Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Sunday, April 4, 2021

MTANIKUMBUKA







MTANIKUMBUKA......

******************

'Mwema aliona isiwe shida, akamuambia muajiri wake, kama waona sifanyi unavyotaka wewe basi naomba umweke mtu mwingine ambaye atakufaa,.....;'

'Unasema nini...nikimweka mtu mwingine wewe huna kazi...unalifahamu hilo usitingishe kibiriti...'akasema kwa kauli ya dharau hivi.

'Kama waona ni sahihi kufanya hivyo sawa, mimi nitafanyaje, ...' akajibu mwema lakini moyoni akawa ana mashaka, je kweli mwajiri wake si atamfukuza kazi.

Muajiri akatabasamu na kusema...

'Sikiliza kama umechoka kazi sawa, wapo watu wenye weledi wa kazi tena vijana wasomi eeh, wewe si unatingisha kibiriti, sio, ...sawa mimi nitatii ombi lako, ....nitaandika kuwa umeaka wewe mwenyewe kuacha kazi, kuwa huwezi kazi....haya nenda uniachie hiyo kazi....' akasema bosi wa kampuni.

'Lakini mim---mi bosi sijasema hivyo....'Mwema hapo akataka kujieleza zaidi

'Hamna cha lakini toka ofisini kwangu....utanijua mimi nani, huwaga sirudi nyumam...toka, toka...'akasema sasa akiashiria kwa mkono, kama kumfukuza hivi.

Mwema akatoka kichwa chini, sasa wasiwasi mashaka,....akijua sasa kazi hana...lakini kwa upande mingine akajielekeza kwa mola wake, na kumuomba ampe subira na ujasiri.

Mwema alikuwa mchapakazi hodari, kila mtu anamfahamu hivyo, akiwahi kazini na kujituma kwa kila aina ya kazi, hakuchoka na wengine walimkebehi wakimwambia, anajipendekeza, na ipo siku ataiacha hiyo kazi ...

Yeye hakusita kuwaambia....

'Mimi natimiza wajibu wangu, wajibu wa kazi ni dhamana kwangu, sifanyi kwa kumuonyesha mtu au kujipendekeza kama mnavyodai...mimi ninajua kwa imani yangu, kazi kwangu ni dhamana, hili nina uhakika, ipo siku mungu ataniuliza, je nikihini dhamana hii, nitampa jibu gani mola wangu, kuwa nilikuwa nafanya kwa ujanja ujanja au...hapana nitafanya na kutii majukumu yangu, kadri ya uwezo wangu......' ilikuwa ndio kauli yake.

'Sawa ngoja tuone....wangapi walikuwa kama wewe wapo wapi, wanajijutia.....jitahidi bwana, na imani yako...hahaha....'wenzake wakamsema kwa dhihaka.

Leo yale waliyosema wenzake yametimia, anaondoka kazini na huenda asilipwe chochote maana kaaamua yeye mwenyewe kujiachisha kazi....kama alivyodai muajiri wake.

******************

Masaa yakaenda kidogo, mara......

'Wema unaitwa na bosi...' ilikuwa sauti ya katibu muhutasi wa meneja...Wema kwa unyonge akaelekea kwa bosi, na kukuta barua ipo mezani....japo awali alijenga ujasiri, lakini kwa muda huo, mwili wote uliisha nguvu

'Haya ulichotaka ndio hicho hapo, ...'akasema bosi, Mwema akasita kuichukua ile barua, sasa akitaka kuomba msamaha.

'Bosi nimekosa....nisamehe....'akaweza kutamka hivyo.

'Sikiliza ndugu, maji yakimwagika hayazoeleki....mmmh...ila nikiri jambo moja....sikupenda uondoke, haraka hivi....lakini kwa vile umetamka mwenyewe hamna shida, nimeshampata mtu wa nafasi yako,....'akasema akijifanya yupo bize.

'Bosi....nisamehe...sikuwa na maana hiyo....'akajitetea Mwema.

'Ni hivi, kazi hauna tena,....eeh, ila, nikuulize jambo la mwisho...wataka nikulipe nini kama ahasante...maana huna cha kulipwa kisheria, si umeamua mwenyewe wataka kuacha kazi...' akasema mkuu huyo

Mwema tana hapo,...hakutaka ubishi, maana kauli yake ya awali ilikuwa kama 'mwanaiona sifai...labda wambadilishe sehemu ya kazi' .....sio mimi nimeaamua kuacha kazi....kuna utata wa kauli yake. na bosi huyo kwa vile moyoni alimuona hafai, akaitumia alivyoona yeye..

Mwema hapo akataka kutoa kauli yake ya mwisho akijua kazi hana, akasema...

'Ila bosi..samahani kama nimekukwanza, mimi na wewe tumetoka mbali, nimekuwa nikijutuma sana..hilo kosa lilitokea ilikuwa ni makosa tu ya kibinadamu, kumbuka tulipotoka bosi....mimi nilisema kwa ushauri, kuwa kama waona kwenye nafasi hiyo sifai.....'

'Sikiliza sitaki ngonjera, chukua barua yako, bye..bye...'akasema bosi, hapo Mwema akachukua barua yake...kiunyonge.

'Hahaha, ulikuwa unatikisa kiberiti...wanajua mimi nilivyo, huwaga sina tabia ya kurudi nyuma kwenye maamuzi yangu ndugu, wewe nenda kazalilike huko mitaani, sitaki hata kukuona tena,...nimeshakuchoka, unasikia, sitaki hata kukuona tena katika maisha yangu, wasikia, aah, wewe nani, eeh....kwaheri...'akasema bosi.

'Sawa nina uhakika ipo siku utaliona kosa lako, na UTANIKUMBUKA BOSI...' Akasema Mwema kwa sauti ya unyonge.

'Ndugu ndugu...mimi nakuuliza tu, wataka tukulipe kiasi gani...kukusaidia tu...maana huna haki hapa, si umetaka wewe mwenyewe...hivi wewe nani..eeh hebu niambie, eeh...mimi bosi nikubembeleze eeh......nimeshakuchoka ndugu yangu, kwanza wanipa hasara tu, kila siku....kwaheri...'akasema bosi.

'Bosi,...ukiniuliza hivyo ....nikupe jibu gani, kama umeshaamua,...wewe wajua, ...mimi nilipeni haki yangu inayaostahiki, ninajua haki yangu ni nyingi sana nilijitolea hapa kazini kwako,...ukikumbuka wapi tulipotoka mimi na wewe.. sasa nini cha kunilipa ni uamuzi wako.....' akasema

'Weeeh..uliwahi kutoa mtaji hapa...haki gani hiyo eeh..., wewe si kibarua tu, huna lolote haki yako ni mshahara wako tu..unasikia,...'akasema kwa nyodo.

'Sawa...vyovyote iwavyo ninajua mimi kiimani, ipo siku nitaipata hiyo haki yangu.....hata kama mtaamua kunidhulumu...'akasema Mwema....

'Hahaha....sijaona mtu mjinga kama wewe..eti nikudhulumu, hivi wewe wajua mali hizi zimetoka wapi..eeh, ni mali za urithi, ...wewe ulikuja hapa nikakuajiri tu....sina jaja ya kukueleza mengi,....haya sawa ngoja nitaongea na mhasibu, tutakulipa mshahara wako mmoja maana ni kukusaidia tu hamna shida ...'akasema na mwema akaondoka.

******************

Malipo aliyoyapata ni mshahara wake mmoja tu....ambao hautamsaidia lolote ukizingatia kuwa yeye pamoja na utendaji wake kazi, bado alikuwa akilipwa mshahara mdogo sana..

'Hiyo ndio haki yangu aliyonijalia mola, kama ipo nyingine mola anajua zaidi, ndio kiukwel moyoni ninajua ninadhulimuwa..lakini ... najua ipo siku nitapata tu....mtoa rizki ni mola...'alisema hivyo wakati akabaidhiwa barua yake na mshshara wake mmoja.
Wengi walimshauri akashitaki...lakini yeye hakukubaliana nao, akafungasha na kuondoka zote...

Wenzake, wengine wakawa wanamkebehi na kusema...

'Sisi tulikuambia,....ukajifanya mcha mungu, eeh,...sasa kipo wapi....eeh, kuwahi ofisin kufanya kazi kama kampuni yako, badala ya kutafuta namna nyingine ya kujiingizia kipato, ,...hahaha....kafie mbele..'wakasema

'Ahsanteni, mimi nawatakia kazi njema,...na ni sameheni kama kwa kufanay hivyo niliwakwaza....' ilikuwa kauli yake ya mwisho, na kutoka getini.

*********
Wiki moja kabla na ndio ilikuwa sababu ya kukwazana na bosi wake, mkewe alikuwa akiumwa, kwahiyo alikuwa kiomba dharura....na hata kuomba kimkopo, ....na hata hivyo hali ya mkewe hakiweza kutengemaa vyema

Siku alipopewa hitimisho la ajira yake anarudi nyumbani, anamkuta mke anaumwa zaidi....na kingine alikuta barua, ...., watoto wamefukuzwa ada, matatizo ndio yakawa yanajileta kwa mkupuo.....hana hili wala lile mke anamuuliza kulikoni, umelipwa nini..

'Nimelipwa haki yangu, waliyoiona wao, ninajau mola anajua zaidi kwa hili, sina haja ya kubishana nao,...mola amenikadria nilipwe hivyo, mengine anajua yeye..'akasema kumuambia mkewe.

'Shilingi ngapi...' mkewe akauliza

'Mshahara mmoja wa mwezi, walikata na lile deni lao, kilichobakia ndio hiki hapa....ukumbuke kuna kodi za serikali,.......'akasema Mwema.

'Nini...!! mume wangu, hivi wewe huna kazi hali ndio hii na mimi ndio hivi naumwa, siwezi kuuza uza vitumbau tena, ....mume wangu watoto wamefukuwa shule, .....tutaishije jamani ...?' akauliza mke machozi yakimlenga lenga.

'Mtoa riziki ni mola, mke wangu....yote haya najua ni kwa mapenzi yake, kama ndivyo kapanga iwe hivyo, ninajua ipo siku atanionyesha njia...nitaenda kuuza njugu, mitaani, kuokota makopo ya plastiki, nitauza vyuma chakavu.......tutapata cha kutusitiri..'akasema na kweli alichukua mfuko akaingia mitaani.

Masiku yakapita maisha yakawa magumu sana kwa Mwema na familia yake, ikabidi mke arudi kwao kidogo, ili yeye aendelee kuhangaika, ilikuwa kwa makubaliano.

'Sawa mke wangu, hali ikiwa vyema nitakuita, nitajitahidi kuwatumia kila senti nitakayoipata...'akasema wakiagana na mkewe.

***********

Huku kwenye kampuni masiki miezi na miaka ikapita.

Kazi zilianza kuyumba, zile kazi ambazo alikuwa akizifanya yeye, zikawa zinafanywa na watu watatu, na bado zikawa hazifanyiki vyema, ujuavyo wengi walishajenga tabia ya kutegea, kufika kazini kupoteza muda tu...kuna muda kampuni ikasimama kidogo, na ilipoanza tena, wengi wa wafanyakazi walipunguzwa.

Ghafla bosi akawa anaumwa, ilianza kidogo kidogo, mara hali ikazidi kuwa mbaya, akapelekwa India kutibiwa, baadae akarudi, lakini hali bado ikaendelea kuwa mbaya

Bosi ikabidi sasa aombe ushauri kwa watu mbali mbali maana hata kazini hawezi kufika, ...huku na huku akaambiwa maradhi yake hayo dawa nzuri ni tiba mbadala.

'Niambieni,..maana nimeshatumia hizo, za Wamerekani, ....kila dawa nimejaribu, eeh....'akasema

'Bosi, hayo maradhi, kuna jamaa mmoja tumesikia ana dawa nzuri....lakini hata mimi sijawahi kukutana naye, nilisikia tu kwa mtu mmoja alikuwa akiiumwa hivyo hivyo.

Ukumbuke hapo miaka imeshapita..pale kazini wanaachishwa na kuajiriwa wapya, kwahiyo wengi wa wafanyakazi waliokuwepo muda huo ni wageni kabisa hawamfahamu hata huyo Mwema..

'Ni nani huyo nipo tayari hata kumpa nusu ya utajiri wangu, nitafutieni...'akasema na wafanyakazi wakahangaika kumtafita huyo mtu.

Huku na huku akaletewa dawa.

'Huyo muuza dawa mwenyewe yupo wapi..?' akauliza.

'Yeye kasema dawa ili ifanye kazi, utimize ahadi yako, ndivyo alivyoelekezwa kila mwenye tatizo huwa anaahidi yeye mwenyewe akipona atafanya nini.. kwa maandishi na wakili....hasa wenye maradhi makubwa kama yako....'akaambiwa na kwa vile yeye alichotaka ni kupona, akasema..

'Sawa kama kweli dawa yake itasaidia mimi nikipona, nitampa moja ya kampuni zangu...muiteni wakili wangu..

Kweli wakili akaja, akaandikisha moja ya kampuni yake kutolewa kwa huyo muuza dawa, pindi akipona maradhi aliyo nayo.

Dawa ikaletwa,...na hata bosi huyo alipodai amuone muuza dawa, muuza dawa hakuweza kupatikana, ...muhimu ikawa yeye kutumia hiyo dawa kwa maelekezo aliyopewa....

Ni kweli tajiri huyu alipona...na aliporidhika kuwa kweli kapona, akawa muda wa kutimza ahadi yake.

Alishauriana na wasaidizi wake, ikawa hana jinsi, wengi walimshauri atimiza ahadi yake.....,ikabidi, hapo ni baada ya kurudi kazi kwake, na kuanza majukumu, alikuwa na kampuni zaidi ya moja, ile aliyoandikisha...ikawa ipo kwenye taratibu za kubadilishwa jina kwa huyo muuza dawa.

Bosi huyo akawa na mihangaiko sasa ya kutafuta wateja, huku na kule, kusafiri nje, ila akatoa maagizo, hiyo kampuni apewe huyo muuza dawa.

Kiukweli bosi huyu kibiashara akawa anayumba..hata kampuni zake alizo nazo, alikuwa akitafuta mtu wa kumuuzia ikabidi apunguze wafanyakazi wengine na wengine wakaenda kuajiriwa kwenye hiyo kampuni aliyompa muuza dawa.

*******

Siku moja tajiri huyu akawa anahitaji nyaraka fulani za kazini za kampuni hiyo aliyoiuza...ilikuwa mambo ya kiutaraibu tu, ikabidi yeye mwenyewe aende kwa yule aliyempa ile kampuni yake, sio yake tena, na alivyosikia kampuni hiyo ilikuwa kifanya vizuri, tofauti na alivyokuwa kwake.

Siku hiyo akafika kwenye kampuni hiyo,....akiomba kuonana na mumiliki mpya ...alifika bila hata taarifa, na kusema....

'Mwenye kampuni hii huyo mganga wa kienyeji yupo wapi?' akauliza

'Yupo nyumbani kwake, labda tumpigia simu...'

'Sawa mpigieni simu, nataka kuonana na yeye, ...kuna mambo muhimu nataka niongee na yeye, uso kwa uso....'akasema

Basi, jamaa akapigiwa simu, jamaa akasema kwa siku hiyo hataweza kupatikana labda siku inayofuata

'Haiwezekani, kwanini...eeh, kampuni nimempa mimi, halafu.....'kabatwa, na kuondoka, maana kiukweli mwenye kampuni hiyo asingeliweza kufika,... ikapangwa siku ya yeye kukutana na huyo jamaa.

Bosi, hiyo akafika siku aliyoahidiwa.....akakaribishwa kwenye chumba cha mkutano...ili kukutana na huyo jamaa. Akawa amekaa anasubiria mara anaingia jamaa

'Oooh...hongera na wewe..umeajiriwa hapa...mimi nataka kuonana na huyo mtaalamu, amenisaidia sana,....aah, niliona mali haina maana....nikampa hii kampuni, naona inazalisha sana, ....ooh..mali,...aah, ....lakini sio kitu maana kiukweli ule ugonjwa nilijiona ninakufa..yupo wapi...'akasema

'Ndio mimi bosi....mwema, aliyekuwa mfanyakazi wako,unakumbuka bosi mimi nilikuwa na karama ya dawa....unakumbuka eeh.

'Haiwezekani, kama ningelijua ni wewe.....oh....ok, hamna shida....'akasema sasa akitahayari.

'Bosi...unajua nilihangaika sana ulipo-eeh niachisha kazi... nikawa naokota chupa za plastiki nauza...baadae likanijia wazo,...mola tu akanielekeza, kindoto, hata sijui nikuelezeje.....basi imani ikanituma hivyo, nifanye dawa.....niendeleze hiyo karama yangu ya asili..ndio nikawa nafanya vyote naokota vyuma chakavu, nauza huku natengeza dawa,

'Kiukweli bosi hizo dawa kwa uwezo wa mola zimewasaidia watu wengi....na hata nilipoambiwa una tatizo....sijui mola alivyonielekeza,....ok, lakini mengine anajua mola..'Akasema Mwema.

'Siamini....'akasema bosi,,,,ajabu alishikwa na kizunguzungu akadondoka....ikawa heka heka tena, baadae akarudi kwake baada ya kupata hizo nyaraka.


WAZO LA LEO: Riziki haigombewi...dhuluma ;lakini ipo siku utadaiwa, ipo siku mwenye haki yake utampa....

Ni mimi: emu-three

No comments :