‘Ofisi yako itakuwa hii hapa, …..’ Maua hakuamini siku hiyo
alipofika mjumbe toka kwa tajiri, mjumbe huyo alitumwa kuja kumuonyesha ofisi
mpya iliyofunguliwa kwa ajili yake. Mwanzoni aliogopa, na hakujuwa nini
akafanye, japokuwa kuandika na hesabu za kawaida hazimpi shida, lakini ile hali
ya kuambiwa kuwa sasa wewe ndiye bosi wa hii ofisi ilikuwa kama miujiza kwake,…
‘Usiwe na wasiwasi binti, wewe ukifika asubuhi, cha kwanza ,
unafungua simu yako,….hii hapa’akapewa simu, na kujikuta akizidi
kuchanganyikiwa kwa miujiza hiyo..
‘Ina maana hii ni simu yangu?’ akauliza.
‘Ya kwako kwa ajili ya kazi,…..’yule jamaa akamwambia, huku
akimkabidhi hiyo simu.
‘Cha kwanza na ni muhimu sana, ukifika, ofisni hapa, kwanza unaangalia
meseji ulizotumia, kuna watu wanahitaji mizigo yao, kuna watu wanahitaji
kulipwa, na ….mengine utayazoea kidogo kidogo……’akaelekezwa, na kujikuta akiwa
kakaaa kwenye meza ya thamani kubwa, na kiti, kama meneja wa
kampuni,…akatabasamu.
‘Nilikuambia mwanangu, bahati haiji mara mbili, hii ndio
bahati yako, inabidi unishukuru sana, na cha muhimu ni kufuatilia kila
ninalokuelekeza..ukivurunda, shauri lako….’akasema mama yake mdogo, walipokuwa
wakiongea.
‘Lakini mama, mbona kazi za ofisini sijawahi kusomea, huoni
kuwa ….’akalalamika.
‘Shule sio lazima uingie darasani,….shule nyingine
unajifunza kutokana na mazingira….sasa anza kusoma, na mimi nitakuwa mwalimu
wako….kwanza anza kujifunza, jinsi gani ya kuvaa, hizo nguo za kijijini achana
nazo,…na unahitajika, kujiremba….’akaanza kufundwa.
Kwakeli Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza, Maua hakutegemea
kuwa ataweza kukaa kwenye ofisi na kuitwa mfanyakazi, akijilinganisha na maisha
ya huko alipotoka na darasa lake la saba, …hakujua yote hayo yana sababu, hakujua
kuwa huenda huo ni mtego wa panya,…huenda ukaja kumnasa.
‘Mwanangu naona mambo yalivyojileta , nilikuwambia hapa
mjini, ….fuata ninavyokualekezea, sasa mungu akupe nini, iliyobakia ni akili
kichwani mwako, …’ mama yake akaendelea kumfunda.
‘Akili kichwani mwangu kwa vipi mama kuna nini zaidi ya hiyo
kazi, ….?’akauliza Maua.
‘Unamuona mtu mwenyewe alivyo, hajatulia, na anahhitaji mtu
wa kumtuliza, huwezi kushangaa makamo kama hayo hajaoa, anaruka huku na huku
kama jogoo, sasa huenda bahati ikaangukia kwako’ mama mdogo akamwambia Maua.
‘Kwa umri kama huo alio nao, ina maana hajaoa….?’ Akauliza
kwa mshangao akikumbuka siku ile alivyomuona akiongea na simu.
‘Mbona nimesikia akiongea na mke wake…na akawa anamwambia
kuwa anampenda sana..’akasema Maua.
‘Hana mke huyo,….eti anampenda sana…hahahaheee…’akacheka
yule mama kwa kicheko kikubwa.
‘Huyo, kila mwanamke anamwambia hivyo hivyo, hizo ni lugha
za wanaume za ulaghai, na akimkuta bwege, akiambiwa hivyo, anajiona kweli
keshapendwa, lakini akimkuta mjanja kama mimi, …’akasema huku akijiangalia, na
Maua akawa anamwangali mama yake huyo kwa mshangao.
‘Usionione hivi mwanangu, mimi hapa nilipo ni kama msomi wa
chuo kikuu…..lakini …..mmh, wewe usijali, nitakufundisha,…cha muhimu ni wewe kusikiliza
maelekezo yangu ninayokuambia….’akamshika mabegani huku akimwangalia moja kwa
moja usoni.
‘Maisha ni mazuri sana, ukiyajulia, na ni mgumu sana,
ukiyakatia tamaa…na usiona watu wanajenga, wana maisha mazuri, ukazania
walipata hivi hivi tu, kuna njia walifanya, wengine wanahangaika sana,…na
hawapati, na kuhangaika huko kupo kwa
namna nyingi, kuna wengine wanatumia njia za mikato, kuna wengine wanafikia
hata kujitolea mihanga, kuna wengine wajanja, wanatumia mbinu za kudanganyana…ili mradi ni akili kichwani
kwako…’akamshika shavuni, akipitisha mkono taratibu, kama mtu anayempaka mtoto
mafuta.
‘Wewe ni mrembo kweli kweli…..una umbo zuri, unavutia, na
ukitumia hizo hazina ulizopewa na muumba, unaweza ukasahahu kabisa kuwa
ulizaliwa kwenye shida, …sasa nataka nianze kukufundisha maisha ya dunia
yalivyo, …..nahisi wakati sasa umefika, ‘akatulia na kugeuka kuangalia nje.
‘Yule jamaa nimejuana naye siku nyingi, na ……sio mbaya,
maana hata mimi muda huo nilikuwa nikitafuta, na bahati mbaya, sina umbo la
mvuto kama la kwako, ingelikwua hivyo, nakuhakikishai sasa hivi ningelikwua
siishi kwenye nyumba hii ya kupanga..’ akawa anaangalia huku na kule kama
kuitizama ile nyumba.
‘Lakini hata hivyo, ….ipo siku , na najua tukiwa na wewe
mambo yatakuwa safi, maisha yatabadilika,…wewe ni jembe, lakini jembe bila
mlimaji sio mali kitu….lazima litumikishwe, na mimi nitahakikisha hatuitupi hii
bahati’akageuka na kumwangalia Maua. Alimwanglia kwa muda akawa anashusha macho
na kumwangalia kifuani, halafu akamwangalia usoni na kusema;
‘Hebu niambie umewahi kuwa na rafiki wa kiume?’ akauliza
huku akimsogelea na akawa anapitisha mkono kifuani , sio kwa karibu sana, alikuwa
kama anaupitisha ule mkono hewani, lakini karibu na kushika sehemu ya kifuani
ya Maua. Maua akawa anashangaa, akawa anajiuliza huyo mama ana nini kwanini
anamfanyia vituko vyote hivyo…, akatizama chini, hakujibu lile swali, …akatulia
‘Usiogope kuniambia, mimi ni mama yako, na nichukuliea kama
rafiki yako, na usinihukuliea kama mtu mzima, nichukulie kama mwenzako, wa umri
kama wako….niambie kila kitu, ili niweze kukusaidia..’akamshika begani na
kumwangalia usoni akasema;.
‘Unaonekana bado hujaguswa ehe….’akasema huku akiwa kama
anamtekenya sehemu ya nyonga, na Maua akasogea mbali, na yeye, na safari hii
akakunja uso, na kumwangali mama yake huyo kwa hasira, akasema.
‘Mama kwanini unaniuliza mambo kama hayo, na kwanini
unafanya kama….’akatulia na kugeuka pembani akakumbuka maneno ya mama yake, na
vitendo kama hivyo, ambavyo yeye alishaambiwa kuwa wanaume wana tabia kama hiyo
kuwafanyia wanawake, na hakutegemea mama yake huyo angemfanyia kama hivyo,
akasema;
‘Mama yangu hapendi,…..mambo kama haya, …na mimi sina rafiki
yoyote wa kiume…’akatulia kwa muda halafu akawa kama kakumbuka jambo akageuka
na kumwangali mama yake. Akashangaa kumuona akitabasamu, na akamuuliza swali
ambalo alitaka kumuuliza mapema;
‘Hivi kama mimi nigelikuwa mtoto wako wa kuzaa,
ungelinifanyia haya unayonifanyia au kwa vile mimi sio mtoto wako wa kunizaa..?’
akauliza.
Yule mama akatabasamu, na akawa kama anawaza, ….na uso
ukakunjamana, na taswira ya usoni ikabadilika, kiwingu cha huzuni kikatanda
usoni, …akainama chini na kusema;
‘Mtoto…..ningelijaliwa kupata mtoto ningelifurahi sana,
lakini nimechelewa…’akawa anaongea kwa huzuni.
‘Nasikitika kuwa,….na najuta, lkini majuto ni mjukuu huja
baada ya matendo… hakuna mtoto aliyebahatika kukaa tumboni mwangu, …kila
aliyejaribu kuingia tumboni mwangu nilimtoa, nikiogopa kuharibu usichana wangu,
na sasa sizani kama ninaweza kupata mtoto tena…’akasema kwa uchungu.
‘Kwanini ulikuwa unafanya hivyo, ulimtoa kwa vipi….ina maana
mama huwezi kupata mtoto tena?’ Maua akawa anauliza maswali mengi kwa wakati
mmoja.
‘Usiulize maswali mengi, ukkiuliza sana utashindwa hata
kuifanya hiyo kazi, mengine hayasimuliwi , yanakuja tu,….na umri unavyokwenda
ndio unaanza kujuta,…..mimi nasikitika kuwa sitapata mtoto tena,…na ….’akawa
anatoa machozi, na Maua akawa anamwangalia wa simanzi, hakujua afanye nini,
baadaye akamsogelea na kumshika kama vile anamkumbatia, akasema;
‘Pole mama sikujua kuwa una matatizo, lakini sielewi kwanini
usipate mtoto….’akasema Maua.
‘Nitapataje mtoto na mimi sina kizazi….’akasema huyo mama
kwa hasira na kuondoka , akimuacha Maua akiwa kaduwaa…
NB: Japo kwa shida pokea sehemu hiyo ndogo, uone uhondo wa
uchungu wa mwana, je kama huyo mama angelikuwa na mtoto, akajua uchungu wa uzazi
angelimfanyia hivyo Maua, ….tuwepo pamoja.
WAZO LA LEO: Usijaribu kuharibu majaliwa ya muumba, kwani
kuna ambao wamediriki kuua watoto, kuwatupa majalalani, kutoa mimba…na mwishowe
wakaharibu hata kizazi, …..baadaye wanajuta ,tukumbuke majuto ni mjukuu
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment