Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, May 10, 2012

Hujafa hujaumbika-34



‘Nilikuwa natoka kazini, nilichelewa kutoka na wenzangu wote walishandoka, na hata mlinzi alikuwa hayupo, aliniomba kuwa anakwenda kununua chochote kwa ajili ya chakula chake cha usiku , na nilipoona anachelewa, nikatoka nje kumwangalia, sikumuona kwa muda huo, nikaona nisirudi tena ndani, nikamsubiri hapo hapo nje, nikiwa nimeegemea gari langu….’akatulia kidogo akimuchia nafasi yule askari usalama amalize kuandika maelezo yake.

‘Mhh, halafu ikawaje…?’ akauliza yule askari mpelelezi.

‘Mara pikipiki mbili zikaja kwa mwendo wa kasi, …niliziona zikija kwa nje,maana pale nilipokuwa niliweza kuona sehemu kubwa ya nje, hasa barabarani….nilijua zinapita lakini mara zikaingia kwa kupitia kweney geti letu….’akasema na kutulia na yule askari kanzu akauliza.

‘Ina maana geti lilikuw awazi?’

‘Geti nilifungua mimi,  nililifungua ili mlinzi akija nisipoteze muda, kumbe ndio niliwapa nafasi ya hawo wenye pikipiki kuingia bila shida. Sijui walijuaje kuwa lipo wazi, au ndio walibahatisha tu, kwani walichofanya, ni hivi, Yule mwendesha pikipiki wa mwanzoni aliusukuma ule mlango wa getini , huku akiwa anaendesha, na kwa vile geti lilikuwa kama limefungwa, lakini niliegesha, tu, akasukuma kwa pikipiki na mguu, ….na kuingia moja kwa moja,na huyo wa pili akafuatia kwa nyuma na wote wakaja usawa ule niliposimama….

‘Hawa kusimamisha mapikipiki yao…?’ akauliza huyo mtu wa usalama.

‘Walikuja uswa wangu, wakanipita na kuanza kunizunguka, huku wakiyavurumisha kwa sauti, wakawa wananizunguka na pikipiki yao, kama mara mbili, halafu,  mara wote wakasimama,…’akatuli ahapo kidogo.

‘Haya ikawaje …?’ akauliza huyo askari .

‘Huwa mara nyingi najihami, hasa nikiona kitu ambacho sio cha kawaida, ….harufu, au vumbi, ….nina mafuta yangu najipaka puani, nimezoea kufanya hivyo, …sijui kwanini,….na waakti wanakuja, nilikuwa anjipata hayo mafuta, najipaka, na walipokuwa wakiyavurumisha mahonda yao kwa sauti ya kutoa moshi, nikajpaka yale mafuta kwa wingi puani,…..

‘Ni mafuta gani hayo…?’ akauliza huyo askari.

‘Unajau mafuta hayo alinipa rafiki yangu mchina, aliniambia ukiyapaka puani , yanasaidia kujilinda na vitu vya kuambukiza, na kama una athirika na mavumbi au harufu au una `alegi’ na vitu kama hivyo, basi ukijipaka hayo mafuta, hutaweza kuathirika , na pia hata kama mtu kakupulizia madawa ambayo yanalewesha na kutia usingizi, ….mafuta hayo huweza kukulinda ,hutaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa.

Hawa waendesha pikipiki,walisimama, na kabla sijawauliza nini lengo lao wakanivamia, na mimi sikukubali kirahisi nikapambana nao, ilikuwa karibu niwashinde, lakini huyo mmoja ndio akatoa leso ambayo nahisi ilikuwa na madawa ya kulevya, ….akanishikisha puani,….sikuwa nimemuona,kamaningemuona nisingelipa hiyo nafasi.

Niliingiwa na kiza na  kupoteza fahamu…na nilipozindukana baadaye kidogo, nikajikuta nipo ndani ya gari wamenilaza kiti cha nyuma, na mbele kwa dereva yupo dereva mwenyewe, pandikiza la baba na pembeni yake yupo mwanamke. Huyu mwanamke alikuwa kavaa wigi lenye nywele ndefu kidogo. Na alipogeuka kuniangalia kwa nyuma, karibu anifume,…niliona kuwa kavaa mawani makubwa meusi.

‘Endesha haraka kidogo maana asije akaindukana huyu mtu, kabla hatujafika….’nikasikia akimwambia dereva wake.

‘Itakuwa maajabu kama atazindukana haraka hivyo…’akasema huyo dereva.

‘Wewe endesha haraka, huwezi jua huenda hayakumuingia vyema, ni vyema kujihami….’akasema huyo mwanadada.

Nilijaribu kutizama wapi tunaelekea ,lakini kwa pale walivyonilaza ilikuwa ni vigumukuinua kichwa bila kuonekana , na sikutaka kabisa wanijue kuwa nipo macho, nikatulia tu, ….

‘Kwahiyo twende wapi bosi wangu,…tunaelekea  kwako au kule kwenye jengo jipya…?’ akauliza yule dereva.

‘Kwenye jengo jipya, kwangu kuna wageni…’akasema huyo mwanamama.

‘Na wewe kwa wageni …..hakuna siku niliwahi kuja kwako nisikukute na wageni, halafu wengi wanatoka nje,…..dili zako kali bosi…’akasema huyo dereva.

‘Umeanza kuwa askari kanzu, au ndio nyie mnatoa siri za watu….chunga sana mdomo wako, ….utakuwa chakula cha mchwa sasa hivi….’akasema huyo mwanamke.

‘Ndio yamekuwa hayo bosi,…nilikuwa nakutania tu…..samhani sana bosi niwie radhi….’akasema huyo derive na kweli alionyesha kuogopa.

‘Kukuwia radhi kwangu ni wewe kutuliza huo mdomo wako, na la sivyo tunajua jinsi gani ya kuutuliza, haya endesha na ukae kimiya, unanitia kichefuchefu nikisia sauti yako….’akasema huyo mwanamke.

‘Sawa bosi, …nimenyamaza…’akasema na kuonyesh amkono wake mdomoni kuwa kaufunga.

*******
Mara gari likasimama na mlango wa gari ukafungulia na mimi nikavutwa kama gunia, hawakunijali, wakanibeba hadi ndani ya nyumba hiyo, ilikuwa mpya, maana harufu za rangi ya nyumba nilizihisi.

Yale mafuta yalinisaidia sana, vinginevyo ningelikuwa bado sijazindukana, kwani hayo mafuta niliyopaka puani, yanapunguza ukali wa madawa kama hayo na wao walijua kuwa sitazindukana kwa muda, mrefu. Nikajifanya bado nimelala, nikajilegeza kweli kweli, huku naangaza huku na kule kwa kujiiba, ili kujua wapi nilipo.

‘Hakikisheni kuna ulinzi wa kutosha na akizindukana niiteni haraka, kuna jambo nataka kujua kutoka kwakwe kabla zoezi la kummaliza halijafanyika…’akasema huyo mwanamama na kuondoka zake.

Hawakunifunga kamba, kwahiyo nilipohakikisha kuwa hawapo, nikainuka na kwenda maeneo ya dirishani , hapo nilitizama kwa nje, kama ninaweza kugundua wapi hapo tulipo, …kulikuwa kimiya kabisa, na kwa mbali nikaona jengo moja refu, na kubhatisha kuona maandishi, yalikuwa na neno `Mbezi…’….nikajua nipo maeneo ya Mbezi,hata jinsi kulivyo kwa nje inaonyesha kabsa kuwa tupo Mbezi.

Mara ghfla mlango ukafunguliwa, na hapo sikuwa na jinsi, akanikuta huyo jamaa nikiwa nimesimama. Yule jamaa akaningalia kwa mshangao, akatabasamu na kusema;

‘Mhh, umeshaamuka ,duuuh, nimekukosa, maana nilitaka nikuwahi ukiwa bado umelala, lakini sasa upo macho….unasemaje, nataka tustarehe kidogo….’akasema huyo jamaa.

‘Wewe kweli umechanganyikiwa , nyie ndio mnaobaka maiti…hivi nani anaweza kustareeh na mtu kama wewe, watu ambao mnatawaliwa na huyo mwanamke, kwanini usiende kustarehe nay eye…’nikasema kwa nyodo.

‘Mhh, unajifanya mgumu, nitakulainisha tu na baadaye utafurahia hichoo nitakachokufanyia,…wenzako wananitafuta, ..mmh, hata hivyo wee dada kwakweli mrembo , sitaweza kuvumilia kuacha uwawe bila ya kukugusa, ….nitasikitika sana wakikumaliza, kabla,… lakini sikubali, mpaka nihakikishe kuwa nimekupata…au upo tayari kutooa ushirikiano….?’akasema huku akinisogelea.

‘Tafadahli….nikamunyoshea kidole kumkanya, yeye hakujali akaanza kunishika shika….
Sikuweza kumpa nafasi hiyo, nikamrukia kwa kigoti, goti likagonga kati kati ya sehemu zake za siri, akainama huku akilalamika kwa maumivu na kabla hajaweza kuinama  vyema, akapata kipigo cha goti jingine kwenye uso, na nilijua kabisa limegonga puani,…. akalala chini, alipojaribu kuinuka nikamuwahi, akaserereka na kugonga ukutani, aliguna, na kwa haraka akageuka, akijua sasa anapambana na mtu, sivyo kama alivyofikiria na kuzarau kuwa ni mwanamke tu….

‘Kumbe wamo, sasa umejitakia nitahakikisha unalegea….’akasemahuku akigeuka kunivamia,name nikaona sasa wewe hujanijua, nikageuza teke la kinyume nyume, akutana nalo, na kutua usoni. Nashukuru sana mafunzo ya karate niliyopewa, maana kila pigo lilienda pale panapostahili na lilifanya kazi yake.

‘We….ooh, ….’akapiga ukulele…..na anilipotaka kumtwangwa teke jingine la kichwani ambalo kama lingelimpata najua kabisa angelipoteza fahamu,….nikasikia chuma kikigonga kichwani, na sauti ya mwisho kusikia ilisema;

‘Kwanini hamkumfunga kamba….mpigeni siandani , asije akazindukana kabla ya zoezi….’ilikuwa sauti ya mwanamke….

Sijui walinipiga na chuma gani kichwani,kwani maumivu makali yalitanda kichwani na giza likanifunika , na sikujitambau tena, hadi hapo nilipozindukana na kujikuta nipo  hapa hospitalini….’akamalizia kuelezea huyu mwanadada.

‘Unaweza kuhisi huyo mwanamke ni yule aliyekuwa katoroga rumande…?’ akauliza askari.

‘Siyo yeye….atakuwa mwanamke mwingine…’akasema mwanadada huyo wakili.

‘Na hawa wanaume waliokuwa wakishirikiana na y eye ukiwaona unaweza kuwatambua?’ akauliza askari.

‘Huyo mmoja niliyepambana naye naweza kumtambua, ila hawo wengine sio rahisi kwa jinsi ilivyokuwa. 
Sikubahatika kuoana sura zao vyema…’akasema huyo mwanadada wakili.

‘Huko Mbezi, unafikiri ni mbezi sehemu ipi..?’akauliza askari.

‘Sijawa na uhakika ni mbezi  ipi, ndio nataka nifanye uchunguzi,nitapagundua tu, maana lile jengo ni refu, na zisani kuwa ni sehemu ya ndani ndani kutoka barabara kuu, itakuwa akribu sana na barabara kuu…hilo nipeni muda, nitawapa jibu nikipagundua…’akasema huyo mwanadada.

‘Huoni kwa sasa hivi ni hatari kwako kuwafuatlia hawo watu,hiyo kazi tuachie wenyewe,…’akasema askari.

‘Nyie fanyeni kazi yenu, na mimi najua nini ninachokifanya….tusiingiliane….’akasema huyo mwanadada.

‘Kwa kibali gani, kuwa unamfanyia nani uchunguzi,maana ujue kuwa utakuwa unaingilia kazi ya askari, labda kama ungetuambia una mtu unamfanyia kazi kwa ajili ya kesi fulani, na umeshapata kibali, hapo tungelikusaidia na hata kukusindikiza, lakini sasa hiyo kesi ipo mikononi mwetu, haikuhusu…’akasema huyo askari.

‘Kwani tatizo hapo ni nini, kwasababu mwisho wa siku ni kwa manufaa yenu,..kesi hiyo inanihusu maana wamenigusa pabaya, ngoja niwaonyeshe kuwa na mimi najua mambo hayo….msijali , nitafuta taratibi zote kisheria….’akasema huyo mwanadada.

‘Tunachoogopa ni kuwa unaweza ukavuruga ushahidi na…..’akasema huyo askari na kabla hajamaliza huyo mwanadada akamdakia na kusema;.

‘Niombe tafadhali afande mimi nivuruge ushahidi,unazarau  kweli wewe,….mimi najau nini ninachokifanya, nyie fanyeni kazi yenu, na mimi niachieni nifanye kazi yangu, ninajua namfanyia nanihiyo kazi na siku ikifika mtajua..’akasema huyo mwanadada na kuniangalia pale niliposimama.

‘Twende zetu….’akaniambi na mimi nikamfuta nyuma.Yule mwanadada alitoka palekwa haraka ,na mii nilijichelewesaha nyuma kidogo, na nilipogeuza kichwa kuwaangalia wale maaskari nikawakuta wanatuangalia kwa makini, na mmojawapo akasema;

‘Fuata nyendo zao hawa watu…..’

******
‘Sasa tunakwenda Mbezi,….lakini kama upo tayari, usije ukasema nakulazimisha, kama una mishe mishe zako nenda,nitajitutumua mwenyewe’akasema na mimi nikamwangalia na kusema;

‘Hata kama ningelikuwa na hizo mishe mishe zangu,ningelizisahau kwa muda,…kwa jili yako, najua unachokifanya kitanisaida hata mimi’nikasema na yeye akatabasamu na kusema;

‘Sawa,  inabidi iwe hivyo, …wakati mwingine inabidi mtu ujitolee, hata kama hutapata kitu, maana kazi zetu hizi ni zina gharama, sio gharama ya pesa tu, zinagharimu hata maisha ya mtu…ndio maana watu wengi wanashindwa kuwa na mawakili,….sasa nakuhitaji kama mlinzi wangu, ila unifuate lhuko ninapokwenda,…mengine tutaongea baadaye, sawa ’akasema kama vile ananiuliza, namimi nikasema.

‘Sawa bosi..mheshimiwa wakili..’nikasema huku tukiwa ndani ya gari lake na nilipotizama kwa nyuma niliona pikipiki ikitufuata .

‘Nahisi kuna mtu anatufuatilia kwa nyuma..’nikasema huku nikiwa na wasiwasi.

‘Nimeshamuona, yule ni askari…usijali nilijua lazima watafanya hivyo, ….badala ya kuwatafuta wahalifu wananifuatilia mimi,…hata hivyo, ni vyema kwetu pia….’akasema.

Moyoni nilijiuliza huyu mwanamke anajiamini nini kiasi hiki, maana huko anapotaka twende nahisi sio sehemu ya kwenda bila askari, hawo ni majambazi wa kimataifa, lakini namshangaa huyu mwanamke hajali i, na isitoshe wale maaskari walihsmuonya kuhusu hilo, na walisema kabisa kama anataka kufanya uchunguzi anatakiwa afuate taratibu, sije akavunja sheria.

‘Hivi huoni kuwa tunakwenda kinyume cha sheria…hapa kweli hatutakuwa tumevunja sheria…?’ nikamuuliza.

‘Sheria ipi tumevunja….hebu niambia nimevunja sheria ipi?’akaniuliza.

‘Askari wamekuonya kuwa tatizo hilo sasa lipo mikononi mwao, usiliingilie, hiyo ni kazi yao, lakini …’na kabla sijamaliza akasema.

‘Sema sheria ipi niliyoenda kinyume nayo,nataka kupajua hapo,.. ?’ akauliza na kunitupi jicho mara moja, halafu aliponiona nipo kimiya, akasema;

‘Nilifikiri unajua baadhi ya mistari ya sheria, …ooh, au unajua ukiongelea mamboya sheria, najua nipo namtu anayeijua,…hata hivyo hebu niambie kazi gani ya kwao nimeiingilia,….?’ Akatulia na kunigeuzia kichwa kuniangalia na alipoona nipo kimiya tena akasema;

‘Naona hujui lolote hapo, ….ulikuwa unakisia kwa uwoga tu,…au sio, usiogope,…hasa ukiwa unatafuta ukweli kwa nia njama, fanya jambo kwa kujiamini,…wao mwisho wa siku watakuja kukusifia, kwasasa lazima wakihami, lakini hawajui nini ninakitafuta ambacho pia ni kwa maslahi yao,…’akatulia huku akiendesha gari kwa makini.

‘Nawezanisjue vifungu vya sheria, lakini najua kuwa tendo fulani ukifanay utakuwa umevunja sheria…’nikajitetea.

‘Unatakiwa uwe makini hasa unapo-ongea neno `kuvunja sheri’….mimi sijavunja sheria, …wewe tuliatu, najua nini ninachokifanya….’akasema huku akiendesha gari ka mwendo wa kasi kidogo, hakuelekea moja kwa moja njia ya Mbezi, tulikwenda kwanza maeneo mengine tukapata supu.

‘Unamuona yule jamaa aliyeshika chupa ya soda, yule ni askari, anatufuatilia sasa mimi naenda chumba cha kunawa, wewe malizia hapa na baadaye toka uchukue boda boda hadi Mwenge, utanikuta huko….’akaniambia na mimi sikukaidi.

Nilisubiri baada ya kumaliza supu, baadaye niakinuka, na yule askari akawa ananiangalia kwa mashaka, maana hakumuoan yule mwanadada pale mezani, na aliniona nikiondoka peke yangu, akainuka haraka na kueleeka chooni, najua atakuwa anakagua chumba cah wanawake.

Mimi nikatoka na kuchukua boda boda, …hadi Mwenge , sikuweza kumuona huyo askari tena. Nilipofika Mwenge nikageuka kuangalia wapi huyu mwanadada yupo mara nisikia honi ya gari ikilia nyuma yangu, nilipogeuka nikaona nii gari  la yule mwanadada.

‘Sasa sikiliza hili gari naenda kuliacha kwa rafiki yangu, tutatumia pikipiki, siunajua kuendesha pikipiki….?’ Akaniuliza.

‘Najua …lakini sina leseni….’nikasema.

‘Usijali…..’akasema na tukaondoka hapo hadi hapo aanposema ni kwa rafiki yake, nilibakia nje wakati yeye anaongea na rafiki yake na baadaye tukakabidhiwa pikipiki, na mimi nikaendesha hadi huko maeneo ya Mbezi.

‘Eneo lenyewe unalijua?’ nikauliza.

‘Nimeshalijua, na nimeshafika ….’akasema

‘Ulifika lini..?’ nikauliza.

‘Usitake kujua mengi, mengine ni kazi yangu…..’akasema kwa sauti nzito.

‘Unaonekana kama askari, ulijifunzia wapi hiyo kazi….?’ Nikauliza.

‘Unapokuwa wakili unatakiwa ujue uaskari, …uwe mkakamavu, ….’ Akasema.

‘Lakini wewe ni mwanamke…huoni kuwa….’nikataka kusema kitu, yeye akanikataiza na kusema.

‘Wewe endesha, nipe muda kuna kitu nakiwaza kwanza….tafadhali…’aaksema na mimi nikamuelewa, na tuliendesha hadi eneo alilonielekeza.

‘Sasa tutaiacha hii pikipiki, kwa rafiki yangu mmoja, huko kweney hilo jingo tunakwenda kwa mguu, hatutakiwi kujulikana, na uwe mwangalifu, hukotunakokwenda huenda tukapambana na watu weney silaha, …lakini kwa vile ni mchana, sizani kama wanaweza kutumia silaha,…najua silaha yaoo kubwa na madawa ya kunusisha puani au sindani za madawa ya kulevya….’akaniambia.

‘Usijali mimi najiamni,….’nikasema na huku nikiwaza huko tunakokwenda tuankwenda kufanya nini,lakini sikutaka kuuliza swali, tukaanza kutembea,ilikuwamawndo kidpgo na baadaye tukafike kwenye jengo,.

‘Jengo lenyewe ndilo hilo hapo, lakini hatutakiwi kuonekana, na cha kufanay sasa hivi ni kusubiri hapa tulipo, huku tukiangalia nani ataingia hapo, nina uhakika kuna mtu muhimu atakuja hapo, kama uchunguzi wangu wa jana hautakwua na makosa….’akasema.

Tulikaa pale kwa muda mrefu, mpaka subira ikaniishia nilalamika na kusema mbona hakna kitu na tunapoteza muda wetu hapo bure, yeye akasema subira huvuta heri tuendelee kusubiri,….

Baadaye sana likaja gari na kusimama pale kwenye lile jengo, ilikuwa taksi, na ile taksi ikaondoka na kumuacha mwanadada mmoja,…Yule mwanadada hakuingia ndani ya lile jengo moja kwa moja, alikwenda hadi kwenye genge lililopo karibu akawa ananunua vitu, na baadaye akaoka na kusimama mbali na jengo, akawa anaangalia huku na kule.

Kama vile anasubiri gari pale,na akawa anatembea taratibu, na baadaye kwa haraka, akaelekea kwenye mlango wa ile nyumba, akasukuma mlango wagetini, na kutokomea huko ndani. Nikamwangalia bosi wangu kuwa atasemaje.

‘Sasa wakati umefika,….kwa jinsi nilivyoona yupo peke yake…sijui kwa huko ndani,sasa, nataka nikupe onyo, tukifika hapo wewe nenda pale getini, ongea na hawo walinzi, hakikisha unaongea nawo kwa muda,….na kama atakuja mtu mwingine, au hawo walinzi wataamua kuingia ndani niashirie kwa kubipu simu yako, mimi mengine niachie mwenyewe….’akasema.

‘Ina maana unataka kwenda kukabiliana na huyo mwanadada peke yako, je kama kuna walinzi ndani itakuwaje….?’ Akauliza.

‘Fanya nilivyokuelekeza…’akasema na mimi nikafanay hivyo.
Wale walinzi walikuwa mbogo, walianiambai hawataki mtu hapo, lakini nikatumia lugha ya kijiweni na kuonge hili na lile mpaka tukaivana, mimi niliwaambia kuwa mwenye jengo hilo ni rafiki yangu wa kike na nataka kuonana naye.

‘Hajatuambia kitu kama hicho,kwanza nani kakuambia kuwa mwenye jengo hili ni mwanamke…?’ akauliza.

‘Nyinyi mnanishangaza kweli, nimeshawaambi kuwa huyo mwanamke ni rafiki yangu, halafu mnauliza nimejuaje….nimejua kwasababu nipo karibu naye, nyie subirini muone akitoka atasema nini, mtaona wenyewe….’nikasema..

‘Sasa sisi haturuhusiwi kabisa mtu kusimama hapa getini,kama unamuhitaji nenda kasimame kule, akitoka utakuja kuonana naye…’akasema huyo askari.

‘Nyinyi si mnataka kuhakikisha kuwa mimi ni rafiki yake au sio,subirini kidogoo, akitoka  mtaona wenyewe,na kama mnabisha ngojeni nikamwambie kuwa nyie vibarua wake mumenizuia, tuone kama hamtafukuzwa kazi wote nyie, mnafanya mchezo eheeh.’nikasema na wao wakaniangalia kwa mashaka na hiyo ilisaidia wakatulia bila kusema neno..

Baadaye kidogo,mlango wa ile nyumba ukafunguliwa na aliyetoka pale ni jamaa kavalia kofia kubwa, alitoka kwa haraka huku akionyesha wasiwasi mkubwa, akaja pale getini na kuwapita walinzi hata bila ya kutoa salamu, na mimi nikashituka. Huyo jamaa aligeuza kichwa na kuniangalia,…nikamkumbuka …ni mmoja wa wale waliokuwa wamembeba huyo wakili mwanadada kule kwenye lile jengo jipya la ghorofa wakiwa na lengo la kumuacha pale adondoke.

‘Huyu ni nani,….alipitia wapi, au ndiye anayekula mpenzi wangu…?’ nikauliza alipoondoka.

‘Hayo ya hapa hayakuhusu, kwanini hukumuuliza mwenyewe alipokuwa hapa…..?’ na kabla sijawajibu, mara simu yangu ikaingia meseji,inasema niende kule tulipoacha pikipiki haraka….nikageuka na kuwaangalia wale walinzi, na baadaye nikasema;

‘Mbona huyu mwanadada hatoki….?’ Nikauliza.

‘Wewe siumedai kuwa unataka kumsubiri, msubiri,…sisi hilo halituhusu hata akikaa humo hadi usiku, ni kwake, sisi tuna wasiwasi gani, labda tusikie kelele za kuumizana, tunaweza tukaenda kusaidia,…hata hivyo sisi hapatumepewaakzi ya kulinda nje, sio huko ndani…’akasema huyu askari.

‘Sawa nimeshindwa mimi,..kazi njema…’nikasema na wao wakacheka na kusema;

‘Yatakushinda,….mwanamke hafuatiliwii kihivyo…pole sana,lakini angalia ukifanya hivyo utakuja kuumia mwenyewe,….’akasema mmoja wapo.
Nikaondoka hadi kule tulipoweka pikipiki, na kumkuta yule mwanadada wakili akiwa katulia huku akionyesha kuwa na mawazo mengi.

‘Imekuwaje?’ nikauliza.

‘Balaa….ukisikia wakili akisema kuna balaa ujue kweli ni balaa….’akasema huku akingalia saa yake.

‘Mungu wangu balaa gani hiyo, maana sikukuona ukiingia wala kutoka kwenye hilo jengo…’nakuliza.

‘Haitakiwi ujue hayo, hebu nikuulize, hukuona mtu akitoka mlangoni wakati upo getini?’ akaniuliza.

‘Ndio alitoka mwanaume mmoja,akiwa kava kofia pana…’nikasema.

‘Huyo ndiye muuaji…’akasema huyo mwanadada wakili.

‘Ndiye muuaji…..!’ nikashangaa, halafu nikauliza kwa haraka. `Muuaji…,kwavipi..?’nikauliza.

‘Kwa nyuma kule kuna sehemu nilishaiona ya kuweza kuruka na kuingia ndani, na ukiingia ndani, kuna ngazi kwa nyumba ya jengo, walikuwa wanaitumia mafundi kwa kupaka rangi. Niliitumia hiyo ngazi, maana kuna sehemu kwa juu badi ipo wazi, unaweza kupenya hadi ndani…ndio wameanza kuiziba hiyo sehemu, haijakamilika, na ndipo nilipotumia kuingia ndani.

‘Ukamkuta huyo mwanadada…..?’nikauliza.

‘Nilimkuta, …hakuamini na hakujua jinsi nilivyoingia, alitaka kupiga ukulele…, nikamtuliza kiaina, …alisema yeye  hataki kuongea na mtu, ndio maana kaja pale kujificha, …’akatulia na kuniangalia.

‘Alikuwa peke yake?’ nikamuuliza.

‘Kwenye maongezi alisema ana mlinzi wake, na hakutaka kusema huyo mlinzi yupo wapi,….na nikambana kwa maswali, mapaka akalainika, na kuanza kukiri kuwa hata yeye hataki kuwemo kwenye hilo kundi, lakini hana jinsi…aandai kuingia kwenye hilo kundi ni rahisi lakini kutoka ni vigumu, na njia rahisi ya kutoka na kifo….’huyo mwanadada akakunja uso kuonyesha kuwa hilo swala linampa shida.

‘Ikafikia muda akaniambia kuwa mimi wananitafuta kwa udi na uvumba, waniue…na hapo akaniambia kuwa sitaweza kutoka salama, …maana kuna watu wananifuatilia kwa karibu kila ninapokwenda, ….na kama wakijua kuwa nipo hapa, hawatasita kuniua….nikamuuliza kwa vipi, akasema …kama mimi ni mbishi ningoje  nitajionea mwenyewe…’akatulia huyo mwanadada.

‘Oh,ningelijua ningetoa msaada,lakini hakuna mtu aliyeingia….’nikasema.

‘Wakati naingia na pale aliponiona, nakumbuka alibonyeza kitu kwenye simu yake, na baadaye akaizima, aliniambia baadaye kuwa angelijua tangu mapema kuwa mimi sio mtu mbaya, angeliizima hiyo simu yake,maana kundi lao wote wana simu kama hiyo inayoonyesha wapi mtu wao alipo, na kama kuna matatizo wanajua jinsi gani ya kumsaidia kwa haraka,….’akatulia kwa muda bila kusema kitu.

‘Mhhh’nikaguna kama kumshitua na yeye akasema;

‘Aliniambia kwa uchungu kuwa alishabonyeza simu yake aliponiona kwasabbu alijua nimekuja hapo kumkamata,…na hiyo simu imeshapeleka taarifa kwenye kundi lao, kuwa yupo kwenye matatizo , licha ya kuwa alishaizima, lakini kwa jinsi anavyolijua kundi lao, watakuwa wameshaanza kumfuatilia kwahiyo akaniomba niondoke hapo haraka. ….

‘Kwanini sasa hukuondoka haraka…?’ nikamuuliza
.
‘Aliponiambia hivyo, nikawa namuuliza maswali muhimi anajibu huku nikitafuta njia ya kutoka kwa haraka,…lakini haikuwa rahisi hivyo…yalitokea mengine makubwa…..’akasema na kutulia.

‘Yalitokeaje, maana sizani kama kulikuwa an mtu mwingine,na hakuna aliyeingia….’nikasema

‘Lazima kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa kwa ndani, …..huyo mwanadada hakutaka kuniambia, lakini alikuwepo mtu mwingine, nahisi ndio huyo mlinzi wake wa karibu…sijui alikuwa wapi muda wote tukiwa tunaongea,na nakumbuka vyema wakati wanaingia, huyo mwandada alionekana yupo peke yake,…..ina maana huyo mlinzi atakuwa aliwahi kuwa humo ndani kabla yake,…..au ….’akatulia kidogo.

‘Kwani kulitokea nini…?’ nikauliza.

‘Wakati naongea na huyo mwanadada, huku naangaza huku na kule,…nakamsogelea yule mwanadada nikitaka nichukue ile simu yake, maana ni ushahidi muhimu sana, na kuhakikisha kuwa hana kitu kinachonasa yale tunayoongea…na yule mwanadada alikuwa akinisihi niondoke humo haraka...’akatulia.

‘Ohh….kwanini hukuondoka,  wewe hukuona  kuwa hpo kuna balaa….’nikasema.

‘Nilikuwa natafuta ushahidi…ambao unatafutwa sana, na huyo mwanadada alikuwa nao,..’akatulia na kuniangalia, halafu akasema.;

‘Nilipomsogelea akasema, niondoke, kwani hakutaka mimi nifie mkononi mwake….na mara nikaona kivuli cha mtu kwenye dirisha, na kwaharaka nikainama chini, nikiwa na lengo la kujificha, huyo mtu niliyemuona asije akaniona, Mungu Mkubwa, na naweza kusema ilitokea hivyo kwa kudra zake,….’akatulia kidogo na kuweka mkono mdomoni.

‘Yaani…. nilichoshuhudia ni risasi ikipenya utosini, kichwani mwa huyo mwanadada niliyekuwa nikiongea naye. Ina maana kama nisingeliinama haraka, hiyo risasai ingelitua kichwani kwangu, ….huyo mtu alikusudia kuniua mimi, lakini kule kuinama kuliponya,…..watakuwa waliweka kiwambo cha kuzua sauti...’ hapo akapangusa uso kwa kiganja cha mkono.

'Ikawaje maana alitaka kukuua wewe , kakukosa,....?' nikauliza.

'Nafikiri atakuwa alichanganyikiwa...kamuua bosi wake,.....mimii nilitambaa kwa haraka, kuondoka pale, huku nimeinua simu yangu inayochukua picha, nilihakikisha nipo mbali ya upeo wake,...kwasababu alikuwa kwa nje, na pazia lilizuia, asingeliweza kuona vyema, wapi nilipo, nilimuona akizungukazunguka hapo dirishani, na baadaye nikasikia sauti ya mtu akikimbia, nilipochungulia dirishani nikamuona akiondoka....'akasema huyo mwana dada.

‘Sasa itakuwaje, ….maana hiyoni kesi ya mauaji, na wewe ulikuwa hapo, ulitoataarifa polisi na je mliongea nini na huyo mwanadada?’ nikamuuliza.

 ‘Kwanza tusubiri, polisi walijue hilo, na kama nitahitajika nitajua nini cha kufanya, ila nataka nijitahidi hadi nimpate huyo jamaa aliyetaka kuniua,… una uhakika ulimuoan sura yake?’ akaniuliza.

‘Ndio nilimuona,na alikuwa na wasi wasi sana….sasa utampataje ?’nikasema na kuuliza hapo hapo.

`Hawo watu najua wapi wanapopatikana, hawo kazi yaoo ni kukodiwa kufanya mauaji,…na mara nyingi wakishafanya hivyo wanapotea kabisa hapa mjini, wanakuja kuonekana baada ya mwaka hivi….sasa natakiwa kumuona kabla hajaondoka, ina maana leo hii tunakwenda huko, upo tayari….?’akaniuliza

‘Duuh, sasa hapo unataka kujiingiza kwenye mdomoo wa chatu….’nikasema.

‘Hawo watu najua wapi wanaishi, lakini inahitaji njia ya kuwashika, hawo kazi yao ni kukodiwa kufanya mauaji, wanatafutwa sana na polisi, na hapa ina maana ili kumpata inahitajika kujiingiza kwenye matatizo, …na mimi mwenyewe sitaweza hii kazi, nitaongea na mkuu wa kituo, ni rafiki yangu mkubwa, lakini hata hivyo nakuhitaji wewe, lakini naogopa kukutia kwenye matatizo, na sitaki uingie huko, sijui nifanyeje…?’ akauliza.

‘Mimi nipo tayari kuingia kwenye matatizo kama mwisho wake hao watu watakamatwa…lakini nisiende jela’nikasema.

‘Hiyo inategemea nguvu za polisi….na hali ilivyo, mambo yanawezekana yakawa mazito, ….kama huyo mwanadada asingeliuliwa, tungelijua mambo mengi sana,…’akasema huku akikunja uso kuonyesha wasiwasi.

`Kwani unamfahamu huyo mwanadada,…ni nani…?’ nikauliza huku nikimuangalia kwa wasiwasi.

‘Ni Kimwana….’akasema.

‘Eti nini una maana ni mke wangu..?’nikauliza huku nikihisi mwili ukinisha nguvu.

NB Mambo yanaanza kuiva, ni nini kitatokea, je ni Kimwana yupi huyo?

WAZO LA LEO: Zarau sio jambo jema katika maisha, mkiwa wawili au kundini, jaribuni kukwepa kuzaraulina, huenda umejaliwa kiakili, kikipato...kinguvu, usije ukamdharau mwenzako kuwa yeye hana kitu, hana nguvu, huwezi jua nini munu alichopa ambacho wewe huna, tukumbuke mzarau mwiba guu huota tende.

Ni mimi: emu-three

No comments :