Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, June 12, 2012

Hujafa hujaumbika-50 hitimisho-8 Nilipofika Kenya nilipokelewa kwa huyo mwanama,maana nilishawasilina anye, na yeye alinipokea akijua namefika hapo kama mwanafunzi wake. Niligundua kuwa kwenye hiyo shule yake kuna wanafunzi toka nchi mbalimbali wapo hapo kupata shule ya ndoa na mahusiano.Kwa kweli huyo mama amejitahidi, na ameweza hilo. Nilihudhuria darasa lake moja, nilipofika tu,kabla sijapata muda wa kukaa naye, nikaamini kuwa kweli huyu mama ni jembe, …

Na hilo darasa dogo tu, nikaamini kuwa kweli ndoa tukiujulia vyema dunia nzima itakwua na upendo amani na faraja…Basi baada ya hilo darasa nikamwendea naye akanipokea kwa hamasa na kuanza kunidadisi;

‘Ulinipigia simu kuwa unakuja hapa kwangu, je umekuja kujiunga na chuo changu, au umekuja na mambo mengine?’ lilikuwa swali la huyu mwanamama. Tofauti na nilivyomfikiria akilini, huyu kweli ni mama na anasthili kuitwa `mama Docta’. Lakini mwili wake na umri wake haviendani, inaonekana ni mtu wa mazoezi,huwezi kabisa kufikiria kuwa ni mama ambaye anataraji wajukuu. Na nilijiuliza kilini kwanini watu wanaigiza jina lake na kujiita `mama docta’.

‘Nimekuja kwa yote, haja yangu ni kupajua kwanza na hatimaye kujisajili, nitakuja wakati mwingine, ila nilikuwa na maongezi mengine na wewe…’nikasema.

‘Haya karibu, lakini nataka kujua maongezi ya namna gani, ya kuhusu haya ninayofundisha au ni maongezi binafsi,maana huwa sitaki kushitukiziwa.Katika kitu nisichokipenda ni maswali ya kushitukiziwa yasiyo na maandalizi,  sisi ni akina mama kila jambo tunahitaji kujiandaa kwanza, ….ndiyo asili yetu, au unasemaje?’ akasema nakuniuliza.

‘Nikweli,…..na ndivyo ilivyo, maandalizi kwanza, …tafiti kwanza, kabla hujafanya au kuongea hilo ulilokusudia…na mimi naamini hilo’nikamwambia na yeye akaniangalia machoni kwa muda halafu akatabasamu.

‘Wewe unanikumbusha mwanafunzi wangu mmoja toka huko Tanzania, alikuwa na akili kama zako, yeye nilitaka abakie nami hapa awe ni mmoja wa walimu wangu, lakini akaondoka kwasaabbu ya wazazi wake, ….’akasema.

‘Ina maana wazazi wake ndio waliomzuia asisome,?’ nikauliza.

‘Wazazi wake walikuwa wakihamia huko kwao, walihamisha biashara yao kwenda Dar ,na kila kitu, basi na huyo mwanafunzi wangu akasema na y eye anaondoka, nilimpenda sana maana alikuwa na kili, na mfuatiliaji mzuri wa mafunzo yangu, na pia alisomea udakitari, …kwa kumpenda walishaanza kumuita `mama docta mtarajiwa….’akasema.

Moyoni nilianza kuingiwa na shauku, `mama Docta mtarajiwa’ ni nani huyo, lakini sikutaka kuonyesha yale niliyokuwa nayo moyoni mapema, nikakaribishwa ofisini kwake, na hapo nilikuta watu wengi wakimsubiri,lakini akanipa kipa umbele.

‘Haya tuongee, maana kama unavyoona hapo nje watu wengi wanahitaji kuniona, hii inaonyesha jinsi gani ndoa zetu zilivyokuwa na matatizo, na wengi walipogundua hilo, wakaondoa aibu, na huja hapa kutaka ushauri, na mafunzo jinsi gani waboreshe ndoa zao…na wengi wanaokuja hapa ni wanawake…kama unavyoona hapo nje….’akasema.

‘Kwanini wanaume hawapendi kuja na ilihali ndoa ni mke na mume..?’ nikamuuliza.

‘Labda kwasababu wengi wanaichukulia hii kama `kitchen party’ kuwa ni maswala ya kina mama, lakini ingelikuwa vyema hata wanaume wangelikuja, na ingesaidia sana,hata hivyo nina mpango wa kuanzisha kitengo hicho, kwanza nimeaanza kuwaandaa walimu wanume….najua watavutia wenzao….’akasema.
Yule docta mama, akaniangalia kwa muda tena machoni,halafu akatabasamu, na kabla sijamuulizia yangu niliyotaka kmuuliza akanitupia swali,;

‘Wewe umeolewa?’

‘Nili……lakini sasa nipo peke yangu…’nikasema kwa mkato, akatabasamu na kusema;

‘Nimehisi hivyo, macho yako yanaonyesha huzuni iliyojificha, ila yana ujasiri wa kukambiliana na matatizo,…kuna dalili kuwa unasononeka, lakini hujakata tamaa,…wewe ni jasiri,…nahisi kuna jambo lilikukwaza….macho yana siri kubwa, …mimi nimekuwa nikiligundua hilo kwa wateja wangu wengi, na ukidadisi sana, utakuta wengi wamejikuta wakisononeka kwasababu ya mapenzi,kwasaababu ya ndoa….zao’akasema.

‘Kwahiyo unahisi kuwa nina matatizo hayo?’ nikamuuliza,

‘Sio nahisi , ni kweli nikuonavyo, una shida au uliwahi kupata shida ambayo imekuwa ikikutaabisha, hasa ya kimapenzi, hebu niambie ilikuwaje kwa mume wako  au mchumba wako…?’ akaanza kuniuliza, na hapo nikagundua kuwa huyu mama hana tofauti na mimi,….kuhusu udadisi wa mamb ya ndani ya nfasi ya mtu,na nikikaa naye tutaivana naye sana, lakini sikuwa na muda huo.

‘Hilo tuliweke kama agenda nikirudi tena..au unasemaje, …’nikasema huku nikiangalia nje watu wakizidi kuongezeka….

‘Mimi nimekuja na mengine, ni mbali kidogo na hayo, labda kwa kujitambulisha tu ,mimi ni wakili, nipo serikalini, lakini nataka kujitoa na kuwa wakili wa kujitegemea, na lengo langu ni kubobea kama wakili wa kusaidia kesi za akina mama,na ili nifanikiwe hilo, nahitaji kujua mengi kuhusu ndoa, akina mama na maingiliano yao akina baba, najua kwako nitafaidika sana, ila hilo tutaliongelea wakati mwingine,…’nikasema lakini kabal sijaongea mengine akaanza kuongea …..

‘Safi kabisa, hilo tutasaidiana na kabla hujaanzisha hiyo ofisi yako kuja kwangu kwanza, nitakufunda, na utawajua akina mama, na jinsi gani wanapata shida na waume zao,….nikuambie ukweli, akina mama wengi, ni wavivu kujifunza,na kama wangelijua hilo, waume  wao wangelikuwa hapa….’akaonyesha kiganja cha mkono.

‘Hebu niambie kuhusu familia yako,…..?’ nikamtupia swali kwa haraka kabla hajaanza kuongea mengine.

‘Kuhusu familia yangu,…..?’ akauliza na bila kutia shaka,akaendelea kuongea kwa haraka, inaonyesha jinsi gani alivyojipanga katika kila swali, na alionyesha alikuwa akiongea haraka ili kwenda na muda akasema;

‘Mimi familia yangu tulijipanga vyema,na hili nilianzia kwa mume wangu, tulipokuwa Ulaya,ambapo ndipo nilikutana na mume wangu, tukajikuta tumependana, kwa mara ya kwanza nilikutana na huyo mume wangu kwenya maktaba ya hpo chuoni, katika kutafutatafuta vitabu, nikajikuta nikimuulizia baadhi ya vitabu..

‘Unapenda sana kusoma mambo ya ndoa, unatarajia kuolewa karibuni nini…?’akaniuliza.

‘Hapana, katika muda wangu wa ziada huwa najaribu kujifunza haya mambo, najua itakuwa sehemu muhimu katik kazi yangu hiii ya udakitari….’nikamwambia,

Basi kila tukikutana naye humo ananitania kwakuniita `mama wa ndoa…’ kwahiyo jina hili la `mama’ lilianzia hpo kwa mume wangu,na kwa vile alikuwa akiniita kila mara  kwa jina hilo `mama wa ndoa,’ hata wenzangu wakawa wananiita hivyo hivyo,…`mama wa ndoa’  hata kabla sijaolewa au kuwa mama kiukweli….na baadaye nilipopata kazi ikabadilika na kuitwa `mama Docta…’

‘Nikawa karibu sana na huyu mwenzangu, hata kabla hatujawa marafiki, tukawa tukikutana tunajadili mambo ya ndoa,maisha ya huku kwetu, na baadaye nikagundua kuwa tunatokea sehemu moja, lakini yeye wazazi wake walihamia Kenya kwa muda mrefu,kabla ya wazazi wangu,…..

Moja likazaa jingine,tukawa marafiki, na urafiki ukageuka kuwa mchumba, na tukiwa huko huko, akaniomba anivalishe pete ya uchumba, na hapo nikastaajabu, yeye hajanijua vyema hata mimi sijamjua vyema, nikimaanisha wazazi na familia zetu, kiundani, keshaamua kunitaka uchumba. Nikaweka pingamizi kuwa mpaka tukirudi nyumbani na kuwafahamisha wazazi wetu ndipo nitakuwa tayari kwa hilo,akanielewa…na kukubaliana nalo.

Kwahiyo huko tukaishi kama marafiki tu,hadi tuliporejea nyumbani, na kuwafahamisha wazazi wetu, ambao walitafutana na walipoelewana na kuchunguzana wakagundua kuwa hatukufanya makosa, na haikuchukua muda tukaoana. Na baadaye tukarudi Ulaya tena kwa masomo yetu, maana kila mmoja alipanga kurudi tena, kwa hatua ya juu.

‘Uaya ikawa kama nyumbani kwetu, maana hata baada ya kumaliza masomo tulipata ajira huko, ila tulihakikisha kuwa familia yetu inajua kwao, tulipozaa watoto, tukawarudiha huku, wakawa wanaishi na bibi zao,ndio maana unaoan wanajua Kiswahili vyema kabisa,hatukutaka kufanya makosa. Labada katika kuishi kwao na bibi zao, hawakupata yale yote tuliyokusidia mimi na mwenzangu, maana tulijipanga vyema jinsi ya kuwalea watoto wetu….kila hatua tulisoma kujua ni nini tufanye….

‘Tukiachia huko, nilikuambia kuwa mimi na mume wangu tulikuwa tukisoma kuhusu ndoa ktikamuda wa zida, 
licha ya kuwa tuliijua yale muhimu, lakini tulifanya tafiti zetu, kwa kusoma vitabu mbalimbali. Hili tulijifunza toka kwa wenzetu wa huko ambao kila jambo kabla ya kulifanya au kuliingilia wanalifanyia utafiti kwanza. Na sisi tukawa tumeiga hiyo tabia, tukajiuliza ndio tumeoana, lakini kwanini tumeoana, kuan nini kunatakiwa kuwe na ndoa, na ni ipi misingi yake mikubwa….nini mahusiano, yanaathiri nini ndoa, na nini kifanyike katika mahusiano….

‘Hili linanishangaza sana,kila siku kuna ndoa, kila siku kupendana, lakini watu hawaangaiki kwanza kutafiti kile  wanachotaka kukifanya, hebu nikuulize hivi kweli unaweza kujua kuendesha gari kabla hujajifunza uderva, hivi kweli unaweza kuwa wakili kabla hujajifunza uwakili….?’ Akaniluza na kabla sijamjibu akasema.

‘Haiwezekani watu wakimbilie kuoana kabla hawajjua nini kwanini wanaoana,na humo ndani ya nda kuna nini, nini mahusiano, yanatakiwa yafanyike vipi… …hili linanipa shida sana,eti wengi wandai halin ahja ya kujifunza kwasababu ni jambo la asili, hiyo ipo kwenye damu, …

Kwa vipi iwe kwenye damu, mungu hajasema tufanya mambo bila  ya kusoma, bila ya kutafiti, katuambia kwanza tusome, ili kujiua dunia, angalia baba yetu Adamu, kwanza alianza kusoma, kwa kuju vitu vyote, majina ya vitu…hata malaika walipoulizwa kuhusu hilo walishindwa baba yetu Adamu akatambua, …..huu ni mfano wa asili kuwa kila jambo kwanza lazima ulisomee….’akatulia.

‘Ndoa nyingi zinaharibika, maisha yanakuwa ya shida,amani hakuna, lakini watu hawajajua kuwa chanzo chake kimeanzia wapi, ni siri kubwa sana …tuliligundua hili mimi na mume wangu, ….watu hawaamini,lakini ndivyo ilivyo, yote hayo yameanzia kwenye ujinga wa kutozijua ndoa,….unaweza usiamini hili, kuwa dunia hii, watu wanauana,watu wanashida, kwasababu ya ujinga wa kutoijua ndoa?’ akaniuliza.

‘Ni ujinga wa kutoijua ndoa,….maana ndoa ndio muhimili wa maisha,ndoa ikiboreka,na kuimarika ni sawa na mti,ni sawa na shina, likiwa imara, mti utakuwa imara, na utazaa matunda bora, ambayo ni manufaa ya baadaye. Halikadhalika, ndoa ikiwa bora, mume mwema na mke mwema, wakawa wanapendana kiukweli, wakajaliana, watakuwa na afya njema,watakuwa na furaha, na mwisho wake watapata Baraka, watazaa watoto ambao watakulia katika malenzi bora…..’akaangalia saa yake,.

‘Unaona hapo, wazazi wamekuwa chanzo cha kutoa kizazi bora, cheye malezi bora, elimu ,afya na malazi na huduma bora upendo na amani, ….imejijenga kwenye familia, nini unatarajia kutoka katikahiyo familia,….’akatulia na kuniangalia.

‘Familia hiyo itazaa matunda mema,…watoto wema, ambao wanakuja kuendeleza kizazi chema, kizazi na kinakuwa katika mtindo huo,na kutokea jamii njema,yenye maadili mema, na ukilikuza hilo linatokea nini taifa jema, je unatarajia nini hapo, kama sio amani, upendo,…sasa niambie vita, njaa, magonjwa, yatatokea wapi,…..hebu niambie, uadui na visasi vya kusalitiana vitatokea wapi,…?’ akaniangalia kwa makini.

‘Sasa hebu chukua kinyume chake utaona matokea yake,….sasa hivi watoto wa mitaani wamejaa kibao, watoto wanazaliwa na kulelewa na mzazi mmoja, watajuaje upendo unatokana na baba na mama,watajuaje, jinsi baba na mama wanatakiwa waishi….visasi chuki, kukata tamaaa, kunatawala dunia, njaa, magonjwa yanagubika dunia,ubinfsi choyo,….nakila aina ya ubaya unatokea, sababu kubwa ni ujinga…ujinga wa kutokufahamu nini maana ya ndoa….

‘Hili sisi tuliliona mimi na mume wangu tukasema hapana, sisi sio watu wa dini..ndio, lakini tunaweza kufanya haya, kama sehemu ya dini, maana kwanza lazima umjenge mtu kiroho, kiupendo,….ili ajijue kuwa yeye ni nani, yeye ni binadamu , na kapewa mamlaka ya kuitawala dunia lakini atawezeje kuitawala dunia kama yeye mwenyewe hajijui, …nakujijua ni pamoja na kujijua ndoa yake, ….wewe hujui ndoa ndoayako utawezaje kuzitawala ndoa za wenzako,….maana uongozi huanzia ndani kwako, huanzia kwako mwenyewe,halafu kwa familia yako, na baadaye kwa jamii….naliona hili mpendwa.

‘Kwakweli tulimuomba mungu sana, ili watu watuelewe, maana tulipoanzisha watu walitafsiri vibaya, labda tunataka kuweka mambo ya siri hadharani,eti tunawafundisha watu mambo ya kihuni,…sio lengo letu hilo, nia na madhumuni yetu ni kujenga jamii, iwe katika mapenzi ya dhati, mke na mume wajijue, kwani wao wakijijua, na kujua yale yaliyopo mbele yao, majukumu yao, ….watapata familia bora kwa vizazi bora….’akasema huku akiangalia saa yake.

‘Naona tuishie hapo kwa upande wangu, una swali jingine kuhusu mimi…..?’ akaniuliza huku akianglia saayake tena na kuangali nje akiogopa watu wanavyozidi kuongezeka..

‘Maswali yapo mengi,ila nilitaka kujua kuhusu watoto wako,…..uliwaleaje,ndio umeniambia ulezi wako kwanza ulianzia kwa bibi yao, lakini je ulipokuwa nao uliwaleaje, na pili nataka kujua kuhusu huyu mwanafunzi wako uliyesema ulimpeda sana, kwanini ulimpenda na je uligundua nini kuhusu yeye…?’ nikamuuliza.

‘Wewe ni wakili, au sio…kuna tatizo limetokea  huko ulipotoka, kuhusu mtoto wangu, au kuhuu huyo mwanafunzi wangu….?’akaniuliza kwa mashaka, na kablasijamjibu akasema;

‘Mimi napenda mtu anayeongea ukweli…., naomba uniambie ukweli…kwasababu ukweli ni siri kubwa katika maisha ,hasa ya ndoa, ukiwa sio mkweli kwa mwezako una walakini, upendo wenu una walakini…..nikaumbie kitu,mimi namume wangu hatufichani kitu,….ananijua kama ninavyomjua mimi…nashangaa eti watu wanaishi ndani ya ndoa, lakini kila mtu ana lake, hata simu haziruhusiwi kuchangiana, unaona tati hapo.., tatizo la kutoisoma ndoa.

‘Nina mengi ya kukuelemisha wewe wakili ,lakimi naenda na muda, wewe kama unataka haya, jiandikishe uwe mwanafunzi wangu, utapata mengi, ama kuhsusu watoto wangu, nitakuambia tu kwa ufupi,jinsi nilivyowalea, na kama nilivyokuambia, ulezi wao mwanzo ulianzia kwangu, maana niliwanyoyesha hadi pale walipofikisha miaka miwili, watoto wangu walikuwa mapacha,….’akasema.

‘Ina maana una watoto mapacha?’ nikauliza,

‘Mimi nilikuwa najua wajua hilo, ooh,hebu ngoja kidogo…’akatoka nje na baadaye akarudi, alikaa kidogo, na mara mlango ukafunguliwa, akaingia binti, akiwa kavalia kidakitari.
Oooh, moyo ukanishituka, maana aliyesimama mbele yangu ni mke wa wakili wetu mkuu, nikabakia nikipepesamacho, sikuficha nikauliza.

‘Wewe umakuja lini huku?’ nikauliza. Wote wakaangua kicheko, na Yule binti akasema kiutani,

‘Nimekuja jana na ndege….’akasema huku akicheka.

‘Mara nyingi watu wanawachangaya watoto hawa na hata wanashindwa kuwatofautisha….huyu sio huyo unayemzungumzia, huyo unayemzungumzia ulimuacha  Dar, ni pacha mwenza wa huyu,wanafanana sana, na tabia zao zinatofautiana kidogo,maana mwenzake huyo wa huko Dar,ana hasira kidogo,….maana asili hazipotei,sisi tunatokea huko Tanzania, mikoa ya ziwa , siunafahamu zile zetu…..’akasema na kucheka.

‘Lakini kwa ujumla mimi niliwalea na kuhakikisha kuwa wanakulia katikamaisha mema,kuna udhaifu wa hapa na pale, kwasababu wakati anaolewa na huyo mume wake,niliwaomba kwanza waje waishi kwangu, niwafunde vyema, lakini mume alipinga,..yule mume ana ule `uume’ ubinafsi…’ akasema huku akionyesha ngumi hewani.

‘Hili nililiona mapema,na tulimkanya sana binti yetu, tukamwambia ndoa njema hujenga na mume au mke mwema,huyo mume wako anaonekana kabisa, sio mume mwema, tulimwambia hilo bila kumficha, lakini yeye akaona kuwa kafika….ndio tatio la kiazazi chetu,…unafundisha kwako, lakini atakutana na jamii nyingine, ambayo ….ooh. Hili ndilo kosa, inatakwia wote wasome waijue ndoa,….Kama Yule mume angelikubali na kukaa na mimi kwa wiki moja tu, angelibadilika,lakini ……mmmh

‘Mimi nilijua kwa vile binti yako katokea hapa kwako chuoni, penye malezi bora, angeliweza kumbadili mume wake?’ nikauliza.

‘Ingeliwezekana, kama mume angalikubali,nina uhakika huo….,maana binti yangu,licha ya kutokupenda sana haya madarasa ya ndoa, lakini nilimfundavyema, lakini hilo halitawezekana kama mume hataki, ….yule mume anaonekana kalelewa ile ya kizamani, mume ni mume tu, amri mkononi…sasa hili halijengi, ndio maana nikasema huo ni ujinga wa kutosoma nini maana ya ndoa,

Unajua nikuambia kuna kusoma mambo ya kawaida, kama sheria, udakitari,.., na kuna kuisoma ndoa,….kila Nyanja  ina maudhui yake, Yule mume kasoma sheria, hajaisomea ndoa nakujiua ndoa ni nini, na hataki kuisoma ndoa akiwa  na mawazo yale ya kurithi tu,…. angelikubali akaisoma ndoa,akatulia na mke wake,mbona ingekuwa raha….

‘Je uliwahi kuongea na huyo mume wabinti yako..?’ nikamuuliza.

‘Mwanzoni alikuja na gia ya heshima,na siku moja nikamuuliza kuwa yey anataka kumuoa binti yangu, je amejiandaje, je anajua majukumu ya ndoa, akanijibu kuwa anajua vyema sana, na amejiandaa sana,…kwasaabu yeye ni wakili, nikajau anasema ukweli, lakini nilipotafiti nikagundua kuwa ni wale wanaosema wanajua…kwasababu wanajua kupandambegu, lakini sio kwa utaalamu,.. eti kwasababu ni mume, eti kwasababu ni mke,yote yanajilta tu….tunajidanganya,…baadaye niliaribu kumuita, akawa kila mara anasema hana nafasi…

‘Sasa uliwezaje kuisadiai ndoa yao..maana nyie ni wazazi kama kuna tatizo lazima mlitatue?’ nikaamuliza.

‘Kuisaidia ndoa yao ingelikuwa rahisi kama mume angelikubali kumsikiliza mke wake, huenda ….mke kajaribu kashindwa, hilo nimejaribu kumuuliza binti yangu,…yeye anasema kajitahidi yale yote anayyajau lakini kashindwa, na inavyoonekana kuna mengi zaidi ya ndoa yao ambayo mimi siyajui, kwani binti yangu hajataka kuniambia ukweli wa ndani, lakini sijakata tamaa, najua jinsi gani ya kuwaingia, nitawaendea huko huko…’akasema.

‘Binti yako hajawahi kukulalamikia..?’ akauliza.

‘Analalamika, lakini mwenyewe kasema hajashindwa, atapambana na mume wake hadi kieleweke,na mimi nawapa muda, …sijataka kuliingilia kiundani sana, namjua vyema binti yangu ni jasiri, pamoja na mengine nimewafundisha watoto wangu ujasiri, wasilegee, wanajua kupambana na maisha,kwa shida na raha, na kwasabaabu kaamua kuliingia pori, basi ajue kuwa kwenye pori kuna miiba…’akasema.

‘Ujasiri huo umewafundishaje…kupigana, au kufanay nini?’ nikaamuuliza huyo mwanamama.

‘Mazoezi ni muhimu sana, wewe kama mzazi kila asubihi waamushe watoto wako, na kabla hawajajichanganya, wape mazoezi,mimi nilianza kuwapa watoto wangu mazoezi wakiwa bado wadogo, kwahiyo wakakulia katika hali hiyo tango utotoni,….mazoezi ya kujihami, karate, na kujikinga , kwa mfano ukikutana na mtu mwenye kisu, utajihami vipi, yote hayo nimewafundisha, wanajua…’akatulia na kuniangalia.

‘Hata kutumia bunduki wanajua…?’nikajikuta namuuliza hilo swali

‘Ndio,….hilo niliwafudisha pia, unajua baba yao anapenda sana maswala ya kulenga shabaha…kuwinda, basi huwa akienda mazoezini anawachukua mabinti zake,..hutaamini, wote ni walengaji wazuri wa shabaha,…na hata baadhi ya wanafunzi wangu wanapenda shabaha piam huwa tunawachukua kwenye mazoeizi ya shabaha, na nikuambie siri moja kubwa kwa kina mama, wakina mama ni walengaji wazuri wa shabaha….’akasema huku akishika kifuani sehemu ya matiti yake.
Niliposikia hivyo moyo ukaanza kwenda mbio, sikutaka kuonyesha hiyo hali, nikauliza swali jingine kwa haraka, Ili kuficha hiyo hali;

‘Lakini hilo linasaidia nini katika maswala ya ndoa?’ nikauliza.

‘Ndoa  ina mambo mengi, kuoana sio sababu ya kuficha vipaji, hilo la shabaha ni moja ya vipaji, ni mazoezi, huwezi jua, wanaweza kujikuta wapo kwenye mashindano yakulenga shabaha ya dunia, tusifiche vipaji eti kwasababu tupo kwenye ndoa.

‘Na wengi wa wanafunzi wangu walipenda hilo zoezi la shabha, na hata huyo binti ninayekuambia kuwa alikuwa mwanafunzi wangu hapa, yeye alikuwa namba moja katika ulengaji wa shabaha, aliweza hata kuwashinda mabinti zangu kwa kulenga shabaha..’akasema….hapo nikagwaya, na kwa haraak nikauliza swali jingine;

‘Hebu niambia,maana mara kwa mara unamtaja huyo mwanafunzi wako,unasema alitokea Tanzania, ina maana alikuja moja kwa moja kama mwanafunzi au ilikujaje kwako…?’ nikamuuliza.

‘Hilo nilikuambia nitakusimulia baadaye, maana ana membo yake mengi, ila kwa ufupi,alitokea huko Tanzania akaja kuishi hapa na wazazi wake,na alikuwa na matatizo ambayo nilikuja kugundua kuwa ni mambo yale yale yanayotokana na ulezi, na misha ya ndoa, …haya hayajifichi, na atharai zake ndio hizo.

`Wao walipokuwa wadogo walijikuta wana ule utundu wa kitoto ,wa kupendana, wengi tumepitia huko, lakini tulikuja kujua kuwa ni utoto, …lakini inategeemea mtu na mtu, alichukuliaje huo mchezo, na pia inategemeana na wazazi na malezi. Kwasababu za malezi inaonyesha hawa, binti na mvulana hawakuwa karibu sana na wazazi wao, ili wajua nini na wakati gani, hakuwahi kupata misaada kama hiyo…ndivyo ilivyojionyesha….’akatulia na kuangalai saa.

‘Sasa athari zake zilikuwa kubwa kwa huyu binti, alijikuta anapenda kupita kiasi, lakini mwenzake hajui kuwa anpendwa kihivyo,….Sasa kutokana na malezi, huyo mvulana ndio wale waliolelewa kiholela, sina uhakika sana hilo kumuhusu huyo mvulana….sikuwahi kuujua undani wa huyo mvulana, lakini nahisi atakuwa alijiingiza kwenye mahusiano mapema, au kusoma vitabu vya mapenzi bila kupata muongozo, na matokeo yake akajenga hisia za kimaumbile haraka, haya mambo yanahitaji shule, na  muongozo hasa kwa watoto, tuwe karibu sana nawatoto wetu katika makuzi yao..,.

‘Nikaumbie ukweli, ndoa ni changamoto,nawazazi wakitulia wakasaidiana, hata watoto wao watakuwa hawana shida, lakini tatizo ni hapo wewe umejitahidi kumlea mtoto wako vyema, anakwenda anakutana na kichwa maji….hapo kutachimbika, maana Yule mtoto wako atakuwa na kazi ya ziada, lakini nina imani kuwa mtoto wakike ukimlea vyema, akajua undani wa ndoa, ni vizuri zaidi, ….tuwalee mabinti zetu, na kuwa karibu nao, ni vyema zaidi.

‘Huyu binti, niligundua kuwa alipata shida na hakukuwa na mtu wa kumsaidia maana wazazi hawakujua hilo mapema, na athari za kisaikolojia zikamtawala akilini, na jinsi alivyozidi kukua akajenga chuki kutokana na wivu,…chuki ile ni pale alipomfumania huyo mvulana wake, na hakujua jinsi gani ya kujitetea, na hata alipokuwa mkubwa ile hali ikawa inamtawala akilini….

Tulimasadia na katika kumhoji ndipo nikagundua kuwa binti huyo ana akili sana…., na ipo siku nitamchukua, kama hajaolewa, nataka tukae naye,….najua akiolewa itakwua shida kumpata, lakini nampenda sana,halafu akiwa na mabinti zangu wanafanana sana, huwa watu wengi wanasema ni ndugu….

‘Kweli wanafanana…’nikajikuta nikisema huku moyoni nikiwa na hamasa ya kujua zaidi lakini haikuwa rahisi muda ulikwisha na isingelikuwa rahisi kumshikilia huyo mama maana nje kulikuwa na watu wengi wanasubiri huduma yake, ….lakini angalau nilichokitaka nimekipata,angalau  kidogo, ni swala laufuatiliaji tu….
Je wewe umegundua nini hapo?

WAZO LA LEO: Jana nilikuwa kwenye hoteli, jamaa akaagiza chakula , yeye na mkewe, aumpenzi wake,chakual kikaletwa cha bei mbaya, wakaanza kula, hata robo haijafika, nikaoan wanalipa na kuondoka, chakual  kile kikawa nii cha kumwaga, soda imenywea robo, imehribika ni ya kumwaga.

Mimi kimawazo, nikaangalia kwa mbali nakuona kile chakula kikutupwa jalalani, na watoto wa mitaani wanakikimilai kukizoa…iliniuma sana moyoni. Kwanini watu wasiagize kile wanachoweza kukimaliza, na ilepesa ya ziada wakawanunulia hawa masikini, hawa watoto wamitaani.  Tukumbuke kuwa riziki ya mungu yaw engine inaweza kupitia mikononi mwako, itoe kwa wenzako…..nikakumbuka usemi wa kutoa moyo, sio utajiri

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Docta mama mke wa mkuu anaweza akawa mshukiwa no 1. Tupe vitu mkuu

emu-three said...

Mkuu vitu hivyo vyaja, ingawaje, mmh, napigika,...inataka moyo!