Nilisogea na kukaa pembeni ya kitanda alipolala huyu
mwanadada wakili, nikamuangalia machoni akiwa bado kajilaza huku akiangali juu,
alionekana mwingi wa mawazo,na mimi hapo hapo mawazo yakaenda mbali zaidi,
lakini sikutaka kusema kitu, ...namuheshimu sana huyu mwanadada, na nilichofanya nikugeuza kichwa na kuangalia pembeni, na yeye
akasema,
‘Najua una hamu sana ya kutaka kujua kuwa nimeolewa na kama
nimeolewa mume wangu ni nani, na kwanini siku ilesikuwa na pete, …pete yangu
hii hapa,mara nyingi siachani nayao tangu siku ile nilipovalishwa na mtu
nilipyemepdna sana…..’akajigeuza na kulala upande upande.
‘Una maana mume wako au sio ,basi nipe namba yake nimpigia aje….ni muhimu sana ajue kuwa
upo hapa, sizani kuwa keshapigiwa simu, au sio….?’ Nikualiza na kuchukua simu yangu
tayari kwa kumpigia nikipewa namba yake.
‘Huwezi kumpata, usihangaike…..’akasema na nilipomuangalia
usoni niliona nuru ya huzuni ikitanda na kitu kama machozi yakija kwa mbali,
lakini aliyazuia, akasema;
‘Wengi wana hamu sana ya kumjua mume wangu, lakini …..’akatulia
na kujinyosha.
‘Kama hupo tayari kuongea kusu hilo,usijilazimishe …unataka utilize
kichwa ili upone haraka…’nikasema.
‘Nimeshapona, mimi sio mtu wa kulala-lala, hapa naona uzia
tu,….akija docta nitamwambia niondoke, sipendi kuwahivi, nataka niwe mhakamani
napambana na kutetea haki, sio kulala,…kilamuda ukipita naona kama napoteza haki
za watu wengi ambao wanastahili kusaidiwa….’akasema na kujaribu kuinuka.
‘Ni kusaidia kuinuka….’nikasema huku nikimsogelea na
kumsaidia kukaa vyema.
‘Usihanagike, nipo fiti….hapa nilipo nahitaji nipate mazoezi
kidogo, huwa nikilala,nikiamuka lazima nipate mazoezi,….’akasema na kunyosha
nyosha mikono na kweli alionekana mkakamavu.
‘Natamani sana nimuone huyo mume wako,….’nikasema
‘Kwanini….na wanini kwako?’ akauliza huku akiendeela
kujinyosha.
‘Ana bahati sana kumpta mke kama wewe…’nikasema.
‘Unichekesha kweli,bahati ipi, na wakati wanaume mpo
wachache na mnaringa, na wanawake tupo wengi, hatuna soko….’akasemana kugeuza
geuza kichwa kujinyosha.
‘Mpo wengi, lakini watu kama wewe wapo wachache sana….’nikasema.
‘Watu kamamimi wapo wengi sana, ila hawapewi nafasi ya
kujiweka kama mimi….huo ndio ukweli, kama wanawake wangelipewa nafasi ya
kusoma, ya kuwa katika hali inayostahili, mbona dunia hiiingekuwa sehemu bora…lakini
wapi…’akatulia na kuangalia mlangoni.
‘Niambie basi kuhusu huyu mume wako, maana nilizania kuwa
nitamkuta hapa, na mpaka sasa hajafiak au yupo nje ya nchi?’ nikamuuliza.
‘Naona sasa ni bora nikuhadithie kisa changu,….cha mume, au
sio, ili nikuondoe dukuduku lako,..kisa change sipendi kuhadithia,sitaki
kujitia unyonge, lakini ngoja tu nikuhadithia. Ni kisa cha kunyang’anywa tonge
mdomoni, sio mbaya ndivyo dunia ilivyo na unatakiwa ukubali ukweli…namshukuru
mungu kwa hilo, kuwa licha ya kuwa niliumia mwanzoni, lakini nilikuja baadaye nikajipa
ujasiri na kuyasahau yale machungu….’akasema na kuinua mkono wake ukiwa na ile
pete.
‘Huwa napenda kuivaa hii pete, ….tangu siku ile
nilipovalishwa, naiona kama ni sehemu yangu ya mwili,…najua ipo siku nitaitoa,
lakini ni mpaka hapo nitakaporizika, na kwanini niitoe wakati nimevalishwa,
ilitakiwa aliyenivalisha ndiye aje aitoe..ni mawazo tu….’akasema na huku
akiizungusha zungusha ile pte kidoleni.
‘Una maana gani kusema hivyo….?’ Nikamuuliza huku nikiwa
natafakari,….
‘Hahaha…waanume bwana,..kwahiyo unataka nikuhadithia kuhusu
maisha ya ndoa,..halafiu iweje,au na wewe unafanya utafiti wa ndoa za
watu,..kamani hivyo tupo sawa, sio mbaya nikikuhadithia hivi sasa, ….upo
tayari?’ akaniuliza name nikamgeukia a kusema;
‘Nipo tayari muheshimiwa wakili….’nikasema huku nikitabasamu….Na
hapo akaanza kunihadithia kisa cha maisha yake ya ndoa,…..
************
‘Wakati nipo chuoni, nilitokea kupendana na mvulana mmoja, tukawa
tumeshibana kweli, , kwasababu ya upole wake , na tabia yake, ilinifanya
nimuone ni mtu muhimu sana katika maisha,natumai hata yeye ililkuwa hivyo
hivyo, na haikupita muda akanitamkia kwa kinywa chake kuwa kanipenda na
angelifurahi niwe rafiki yake.
‘Nakuomba sana tusianze mambo hayo,maana nimetokea kwenye
historia ambayo nisingelipenda , kujitonesha kidonda kilichoanza kunywea, na
hata kuyahatarisha maisha yangu ya baadaye…’nikamwambia huyo mvulana.
‘Kwani kupendana kunahatarisha maisha yako, mimi sina nia
mbaya kwako, nia yangu ni nyeupe kabisa, Sitaki kukudanganya,….ninachotaka ni
kuwa tuwe marafiki wa kweli,..na hata
ikibidi ukirizika na mimi tuje tufunge ndoa…’akaniambia waziwazi.
‘Muda huo bado,nia na lengo langu ni kusoma…. hadi nifikie
sehemu ambayo nitarizika nayo, tupo marafiki tangia hapo,..kwani hatupo
marafiki?’nikamuuliza. Unajua tena wanaume hawakubali kushindwa,alinibembeleza,na
ikawa kama kero, kila tukipata nafasi ya kuongea inaipenyeza hiyo hoja yake.
‘Sikiliza mimi nitakupa jibu baada ya kumaliza mitihani
yetu…naomba unipe nafasii ya kusoma, nisingelipenda jambo jingine liingile
akili yangu kwa sasa…’nikamwambia. Na yeye akanielewa ,na basi ikafikia muda
wakumaliza mitihani, na kabla hatujaondoka maeneo ya chuo akanifuta na hapo
hapo akadai jibu nililomuahidi…..wanaume mking’ang’ania kitu,….
‘Jibu langu kwa sasa ni hapana, nahitaji muda wa kujiweka
vyema, kwanza maisha yetu ya kujuana ni ya hapa hapa chuoni,sikujui huko
utakako, na huenda mila na dsuturi zetu zikasigishana, …wazazi wako wanaweza
wakawa na malengo mengine ikizingatia kuwa wewe ni mtoto wakwanza wakiume,…sitaki
kuleta migangono katika familia za watu..’nikamwambia.
‘Basi tupange siku twende kwetu, ….na mimi nipo tayari
kwenda kwenu, unaonaje,…mimi nakuhakikishia kuwa nitakulinda na utaiona familia
yetu ilivyo,ni wakarimu na hawana shida kabisa….hawapendi kuingilia maisha ya
watoto wao yenye faida,…hilo nakuhakikishia…’akasema nami nikakubali kuwa anipe
wiki mbili za kujiandaa, maana lazima nikapate kibali toka kwa walezi wangu.
Kwakweli nilishampenda huyo mvulana na moyoni mwangu
nilisharizika naye, mengine yalikuwa ni mambo tu ya kujirizishana kwa nafsi
zetu, ….na siku hiyo tuliyopanga kuwa nitakuwa tayari kusafiri,akaja kwetu
nilipokuwa nikiishi na alinikuta nimeshajindaa, tukafunga safari hadi kwako
mikoani.
Kwakeli ni familia iliyojitosheleza,kwani nilikuta kwao wana
nyumba nzuri, wana miradi ya kuwakimu, na hata usafiri wa familia, na wenyewe
walionekana wakarimu tu,…nikafurahi sana na yeye akanitambulsiha kwako
kamamtarajiwa wake,sikupenda iwe hivyo haraka, lakini angesemaje kwa wazazi
wake, …
‘Mbona haraka hivyo,kwanza hatujamjua huyu binti vyema
…’akalalamika baba baada ya kumuita mtoto wake pembeni, na mimi nilibakia pale
na mama, baadaye mama naye akaitwa na nikasikia akisema;.
‘Baba Nanihii unataka kumjua vyema kwa vipi,, ..wao
walishajuana toka huko chuoni,sisi hatuhitaji kumjua zaidi,hebu niambie
utafunga safari hadi huko kwao anapotoka ili umjue maisha yao na familia yao
,maisha ya siku hizi ni kuelewana, ..kama mwanetu karizika naye, hewala’akasema
mama kwani alishanipenda .
Basi tukakaa hapo kwa wiki moja halafu nikaomba nirudi
kwetu,na mwenzangu akadai kuwa kabla ya kuondoak hapo lazima tufunge uchumba.
Ujue nilikuwa sijakubaliana na hilo ombi,na hakutaka kunilazimsha, na siku hiyo
akalitamka tena hilo ombi,….nikamwambia bado muda muafaka, hakukata tamaa.
Kumbe wao kama familia waliandaa sherehe, waliyoiita ya
kuniaga, lakini kumbe sio kuniaga tu, ila walivyoniambai mwanzoni ni kuwa
wameamua kunifanyoa sherehe maalumu kwa ajili yangu.
‘Kwanini muahangaike hivyo…’nikasema na yeye akaniambia hilo
ni swala dogo tu, na akaniomba nijiandae vyema, na hata nguo maalumu
ikanunuliwa kwa ajili yangu.
Basi nikiwa chumbani kwangu, mara huyo mvulana akaja,….alikuwa
akiniheshimu sana, tangu tufike hapo, alihakikisha hafiki chumbani kwangu mpaka
kwa ruhusa yangu, na siku hiyo hiyo alifanya hivyo,akagonga mlango, nami
nikamuitikai aingie ndani.
‘Unaonekana mrembo kuliko siku zote,sitamani uondoke, kabisa…’akasema
‘Nashukuru,hata hivyo lazima niondoke,ujue mimi ni mtoto wa
watu, hatujafunga ndoa itakuwa ni maajabu nikikaa huku kwa muda
mrefu…’nikasema.
‘Ni kweli lakini kabla ya kuondoka , kuna hicho kijisherehe
kidogo ,tunataka kukuaga kama familia…tumekupedna sana hata wazazi wangu
wamefurahishwa na tabia yako, wanasema kweli wewe unastahili kuingia nyumba hii…’akasema
nami nikasema hakuna shida, muda ndio utakao-ongea.
Tukiwa ndani ya sehemu maalumu waliyoiandaa kwa hiyo sherehe
fupi, wazazi wakongea na kutoa nasaha zao huku wakinisifia kwa maneno mengi na
abadaye wakasema kijana wao ana la kuongea ;
‘Kijana wetu katuambia ana maneno ya kuongea mbele yenu,….hebu
njoo huku mbele maana wewe ndiye ulitakiwa uongee sana kwa ajili ya mwenzako anayeondoka….’akasema
baba
Yule mvulana akapita mbele, na kusalimia kwa adabu, akaongea
kidogo,halafu akaniita nipite mbele.Bila hili wala lile nikaenda na tukawa
tumesimama mbele ya wanafmilia na wageni waalikwa, nikashngaa mwenzangu anapiga
magoti mbele yangu, akatoa kiboksi chete pete, na kusema ananiomba uchumba…watu
wakashangilia na mimi hapo nikaingiwa na aibu,, maana sikutegemea kabisa kuwa
itakuwa hivyo, na kwa heshima ya familia yao nikashindwa kusema lolote zaidi ya
kukubali, nikavalishwa pete.
Basi sherehe ikaendelea na baadaye tukaeleeka kila mtu
chumbani kwake, na kabla sijajiandaa kulala mara mlango wangu ukagongwa,
akaingia huyo mvulana.
Na kwa vile tulishakuwa wachumba tena , mipaka ya kuingia kwangu
ikawa imelegezwa kidogo, na usiku huo alipokuja tuliongea sana, na hata kufikia
hatua ambayo sikuweza kumkataza kulala humo, na kawa mara ya kwanza nikaweza kukutana
kimwili na huyo mvulana, sikutaka iwe hivyo kabla ya ndoa, lakini kwa hali
ilivyokuwa nilishindwa kusema hapana….sisi wanawake tuna mitihani sana, lakini
inatakiw auajsiri kusema hapana….
Basi kesho yake tukaagana na hapo ndipo nilipoona kuonja
mitahani ya mapenzi, maana sikutamani kabisa niondoke, nilitaka nibakie naye, moyo,
mwili akili ilishakubali kuwa naye, lakini ndio hivyo tena safari ilishapangwa
na ikabidi niondoke. Yeye alitarajia kuja huku mjini baada ya mwezi na kitu
hivi, kwani walikuwa na mipangilio yao ya kifamilia. Kwakweli njiani nilikuwa
nikimuwaza yeye tu. Ndio mapenzi ya mwanzo yalivyo, ….
Sikuamini tukawa tukiwasilina kila siku kila muda nilipopata
nafasi, na mwezi ukaisha,na hapo nikahisi mabadiliko ya mwili,nilikuja kugundua
kuwa nimepata uja uzito nisio utarajia….nikahamanika, sikupenda kabisa iwe
haraka hivyo na pia nikaona aibu kumwambia huyo mwenzangu ukweli. Na baada ya
mwezi na nusu akaja hapa Dar, alipokuja nilishindwa kumwambia lolote kuwa nina
uja uzito wake. Hakukaa sana akarejea kwao.
Alipoondoka kilipita kipindi cha miezi mwili, nami nikawa na
wasiwasi jinsi gani nitamwambia na muda mrefu ukapita tena, na siku moja
akanipigia simu kuwa ana mazungumzo muhimu na mimi….nikajua ndio hilo swala la
kufunga ndoa,nami nikafurahi moyoni,….
‘Utakuja au tutazungumzaje na wewe upo mbali………..?’ nikamauuliza.
‘Tutaonge kwenye simu maana hata hivyo nina safari ya kwenda
nje ….naenda kusoma zaidi…..familia yangu imenishauri hivyo nami siwezi
kuikatalia, nitapita huko mara moja, uje uwanja wa ndege….maana sitakuwa na
muda w akuja kukuonanyumbani kwenu,….natamani iwe hivyo, lakini safari
ilivyopangwa imekuwa kama haraka, kinyume na matarajio yangu…’akanimbia nami
nami nikamkubali ingawaje nilipenda aje tukutane uso kwa uso…
Basi siku hiyo ya safari yake, nikafika uwanja wa ndege, na
alifika kwa ndenge ndogo, na siku hiyo hiyo anaondoka kwenda ulaya, kwahiyo
hatukupata muda wa kuongea vyema, tuliongea mambo ya kawaida na pale nilipotaka
kumgusia hilo swala langu akaja tafiki yake, wakawa na mazungumzo ambayo
yaliishia muda ndege inataka kuondoka na yeye tukaagana tu.
‘Usijai nikirudi tu tunafunga ndoa….’akasema na pale pale
akakumbuka na kuniachia simu yake. Akasema ;
‘Najau wewe ni mtu muhimu kwangu , nakuachia hii simu yangu,
…sihitaji kusafiri nayo huko nitanunua nyingine..kama kuna mawasiliano yoyote
waambie kuwa sipo’akanipa nami sikuwa na kipingamzi.
Akaondoka na nikabakia nikiwa na mtihani, maana nilijiona
mjinga, kwanini sikumwambia muda wote huo, na nitawambiaje wanafamilia hasa
familia yangu au familia ya mwenzangu, na wakati umeshapita muda mrefu kama huo,nikasema
potelea mbali, nitamwambia mwenyewe kwenye simu,
Hutaamini hilo, kila muda tulipokuwa tukionge kwenye simu,
kila nilipotaka kumgusia hilo swala,kunatokea kizuizi fulani,ama mawasiliano
yanakuwa mabovu, au salio linakwisha au sababu yoyote ambayo inafanya
tuahirishe mzunguzmo yetu, siku sikazidi kwenda mbele, ….
Ikafika muda hakuna mawasiliano na yeye tena akipatikana anadai
kuwa yupo na shughuli nyingi za masomo na mara hata simu yake ikawa haipatikani
tena….nikaona sasa hili litakuwa tatizo siku moja nikaona ni bora niifahamishe
familia yao kuwa nina ujauzito wa mtoto wao, na siku hiyo nikaamua nitumie simu
yake ambayo tangia aondoke nilikuwa siitumii, nilikuwa nimeizima kabisa.
Nilipoiwasha tu, kukaingia ujumbe, na ujumbe, ujumbe, na mtumaji
alionekana ni yule yule na nilipousoma huo
ujumbe mmoja nikajikuta nikipepesuka, nilijisikia vibaya sana, nikawa na hali mbaya
ambayo sijawahi kuihisi, na ukizingatia na hali niliyokuwa nayo,basi mambo
yakazidi kuwa mbaya.
Baadaye nikajipa moyo nikasoma huo ujumbe vyema, ulisema
hivi;
‘Mpenzi tangu uondoke mimi sijisikii vyema, unakumbuka nilikuambiai
kuwa nahisi nia uja uzito wako, na sasa miezi miwili, ….naomba uwafamishe
wazazi wako ili taratibu zote zifanyike, ….’, nIliusoma ule ujume vyema ,labda iwe umetumwa kimakosa, lakini
jina la mtumaji lipo waziwazi na jina la
mtumiwa katajwa kabisa kwenye hiyo simu, jina na la huyo mvulana.
Nikaona isiwe tabu , nikaamua kumpigia huyo mwenye ujume
nikijifanya mimi ni dada wa huyo mvulana , na huyo mwadada akaupokea tukaongea
kama mawifi, nikamwambia simu yake kaka kaiacha kwangu na nimeona ujumbe wake,
je ni kweli kuwa yeye ni mjamzito.
‘Ndio ni kweli unajua tulipendana sana na kaka yako,…kila
akija likizo tunakutana, mara nyingi nilimshauri tutumie kinga lakini hapendelei
hivyo, na sasa safari hii mambo yameharibika, nimejikuta na ujauzito wake,…lakini
hata hivyo alishaniambia kuwa nisiwe na wasiwasi…atanio tu…hataki mtoto wake
azaliwe bila baba’akasema.
‘Mbona nilisikia kuwa ana mchumba mwingine toka huko Dar, na
aliwahi hata kumtambulsha kwa wazizi wake…?’ nikamuuliz a kiujanja.
‘Ndio ilitokea hivyo, na iliniuma sana, na sikutana
kumwingilia,…nikijua yeye ndiye muamuzi,… ila baadaye alikuja kwangu na
kuniomba samahani kuwa alipitiwa tu, sasa yupo tayari kuwa na mimi, name sikujivunga,
nahisi hapo ndipo mimba ilipoingia….kwakweli nampenda sana kaka yako, kama
angelinidanganya,ningelikunywa sumu….’akasema.
Fikiria mwenyewe hali kama hiyo, hata hivyo sikukata tamaa, nikawapigia
wazazi wake simu kuhakikisha hilo na wao wakasema kuwa ni kweli kuwa mtoto wao
alikuja akawaambia kuwa anapenda amuoe mchumba wake wa zamani kwasababu alitaka
mtu anayetoka kwao….na alishaharibu…keshampa ujauzito…’wakaniambia hivyo na
siku niliposikia kauli hiyo toka kwa wazazi wao, tumbo lilinikata sana…nikawa
najisikia vibaya kuliko, na siku hiyo hiyo nikapokea simu toka kwa huyo
mvulana.
‘Haya niambie kwanini umefikia hatua hiyo ya kunidanaganya
kumbe una mtu mwingine…’nikamwambia mapem kablahatujaanza mazungumzo mengine.
‘Ndio maana nimekupigia,nilitaka kukuambia kuwa bahati mbaya
nimempa mtoto wa watu mimba, na nimeona nisimtese, …na nisingelipenda awe na
mtoto asiye na baba, kwahiyo nitamuoa yeye tu…samahani sana….ila nakuomba
tuzidi kuwa marafiki,nakuomba sana unisamehe, ..najua nitakuwa nimekuumiza sana,
lakini imetokea hivyo..nashindwa hata la kukuambia….tufanyeje’kwakweli hayo
mazungumzo yaliyofuata sikuweza kuyasikia, nilidondoka chini…huku nasema.
‘Je na mimi kama nina mimba yako utasemaje?’ nikasikia
akisema.
‘Hiyo
itakuwa siyo mimba yangu…’niliposikia hivyo, kiza kikatanda usoni, na mara nikadondoka chini na kupoteza fahamu huku maumivu kwenye tumbo, yakiwa makali sana….
NB: Jamani leo nimebanwa na mtandao unasua sua...kidogo kidogondio mwendo.
WAZO LA LEO: Unajiskiaje pale mwenzako uliyemtegemea anakumabia mimi na wewe basi, au ukasikia kuwa kapata mwingine ...inauma sana,....lakini ukumbuke yote ni majaliwa ya mungu, huenda imetokea hivyo kwa kukuokoa na jambo, au ili ukutane na mwingine ambaye ndiye chagua la mungu. Kama imekutokea hivyo, shukuru na usihamanike...vuta subira
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Nimependa wazo lako la leo. Inauma ndiyo lakini inabidi iwe hivyo itabidi uyakubali yaliyotokea na kuendelea na maisha. Ahsante na nakutakia kazi njema maana kila ukiingia hapa unatoka na faida.
Post a Comment