Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, July 22, 2010

kinga ni bora kuliko tiba

 Sasa kama zamani, unadunda ukijikwaa unatibiwa…’ kauli hii ilinifanya nigeuke kumwangalia huyu mwanadada na macho yangu yaliona haya kumwangalia mara mbili, kwani kivazi alichovaa ni aibu tupu. Lakini sikujali hayo nilikuwa na hamu yakusikia ana maana gani na kauli yake hiyo. Mwanzoni nilifikiri anaongelea matangazo ya tigo kumbe anamaana nyingine tofauti.


‘Sasa ndio kusema hutajikinga, usijidanganye shosti, mara ngapi tumesikia kauli kama hizo, wewe angalia maisha yako na kama zipo hizo dawa unajuaje zitakuwa bure, na zikiwa bure mapaka uzipate unafikiri itakuwa rahisi kama chanjo za ndui…’ dada mwingine ambaye naye kuvaa kwake ni kule kule kwa kuwatia majaribu wanaume akamuuliza mwenzake kwamakini.

Malaria Clinic in Tanzania helped by SMS for L...Image via Wikipedia
‘Wewe, hii inaletwa na wazungu, unawajua wazungu hawabahatishi, wakisema hii safi ni safi, na kama wanaleta wao itakuwa bure buree. Mimi sasa napanga mishemishe zangu, najua mambo yataiva tu…’ akasema Yule dada wa mwanzo.

Kumbe `kama zamani ‘ wana maana yao, na walilenga tangazo lililosikika kuhusiana na dawa ya ukimwi ambayo tumesikia kuwa huenda imepatikana kwa asilimia Fulani na italetwa hapa nchini. Sijui kupatikana huko kwa dawa hiyo kupo kwenye majaribio au ndio imeshaathibitishwa kuwa kweli inatibu, na kwanini ikimbiziwe Tanzania, au ndio imeshasambazwa duniani!
 http://www.iavi.org/research-development/Pages/is-an-AIDS-vaccine-possible.aspx

Kwa vyovyote itakavyokuwa dawa ni dawa, na kutibu kwake sio lazima iwe mia kwa mia, na inaweza ikatibu mwingine na mwingine isiwezekane. Kwa mfano wa madawa ya malaria, wengine wanapona wengine hawaponi na wengine hawapatani nazo kwasababu ya `sulphur’ iliyomo ndani yake na vitu kama hivyo. Je wewe unajuaje itakufaa?

Cha muhimu ni `kinga’ na kujua nini kinachosababisha ugonjwa huo ili ujihadhari nacho. Kinga ya malaria nii kupambana na mbu na mazalia yake na kuhakikisha unatumia neti. Na kinga ya ukimwi ni kuacha uzinzi na vinavyotokana na ushawishi wake. Uzinzi, au zinaa au umalaya au maambukizi mengine ndiyo yanayokufikisha kuupata huu ugonjwa, kwanini tusiyakwepe tukawa huria, kuliko kusimama katikati ya barabara na kusema ngoja nigongwe nikiumia si dawa zipo nitatibiwa! Hapo ni kukosa hekima na busara.

Kama walivyosema wahenga `kinga ni bora kuliko tiba, basi nasi kama tuna busara ni bora tukajikinga na vinavyochangia kuleta ugonjwa huu, ili hata dawa ikija isije ikatukuta tupo taabani hata kutibiwa kwenyewe kukawa kwa mashaka mashaka na huenda isiwezekane kabisa kwa kuangalia utibabu wa magonjwa mengine unavyosumbua. Na pia inaweza ikaleta usugu au kushindwa kuhimili ukali wa vijidudu hivyo, kwani navyo hujibadilibadili kama kinyonga.

Mimi wenu,
emu-three
Enhanced by Zemanta

3 comments :

Anonymous said...

Kwani ni mara ya kwanza kusikia kuwa dawa ya ukimwi imepatikana, nyie mnaopenda hiyo starehe hasa ya uzinzi hiki ni onyo kwa muumba, ni vyema tukaacha na kutubia kuliko kufurahia eti dawa sasa ipo tuanze kale ka mchezo ka zamani, tutaangamia sote tusipoangalia

Unknown said...

Nimepita nami kusoma Diary hii.
Nimevutiwa nayo, na nitakuwa nikipita mara kwa mara humu kupata changamoto.....ahsante kaka

emu-three said...

Karibu sana Shabani jisikie upo kwako, na pia unaweza kuwakaribisha wengine, napia unaweza kujisajili kwenye marafiki, ili tuweze kuliendeelza gurudumu hili la blogs pamoja.