Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, April 25, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-45



‘Ina maana huyo mlinzi alikwenda sehemu ya kuegesha magari, na akaweza kuiona hiyo nyundo, ni kutoka kwenye gari la nani?’.

‘Nyundo hiyo ilipatikana kutoka kwenye gari la mdada....’

‘Oh, mbona sielewi....’

Tuendelee na kisa chetu, ...

‘Huelewi nini hapo?’ akaniuliza mpelelezi, akiangalia saa yake

‘Unasema hiyo nyundo ilipatikana kutoka kwenye gari la mdada, ilifikaje hapo, ni mpango wa mdada, au?’ nikauliza swali nikiwa na mlolongo wa maswali mengi kichwani.
Mpelelezi akaniangalia usoni, na huku akikunjua uso na kujenga tabasamu, akasema;

‘Sasa nakuona una shauku ya kufahamu kila kitu, mhh, sio mbaya, lakini kama unataka kufahamu kila kitu na wewe ushiriki, ukweli wako utafanya tukio zima libainike, na haki itendeke...’akasema na mimi nikainama chini.

‘Hivi wewe unayafurahia haya yote, dhuluma, ubadhirifu, udanganyifu, wizi,...mauaji,....hebu niambie haya yataendelea mpaka lini, ...inaniuma sana, hasa nikiona wanyonge wanatumiwa kama chambo,....angalia kukitokea vurugu wanaoumia ni akina nani.....sasa hili haliwezi kuisha kama wengine hatutajitoa mhanga....’akasema

‘Mhanga...?’ nikauliza kwa mshangao

‘Mhh, elewa unavyoelewa,..cha msingi, ni kuwa na huruma ya kweli kutoka kwenye moyo wako, na huruma ya kweli ni kuwajibika,...kila mmoja kwenye fani yake, na kuhakikisha, haki inatendeka...tatizo viongozi ndio wanao-ongoza kwenye ubadhirifu, anataka gari zuri, maisha mzuri...bila ya kumjali huyu mtu anayepigika wacchini yake....’akaniangalia usoni na kusema;

‘Hivi nikuulize, bila ya huyu mtu wa chini, mvuja jasho, mtafuta masoko, ...muendesha mashine, hicho kipato kingelikuwepo...lakini kwenye bajeti, gharama nyingi ni kwa viongozi, sasa ngoja ifike kwenye kubana matumizi, kwenye kupunguza gharama, mtu wa kwanza kuangaliwa na huyu...wa chini, sio yeye, kusema nipunguze gharama zangu, huku haguzi, kwa namna hiyo, amani haitakuwepo, na amani ya kweli huanzia kwenye mioyo yetu...

‘Mimi nimejaribu kufuatilia na kusoma viongozi wa zamani hasa wa kwenye vitabu vya dini, kiongozi wa enzi hizo, yeye alikuwa haangalii masilahi yake kwanza...hashibi kwanza mpaka ahakikishe watu wake wameshiba, je kwa karne hizi unaweza kumpata kiongozi kama huyo....angalau, asema mimi sitaki gari la gharama, maana mahospitali hayana dawa...yupo wapi..hakuna...sasa tufanyeje..’akaangalia saa yake.

‘Tufanyeje?’ nikamuuliza

‘Tutafanya nini, wakati watu hamtaki kusema ukweli, semeni ukweli, kuhusu ubaya wa viongozi wenu, mumewachagua wenyewe, ...mna haki ya kuwauliza kila wanachokifanya, lakini kwa nia njema, sio kwa majungu..ni haki yako kumuuliza, nay eye ni haki yake kujieleza, sio aulizwe halafu anakuja juu...utakujaje juu, wakati mwajiri wako anakuuliza...naona ajabu kabisa...’akasema

‘Mhh, muajiri wako, ina maana mwananchi ndio mwajiri wa kiongozi wake...?’ nikauliza

‘Kiukweli nio hivyo, ila kinadharia,...sio rahisi, kiongozi akishashika madaraka wewe huna usemi mbele yake, ...hilo linakuwa ni tatizo..na huyu iongozi hataogopa kufanya dhuluma,...keshakuwa juu ya sheria,...unapofanya ubaya, kinyume cha utaratibu umeshajivika ukubwa juu ya hiyo sheria uliyoivunja, au sio...’akasema huku akionyesha kukerwa na kitu.

‘Hebu nikuulize swali, umesema huyo mlinzi alikwenda kwenye gari la mdada akachukua nyundo, alijuaje kuwa kuna nyundo kwenye hilo gari?’ nikamuuliza nikiona ninaweza kuachana naye bila kujua undani wa hilo tukio.

‘Ndio, inavyoonekana alifahamu kuwa kuna kitu kama hicho, lakini sio lazima kwamba hivyo vitu vilikuwepo hapo kwa malengo hayo....’akasema.

‘Hukumuuliza huyo mlinzi akakuambia ukweli, huenda kweli ilipangwa iwe hivyo?’ nikamuuliza

‘Mlinzi hajaongea yote hayo,..na haajwahi kusema ukweli kuwa yeye aliacha lindo na kuingia ndani ya jengo,..au kuwa alikuja mtu akamuagiza kufanya hivyo... hajawahi kumwambia mtu yoyote hadi sasa, hiyo imekuwa ni siri yake tu....’akasema

‘Oh, sasa wewe umafahamu vipi hayo yote?’ nikamuuliza nikisahahu kabisa kuwa natakiwa kurudi hotelini haraka. Yeye kwanza akaniangalia , halafu akaangalia saa yake, na kusema;

‘Mdada atakuwa anakutafuta...’akasema na mimi nikawa kama mtu aliyepigwa kibao usoni, nikainuka, nikitaka kuondoka, na yeye akasema;

‘Usiwe na haraka kihivyo, haraka haraka haina baraka, ...waliotunga huo usemi walikuwa na maana yao nzuri tu, na japokuwa sisi tunaharibu maana yake halisia, ...’akatulia kidogo

‘Ina maana kuwa, kabla ya kufanya jambo, hebu jaribu kulipangalia..usikurupuke tu,...wewe, sasa unataka kuinuka na kuondoka, hujaangalia mazingira, je kuna usalama, umeshasahau kuwa unafuatiliwa, kuna jamaa nje bado anakutafuta....kuwa makini, usiwe mtu wa kuharakisha bila mpangilio...’akasema huku akiangalia upande wan je.

‘Ok, haya hebu nijibu swali langu wewe ulijuaje yoye hayo, kama mlinzi hakuwahi kumwambia yoyote?’ niamuuliza.

‘Mimi ni mpelelezi, na hiyo ndio fani yangu,....’akasema na kuangalia saa na akalivuta kofia lake na kuficha sehemu kubwa ya uso, akavaa mawani yake. Mimi nikawa na hamu ya kufahamu ukweli lakini muda ulikuwa umekwenda sana,..nikasema;

‘Kwanini hutaki kuniambia, na wakati huo huo, wewe umesema unataka mimi niwe pamoja nawe, katika kulimaliza hili tatizo, je mimi nitakuamini vipi, ....?’ nikamuuliza

‘Tatizo lako, hujiamini,...unaperekeshwa tu,..kwanza jiamini, pili fahamu ni kitu gani unachotaka kukifanya, kwa dhumuni gani, je kuna faida au hasara...wewe si mhasibu bwana, hayo mbona ni moja ya kanuni zenu...’akasema huku akizidi kuangalia nje.

‘Mhh, kwahiyo...?’ nikauliza

‘Kwanza hujataka kuniambia ukweli, mengi nimeyafahamu kutokana na juhudi zangu mwenyewe, ...lakini kwa hivi sasa huna ujanja, ni mawili uwe na mimi ili tulitumikie taifa letu kwa masilahi ya wananchi..huko ndiko kujitoa mhanga nilikokusudia usije ukapotosha kauli yangu, maana watu siku hizi wanapenda kudokoa kauli za watu, vipande vipande, na kujenga hoja za uzushi...unamdanganay nani, wananchi...tuwe wakweli wa ukweli....’akasema

‘Sasa ili kama unataka uwe na mimi, unahitajika kujitoa mhanga kiukweli...ni hatari, lakini mwisho wa siku, utakuwa umeitetea jamii, na hilo ndilo muhimu, jamii kwanza, watu wako kwanza...wewe na masilahi yako iwe baada ya watu wako kushiba,..unaweza hiyo...sio rahisi, lakini kama huwezi, njia ya pili na kujiunga na hilo kundi la wajanja wajanja waliojipenyeza kwenye mtandao (system)  kwa kufanikisha masilahi yao...’akasema

‘Hapo inakuwa ngumu, kwanza sijui kwa vipi, pili, ni nani wa kumuamini, na tatu mimi sio askari...’nikasema

‘Hahaha, hapo ndipo ninapomsifikia baba wa taifa kuhusu JKT, ni muhimu kila mtu akapitia jeshini, akajijua, akajenga ujasiri wa kujilinda na kuilinda jamii....kila mtu anastahiki kuwa ni askari...ni muhimu sana....’akasema na kusimama kwa haraka, kwa haraka akawa kapitisha macho sehemu yote ya hapo ndani na kusema;

‘Sasa muda umekwenda sana, rudi hotelini kwako, na jipange jinsi ya kuongea na mdada,...nahisi mnaweza kukutana naye, au keshafiak hotelini kwako anakusubiria,.. ila na kupa kama tahadhari, usije ukamwambia kuwa tulikutana mimi na wewe, ukimwambia utajiharibia wewe mwenyewe, mimi sina shaka, kwani hiyo ni kazi yangu...ila kwako wewe....’akasema akiinuka na kugeuka kuondoka

‘Mimi nina maswali mengi ya kukuuliza, lakini kweli naona muda umekwisha, na sijui nitamdanganya vipi mdada nikikutana naye...’nikasema

‘Hiyo ni kazi yako...na hayo maswali uliyo nayo, yahifadhi hadi hapo utakapokuwa tayari kushirikiana na mimi,....vinginevyo, nakutakia kazi njema, au jela njema, na kama wataamua kukurudisha tena huko mahabusu, ...sijui,....’akasema huku akiinua mguu hatua ndogo ndogo kuondoka na mimi nikawa nimeshasimama, na kuanza kutembea

‘Hawawezi kunirudisha huko....’nikasema nikijipa matumaini.

‘Unajiamini vipi wewe, ok, ni muhimu kujiamini, lakini je kweli una uhakika na hilo?’ akaniuliza

‘Mdada kasema hawawezi kufanya hivyo....’nikasema na kumfanya ageuka kuniangalia halafu akaangalia kitu kwenye dirisha na kusema;

‘Jamaa yako huyooo, anaondoka, naona kashakata tamaa, au kaitwa na wakubwa zake, na hapo inaonyesha kuna jambo,.....’akasema

‘Jamaa yupi..na jambo gani hilo?’ nikauliza

‘Huyo jamaa aliyekuwa akikufuata nyuma,...nahisi kaitwa na bosi wake na naona ni kwa haraka,  kuchukua pikipiki, na muondoko wake, sio wa kuhakikisha kuwa kazi aliyotumwa kaimaliza hii inaashiria kuna jambo huko...ngoja niondoke, ....’akasema

‘Sasa mimi nifanye nini, huenda mdada keshafika hotelini ?’ nikauliza

‘Usijali, nenda kakabiliane naye kama askari..jiamini, na utafanya nini, hiyo ni kazi yako...tutaonana hivi punde...’akasema akitoka kwenye hicho chumba, na kuelekea barabarani

Mimi nikatulia kwa muda, nikaangalia dirishani, na sikuona dalili ya mtu wa mashaka, nikatoka nje, sikumuona tena huyo mpelelezi na wala sikujua kaelekea wapi, mimi nikaamua kuangalia hamsini zangu, na wakati nataka kuchanganya mwendo mara nikasikia mtu akiniita jina nyuma yangu..

‘Oh ni nani huyu tena....’nikajiuliza kimoyomoyo nikiogopa kugeuka

NB: Ni nani huyu tena


WAZO LA LEO:Ubaya, majanga ,wizi, na hujuma mbali mbali, zinafanywa na sisi wenyewe, na hata kama sio wewe mwenyewe moja kwa moja, lakini jirani yako, jamaa yako au kiongozi wako ndiye anayefanya  hayo na unafahamu na unamfahamu kuwa anafanya hayo yote, lakini kwa sababu mbali mbali hutaki kumfichukua...

'Ndio hutaki kusema ukweli kwa vile, huenda mnakula naye,au ni mwenzetu, au, anakukatia kitu kidogo. Sasa hali ikiwa mbaya, wewe unakuwa wa kwanza kulalamika, huoni kuwa chanzo ni wewe...jichunge nafsi yako, chunga majirani zako, kwa kuwa wa kwanza kujilinda, na kuilinda jamii yako, kwa kusema ukweli hata kama ukweli huo utakuumiza wewe mwenyewe.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Nipo na wewe, twende kazi