Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, April 12, 2013

Ni nani kwa kumfunga paka(simba) kengeleSimba alikuwa katulia pembeni, akiwa katunisha misuli yake, na meno makali yalionekana wazi, yakiashiria kuwa yapo tayari kukatakata vipande vya nyama kwa yoyote itakayoingia kinywani mwake.  Kwa mbwembwe, akayataraza makucha yake kwenye nyasi, na nyasi zikakatika katika vipande, bila kujali kuwa hizo nyasi ndizo zinazomuwezesha kuishi kwenye hali bora.

Upande wa pili walikuwepo wanyama wengine, ambao wengi wao ndio chakula cha simba, waliona wakutane wajadiliane jinsi gani watakavyoweza kupambana na huyo simba, kwani wao wamekuwa kitoweo cha mnyama huyo, ambaye kila kukicha alikuwa akiwashukia na kuwararua bila huruma.

Mnyama wa kwanza akasema; ‘Jamani hivi kwa umoja wetu tunashindwaje kumdhibiti huyu simba, akija hapa tunajikusanya kwa pamoja, tunamkabili huyu adui yetu.?’

‘Tatizo wengi wetu kama unavyotuona ni wanyonge, hatuna nguvu,…lakini pia  hata tukikaa pamoja, watoto wetu wanachezacheza ovyo, na kama unavyomuona akitukosa sisi anawakimbilia watoto wetu, ….’akasema mnyama mwingine.

‘Kwahiyo tufanyeje?’ akauliza mmoja wa wanyama.

‘Hatuna jinsi, sisi wanyonge, iliyobakia kwetu ni kula nyasi kwa wingi, ..tukila nyasi kwa wingi , tutakuwa na miili mikubwa , kama hawo wanyama wengine wanaogopewa na simba, tunaimani kuwa  huyu simba atatuogopa na sisi…’akatoa maoni mmoja wa wanyama hao na kweli maoni hayo yakaonekana yana maana kwao.

Wanyama wale wakawa wanafuata mawazo hayo ya mnyama mwenzao ya kula majani kwa wingi, na kweli majani yakawa yanaliwa kwa wingi,  na matokeo yake ni kuwa mbuga za majani zikawa kama vichaka, …., na matokea yake mvua zikawa haba, kwani kama ujuavyo mvua zinatokana na miti na majani,  na miti na majani yamekuwa yakitafunwa na hawa wanyama kwa fujo, bila kujali hiyo athari.

Simba, akawa anameza mate kwa tamaa, japokuwa hakuweza kuwala wanyama wakubwa kama ilivyo kawaida yake, kwa vile walikuwa wakimpa shida, lakini aliweza kuwala watoto wao walionona…kwake yeye, hajali kwani japokuwa anawakosa wanyama wakubwa, lakini bado vipo vitoto, vilivyonona.


Haya ndio maisha yetu, ….Serikali, ipo ikisubiri kodi za wafanyabiashara, bila wao shughuli zao haziwezi kwenda, wafanyabiashara hawa na wawekezaji, kila kukicha wanabuni mbinu mbali mbali ili waweze kujiendesha kwa faida, na hata kukwepa kodi.  Na kila wakiona wamekwama, sehemu ya kukimbilia na kuwabana walaji kwa kupandisha nauli, au bei za vitu vyao.Leo wafanaybisahara wa usafiri, wameona ili kuweza kumudu gharama za usafiri, ni kupandisha nauli, wanayempandishia nauli ni mwananchi, …sio serikali , ambayo wengi wanainyoshea kidole. Kwani wao ndio walioweka kodi kwenye vipuri, wao ndio wanaotakiwa kuweka miundo mbinu ziwe bora, wao ndio wasimamizi wa shughuli mbali mbali za kuwewezesah kwenye huduma zao.

Lakini badala ya kumkabili huyo serikali,….kwa kulipa kodi ipasavyo,au kwa kumgomea huyu serikali kuwa wasilipe kodi kwani kado zao hazifanyi yale yanayostahili kwao….wao wanamgeukia mlaji, mtumiaji, kwa kisingizio kuwa, hata mzalishaji, anapoona gharama zake ni kubwa, atakachofanya ni kupandiha bei bidhaa zake ili aweze kupata faidi.

Wengine wameshau kabisa wao ni watoa huduma , na haingelihitjaji sana kuwa na faida kubwa ukijilingaisha na makampuni, kama hawapati fadia, mbona kila kituo wanatoa pesa za bure kwa wapiga debe ambao hata kazi ya kupiga debe hawajaifanya, na hata kuweka wale wanaoitwa `maday-worker' huku madereva halisi wakikimbilia nyumba ndogo,..... Ndio maana wakapewa mbinu za kujibadili na kuwa makampuni, ili wazipate hizo faida nono, kama hawo....!

Kwa mtaji huu wao wanataka kunona , ili waweze kuwa makampuni makubwa, ili serikali iwaogope, kama wanyama wanavyomuogopa simba, bila kujali kuwa wanyemkomoa sio serikali, ni mwananchi….oh ama kweli, wakipambana mafahali wawili mwisho wa siku zinazoumia ni nyasi.

Kwanini kila jambo linalowakwaza hawa wafanyabiashara , makampuni, madakitari, nk, hasira zao wanazipeleka kwa wananchi? Swali hilo likaulizwa na wanyonge kwenye daladala.

‘Kwani serikali ni nani?’ akauliza mzee mmoja

‘Serikali ni wewe na mimi, lakini kuna watendaji ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuwezesha hizo shughuli, hawo ndio serikali, na kwa maneno mengine, serikali ni wale watu walioajiriwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia shughuli zao…’akasema mzee mwingine.


‘Kwahiyo ndio maana makampuni, wafanyabiashara, madakitari, wakikwama wanagoma, na wanayemgomea ni mwajiri wa hawa wanaoitwa serikali. Tusilalamike, kosa ni letu sote wananchi, kwa vile tumewaajiri watu wasio na masilahi na wao.

‘Tatizo jingine ni kuwa, watendaji hawa walioajiriwa kama serikali ndio hawo hawo wafanyabishara, ndio hawo hawo wenye hisa kwenye makampuni mbalimbali, ndio hawo hawo wawekezaji kwenye usafiri, nk, je hapo unategemea nini, ….

Unategemea kuwa huyu mfanyabishara atawatetea wananchi, ili yeye apate hasara, haiwezeani, Na hapo ndio unakumbuka busara za wazee wetu walioliona hilo, kuwa mtendaji wa serikali hahitajiki kuwa hisa mbili, huko serikalini na huyo huyo ni mfanyabiashara, muwekezaji,….

Muda umefika, kwenu nyie, waajiri wa serikali, kuchambua pumba na mchele, ….na hilo linawezekana, tuhakikishe wale tunaowaajiri kweli wana maslahi na sie,…kwani ukiangalia mali yake kama kigezo cha kumuajiri, siku akiwa madarakani, hatakuangalia wewe, yeye ataangalia mali yake kwanza.

‘Chagueni viongozi bora, kwa maslahi yenu…vinginevyo, tutabakia kulia kila siku…..vinginevyo, tutageuzwa kuwa majani, wa kutafunwa huku wenzetu wananona, …..wakimuogopa Simba, Simba ambaye sisi tunaweza kumdhibiti, kwani anaishi kwenye mapori yetu, au sio

Swali ni nani wakumfunga paka kengele?

NB: Kisa chetu kinaendelea bado naweka mambo sawa, lakini nimeona niitoe hii kwenye diary yangu,

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Tumekupata mkuu,lkn wao watakusikia?

Anonymous said...

I absolutely love your blog.. Great colors & theme. Did you create this website yourself?

Please reply back as I'm wanting to create my very own website and would like to know where you got this from or what the theme is called. Thanks!

Also visit my web page ... landing page