Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, March 6, 2020

HII IMETOKEA WAPI?

Muendesha mashitaka, akutikisa kichwa kama kusikitika, baadae akasema
'Vyovyote iwavyo mimi nimechoka na kesi zenu,..kama hakuna ushahidi wa kutosha, nitashinikiza kesi hii ifutwe.
'Kesi ipo na kiongozi wa kundi, aliyeanzisha genge la chuma ulete, akiwa hajulikana, atajulikana..
Tuendelee na kisa chetu
******
'Sisi sio wamiliki wa hii kampuni, ...'wakajitetea, washitakiwa walipofikishwa mahakamani.
'Wamiliki wa hizo kampuni ni nani na wapo wapi..?' wakaulizwa
'Kiukweli hatuwajui..sisi mara nyingi tunapata maagizo, ya maandishi au ya simu...lakini hao wamiliki wenyewe hatujawahi kuwaona..'wakasema hivyo.
Haiwezekani...
'Ni watu wasiojulikana...?' akauliza muendesha mashitaka na watu wakacheka.
'Kama utapenda kusema hivyo..lakini huo ndio ukweli, mkitushitakia sisi sio haki...'akasema
'Kwa kauli zenu za ushahidi mumekuwa mkitumia maneno hayo, watu wasiojulikana,..mtapelekwa kusipojulikana si ndio hivyo, je nyie mpo tayari kubeba dhamana ya wakubwa zenu..?' wakaulizwa
Wakili mtetezi akaingilia kati, akisema, wateja wake wanalazimishiwa kesi isiyowahusu, kwani kesi hiyo inawahusu wamiliki wa kampuni, na wateja wake ni watendaji tu...hapo kukatokea malumbano ya kisheria hadi hakimu akaingilia kati.
'Hao wamiliki wenu wapo wapi...mahakama inatoa amri, hao wamiliki wa hizo kampuni, wawepo mahakamani, kama hawapo nyie ndio mtabeba dhamana...'akasema hakimu.
Kesi iliahirishwa...
Pamoja na kuahirishwa kwa kesi waliokamatwa, hawakukubaliwa dhamana , watendaji hao waliendelea kushikiliwa hadi hapo wenye kampuni watakapofikishwa mbele ya hakimu...
******
Taarifa iliyokuja baadae ni kuwa mumiliki mmojawapo, ni mgonjwa.
'Mumiliki huyo, anaumwa, alipata ajali na amesafirishwa nje kwa matibabu...'
Nyaraka zikatolewa, .....
Hata hivyo, kesi iliendelea, ili ikibidi waliokamatwa waachiliwe au wapewe dhamana.
Wakili muendesha mashitaka, akamsimamisha mtu wa jamii,...
'Huyu mtu mnamleta kama nani...?' akaulize wakili mtetezi.
'Ni shahidi...'akaambiwa, na mtu wa jamii, akasimama, akaanza kuelezea kuhusu alichokigundua kwenye genge hilo linalojiita genge la chuma ulete..
Kila mara alisimamishwa na wakili mtetezi, akipinga baadhi ya maelezo, na wakati mwingine wakili huyo mtetezi, akadai, kuwa maelezo hayo, yanawahusu watu wasiokuwepo.
'Watu wasiojulikana...'akasema muendesha mashitaka.
'Watajulikana tu..'akasema mtu wa jamii.
'Ndugu muheshimiwa hakimu, ili hii kesi iliyopo mbele yako, iweze kuwabaini hao watu wasiojulikana, tunaomba ndugu Jeuri afikishwe mbele mahakama yako tukufu.
'Jeuri ndio nani...?'akauliza hakimu...
'Yeye sio mshitakiwa...'akalalamika mtetezi.
'Yupo kwenye orodha ya washitakiwa, lkn hajaweza kupatikana..'akasema muendesha mashitaka.
'Yeye ni shemeji ya mtu mmoja aliyepotea, akiwa mgonjwa, tunaomba mtu huyu aitwe, ili atoe ushahid wa watu wasiojulikana
'Hata hivyo wewe ni shahidi,toa ushhodi wako uondoke, kwanini wewe shahidi unahitajia shahid , hiyo sio kazi yako..'akasema wakili mtetezi.
Hakimu akaingilia kati...
'Huyo mtu, Jeuri, au mbabe, ana ushahidi gani wa kumpata mumiliki wa hizo kampuni,..maana tumeambiwa mwenye kampuni anaumwa,..?' akuliza hakimu.
'Ndugu muheshimiwa hakimu, Jeuri, au mbabe, ametoweka, siku mumiliki wa kampuni aliposafirishwa nje kutibiwa,...
'Sio kweli, Jeuri, amekuwa akiumwa hata kabla, ushahidi upo..'akasema wakili.
'Kuumwa kupo, sawa..lakini huyo mgonjwa yupo wapi, kwanini anafichwa, polisi wanataka kujiridhisha.. 'akasema mtu wa jamii.
'Kwa maelezo ya dakitari, Jeuri, hatakiwi kusumbuliwa, hali aliyo nayo, yahitajua utulivu..
'Wakili wewe unatekeleza kazi yako kusheria, unahitajika kumtetea mteja wako, lkn sio kwa kukiuka sheria, je ikibainika kuwa wewe unajua kuwa mteja wako, ni mvunjifu wa sheria na wewe unamlinda..
'Hiyo sio kazi yako, mimi namtetea mteja wangu, hata jambazi muuaji, anastahiki kutetewa kwa mujibu wa sheria...
'Kwahiyo unakubali kuwa mteja wako ni jambazi, na anastahiki kutetewa..
'Nimetolea mfano, na Jeuri, hajashitakiwa hapa kama mshitakiwa.
'Mteja wako anaumwa nini
'Hiyo ni kutaka kutoa siri za mgonjwa ambaye sio mshitakiwa.
'Ndugu hakimu, wakili mtetezi hataki kulibainisha hilo kwasababu, ugonjwa wake, unasababu za kuficha ukweli wa watu wasiojulikana.
'Kwa vipi...'akauliza hakimu.
'Muheshimiwa hakimu, kwa vile ipo haki ya kulinda siri za mgonjwa, kama alivyotaka wakili mtetezi, tunaomba mahakama yako, imtembelee mgonjwa hosp
'Ili iweje..
'Ili ukweli wa watu wasiojulikana ubainike...kwanini Jeuri aumwe, azidiwe, kipindi hichohicho, mshukiwa mkuu, ameumwa, na kusadikiwa,..
Wakili mtetezi, akaingiza pingamizi, na hakimu akauliza.
'Huyo mgonjwa kalazwa hospitali gani...
'Ndugu muheshimiwa hakimu, huyu mtu akipatikana atafumbua fumbo kubwa la kitendawili hiki cha watu wasiojulikana, ...nimesikia kuwa naye anaumwa,..hali yake ni mbaya, je na yeye yupo hapa nchini, au kasafirishwa kwa matibabu..?
Wakili mtetezi, akajaribu kujitetea, lakini mwishowe wake ikakubalika kuwa huyo jamaa atafutwe aletwe mbele ya mahakama..kesi ikaahirsihwa,....
Siku ya mahakama iliyofuata, ukumbu ulijaa sana, maana kuna fununu, kuwa watu wasiojulikana watajulikana siku hiyo...
'Hao watu ni muumiani..wanakula watu, wanaua watu, wamepoteza watu wengi...'watu wakasema na magazeti ya udakiu yakazidisha kwa kusema,..'mumiliki wa kampuni hiyo ni friimathoni....
'Waongo hao....ni wajanja fukani..
Siku ya kesi ikafika, na ulinzi mkali ukaimarishwa,...
Koorti.....hakimu akaingia, na swali la kwanza, je shahid ambaye anahitajika kutoa ushahid wa watu wasiojulikana kapatikana...
'Ndugu hakimu, shahidi aliyehitajika, hali yake ni mbaya, yupo hospitalini, hataweza kuhuddhuria mahakamani...'akasema wakili mtetezi..
'Huyo mtu, hali yake sio mbaya kihivyo, wanavyodai muheshimiwa hakimu, mtu huyu hatakiwi kuhudhuria mahakamani kwasababu siri yao kubwa itagundulikana...'akasema mtu wa jamii.
'Siri gani...?' akauliza hakimu, na wakili mtetezi akaingilia kati, na swali hilo, likawa limezimishwa, hata hivyo, haklimu akahitajia, mahakama ihamie huko alipo huyo mgonjwa akamshuhudie yeye mwenyewe. hapo likazuka zogo la ubishani, lakini hakimu na hikimu, huwezi kubishana naye..
Ni mimi: emu-three

No comments :