‘Mimi hapo sielewi,nakuona unaongea
tu, lakini sijakuelewa, hebu nieleze kwanini huyu mtu aliuwawa, na huyo muuaji
aliwezaje kuingia, na kufanya hayo bila ya hata mimi kufahamu?’ nikauliza
‘Mlinzi....’akasema.
‘Mlinzi ana nini?’ nikauliza
‘Ukiangalia mandhari ya lile jengo, utaona kuwa jengo
nzima, limezungukwa na ukuta mrefu,uliowekwa waya za umeme na nyaya za
usalama...ina maana mtu akizigusa tu, sio tu atashikwa, au kurushwa na huo
umeme, lakini pia kutatokea milio ya hatari....sijui kwanini mdada, alifanya
hayo yote,...anajilinda sana....’akasema
‘Labda ni
kutokana na pesa anazopata....’nikasema
‘Ukiangalai
hilo huo ukuta kwanza nimrefu, na pili hata kama utakuwa na ujuzi wa kuziharibu
hizo nyaya za umeme, ukapanda juu, ili uruke ndani, huko ndani nako kama
ulivyoona unakutana na nyaya za seng’enge, zailizozungukwa na miti ya michongoma....
'Miba ya michongoma hiyo ni mikali sana, kwahiyo kwa yoyote yule, atakayejaribu kufanya hivyo, ni
lazima awe amejiandaa, na kupajua sana,....sizani kuna mtu anaweza kufanya
hivyo, utajiumiza bure, kwahiyo...uwezekano wa mtu kupanda ukuta
haupo....’akasema.
‘Kwahiyo ina
maana gani, kuwa hakuna mtu aliyeingia, au kama kaingia ni lazima kapitia kwa mlinzi,
je mlinzi alikuwa wapi, alilala, au alitoka nje kidogo, au, hapo sieleai?’
nikauliza
‘Yule mlinzi
ni mjuzi wa kazi yake, huwezi kupita pale bila ya yeye kukuona,na hata kama
atapitiwa na usingizi, hisia zake ni kali sana, ni lazima atashituka, ...na
asingeliweza kuondoka na kuliacha hilo lindo bila kumuarifu bosi wake
ndani...namfahamu sana huyo mlinzi nimefuatilia utendaji wake wa kazi,
...hawezi kufanya uzembe wa namna hiyo...’akasema
‘Kwahiyo
unataka kusema nini kuhusu huyo mlinzi?’ nikauliza nikiwa bado
nimechanganyikiwa
‘Kuna
maelezo kayaficha,na kunifanya nimuhisi huyu mlinzi vibaya, kuwa anahusika kwa
namna moja au nyingine kulifanikisha zoezi zima la hicho kilichotokea hapo,
japokuwa sina ushahidi wa moja kwa moja, na siwezi kusema yeye ndiye aliyemuua
mtoza ushuru...’akasema
‘Una uhakika
gani na hilo?’ nikamuuliza na yeye hakutaka kunijibu swali langu moja kwa moja
akawa anaendelea kutoa maelezo
‘Kwa
vyovyote vile, ni lazima mtu aliyeingia ndani aliwasialiana naye kabla au, hata
kaam sio kabla, lakini kuna maongezi yalifanyia hadi kukubaliana, sijui labda
ni kwa malipo fulani,au kuna ushirika kati ya mlinzi na mtu mwingine....siwezi
kuamini moja kwa moja, kuwa mlinzi aliondoka pale kwa kuhadaiwa,....’akatulia
kidogo.
‘Kuhadaiwa
kwa vipi?’ nikamuuliza
‘Kuwa
alifika mtu akamvunga vunga, na huenda akatokea mtu mwingine akapita kwa
siri..hiyo inawezekana sana, lakini kwa jinsi mlinzi alivyofanya, inaonyesha
wazi kuna mashikamano, kuna makubaliano, kati ya mlinzi na huyo mtu mwingine....kwani
mlinzi aliondoka na kuacha lindo,akaingia ndani, na je alipoingia ndani
alifanya nini, ?’ akawa kama anauliza
‘Sijakuelewa,
wewe umesema huyo mlinzi hawezi kuacha lindo lake na kuondoka bila kuomba
kibali kwa bosi wake, je huo muda alioondoka aliwasiliana na nani, na alimuacha
nani lindo?’ nikamuuliza
‘Alipoondoka
hapo lindoni, alihakikisha kuwa kuna mtu kamuachia hiyo kazi, , ...’akasema
‘Mbona
unaongea kama vile ulikuwepo, alimuachia nani?’ nikamuuliza
‘Huyo
mlinzi, alimuacha mtu hilo lindo, baada ya wawili hao kuongea kwa muda mfupi,
na huyo mlinzi akaelekea ndani ya jengo, ....’akasema mpelelezi
‘Mhh, hapo
sikuelewi, ....kufanya nini, au unazungumzia ule muda mlinzi aliokuja kuniarifu
kuwa kuna mgeni kaja?’ nikamuuliza
‘Hayo
yalitokea kipindi wewe upo ndani, na huyo marehemu,na ni kama walishafahamu
kuwa ndani kuna tatizo, hapo sijapata uthibitisho wa moja kwa moja, bado kuna
kitu hakijakaa sawa,...nakueleza haya nikiwa na uhakika nayo...’akasema
‘Una uhakika!...mmh,
kwa vipi?’ nikauliza nikionyesha mshangao
‘Ilikuwa
hivi,..wakati nyie mpo ndani, alifika mtu kuonana na mlinzi, huyo mtu alivaa
kofia pana na miwani, waliongea kidogo na huyo mtu akawa anacheka kuashiria
kufurahishwa na jambo, na ilivyoonyesha, mtu huyo anafahamiana na huyo mlinzi...’akatulia
kidogo.
‘Kiukweli...waliongea
kama marafiki wanaojuana, sasa sina uhakika kama walikuwa wanajuana kabla au ni
ujanja wa huyo mtu,hapo sijawa na uhakika wa moja kwa moja, lakini kwa mtizamo
wa haraka huyo mtu anafahamiana na na huyo mlinzi, kwani alivyofika na kuongea
na yule mlinzi,walikubaliana kwa haraka sana...’akatulia
‘Kwahiyo,
ninaweza kusema kuna kitu kati ya huyo mtu na huyo mlinzi, na mlinzi hakulisema
hilo na hataki kusema hivyo, wao walipomaliza kuongea tu yule mlinzi akaondoka
kwenye lindo lake na kuelekea ndani, nafikiri alitumwa kitu fulani na huyo mtu
...’akasema
‘Alitumwa
kitu, kitu gani...?’ nikauliza
‘Huenda ndio
hicho hicho alichokuwa akikitafuta marehemu, huenda kuna kitu kingine, hapo
hakujafahamika vyema...’akasema
‘Sasa, hebu
...sijaelewa hapo, huyo mtu aliyefika na kuongea na mlinzi ni mtu gani,mbona
humuelezi , ina maana huyo mtu hafahamiki, na ooh, ina maana hayo yote
uliyapatia kutoka kwa nani, ni mlinzi, alikuelezea au...?’ nikauliza
‘Ninachotaka
uelewe hapa ni kuwa huyu mlinzi ana mafungamano na huyo mtu, na nahisi
wanajuana kabla, ndio maana alipofika tu, na kutoa maagizo huyo mlinzi
hakupinga, akaondoka na kuingia na ndani, sasa yaliyotokea huko ndani ndio sina
uhakika nayo...’akasema
‘Mlinzi...hakukuelezea,
mbona mimi sikumuona...hapana sizani kama ni kweli....’nikasema
‘Kama
sikweli, ni nani alikupiga na nyundo kichwani...ni lazima kuna mtua liingia,
akaweza kufanya hayo...hebu fungua akili yako vyema....’akasema huyo mpelelezi.
‘Mimi
ninachotaka kufahamu kwanza, ni jinsi gani ulivyoyafahamu hayo, ni mlinzi
alikuelezea hivyo?’ nikamuuliza, na huyo mpelelezi bila kujibu swali langu moja
kwa moja akaendelea kuongea;
‘Ninachotaka
kufahamu zaidi, ni jinsi gani huyu mlinzi alivyomfahamu mdada,...hapo kuna kitu
kingine muhimu sana,... kwani hajafanya kazi kwa huyo binti kwa muda mrefu wa
kumfahamu mdada kihivyo, unaona hapo....,lakini inavyoonyesha, ni kuwa alikuwa
anafahamu matatizo ya mdada, na jinsi gani ya kupambana naye, ndio yeye ni
askari ana mbinu nyingi, lakini sio kwa jinsi ilivyotokea, hapo nahitajia
kupaangalia...’akatulia
‘Bado mimi
hapo sijakuelewa, kama mlinzi aliweza kukuelezea yote hayo, jinsi alivyoweza
kuacha lindo la kuelekea ndani kutokana na maagizo ya huyo mtu usiyetaka
kumtaja ni nani, basi angeliweza kukuelezea jinsi alivyomfahamu mdada, au sio?’
nikauliza.
‘Nimeshakuambia
kuwa mlinzi ameweza kuongea , lakini kuna mambo anayaficha, hataki kuyaweka
wazi, na ni kutokana na jinsi alivyoshibana na huyo mtu wake...nimeongea naye
mara kadhaa na hata kutoa shinikizo la kumtisha, lakini hakuweza kunifafanulia
zaidi,inaonyesha kuwa hapo alipokuwa kwa mdada, pia alikuwa kazini kwa ajili ya
mtu fulani,....’akatulia
‘Kwa maelezo
yako, ina maana huyo mlinzi anaweza kuhusika na mauaji ya mtoza ushuru?’
niamuuliza
‘Kwa maelezo
yake binafsi,hahusiki, .....’akasema
‘Umemwamini
?’ nikamuuliza
‘Siwezi
kumwamini moja kwa moja, ndio maana nataka ushirikiano wako, ...nikiweza kujua
ukweli wa kilichotokea ndani, ninaweza kupata uhalisia wa tukio zima, na
itaniwezesha mimi kuweza kukusanya ushahidi zaidi na kuimaliza hii kesi haraka
iwezekanavyo....japokuwa kwa hali ilivyo
itakuwa vigumu sana kumshawishi hakimu.....’akasema
‘Mhh, hebu
niambie ukweli, ...ni mlinzi aliyeweza kukuelezea yote hayo, na kwanini polisi
hawajamkamata, ?’ nikauliza
‘Polisi wana
namna yao ya utendaji wa kazi, kwa hivi sasa, kama nilivyokuelezea, wanafanya
kutokana na maagizo waliyopewa, hata hivyo, huwezi kujua, ....huenda wanavuta
muda, kuchukua hatua fulani, mimi nafanya kazi kwa namna yangu, siingiliani na
hao watu....’akaangalia saa yake.
‘Hebu
niambie mlinzi alivyokuelezea, kwa jinsi alivyoweza kushawishiwa na huyo mtu
akaacha lindo na kuingia ndani kupambana na mdada,...?’ nikamuuliza
‘Elewa
hivyo, mlinzi aliongea na huyo mtu akapewa maagizo, na mlinzi bila kupoteza
muda, akaondoka na kuingia ndani, hakuingia ndani moja kwa moja, alikuwa
akiangalia mara kwa mara kupitia dirishani, kuona ni kitu gani kinaendelea huko
ndani, na alipoona kuna nafasi ya kufanya hivyo, akaingia ndani....’akatulia na
kuniangalia
‘Ndio maana
nakuambia kuwa huyu mlinzi alishamfahamu mdada, na alishajua ni wakati gani wa
kuweza kupambana naye, ..ni mahesabu ya hali ya juu yaliyotumika...’akasema
‘Mimi
ningelimuona huyo mlinzi akiingia, sizani, kama aliingia, na alipitia wapi....’nikasema
‘Kitu alichotumia
kama silaha ni nyundo tu,...ile nyundo hata polisi hawakufanikiwa kuipata,
kwani baada ya hilo tukio, ilipotea kabisa...., lakini hiyo nyundo ilikuwa
ndani ya gari, na yeye ni kama alifahamu kuwa kuna kitu kama hicho kwenye hilo
gari,....’akasema
‘Ina maana
huyo mlinzi likwenda sehemu ya kuegesha gari, na akaweza kuiona hiyo nyundo, ni
kutoka kwenye gari la nani?’ nikauliza maana siku hiyo ya tukio kulikuwa na
magari mawili, moja la mdada, na jingine la marehemu.
‘Nyundo hiyo
ilipatikana kutoka kwenye gari la mdada....’akasema
‘Oh, mbona
sielewi....’nikasema
NB: Hata
mimi sielewi,...ngoja tuone sehemu ijayo,...
WAO LA LEO: Ili kuwa na yakini na jambo lolote,
ni muhimu kufanya utafiti kabla hujahitimisha kauli yako. Watu wengi wanaona
kuwa, kuongea vyema, kutoa propaganda,
kushawishi hata kama ni ubishani ni namna ya kuonyesha kuwa unafahamu jambo, hata kama halina ukweli, halina uhakika,lakini
kwa vile lengo ni kufanikisha jambo kwa masilahi, basi upo tayari kutumia mdomo
kushawishi watu wakubaliane nalo. Tusifanya hivyo, kwani hatima ya uongo ni
kuja kuumbuka tu.
1 comment :
Bravooh, i salute u friendo, kazi nzuri, ubarikiwe sana, tena sana
Post a Comment