‘Hata wenye
akili wana kasoro ya akili,..’ akasema babu yangu
‘Kwa vipi
babu…?’ nikamuuliza babu, huku nikijiandaa , maana babu anaanzia mbali.
‘Wengi
wanawaona wale walio na mtindio wa ubongo, au ‘vichaa’ au ‘wendawazimu’ kama
wanavyopenda kuwaita kuwa wao hawana akili…kumbe kila mwanadamu..pamoja ya huko
kujiona ni mkamilifu bado ana kasoro kwenye akili yake, kwahiyo kila mtu,
anaweza kuwa..’kichaa’ bila kujijua…’akasema.
‘Mhh, babu…sio
kweli…’nikasema
‘Nikuulize,
hujawahi kusikia docta bingwa wa maradhi ya kansa, au kifua kikuu, anakufa kwa
ugonjwa huo huo, yeye amekuwa mtumiaji wa gongo, anavuta sigara, au anavuta
bangi..na matokea yake anakuja kupatwa na maradhi hayo hayo ambayo yeye ni
bingwa wa kuyatibu…’akasema kama ananiuliza
‘Haiwezekani
babu mtu mpaka awe dakitari, atakuwa na akili sana…’nikasema
‘Haya tuuache
mfano huo wa wataalamu…, tuangalia mfano wa maisha yetu ya kila siku ya watu wa
kawaida…wewe una safari, umefika kituoni, gari linakuja limejaa kupita kiasi
kwa vile una haraka, au hata huna haraka, wewe unaingia tu,…huku unafahamu gari
kujaza kupita kiasi ni hatari, wewe unajipenyeza ndani ya hilo gari, au unaning’inia
mlangoni kwa shida…huku unajua ni hatari
kwako..
Au mfano
mwingine,…wewe ni dereva unaendesha gari kwa mwendo kasi, wakati unajua ni
hatari…wewe kweli una akili hapo…, kwanini unafanya hivyo,..kwa vile kuna
uwalakini kwenye akili zako, hujataka kufikiria zaidi,…umepungukiwa na
kufikiria hatari ya mbele…na unaendesha hivyo unapatwa na ajali,…je wewe ulitumia
akili yako vyema, je wewe sio kichaa…?’
akaniuliza
‘Hahaha babu…huwezi
kujiita kichaa hapo…’
‘Kuna mtendo
tunatenda, ambayo, hatuoni hatari yake tunapoyatenda,…lakini ni hatari, na
tutaiona hatari yake ‘ ni hatari’ pale hatari ikishatokea, na hapo tutaanza
kujilaumu…kwanini, kwanini…sio kwanini, akili za kufikiria zaidi hatuna…tuna
mapungufu ya akili, tuna nini, upunguani fulani, lakini wenyewe hatujijui..…’akasema
‘Ni wangapi
wanafanya mambo ambayo ni ya aibu, kwenye jamii….siwezi hata kuyataja, mengine hata wanayafanya
wanaogopa kuyafanya…lakini wanaonekana wana akili kwenye jamii kwa vile…hatuwaoni
hivyo, ….’akasema babu akiniangalia.
‘Lakini hiyo babu…huo sio, eeh, sawa na ukichaa, wa yule anayetembea uchi,
akala majalalani uchafu, eeh, sio ndio huyo tunayemuita kichaa…’nikasema
‘Anayetembea
uchi, hamtembei uchii sasa hivi, eeh…hamfanyi mambo hayo, niambie ukweli…’akasema
babu, hapo nikabakia kimia, na aliponiona nipo kimia akaniuliza swali;
‘Hebu
nikuulize swali, kwani, ‘Ukichaa’ au wendawazimu, ni nini mjukuu wangu kwa jinsi unavyoelewa wewe….?’ Akaniuliza
akiniangalia machoni.
‘Ni matatizo
ya akili, mapungufu ya akili,…yanayokufanya usiwe na akili za kawaida ukawa
unatenda matendo yasiyo ya kawaida,…bila kufikiria au kuogopa,..ni yule
anyefanya matendo yasiyo ya ki-kawaida, kama mtu utakiwavyo uwe,…’nikasema
nikijaribu kuwaza nijuavyo mimi kwa wakati huo.
‘Sawa kabisa
mjukuu wangu…’akasema na kuniangalia machoni….
‘Je yule
anayefanya matendo yenye kumuweka
hatarini, kiafya, yenye kukufanya uwe kwenye hatari kiusalama, yenye kukufanya
ufanye jambo ambalo sio la kawaida kutokana na taaluma yako, au kutokana na
utaratibu ulivyo, ukiyafanya hayo, sio umefanya kwa kutokufikiria, na huko
kutokufikiria nini, sio ndio umefanya kwa kutokutumia akili yako vyema …na huko
kutokufikiria vyema ni nini… sio ndio ukichaa huo au...?’ akauliza na mimi hapo
nikacheka.
Sina nia ya
kumkashifu mtu, ila nimeliwaza sana hili, kuwa kumbe sisi sote tuna madhaifu
hayo…ni mara ngapi tumedandia magari, yakiwa yamejaa kupita kiasi tukijua ni
hatari, …na hata kuning’inia milangoni,,… ni mara ngapi tunapanda pikipiki bila
kofia za kinga, ni mara ngapi tunaendesha magari kwa mwendo kasi wenye kuhatarisha
maisha…au kuendesha sehemu zenye hatari.. ..ni mifano michache tu…
Na ni mara
ngapi, tumekula vyakula ambavyo sio salama, ni mara ngapi tumekunywa vinywaji
hatari kwa afya zetu, kuvuta sigara, bangi nk..…na ni mara ngapi tumefanya
mambo ambayo yanatuweka hatarini, mfano kugushi,
kudanganya, kutokuwajibika kwenye kazi zetu,..kudhulumu nk…je tunapoyafanya
haya tumetumia akili zetu vyema, tujiulize tu…
Jeee, kwa
kufanya hivyo, kufanya ‘utofauti’ na hali inayotakiwa,..tukaacha kufikiria
hatari ya hilo jambo, au uhalali wa hilo
jambo, au usalama wake,…hatujawa na ‘uwalakini’… je hapo tunapofanya hivyo,
akili zetu zipo kamili, kweli… eeh,…tusijidanganye, ..kakichaa kadogo kadogo tunako,…kumbe
tunako…
Hahahaha
kumbee, ahsante babu,
Hata mimi au
wewe tuna mapungufu hayo ya akili, ya kutokufikiria hatari ya jambo, kabla ya
kulitenda, basi ili tusiwe hivyo, eeh, ndugu zanguni,… kabla ya kufanya jambo
lolote…, TUFIKIRIE KWANZA, TUTAFAKARI KWANZA, TUJENGE HOJA, JE NIKIFANYA HIVI
NI NINI KITAKUJA KUTOKEA BAADAE,..Tusifanye jambo, kabla ya kutumia akili zetu
vyema.
SOMA KISA CHA 'DUNIA YANGU...' utaliona hili....
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment