Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, September 25, 2012

Mbio za sakafuni huishia ukingoini -sehemu tatu-3

Mbio zangu za kisiasa naona ndio zimeishia hapa,  maana kama unavyoniona hapa nipo kitandani, sina hata uwezo wa kusimama jukwaani, niachopigania sasa ni afya yangu, lakini nitapigaia kwa mikono mitupu, …ndio hapo hapo nazidi kujiumiza, maana kila kitu nilishakiingiza kwenye mambo ya kisaisa, nikitarajia nitashinda, lakini nianavyo sasa hizi zimekuwa ni mbio za sakafuni ambazo mwisho wake umeishia hapa kitandani, sasa hapa nategemea miujiza ya mugu tu..’akasema rafiki yangu kwa uchungu, huku akiagalia mkono wagu ambao ulikuwa hauna nguvu.

‘Usikate tamaa rafiki yangu, kuumwa sio mwisho wa kuishi, utapona na unaweza ukaingia jukwaani tena, hayo yote ni majaribio ya kimaisha’nikampa moyo.

‘Hiyo ni kupeana moyo, kiuzoefu, uapokumbwa na maradhi kama haya, uwezo unapungua kwa kiasi kikubwa, na wengi hawadumu, nimewaona, na ni bora ujuachie, …mimi naona niwaachie hawo wezangu ambao wanajiona wana pesa, kwani kwao pesa sio tatizo’akasema na kukunja uso.

‘Lakini hebu niambie, kwanini ukajiingiza katika mambo mengine ambayo ulijua kabisa yatakuharibia kisiasa?’ nikamuuliza.

‘Unapokuwa na wenzako  na katika mjumuiko wa watu, mara nyingi akili yako inatekwa na yale yaliyopo, huwezi ukajitenga, na mara nyingi hufikirii upande mwingine wa shilingi,  kwani unajiuliza mbona wenzako wanafanya ,na baya zaidi ni pale yule ambaye ulitegemea ndiye muongozaji wako, ndiye anayekushwishi ufanye hivyo. Sikujua mazara yake yatakuja kuwa hivi. Kwa ujumla nilijiisahau kuwa humo humo kuna ambao hawakutakii mema, cha ajabu ni kuwa hawo watu  ni miongoni mwa wenzako’akasema.

‘Kwahiyo kwa ujumla unataka kusema kuwa umeshindwa, na umeshajitoa kama alivyokuamrisha huyo adui yako?’ nikamuuliza.

‘Sio kwasababu yake, unaweza uaksema hivyo, kwani hata hivyo, sina jinsi imebidi, kwani iabidi  nijitoe, maana wenzangu huko walipofikia ni kubaya, …kama wanafikia kutoa kafara za roho za watu kwa ajili ya mambo haya ya kupita tu, basi,bora mimi nijitoe tu’akasema na mimi nikamwangalia kwa makni nikijiuliza anasema hivyo kwa sababu ya afya yake au kuna jambo jingine.

‘Ndugu yangu nimepatwa na mitihani mingi sana katika uwanja huu wa siasa, na sikutegema kuwa leo ningekuwa hapa kitandani, lakini huenda yote yametokea ili niweze kujifunza ukweli, nanikweli nimejifunza, kuwa binadamu yupo tayari kuua ili tu ajinufaishe nafasi yake, marafiki , ndugu, wanafikia hatua hawajali tena urafiki wao au udugu wao, inasikitisha sana, ….’akasita kusema zaidi.

‘Hapo kuna Jambo unanificha, kwani kuna nini kilitokea?’ nikamuuliza.

‘Kuna mauaji yalitokea, na hadi sasa sijamgundua ni nani hasa aliyefanya hivyo, ila kwa juu, juu ninaweza kusema ni huyo adui yangu ambaye alifanya mpango huo ili iwe kashfa kwangu, labda ni yeye, lakii alivyonipigia simu anadai kuwa sio yeye, ila anataka kutumia nafsii hiyo kuniangamiza kama sitakubali matakwa yake, na wenzake’akasema.

‘Kwahiyo ina maana sio wewe uliyeua, na kwa ujumla hata polisi hawakuwahi kukushikilia wewe kama mshukiwa?’ akaulizwa.

‘Sijaua, na kushukiwa kupo, ila ndio hivyo mchezo ulichezwa na mwisho wa siku mambo yakazimwa kinamna,lakini kesi ya kushukiwa bado ipo, imetulizwa kinamna, na hapa  ninavyosema hivi huenda nikipona hapa naweza kufikishwa mahakamani, kama wenzangu wataamua kulifuatilia hili swala kama walivyodai’akasema.

‘Kwanini hukufanya uchunguzi binafsi ukagundua I nani yupo nyuma ya jambo hili, wewe mwenyewe?’akaulizwa.

`Niliamua kufanya hivyo, lakini mwisho wa siku nikajikuta nagundua mambo mengine ambayo hadi sasa siyaamini, na hata huyu adui yangu alinikanya kuwa kama nataka kujiletea matatizo zaidi niendelee na uchunguzi wangu,kwani anadai kuwanitagundua mabaya zaidi ya hayo, sikumuelewa kabisa.

‘Hayo si maneni ya vitisho tu, ungelifanya uchunguzi bila hata ya yeye kujua kwani haiwezekani?’nikamuuliza.

‘Ndivyo nilivyofanya, lakini utafanyaje uchunguzi wewe mwenyewe , kama unavyojua ili ujue ni nini kilitokea lazima kuwahoji watu, na hawo utakaowahoji wanayafikisha hayo maneno kwa jamaa, kwani yeye kwa ajili ya pesa zake anajulikana sana, kwahiyo imekuwa ni ngumu, na wenzangu walinishauri nisihangaike na huo uchunguzi, wao wanajua nini la kufanya.

‘Kwani ilikuwaje?’ nikaumuuliza, na yeye akainua kichwa na kuangalia huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna anayetusikiliza , na alipoona hakuna mtu, akasema;

Siku ile baada ya kutoka kwenye kikao, kama kawaida yetu, huwa tunakunywa kidogo, na huwezi kunywa peke yako, tukawa na akina dada wakutuliwaza, maana kazi zetu hizi zina mawazo sana, sasa inabidi unywe kidogo, na ukinywa, unatakiwa upate mtu wa kukuliwaza,ndivyo hata wenzangu walivyonishauri, mwazoi nilipinga sana hili swala, lakini ibilisi wa mtu ni mtu …’akasema na kutulia.
Sikutaka kumuuliza kuwa `hiyo ni lazima au ni tabia tu’ nikanyamaza ni mpe muda wa kujielezea.

‘Tabia hiyo sikuipenda, lakini ilinibidi nijiunge na kundi, maana nisingejitenga na wenzangu, nilishawishiwa, nikashawishika, nikaonja asali, na kweli muonja asali haonji mara moja nikawa nami nimelowea, nikawa kwenye mkumbo.’akasema.

`Basi ilikuwa kila baada ya kikao, ukishakunjwa, na …ni lazima utafute wa kukuliwaza,labda kiuashauri kwa wenzangu ambao watakutana na mambo haya kama wana wake, wajitahidi kwenda na wake zao ili kupunguza hii tabia, lakini wengi hawapendi hilo’akasema

‘Siku hiyo kama kawaida, nilimchukua  bibie mmoja, ambaye nilishajenga mazoea naye, na kweli alinivutia sana ,ukiwa naye, sio tu anakuliwaza, lakini anakupa siri zamaisha, anakupa mawazo ambayo ukisimama kwenye jukwaa ukiongea, watu wanakushangilia, …ana kipaji cha kuwasoma watu, na alikua akinipa siri za ndani ambazo nilikuwa sizijui, namshukuru sana, na kama angelikuwa hai angelinisadia sana.’akasema na kuangalia huku na kule.

‘Una maana gani kusema kama angelikuwa hai, ina maana yeye ndiye aliyeuliwa?’ nikamuuliza.

‘Hawa washenzi wasikie hivi hivi tu, hili najua ni njama zao, walishagundua kuwa huyo mtu wao anatoa siri badala ya kugundua kuwa huyo mwanadada hafanyi kile walichomuagizia’akasema.

‘Ina maana alikuwa mtu wao?’ nikamuuliza, na y eye akacheka, na kuangalia tena huku na kule,

‘Kama asingelikuwa mtu wao, sasa hivi ningelikuwa jela, ndio maana mambo hayo waliyanyamazisha ki-aina. Na yule mwanamke alishaamua kuwa mtu wagu, nasikitika sana, ……’akasema na kuonyesha kweli kuna jambo lililotokea ambalo lilimuuma sana.

‘Sasa kwanini hukuwafahamisha polisi wakafuatilia kiundani?’ ikamuuuliza.

‘Kwa hali kama hiyo usingeliweza kuwaambia polisi chochote, ningejichogea tu, a ukizingatia hali mazingira yenyewe ya siku hiyo’akasema.

‘Sasa hebu niambie, huyo mwanamke aliuliwa au yeye ndiye aliyehusika katika kufaya mauaji?’nikamuuliza.

‘Mimi nilikuwa naoga, baada ya kujaribu kuwasiliana na mke wangu nyumbani bila majibu, nikawa sina raha, hata usingizi ukawa haupatikani, basi, nikamuomba mwenzangu, huyo mwanadada iliyekuwa kuwa sijisikii vyema ngoja nijimwagie maji kidogo, wakati naoga nikasikia ndio nikasikia mlio wa bunduki, natoka kule bafuni kuangalia kitandani, …oh, basi tena.

‘Basi tena vipi?’ nikamuuliza.

‘We acha tu

NB: Mambo bado magumu, mengi yapo juu ya uwezo wangu, lakii itajitahidi nikimalize hiki kisa hata kwa ufupi tu.

WAZO LA LEO: Kuua ni zambi zambi kubwa sana, sasa hivi watu wanaona ni rahisi tu kuua, utu umetoweka, ubinadamu haupo tena. Jamani hebu tujiulize tuauwezo gani wa kuumba, a kuweka rohoo ya mtu, hadi tufikie kuitoahiyo roho ya mt,  asiye a hatia, je utakuja kusema nini mbele ya muumba…,?

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Kaka usivunjike moyo, kaza buti, mungu yupo na wenye kusubiri, na wakatenda mema. Hii ni kazi ya mkono wako, ina baraka,utafanikiwa tu.

Rachel siwa Isaac said...

Ndugu wa mimi, Kazi nzuri sana,MUNGU yu pamoja yote ni Mapito.kila kitu kitakwenda sawa.MUNGU anatosha.
Pamoja Daima.....