Nilipofika Kenya nilipokelewa kwa huyo mwanama,maana
nilishawasilina anye, na yeye alinipokea akijua namefika hapo kama mwanafunzi
wake. Niligundua kuwa kwenye hiyo shule yake kuna wanafunzi toka nchi
mbalimbali wapo hapo kupata shule ya ndoa na mahusiano.Kwa kweli huyo mama
amejitahidi, na ameweza hilo. Nilihudhuria darasa lake moja, nilipofika
tu,kabla sijapata muda wa kukaa naye, nikaamini kuwa kweli huyu mama ni jembe,
…
Na hilo darasa dogo tu, nikaamini kuwa kweli ndoa tukiujulia
vyema dunia nzima itakwua na upendo amani na faraja…Basi baada ya hilo darasa
nikamwendea naye akanipokea kwa hamasa na kuanza kunidadisi;
‘Ulinipigia simu kuwa unakuja hapa kwangu, je umekuja
kujiunga na chuo changu, au umekuja na mambo mengine?’ lilikuwa swali la huyu
mwanamama. Tofauti na nilivyomfikiria akilini, huyu kweli ni mama na anasthili
kuitwa `mama Docta’. Lakini mwili wake na umri wake haviendani, inaonekana ni
mtu wa mazoezi,huwezi kabisa kufikiria kuwa ni mama ambaye anataraji wajukuu.
Na nilijiuliza kilini kwanini watu wanaigiza jina lake na kujiita `mama docta’.
‘Nimekuja kwa yote, haja yangu ni kupajua kwanza na hatimaye
kujisajili, nitakuja wakati mwingine, ila nilikuwa na maongezi mengine na
wewe…’nikasema.
‘Haya karibu, lakini nataka kujua maongezi ya namna gani, ya
kuhusu haya ninayofundisha au ni maongezi binafsi,maana huwa sitaki kushitukiziwa.Katika
kitu nisichokipenda ni maswali ya kushitukiziwa yasiyo na maandalizi, sisi ni akina mama kila jambo tunahitaji
kujiandaa kwanza, ….ndiyo asili yetu, au unasemaje?’ akasema nakuniuliza.
‘Nikweli,…..na ndivyo ilivyo, maandalizi kwanza, …tafiti kwanza,
kabla hujafanya au kuongea hilo ulilokusudia…na mimi naamini hilo’nikamwambia na
yeye akaniangalia machoni kwa muda halafu akatabasamu.
‘Wewe unanikumbusha mwanafunzi wangu mmoja toka huko
Tanzania, alikuwa na akili kama zako, yeye nilitaka abakie nami hapa awe ni mmoja
wa walimu wangu, lakini akaondoka kwasaabbu ya wazazi wake, ….’akasema.
‘Ina maana wazazi wake ndio waliomzuia asisome,?’ nikauliza.
‘Wazazi wake walikuwa wakihamia huko kwao, walihamisha
biashara yao kwenda Dar ,na kila kitu, basi na huyo mwanafunzi wangu akasema na
y eye anaondoka, nilimpenda sana maana alikuwa na kili, na mfuatiliaji mzuri wa
mafunzo yangu, na pia alisomea udakitari, …kwa kumpenda walishaanza kumuita
`mama docta mtarajiwa….’akasema.
Moyoni nilianza kuingiwa na shauku, `mama Docta mtarajiwa’
ni nani huyo, lakini sikutaka kuonyesha yale niliyokuwa nayo moyoni mapema,
nikakaribishwa ofisini kwake, na hapo nilikuta watu wengi wakimsubiri,lakini
akanipa kipa umbele.
‘Haya tuongee, maana kama unavyoona hapo nje watu wengi wanahitaji
kuniona, hii inaonyesha jinsi gani ndoa zetu zilivyokuwa na matatizo, na wengi
walipogundua hilo, wakaondoa aibu, na huja hapa kutaka ushauri, na mafunzo
jinsi gani waboreshe ndoa zao…na wengi wanaokuja hapa ni wanawake…kama
unavyoona hapo nje….’akasema.
‘Kwanini wanaume hawapendi kuja na ilihali ndoa ni mke na
mume..?’ nikamuuliza.
‘Labda kwasababu wengi wanaichukulia hii kama `kitchen
party’ kuwa ni maswala ya kina mama, lakini ingelikuwa vyema hata wanaume
wangelikuja, na ingesaidia sana,hata hivyo nina mpango wa kuanzisha kitengo
hicho, kwanza nimeaanza kuwaandaa walimu wanume….najua watavutia wenzao….’akasema.
Yule docta mama, akaniangalia kwa muda tena machoni,halafu
akatabasamu, na kabla sijamuulizia yangu niliyotaka kmuuliza akanitupia swali,;
‘Wewe umeolewa?’
‘Nili……lakini sasa nipo peke yangu…’nikasema kwa mkato,
akatabasamu na kusema;
‘Nimehisi hivyo, macho yako yanaonyesha huzuni iliyojificha,
ila yana ujasiri wa kukambiliana na matatizo,…kuna dalili kuwa unasononeka, lakini
hujakata tamaa,…wewe ni jasiri,…nahisi kuna jambo lilikukwaza….macho yana siri
kubwa, …mimi nimekuwa nikiligundua hilo kwa wateja wangu wengi, na ukidadisi
sana, utakuta wengi wamejikuta wakisononeka kwasababu ya mapenzi,kwasaababu ya
ndoa….zao’akasema.
‘Kwahiyo unahisi kuwa nina matatizo hayo?’ nikamuuliza,
‘Sio nahisi , ni kweli nikuonavyo, una shida au uliwahi
kupata shida ambayo imekuwa ikikutaabisha, hasa ya kimapenzi, hebu niambie
ilikuwaje kwa mume wako au mchumba
wako…?’ akaanza kuniuliza, na hapo nikagundua kuwa huyu mama hana tofauti na
mimi,….kuhusu udadisi wa mamb ya ndani ya nfasi ya mtu,na nikikaa naye
tutaivana naye sana, lakini sikuwa na muda huo.
‘Hilo tuliweke kama agenda nikirudi tena..au unasemaje,
…’nikasema huku nikiangalia nje watu wakizidi kuongezeka….
‘Mimi nimekuja na mengine, ni mbali kidogo na hayo, labda
kwa kujitambulisha tu ,mimi ni wakili, nipo serikalini, lakini nataka kujitoa
na kuwa wakili wa kujitegemea, na lengo langu ni kubobea kama wakili wa
kusaidia kesi za akina mama,na ili nifanikiwe hilo, nahitaji kujua mengi kuhusu
ndoa, akina mama na maingiliano yao akina baba, najua kwako nitafaidika sana,
ila hilo tutaliongelea wakati mwingine,…’nikasema lakini kabal sijaongea
mengine akaanza kuongea …..
‘Safi kabisa, hilo tutasaidiana na kabla hujaanzisha hiyo
ofisi yako kuja kwangu kwanza, nitakufunda, na utawajua akina mama, na jinsi
gani wanapata shida na waume zao,….nikuambie ukweli, akina mama wengi, ni
wavivu kujifunza,na kama wangelijua hilo, waume wao wangelikuwa hapa….’akaonyesha kiganja cha
mkono.
‘Hebu niambie kuhusu familia yako,…..?’ nikamtupia swali kwa
haraka kabla hajaanza kuongea mengine.
‘Kuhusu familia yangu,…..?’ akauliza na bila kutia
shaka,akaendelea kuongea kwa haraka, inaonyesha jinsi gani alivyojipanga katika
kila swali, na alionyesha alikuwa akiongea haraka ili kwenda na muda akasema;
‘Mimi familia yangu tulijipanga vyema,na hili nilianzia kwa
mume wangu, tulipokuwa Ulaya,ambapo ndipo nilikutana na mume wangu, tukajikuta
tumependana, kwa mara ya kwanza nilikutana na huyo mume wangu kwenya maktaba ya
hpo chuoni, katika kutafutatafuta vitabu, nikajikuta nikimuulizia baadhi ya
vitabu..
‘Unapenda sana kusoma mambo ya ndoa, unatarajia kuolewa
karibuni nini…?’akaniuliza.
‘Hapana, katika muda wangu wa ziada huwa najaribu kujifunza
haya mambo, najua itakuwa sehemu muhimu katik kazi yangu hiii ya
udakitari….’nikamwambia,
Basi kila tukikutana naye humo ananitania kwakuniita `mama
wa ndoa…’ kwahiyo jina hili la `mama’ lilianzia hpo kwa mume wangu,na kwa vile
alikuwa akiniita kila mara kwa jina hilo
`mama wa ndoa,’ hata wenzangu wakawa wananiita hivyo hivyo,…`mama wa ndoa’ hata kabla sijaolewa au kuwa mama kiukweli….na
baadaye nilipopata kazi ikabadilika na kuitwa `mama Docta…’
‘Nikawa karibu sana na huyu mwenzangu, hata kabla hatujawa
marafiki, tukawa tukikutana tunajadili mambo ya ndoa,maisha ya huku kwetu, na
baadaye nikagundua kuwa tunatokea sehemu moja, lakini yeye wazazi wake
walihamia Kenya kwa muda mrefu,kabla ya wazazi wangu,…..
Moja likazaa jingine,tukawa marafiki, na urafiki ukageuka
kuwa mchumba, na tukiwa huko huko, akaniomba anivalishe pete ya uchumba, na
hapo nikastaajabu, yeye hajanijua vyema hata mimi sijamjua vyema, nikimaanisha
wazazi na familia zetu, kiundani, keshaamua kunitaka uchumba. Nikaweka
pingamizi kuwa mpaka tukirudi nyumbani na kuwafahamisha wazazi wetu ndipo
nitakuwa tayari kwa hilo,akanielewa…na kukubaliana nalo.
Kwahiyo huko tukaishi kama marafiki tu,hadi tuliporejea
nyumbani, na kuwafahamisha wazazi wetu, ambao walitafutana na walipoelewana na
kuchunguzana wakagundua kuwa hatukufanya makosa, na haikuchukua muda tukaoana.
Na baadaye tukarudi Ulaya tena kwa masomo yetu, maana kila mmoja alipanga
kurudi tena, kwa hatua ya juu.
‘Uaya ikawa kama nyumbani kwetu, maana hata baada ya
kumaliza masomo tulipata ajira huko, ila tulihakikisha kuwa familia yetu inajua
kwao, tulipozaa watoto, tukawarudiha huku, wakawa wanaishi na bibi zao,ndio
maana unaoan wanajua Kiswahili vyema kabisa,hatukutaka kufanya makosa. Labada
katika kuishi kwao na bibi zao, hawakupata yale yote tuliyokusidia mimi na
mwenzangu, maana tulijipanga vyema jinsi ya kuwalea watoto wetu….kila hatua
tulisoma kujua ni nini tufanye….
‘Tukiachia huko, nilikuambia kuwa mimi na mume wangu
tulikuwa tukisoma kuhusu ndoa ktikamuda wa zida,
licha ya kuwa tuliijua yale
muhimu, lakini tulifanya tafiti zetu, kwa kusoma vitabu mbalimbali. Hili
tulijifunza toka kwa wenzetu wa huko ambao kila jambo kabla ya kulifanya au
kuliingilia wanalifanyia utafiti kwanza. Na sisi tukawa tumeiga hiyo tabia,
tukajiuliza ndio tumeoana, lakini kwanini tumeoana, kuan nini kunatakiwa kuwe
na ndoa, na ni ipi misingi yake mikubwa….nini mahusiano, yanaathiri nini ndoa,
na nini kifanyike katika mahusiano….
‘Hili linanishangaza sana,kila siku kuna ndoa, kila siku
kupendana, lakini watu hawaangaiki kwanza kutafiti kile wanachotaka kukifanya, hebu nikuulize hivi
kweli unaweza kujua kuendesha gari kabla hujajifunza uderva, hivi kweli unaweza
kuwa wakili kabla hujajifunza uwakili….?’ Akaniluza na kabla sijamjibu akasema.
‘Haiwezekani watu wakimbilie kuoana kabla hawajjua nini
kwanini wanaoana,na humo ndani ya nda kuna nini, nini mahusiano, yanatakiwa
yafanyike vipi… …hili linanipa shida sana,eti wengi wandai halin ahja ya
kujifunza kwasababu ni jambo la asili, hiyo ipo kwenye damu, …
Kwa vipi iwe kwenye damu, mungu hajasema tufanya mambo bila ya kusoma, bila ya kutafiti, katuambia kwanza
tusome, ili kujiua dunia, angalia baba yetu Adamu, kwanza alianza kusoma, kwa
kuju vitu vyote, majina ya vitu…hata malaika walipoulizwa kuhusu hilo
walishindwa baba yetu Adamu akatambua, …..huu ni mfano wa asili kuwa kila jambo
kwanza lazima ulisomee….’akatulia.
‘Ndoa nyingi zinaharibika, maisha yanakuwa ya shida,amani
hakuna, lakini watu hawajajua kuwa chanzo chake kimeanzia wapi, ni siri kubwa
sana …tuliligundua hili mimi na mume wangu, ….watu hawaamini,lakini ndivyo
ilivyo, yote hayo yameanzia kwenye ujinga wa kutozijua ndoa,….unaweza usiamini
hili, kuwa dunia hii, watu wanauana,watu wanashida, kwasababu ya ujinga wa
kutoijua ndoa?’ akaniuliza.
‘Ni ujinga wa kutoijua ndoa,….maana ndoa ndio muhimili wa
maisha,ndoa ikiboreka,na kuimarika ni sawa na mti,ni sawa na shina, likiwa
imara, mti utakuwa imara, na utazaa matunda bora, ambayo ni manufaa ya baadaye.
Halikadhalika, ndoa ikiwa bora, mume mwema na mke mwema, wakawa wanapendana kiukweli,
wakajaliana, watakuwa na afya njema,watakuwa na furaha, na mwisho wake watapata
Baraka, watazaa watoto ambao watakulia katika malenzi bora…..’akaangalia saa
yake,.
‘Unaona hapo, wazazi wamekuwa chanzo cha kutoa kizazi bora,
cheye malezi bora, elimu ,afya na malazi na huduma bora upendo na amani,
….imejijenga kwenye familia, nini unatarajia kutoka katikahiyo
familia,….’akatulia na kuniangalia.
‘Familia hiyo itazaa matunda mema,…watoto wema, ambao
wanakuja kuendeleza kizazi chema, kizazi na kinakuwa katika mtindo huo,na
kutokea jamii njema,yenye maadili mema, na ukilikuza hilo linatokea nini taifa
jema, je unatarajia nini hapo, kama sio amani, upendo,…sasa niambie vita, njaa,
magonjwa, yatatokea wapi,…..hebu niambie, uadui na visasi vya kusalitiana
vitatokea wapi,…?’ akaniangalia kwa makini.
‘Sasa hebu chukua kinyume chake utaona matokea yake,….sasa
hivi watoto wa mitaani wamejaa kibao, watoto wanazaliwa na kulelewa na mzazi
mmoja, watajuaje upendo unatokana na baba na mama,watajuaje, jinsi baba na mama
wanatakiwa waishi….visasi chuki, kukata tamaaa, kunatawala dunia, njaa,
magonjwa yanagubika dunia,ubinfsi choyo,….nakila aina ya ubaya unatokea, sababu
kubwa ni ujinga…ujinga wa kutokufahamu nini maana ya ndoa….
‘Hili sisi tuliliona mimi na mume wangu tukasema hapana,
sisi sio watu wa dini..ndio, lakini tunaweza kufanya haya, kama sehemu ya dini,
maana kwanza lazima umjenge mtu kiroho, kiupendo,….ili ajijue kuwa yeye ni
nani, yeye ni binadamu , na kapewa mamlaka ya kuitawala dunia lakini atawezeje
kuitawala dunia kama yeye mwenyewe hajijui, …nakujijua ni pamoja na kujijua
ndoa yake, ….wewe hujui ndoa ndoayako utawezaje kuzitawala ndoa za
wenzako,….maana uongozi huanzia ndani kwako, huanzia kwako mwenyewe,halafu kwa
familia yako, na baadaye kwa jamii….naliona hili mpendwa.
‘Kwakweli tulimuomba mungu sana, ili watu watuelewe, maana
tulipoanzisha watu walitafsiri vibaya, labda tunataka kuweka mambo ya siri
hadharani,eti tunawafundisha watu mambo ya kihuni,…sio lengo letu hilo, nia na
madhumuni yetu ni kujenga jamii, iwe katika mapenzi ya dhati, mke na mume
wajijue, kwani wao wakijijua, na kujua yale yaliyopo mbele yao, majukumu yao,
….watapata familia bora kwa vizazi bora….’akasema huku akiangalia saa yake.
‘Naona tuishie hapo kwa upande wangu, una swali jingine
kuhusu mimi…..?’ akaniuliza huku akianglia saayake tena na kuangali nje
akiogopa watu wanavyozidi kuongezeka..
‘Maswali yapo mengi,ila nilitaka kujua kuhusu watoto
wako,…..uliwaleaje,ndio umeniambia ulezi wako kwanza ulianzia kwa bibi yao,
lakini je ulipokuwa nao uliwaleaje, na pili nataka kujua kuhusu huyu mwanafunzi
wako uliyesema ulimpeda sana, kwanini ulimpenda na je uligundua nini kuhusu
yeye…?’ nikamuuliza.
‘Wewe ni wakili, au sio…kuna tatizo limetokea huko ulipotoka, kuhusu mtoto wangu, au kuhuu
huyo mwanafunzi wangu….?’akaniuliza kwa mashaka, na kablasijamjibu akasema;
‘Mimi napenda mtu anayeongea ukweli…., naomba uniambie
ukweli…kwasababu ukweli ni siri kubwa katika maisha ,hasa ya ndoa, ukiwa sio
mkweli kwa mwezako una walakini, upendo wenu una walakini…..nikaumbie kitu,mimi
namume wangu hatufichani kitu,….ananijua kama ninavyomjua mimi…nashangaa eti
watu wanaishi ndani ya ndoa, lakini kila mtu ana lake, hata simu haziruhusiwi
kuchangiana, unaona tati hapo.., tatizo la kutoisoma ndoa.
‘Nina mengi ya kukuelemisha wewe wakili ,lakimi naenda na
muda, wewe kama unataka haya, jiandikishe uwe mwanafunzi wangu, utapata mengi,
ama kuhsusu watoto wangu, nitakuambia tu kwa ufupi,jinsi nilivyowalea, na kama nilivyokuambia,
ulezi wao mwanzo ulianzia kwangu, maana niliwanyoyesha hadi pale walipofikisha
miaka miwili, watoto wangu walikuwa mapacha,….’akasema.
‘Ina maana una watoto mapacha?’ nikauliza,
‘Mimi nilikuwa najua wajua hilo, ooh,hebu ngoja kidogo…’akatoka
nje na baadaye akarudi, alikaa kidogo, na mara mlango ukafunguliwa, akaingia
binti, akiwa kavalia kidakitari.
Oooh, moyo ukanishituka, maana aliyesimama mbele yangu ni
mke wa wakili wetu mkuu, nikabakia nikipepesamacho, sikuficha nikauliza.
‘Wewe umakuja lini huku?’ nikauliza. Wote wakaangua kicheko,
na Yule binti akasema kiutani,
‘Nimekuja jana na ndege….’akasema huku akicheka.
‘Mara nyingi watu wanawachangaya watoto hawa na hata
wanashindwa kuwatofautisha….huyu sio huyo unayemzungumzia, huyo unayemzungumzia
ulimuacha Dar, ni pacha mwenza wa
huyu,wanafanana sana, na tabia zao zinatofautiana kidogo,maana mwenzake huyo wa
huko Dar,ana hasira kidogo,….maana asili hazipotei,sisi tunatokea huko
Tanzania, mikoa ya ziwa , siunafahamu zile zetu…..’akasema na kucheka.
‘Lakini kwa ujumla mimi niliwalea na kuhakikisha kuwa
wanakulia katikamaisha mema,kuna udhaifu wa hapa na pale, kwasababu wakati
anaolewa na huyo mume wake,niliwaomba kwanza waje waishi kwangu, niwafunde
vyema, lakini mume alipinga,..yule mume ana ule `uume’ ubinafsi…’ akasema huku
akionyesha ngumi hewani.
‘Hili nililiona mapema,na tulimkanya sana binti yetu,
tukamwambia ndoa njema hujenga na mume au mke mwema,huyo mume wako anaonekana
kabisa, sio mume mwema, tulimwambia hilo bila kumficha, lakini yeye akaona kuwa
kafika….ndio tatio la kiazazi chetu,…unafundisha kwako, lakini atakutana na
jamii nyingine, ambayo ….ooh. Hili ndilo kosa, inatakwia wote wasome waijue
ndoa,….Kama Yule mume angelikubali na kukaa na mimi kwa wiki moja tu,
angelibadilika,lakini ……mmmh
‘Mimi nilijua kwa vile binti yako katokea hapa kwako chuoni,
penye malezi bora, angeliweza kumbadili mume wake?’ nikauliza.
‘Ingeliwezekana, kama mume angalikubali,nina uhakika huo….,maana
binti yangu,licha ya kutokupenda sana haya madarasa ya ndoa, lakini nilimfundavyema,
lakini hilo halitawezekana kama mume hataki, ….yule mume anaonekana kalelewa
ile ya kizamani, mume ni mume tu, amri mkononi…sasa hili halijengi, ndio maana
nikasema huo ni ujinga wa kutosoma nini maana ya ndoa,
Unajua nikuambia kuna kusoma mambo ya kawaida, kama sheria,
udakitari,.., na kuna kuisoma ndoa,….kila Nyanja ina maudhui yake, Yule mume kasoma sheria,
hajaisomea ndoa nakujiua ndoa ni nini, na hataki kuisoma ndoa akiwa na mawazo yale ya kurithi tu,…. angelikubali
akaisoma ndoa,akatulia na mke wake,mbona ingekuwa raha….
‘Je uliwahi kuongea na huyo mume wabinti yako..?’
nikamuuliza.
‘Mwanzoni alikuja na gia ya heshima,na siku moja nikamuuliza
kuwa yey anataka kumuoa binti yangu, je amejiandaje, je anajua majukumu ya
ndoa, akanijibu kuwa anajua vyema sana, na amejiandaa sana,…kwasaabu yeye ni
wakili, nikajau anasema ukweli, lakini nilipotafiti nikagundua kuwa ni wale
wanaosema wanajua…kwasababu wanajua kupandambegu, lakini sio kwa utaalamu,..
eti kwasababu ni mume, eti kwasababu ni mke,yote yanajilta tu….tunajidanganya,…baadaye
niliaribu kumuita, akawa kila mara anasema hana nafasi…
‘Sasa uliwezaje kuisadiai ndoa yao..maana nyie ni wazazi
kama kuna tatizo lazima mlitatue?’ nikaamuliza.
‘Kuisaidia ndoa yao ingelikuwa rahisi kama mume angelikubali
kumsikiliza mke wake, huenda ….mke kajaribu kashindwa, hilo nimejaribu
kumuuliza binti yangu,…yeye anasema kajitahidi yale yote anayyajau lakini
kashindwa, na inavyoonekana kuna mengi zaidi ya ndoa yao ambayo mimi siyajui,
kwani binti yangu hajataka kuniambia ukweli wa ndani, lakini sijakata tamaa,
najua jinsi gani ya kuwaingia, nitawaendea huko huko…’akasema.
‘Binti yako hajawahi kukulalamikia..?’ akauliza.
‘Analalamika, lakini mwenyewe kasema hajashindwa, atapambana
na mume wake hadi kieleweke,na mimi nawapa muda, …sijataka kuliingilia kiundani
sana, namjua vyema binti yangu ni jasiri, pamoja na mengine nimewafundisha
watoto wangu ujasiri, wasilegee, wanajua kupambana na maisha,kwa shida na raha,
na kwasabaabu kaamua kuliingia pori, basi ajue kuwa kwenye pori kuna
miiba…’akasema.
‘Ujasiri huo umewafundishaje…kupigana, au kufanay nini?’
nikaamuuliza huyo mwanamama.
‘Mazoezi ni muhimu sana, wewe kama mzazi kila asubihi waamushe
watoto wako, na kabla hawajajichanganya, wape mazoezi,mimi nilianza kuwapa
watoto wangu mazoezi wakiwa bado wadogo, kwahiyo wakakulia katika hali hiyo
tango utotoni,….mazoezi ya kujihami, karate, na kujikinga , kwa mfano ukikutana
na mtu mwenye kisu, utajihami vipi, yote hayo nimewafundisha, wanajua…’akatulia
na kuniangalia.
‘Hata kutumia bunduki wanajua…?’nikajikuta namuuliza hilo
swali
‘Ndio,….hilo niliwafudisha pia, unajua baba yao anapenda sana
maswala ya kulenga shabaha…kuwinda, basi huwa akienda mazoezini anawachukua
mabinti zake,..hutaamini, wote ni walengaji wazuri wa shabaha,…na hata baadhi
ya wanafunzi wangu wanapenda shabaha piam huwa tunawachukua kwenye mazoeizi ya
shabaha, na nikuambie siri moja kubwa kwa kina mama, wakina mama ni walengaji
wazuri wa shabaha….’akasema huku akishika kifuani sehemu ya matiti yake.
Niliposikia hivyo moyo ukaanza kwenda mbio, sikutaka
kuonyesha hiyo hali, nikauliza swali jingine kwa haraka, Ili kuficha hiyo hali;
‘Lakini hilo linasaidia nini katika maswala ya ndoa?’
nikauliza.
‘Ndoa ina mambo
mengi, kuoana sio sababu ya kuficha vipaji, hilo la shabaha ni moja ya vipaji,
ni mazoezi, huwezi jua, wanaweza kujikuta wapo kwenye mashindano yakulenga
shabaha ya dunia, tusifiche vipaji eti kwasababu tupo kwenye ndoa.
‘Na wengi wa wanafunzi wangu walipenda hilo zoezi la shabha,
na hata huyo binti ninayekuambia kuwa alikuwa mwanafunzi wangu hapa, yeye
alikuwa namba moja katika ulengaji wa shabaha, aliweza hata kuwashinda mabinti
zangu kwa kulenga shabaha..’akasema….hapo nikagwaya, na kwa haraak nikauliza
swali jingine;
‘Hebu niambia,maana mara kwa mara unamtaja huyo mwanafunzi
wako,unasema alitokea Tanzania, ina maana alikuja moja kwa moja kama mwanafunzi
au ilikujaje kwako…?’ nikamuuliza.
‘Hilo nilikuambia nitakusimulia baadaye, maana ana membo
yake mengi, ila kwa ufupi,alitokea huko Tanzania akaja kuishi hapa na wazazi
wake,na alikuwa na matatizo ambayo nilikuja kugundua kuwa ni mambo yale yale
yanayotokana na ulezi, na misha ya ndoa, …haya hayajifichi, na atharai zake
ndio hizo.
`Wao walipokuwa wadogo walijikuta wana ule utundu wa kitoto
,wa kupendana, wengi tumepitia huko, lakini tulikuja kujua kuwa ni utoto,
…lakini inategeemea mtu na mtu, alichukuliaje huo mchezo, na pia inategemeana
na wazazi na malezi. Kwasababu za malezi inaonyesha hawa, binti na mvulana hawakuwa
karibu sana na wazazi wao, ili wajua nini na wakati gani, hakuwahi kupata
misaada kama hiyo…ndivyo ilivyojionyesha….’akatulia na kuangalai saa.
‘Sasa athari zake zilikuwa kubwa kwa huyu binti, alijikuta
anapenda kupita kiasi, lakini mwenzake hajui kuwa anpendwa kihivyo,….Sasa
kutokana na malezi, huyo mvulana ndio wale waliolelewa kiholela, sina uhakika
sana hilo kumuhusu huyo mvulana….sikuwahi kuujua undani wa huyo mvulana, lakini
nahisi atakuwa alijiingiza kwenye mahusiano mapema, au kusoma vitabu vya
mapenzi bila kupata muongozo, na matokeo yake akajenga hisia za kimaumbile
haraka, haya mambo yanahitaji shule, na muongozo hasa kwa watoto, tuwe karibu sana
nawatoto wetu katika makuzi yao..,.
‘Nikaumbie ukweli, ndoa ni changamoto,nawazazi wakitulia
wakasaidiana, hata watoto wao watakuwa hawana shida, lakini tatizo ni hapo wewe
umejitahidi kumlea mtoto wako vyema, anakwenda anakutana na kichwa maji….hapo kutachimbika,
maana Yule mtoto wako atakuwa na kazi ya ziada, lakini nina imani kuwa mtoto
wakike ukimlea vyema, akajua undani wa ndoa, ni vizuri zaidi, ….tuwalee mabinti
zetu, na kuwa karibu nao, ni vyema zaidi.
‘Huyu binti, niligundua kuwa alipata shida na hakukuwa na
mtu wa kumsaidia maana wazazi hawakujua hilo mapema, na athari za kisaikolojia
zikamtawala akilini, na jinsi alivyozidi kukua akajenga chuki kutokana na wivu,…chuki
ile ni pale alipomfumania huyo mvulana wake, na hakujua jinsi gani ya kujitetea,
na hata alipokuwa mkubwa ile hali ikawa inamtawala akilini….
Tulimasadia na katika kumhoji ndipo nikagundua kuwa binti
huyo ana akili sana…., na ipo siku nitamchukua, kama hajaolewa, nataka tukae
naye,….najua akiolewa itakwua shida kumpata, lakini nampenda sana,halafu akiwa
na mabinti zangu wanafanana sana, huwa watu wengi wanasema ni ndugu….
‘Kweli wanafanana…’nikajikuta nikisema huku moyoni nikiwa na
hamasa ya kujua zaidi lakini haikuwa rahisi muda ulikwisha na isingelikuwa
rahisi kumshikilia huyo mama maana nje kulikuwa na watu wengi wanasubiri huduma
yake, ….lakini angalau nilichokitaka nimekipata,angalau kidogo, ni swala laufuatiliaji tu….
Je wewe umegundua nini hapo?
WAZO LA LEO: Jana
nilikuwa kwenye hoteli, jamaa akaagiza chakula , yeye na mkewe, aumpenzi
wake,chakual kikaletwa cha bei mbaya, wakaanza kula, hata robo haijafika,
nikaoan wanalipa na kuondoka, chakual
kile kikawa nii cha kumwaga, soda imenywea robo, imehribika ni ya
kumwaga.
Mimi kimawazo, nikaangalia kwa mbali nakuona kile chakula
kikutupwa jalalani, na watoto wa mitaani wanakikimilai kukizoa…iliniuma sana
moyoni. Kwanini watu wasiagize kile wanachoweza kukimaliza, na ilepesa ya ziada
wakawanunulia hawa masikini, hawa watoto wamitaani. Tukumbuke kuwa riziki ya mungu yaw engine inaweza
kupitia mikononi mwako, itoe kwa wenzako…..nikakumbuka usemi wa kutoa moyo, sio
utajiri
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Docta mama mke wa mkuu anaweza akawa mshukiwa no 1. Tupe vitu mkuu
Mkuu vitu hivyo vyaja, ingawaje, mmh, napigika,...inataka moyo!
Post a Comment