Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, June 11, 2012

Hujafa hujaumbika-49-Hitimisho-7
 ‘Siku ile ya tukio, kama ilivyojulikana shabaha ilikuwa kuuliwa mimi, na aliyepewa kazi hiyo ya kuniua mimi ni dereve wa Kimwana,ambaye alipokea taarifa hiyo toka kwa bosi wake,…hapa kwanza tutajiuliza bosi wake huyo alikuwa ni nani, ….? Maana Kimwana ndiye anayejulikana kuwa ni bosi wake,…kumba kuna bosi mwingine mwenye mamlka zaidi ya Kimwana, ni Sokoti, au ninani, kazi kubwa hapa ni kumtafuta huyo bosi wa huyu dereva, nikaiweka kama kazi maalumu ya kufuatilia.

Lakini tukumbuke kuwa risasi iliyotoka kwenye bastola ya huyo dereva sio hiyo iliyomuua Kimwana, hili polisi wenyewe walikuja kulithibitisha, na baadaye tukagundua risasi ya iliyotoka kwenye bastola, ikiwa imezama kwenye mifuko ya cement,ambayo ndiyo iliyotoka kwenye bastola ya dereva,swali likaja risasi iliyomuua Kimwana ilitoka kwenye bunduki ipi,na hili…lilikuja kunipa ufumbuzi Fulani tutauona baadaye

Na kweli polisi walipochunguza waligundua kuwa  ile risasi iliyokuwa ndani ya mwili wa Kimwana, haikuwa ya bastola, ilikuwa tofauti na risasi  ya bastola,  ile risasi ilitoka kwenye silaha kubwa, na hili lilikuja kugunduka baadaye baada ya mimi kugundua hiyo risasi iliyokuwa imetumbukia kwenye mfuko wa cement….swali likaja ,hii bunduki ilikuwa ikimilikiwa na nani,….

Kwahiyo kwa kipengele hicho ni kuwa muuaji alikuwa mbali na jengo, na polisi waligundua kuwa huyo muuaji atakuwa alikuwa kwenye jengo la pili yake, ambalo ni refu, na ukiwa pale unaona jengo hilo ambapo nilikuwa nimesimama mimi na Kimwana, na unamuona vyema mtu akiwa kasimama ndani ya kile chumba, lakini dirisha hilo lina kiyoo, chenye matundu ambayo yanaweza kupitisha risasi.Ukumbuke jingo hilo lilikuwa halijaanza kutumika.

Ina maana huyo muuaji, ana sifa kubwa ya kulenga shabaha, kwasababu ile risasi ilitakiwa kupenya kwenye moya ya matundu madogo yaliyokuwa kwenye hilo dirisha, na kwa umbali ule, alitakiwa mtu mwenye shabaha kali, ili isiweze kukosea, na kama angeliweza kukosea, kile kiyoo kingeliweza kusambaratika na kupiga ukulele ambao ungeliwashitua watu wengine,….

Ni hapo nikapata swali jingine, je , huyo muuaji alikuwa na lengo la kuniua mimi au Kimwana ?  maana kamanisingeliinama huenda hiyo risasi ingelinipata mimi,lakini ukichunguza kwa makini sehemu niliyokuwa nimesimama,hata kama nisingeliinama, angeliweza kumpiga Kimwana bila ya mimi kuzurika,…

Kwahiyo hapo Jibu lipo wazi kuwa huyo muuaji alikuwa na lengo la kumuua Kimwana,sio mimi,….kwahiyo kwa mtizamo huo huyo muuaji alikuwa na kisasi na Kimwana, sio mimi, tofauti na dereva ambaye alitakiwa kuniua mimi, ili nisije kuitoa siri, ambayo walijua nimeshaipta toka kwa Kimwana.

Je, huyo mlenga shabaha, alijua kuwa huyo dereve anataka kuniua mimi, na je alijuaje kuwa hiyo risasi itanikosa mimi. Hapo ndipo utagundua kuwa, lengo la huyo bosi, ilikuwa tuuliwe sote wawili, kwanza dereve aniue mimi, na wakati huohuo, huyo mlenga shabaha amuue Kimwana, …..

Hapo utagundua kuwa huyo mlenga shabaha, alikuwa ndiye huyo huyo bosi aliyekuwa akitoa amri kuwa dereva aniue mimi, alikuwa akiwaona wote toka jengo lile, na pale aliposimama, alikuwa akimuona dereve akilenga shabaha, na yeye akalenga shabaha yake hapo hapo,….

Ukiangalia hizo sifa utaanza kugundua jambo, kuwa huyo muuaji wa Kimwana, kuwa ana sifa ya kulenga shabaha, na pili ni bosi wa dereva, hata kama sio bosi, basi atakuwa na mafungamano na huyo dereva. Na ukumbuke kuwa hata baaada ya polisi kutumia mbinu mbalimbali,huyo dereva mpaka sasa hajaweza kukiri kuwa ni nani aliyemtumia huo ujumbe, inaonyesha dhahiri, hana uhakika, ni nanikati ya hawo mabosi wake….

Polisi walichunguza hiyo namba ya simu, wakagundua kuwa ni namba isiyo na jina,na haikuweza kufahamika ni nani aliyemtumia huo ujumbe na hata kumpigia hiyo simu, maana kuna ujumbe na simu, na je vyote hivyo viwili vilitoka kwa mtu mmoja…..!

Huyo dereva alidai kuwa yeye anapigiwa simu za namna hiyo na watu wengi, hasa inapofikia hatua ya kufanya jambo kubwa kama hilo na wapigaji hawajiweki wazi, lakini kwa siku ile alijua kuwa imetoka kwa Sokoti,…lakini baadaya tukio aligundua kuwa sio yeye, …sasa alikuwa nani mwingine, polisi wanasema walijaribu kila njia ili aweze kumjua huyomtu mwingine, lakini hakuweza, huenda anamficha,….nahata walipomuuliza kuwa huyo aliyepiga simu alikuwa mke au mume, alisema,suti likuwa kama mtu aliyefunika mdomo, huwezi kuitambua ila ilikuwa besi nzitoo la kiume au lakike lakuigiza,…

‘Sauti livyosikika ilikuwa huwezi kujua ni ya kike au ni ya kiume, ina maana mpigaji aliweka kitu mdomoni, hata hivyo polisi walisema kwenye maelezo yao kuwa huyu jamaa inaonekana alikuwa akidanganya, …..kwa uchunguzi wangu, alikuwa hadanganyi, hakuwa an uhakika kabisa aliyempigia ni nani….

Mpaka hapo tutakuwa na mambo ya kuunganisha ilikumpata huyo muuaji, kwanza awe na shabaha ya kulenga kwa mbali kwa kutumia bunduki, pili awe ni bosi wa huyo dereva,tatu awe pesa, na zaidi awena nakisasi na huyo binti, …nasema awe nazo, maana alimuahidi kumlipa huyo dereva pesa nyingi,na zaidi awe ni mtu muhimu wa huyo dereva, maana hata mbinu zilipotumika kwa huyo dereva ili kumtaja ni nani, haikusaidia kitu.Polisi wakihisi anajua jambo, lakini sio kweli…wengi ndani ya kundi hilo walikuwa hawajui nini kinaendelea nyuma ya pazia.

Tulifuatilia maisha ya Sokoti, katika ulengaji wa shabaha, tukakuta kuwa sio mtaalamu sana wa kulenga shabaha, kwahiyo sifa mojawapo hapo hana, lakini ana sifa kubwa kuwa ni bosi wa huyo dereva, na ni bosi wemye mamlaka, akitoa amri hutekelezwa.

Docta mama ndiye bosi tunayemjua toka awali hata Sokoti alikuwa nyuma yake,je alikuwa akiweza kutoa amri kwa huyu dereva,….lakini swali  jingine likaja hapo  nidocta mama yupi, ukumbuke docta mama kwenye kundi hili wapo  watatu. Wa kwanza ni mke wa wakili wetu mkuu wa kitengo, wa pili ni Yule mchumba wa Msomali wa kijijini na watatu hajulikani sana, lakini yupo ambaye alishika nafsi hiyo baada ya binti wa kijijini kuaga kuwa anakwenda Kenya.

Je kati ya hawa ni nani anasifa hizo hapo juu, hakuna kumbukumbu za kipolisi zilizothibitisha kuwa hawo akina mama, kama wanavyoitwa kuwa wanajua kulenga shabaha, licha ya kuwa wanasifa za ubosi.
Lakini hebu turejee nyuma, kipindi mauaji haya yanatokea, je,ni nani kati ya hawo watatu alikuwa ndiye kashikili nafasi ya udocta-mama? Hili tutakuja kulijua baadaye, …….

Polisi walifikia hatua wakagonga ukuta, na wakawa kama wanapoteza muda tu, huku wakisema mauaji hayo ni yakulipiza kisasi, na ni wao wenyewe kwa wenyewe, haina haja ya kuhangaika sana. Kwangu mimi ilikuwa ni changamoto. Niliingiwa na hamu ya kumjua ni nani hasa muuajii wa Kimwana na alikuwa an lengo gani hasa,na ukumbuke nilikuwa namtetea Msomali ambaye alijikuta akiingia matatani kila hatua.

********

Kwangu mimi ilikuwa  ni changamoto, sikukubali kushindwa, nilikuwa na hamu sana ya kumpata muuaji, na kwa uchunguzi wa mwanzo,nilikuwa nimeshajua sifa ambazo nikizifuatilia nitampata huyo muuaji,. …nikaanza kuwa karibu na kila aliyeshukiwa, na kuchunguza historia zao kiundani. Ilikuwa sio kazi rahisi mtu kukuambai undani wake, lakini hatau kwa hatua iliwezekana.

Mimi katika kisa hiki niliweka sifa kubwa ya tukio kuwa ni tukio lililogubikwa na maisha ya ndoa,kwa hiyo 
kwangu kila muhusika nilimuangalia katika mfumo huo. Nikadadisi mahusiano yake na mwenzake,….na kila niliyemuhoji, nikakuta ana matatizo yanayofanana, ….angalai wahusika wote kwenye kundi, wana matatizo kamahayo,……lakini lengo langu kubwa lilikuwa kwa wahusika wakuu,….wakili wetu muu, Sokoti , …na mamaDocta, lakini mama Docta anafungamana na mumewe,…na isingelikuwa rahisi kwa mume wake kuniambia lolote…nikatafuta upenyo kwa kupitia kwa Yule binti yao,ambaye anawajua sana.

Sokoti, ana matatizo ya kusalitiwa na mchumba wake, na Kimwana ni mmojawapo, lakini pia Kimwana alikuwa msaliti wake katika shughuli zao, kwahiyo huyu ana kuwa mshukiwa mkubwa sana. Lakini hana sifa ya kulenga shabaha, na pia tulipomdadidi sana huyo dereva, alisema kuwa yeye alikuwa mra zote anafuta amri kutoka kwa docta mama.

‘Ina maana kama Sokoti angekuambia kuwa anataka kufnay jambo lolote ili akulipe ungalifanya ?’ tulimuuliza.

‘Kwa yoyote, kama ataniahidi pesanyingi ningelifanya, lakini naangalia na usalama wangu, je nitalindwa vipi,….Sokoti angeliweza kunilinda, kwasababu ya wakili wetu wa kundi, lakini wakili wa kundi alishaanza kuingiwa wasiwasi na  kundi,….’

‘Kwanini,….?’ Nikamuuliza.

‘Kwasababu yeye alikuwepo hapo kwa ajili ya Docta mama, na Docta mama akawa kajitoa kwenye hilo kundi…..?

‘Unamzungumizia Docta mama yupi?’ nikamuuliza huyo jamaa, akaniuliza kwa mshangao.

‘Kwani Docta mama wapo wangapi,mimi namjua mmoja tu ,sijui kama kuna docta mama mwingine….’akasema huyo dereva,na hapo nikajua kuwa siri ya docta mama tulikuja kuigundua sisi wenyewe, lakini wengi ndani ya kundi hilo hawakujua mchezo uliokuwa ukitendeka humo ndani ya kundi.

Docta mama walikuwa watatu, na hata polisi walikuja kugundua hili baada ya mimi kuwafahamisha hilo, nilipowaletea picha za hawo madoctamama, ilikuwa vigumu kuligundua hilo na ilikuwa kama mshangao, maana sura , maumbile na tabia za hawa akina mama watatu zinafanana kwa karibu sana,….lakini katika maisha halisi hawakuonekana kuwa karibu ,yaani kila mmoja alikuwa kama hamjui mwingine.

‘Polisi hawakuwa na haja sana na hawa kina mama, wao walikuwa wanangaika kumpata wakili wetu mkuu, na Sokoti ambao hawaonekani, na kwao wao hawo ndio muhimu sana….

Kwangu nilishaanza kugundua siri kubwa ya hilo kundi, lakini kama ningeliropoka kwamuda ule, maisha yangu yangelikuwa hatarani, kwani miongoni mwetu, kulikuwa na watu wanaotumiwa na hilo kundi, nasikuweza kuwajua ni akina nani, nilisubiri wakati muafaka wa kuliweka hilo hadharani,na hata hivyo kwawkati kamahuo, hata kamaningeliwaambai polisi hawangeniamini, ….

*******

Siri ya kundi ilianza kuvuja pale nilipokutana na wakili wao wa kundi, kipindi anapambana na mimi kwenye ulingo wa mahakama. Alipoona kuwa haelewani na kundi na mama docta keshaondoka, akaamua kujitoa, alipewa masharti kuwa kama anataka usalama wake aondoke nchini, na utaratibu ukafanywa kuwa  anakwenda kusoma. Ni  kweli alikwenda kusoma, lakini haikuwa ni lengo lake la karibu, hilo lilikuja kwa shinikizo la hilo kundi,wakamlipia kila kitu akaondoka.

Siku anaondoka, akaniachia ujumbe mfupi kwenye simu yangu,…., kuwa mama Docta hayupo kwenye kundi tena, ila kuna mtu mwingine ameshika nafasi yake, na kila kitu kimebakia kama vile mama Docta yupo, kwahiyo tuwe makini na hilo. Nilihangaika sana kupata maelezo yake, lakini sikuweza kumpata.

Nilipogundua kuwa mama docta hayupo, na kwa taarifa zilizokuwepo kwenye kundi ni kuwa mama docta karudi kwao Kenya, nikawa nhangaika kujua huyo mama docta aliyekuwa kwenye hilo kundi ni nani, kwakweli ilikuwa ni vigumu sana kumpata, na hata nilipofika kwenye darasa lao sikuruhusiwa kuingia, na hata niliposubiri nimuone akitoka kwa siri,sikuweza kumuona, hakuwa rahisi…..sikujali sana kwa muda huo,…..

Mungu ni mkubwa, nikapata mzigo, ulikuwa nimkanda ule uliokuwa ukionyesha yale aliyofanya wakili wetu mkuu,nilipoupata na maelekezo kuwa niufanyie kazi, sikuelewa kuna nini nikifanye kazi, nikawa sihangaiki nao sana, hadi pale nilipokwenda kuonana na yule binti anayeishi kwa wakili wetu mkuu,pale nikafunguka macho. Katika maelezo yake aliniambia kuwa kuna dada mmoja huwa alikuja mara mbili, wanafanana sana na mke wa wakili wetu mkuu…..!

Siku ile nilipoingia ndani ya kupekua chumba cha wakili wetu mkuu, nilikuta mkanda kama ule niliotumiwa upo pale ndani, na ule mkanda nilioukuta pale ulikuwa haujafanyiwa uchakachuajia, nikagundua kitu, kuna sehemu kubwa ilikuwa imeondolewa katika mkanda niliotumiwa, seehmuhiyo niliikuta kwenye mkanda huo uliokuwa humo ndani,…sehemu hii niliyoikuta humo, ilionyesha Kimwana anasikiliza simu, na kwenye na ilionyesha dhahiri kuwa anapokea maelekezo Fulani, kwani aliuliza

‘Tayari yupo chumbani nifanye nini,….?’akatulia na alionyesha kukunja uso, halafu akapiga piga miguu chini, akasema;

‘Mimi naogopa, huyu ni mtu wa serikali, mimi nitaishije hapa mjini…’akatulia na kusikiliza.

‘Sawa, lolote likitokea tusija kulaumiana,….’halafu akatulia na ilionyesha mpigaji keshamaliza, akasimama kwa muda na mara mlio wa simu nyingine ukalia, akapokea na kusema kwa unyenyekevu.

‘Ndio Docta mama, lakini bosi kaniambia nifanye kweli….’akasema.

‘Ndio wewe ndio bosi mkubwa, lakini…’baadaye akakata simu.

Kuna bosi na bosi mkuu,….na sehemu hiyo ikaja kuondolewa, kwanini ikaondolewa kwenye mkanda niliotumiwa, na inaonyesha wazi aliyenitumia hakutaka sehemu hiyo niione, na huu mkanda wenye sehemu zote, ulikujaje kwa huyu mkuu wetu wa upepeleziwakitengo.

Kwenye mkanda huo nilioutumiwa sehemu hiyo iliyoondolewa, iliongozewa tukio jingine ambapo kuna mke na mume wanazozana, na mume akaondoka,na mke akabakia akiwa kashika shavu, na maneno yakapita mbele ya uso wake,huku machozi yakimtoka na alionyesha uso wa kusikitika, na mbeleya uso wake yakapita maneno yameandikwa ,hujafa hujaumbika,

Haya maneno nilikuja kugundua kuwa yana siri kubwa sana ndani yake, na ndio uliokuwa ufunguo, wa kuniwezesha kuyagundua haya, na ndipo nikapanga niende nikakutane na Docta mama mwenyewe, huko Kenya,na huko niligundua mengi  na hata kumpata muhusika mkuu, ….’akatulia kwa muda mpaka nikashindwa kuvumilia na kusema;.

‘Ina maana huyo muhusika mkuu ndiye muuaji wa Kimwana?’ nikauliza na yeye akaniangalia kwa uso unoonyesha tafakari, uso unaoonyesha huzuni, alikuwa ananiangalia lakini ilionyesha wazi kuwa ingawaje macho yananiangalii mimi, lakini mawazo yake yalikuwa mbalii , ….halafau akabenua mdomo, na kutabasamu……halafu akasema;

‘Hujafa hujaumbika….’

NB: Samahanini, mtaona kama nzunguka hapo hapo, lakini ndivyoo kisakilivyonifikia, na kama nitakwenda moja kwa moja, yatabakia maswali mengi….hapa najaribu  kudadavua mbinu za kipelelezi.

WAZO LA LEO:Ulimi ni mwepesi sana kunena,na likitoka neno sio rahisi tena kulirejesha, tujaribu kuwa makini katika yale tunayotaka kusema,….na ajabu iliyoje, watu ni wepesi kuongea,kuliko kutenda, na hili likanikumbusha methali moja isemayo, ada ya mja ni hunena, muungwana ni vitendo


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Simon Kitururu said...

Nje kidogo ya topiki!.....NIPO Kijiweni hapa AISEE Ambiere!Usione kimya... SI KIMYA kina MSHINDO?@M3

emu-three said...

Hamna shida mkuu,najua majukumu yalivyo, tupo pamoja AMBIERE!