‘Ina maana huyo mlinzi alikwenda
sehemu ya kuegesha magari, na akaweza kuiona hiyo nyundo, ni kutoka kwenye gari
la nani?’.
‘Nyundo hiyo ilipatikana kutoka
kwenye gari la mdada....’
‘Oh, mbona sielewi....’
Tuendelee na
kisa chetu, ...
‘Huelewi
nini hapo?’ akaniuliza mpelelezi, akiangalia saa yake
‘Unasema
hiyo nyundo ilipatikana kutoka kwenye gari la mdada, ilifikaje hapo, ni mpango
wa mdada, au?’ nikauliza swali nikiwa na mlolongo wa maswali mengi kichwani.
Mpelelezi
akaniangalia usoni, na huku akikunjua uso na kujenga tabasamu, akasema;
‘Sasa
nakuona una shauku ya kufahamu kila kitu, mhh, sio mbaya, lakini kama unataka
kufahamu kila kitu na wewe ushiriki, ukweli wako utafanya tukio zima libainike,
na haki itendeke...’akasema na mimi nikainama chini.
‘Hivi wewe
unayafurahia haya yote, dhuluma, ubadhirifu, udanganyifu, wizi,...mauaji,....hebu
niambie haya yataendelea mpaka lini, ...inaniuma sana, hasa nikiona wanyonge
wanatumiwa kama chambo,....angalia kukitokea vurugu wanaoumia ni akina
nani.....sasa hili haliwezi kuisha kama wengine hatutajitoa mhanga....’akasema
‘Mhanga...?’
nikauliza kwa mshangao
‘Mhh, elewa
unavyoelewa,..cha msingi, ni kuwa na huruma ya kweli kutoka kwenye moyo wako,
na huruma ya kweli ni kuwajibika,...kila mmoja kwenye fani yake, na
kuhakikisha, haki inatendeka...tatizo viongozi ndio wanao-ongoza kwenye
ubadhirifu, anataka gari zuri, maisha mzuri...bila ya kumjali huyu mtu
anayepigika wacchini yake....’akaniangalia usoni na kusema;
‘Hivi
nikuulize, bila ya huyu mtu wa chini, mvuja jasho, mtafuta masoko, ...muendesha
mashine, hicho kipato kingelikuwepo...lakini kwenye bajeti, gharama nyingi ni
kwa viongozi, sasa ngoja ifike kwenye kubana matumizi, kwenye kupunguza
gharama, mtu wa kwanza kuangaliwa na huyu...wa chini, sio yeye, kusema
nipunguze gharama zangu, huku haguzi, kwa namna hiyo, amani haitakuwepo, na
amani ya kweli huanzia kwenye mioyo yetu...
‘Mimi
nimejaribu kufuatilia na kusoma viongozi wa zamani hasa wa kwenye vitabu vya
dini, kiongozi wa enzi hizo, yeye alikuwa haangalii masilahi yake
kwanza...hashibi kwanza mpaka ahakikishe watu wake wameshiba, je kwa karne hizi
unaweza kumpata kiongozi kama huyo....angalau, asema mimi sitaki gari la
gharama, maana mahospitali hayana dawa...yupo wapi..hakuna...sasa tufanyeje..’akaangalia
saa yake.
‘Tufanyeje?’
nikamuuliza
‘Tutafanya
nini, wakati watu hamtaki kusema ukweli, semeni ukweli, kuhusu ubaya wa
viongozi wenu, mumewachagua wenyewe, ...mna haki ya kuwauliza kila
wanachokifanya, lakini kwa nia njema, sio kwa majungu..ni haki yako kumuuliza, nay
eye ni haki yake kujieleza, sio aulizwe halafu anakuja juu...utakujaje juu,
wakati mwajiri wako anakuuliza...naona ajabu kabisa...’akasema
‘Mhh,
muajiri wako, ina maana mwananchi ndio mwajiri wa kiongozi wake...?’ nikauliza
‘Kiukweli
nio hivyo, ila kinadharia,...sio rahisi, kiongozi akishashika madaraka wewe
huna usemi mbele yake, ...hilo linakuwa ni tatizo..na huyu iongozi hataogopa
kufanya dhuluma,...keshakuwa juu ya sheria,...unapofanya ubaya, kinyume cha
utaratibu umeshajivika ukubwa juu ya hiyo sheria uliyoivunja, au sio...’akasema
huku akionyesha kukerwa na kitu.
‘Hebu nikuulize swali, umesema huyo mlinzi alikwenda kwenye gari la mdada akachukua
nyundo, alijuaje kuwa kuna nyundo kwenye hilo gari?’ nikamuuliza nikiona
ninaweza kuachana naye bila kujua undani wa hilo tukio.
‘Ndio,
inavyoonekana alifahamu kuwa kuna kitu kama hicho, lakini sio lazima kwamba
hivyo vitu vilikuwepo hapo kwa malengo hayo....’akasema.
‘Hukumuuliza
huyo mlinzi akakuambia ukweli, huenda kweli ilipangwa iwe hivyo?’ nikamuuliza
‘Mlinzi
hajaongea yote hayo,..na haajwahi kusema ukweli kuwa yeye aliacha lindo na
kuingia ndani ya jengo,..au kuwa alikuja mtu akamuagiza kufanya hivyo...
hajawahi kumwambia mtu yoyote hadi sasa, hiyo imekuwa ni siri yake
tu....’akasema
‘Oh, sasa
wewe umafahamu vipi hayo yote?’ nikamuuliza nikisahahu kabisa kuwa natakiwa
kurudi hotelini haraka. Yeye kwanza akaniangalia , halafu akaangalia saa yake,
na kusema;
‘Mdada
atakuwa anakutafuta...’akasema na mimi nikawa kama mtu aliyepigwa kibao usoni,
nikainuka, nikitaka kuondoka, na yeye akasema;
‘Usiwe na
haraka kihivyo, haraka haraka haina baraka, ...waliotunga huo usemi walikuwa na
maana yao nzuri tu, na japokuwa sisi tunaharibu maana yake halisia, ...’akatulia
kidogo
‘Ina maana
kuwa, kabla ya kufanya jambo, hebu jaribu kulipangalia..usikurupuke tu,...wewe,
sasa unataka kuinuka na kuondoka, hujaangalia mazingira, je kuna usalama,
umeshasahau kuwa unafuatiliwa, kuna jamaa nje bado anakutafuta....kuwa makini,
usiwe mtu wa kuharakisha bila mpangilio...’akasema huku akiangalia upande wan
je.
‘Ok, haya
hebu nijibu swali langu wewe ulijuaje yoye hayo, kama mlinzi hakuwahi kumwambia
yoyote?’ niamuuliza.
‘Mimi ni
mpelelezi, na hiyo ndio fani yangu,....’akasema na kuangalia saa na akalivuta
kofia lake na kuficha sehemu kubwa ya uso, akavaa mawani yake. Mimi nikawa na
hamu ya kufahamu ukweli lakini muda ulikuwa umekwenda sana,..nikasema;
‘Kwanini
hutaki kuniambia, na wakati huo huo, wewe umesema unataka mimi niwe pamoja
nawe, katika kulimaliza hili tatizo, je mimi nitakuamini vipi, ....?’
nikamuuliza
‘Tatizo lako,
hujiamini,...unaperekeshwa tu,..kwanza jiamini, pili fahamu ni kitu gani
unachotaka kukifanya, kwa dhumuni gani, je kuna faida au hasara...wewe si
mhasibu bwana, hayo mbona ni moja ya kanuni zenu...’akasema huku akizidi
kuangalia nje.
‘Mhh,
kwahiyo...?’ nikauliza
‘Kwanza
hujataka kuniambia ukweli, mengi nimeyafahamu kutokana na juhudi zangu
mwenyewe, ...lakini kwa hivi sasa huna ujanja, ni mawili uwe na mimi ili
tulitumikie taifa letu kwa masilahi ya wananchi..huko ndiko kujitoa mhanga
nilikokusudia usije ukapotosha kauli yangu, maana watu siku hizi wanapenda
kudokoa kauli za watu, vipande vipande, na kujenga hoja za
uzushi...unamdanganay nani, wananchi...tuwe wakweli wa ukweli....’akasema
‘Sasa ili
kama unataka uwe na mimi, unahitajika kujitoa mhanga kiukweli...ni hatari, lakini
mwisho wa siku, utakuwa umeitetea jamii, na hilo ndilo muhimu, jamii kwanza,
watu wako kwanza...wewe na masilahi yako iwe baada ya watu wako
kushiba,..unaweza hiyo...sio rahisi, lakini kama huwezi, njia ya pili na
kujiunga na hilo kundi la wajanja wajanja waliojipenyeza kwenye mtandao (system) kwa kufanikisha masilahi yao...’akasema
‘Hapo
inakuwa ngumu, kwanza sijui kwa vipi, pili, ni nani wa kumuamini, na tatu mimi
sio askari...’nikasema
‘Hahaha,
hapo ndipo ninapomsifikia baba wa taifa kuhusu JKT, ni muhimu kila mtu akapitia jeshini,
akajijua, akajenga ujasiri wa kujilinda na kuilinda jamii....kila mtu
anastahiki kuwa ni askari...ni muhimu sana....’akasema na kusimama kwa haraka,
kwa haraka akawa kapitisha macho sehemu yote ya hapo ndani na kusema;
‘Sasa muda
umekwenda sana, rudi hotelini kwako, na jipange jinsi ya kuongea na mdada,...nahisi
mnaweza kukutana naye, au keshafiak hotelini kwako anakusubiria,.. ila na kupa
kama tahadhari, usije ukamwambia kuwa tulikutana mimi na wewe, ukimwambia
utajiharibia wewe mwenyewe, mimi sina shaka, kwani hiyo ni kazi yangu...ila
kwako wewe....’akasema akiinuka na kugeuka kuondoka
‘Mimi nina
maswali mengi ya kukuuliza, lakini kweli naona muda umekwisha, na sijui
nitamdanganya vipi mdada nikikutana naye...’nikasema
‘Hiyo ni
kazi yako...na hayo maswali uliyo nayo, yahifadhi hadi hapo utakapokuwa tayari
kushirikiana na mimi,....vinginevyo, nakutakia kazi njema, au jela njema, na kama
wataamua kukurudisha tena huko mahabusu, ...sijui,....’akasema huku akiinua
mguu hatua ndogo ndogo kuondoka na mimi nikawa nimeshasimama, na kuanza
kutembea
‘Hawawezi
kunirudisha huko....’nikasema nikijipa matumaini.
‘Unajiamini
vipi wewe, ok, ni muhimu kujiamini, lakini je kweli una uhakika na hilo?’
akaniuliza
‘Mdada
kasema hawawezi kufanya hivyo....’nikasema na kumfanya ageuka kuniangalia
halafu akaangalia kitu kwenye dirisha na kusema;
‘Jamaa yako huyooo,
anaondoka, naona kashakata tamaa, au kaitwa na wakubwa zake, na hapo inaonyesha
kuna jambo,.....’akasema
‘Jamaa yupi..na
jambo gani hilo?’ nikauliza
‘Huyo jamaa aliyekuwa
akikufuata nyuma,...nahisi kaitwa na bosi wake na naona ni kwa haraka, kuchukua pikipiki, na muondoko wake, sio wa
kuhakikisha kuwa kazi aliyotumwa kaimaliza hii inaashiria kuna jambo
huko...ngoja niondoke, ....’akasema
‘Sasa mimi
nifanye nini, huenda mdada keshafika hotelini ?’ nikauliza
‘Usijali,
nenda kakabiliane naye kama askari..jiamini, na utafanya nini, hiyo ni kazi
yako...tutaonana hivi punde...’akasema akitoka kwenye hicho chumba, na kuelekea
barabarani
Mimi
nikatulia kwa muda, nikaangalia dirishani, na sikuona dalili ya mtu wa mashaka,
nikatoka nje, sikumuona tena huyo mpelelezi na wala sikujua kaelekea wapi, mimi
nikaamua kuangalia hamsini zangu, na wakati nataka kuchanganya mwendo mara
nikasikia mtu akiniita jina nyuma yangu..
‘Oh ni nani
huyu tena....’nikajiuliza kimoyomoyo nikiogopa kugeuka
NB: Ni nani
huyu tena
WAZO LA LEO:Ubaya, majanga ,wizi, na hujuma
mbali mbali, zinafanywa na sisi wenyewe, na hata kama sio wewe mwenyewe moja
kwa moja, lakini jirani yako, jamaa yako au kiongozi wako ndiye anayefanya hayo na unafahamu na unamfahamu kuwa anafanya hayo yote, lakini kwa sababu mbali mbali hutaki kumfichukua...
'Ndio hutaki kusema
ukweli kwa vile, huenda mnakula naye,au ni mwenzetu, au, anakukatia kitu kidogo.
Sasa hali ikiwa mbaya, wewe unakuwa wa kwanza kulalamika, huoni kuwa chanzo ni
wewe...jichunge nafsi yako, chunga majirani zako, kwa kuwa wa kwanza kujilinda,
na kuilinda jamii yako, kwa kusema ukweli hata kama ukweli huo utakuumiza wewe
mwenyewe.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Nipo na wewe, twende kazi
Post a Comment