Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, July 23, 2010
usione vyaelea vimeundwa
Kelele za kuzomea na mirunzi ilinifanya nigeuze shingo upande wa pili wa barabara na kujaribu kutafiti ni kitu gani kimewasisimua wakazi wa hapa Mombasa. Nilihisi mwizi au mtu kagongwa na gari, lakini haikuwa hivyo kwani makelele hayo yalikuwa mbali kidogo na barabarani. Nikaamua kusogea karibu ili nami kisinipite cha wapita njia, na mara macho yangu yakaelekea kule wengi walipoelekeza macho yao, Oh nikabakia kuguna na kusema kimoyoni inawezekana kweli yale ni maumbile yake au kuna maigizo ndani yake.
Mbele yetu alikuwa akipita dada mmoja mrembo, na kilichovutia wengie sio urembo wake, ni sio yale madaha yake ya kutembea kama warembo wanogombea urembo wa dunia, na sio mavazi yake ambayo sio tofauti na mavazi wanaovaa akina dada wengi siku hizi ya suruali za kubana, bali ni maumbile yake, ambayo licha kuwa kavaa suruali ya kubana lakini yalikuwa tofauti na akina dada wengine, yalizidi ukubwa na alikuwa akiyatingisha kimadaha.
'Dawa za kichina hizo, humpati mtu hapa?' nikasiki kaka mmoja aliyekaa karibu yangu akisema kwa sauti
'Ina maana yale sio maumbile yake ya kawaida?' nikadadisi
'Wewe una maana huoni ukweli, ndio nyie mtakaoingizwa mjini na kumchukua mkidhani ni maumbile ya kawaida. Yule katumia dawa za kichina za kukuza makalio na mapaja. Wengi wana mjua yule dada tangu akiwa mdogo. Si mtoto wa mzee wa jirani yangu yule. Aliondoka hapa kwenda kusoma Ulaya aliporudi hatukuamini kuwa ndiye yuleyule mtoto mrembo tuliyemjua, kajazia kupita kiasi. Na kule sio kujazia, ni madawa, kwani kujazia kwa asili tunakujua sisi' akasema huyo jamaa
Mimi sikupenda kupingana naye au kukubaliana naye, huenda kweli katumia hayo madawa, au ni maumbile yake yamekuwa kutokana na mazoezi . Nikawa najiuliza kimoyoni ni kwanini watu wahamanike na mambo yasiyowahusu.
'Kwani kuna ubaya gani mtu akiwa vile, je kwanini pia mtu atumie madawa hayo ili kukuza sehemu za mwili wake? Ninini tunataka au tunataka kumfurahisha au kumuonyesha nani' nikajiuliza maswali hayo kichwani na bahati nzuri nikasikia mwanamke mmoja akisema hivi;
'Sisi wanawake wakati mwingine tunazidisha manjonjo yetu, na ni wepesi sana kuiga mambao ambayo ukiangalia yanaweza kutuasiri afya zetu, na yote ni kwasababu ya kutokujiamini. Yule dada ni mrembo hata kama asingeharibu mwili wake kiasi kile kama ni dawa au sijui kafanyaje mwili ukawa vile, bado ni mrembo na angeppata wanaume au mwanaume wa kumuuoa, sasa sijui ni nini anakitafuta zaidi. Ni urembo wa kujifurahisha au ni uhuni tu ili wanaume wakugombee, sijui lakini mimi naona anatuzalilisha wanawake na kwanini atembee vile kimbwebwe' akamaliza yule mwanamamama.
' Lakini swala la kuiga sio akina mama peke yao hata wanaume wanafanya hivyohivyo, angalaia yule kaka alivyovaa suruali yake ina maana hawezi kuipandisha juu mpaka aivalie katikakati ya makalio(hakutumia neno hilo)?' akasema yule dada.
`Kuiga hakukatazwi ilimradi uige ukijue faida na hasara ya unachokiiga, kwasababu kwa mfano mimi nilisikia zamani kuwa waliokuwa wakivaa hereni kwa upande wa wanaume walikuwa wakijieleza kuwa wao ni nani katika jamii, kuwa ni mashoga. Sasa kwasababu waliokuwa wakivaa vile ni watu mashuhuri katika jamii watu wakaona kuwa ni sifa au fasheni kuvaa vile wakaiga na ikawa sio maana yake tena ile ya awali. Sasa tunapoiga ni vyema kwanza tukajua maana hasa ya kile tunachokiiga kwani vingine vina gharama sana kuvihudumia, unaweza ukaiga mwishowe huduma zake ukashindwa na matokeo yake ni kudhadhdlilika. kwani walisema wahenga usione vyaelea vimeundwa' akamalizia yule mama wa makamo.
Je wenzangu mnasemaje kwa hili. Tunapovaa nguo za ajabuajabu tuntafauta nini, kupendwa kupendeza, au kujifurahisha.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Bado sitaelewa kwa nini soma na hapa http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/03/walianza-wanawake-na-sasa-ni-wanaume.html.
Uvaaji wa mtu ni utawala binafsi hauruhusiwi kuingiliwa, labda mtu katembea uchi hapo unaweza kusema, lakini eti mtu kavaa nguo inabana au imevuka magoti ndio watu waseme vibaya nafikiri huko nikuingiliana uhuru wa mtu binafsi.
Na huko kukuza mnachoita makalio, mimi naona hakuna ubaya labda kiafya kama inamadhara ni kazi ya wataalamu kuwaambia wananchi, vinginevyo sioni ubaya, hayo ni matakwa binafsi.
Unajua viti vingine nikujiumiza roho bure, kama hupendiachana nacho achia wengine wafanye, ikibidi fumba macho. Vinginevyo tunajirudisha nyuma kwa kuangalia uzamani na kutaka uwe hivyo kitu ambacho hakiwezekani
Vitu vingine ni uhaba wa elimu. Na sio kwamba natukana ila hakuna jinsi nyingine yakuelezea zaidi ya kusema ni uelewi mdogo wa kutafakari. Maumbile unaweza ukayajenda kwa mazoezi hiyo ni kiasili lakini ukiamua kutumia madawa unalazimisha na hatimaye unaweza ukazua kansa. Nini watu wanatka ni sifa za hapokwa hapo kwani kama ni kupendwa jiulize hawo wanaopendwa wana hayo makalio makubwa, na makalio ndiyo ynayoleta raha, sijui nasema huo ni uhaba wa kutafakari.
N hawo wanavaa kata nanihii ni wao ni kama hawo hawana la kujifunza la maana ila kuiga, kwanini msiige kurusha ndege au kuwa madakitari mnaiga vile ambavyo havileti maana. Wengine chupi chafu mnatuonyesha za nini, malakio yamekakamaa hayana hata mvuto unamuonyesha nani.
Saamahani kama nimekosea lakini inakera
Lakini ikumbukwe kuwa wanawake wamefikia hapo walipofikia, yaani kutafuta uzuri wa nje kiasi cha kuhatarisha maisha yao, baada ya kugundua soko lilipo.
Inasemekana wanaume wengi wa Kiafrika wanapenda wanawake wenye makalio makubwa na nyonga mithili ya namba nane. na baada ya kugundua udhaifu huo, nao ikabidi wautafute kwa gharama yoyote, na ndio maana Wachina ambao ni mahodari wa kunusa eneo la kuwekeza wakaelekeza utafiti wao huko wakijua kuwa watapata soko kubwa Afrika, kitu ambacho wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Hivi dada zetu hawashangai wanawake wa Kichina hawahangaiki na ujinga huo?
Kutokana na utandawazi, hapa Dar es salaam katika kumbi za starehe kuna makahaba wanaojiuza wakiwemo hao Wachina, lakini hawana makalio makubwa na soko lao liko juu, na ndipo ninapofikia mahali pa kujiuliza kulikoni dada zetu?
Ujinga unapopewa nafasi na werevu hutoweka, na ndo sababu dada zetu wanahangaika usiku kucha kuutafuta urembo nje yao na hiyo inatokana na kutojiamini.
Niishie hapa nisijefungua darasa la utambuzi.
Kwanza kulikuwa na kujichubua - watu wanajibabua ngozi mpaka ngozi halisi nyeusi ya Kiafrika inakuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kuhimili mionzi ya jua. Bado hatujajua athari halisi za tabia hii lakini sitashangaa kama kutakuwa na ongezeko la kansa ya ngozi huko mbele. Eti Mwafrika aliyekuwa akishinda juani akilima na kuchunga mifugo yake sasa aanze kufa na kansa ya ngozi!
Halafu kuna hili la Mchina. Sina uhakika kama mabinti hawa wamewahi kufikiria siku moja watakapozeeka (kama watazeeka) wataonekanaje. Na madhara ya madawa haya ni nini hasa kwa viungo vya ndani kama figo na ini - viongo vya muhimu sana katika kusafisha mwili. Na serikali yetu nayo imekaa kimya tu badala ya "kuyachakachua" madawa haya na kujua makemikali yaliyomo kisha kuanzisha kampeni ya kuwaelimisha dada zetu kama makemikali hayo yataonekana kuwa na madhara.
Kama alivyosema mtambuzi Kaluse - uzuri kamwe hautafutwi nje...Ngoja tuone itakuwaje. Mada nzuri!
Post a Comment