Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 3, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-69


‘Kwahiyo nimpigia simu huyo mpelelezi nimuambie kuwa huo mzigo ninao hapa kwako,au sio?’nikauliza huku nikitoa simu yangu tayari kwa kumpigia simu mpelelezi, baada ya kuona mdada anakasirikia, na yeye akasema kwa haraka;

‘Huu mzigo hautakiwa kabisa kuwa hapa kwangu, nilichofanya mimi nikuuondoa pale kwako kwa muda ili polisi wasiuone, kwasababu hata hivyo huwezi kujua hao polisi wana nia gani na huo mzigo, inawezekana ni kundi ambalo linataka kuhakikisha unafungwa...’akasema

‘Ukumbuke kuwa mimi niliuchukua kwa nia ya kukuokoa, na hapa nimeshapoteza muda mwingi, ulitakiwa uwe umeshaondoka,....’akasema akiangalia saa yake.

‘Sasa....?’ akauliza

‘Mimi nitaurudisha pale kwako,na wewe wasiliana na mpelelezi wako haraka iwezekanavyo mtafute njia ya kukabidhiana huo mzigo, huo mzigo ni bomu, yeye atajua jinsi gani ya kufanya,….’akasema na mimi nikawa kimiya akasema kwa ukali;

‘Unanisikia mpigie kwa wakati wako, sasa hivi utoke humu ndani, umenielewa,au bado una msimamo wako, ....?’ akauliza

‘Nipo na wewe, japokwua sipendelei kabisa....’nikasema

‘Sasa wewe ondoka,huu mzigo utaukuta huko kwako..’akasema mdada akitizama pale kabatini na kuangalia saa yake na mimi nikainuka kuondoka, na ghafla nikamuuliza swali

‘Sasa huo mzigo utafikaje huko kwangu, maana nakuona upo mwenyewe au utawaita vijana wako….?’nikamuuliza na yeye akawa haniangalii, alikuwa akitizama nje kwa kupitia dirishani halafu akasema;

‘Hiyo sio kazi yako,…nimeshakuambia uondoke, usipoteze muda, muda sasa hivi ni mali....’akasema na mara tukasikia mlango ukigongwa, na mdada akasimama kwa haraka,na kuelekea pale mlangoni.

Mimi nikiwa na wasiwasi nikatega sikio kumsikiliza anaongea na nani, kumbe alikuwa mlinzi wake, akawa anaongea na mlinzi wake, na baadaye nikasikia akisema;

‘Muite huyo mtu ni mtu wangu ....’akasema mdada na kutoka nje kabisa, nilisikia mlinzi akisema;

‘Sawa bosi....’akasema huyo mlinzi na kukawa kimiya kidogo, halafu nikasikia mdada akiongea na mtu mwingine kwa sauti ya taratibu sikuweza kusikia wanachozungumza, ulipita muda kidogo, baadaye mdada akarudi ndani na alionekana hana raha, akasema;

‘Hali sio shwari kabisa, mambo yameharibika,...’akasema mdada, na safari hii akaja kukaa karibu na mimi, na alikuwa akiongea kwa sauti ya ndogo kama vile hataki mtu mwingine asikie, alionyesha ile hali ya kujiamini imemuondoka, ikabidi nimuulize

‘Kwani vipi mdada mbona umebadilika ghafla, kuna nini zaidi...?’ nikauliza nikiwa na wasiwasi na yeye akaniangalia na kusema;

‘Polisi.....’akasema mdada akiangalia kule kwenye kabati lake.

*********

Tuendelee na kisa chetu kwa kumalizia sehemu hii iliyokuwa imebakia kabla hatujaingia kwenye hitimisho.

‘Wamekuja au?’ nikauliza

‘ Polisi wamefika tena hotelini kwako kufanya upekuzi, na wamesema watafanya msako huo kila kona na inavyoonekana wamejigawa makundi mawili, kundi jingine lipo njiani kuja hapa kutafuta huo ushahidi....’akasema

‘kwahiyo kuna mtu kawaambia kuwa huo mzigo ulihamishwa au wamejuaje mpaka waendelee kuutafuta?’ nikamuuliza

‘Kama kulivyo na watu wangu ndani ya kundi lao, ndivyo na wao walivyo na watu wao ndani ya kundi langu, na sio rahisi kuwabaini watu wao...nilijaribu kuwachuja watu wangu lakini sikuambilia kitu, cha muhimu ni kuwahiana tu,….’akasema mdada na mimi nikamuangalia mdada, ambaye alisimama na kusema;

‘Kwasasa tunahitajika kufanya jambo la haraka, maana hao jamaa wapo njiani, hapa hatuna muda wa kupoteza….’akasema mdada akichukua simu yake kuongea na watu wake.
‘Kwahiyo utafanya nini?’ nikamuuliza nikiangalia mlangoni nikijua hao askari wanaweza kuja hapo , na mimi sikupenda wanikute hapo.

‘Mimi nitafanya nini au wewe utafanya nini, hivi huoni kuwa hili bomu ni kwako…mimi nafanya kukusaidia tu….’akasema akielekea kwenye kabati akitaka kulifungua, na mara simu yake ikaita, akasikiliza kwa muda, halafu akageuka kuniangalia huku akiendelea kuongea na simu, na alipomaliza akasema

‘Mmm, naona uondoke wewe na mzigo wako...’akasema mdada akiwa kashikilia ufunguo wa kabati lake

‘Mdada, nitawezaje kuondoka nao.....na nyie mliokuja nao ndio mnaweza kujua jinsi gani ya kutoka nao, kunipa mimi ni kutaka nishikwe nao...’nikasema

‘Sikiliza nikuambie, wewe kwa sasa mpigie simu mpelelezi mkutane mahali,...ni muhimu sana mzigo huo ukawa kwa mtu mwaminifu, mimi siwaamini hao polisi ....’akasema

‘Lakini....’nikataka kujitetea, na yeye akasema;

‘Lakini nini, fikiria jinsi ya kufanya, mimi sishindwi kuurudisha huu mzigo hapo kwako, lakini nina shaka kuwa pale watakuwa wameshaweka mitego, ukifika tu, watakuwahi, na hapa hautakiwi kabisa uonekane, na wakifika hapa watapekua kila mahali, unaona jinsi ilivyo, ni muhimu huu mzigo utoke hapa haraka iwezekanavyo, na siwezi kuwatumia vijana wangu kwa sasa, watashukiwa...’akasema

‘Sasa....ngoja mimi nimpigie simu mpelelezi...aja hapa kuliko mimi kutoka nao.’nikasema na mdada akawa anafungua lile kabati

Nilipiga namba ya mpelelezi, na simu ikawa inaita tu, mpelelezi hakupokea hadi ikakatika, na kwa hali ile nikawa nimechanganyikiwa, nikageuka kumuangalia mdada, na mdada akawa ameshafungua kabati lake, akanuliza

‘Vipi....?’ akauliza

‘Hapokei simu, inaita tu.....’nikasema

‘Ngoja tuone tutafanya nini...'akasema mdada, na huku akiwa kashikilia mlango wa lile kabati, alikuwa hajatoa ule mfuko.

'Muda umekwenda sana, na ni muhimu huu mzigo utoke hapa, na ni lazima ufike mikononi mwa mpelelezi, vinginevyo, ...’akasema na akageuka kuongea na watu wake, na alipomaliza kuongea na simu akasema;

‘Naona polisi wapo njiani, walitakiwa wawe wameshafika hapa, lakini cha ajabu kundi hilo limepitia ofisini kwao kwanza, na walifanya kikao kidogo, halafu wakatoka, na sasa wanakuja huku, nafikiri walikwenda kupata kibali rasimi...'akasema huku kashika kichwa akiwaza

'Kwahiyo?' nikauliza

'Unajua wakati mwingine inabidi ufanya hata yale yasiyofanyika, ili tu uweze kuokoa kitu muhimu, nikuambie ukweli, huu mzigo sasa ni kitu muhimu sana, kwa polisi, wakiupata hatujui lengo lao litakuwaje, lakini kwa mtizamo wa haraka, wewe utakwenda jela....mahabusu...'akasema

'Na wewe?' nikauliza

'Mimi...!?' akasema kama anashangaa na baadaye akasema;

'Mimi usiwe na shaka nami, najua jinsi gani ya kujitetea hofu ni kwako...'akasema kwa kujiamini

'Kwahiyo....'nikasema nikiwa natafuta njia ya kukwepa kuondoka na huo mzigo, kwangu mimi nilishaona ni bomu kubwa sana, na mdada akatabasamu na kusema;

'Sasa tunataka tucheze mchezo, ...unatakiwa utoke hapa kama mdada, unanielewa,...’akasema

‘Nini, kama nani, mdada usilete mambo yako tena...’nikasema

‘Wewe subiri....’akasema na kuingia chumbani kwake, na alipotoka akawa katoka na nguo zake za kike, na vipodozi, mawigi, na...

‘Mdada unataka kufanya nini?’ nikauliza nikiangalia vile vitu alivyobeba,

‘Wewe subiri, ujanja kuwahi,...’akasema na kuanza kunikarabati usoni....

NB:Je watafanikiwa

WAZO LA LEO: Wakati wengine wanalia watakula nini, kuna wengine wanamwaga, kuna wengine wanatumia pesa nyingi tu kwa sherehe ambayo ingefanyika kwa gharama ya kawaida, yote haya yanafanyika kutokana na utofauti wa kipato, au kwa kujifaharisha tu.


Haikatazwi kufanya hivyo,kwani hayo ni maamuzi binafasi, lakini mnaonaje nyie mnaotumia mamilioni ya mapesa, katika bajeti zenu za harusi, mkaweka fungu la kuwasaidia mayatima, masikini na wasiojiweza, nafikiri mkifanya hivyo sherehe zenu zitaleta tija sana, na baraka zitaongezeka.

 Kwanini tuweke fungu kubwa kwa vinywaji kula, na sijui nini mwisho wake ni kufuru tu. Jamni tuwajali mayatima, tuwajali wasiojiweza, hiyo kwetu ni ibada kuliko hizo sherehe za kufuru.
Ni mimi: emu-three

No comments :