‘Siku ile ya tukio, kama ilivyojulikana shabaha ilikuwa
kuuliwa mimi, na aliyepewa kazi hiyo ya kuniua mimi ni dereve wa Kimwana,ambaye
alipokea taarifa hiyo toka kwa bosi wake,…hapa kwanza tutajiuliza bosi wake
huyo alikuwa ni nani, ….? Maana Kimwana ndiye anayejulikana kuwa ni bosi wake,…kumba
kuna bosi mwingine mwenye mamlka zaidi ya Kimwana, ni Sokoti, au ninani, kazi
kubwa hapa ni kumtafuta huyo bosi wa huyu dereva, nikaiweka kama kazi maalumu
ya kufuatilia.
Lakini tukumbuke kuwa risasi iliyotoka kwenye bastola ya
huyo dereva sio hiyo iliyomuua Kimwana, hili polisi wenyewe walikuja kulithibitisha,
na baadaye tukagundua risasi ya iliyotoka kwenye bastola, ikiwa imezama kwenye
mifuko ya cement,ambayo ndiyo iliyotoka kwenye bastola ya dereva,swali likaja
risasi iliyomuua Kimwana ilitoka kwenye bunduki ipi,na hili…lilikuja kunipa
ufumbuzi Fulani tutauona baadaye
Na kweli polisi walipochunguza waligundua kuwa ile risasi iliyokuwa ndani ya mwili wa
Kimwana, haikuwa ya bastola, ilikuwa tofauti na risasi ya bastola,
ile risasi ilitoka kwenye silaha kubwa, na hili lilikuja kugunduka
baadaye baada ya mimi kugundua hiyo risasi iliyokuwa imetumbukia kwenye mfuko
wa cement….swali likaja ,hii bunduki ilikuwa ikimilikiwa na nani,….
Kwahiyo kwa kipengele hicho ni kuwa muuaji alikuwa mbali na
jengo, na polisi waligundua kuwa huyo muuaji atakuwa alikuwa kwenye jengo la
pili yake, ambalo ni refu, na ukiwa pale unaona jengo hilo ambapo nilikuwa
nimesimama mimi na Kimwana, na unamuona vyema mtu akiwa kasimama ndani ya kile
chumba, lakini dirisha hilo lina kiyoo, chenye matundu ambayo yanaweza
kupitisha risasi.Ukumbuke jingo hilo lilikuwa halijaanza kutumika.
Ina maana huyo muuaji, ana sifa kubwa ya kulenga shabaha,
kwasababu ile risasi ilitakiwa kupenya kwenye moya ya matundu madogo yaliyokuwa
kwenye hilo dirisha, na kwa umbali ule, alitakiwa mtu mwenye shabaha kali, ili
isiweze kukosea, na kama angeliweza kukosea, kile kiyoo kingeliweza kusambaratika
na kupiga ukulele ambao ungeliwashitua watu wengine,….
Ni hapo nikapata swali jingine, je , huyo muuaji alikuwa na
lengo la kuniua mimi au Kimwana ? maana
kamanisingeliinama huenda hiyo risasi ingelinipata mimi,lakini ukichunguza kwa
makini sehemu niliyokuwa nimesimama,hata kama nisingeliinama, angeliweza
kumpiga Kimwana bila ya mimi kuzurika,…
Kwahiyo hapo Jibu lipo wazi kuwa huyo muuaji alikuwa na
lengo la kumuua Kimwana,sio mimi,….kwahiyo kwa mtizamo huo huyo muuaji alikuwa
na kisasi na Kimwana, sio mimi, tofauti na dereva ambaye alitakiwa kuniua mimi,
ili nisije kuitoa siri, ambayo walijua nimeshaipta toka kwa Kimwana.
Je, huyo mlenga shabaha, alijua kuwa huyo dereve anataka
kuniua mimi, na je alijuaje kuwa hiyo risasi itanikosa mimi. Hapo ndipo
utagundua kuwa, lengo la huyo bosi, ilikuwa tuuliwe sote wawili, kwanza dereve
aniue mimi, na wakati huohuo, huyo mlenga shabaha amuue Kimwana, …..
Hapo utagundua kuwa huyo mlenga shabaha, alikuwa ndiye huyo
huyo bosi aliyekuwa akitoa amri kuwa dereva aniue mimi, alikuwa akiwaona wote
toka jengo lile, na pale aliposimama, alikuwa akimuona dereve akilenga shabaha,
na yeye akalenga shabaha yake hapo hapo,….
Ukiangalia hizo sifa utaanza kugundua jambo, kuwa huyo
muuaji wa Kimwana, kuwa ana sifa ya kulenga shabaha, na pili ni bosi wa dereva,
hata kama sio bosi, basi atakuwa na mafungamano na huyo dereva. Na ukumbuke
kuwa hata baaada ya polisi kutumia mbinu mbalimbali,huyo dereva mpaka sasa
hajaweza kukiri kuwa ni nani aliyemtumia huo ujumbe, inaonyesha dhahiri, hana
uhakika, ni nanikati ya hawo mabosi wake….
Polisi walichunguza hiyo namba ya simu, wakagundua kuwa ni
namba isiyo na jina,na haikuweza kufahamika ni nani aliyemtumia huo ujumbe na
hata kumpigia hiyo simu, maana kuna ujumbe na simu, na je vyote hivyo viwili
vilitoka kwa mtu mmoja…..!
Huyo dereva alidai kuwa yeye anapigiwa simu za namna hiyo na
watu wengi, hasa inapofikia hatua ya kufanya jambo kubwa kama hilo na wapigaji
hawajiweki wazi, lakini kwa siku ile alijua kuwa imetoka kwa Sokoti,…lakini
baadaya tukio aligundua kuwa sio yeye, …sasa alikuwa nani mwingine, polisi
wanasema walijaribu kila njia ili aweze kumjua huyomtu mwingine, lakini
hakuweza, huenda anamficha,….nahata walipomuuliza kuwa huyo aliyepiga simu alikuwa
mke au mume, alisema,suti likuwa kama mtu aliyefunika mdomo, huwezi kuitambua
ila ilikuwa besi nzitoo la kiume au lakike lakuigiza,…
‘Sauti livyosikika ilikuwa huwezi kujua ni ya kike au ni ya
kiume, ina maana mpigaji aliweka kitu mdomoni, hata hivyo polisi walisema kwenye
maelezo yao kuwa huyu jamaa inaonekana alikuwa akidanganya, …..kwa uchunguzi
wangu, alikuwa hadanganyi, hakuwa an uhakika kabisa aliyempigia ni nani….
Mpaka hapo tutakuwa na mambo ya kuunganisha ilikumpata huyo
muuaji, kwanza awe na shabaha ya kulenga kwa mbali kwa kutumia bunduki, pili
awe ni bosi wa huyo dereva,tatu awe pesa, na zaidi awena nakisasi na huyo
binti, …nasema awe nazo, maana alimuahidi kumlipa huyo dereva pesa nyingi,na
zaidi awe ni mtu muhimu wa huyo dereva, maana hata mbinu zilipotumika kwa huyo
dereva ili kumtaja ni nani, haikusaidia kitu.Polisi wakihisi anajua jambo,
lakini sio kweli…wengi ndani ya kundi hilo walikuwa hawajui nini kinaendelea
nyuma ya pazia.
Tulifuatilia maisha ya Sokoti, katika ulengaji wa shabaha,
tukakuta kuwa sio mtaalamu sana wa kulenga shabaha, kwahiyo sifa mojawapo hapo
hana, lakini ana sifa kubwa kuwa ni bosi wa huyo dereva, na ni bosi wemye
mamlaka, akitoa amri hutekelezwa.
Docta mama ndiye bosi tunayemjua toka awali hata Sokoti
alikuwa nyuma yake,je alikuwa akiweza kutoa amri kwa huyu dereva,….lakini swali
jingine likaja hapo nidocta mama yupi, ukumbuke docta mama kwenye
kundi hili wapo watatu. Wa kwanza ni mke
wa wakili wetu mkuu wa kitengo, wa pili ni Yule mchumba wa Msomali wa kijijini
na watatu hajulikani sana, lakini yupo ambaye alishika nafsi hiyo baada ya
binti wa kijijini kuaga kuwa anakwenda Kenya.
Je kati ya hawa ni nani anasifa hizo hapo juu, hakuna
kumbukumbu za kipolisi zilizothibitisha kuwa hawo akina mama, kama wanavyoitwa
kuwa wanajua kulenga shabaha, licha ya kuwa wanasifa za ubosi.
Lakini hebu turejee nyuma, kipindi mauaji haya yanatokea,
je,ni nani kati ya hawo watatu alikuwa ndiye kashikili nafasi ya udocta-mama?
Hili tutakuja kulijua baadaye, …….
Polisi walifikia hatua wakagonga ukuta, na wakawa kama wanapoteza
muda tu, huku wakisema mauaji hayo ni yakulipiza kisasi, na ni wao wenyewe kwa
wenyewe, haina haja ya kuhangaika sana. Kwangu mimi ilikuwa ni changamoto.
Niliingiwa na hamu ya kumjua ni nani hasa muuajii wa Kimwana na alikuwa an
lengo gani hasa,na ukumbuke nilikuwa namtetea Msomali ambaye alijikuta akiingia
matatani kila hatua.
********
Kwangu mimi ilikuwa
ni changamoto, sikukubali kushindwa, nilikuwa na hamu sana ya kumpata
muuaji, na kwa uchunguzi wa mwanzo,nilikuwa nimeshajua sifa ambazo
nikizifuatilia nitampata huyo muuaji,. …nikaanza kuwa karibu na kila
aliyeshukiwa, na kuchunguza historia zao kiundani. Ilikuwa sio kazi rahisi mtu
kukuambai undani wake, lakini hatau kwa hatua iliwezekana.
Mimi katika kisa hiki niliweka sifa kubwa ya tukio kuwa ni
tukio lililogubikwa na maisha ya ndoa,kwa hiyo
kwangu kila muhusika
nilimuangalia katika mfumo huo. Nikadadisi mahusiano yake na mwenzake,….na kila
niliyemuhoji, nikakuta ana matatizo yanayofanana, ….angalai wahusika wote
kwenye kundi, wana matatizo kamahayo,……lakini lengo langu kubwa lilikuwa kwa
wahusika wakuu,….wakili wetu muu, Sokoti , …na mamaDocta, lakini mama Docta
anafungamana na mumewe,…na isingelikuwa rahisi kwa mume wake kuniambia lolote…nikatafuta
upenyo kwa kupitia kwa Yule binti yao,ambaye anawajua sana.
Sokoti, ana matatizo ya kusalitiwa na mchumba wake, na
Kimwana ni mmojawapo, lakini pia Kimwana alikuwa msaliti wake katika shughuli
zao, kwahiyo huyu ana kuwa mshukiwa mkubwa sana. Lakini hana sifa ya kulenga
shabaha, na pia tulipomdadidi sana huyo dereva, alisema kuwa yeye alikuwa mra
zote anafuta amri kutoka kwa docta mama.
‘Ina maana kama Sokoti angekuambia kuwa anataka kufnay jambo
lolote ili akulipe ungalifanya ?’ tulimuuliza.
‘Kwa yoyote, kama ataniahidi pesanyingi ningelifanya, lakini
naangalia na usalama wangu, je nitalindwa vipi,….Sokoti angeliweza kunilinda,
kwasababu ya wakili wetu wa kundi, lakini wakili wa kundi alishaanza kuingiwa
wasiwasi na kundi,….’
‘Kwanini,….?’ Nikamuuliza.
‘Kwasababu yeye alikuwepo hapo kwa ajili ya Docta mama, na
Docta mama akawa kajitoa kwenye hilo kundi…..?
‘Unamzungumizia Docta mama yupi?’ nikamuuliza huyo jamaa,
akaniuliza kwa mshangao.
‘Kwani Docta mama wapo wangapi,mimi namjua mmoja tu ,sijui kama
kuna docta mama mwingine….’akasema huyo dereva,na hapo nikajua kuwa siri ya
docta mama tulikuja kuigundua sisi wenyewe, lakini wengi ndani ya kundi hilo
hawakujua mchezo uliokuwa ukitendeka humo ndani ya kundi.
Docta mama walikuwa watatu, na hata polisi walikuja kugundua
hili baada ya mimi kuwafahamisha hilo, nilipowaletea picha za hawo madoctamama,
ilikuwa vigumu kuligundua hilo na ilikuwa kama mshangao, maana sura , maumbile
na tabia za hawa akina mama watatu zinafanana kwa karibu sana,….lakini katika
maisha halisi hawakuonekana kuwa karibu ,yaani kila mmoja alikuwa kama hamjui
mwingine.
‘Polisi hawakuwa na haja sana na hawa kina mama, wao
walikuwa wanangaika kumpata wakili wetu mkuu, na Sokoti ambao hawaonekani, na
kwao wao hawo ndio muhimu sana….
Kwangu nilishaanza kugundua siri kubwa ya hilo kundi, lakini
kama ningeliropoka kwamuda ule, maisha yangu yangelikuwa hatarani, kwani
miongoni mwetu, kulikuwa na watu wanaotumiwa na hilo kundi, nasikuweza kuwajua
ni akina nani, nilisubiri wakati muafaka wa kuliweka hilo hadharani,na hata
hivyo kwawkati kamahuo, hata kamaningeliwaambai polisi hawangeniamini, ….
*******
Siri ya kundi ilianza kuvuja pale nilipokutana na wakili wao
wa kundi, kipindi anapambana na mimi kwenye ulingo wa mahakama. Alipoona kuwa
haelewani na kundi na mama docta keshaondoka, akaamua kujitoa, alipewa masharti
kuwa kama anataka usalama wake aondoke nchini, na utaratibu ukafanywa kuwa anakwenda kusoma. Ni kweli alikwenda kusoma, lakini haikuwa ni
lengo lake la karibu, hilo lilikuja kwa shinikizo la hilo kundi,wakamlipia kila
kitu akaondoka.
Siku anaondoka, akaniachia ujumbe mfupi kwenye simu yangu,….,
kuwa mama Docta hayupo kwenye kundi tena, ila kuna mtu mwingine ameshika nafasi
yake, na kila kitu kimebakia kama vile mama Docta yupo, kwahiyo tuwe makini na
hilo. Nilihangaika sana kupata maelezo yake, lakini sikuweza kumpata.
Nilipogundua kuwa mama docta hayupo, na kwa taarifa
zilizokuwepo kwenye kundi ni kuwa mama docta karudi kwao Kenya, nikawa
nhangaika kujua huyo mama docta aliyekuwa kwenye hilo kundi ni nani, kwakweli
ilikuwa ni vigumu sana kumpata, na hata nilipofika kwenye darasa lao
sikuruhusiwa kuingia, na hata niliposubiri nimuone akitoka kwa siri,sikuweza
kumuona, hakuwa rahisi…..sikujali sana kwa muda huo,…..
Mungu ni mkubwa, nikapata mzigo, ulikuwa nimkanda ule
uliokuwa ukionyesha yale aliyofanya wakili wetu mkuu,nilipoupata na maelekezo
kuwa niufanyie kazi, sikuelewa kuna nini nikifanye kazi, nikawa sihangaiki nao
sana, hadi pale nilipokwenda kuonana na yule binti anayeishi kwa wakili wetu
mkuu,pale nikafunguka macho. Katika maelezo yake aliniambia kuwa kuna dada
mmoja huwa alikuja mara mbili, wanafanana sana na mke wa wakili wetu mkuu…..!
Siku ile nilipoingia ndani ya kupekua chumba cha wakili wetu
mkuu, nilikuta mkanda kama ule niliotumiwa upo pale ndani, na ule mkanda
nilioukuta pale ulikuwa haujafanyiwa uchakachuajia, nikagundua kitu, kuna
sehemu kubwa ilikuwa imeondolewa katika mkanda niliotumiwa, seehmuhiyo
niliikuta kwenye mkanda huo uliokuwa humo ndani,…sehemu hii niliyoikuta humo,
ilionyesha Kimwana anasikiliza simu, na kwenye na ilionyesha dhahiri kuwa anapokea
maelekezo Fulani, kwani aliuliza
‘Tayari yupo chumbani nifanye nini,….?’akatulia na
alionyesha kukunja uso, halafu akapiga piga miguu chini, akasema;
‘Mimi naogopa, huyu ni mtu wa serikali, mimi nitaishije hapa
mjini…’akatulia na kusikiliza.
‘Sawa, lolote likitokea tusija kulaumiana,….’halafu akatulia
na ilionyesha mpigaji keshamaliza, akasimama kwa muda na mara mlio wa simu
nyingine ukalia, akapokea na kusema kwa unyenyekevu.
‘Ndio Docta mama, lakini bosi kaniambia nifanye kweli….’akasema.
‘Ndio wewe ndio bosi mkubwa, lakini…’baadaye akakata simu.
Kuna bosi na bosi mkuu,….na sehemu hiyo ikaja kuondolewa,
kwanini ikaondolewa kwenye mkanda niliotumiwa, na inaonyesha wazi aliyenitumia
hakutaka sehemu hiyo niione, na huu mkanda wenye sehemu zote, ulikujaje kwa
huyu mkuu wetu wa upepeleziwakitengo.
Kwenye mkanda huo nilioutumiwa sehemu hiyo iliyoondolewa, iliongozewa
tukio jingine ambapo kuna mke na mume wanazozana, na mume akaondoka,na mke
akabakia akiwa kashika shavu, na maneno yakapita mbele ya uso wake,huku machozi
yakimtoka na alionyesha uso wa kusikitika, na mbeleya uso wake yakapita maneno
yameandikwa ,hujafa hujaumbika,
Haya maneno nilikuja kugundua kuwa yana siri kubwa sana
ndani yake, na ndio uliokuwa ufunguo, wa kuniwezesha kuyagundua haya, na ndipo
nikapanga niende nikakutane na Docta mama mwenyewe, huko Kenya,na huko
niligundua mengi na hata kumpata
muhusika mkuu, ….’akatulia kwa muda mpaka nikashindwa kuvumilia na kusema;.
‘Ina maana huyo muhusika mkuu ndiye muuaji wa Kimwana?’
nikauliza na yeye akaniangalia kwa uso unoonyesha tafakari, uso unaoonyesha huzuni,
alikuwa ananiangalia lakini ilionyesha wazi kuwa ingawaje macho yananiangalii
mimi, lakini mawazo yake yalikuwa mbalii , ….halafau akabenua mdomo, na
kutabasamu……halafu akasema;
‘Hujafa hujaumbika….’
NB: Samahanini, mtaona kama nzunguka hapo hapo, lakini
ndivyoo kisakilivyonifikia, na kama nitakwenda moja kwa moja, yatabakia maswali
mengi….hapa najaribu kudadavua mbinu za
kipelelezi.
WAZO LA LEO:Ulimi ni mwepesi sana kunena,na likitoka neno
sio rahisi tena kulirejesha, tujaribu kuwa makini katika yale tunayotaka
kusema,….na ajabu iliyoje, watu ni wepesi kuongea,kuliko kutenda, na hili
likanikumbusha methali moja isemayo, ada ya mja ni hunena, muungwana ni vitendo
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Nje kidogo ya topiki!.....NIPO Kijiweni hapa AISEE Ambiere!Usione kimya... SI KIMYA kina MSHINDO?@M3
Hamna shida mkuu,najua majukumu yalivyo, tupo pamoja AMBIERE!
Post a Comment