Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 1, 2013

Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-54
‘Kumbe huyu mtoto anayeishi naye hapa sio wa kwake,….huenda amechukuliwa ili ikifikia muda wake, afanyiwe kama alivyofanyiwa yeye…..akasema kimoyo moyo, `Namsikitia sana binti wa watu , maana naona hali ya usichana inaanza kumuingia, mwili unaanza kumpendeza…na dhamira na malengo ya mashetani hawa itatimia, na watamfanyia kama walivyonifanyia mimi….’akasema Maua akiendelea kusimulia kisa hiki.

‘Utajiri wa huyu mtu umefangamana na mambo ya kishirikina, na ndio maana anatafuta wasichana wabichi…uwe makini…’akakumbuka maneno ya rafiki yake mmoja aliyefika ofisini kwake siku moja kumtembelea….

*******

‘Na ole wako ukimwambia……huyo ni mtoto wangu, …’akasema mama yake mdogo kwa hasira, pale Maua lipojaribu kumuuliza swali, alipokumbuka ile kauli yake aliyosema kuwa yeye hazai kwa vile hana kizazi.

‘Mama huna kizazi, …ina maana huyu mtoto unayeishi naye hapa sio wa kwako wa kumzaa, mbona, mnafanana….?’ Akauliza

Yule mama alimtizama kwa hasira, na akawa kama kakumbuka jambo, akakumbuka kuwa kaongea hata yale aliyokuwa hataki kuyasema kwa watu, …..akamsogelea Maua na kumshika kwa nguvu begani, na kumtolea macho yaliyojaa hasira, chuki….na ndipo akasema;

‘Na ole wako ukimwambia……’akatulia na kama vile kakumbuka kitu , kuwa hakutakiwa kufanya hivyo, akasema kwa sauti ya kujilazimisha, sauti ya upole,…..

‘Huyo ni binti yangu…ehe..huoni tunavyofanana….’akageuka na kutizama nje…kuficha yale macho yake ambayo yalishaanza kujaa ukungu, ukungu wa machozi, majonzi, ….japokuwa kwa mbali, husuda, chuki, na roho mbaya, ilikuwa imeshika kasi, na hakujali hayo anayotarajia kuyafanya…

*********

Maua akiwa kachoka na kazi za ndani, akaenda kwenye sofa na kukaa, na hapo hapo usingizi wa mang’amu ng’amu ukamnyemelea na kabla hajazama kwenye usingizi , ndipo akakumbuka maisha yake ya nyuma, …..na siku ikaanza kuita…

‘Maua mbona hupokei hiyo simu, umesahau kuwa sasa hivi wewe ni mfanyakazi wa Tajiri, na moja ya masharti ya kazi yako ni kuwa uwe tayari kwa wakati wowote, iwe ni usiku au mchana, ukiitwa , unahitajika kuitika….ukumbuke mwenzako kashika mpini, anaweza kukuzalilisha nay ale yaliyotokea siku ile…’mama yake akamwambia pake simu ilipolia kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Maua aliposikia hivyo, akainuka haraka, na kupiga miayo,..na akili yake ikawa imenasa hayo maneno, `yale yaliyotokea siku ile,….’akaisogelea ile simu huku akilalamika;

‘Lakini mama mbona ni usiku  sana….’akasema huku akiishika ile simu, na akaona ikionyesha ni saa sita za usiku

‘Jamani saa sita za usiku, ….’akalalamika, na akawa keshabonyeza kitufe cha kupokelea na sauti ikasikika kwenye simu; Sauti iliyomfanya apoteze usingizi wote, na akili ikawa imevurugika, akawa kama kachanganyikiwa, an jasho likaanza kumtoka, hasira, chuki, kichefuchefu kikamzonga, akawa anatamani kuitupa ile simu, lakini hakuweza, ilikuwa imeganda mkononi kama imewekewa gundi,….akasikia maneno yale yakipenya kwenye ubongo wake;

‘Wewe mwanamke kwanini hupokei simu yangu,….hujapewa maagizo yangu, …..mwambie mama yako akulete ofisini haraka, ….’sauti ikasema, na hapo hapo Maua  akainuka pale kitandani haraka, alihis kichefu chefu mwili wote ukafa ganzi, …akili ikashindwa kufikiria, na hisia za kichefu chefu zikamjaa na akainuka haraka kukimbilia bafuni.

‘Ni nani aliyekupigia?’ akauliza mama mdogo akimfuatilia kwa nyuma.

‘Ni huyu mtu wako, eti anasema unipeleke ofisini usiku kama huu,, …..mama jamani mbona hivi, habeu angalia muda, saa sita za usiku, huko ofisini tunakwenda kufanya nini , mimi siendi kwanza najisiki vibaya’akasema.

‘Ina maana keshafika tena,….najua safari hii itakuwa kafika na pesa nyingi….na hushukuru kuwa bado anakujali, ingelikuwa wengine, asingelisumbuka kabisa, keshapata alichokita, anahitaji nini tena, …hata hivyo, hali uliyo nayo ni vyema ukaiweka wazi kwake….haya jiandae twende…’akasema mama yake, huku akionyesha kufurahia.

‘Mama…muda huu twende wapi, kuna kazi gani za usiku…’akalalamika Maua.

‘Kazi za huyo jamaa hazina muda maalumu, wewe jiandae twende, nilishakuambia kuwa wakati ndio huu, usipoutumia vyema, utabakia huna kitu….na mzigo huo utaubeba peke yako, nilishakuambia tukautoe..ukabisha, haya twende huko …..’akasema mama.

‘Hapana mama, mimi najisikia vibaya,….siwezi tena,…..mlichonifanyia safari ile, sitakisahau tena….najuta kwanini nilikubali kuingia kwenye mambo yenu,…..yaani hapana…’akasema Maua akikumbuka matukio yaliyotokea miezi miwili iliyopita, matukio ambayo yalibadili maisha yake yote, na akasimama akimwangalia mama yake, akiwa keshajiandaa,…na hapo kumbukumbu za nyuma zikaanza kumtawala kwenye kichwa chake…

*********

‘Bwana mkubwa anakuja leo, unahitajika kujiandaa, na ujio wake ni wa kipekee kabisa, kwani anakuja kwa ajili yako, na anakuja na wageni wake mashahuri,…’akaambiwa na tarishi wa tajiri,

‘Anakuja saa ngapi, mbona hajaniandikia ujumbe wowote kwenye simu…?’ akauliza.

‘Hiyo ndio kawaida yake,… ndio hivyo, haitakiwi kujulikana anakuja saa ngapi,….nimeambiwa nikuambie wewe tu, kwa vile unahitajika kuwa tayari kwa ajili yake’akasema huyo jamaa

‘Tayari kwa vipi,..?’ akauliza Maua kwa mashaka.

‘Kamuulize mama yako atakuelekeza..’akasema huyo tarishi akitabasamu, na hakuongea zaidi akaondoka. Na baadaye Maua akafika nyumbani na kumuelezea mama yake kuhusu huo ujumbe alioupata.

‘Safi kabisa….’akasema mama yake huku akionyesha kutokushangaa, ilikuwa kama vile anafahamu mengi kuhusiana na huyo mtu…`mtu wake’ kama alivyozoea kumtaja mbele ya mama yake huyo.

‘Safi kwa vipi mama…mama huyu mtu wako mna mipango gani na mimi, mbona siwaelewi?’ akauliza Maua, na mama akawa hasemi kitu, akachukua karatasi na kalamu, na akawa anaandika namba, zikionyesha ni tarakimu za pesa, ….na alipomaliza, akamwangalia Maua, na kusema;

‘Tukipata milioni tano,…..moja wewe, moja mama yako na nyingine tunaweka akiba….’akasema huku akitikisa kichwa kuonyesha anakubalina na mahesabu yake na kutulia akimkagua Maua kuanzia kichwani hadi miguuni.

‘Milioni tano kutoka wapi?’ akauliza Maua.

‘Hilo sio swali la msingi kwa sasa, cha muhimu…ni wewe kujiandaa….sikiliza, unatakiwa uvae lile gauni nililokununulia,…na uje hapa kwanza ni kurembe, urembeke….sasa tunaingia kazini, na ili upate malipo halali ya kazi yako, ni lazima ufanye kazi…usifikiri kazi ni hiyo ya kukaa ofisini tu…hiyo ilikuwa ni matayarisho tu, kazi sasa ndio hiyo inakuja….’na kabla hajamaliza simu ya yule mama ikaita.

‘Haloh,..ooh umeshafika…basi tusubiri tunakuja….usiwe na wasiwasi, kabisa….nakuhakikisha kuwa ni ngoma mbichi…mwenyewe utaona, sawa, kama nakudanganya…usinipe chochote….sawa tunakuja….’akasema mama na kuanza kumuharakisha Maua,…

‘Tayari bosi keshafika, na safari hii kafikia hoteli kubwa ya kitalii…twende haraka, …’akasema na kumshika Maua mkono, wakaondoka huku Maua akilalamika kuhusu kile kivazi alichoambiwa akivae, alijiona kama yupo uchi.

‘Mama mimi siwezi kwenda mbele ya watu nikiwa nimevaa nguo kama hii…’akalalamika

‘Kwani wewe ulitakaje, ..ulisema unataka kuwa mwanamitindo, au sio, ukataka uwe muigizaji au sio, hebu niambie kazi hizo zote hazikuhusu kuangaliwa na watu?’akamshika mkono kwa nguvu, hadi Maua akasikia maumivu.

‘Mama unaniumiza….’akalalamika.

‘Kama hutaki nikumize fauata ninayotaka …fuata masharti ya mkataba wako wa ajira..unafikiri milioni zoet hizo utazipata hivi hivi tu…’akaambiwa.

‘Mimi sijakuambia kuwa nataka milioni, kwanza mbona mimi sijaongea lolote kuhusu malipo na huyo mtu wako’akasema.

‘Nimeshaongea naye, kakubali……’akasema

‘Kakubali kuhusu nini?’ akauliza Maua.

‘Sasa hayo maswali yako yananikera…wewe fuata ninavyokuambia, mengine yatajileta yenyewe…’akaambiwa na wakawa wameshafika hpo hotelini.

Walipofika tu wakakaribishwa kwenye meza iliyokuwa imeandaliwa kinamna yake, …na maua yalikuwa yamepambwa, kila kona kuizunguka meza hiyo ….

‘Hapa kuna harusi?’ akauliza Maua,akiangalia yale mapambo, …akawa anaonyesha uso wa furaha kwani yeye ni mpenzi mkubwa wa mapambao hasa maua…

‘Hahaha…..unaanza kuvutika au sio…..uzuri una raha yake, ningelifanyiwa mimi hivi, mbona ningefurahi, lakini ..mmh, kweli penya miti, hakuna wajenzi’akasema mama na mara hali ikabadilika, kwani yule tajiri alikuwa anakuja na watu waliokuwa pembeni, wengine wakasimama, kuonyesha heshima zao, yule tajiri akawa anawapita bila kuwajali, na nyuma yake kulikuwa na wapambe wake, waliojazia vifua, suti nyeusi, na miwani ya kuficha macho,ilikuwa haitoki usoni.

‘Karibuni sana….’akasema huyo tajiri, na macho yake yakatua kwa Maua, akatabsamu,…..

‘Mhh, mambo sio hayo,…akageuka kuwaangalia watu waliokuwepo hapo, akasema;

‘Siipendi hii hali, ilitakiwa tubakie mimi na wewe tu, lakini, hakuna jinsi…’akageuka na kumwangalia mama mdogo wa Maua akasema;

‘Nakushukuru mama ….mhhh, mama mkwe….;’ kaguza jicho kumwangalia Maua na huku akimminyia jicho moja, kama anakonyeza, na Maua akawa keshajua kuwa hiyo ndio tabia ya huyo mtu kumkonyeza konyeza, kitendo ambacho hakuwa anakipenda.

‘Wewe njoo ukae hapa karibu na mimi….’akasema Tajiri, na Maua kwa aibu akainuka pale alipokuwa kakaa na mama yake, na alifanya hivyo baada ya kufinywa na mama yake kuashiriwa kuwa afanye hivyo . Hatua ya vinywaji, ikaanza, …vinywaji baridi,..na Maua akanywa juisi…

‘Usiogope kula hii yote ni kwa ajili yako….’akaambiw ana huyo tajiri.
Baadaya chakula …..baadaye kikaletwa kinywaji kikali…na meza ikabadilika…Maua alishajiona kushiba, lakini …

 ‘Unatakiwa leo uonje kinywaji kikali….’akaambiwa, na Maua akakataa kata kata….
‘Mimi sinywi pombe….’akasema na hakumbuki ilikuwaje, ila anachokumbuka ni kuwa alitoka kidogo kwenda haja, na aliporudi, akachukua kinywaji chake cha juisi, na lipokunywa, akahisi macho yakiwa mazito…..na hata alipojitahidi kuyalazimisha kuona vyema hakuweza,…na ikawa kama anavutika kufanya jambo, mwili ulikuwa sio wake tena…na akawa anasikia..sauti ikisema ..

‘Kunywa…..’na aakachukua gilasi na kunywa…hakuangalia nini kilichokuwepo kwenye gilasi iliyopo mbele yake akawa anakunywa,..na kila akiiweka mdomoni, haibandui mapaka gilasi ilipokuwa nyeupe, na akiiweka mezani, anasikia sauti ile ikisema `kunywa,’ na anakunywa…akawanywa na kunywa, na hakuweza kujijua tena,….

********

Alipozindukana alijikuta yupo kwenye kitanda kikubwa cha kifahari…..akageuza kichwa, akahisi maumivu makali, …..

‘Kichwa…..’akalalamika huku akishika kichwa chake….

‘Mleteeni dawa,…..na kinywaji cha kawaida,…kitamfaa kuondoa hiyo hali…’akasikia sauti, sauti iliyomfanya azindikane, na mwili ukawa unahisi uwoga..akainuka haraka na kukaa kitandani, akajikuta yupo mtupu…akalivuta shuka na kujifunika, huku akionyesha kuogopa….

‘Hahaha…sasa hivi unaona aibu..mbona jana ulikuwa unafanya mambo ambayo sikuwahi kuhisi kuwa binti mdogo kama wewe unaweza kuyafanya…’akasema yule mwanume akiwa kafunga taulo kiunoni, aliinuka pale alipokuwa kaka, na kifuani alikuwa mtupu…minyama ya uene, ikawa inacheza cheza mwilini, akitembea kusimama pale alipokaa Maua.

Maua, akawa amekaa na kujikunyata, mikono ikawa imeshikilia miguu, na kichwa kikawa kimelalia kwenye magoto yake….na akainua kichwa na kumwangalia yule mbaba, akasema kwa kushangaa,….

‘Eti nini….’akasema Maua huku akizidi kujikunyata na kuhakikisha lile shuka la kitandani, limemfunika kila sehemu ya mwili wake, kuacha kichwa tu….

‘Usihangaike, ….najua akilini mwako, utasema labda nimekulazimsiha,…..sijakulazimisha kabisa…umeyafanya hayo kwa hiyari yako mwenyewe, na ushahidi ninao,….’akasema yule mbaba, na kucheka kicheko cha dharau.

Maua akashika shavu kwa huzuni….

‘Mimi silazimishi mtu,…hata siku moja, ….kama ubaisha ngoja nikuonyeshe ushahidi, ili usione kuwa nimefanya haya kwa kukulazimisha….’akasema yule mtu na kwenda mbele, kulikuwa na runinga iliyowekwa kwenye meza,…na akatoa mkanda wa video kwenye mkoba wake, akauweka mkanda kwenye kitufe cha kuchezea mkanda na ile runinga ikaanza kuonyesha,…

Maua alibakia mdomo wazi, hakuamini yale aliyoyaona, hakuamini kuwa ni yeye aliyekuwa akifanya hivyo,….mambo ya aibu,…hakutaka kuyaangalia, kwanza akainama na kuficha uso wake, na baadaye bila kujali kuwa yupo uchi, akainuka na kwenda kuutoa ule mkanda, akahakikisha kuwa umeharibika kabisa…akavunja vunja…..

‘Hahaha…unaona aibu, kwa hayo…mbona kitu kidogo sana hicho…..usihangaike, sina nia mbaya na wewe…na usizanie kuwa ninaweza kwenda kukuonyesha hadharani, hapana, ila nilitaka kukuonyesha kuwa sikukufanyia hayo kwa kukulazimisha….na nataraji, ujira wako, utaupata kama kawaida, na mengine yatafuata,….kama upo hiyari….kama unataka kuwa na mimi….sikulazimishi….mimi nimeshatimiza wajibu wangu…na haya yote ni kwa ajili ya kuwatafutia nyie mali,….watoto wazuri kama nyie mnahitaji raha…sasa raha ni gharama, na gharama inahitaji pesa…na pesa haziji hivi hivi, …’akatulia

‘Laana itawashukia nyie wote….masikini mie, nitauweka wapi uso wangu….sikujua haya yote kumbe ni ….jamani, tumewakosea nini nyie…ina maana umasikini wetu ndio unatufanya tuzalilike hivi…nashukuru sana…’akasema na haraka bila kujali kuwa yupo uchi, akageuka huku na kule kutafuta nguo ya kuvaa, akakiona kile kigauni alichokuwa kakivaa usiku, akakivaa,…

Hakuamini kuwa alivaa nguo kama ile usiku ….kwake yeye ilikuwa kama nguo ya mtoto, na akajaribu kukivuta chini kile kigauni kishuke chini, kwani kilikuwa kinavutika, lakini hakikuweza kufika kwenye mgaoti,….hakuamini…ina maana keshakuwa Malaya..

‘Mungu wangu….nimefanya nini….nimefanya nini…’akaanza kulia, akageuak huku na kule, ..baadaye akatoka na kwenda bafuni, kule akachuchumaa na kuanza kutapika, alihisi mwilini kaingiwa na uchafu, uchafu ambao, kama ingelikuwa uwezo wake, angeliuatpika wote, na mara, akahisi maumivu makali, tumboni na sehemu zake za siri….akakunja uso…..huku akiendelea kusema;

 ‘Nimefanya nini masikini…nimefanya nini mie binti wa mama masikini….’

Akatoka mle ndani,…na alipofika kule chumbani hakumkukuta yule tajiri..akaangali huku na  kule, hakujua anatafuta nini….akaona dawa, zimewekwa pale mezani…..zilikuwa dawa za kichwa alizoletewa,..akaona hazifai….akatoka nje, na kwenda kwenye duka la dawa akanunua dawa za malaria.

Alirudi chumbani kwake, akachukua maji, kwenye gilasi, akazimimina zile dawa kwenye mkono, bila kusubiri, akazitupi zote mdomoni….akachukua maji kwenye gilasi, akanywa, na japokuwa zilikuwa chungu, lakini alizimeza kwa haraka, hadi zote zikaisha….baadaye tumbo likaanz akuuma,

‘Mama..nakufaa…’akaanza huku akishikilia tumbo na kujinyonga nyonga, maumivi aliyosikia yalikuwa makali sana, hakutegemea kuwa itakuwa hivyo, akili ikawa inajuta, …akaanza kuhisi kizunguzungu…mauimvi yakawa yanazidi kila sekunde,i…hakuweza kuvumilia zaidi akapiga ukulele wa kuomba msaada, ukelele uliojaa chumba kizima, ukulele huo ukasikika nje, …

Watu wlaipofika walimkuta sakafuni akiwa anatoa mapofu mdomoni…

‘Amejiua…..’ikawa ndiyo sauti ya mwisho kusikia kabla hajazama kwenye kiza kinene.

NB: Ndio hayo kwa leo….

WAZO LA LEO: Pole sana kwa wale waliowahi kukutwa na machungu,….mengine yakulazimishiwa, tusikate tamaa, yote tumkabidhi mungu, na tuwe na subira, ….mungu yupo pamoja na wale wote wanaomtegemea na kuvuta subira wakati wa shida.
NAWATAKIA IJUMAA NJEMA.


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Hello there! Do you know if they make any plugins to protect against hackers?
I'm kinda paranoid about losing everything I've
worked hard on. Any recommendations?
Have a look at my blog post :: jeremy scoot

Anonymous said...

Hi friends, good post and good arguments commented at this place, I am actually enjoying by these.
Here is my page - silver jeremy scott wings

Anonymous said...

Thanks for finally writing about > "Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-54" < Liked it!
Look at my homepage reviews of anti aging products

Anonymous said...

HONGERA SANA MKUU, NAKUAMINIA

Yasinta Ngonyani said...

Bonge la wazo..Tupo pamoaja ndugu wangu. Ama kweli wewe nakuamini kwa visa tu...

Anonymous said...

Great info. Lucky mme I discoѵered your site by chance (stumbleupon).
Ι have book marκed it for later!


mу website - Testo Xl