Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, November 15, 2010
Asiye na bahati habahatishi-2
Polisi ya idara ya upelelezi ilikuwa imemaliza kuandika maelezo yake na mkuu wa idara hiyo alitakiwa kukutana na waandishi wa habari , lakini alikuwa na mashaka juu ya maelezo yale, na akawa anajadili akilini mwake hicho atakacho kieleza kwa waandishi wa habari. Kutokana na uchunguzi wao , waligundua kuwa huyu mwanadada alitaka kujiua kutokana na mikasa ya maisha yaliyomzonga. Lakini kwa mara nyingi mtu anayetaka kujiua anaacha ujumbe au anakiri mwenyewe kuwa alitaka kujiua kwasababu kadhaa, kama hakufanikiwa kujiua. Lakini kwa maelezo yaliyopo mshukiwa kakataa kabisa kuwa hakutaka kujiua!
Aliwaza sana akaona kama atawaambia waandishi wa habari haya maeelezo, halafu baadaye igundulike vinginevyo, kazi yake inaweza ikaingia doa. Na mjomba wa huyu mtoto anayeishi naye ni mtu muhimu sana serikalini, akaona ni vyema avute muda na kama ikiwezekana afanye uchunguzi wake binafsi, ili kuhakiki maelezo aliyopewa na watendaji wake. Wakati mwingine inabidi uhakiki kwa vitendo, kama mkuu, vinginevyo unaweza ukathibitisha kitu chenye makosa. Akamuita msaidizi wake na kumwambia anataka wafuatane naye hadi hospitalini ili kama inawezekana akaongee na huyo mshukiwa ili kuhakiki baadhi ya maelezo.
‘Kwani kuna makosa mkuu…naona tukio lenyewe linajieleza, huyu binti aliandamwa na mikosi mmoja baada ya mwingine, nafikiri akaona hatua iliyobaki ni kujiondoa duniani, ushahidi tumeupata kwa wanafamilia wenyewe na dawa alizokunywa, hii ipo wazi mkuu, au unafikiriaje …’ masaidizi wake akashangaa, kwani tukio hilo kwakwe aliliona ni dogo sana, halistahili mkuu wake kuliingilia kati.
‘Hapana, nimevutiwa na maelezo yake, na hii ni kawaida kuhaikiki hizi kazi kwa vitendo, hata hivyo, huyu jamaa, mjomba wa huyu binti siunajua ni mtu muhimu sana serikalini, kama tutatoa haya maelzo kama yalivyo, halafu baadaye ionekane hatukufanya kazi vyema, tutakuwa matatani…..’ akasema huku anaingia ndani ya gari kuelekea hospitalini.
Alipoingia kwa dakitari, akaambiwa dakitari yupo na mgonjwa ambaye amefanyiwa operesheni karibuni, kwani keshazindukana. Yule askari aliposikia hivyo akakimbilia kule wodini, na akakuta dakitari anamhoji Yule mgonjwa. Yule mgonjwa alikuwa akilia, na mara nyingi alikuwa akikataa kuwa yeye hakuwa na nia ya kujiua, na hajui iliokeaje akameza vidonge vingikiasi hicho. Wakati anamhoji aliingia dakitari mtaalamu wa maswala ya akili, akasikiliza yale mahojiano, baadaye akamuomba daktari muuguzii ampe muda wa kuongea na huyo mgonjwa.
Yule askari mpelelezi mkuu wa kituo alishafika humo wodini, akaona ni muda muafaka wa yeye kupata undani wa tukio hilo, akasogea karibu, ingawaje Yule dakitari mtaalamu wa mambo ya akili , hakupendezewa kuwemo kwake, kwani alitaka uhuru wa mgonjwa kujielezea bila vikawazo. Kwa wakati huu mgonjwa alikuwa hajali nani ni nani yupo mbele yake, yeye akili yake ilikuwa ikijilaumu kwa kosa alilofanya. Alijiuliza moyoni, ana nini, kwanini ajiue? Mbona haaelewi nini kimemfanya afanye hivyo, na hata jamii ataiambia nini ili imuelewe!
Kichwa kikawa kinamuuma kwa kuwaza sana, na hata kujiona kama anachanganyikiwa. Alioshinwa awaambie nini hawa watu wanaomuuliza maswali ili wamuelewe vyema,.Na wakati anatafakari la kuongea akili yake ikamkumbusha maisha yake ya nyuma, na mara nyingi mawazo kama haya humjia kama picha ya vipandevipande, ikiisha moja inaweza ikaunganishwa na habari nyingine na iliyoanza.
Wakati mwingine mawazo haya humjia kama ndoto, na wakati mwingine yanamfanya awe kama mtu aliyepagawa akabakia kaduwaa kama mgonjwa wa madawa ya kulevya, na hili likimzidi sana , anakimbilia kulala,. Yeye alihisi kuwa huenda kumbukumbu hizi, zinzjaribu kumuelezea maisha yale yalivyo kuwa ya mikosi, na kujihisi mtu asiyekuwa na bahati katika dunia hii.
Aliikumbuka sana siku ile alipokuwa anasubiri kufunga ndoa na mpenzi wake wa awali,na kwa kumbukumbu zake hapo ndipo alipoanza kupata mikosi isiyokatika. Akaguna na kusema kweli, Bahati haikuwa yangu, labda muda huu ningekuwa nchi za nje nikiwa na Furaha na mume wangu, lakini…sijui nimekosa nini, au mimi ndiye wale miongoni mwa watu waliozaliwa bila bahati, je nina mkosi, je ni kwanini iwe mimi tu…akaanza kulia huku anaikumbuka siku ile ilivyokuwa.
‘Tausi mbona hujavaa gauni la harusi, huoni muda unapita..’ alikuwa shangazi yake ambaye alikuwa akitoka na kuingia ili kuona mambo yanenda vyema, lakini kila alipoingia chumba cha bibi harusi alimkuta mara anajiangalia kwenye kioo, mara anamkuta anakunja nguo, na sasa kamkuta kalala kabisa.
‘Aaah, shangazi mimi nimechoka, kwani ni lazima kuolewa, kwanza ili iweje, akina dada wakubwa zangu hawajaolewa, na bado wapo nyumbani na wazazi wetu, kwanini mimi mdogo mtu niolewe kabla yao…aaah, mimi sitaki kuolewa…’ Akajilaza kitandani na kweli usingizi ukamchukua na kumuacha shangazi yake mdomo wazi akishangaa nini kimemtokea mtoto wao.
Ikabidi aende kumuita mama mtu na kumhadithia nini kinachoendela kwa mtoto wake. Mama mtu akaja haraka na kumkuta binti yao kauchapa usingizi wa nguvu.
‘Unasema nini wewe mtoto, unataka kuleta mkosi gani katika familia hii, wageni wameshafika na wewe unasubiriwa uingie chumba cha kufungia ndoa, bado unasuasua, halafu sasa unasema hutaki kuolewa, haiwezekani, vaa nguo twende…’shangazi, na mama mtu wakamvuta pale kitandani kwa nguvu, na kumshikisha gauni la harusi, lakini bibi harusi mtarajiwa alikuwa kama mtu aliyekunywa madawa ya kulevya, kalegea na kujidosha kitandani kwa usingizi.
‘Hili sasa balaa…’ akasema mama mtu huku akiwa kashika kichwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
‘Twamtaka mke wetu…twamtaka mke wetu..’ kelele za wapambe nje zikazidi. Na shangazi mtu, mama mtu, hata dada mtu na wengine wakaingia chumba cha bibi harusi kutaka kujua nini kulikoni. Waakakuta kisanga kinachoendelea, bibi harusi kauchapa usingizi na akiamusha anajilegeza kama mtu aliyelewa madawa ya kulevya, hana habari kabisa kuwa anasubiriwa nje kwa hamu. Shangazi akamchapa kibao cha nguvu bibi harusi, …lololo. Akawa kafanya kosa, binti Yuleakakurupuka kama mwehu na kulitupa gauni na mara huyo akatoka nje mbio ….
Watu waliokuwepo hapo nje hawakujua nini kinaendela ndani, na wengi hawakujua ni nani hasa bibi harusi, kwahiyo alipotoka nje, akiwa kava nguo za kawaida watu walijua ni mtu baki tu. Mara wakatoka ndugu kumfukuzia wapi alipokwenda lakini haikujulikana mara moja kaelekea wapi na muda ukawa unakwenda. Hatimaye muoaji akakata tama ya kusubiri, akamtuma mshenga wake aulizie kikwazi kipo wapi.
‘Waambie tunaondoka saa nne kuelekea Arusha, ili mipango wa usafiri kwenda zangu Marekani ukafanikiwe na ninatakiwa kuwa na huyo mchumba wangu kesho kwa aili ya kupata visa na mambo mengine, sasa …sijui…’ akasema muaoji huku kachanganyikiwa.
Bwana harusi aliwaza sana, kwanini harusi hii inasuasua, harusi yenyewe imekuwa ikiahirishwa ahirishwa, mara binti anaumwa , mara kuna hili limetokea ilimradi ilikuwa harusi ambayo ilimpa wakati mgumu muoaji. Alikumbuka jinsi alivyokutana na huyo binti, mkewe mtarajiwa kwa mara ya kwanza. Alivutika naye mara moja, na wakati huo walikuja kijijini kutafuta mke mwema, kwani jamaa alitaka kuoa, na alitaka aoe mke wa Kitanzania, ili aende naye Mareakani, mahala anapofanyia kazi. Lakini tatizo lilikuwa nani, na wakati wote haukubahatika kuwa na rafiki wa kike toka nyumbani Tanzania , hana msichana yoyote ambaye anamjua kuwa anaweza kuwa mchumba wake.
Alichofanya ni kuwapa kazi hiyo ndugu zake na wazazi wake kuwa anakuja nyumbani kwenye likizo, na angefurahi kupata mke wa kurudi naye Marekani. Wazazi wake walijitahidi sana, na wakapata msichana waliyeona anafaa na ana sifa zote za mke mwema. Kwahiyo alipofika nyumbani akaambiwa wapi msichana huyo alipo, kinachotakiwa ni kwenda waonane na huyo msichana, ili kama atamkubali , ndoa ifungwe . Walimwambia kwa upande wa msichana yeye hakuwa na tatizo alikuwa tayari kwa muda wowote.
Akamtafuta rafiki yake wa zamani kuwa amsindikize nyumbani kwa huyo msichana, Wakati wapo njiani kuelekea kwenye hiyo nyumba ya binti walipoelekezwa, wakakutana na binti mmoja kabeba ndoo ya maji akiwa katokea kisimani. Jamaa akavutika naye, moyoni akasema huyu ndiye kama ingelikuwa chaguo langu angenifaa kuwa mke wangu, lakini simjui na wazazi wake siwajui, na hata wazazi wangu sijui kama wanamjua na hata kama wanamjua labda wazazi wasingependelea kutokana na historia za familia , lakini sijui labda hilo chagua lao ni bora zaidi. Hata hivyo akaamua kumuongelesha Yule binti.
Yule binti kama walivyo mabinti wengi wa kijijini akawa anakataa kuongea na wageni asiwajua vizuri, lakini alipojitambuslisha akamgundua, lakini yeye hakutaka kujitambuslisha zaidi hata pale alipoulizwa yeye ni nani na anatokea wapi hakutaja jina halisi akataja ukoo wao tu ambao ukoo huwa unajumuisha watu wengi. Jamaa akasema moyoni huenda ndiye binti niliyetafutiwa, kama Ndiyo yeye mambo safi kabisa.
Wakawa wameongozana na huyo binti huku wakijaribu kila njia kumdadisi zaidi lakini hawakupata kitu, na walipofika njia panda, Yule binti alikatisha na kuelekea njia nyingine na wao walifita njia waliyoelekezwa. Jamaa akasema mbona huyu binti anaeleka kwingine, inawezekana sio yeye. Akajisemea moyoni, nitamtafuta tu kabla sijatoa uamuzi wa huyo binti mwingine nilielekezwa kwake.
Walipofika ile nyumba waliyoelekzwa wakakaribishwa vizuri, na kwa vile taarifa ilishafika, ila wakwe hawakutarajia ujio wa siku hiyo, ila walifurahi sana na tratibu za kumwandalia mgini rasmi zikawa zinaendelea , huyku jamaa kiroho kikimdunda kumjua huyo binti aliyechaguliwa na wazazi wake. Waliongea kidogo na wakwe watarajiwa na baadaye akaitwa shangazi mtu, huyu mara nyingi kijijini ndiye muunganishaji wa wananda watarajiwa.
Shangazi mtu akaja akiwa kaongozana na msicha mmoja, wakasalimiana na wakwe yaani baba na mama wa binti wakaondoka na kumuachia ukumbi shangazi mtu , shangazi alikuwa mchehi na mweny utani mwingi. Jamaa akawa anaongea huku anamtizama Yule binti kwa macho ya kujiiba, akasema moyoni, kweli huyu binti ni mrembo, aibu na tabia njema, lakini akili yangu hainiachi kumfikiria Yule binti wa njiani, naona nimempenda yeye zaidi, sasa nifanyeje!
Baadaye shnagazi mtu akajifanya kaitwa ndani na kuwaacha yeye na binti , ilikuwa mbinu ya kuwapa nafasi ya kuongea, na yeye akajua hilo. Akajitahidi kuongea na binti huyo na kumhoji mambo mbalimbali, huku mawazo yake yakitafuta njia nyingine ya kukatisha hayo mazungumzo akatoe taarifa kwa wazazi wake kuwa kampata binti mwingine anayem,taka, kuliko huyo waliyemchagulia.
Na wakati wanaongea mara akaja binti mwingine akiwa kabeba sinia liliwekwa gilasi na vinywaji, akasogea mezani na mara kitambaa alichokuwa kajitanda kichwani kikamdondoka na kumuacha kichwa wazi. Looh, jamaa akashituka, na kusema moyoni huyu si ndiye Yule binti wa njiani, uzuri umezidi mara dufu, akamwangalia kwa makini. Akasema kwli Ndiyo yeye, kwani kule alikuwa kajifunga khanga karibu mwili mzima , sasa hapa kava gauni tupu kna hicho kitambaa chepesi alichokuwa kajifunika kichwani na kushuka kama ushungi usoni. Kilipomtoka kwa nbahati mbaya akamuona sura yae vizuri. Ndiyop yeye.
‘Huyu ni mdogo wangu, anaitwa …’ Yule mdogo mtu akamziba mdogo dada yake asiseme jina
‘Kwanini hutaki nijue jina lako, ningefurahi kuwajua wote , eti kuna ubaya gani’ akauliza jamaa kwa bashasha.
‘Inatosha kumjua dada, kwa vile ni mchumba wako, mimi utanijua baadaye…’ akasema huku anamimina kinywaji kwenye gilasi. Na alipoondoka jamaa akabakia mdomo wazi akiangalia kule mlangoni alipotokea Yule binti.
‘Huyu ndiye malikia wangu, sikubali…’ akajikuta anasema kwa sauti, hata Yule msichana mwingine dada mtu aliyekaa naye akabakia ameduwaa, kwa jinsi jamaa alivyomkodolea jicho mdogo wake na kauli yake hiyo aliyoitoa sasa hivi., mmmh, .... Binti wa watu akabakia kuduwaa , akatahayari, na.....
***
Naona tuishie hapa kwa leo, kwa swali kuwa ilikuwaje?
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Jamani M3 Mbona kidogo harafu umepotea mpendwa nini tatizo mpaka niakaanza kujiuliza au uko nje kikazi??????? just why hujatuwekea mambo mapya?? but all in all nimefurahi kwa vile umerudi. Kinaonekana kitakuwa kikali kama vilivyotangulia.
Nashukuru kwa dua yako mpendwa Jane, labda siku moja nitapata nafasi hiyo ya kwenda nje kikazi!Kwa ujumla nilibanwa sana, computa ilikuwa haishikiki, kwani kazi za kutoka kwenda mjini, bank, mara TRA, ...na kote huko unasimama foleni mpaka miguu inalalama.
Nitajitahidi kuwepo kwani wapendwa wangu ni muhimu sana. Kisa hiki nilikipata kwa ufupi sana, kwahiyo inabidi mwenyewe nicheze na `hoja' ili kiwe cha mvuto, natumai sitawavunja moyo. karibuni sana
Pole mpenzi i can imagen hizo foleni ikifika bank haina mfano na TRA hasa mwisho wa mwezi watu wanaenda kulipia unaweza kuanguka kwa ajili ya kuchoka hicho ndo kilinikimbiza dar na kuja mkoani. But all in all mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako, maana kweli kila ninapofungua ukurasa huu lazima nijifunze kitu kipya so najitahidi kadri ya uwezo wangu kuchungulia mara kwa mara. Nisaidie M3 nataka kujisajili niwe member wa link yako but inagoma, msaada please. Stay blessed
Ukitaka kujisajili katika blog unaangalia pembeni kwenye sehemu iliyoandikwa marafiki (Follow) unapabofya, .patatokea kisanduku chenye Google, twitter na yahoo. kwahiyo wewe kama una e-mail ya Google utabofya google, kama una e-mail ya yahoo utabofya yahoo, halafu itatokea sehemu ya kuweka e-mail adress yako na password ya hizo e-mail. ukikamilisha hapo unafuta maelezo, nabaadaye kama unapicha unaweza ukaiweka kwa kufuata maelezo yatakayotolewa mumo kwa mumo. Kama ukishindwa nijulishe!
M3 BIG UP.
SINA ZAID NASUBIR. POLE SANA NA MAJUKUMU.
BN
M3 BIG UP.
SINA ZAID NASUBIR. POLE SANA NA MAJUKUMU. YAANI!!!!!!!!!!!!!!!! WE ACHA TU, UMEBARIKIWA.
BN
Post a Comment