Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, November 11, 2010
Asiye na bahati habahatishi-1
King’ora cha gari la wagonjwa kilisikika, na watu wengi wakawa na hamu ya kujua kuna nini tena, mambo ya uchaguzi yameisha watu wanatka kuishi kwa amani, na huku maeneo yajulikanao kwa watu kama maeneo ya uswahilini, kitu kidogoo ni habari kubwa ya kujaza ukurasa wa gazeti. Na ujuavyo kwa maeneo kama haya watu hawapitwi na jambo, kwani wengi wapo kijiweni hawana kazi kwahiyo umbea na ufutiliaji wa hata yale yasiyowahusu ni moja ya kazi zao za kupoteza muda.
Kwa wale wasiopitwa na kitu waliamua hata kuomba baiskeli kwa jirani na kufuatilia ili kufuatilia nini kulikoni, na kweli jamaa wengi waliamua kulifuatilia hilo gari la wagonjwai hadi pale hilo gari liliposimama kwenye nyumba moja kubwa, iliyozungushiwa geti . Na liliposimama tu wahudumu walitoka ndani ya gari kwa haraka na kuingia ndani ya nyumba moja nzuri iliyozungushiwa ukuta.
Watu wakaanza kuongezea, mmoja baada ya mwingine nje ya ile nyumba huku kila mmoja akisema lake, na minong’ono ya watu wengu huwa ni sauti kuu. Naa wakati wananong’onezana, mara machela ya kubebba wagonjwa ikatolewa na kuingizwa ndani ya nyumba ile, na baada ya muda, maragari la polisi likawasili na askari waliovalia nguo sare zao wakaingia ndani ya nyumba ile. Na hapo minong’ono ikazidi ikisema lazima kuna uhalifu umefanyika ndani ya nyumba hiyo.
‘Nyumba za wakubwa hizi hazikosi ufisadi, kuna kitu humo, huenda wameuna…’ ilimradi kila mwenye lake kichwani akaona alitoe.
Baada ya dakika chache machela ile ilirudi toka ndani ikiwa imebeba mwili unaosadikika ni wa mgonjwa au maiti. Hapo hata wapiga picha na waandishi wa vichochoroni wakaona wasipitwe na jambo wakachukua picha zile za chapuchapu, na hata za macho ilimradi kila aliyena asikose cha kuonyesha au kuelezea kama vile alihusika katika tukio hilo angalau hata kwa uongo.
Askari polisi nao walitoka baadaye na kulifuatilia lile gari la wagonjwa kwa nyuma, na hapo watu wakaaanza kusambaa. Kesho yake maandishi makubwa yakaonekana kwenye vichwa vy vyombo vya habari hasa yale ya udaku yakikoleza na chumvi. ‘MSICHA MMOJA AAMUA KUJIUA BAADA YA KUKOSA BAHATI YA KUOLEWA…’ Mengine yaliona aibu yakaandika `Msichana mmoja ataka kujiua kwa dawa.’na kichwa kilichonivutia ni kile kilichosema `Ama kweli asiye na bahati habatishi, dada kanywa dawa kujiua’
Kwenye maelezo ya magazeti haya hayakuweza kuandika maneno yenye uhakika kuwa ni kwasababu gani msichana huyo alitaka kujiua zaidi ya maneno ya kusadikika na dhana zisizo na uhakika, kwani hakuna aliyekubali kueleza chochote hata polisi walichosema ni kuwa msichama huyo jina limehifadhiwa amekunywa madawa mengi na haijajulikana ni kwanini.
Kesho yake mdau wetu mmoja alitembelea ile hospitali akiwa na sare za udakitari, kwani ingawaje ni mwandishi wa kujitegemea lakini kazi yake rasmi ni ya udakitari na ana hospitali yake binafsi na mara nyingi anaalikwa kufanya kazi kwenye hii hospitali alipoletwa huyu mgonjwa au maiti. Na bahati nzuri katika pilikapilika zake akaitwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kusaidiana kuokoa maisha ya huyo binti, amabye alikuwa kwa muda ule amepoteza fahamu kabisa, na haijulikani hatima yake.
Na katika kuhangaika, Yule mgonjwa bahati akazindukana baada ya kuwekewa maji na huduma za mwanzo. Alianza kwa kulia maumivu ya tumbo na kulalamika huku na kule kuwa tumbo linamuuma sana. Na madakitari waliomchunguza wakaona hali ile haifai kwenye hiyo hospitali, inahitajika apelekwe hospitali kubwa kwa ajili ya upasuaji,kwani kwa maelezo ya wanafamilia inasadikiwa kuwa kanywa nyingi, kutokana na pakiti iliyoguinduliwa pale mezani. Na hata alipozindukana alisema yeye alikuwa akinywa dawa hizo, lakini hakujua kuwa kanywa nyingi kiasi hicho.
Madakitari walipompima walisema dawa alizokunywa sio tu zimeleta madhara kwa huyu mwanadada bali pia zimeharibu mimba ya miezi sita tumboni, kwahiyo ikawa haina jinsi zaidi ya kufanyiwa upasuaji na kuondoa kiumbe kilichopo ili kuokoa maisha ya mwana dada huyo.
‘Mwacheni afe, kwanini anywe madawa yote hayo, inaonekana alikuwa anataka kujiua,..’ akasema nesi mmoja.
‘Wewe sister usiseme hivyo, unajuaje kuwa alitaka kujiua haya mambo wazungumze watu wa mitaani na sio wewe na kazi yako..’ akazungumza jamaa mmoja anayesadikiwa ni ndugu wa karibu wa huyo msichana aliyekunywa madawa mengi.
Mdau wetu alinitonywa kuwa huyo msichana yupo katika hali mbaya na yakwamba asipofanyiwa upasuaji wa haraka huenda akapoteza maisha. Lakini alichogundua ni kuwa huenda msichana huyo hakuwa na dhamira ya kujiua, kwani kila alipokuwa akilalamika alikwa akisema yeye hakukusudia kujiua alikunywa dawa tu kama kawaid, kumbe alikuwa kapitiliza vipimo. Lakini cha kushangaza alipoulizwa alikunywa vidonge vingapi, hakuweza kusema idadi halisi yeye aisema kuwa alijikuta amekunywa kipakiti kizima alichopewa toka hospitali kwa ajili ya tiba ya malaria.
‘Huyo msichana ana akili timamau kweli,,’ nikamuuliza mdau wetu
‘Anayo akili safi kabisa na mimi namjua ingawaje sio kwa undani sana’ akasema mdau wetu na akaahidi kufuatilia tukio hilo kwa karibu ili kujua nini kilichomfanya msichana huyo mrembo kumeza madawa yote hayo, huku akidai kuwa hakuwa na dhamira hiyo.
Naona tuachie hapa ili tuweze kukusanya maelezo yote ya kisa hiki, nawaomba tuwe pamoja kwenye sehemu ya pili.
mimi: emu-three
12 comments :
Yaani ni kisema wewe mkali namaanisha mkali kweli kweli. Du! tumetoka kwenye kutembelea huku tu usingizini sasa twaingia kwenye kupoteza kumbukumbu. Haya mie nasubiri sehemu ya pili hadi ya mwisho, keep it up maana kazi zako si za kitoto. All the best my dear mungu akupe afya njema na nguvu tele ili tuendelee kujifunza kutoka kwako.
mmh haya ngoja tuone itakuaje ..ina maana alikunywa dawa bila kujijua ??
Nimenakilisha stori zako zote na kuziweka pamoja kama kijarida fulani hivi. Niko nazisoma pole pole. Kwa hivyo usiponisikia hapa mara kwa mara usitie shaka. Tuko pamoja!
U mwandishi mzuri sana; na kama Elisa alivyosema huko nyuma pengine itabidi utafute gazeti lenye wasomaji wengi uzipeleke huko ili ziweze kusomwa na watu wengi - hata kule kwa Shigongo sawa tu. Ni hadithi zenye kugusa sana na zinaonyesha mapambano na mitihani tunayokutana nayo maishani kwa ufasaha zaidi. Mtu wa kawaida anaweza kujisoma humo na kujiona. Na baadaye itakuwa vyema ukizichapisha kabisa kama kitabu.
Kinachovutia zaidi ni kwamba mwenyewe umeamua kuwa "anonymous" - kimyaaa, hakuna jina, hakuna picha wala nini. Unakamua tu kimya kimya. Safi sana!
Nitaendelea kukufuatilia daima.
Hii nimeanza nayo. Na wakati nakusanya nguvu za matoleo yaliyopita, ninataka ku-keep up na hii.
Huyu dada alitaka kupona kwa siku moja (may be)
Lol
Haya ndugu. Tukingali pamoja kwenye changamsha bongo hii.
KIPAJI KI-NDANI MWAKO
ASANTE
Hadithi njoo utamu kolea!
"Kinachovutia zaidi ni kwamba mwenyewe umeamua kuwa "anonymous" -Matondo.
Mtizamo wangu ulikuwa kazi yangu ndiyo ijitambulishe kama mimi. Nilikuwa naogopa kuwa huenda nihisivyo kuwa najua kwa mtizamo wa wanajamii sijui kitu. Unaweza ukajiona unajua kitu fulani, kumbe kwa wenzako ni `upuuzi'.
Kweli kuna haja ya kuandika visa hivi kwenye magazeti makubwa kama ya akina Shigongo. Lakini je utapata nafasi hiyo? Nitafanya hivyo kama kweli wapenzi wangu mtaniunga mkono ni kuniambia sasa unafaa `kujitoa hadharani' Lakini kwa sasa ngoja nijenge uzoefu huu!
Nashukuruni sana kwa kunipa moyo na kukubali kuwa `najaribu' nangoja siku ya kuambiwa `unaweza' basi nafikiri nami nitajitambulisha rasmi, na sio `anonyimous'
Haiyumkini alikuwa hajui madhara ya dawa hizo za malaria, au alipewa maelekezo kutoka hospitali yasiyokamailika (Kama kawaida ya hospitali zetu) au malaria ilisha anza kupanda kichwani na alichokuwa anafanya hana kumbukumbu sahihi!
Mwisho wa stori hii utanena.
Enhe enhe enheeeeeeeeeeee, mambo mazuri mengine yanaanza, najibanza hapa hapa siendi kwengine
Hata usipojitambulisha, mimi nasema ambalo niliwahi kusema. UNAWEZA
Na licha ya kuunga mkono idea ya kuchapa kwenye magazeti, natanguliza suala la KUTOA KIJARIDA.
Hicho kitakuwa chako, kitahusu wewe na kazi zako na sio kuonekana kuwa na MRENGO WA WALE WACHAPAO MAGAZETI
BARAKA KWAKO NDUGU
Mhh, jamani Ijumaa imepita hivihivi, mnisamehe sana, nilibanwa na kazi za watu, msiwe na wasiwasi, sehemu ya pili ipo, ni swala la kuiweka hewani tu, mnisubiri kidogo, nimalaizane na majukumu!
Nashukuru sana kwa maoni yenu wadau wenzangu, nami nitajitahidi kuyafanyia kazi. Karibuni sana, kisa kinaendelea tuwepo karibu!
heeh jamani na jumamosi pia imepita na jumapili...sasa jumatatu..mmh..una mpango gani na sisi
Oh, samahanini sana wapendwa wangu, sehemu ya pili imeshakamilika, lakini nafasi ya ku-edit na kuiweka hewani inachelewa kidogo kwa sababu waajiri wangu wamenikalia kichwani. Lakini msijali, naitoa sasa hivi..! Kama kutakuwa na makosa kidogo muniwie radhi!
Post a Comment