Bindamu tusingejaliwa
kusahau, natumai nisingelijiingiza kwenye ushawishi wa mama mdogo, kwa jinsi walivyonifanyia, ilifikia hatua
nilitaka kukimbia na kwenda kuishi sehemu nyingine, lakini nlijiuliza
nitakwenda kuishi wapi, na je huko nitakapokwenda nitapata usalama gani, na
hali niliyokuwa nayo. Ilifikia mahali nilishaapa kama mambo ndiyo hayo, basi ni
bora nirudi kijijini kwa mama yangu, lakini haikuwa rahisi hivyo….ikia hatia
niliipa kulipiza kisasi, lakini kwa vipi, ……
``Siku hiyo nilikuwa
nimechoka baada ya kazi za ndani, nilipata ujumbe kuwa tajiri amefika na
anataka kuonana na mimi, kwanza nllizarau, lakini baadaye ukaja ujumbe ukisema
kuwa tajiri anataka kunipa mikanda ya matendo yangu, ..’Maua akaendelea
kuhadithia kisa hiki.
****
`Mkanda wa matendo yangu…..!?’ Maua akajiuliza huku akijaribu
kuwaza, akaendelea kusoma ule ujumbe , sasa hivi akiwa na akili mbili, moja
ikiendelea kusoma ule ujumbe , na akili nyingine aikijaribu kukumbuka hayo
mtendo ni matendo gani.
‘Kila nikiangalia mkanda wako nashindwa kulala, sijawahi
kufanyiwa hivyo kabla,….ulikuwa kama mwigiza picha aliyejitokeza toka
kusikujulikana, na kuwa nyota wa picha….nimeshindwa kuvumilia, na naona
nikufanye kweli uwe nyota ya maisha yangu….’ Ule ujumbe ukakatika na kuendelea
kwenye sehemu nyingine.
‘Mkanda gani huo….’Maua akaendelea kujiuliza.
‘Najua wengi watasema na kukunyoshea kidole, wakitizama
matendo yangu , umri wangu, ….lakini yote hayana maana kama kwani maisha, raha,
…ni ukiwa na pesa, na mimi sijivuni, lakini pesa kwangu sio tatizo ,na mrembo
kama wewe unahitaji mahali kama kwangu, ili uwe nyota ang’avu, nyota
itakayongara katika moyo wangu, na kumulika maisha yangu mapya…..kwa ujumla
nimechoka, na nahitaji kupumzika….’ule ujumbe ukakatika tena na kuendelea
sehemu nyingine.
‘Na bado utachoka sana, kwa hili ulilonofanyia, nahakikisha
na wewe yatakupata makubwa,….’akasema kwa sauti na huku akiendelea kusoma huo
ujumbe
`Sasa nahitaji kutulia na kuwa mtu mwingine, na nimegundua
mtu pekee ninayeweza kutulia naye, na kuituliza nafsi yangu , sio mwingine ni
weye nyota, nuru, na ua la moyo wangu, na nakiri, aliyekupa jina hilo la Maua, hakukosea,…kweni
wewe ni Ua,..uwa waridi….’ule ujumbe ukakatika tena.
‘Na kwa jili hiyo,.. sasa naona bora nisiwe na huu mkanda
wako, na kuungalia kama picha, huku nikikuona kama nyota wa hiyo picha, nahitaji
uwe kweli ndani ya maisha yangu…na kama haitawezekana, basi sina budi kuuza huu
mkanda …ili nisifanye hivyo, nakuomba ufike ofisini , ili uje uharibu mwenyewe huu
mkanda, kabla haujachukuliwa na watu wengine….’ujumbe ukakatika.
‘Mkanda gani huu?’ akajiuliza na kabla hajawaza vyema,
ujumbe ukaingia tena, na alipofungua akakuta ni sehemu ndogo ya ujumbe ikimalizia
na sehemu hii ilikiwa na maneno machache, ikasema;
‘Kama umesahau, mkanda ninaoxungumiza ndio ule uliokufanya
utake kujiua…kwanini ulifikia uamuzi huo, wakati mimi nakupenda…usirudia tena
upuuzi huo, na kwa kukujali, nitahakikisha naharibu mikanda yote, lakini nataka
uje uiharibu mwenyewe…..’ukamalizika huu ujumbe.
‘Mikanda…?!...’akajikuta kihema kwa hasira, na kumbe ni ule
upuuzi wenu mlionifanyia…ngoja nifike hapo, sijali kuwa wewe ni
tajiri…..’akatoka nje na kwenda jikoni, kule akachukua kisu kidogo, akakinoa na
kukiweka kwenye mkoba wake….
**********
Mama mdogo alipofika, alitulia kwanza , na alionakana mwingi
wa mawazo, na kutokana na hli ngumu waliyokuwa wakikabiliana nayo, ilimfanya
huyo mama aonekane mzee kabla ya umri wake. Akakaa kwa muda kwenye sofa bila
kusema neno, na baadaye akasema….
‘Huyu jamaa yako kaja na anasema anataka kuonana na wewe
haraka iwezekanavyo…na nahisi kuna jambo la muhimu kaja nalo, ni bora tu
twende, kwani huyu jamaa akiamua jambo lake harudi nyuma, na ukumbuke ni mtu mwenye kujulikana na kuheshimika kwa
ajili ya utajiri wake…’akasema mama mdogo.
‘Kama utajiri ni wa kwake,….haunihusu kamwe…’kabla
hajamaliza akasikia tumbo likumuuma….akahisi hali ambayo imeanza kujijenga
mwilini. Hali ambayo hata mama yake mdogo alishaihisi na kumwambia wazi wazi….
‘Maua unaonekana una uja uzito, hebu niambie ukweli huo uja
uzito ni wanani?’ akauliza mama yake siku hiyo alipomgundua…
‘Mama mimi sina uja uzito,…’akasema Maua.
‘Mimi sio mtoto mdogo, dalili zote zinajionyesha, ….sasa
anona umelikoroga, sijui hata huo uanamitindo utaupata tena, …..umeharibu kila
kitu, …ni mwanaume gani kafanya mambo hayo, maana sitaweza kulea kiumbe cha
mtu, …’akasema mama.
‘Mimi sina mwanaume yoyote, na wala sijui…..nyie ndio mnajua
zaidi yangu’akasema akikumbuka jana yake, baada ya kuendelea kujiskia vibaya
aliamua kwenda kumuona dakitari,…lakini hata baada ya vipimo kumwambia hivyo,
bado alikuwa hajaamini….
***********
Maua alianza
kujisikia vibaya, akawa anahid kuchoka, na hali isiyo ya kawaida mwilini, na
akamwambia mama yake mdogo kuwa anajisikia vibaya…
‘Labda una malaria nenda ukapime, ….kwanza tangu uje hapa
Dar, sijawahi kukusikia ukiumwa, na ni bora ukapime sasa hivi usijea uakzidiwa
hapa nikahngaika usiku, …pesa ya kukodi taksi tutapata wapi.
Maua akajiandaa na
kuondoka kwenda kupima, na alipofika kwa docta, akajielezea na dakitari
akamwambia akapime mkojo na damu, …na baada ya vipimo akafika tena kwa huyo dakitari
waliyemwambia akapima mkojo na damu…
‘Vipimo vyako havionyeshi tatizo,..huna malaria, na huku
kwenye mkojo, mmh, inonyesha una uja uzito..’
Maua alihisi kitu kimegonga kichwani, na akili ikawa
haifanyi kazi kwa muda, akatulia na akili ilipokaa sawa, akawa kama anataka
kusimama, na kumkodolea macho docta.
‘Eti nini?’ akauliza kwa hasira.
‘Huna tatizo kubwa, hii ni hali ya kawaida, …vipimo vyetu
vinaonyesha una uja uzito…na ni vyema ukatu....’akaambiwa na dakitari, ambaye
alikuwa anamwangalia kwa makini, kwani alishahisi huyo mwanadada, hakuwa tayari
kupokea taarifa hiyo, na hata kabla hajamaliza kuelezea Maua akawa keshasimama
‘Uja uzito? ‘akauliza na kugeuka nyuma , kama vile anahisi
kuwa aliyekuwa akipewa taarifa hiyo sio yeye, kuna mtu mwingine nyuma yake, na
alipoona yupo yeye na dakitari, akishika kichwa, akasema kwa sauti isiyo ya kwake
‘Uja uzito huo kanipa nani?’ sasa akaguka kumwangali yule
dakitari kwa hasira, na dakitari
akaegemea kiti chake akimwangalia huyo binti kwa makini, …na alishangaa, kwani
sauti aliyotoa yule binti, ilikuwa ya besi, ya mwanaume
‘Sijui..?’ dakitari akasema huku akionyesha uso wa kushangaa
na mkono wake mwingine ukawa umebonyeza kitufe , ambacho hutoa ishara kwa wanausalama,
waje kutoa msaada.
`Unasema nini…haiwezekani, haiwezekani, kiti wangu …umefanya
nini…ni lazima uniambie hii mimba imetoka wapi….’sauti ya kiume nikatoka kwa
yule binti, na akawa anamsogelea dakitari. Dakitari, akawa anainuka pale kwenye
kiti,..lakini kabla hajainuka vyema akawa keshahikwa shati na koto lake la
kidakitari, ….
‘Tulia…..tulia..wewe…..’akawa anajisema huku akizidi
kubonyeza kitufe cha kutoa ishara, lakini hakuweza kufanya hivyo zaidi, kwani
aliinuliwa kama mtu anayeinua mtoto na kubwaga chini..aliona vinyota vikitanda
gizani, na kabla hajapotewa na fahamu mlango ukawa umefunguliwa.
‘Kuna tatizo gani dakitari…’wakauliza wale walinzi, na
walipoona dakitari yupo chini, wakamgeukia yule mgonjwa, ambaye aliwaangalia
kwa macho ya kutisha, na mlinzi mmoja akagundua hiyo hali, akatoa pingu, lakini
hakuweza kufanya hivyo, …..alishikwa na kubwagwa chini…mwenzake alipoona hivyo,
akapiga filimbi ya hatari.
Walifika walinzi wengine na madakitari, na chumba kikajaa
watu, ….na dakika chake wengi, walitoka wakikimbia, hadi dakitari mmoja
alipofanikiwa kumdunga sindano ya usingizi, huyo mgonjwa, na alipoishiwa nguvu,
alidondoka chini, ….
Maua alipozindukana alijikuta yupo chumba maalumu akiwa
kafungwa kamba, akashikwa na mshangao; akamuuliza mlinzi mmoja aliyekuwa
kasimama mbali na yeye. Yule mlinzi alionekana akiwa na wasiwasi, na hakutaka
kabisa kumsogelea.
‘Kwanini mumenifunga kamba?’ akauliza Maua.
‘Kwasababu umepandisha na unaleta fujo, wewe una mashetani,
eeh?’ akauliza bado akiwa na amshaka.
‘Nina mashetani…mbona sikuelewi, mashetani hayo yametoka
wapi?’ akauliza Maua, akiwa anashangaa.
‘Kama ulikuwa hujui, sas aujue kuwa una mashetani, na kama
usipoyashughulikia yatakuharibu huo usichana wako’akasema huyo mlinzi.
‘Mikono yangu inauma, nifungueni hii kamba…’akasema Maua, na
yule mlinzi alipoona kuwa huyo binti hana matatizo tena akamuita dakitari, na
baadaye akafunguliwa na kupelekwa mbele ya dakitari,….dakitari huyo alikuwa
mtaalamu wa mambo ya akili, akaanza kumhoji Maua kwa undani.
‘Hebu niambia binti una matatizo gani?’ akauliza
‘Mimi nilikuja kupima, maana hali yangu, imekuwa sio njema,
najiskia kuchoka, kizunguzungu, na kichfu chefu,…na natamini kulala tu muda
wote,…..na…’akawa anajielezea huku yule dakitari akiendelea kusoma kado yake
aliyoandikiwa na dakitari mwenzake ambaye alishaondoka kwenda kupimzika, baada
ya kutibiwa, ….kutokana na majeraha aliyoyapata.
Dakitari yule alimhoji kwa muda, na baadaye akaandika kwenye
kadi yake, na kumwambia afike sehemu ya dawa akachukue dawa, na baada ya wiki
arudi tena hapo hospitalini.
‘Kwani mimi nina matatizo gani?’ akauliza Maua
‘Tatizo lako linatokana na uja uzito…na mengine tutayajua
baadaye, tukiendelea na uchunguzi, ila ningekushauri ukija safari nyingine
ufike na mama yako, au mume wako…’akasema yule dakitari
‘Hapana dakitari, ……..kuna makosa yamefanyika, nahitaji
kupima tena….’akasema na kabla docta hajasema kitu, akondoka, na hakurudi tena
kupima, hadi leo alipopata taarifa hii kuwa anahitaji kuonana na huyo tajiri
***************
‘Eti sisi ndio tunajua, yaani wewe ufanye ufusuka wako, ubebeshwe
mimba, halafu uje kutusakizia sisi, mimi nitajuaje mwanaume aliyekubebesha hiyo
mimba….hebu niondolee upuuzi huo’akasema mama mdogo.
‘Nyie ndio mlionikamatisha na kufanya nibakwe siku
ile…..kama ni mimba basi ndio nyie mlionipa…’akasema Maua huku akianza kulia.
Na yule mama akainama chini, hakuweza kusema neno. Akainuka na kwenda kwenye
shughuli zake.
Maua akibakia akiwaza, akawa anawa maisha yake
yatakavyokuwa, na akikumbuka maisha ya mama yake, aliyowahi kumsimulia,
alijiona mwenye bahati mbaya;
‘Ina maana hali iliyompata mama ndio imenipata na
mimi..kwanini ….hapana haiwezekani, sikubali, kwanini…..’akawa analia huku
akishika kichwa , maumivu yakaanza kumjia, na hali isiyo ya kawaida ikaanza
kujijenga kichwani, akakumbuka dawa aliyopewa na mtaalmu mmoja, kuwa akijisikia
hali kama hiyo ainuse.
Alipoinusa na kupiga chafya akajihisi ana mang’amung’amu ya
usingizi na hapo taswira ya mwanamke asiyemfahamu ikawa umesimama mbele yake,
mwanamke yule akawa anaongea, lakini hakuweza kusikia sauti yake, ilikuwa kama
anawa ni nini huyo mwanamke anamwambia.
‘Mjukuu wangu, matatizo hayo uliyo nayo ni makubwa,
yanahitaji urudi kwenu,….ufike msitu , sehemu ulipozaliwa, huko,….utaweza
kumpata mtu atakaye kusaidia kuondoka hayo yaliyopo kichwani mwako, lakini hata
hivyo…mzigo uli nao hautakuwezesha kuingia huo msitu, kwani ni nuksi….kwanza
itabidi usubiri mpaka ujifungue…
‘Mpaka nijifungue, kwani mimi ni mja mzito?’ akauliza
‘Ndio,….ndio…..ndio…..lakini ni mkosi….oh, mkosi mkubwa’ile
sauti ikawa inasema hivyo hivyo.
`Mkosi gani , na nani kanipa huu uja uzito?’ akauliza.
‘Unamfahamu sana…na hayo ndio matokea mabaya yanayokikabili
kizazi kipya,….maisha yenu yamagubikwa na mitihani mingi, …ninawasikitikia
sana, …..’ile sauti ilikuwa kama inafifia.
‘Lakini mbona sina makosa….’akalalamika Maua.
‘Najua huna makosa, ….lakini ni lazima hayo yatokee, …..siku
ukirudi kwa mama yako utagundua yote, na poleni sana, kwa hayo yote, ..cha
muhimu usikate tamaa…..kwaheri’ ila taswira ikaondoka na Maua akaamuka na mbele
yake alikuwa kasimama mama yake mdogo.
‘Ina maana hujajiandaa?’ akauliza kwa hasira.
‘Kujiandaa kwenda wapi?’ akauliza Maua.
‘Hivi wewe una nini lakini,…hali uliyo nayo, siyo ya kukaa
kimiya, kama huyo jamaa keshafika ni lazima twende kwake, na ukifika ujielezee,
usifiche kitu, na najua atakupa ushirikiano, na akikataa tutamstishai
kumshiktakia, najua haogopi…’akasema mama mdogo.
‘Mimi sitaki matatizo na mtu,….tutafute nauli, nitarudi
nyumbani kwa mama yangu…’akasema Maua huku machozi yakimtanda usoni.
‘Kwa mama yako, kwani yeye ndiye aliyekupa huo uja uzito?’
akauliza mama mdogo.
‘Nasikitika sana, kwani ulinichukua ukimdanganya mama kuwa
unanileta huku, kunisomesha na kuniwezesha, na kumbe nia na lengo lako lilikuwa
hivi….nashukuru sana mama, na mungu atakulipa’akawa anasema huku akilia.
‘Acha utoto huo..maji yameshamwangika,..hapo hakuna jinsi,
lazima tupambane, …najua utanilaumu kwa hilo, na mama yako atanilaumu sana,
lakini lengo na nia yangu ilikuwa njema,…kupata mafanikio, unafikiri hili ni
tatizo, mbona mimi haya nilishayapaat sana, mbona bado naishi….’akasema huku
akionyesha kutojali.
‘Kwahiyo unawaambukiza wenzako…ili wafuate maisha yako, na
unawafanyia watoto wa wenzako kwa vile huna uchungu nao, ….kama ingelikuwa ni
mtoto wako ungelimfanyia hivi….mama, utanisamehe sana, lakini wewe ni ibilisi…sina
jina jingine linalofaa kukuita wewe’akasema Maua.
‘Mimi ni ibilisi, sio…yaani kukutoa kule kijijini kuja
kukutafutia maisha , leo hii nimekuwa ibilisi, nashukuru sana…hata hivyo,
jiandae twende, huko ni lazima twende, hata kwa kama ni kukubeba nitakubeba, ni
lazima tukamuone huyo jamaa…
Maua akasimama, na kabla hajainua mguu, akahisi mwili
kuishiwa nguvu,….kizungu zungu, kikatanda usoni, na hapo hapo wakasikia mlio wa
gari, na honi, na …Maua akapoteza fahamu.
********
NB: Sehemu hii nimeiandika kwa haraka asubuhi asubuhi,
huenda hajakaa vyema,
WAZO LA LEO:
Tunapofanya mabaya, tusiwashawishi wengine wafanye hayo mabaya , eti ili na wao
yawasibu hayo yaliyokukuta wewe. Ni vyema tukawa waalimu wazuri, na sio kuwa walimu wabaya, na kuwa wa Ibilisi, wa kushawishi
kufanya ubaya.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
If you have had situation going your own home, some of our companies may well take you approximately the whole set of family home for their B . C . drivers license. The service plan is very little internet site monetary cost. Satisfy twenty-four hours a day you can ask some of our staff in touch you and me article. http://www.vancouverhomesrealestate.com/
Post a Comment