Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, July 21, 2010
Vyote ving'aavyo sio dhahabu
'Mimi nitachangia elifu ishirini' nikasema kwa uhakika.
'Aaaah, ipi wewe, aaah, untuangusha, aaah, hapana bwana, aaaah...' kelele zikajaa ukumbini na kuikuta natahayari nishindwe la kusema.
'Wewe ni mwanandugu na mwanandugu anatakiwa ataje kima cha juu kuliko wote waliohudhuria, tunajua shughuli ni yetu wote, lakini wapo wahusika wakuu, waowaji au waolewai , hawa wanatakiwa waonyeshe mfano, sasa onyesha mfano kwa kutaja kima ambacho hakijatajwa' akasema mwenyekiti na watu wakampigia makofi.
'Kima cha juu kuliko wote, hivi kima cha juu walichotaja ni shilingi ngapi, nakumbuka mzee mmoja alisema atatoa laki moja...ooh, laki moja nitaipata wapi na mshahara wenyewe huu' nikajikuta namunyamunya maneno, mwishowe nikasema kwa ujasiri.
'Ndugu mwenyekiti, kama ulivyosema shughuli ni ya watu wote, na harusi siku hizi haina mtu, ilimradi umeiweka mikononi mwa watu ndio maana tuna wewe mwenyekiti na katibu, hatukusema mwanandugu ndiye awepo hapo mbele. Nogopa sana kuwa `mnafiki'...' nilipotaja neno hili watu wote wakaguna. Na mwenyekiti akaona nitamuangusha akasema nikae.
'Huyu naona hajajiandaa vyema lakini kama wanandugu muandike laki moja...' akasema mwenyekiti, na watu wakashngilia sana. Kwa kuinua vitambaa juu na vigelegele..
Baada ya kikao mwenyekiti aliniita pembeni akaniambia kuwa yeye anauzoefu na shughuli nyingi, na unaposimamishwa mwanandugu unatakiwa utaje tu kiasi kikubwa ili kuwavutia waalikwa wengine watoe zaidi hata kama huna, hata kama hutaweza kukitoa hicho kiwango kwasababu bishara ni matangazo. Najua ulitaka kusema nini pale... ndio maana nikakukalisha na sitaki useme nini ulichokususdia kusema sasa hivi kwasababu naelewa unataka kusema nini. Wewe kaa kimya na toa hicho utakachopata mwisho wa siku utaona kazi yangu ilivyo...' akaondoka yule mwenyekiti.
Kwakweli nilibakia nikiwaza nikisema hivi mbona tunaipeleka dunia kwa kasi za ajabu, manake uongo unakuwa ndio matangazo ya biashara. Ili upate kitu unatakiwa uwadanganye watu ili wavutike na kitu chako, hata kama hakina sifa uliyoitangaza. Hii hali ndiyo inayotufanya tununue bidhaa mbovu na kusingizia Wachina, kumbe ni sie wenyewe tumeenda kuagiza kwa watu kama wa hapa kwetu Gerezani . Kwanini tusiseme ukweli na mwisho wa siku mteja akaamua mwenyewe kusuka au kunyoa...najua utasema hutapata faida, lakini je unayemuuzia atapata faida..hapana huo ni ubinfsi na uchoyo na nasikitika kusema huo ni unafiki.
Maisha yetu ya Kitanzania yamegubikwa na ujanja-ujanja, ndio maana wakasema eti nchi hii yetu inaitwa bongo, manake usipotumia akili utakufa na njaa, danganya ilimradi usiibe, na nashindwa kabisa kujua tafsiri halali ya kuiba, kwani kudanganya sio kuiba? Hahahaha, jamaa anasema kuiba ni kutumia nguvu, au kuchukua kitu bila ridhaa ya mwenyewe, lakini ukidanganya na mwenyewe akaridhika na kutoa hela yake kukupa huko sio kuiba, ni kutumia akili(bongo)! Hapa nikahema na kushindwa kuamini kumbe ndio maana potofu ya BONGO na ndio maana tumefikia hapa, kutumia ujanja kunufaika na kumtia mwenzako hasara ndio bongo.!
Haya uchaguzi unakuja na wataalam wa kutumia bongo zao wanakuja. Wepesi sana kushawishi na hutaamini yule ambaye watu walikuwa wakimlaani miaka mitano iliyopita na kuapa kuwa hawatamchagua tena ndiye atakayepita kwa kishindo. Kwasababu keshatusoma udhaifu wetu, na anajua wapi pa kuanzia na mwisho wa siku mtampigia makofi na sio makofi tu na kula yake mtaipamba kwa maua waridi. Apite huyo, anafaaa sana muachieni amalizie kazi yake hiyo...nk
Hata kama biashara ni matangazo, kwanini sisi wanunuzi tusionje kwanza, na kuhakikisha nembo ya tibiesi ipo na kama tumeonja tumeona haikidhi haja na nembo haipo kwanini tuendelee kununua, na kama tunanunua hataka kama, kwasababu ina mvuto, ni nani atakayeumia mwisho wa siku kama sio wewe na familia zetu. Tukipata majibu na tukatumia busara zetu huenda mwisho wa siku tukaweza kuchagua kilicho bora,kwani vyote vinga'avyo sio dhahabu.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Nimesema mara nyingi NAILILIA ZAMANI kwani siku hizi kila kitu biashara tu. Karibuni tu tutasikia hata kuzikana ni mpaka kutoa michango na labda nisemavyo hivi ni tayari ipo. Biashara Biashara biashara. kaazi kwelikweli...
Lakini wewe kaka mtu huwezi kuchangia kuchangia kidogo kuliko wajumbe wengine, hata hivyo sidhani ni lazima mtu uchangie kuliko uwezoo wako, ukaibe
Harusi siku hizi ni kununua gari, mamilioni yanateketea kwa siku hii moja, na yote yanaenda tumboni mwisho wa siku wanaharusi wanatafuta hela ya kodii ya nyumba hawana...
Post a Comment