Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 28, 2010

Tayari wamekwisha-anzaa

 'Leo vipi watu wote mnaumwa mafua au mumepima na kugundulika na TB, manake wote mumejifunika ki-ninja...'sauti ilikatishwa na vumbi kali lililokuwa likiingia toka dirishani, na watu wote mle ndani wakaanza kukohoa.  Na bado nikawa nimeshikwa na mshanga kuona gari likienda kwa kai isivyokuwa na kawaida, kwani barabara yetu ni sehemu ya mwendo wa kuruka vihunzi kwa magari. Na huko utayapata magari ya vituo vyote, Tegeta hadi mwenge, Mbagala hadi Kariakoo, Ubungo hadi Kimara, Kibiti hadi Utete, nk. Na mengi ya magari haya ni spana mkononi.
 'Jamani vipi leo, gari hili halisikii mashimo, manake huu mwendo sijauona karibu miaka mitano iliyopita' akasema jamaa mmoja
'Gari hili limenunuliwa spring mpya zinazoendana na barabara hii msione ajabu' akasema kondakta.
 Mara vumbi likatimkia ndani ya gari na sasa ilibidi kila mmoja achungulie nje, mbona leo vumbi limezidi, na kwa mshangao tuliona dalili za barabara kuchongwa. Siunajua tena sisi huku tunaondoka alifajiri saa kumi na moja na tunarudi saa hizi saa tatu kasoro, na hapo tumewahi, ofisinii umetoka saaa kumi na moja lakini kwasababu ya foleni za magari unajikuta masaa matatuu hadi manne unayapotezea ndani ya gari. Na unafika maeneo ya kwetu unakuta giza totoro, wenye umeme wameshauchukua kwa mgawo usio rasmi.

'TAYARI WAMEKWISHA-ANZA' Mmmoja akaigiza lile tangazo la Zain, na watu wakaangua vicheko. Na hapo mjadala wa barabara za kampeni, au za uchaguzi ukaanza.
 Mimi sikupenda sana kuisikiliza wanayoongea, nilikuwa nimegubikwa na mawazo, hasa katika swala la afya za watu hasa watoto. Hatukatai kuchonga kwa hizi barabara kwani sio mara ya kwanza na mara nyingi huchongwa kipindi kama hiki, lakini labda wangemwagia maji kwanza, na kiukweli barabara hizi sio za kuchongwa ni za kumwagia kifuzi kinachoganda ili kuziba mashimo yaliyochimbika, unapochonga uanzidi kuleta mashimo, kwani mvua zikinyesha maji hayana pa kwenda na mahandaki yanaongezeka.
 Labda ni ndio utengenezaji wa awamu kwa awamu baadaye watajaza kifuzi , ili kuifanya barabara iwe imara, na hilo ndilo tunaloliombea, lakini kama ni mtindo ule ule wa zamani barabara zinachongwa wananchi wanabwia vumbi, vikohozi na mafua vinakuwa wageni mungu atawalaani.
 Na kama ndio huo usemi wa `tayari wameshaanza'  kutubiga changa la macho, ilii wananchi waweze kutoa kula yao kwenu, ipo siku mtaumbuka, kwani wananchi sio wajinga kiasi hicho. Wananchi wa Tanzania ni wavumilivu sana, wanatoa hata haki yao ya msingi ili tu mmoja afaidi yeye na familia yake lakini siku wakiamua ....sijui.
 Labda ni mawazo yetu mabaya, labda ni kule kutokuona barabara hii ikishughulikiwa kwa muda mrefu , na labda imetokea tu kuwa muda wa kuikarabati barabara hii umeangukia kipindi cha kampeni, kama ni hivyo Mungu awazidishie na mshinde kwa kishindo, lakini tunaomba namna ya kuzuia hili vumbi, kwani ukifika ofisini wanauliza huyu jamaa katoka mikoani na basi la asubuhi nini! Na mabosi wetu wengine wanaanza kukuhoji kuhusu usafi wa nguo na viatu, hawajui tumetoka wapi. Siujanjua tena wao viyoyozi ni chumbani hadi ofisini, atapatia wapi vumbi!
 Huu ni wakati muafaka wa wanachi kuhoji haki yetu ya kimsingi, je ahadi zetu za miaka mitano zimetimia, na kama bado ninini sababu, najua majibu ni rahisi kwa wapendwa wetu lakini na sisi wananchi tuna akili na hekima za kupambanua ukweli na uwongo, na maamuzi ya msingii tunayo sisi wenyewe. Hakikisha una kadi yako ya kupiga kura, hiyo ni moja ya zana za kutetea haki yako, na siku ikifika hakikisha unawahi msitari wa mbele ili usibahatishe shabaha yako. Mungu ibariki Tanzania, na watu wake!

Ukipenda hii soma pia zifuatazo:-

http://miram3.blogspot.com/2009/08/leo-tarehe-27-08-2009-niliona-niitoe.html
http://miram3.blogspot.com/2009/08/ndani-ya-diari-yangu.html
http://miram3.blogspot.com/2009/09/serikali-za-mitaa.html



emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Hawa wanatuvunga tu ili wapate kura, lakini ipo siku zitawatokea puani