Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 11, 2010

Utangulizi wa kisa kipya-asiye na bahati habahatishi!

Wakati mwingine watu hukutana na mikasa bila makusidio yao, kwa kutokujua au kwa kutokuwa na ufahamu wa chanzo la tatizo hilo. Wapo watu wamehukumiwa au jamii kuwaona hawafai na hata kulaumiwa kutokana na tatizo fulani, ambalo linatokana na sababu zilizojificha, na kama lingedundulika mapema, huenda matatizo hayo yasingetokea. Wakati mwingine inakuwa kama kuangalia matawi bila kujali shina, na mizizi.


Kisa kijacho kinaibua hisia za ndani za mwanadada aliyehisiwa kutaka kujiua kwa kuhisi yeye ana mikosi, lakini wakati alipoulizwa kwanini alitaka kujiua yeye alidai hakukusudia hivyo na hakumbuki kuataka kujiua! HAKUMBUKI, hii hakumbuki ikamkuna mtaalamu wa mambo ya akili.

Katika kuhangaika kumsaidia huyu mwanadada, mtaalamu wa mambo ya akili, aliamua kuingilia hili swala bila kujali gharama, na mwisho wa siku aligundua ugonjwa ambao hata familia ilikuwa haikugundua hilo. TATIZO LA KUSAHAU. Wengi wanaona kuwa ni tatizo la kawaida tu, na humtokea kila mtu. Lakini kuna kuzidi kiasi.

Nilipopata hiki kisa, niliona nitafiti zaidi kuhusiana na hili, je kusahau kunaweza kumfanya mtu akafanya mambo hata ya kuhatarisha maisha yake. Niliona nimtembelee `Subi, a Nurse (RN) ‘ kwangu mimi nitamtambua kama dakitari "Subi" , na nikakutana na makala yake inayoelezea tatizo hili, soma makala hiyo kwa kubofya hapa:

http://www.afyachoice.com/2/post/2009/11/ugongwa-wa-kusahau-alzeheimers.html.

Na niliposoma makala hii nami, nikapata nguvu za kukielezea kisa hiki ambacho kwa jina kinaitwa, tutakiita `ASIYE NA BAHATI HABAHATISHI’.

Katika utangulizi huu wa kisaki kisa, ni kutaka kukuweka bayana kuwa wakati mwingine ni vyema tukio linapotokea tukajarbu kufanya uchunguzi wa kina, kwanini hilo tukio limetokea, na ukidadisi zaidi utagundua kumbe kuna chanzo kilichojificha ambacho kwa kukigundua utakuwa umesaidia sio tu kwa mlengwa bala hata kwa jamii nyingina. Mimi naona ajabu kuwa wanaofanya tafiti kama hizi ni wanasayansi tu, kwanini katika maisha ya kawaida tusifanye hivyo, na kwa kufanya hivyo tunaweza tukagaunuda mengi, ili kurahisisha tatizo hilo baadaye.

Kisa hiki kinatoa fundisho kuwa tuwe wadadisi wa kila jambo, huenda tukajisaidia wenyewe na hata kuwasaidia tuwapendao, kwani watu wengine hukata tamaa za maisha kwa kukosa msaada wa kiutafiti. Na utafiti mwingine sio lazima uende hospitalini, unaweza ukaangalia historia ya tukio linalojirudia rudia ukagundua kuwa kuna sababu muhimu. Je nifanyaje, nikamuone nani?

Nawapongeza sana wataalamu, au madakitari bingwa wa matatizo fukani au wa magonjwa Fulani,kwani wao hawarukii kuangalia tatizo au gonjwa, wanajaribu kuangalia kiini na nini chanzo chake na hatimaye wanakuja na tiba ambayo huondoa tatizo na kiini chake.

Kisa chetu hiki ni miongoni mwa mfululizo wa visa vyenye mkono wa kitaalamu na tunavitoa ili jamii isikimbilie kuangalia tu tukio au tatizo . Na hili tunaweza kulifanya kwa watoto wetu, kwa kuwachungua bado wakiwa wadogo, kwanini mtoto wangu hasikii nikimwambia hili, kwanini mtoto wangu ana kuwa na tabia ya kunyamaza kimya, kwanini mtoto wangu anakuwa na tabia hii. Kwa kudadisi huku na kuchunguza mienendo ya watoto wetu tunaweza tukawasaiida mapema kabla tatizo hilo halijakuwa na kumletea madhara..

Karibuni sana, kwenye kisa kipya cha `Asiye na bahati habatishi’ Na tutaanza moja kwa moja na tukio lilivyoanza. Kwenye sehemu ya kwanza.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Ni kweli M3, Nimpenda huu utangulizi na najua kinakuja kitu chenye mafundisho, sio kuburudisha tu, lakini ukisoma unakuwa na mwamko fulani. Wewe sasa unaonyesha ulivyokomaa kiuandishi!
Una vitabu vingapi? ningependa kupata nakala moja, manake sidhani kama hujaandika kitabu hata kimoja!

Simon Kitururu said...

Sijui kwanini sijapenda umeweka utangulizi huu ingawa sijui stori yenyewe. Nahisi kama umenikata baadhi ya utamu wa kusoma stori huku nikijaribu kubunia ni nini hasa kiini cha fundisho au ni nini stori inataka nistukie kutokana na imajinesheni zangu mwenyewe.

Na sijui kwanini ningependa ungekuwa unaweka kitu kama hiki kwenye hitimisho baada ya siye wakereketwa wa stori zako kumaliza kukusoma.

Ni mtazamo wangu tu Mkuu!

Pamoja sana Mkuu!

emuthree said...

Ni kweli mkuu, SIMON, hata mimi nimeiona hiyo, kwani kwa kutoa huo utangulizi umekuwa ukinibana niendano sana na wenyewe. Lakini ni kwasababu ni tukio lenye ukweli, sio tamithilia, ndio maana nikaamua kiweka kila kitu hadharani.
Nashukuru sana kwa wazo hili, nitajitahidi kufanya hivyo kwenye visa vingine.
Karibuni sana, na michango kama hii naipenda sana, kutoa wazo iweje, kama kuna kosa lirekebishwe, kwanii utamu wa kitu nii kila mtu akionje!