alikuwa hajiamini kuwa kazi ipo au ndio basi tena, na kurudi tena serikalini aliona hatapata maslahi kama hapo, na je hata hivyoo watampokea wakati aliondoka kienyeji….hata hivyo hakukata tamaa akijua kuwa yeye au wenzake hakuna aliyefanya makosa ni uzembe wa mngonjwa mwenyewe tu….sasa sijui ndiyo hivyo anaitwa kwa dakitari mkuu ili kupewa barua ya kusimamishwa au kuendelea na kazi..
Rose alifika chumba cha dakitari mkuu, na kabla hajagonga mlango akasikia mtu akija kwa nyuma yake, na alipogeuka akajikuta ana kwa ana na Docta Mkuu, Docta Adamu, alimuona akiwa bado kweney vazi la kikazi…balaa …..anaonekana kakunja uso hii ni ishara mbaya , ngoja nimsikilize kwanza
‘Shikamooo bosi….’ Akasema Rose akiwa kashikwa na kigugumizi..
‘Usiniambie umerudi toka likizo na hutaki kuja kutoa taarifa…na ulikuwa wapi wakati wenzako tunahangaika kwenye chumba cha uchunguzi, unafikiri kwa namna hiyo utafikia malengo yako, kazi ya udakitari ni wito, kujituma, umeenda likizo umeshalemaa, sema kama unataka nikuongezee siku …na ujue zikiisha na kazi imekweisha..njoo ndani kuna kazi maalumu kwako ’ akasem Docta Adam, huku akimkaribia Docta Rose, akashngaa Bosi wake ananyosha mkono wa kusalimiana naye. Naye kwa wasiwasi akaonyosha mkono wake laini..
‘Bosi ndio nilikuwa ..nilitoka kidogo kupata chochote…siunajua tena nilishazoea kula…sasa kupoteza muda wa kula ..’ akasema Rose huku akijiumauma, na wakati huo akitikiswa mkono kwa ile salamu ya kiume, ya kutikisana mikono…aliposhikwa na ule mkono wenye nguvu na kutikiswa alisikia kama bega linataka kutoka…
‘Sikiliza kwa makini , kuna mgonjwa kaletwa hapa, na huu ndio mtihani wako wa kuendelea na kazi hapa, vinginevyo utarejea huko ulikoharibu na sizani kama utapokelewa, ….najua unalijua hilo…na ukiacha hapa hata cheti chao kitaharibika siunajua hilo sasa kazi kwako. Sikiliza kwa makini…huyu mgonjwa hajulikani ni nani…kuna habari toka vyombo vya usalama, kuwa kuna watu ambao wanatafutwa…usiniulize kwanini, kama ujuavyo nchi yetu bado inaandamwa na vita!
Docta Adamu akawa anafungua mlango wa ofisini kwake huku anaongea na kusema `Sasa hatujui huyu kama ni mmojawapo wa hao wanaotafutwa au ni mtu baki, ila kaokotwa ufukweni, kwa taarifa za siri na iwe siri yako, huyu anaweza akawa mmoja ya watu wanaotafutwa, sasa, kazi kwako kuhakikisha anakuwa katika mikono yako, ujue ni nani, ujue anataka nini, ujue kilitokea kitu gani mpaka akafika hapa, na ole wako akitoroka…ukumbuke huo ndio mtihani wako wa kuamua kuwa unaendelea na udakitari au unataka kwenda kula-kula nyumbani…hata hivyo nina barua yako toka huko ulikochafua, sijui kama…inasemaje, huenda unatafutwa, sijui…hilo huko halihusu sana,…lakini hata hivyo…ok wewe soma hiyo barua halafu utaniambia inasemaje nisije nikawa nakupa kazi kumbe huhitajiki tena hapa…
Rose alijikuta akiishiwa na nguvu, barua toka serikalini, wizara ya afya… ina maana wameshajua kuwa nipo hapa na huyu dakitari wangu keshanijua kuliko alivyopanga kuwa atafanya kazii huku anatafuta mwanya wa kwenda nje kuongeza elimu yake, ina maana …hapana haiwezekani, kama ni hivyo hatakuwa na maisha mazuri hapa kazini, ni bora arudi serikalini akawapigie magoti,….lakini hapana kwanini nirudi serikalini , ….siwezi kuogopa, lazima nipambane kijasiri, na siri ya kazii kama hizi ni ujasiri…akapiga moyo konde na kumfuata docta mkuu ndani ili pate maelezo ya huyo mgonjwa au na kupewa hiyo barua , na ili ajue moja kuwa ni hitimisho la kazi aui…….
NB. Haya haya, hapa ni uwanja wa madakitari, hawa ni watu muhimu sana katika kisa hiki, ...kutana na Dakitari Rose, mtaona makali yake kwenye kisa hiki. Tuendelee kuwepo
Ni mimi: emu-three
3 comments :
daah sitamani iishe. poa bwana tunasubiri uhondo zaidi
mambo jamani ivi kumbe amekaa eda ya bure m3 wewe hodari nakupa 100
big up
M3 me hapo hata cjapapata pata fresh pamenchanganya kdgo ila pia kinavutia hcho kisa cha madaktar chaleta hamasa ya kufatilia kujua kilichopo nyuma yao hao Dk.Rose,Dk.Adam na huyo Mgonjwa yan am consly 2 continue... Pia ts gud idea kuwa na visa mchanganyiko Keep t up gal
Post a Comment