‘Kumbe huyu mtoto
anayeishi naye hapa sio wa kwake,….huenda amechukuliwa ili ikifikia muda wake,
afanyiwe kama alivyofanyiwa yeye…..akasema kimoyo moyo, `Namsikitia sana binti wa
watu , maana naona hali ya usichana inaanza kumuingia, mwili unaanza
kumpendeza…na dhamira na malengo ya mashetani hawa itatimia, na watamfanyia
kama walivyonifanyia mimi….’akasema Maua akiendelea kusimulia kisa hiki.
‘Utajiri wa huyu mtu
umefangamana na mambo ya kishirikina, na ndio maana anatafuta wasichana wabichi…uwe
makini…’akakumbuka maneno ya rafiki yake mmoja aliyefika ofisini kwake siku moja
kumtembelea….
*******
‘Na ole wako ukimwambia……huyo ni mtoto wangu, …’akasema mama
yake mdogo kwa hasira, pale Maua lipojaribu kumuuliza swali, alipokumbuka ile
kauli yake aliyosema kuwa yeye hazai kwa vile hana kizazi.
‘Mama huna kizazi, …ina maana huyu mtoto unayeishi naye hapa
sio wa kwako wa kumzaa, mbona, mnafanana….?’ Akauliza
Yule mama alimtizama kwa hasira, na akawa kama kakumbuka
jambo, akakumbuka kuwa kaongea hata yale aliyokuwa hataki kuyasema kwa watu, …..akamsogelea
Maua na kumshika kwa nguvu begani, na kumtolea macho yaliyojaa hasira, chuki….na
ndipo akasema;
‘Na ole wako ukimwambia……’akatulia na kama vile kakumbuka
kitu , kuwa hakutakiwa kufanya hivyo, akasema kwa sauti ya kujilazimisha, sauti
ya upole,…..
‘Huyo ni binti yangu…ehe..huoni tunavyofanana….’akageuka na
kutizama nje…kuficha yale macho yake ambayo yalishaanza kujaa ukungu, ukungu wa
machozi, majonzi, ….japokuwa kwa mbali, husuda, chuki, na roho mbaya, ilikuwa
imeshika kasi, na hakujali hayo anayotarajia kuyafanya…
*********
Maua akiwa kachoka na kazi za ndani, akaenda kwenye sofa na
kukaa, na hapo hapo usingizi wa mang’amu ng’amu ukamnyemelea na kabla hajazama
kwenye usingizi , ndipo akakumbuka maisha yake ya nyuma, …..na siku ikaanza
kuita…
‘Maua mbona hupokei hiyo simu, umesahau kuwa sasa hivi wewe
ni mfanyakazi wa Tajiri, na moja ya masharti ya kazi yako ni kuwa uwe tayari
kwa wakati wowote, iwe ni usiku au mchana, ukiitwa , unahitajika kuitika….ukumbuke
mwenzako kashika mpini, anaweza kukuzalilisha nay ale yaliyotokea siku ile…’mama
yake akamwambia pake simu ilipolia kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Maua aliposikia hivyo, akainuka haraka, na kupiga miayo,..na
akili yake ikawa imenasa hayo maneno, `yale yaliyotokea siku ile,….’akaisogelea
ile simu huku akilalamika;
‘Lakini mama mbona ni usiku sana….’akasema huku akiishika ile simu, na
akaona ikionyesha ni saa sita za usiku
‘Jamani saa sita za usiku, ….’akalalamika, na akawa
keshabonyeza kitufe cha kupokelea na sauti ikasikika kwenye simu; Sauti
iliyomfanya apoteze usingizi wote, na akili ikawa imevurugika, akawa kama
kachanganyikiwa, an jasho likaanza kumtoka, hasira, chuki, kichefuchefu
kikamzonga, akawa anatamani kuitupa ile simu, lakini hakuweza, ilikuwa imeganda
mkononi kama imewekewa gundi,….akasikia maneno yale yakipenya kwenye ubongo wake;
‘Wewe mwanamke kwanini hupokei simu yangu,….hujapewa maagizo
yangu, …..mwambie mama yako akulete ofisini haraka, ….’sauti ikasema, na hapo
hapo Maua akainuka pale kitandani
haraka, alihis kichefu chefu mwili wote ukafa ganzi, …akili ikashindwa
kufikiria, na hisia za kichefu chefu zikamjaa na akainuka haraka kukimbilia
bafuni.
‘Ni nani aliyekupigia?’ akauliza mama mdogo akimfuatilia kwa
nyuma.
‘Ni huyu mtu wako, eti anasema unipeleke ofisini usiku kama
huu,, …..mama jamani mbona hivi, habeu angalia muda, saa sita za usiku, huko
ofisini tunakwenda kufanya nini , mimi siendi kwanza najisiki vibaya’akasema.
‘Ina maana keshafika tena,….najua safari hii itakuwa kafika
na pesa nyingi….na hushukuru kuwa bado anakujali, ingelikuwa wengine,
asingelisumbuka kabisa, keshapata alichokita, anahitaji nini tena, …hata hivyo,
hali uliyo nayo ni vyema ukaiweka wazi kwake….haya jiandae twende…’akasema mama
yake, huku akionyesha kufurahia.
‘Mama…muda huu twende wapi, kuna kazi gani za
usiku…’akalalamika Maua.
‘Kazi za huyo jamaa hazina muda maalumu, wewe jiandae
twende, nilishakuambia kuwa wakati ndio huu, usipoutumia vyema, utabakia huna
kitu….na mzigo huo utaubeba peke yako, nilishakuambia tukautoe..ukabisha, haya
twende huko …..’akasema mama.
‘Hapana mama, mimi najisikia vibaya,….siwezi
tena,…..mlichonifanyia safari ile, sitakisahau tena….najuta kwanini nilikubali
kuingia kwenye mambo yenu,…..yaani hapana…’akasema Maua akikumbuka matukio
yaliyotokea miezi miwili iliyopita, matukio ambayo yalibadili maisha yake yote,
na akasimama akimwangalia mama yake, akiwa keshajiandaa,…na hapo kumbukumbu za
nyuma zikaanza kumtawala kwenye kichwa chake…
*********
‘Bwana mkubwa anakuja leo, unahitajika kujiandaa, na ujio
wake ni wa kipekee kabisa, kwani anakuja kwa ajili yako, na anakuja na wageni
wake mashahuri,…’akaambiwa na tarishi wa tajiri,
‘Anakuja saa ngapi, mbona hajaniandikia ujumbe wowote kwenye
simu…?’ akauliza.
‘Hiyo ndio kawaida yake,… ndio hivyo, haitakiwi kujulikana
anakuja saa ngapi,….nimeambiwa nikuambie wewe tu, kwa vile unahitajika kuwa
tayari kwa ajili yake’akasema huyo jamaa
‘Tayari kwa vipi,..?’ akauliza Maua kwa mashaka.
‘Kamuulize mama yako atakuelekeza..’akasema huyo tarishi
akitabasamu, na hakuongea zaidi akaondoka. Na baadaye Maua akafika nyumbani na
kumuelezea mama yake kuhusu huo ujumbe alioupata.
‘Safi kabisa….’akasema mama yake huku akionyesha
kutokushangaa, ilikuwa kama vile anafahamu mengi kuhusiana na huyo mtu…`mtu
wake’ kama alivyozoea kumtaja mbele ya mama yake huyo.
‘Safi kwa vipi mama…mama huyu mtu wako mna mipango gani na
mimi, mbona siwaelewi?’ akauliza Maua, na mama akawa hasemi kitu, akachukua
karatasi na kalamu, na akawa anaandika namba, zikionyesha ni tarakimu za pesa,
….na alipomaliza, akamwangalia Maua, na kusema;
‘Tukipata milioni tano,…..moja wewe, moja mama yako na
nyingine tunaweka akiba….’akasema huku akitikisa kichwa kuonyesha anakubalina
na mahesabu yake na kutulia akimkagua Maua kuanzia kichwani hadi miguuni.
‘Milioni tano kutoka wapi?’ akauliza Maua.
‘Hilo sio swali la msingi kwa sasa, cha muhimu…ni wewe
kujiandaa….sikiliza, unatakiwa uvae lile gauni nililokununulia,…na uje hapa
kwanza ni kurembe, urembeke….sasa tunaingia kazini, na ili upate malipo halali
ya kazi yako, ni lazima ufanye kazi…usifikiri kazi ni hiyo ya kukaa ofisini
tu…hiyo ilikuwa ni matayarisho tu, kazi sasa ndio hiyo inakuja….’na kabla
hajamaliza simu ya yule mama ikaita.
‘Haloh,..ooh umeshafika…basi tusubiri tunakuja….usiwe na
wasiwasi, kabisa….nakuhakikisha kuwa ni ngoma mbichi…mwenyewe utaona, sawa,
kama nakudanganya…usinipe chochote….sawa tunakuja….’akasema mama na kuanza
kumuharakisha Maua,…
‘Tayari bosi keshafika, na safari hii kafikia hoteli kubwa
ya kitalii…twende haraka, …’akasema na kumshika Maua mkono, wakaondoka huku
Maua akilalamika kuhusu kile kivazi alichoambiwa akivae, alijiona kama yupo
uchi.
‘Mama mimi siwezi kwenda mbele ya watu nikiwa nimevaa nguo
kama hii…’akalalamika
‘Kwani wewe ulitakaje, ..ulisema unataka kuwa mwanamitindo,
au sio, ukataka uwe muigizaji au sio, hebu niambie kazi hizo zote hazikuhusu
kuangaliwa na watu?’akamshika mkono kwa nguvu, hadi Maua akasikia maumivu.
‘Mama unaniumiza….’akalalamika.
‘Kama hutaki nikumize fauata ninayotaka …fuata masharti ya
mkataba wako wa ajira..unafikiri milioni zoet hizo utazipata hivi hivi
tu…’akaambiwa.
‘Mimi sijakuambia kuwa nataka milioni, kwanza mbona mimi
sijaongea lolote kuhusu malipo na huyo mtu wako’akasema.
‘Nimeshaongea naye, kakubali……’akasema
‘Kakubali kuhusu nini?’ akauliza Maua.
‘Sasa hayo maswali yako yananikera…wewe fuata
ninavyokuambia, mengine yatajileta yenyewe…’akaambiwa na wakawa wameshafika hpo
hotelini.
Walipofika tu wakakaribishwa kwenye meza iliyokuwa
imeandaliwa kinamna yake, …na maua yalikuwa yamepambwa, kila kona kuizunguka
meza hiyo ….
‘Hapa kuna harusi?’ akauliza Maua,akiangalia yale mapambo, …akawa
anaonyesha uso wa furaha kwani yeye ni mpenzi mkubwa wa mapambao hasa maua…
‘Hahaha…..unaanza kuvutika au sio…..uzuri una raha yake,
ningelifanyiwa mimi hivi, mbona ningefurahi, lakini ..mmh, kweli penya miti,
hakuna wajenzi’akasema mama na mara hali ikabadilika, kwani yule tajiri alikuwa
anakuja na watu waliokuwa pembeni, wengine wakasimama, kuonyesha heshima zao,
yule tajiri akawa anawapita bila kuwajali, na nyuma yake kulikuwa na wapambe
wake, waliojazia vifua, suti nyeusi, na miwani ya kuficha macho,ilikuwa haitoki
usoni.
‘Karibuni sana….’akasema huyo tajiri, na macho yake yakatua
kwa Maua, akatabsamu,…..
‘Mhh, mambo sio hayo,…akageuka kuwaangalia watu waliokuwepo
hapo, akasema;
‘Siipendi hii hali, ilitakiwa tubakie mimi na wewe tu,
lakini, hakuna jinsi…’akageuka na kumwangalia mama mdogo wa Maua akasema;
‘Nakushukuru mama ….mhhh, mama mkwe….;’ kaguza jicho
kumwangalia Maua na huku akimminyia jicho moja, kama anakonyeza, na Maua akawa
keshajua kuwa hiyo ndio tabia ya huyo mtu kumkonyeza konyeza, kitendo ambacho
hakuwa anakipenda.
‘Wewe njoo ukae hapa karibu na mimi….’akasema Tajiri, na
Maua kwa aibu akainuka pale alipokuwa kakaa na mama yake, na alifanya hivyo
baada ya kufinywa na mama yake kuashiriwa kuwa afanye hivyo . Hatua ya
vinywaji, ikaanza, …vinywaji baridi,..na Maua akanywa juisi…
‘Usiogope kula hii yote ni kwa ajili yako….’akaambiw ana
huyo tajiri.
Baadaya chakula …..baadaye kikaletwa kinywaji kikali…na meza
ikabadilika…Maua alishajiona kushiba, lakini …
‘Unatakiwa leo uonje kinywaji kikali….’akaambiwa, na Maua
akakataa kata kata….
‘Mimi sinywi pombe….’akasema na hakumbuki ilikuwaje, ila
anachokumbuka ni kuwa alitoka kidogo kwenda haja, na aliporudi, akachukua
kinywaji chake cha juisi, na lipokunywa, akahisi macho yakiwa mazito…..na hata
alipojitahidi kuyalazimisha kuona vyema hakuweza,…na ikawa kama anavutika
kufanya jambo, mwili ulikuwa sio wake tena…na akawa anasikia..sauti ikisema ..
‘Kunywa…..’na aakachukua gilasi na kunywa…hakuangalia nini
kilichokuwepo kwenye gilasi iliyopo mbele yake akawa anakunywa,..na kila
akiiweka mdomoni, haibandui mapaka gilasi ilipokuwa nyeupe, na akiiweka mezani,
anasikia sauti ile ikisema `kunywa,’ na anakunywa…akawanywa na kunywa, na
hakuweza kujijua tena,….
********
Alipozindukana alijikuta yupo kwenye kitanda kikubwa cha
kifahari…..akageuza kichwa, akahisi maumivu makali, …..
‘Kichwa…..’akalalamika huku akishika kichwa chake….
‘Mleteeni dawa,…..na kinywaji cha kawaida,…kitamfaa kuondoa
hiyo hali…’akasikia sauti, sauti iliyomfanya azindikane, na mwili ukawa unahisi
uwoga..akainuka haraka na kukaa kitandani, akajikuta yupo mtupu…akalivuta shuka
na kujifunika, huku akionyesha kuogopa….
‘Hahaha…sasa hivi unaona aibu..mbona jana ulikuwa unafanya
mambo ambayo sikuwahi kuhisi kuwa binti mdogo kama wewe unaweza kuyafanya…’akasema
yule mwanume akiwa kafunga taulo kiunoni, aliinuka pale alipokuwa kaka, na
kifuani alikuwa mtupu…minyama ya uene, ikawa inacheza cheza mwilini, akitembea
kusimama pale alipokaa Maua.
Maua, akawa amekaa na kujikunyata, mikono ikawa imeshikilia
miguu, na kichwa kikawa kimelalia kwenye magoto yake….na akainua kichwa na
kumwangalia yule mbaba, akasema kwa kushangaa,….
‘Eti nini….’akasema Maua huku akizidi kujikunyata na
kuhakikisha lile shuka la kitandani, limemfunika kila sehemu ya mwili wake,
kuacha kichwa tu….
‘Usihangaike, ….najua akilini mwako, utasema labda
nimekulazimsiha,…..sijakulazimisha kabisa…umeyafanya hayo kwa hiyari yako
mwenyewe, na ushahidi ninao,….’akasema yule mbaba, na kucheka kicheko cha
dharau.
Maua akashika shavu kwa huzuni….
‘Mimi silazimishi mtu,…hata siku moja, ….kama ubaisha ngoja
nikuonyeshe ushahidi, ili usione kuwa nimefanya haya kwa
kukulazimisha….’akasema yule mtu na kwenda mbele, kulikuwa na runinga
iliyowekwa kwenye meza,…na akatoa mkanda wa video kwenye mkoba wake, akauweka
mkanda kwenye kitufe cha kuchezea mkanda na ile runinga ikaanza kuonyesha,…
Maua alibakia mdomo wazi, hakuamini yale aliyoyaona,
hakuamini kuwa ni yeye aliyekuwa akifanya hivyo,….mambo ya aibu,…hakutaka
kuyaangalia, kwanza akainama na kuficha uso wake, na baadaye bila kujali kuwa
yupo uchi, akainuka na kwenda kuutoa ule mkanda, akahakikisha kuwa umeharibika
kabisa…akavunja vunja…..
‘Hahaha…unaona aibu, kwa hayo…mbona kitu kidogo sana hicho…..usihangaike,
sina nia mbaya na wewe…na usizanie kuwa ninaweza kwenda kukuonyesha hadharani,
hapana, ila nilitaka kukuonyesha kuwa sikukufanyia hayo kwa kukulazimisha….na
nataraji, ujira wako, utaupata kama kawaida, na mengine yatafuata,….kama upo
hiyari….kama unataka kuwa na mimi….sikulazimishi….mimi nimeshatimiza wajibu
wangu…na haya yote ni kwa ajili ya kuwatafutia nyie mali,….watoto wazuri kama
nyie mnahitaji raha…sasa raha ni gharama, na gharama inahitaji pesa…na pesa
haziji hivi hivi, …’akatulia
‘Laana itawashukia nyie wote….masikini mie, nitauweka wapi
uso wangu….sikujua haya yote kumbe ni ….jamani, tumewakosea nini nyie…ina maana
umasikini wetu ndio unatufanya tuzalilike hivi…nashukuru sana…’akasema na
haraka bila kujali kuwa yupo uchi, akageuka huku na kule kutafuta nguo ya
kuvaa, akakiona kile kigauni alichokuwa kakivaa usiku, akakivaa,…
Hakuamini kuwa alivaa nguo kama ile usiku ….kwake yeye
ilikuwa kama nguo ya mtoto, na akajaribu kukivuta chini kile kigauni kishuke
chini, kwani kilikuwa kinavutika, lakini hakikuweza kufika kwenye mgaoti,….hakuamini…ina
maana keshakuwa Malaya..
‘Mungu wangu….nimefanya nini….nimefanya nini…’akaanza kulia,
akageuak huku na kule, ..baadaye akatoka na kwenda bafuni, kule akachuchumaa na
kuanza kutapika, alihisi mwilini kaingiwa na uchafu, uchafu ambao, kama
ingelikuwa uwezo wake, angeliuatpika wote, na mara, akahisi maumivu makali,
tumboni na sehemu zake za siri….akakunja uso…..huku akiendelea kusema;
‘Nimefanya nini
masikini…nimefanya nini mie binti wa mama masikini….’
Akatoka mle ndani,…na alipofika kule chumbani hakumkukuta
yule tajiri..akaangali huku na kule, hakujua
anatafuta nini….akaona dawa, zimewekwa pale mezani…..zilikuwa dawa za kichwa
alizoletewa,..akaona hazifai….akatoka nje, na kwenda kwenye duka la dawa
akanunua dawa za malaria.
Alirudi chumbani kwake, akachukua maji, kwenye gilasi,
akazimimina zile dawa kwenye mkono, bila kusubiri, akazitupi zote
mdomoni….akachukua maji kwenye gilasi, akanywa, na japokuwa zilikuwa chungu,
lakini alizimeza kwa haraka, hadi zote zikaisha….baadaye tumbo likaanz akuuma,
‘Mama..nakufaa…’akaanza huku akishikilia tumbo na kujinyonga
nyonga, maumivi aliyosikia yalikuwa makali sana, hakutegemea kuwa itakuwa
hivyo, akili ikawa inajuta, …akaanza kuhisi kizunguzungu…mauimvi yakawa
yanazidi kila sekunde,i…hakuweza kuvumilia zaidi akapiga ukulele wa kuomba
msaada, ukelele uliojaa chumba kizima, ukulele huo ukasikika nje, …
Watu wlaipofika walimkuta sakafuni akiwa anatoa mapofu
mdomoni…
‘Amejiua…..’ikawa ndiyo sauti ya mwisho kusikia kabla
hajazama kwenye kiza kinene.
NB: Ndio hayo kwa leo….
WAZO LA LEO: Pole
sana kwa wale waliowahi kukutwa na machungu,….mengine yakulazimishiwa, tusikate
tamaa, yote tumkabidhi mungu, na tuwe na subira, ….mungu yupo pamoja na wale
wote wanaomtegemea na kuvuta subira wakati wa shida.
NAWATAKIA IJUMAA NJEMA.
Ni mimi:
emu-three
6 comments :
Hello there! Do you know if they make any plugins to protect against hackers?
I'm kinda paranoid about losing everything I've
worked hard on. Any recommendations?
Have a look at my blog post :: jeremy scoot
Hi friends, good post and good arguments commented at this place, I am actually enjoying by these.
Here is my page - silver jeremy scott wings
Thanks for finally writing about > "Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-54" < Liked it!
Look at my homepage reviews of anti aging products
HONGERA SANA MKUU, NAKUAMINIA
Bonge la wazo..Tupo pamoaja ndugu wangu. Ama kweli wewe nakuamini kwa visa tu...
Great info. Lucky mme I discoѵered your site by chance (stumbleupon).
Ι have book marκed it for later!
mу website - Testo Xl
Post a Comment