UHURU HOYEE...
Uhuru sio kitu cha mchezo, ni jambo la kifahari la taifa,
Hapa inatakiwa uzalendo, kila mtu aiheshimu siku hii. Siku hii isiishie kusherehekea tu kwa wakubwa, ilitakiwa hata makazini, siku kama ya leo wanapata posho ya kujipongeza wao na familia zao.
Siku hii tusahau tofauti zetu za kisiasa, viongozi wa chama waungane na kiongozi wa nchi, washikane mikono na kuiazimisha siku hii muhimu kwa Taifa…
''Na kulitakiwa kuwe na kombe maalumu la Uhuru, mabingwa wa michezo mbali mbali wanashindana..hitimisho liwe tarehe 9 December,…kombe liwe la kipekee…''
Tukumbuke kuwa wapo waliomwaga damu zao ndio maana hii leo tunajivunia Tanzania, mola awalaze mahali pema peponi mashujaa hao.
Wapo pia walipoteza viungo vya mwili…kama bado wapo hai mungu awape subira, lakini wapo pia walipoteza mali, nk…leo hii tunajivunia Tanzania.
Nawashangaa wale wanaobeza, wakisema eti aheri tungeliendelea kutawaliwa huenda tusingelikuwa masikini hivi, Hawajui kuwa uhuru ndio umemfanya waongee hivyo, watembee hivyo kwa uhuru kutoka kwao hadi miji mingine,
Wameshau kuwa watoto wao wana soma hivyo sababu ya uhuru,..hata leo hii wanajinadi na kujinasibisha kwa hili au lile, wangelijua, wakawauliza mababu zao…Uhuru ni jambo la kifahari lilimfanikisha amiliki hata aridhi, nyumba nak….
Tujipongeze kwa pamoja,..kwa kusema UHURU HOYEE….
Blog yenu ya Diary yangu, na ukurasa wake wa Facebook, unaungana na Watanzania wote kujipongeza kwa siku hii muhimu....hongera Watanzania, na viongozi wake ...
Na tunamuomba mola awalaze mahali pema peponi wazee wetu wote waliopigania uhuru, hadi kifikia hitimisho la kuitwa watanzania huru.
Ni mimi: emu-three
No comments :
Post a Comment