Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 17, 2018

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-34


Mara mlango ukafunguliwa aliyeingia sasa alikuwa mpelelezi yule anayeshughulia maswala ya deni,..alitutupia jicho, bila kusema neno,..akaingia ndani.

Kwa haraka akatembea hadi pale alipokaa mwenzake,  mwenzake akasimama, wakawa wananong'onezana jambo...na kuanza kuteta kwa sauti ndogo kwa dakika moja hivi.
.
Yule mpelelezi wa ajali, sasa akatoka sehemu aliyokuwa amekaa, ambapo walitenganishwa na meza na huyo mwenzake sasa akatoka kabisa na kuja hapo aliposimama mwenzake mwenzake na kumshika mkono, ikawa kama anamtaka watoke wakaongele nje..

'Una uhakika,...?' akauliza na mwenzake akatikisa kichwa kukubali, bila kusema neno

'Haiwezekani...ok, ok, laini hiyo sasa ni hatua nzuri, maana walifikia kuniandikia barua ya onyo, sasa watasemaje, ok, vipi kuhusu hii kezi yetu...?' akauliza huyu mpelelezi wa ajali.

'Yah, ipo pa zuri sasa, ipo kesi ya kupeleka mahakamani, ngoja tumalizane na hao watu, ...'akasema huyo mwenzake

Wakawa sasa wakiongea, kwa sauti ya kawaida  huku wakitembea kuelekea mlango wa kutokea nje..., walipofika pale nilipo, wakawa wamesimama, sasa wakapunguza sauti , wakawa wanaongea kwa suti ndogo, kwa pale nilipokaa mimi nilikuwa nawasikia japokuwa kwa shida;

‘Nimeona kama mumekuja na watu ...ni wahalafu wa nini hao, au ni watu wanaohusiana na hii kesi yetu…?’ akauliza 

‘Ndio…wanahusiana na hii kesi yetu....hao watu ni muhimu sana kwetu...tulitaka tuwakamate hata  familia zao hao watu tunaowatafuta,lakini tumeziacha kwanza kama mtego...'akasema

'Mhh..ni sawa..kazi nzuri...'akasema

'Unajua... hao watu wawili waliotoroka ni muhimu sana kwetu, tukiwapata tutakuwa tumekamilisha , na kesi itaenda mahakamani…’akasema.

'Lakini ...kwa, kosa...bado sijawaaah.. ..'akasema bila kumalizia, sikusikia alichoongea mbele yake.

'Kosa lipo...bila shaka,.wizi, na...mengine utakuja kuyasikia, ..ushahidi ukikamilika, sio kitu kidogo..watu wa ustawi wa jamii wamekuja juu kweli, wamewaendea hadi wakubwa, yaonekana hapa kwetu kuna tatizo, sasa mimi siwezi kulikubali hilo,...'akasema huyo aliyeingia

'Ujue hao watu wana pesa, watatafuta mawikili, kama hatutakamilika , itakuja kutuumbua sisi wenyewe, mimi bado sijaona ushahidi bado, kuna eeh, ...'sauti ikawa haisikiki zaidi, na yule mpelelezi akarudi mezani na kuchukua ile bahasha.

'Sijui kama hii itakusaidia.....'akasema mpelelezi huyo

'Itasaidia...una uhakika haijaguswa na....huyo aliyeileta...?'akasema akikagua ile bahasha, 

'Kasema hajaigusa....'akaambiwa

'Basi ngoja...nimalizane na hao watu, ihifadhi kwanza...'akasema akimrejeshea huyo mwenzake.

Baadae wakawa wanaongea kwa taratibu sana sikuzikia kitu, ...halafu sauti ikaja kusikika tena...

‘Na ni nani hao mliowakamata,. hao mliokuja nao..?’ akauliza

‘Ni jamaa wawili, wanahusiana na hao watu tunaowatafuta....'akasema

'Huyo mmoja ni msaidizi wa mtaalamu, yeye kazi yake kubwa ni kutumwa huku na kule anajua mengi kumhusu mwenzake,...kuna mambo tunahitajia kuyafahamu, ya undani kumuhusu huyo mtu anayeitwa mtaalamu...sivyo kama anavyoonekana...'akasema


'Oh...kumbe...'akasema

'Tumegundua mengi...sasa huyu  anadai..mwenzake anaweza akawa kwenye hali mbaya kutokana na uchunguzi wake…’akasema

‘Hali mbaya kwa vipi...?' akauliza

'Wakati anatoroka kumbe mlinzi wetu mmoja alimuona, akamrushia risasi ikamjeruhi, sasa huyu kafahamu vipi, maana kasema mtaalamu yupo kwenye hali mbaya,..yeye anadai eti, kaona kwenye kiona mbali chao..'akasema

'Kiona mbali, ndio nini hicho....?' akaulizwa

'Ramli...hahaha, ndivyo alivyosema...'akasema mpelelezi.

'Kasema nini zaidi..?' akauliza

‘Bado,...anazidi kusema yeye hajui, hata yeye anamtafuta sana huyo jamaa kwani kuna pesa alimkopesha, na yeye hiyo pesa, alichukua kwenye vikundi vyao...na jamaa alimuhakikishia kuwa pesa hiyo atairejesha, maana kuna mnada mkubwa utafanyika,…’akasema

'Mnada mkubwa...! ? ndio huo wa nyumba ya mjane na watoto..?' akauliza

'Ndio huo ,..sasa jiulize ni pesa kiasi gani cha kuwagaia watu wote hao, kama si kuna jambo limejificha hapo, na hapa inaonekana hata benki wanahusika na hilo.....'akasema

'Umeweza kuongea na benki...?' akauliza

'Mzungumzaji wao hayupo, ila nimewasiliana naye kwa simu, kanielezea mambo mengi sana,..yeye anaweza kuwa shahidi muhimu...kama naye hahusiki...'akasema

'Duuh..sasa eeh, naanza kuiona picha kamili,...'akasema

'Sasa hao watu wawli uliowaleta, unahisi wanaweza kusaidia, maana chumba cha mahubusu kimejaa ..?' akauliza

'Muhimu ni kuwapata hao wahusika wawili, ..., hawa tunawatumia tu, ngoja tuone ushirikiano wao upoje...'akasema huyo mwingine.

‘Kwahiyo kwa kifupi mpaka sasa hamjafahamu wapi alipo huyo mtaalamu..?’ akauliza

‘Bado,..yaani kapotea kinamna, hata yule mwanamke wake naye haonekani, tulijua kajificha kwake, naye huyo kapotea, yawezekana wapo pamoja... ila tutafahamu tu wapi alipo…kila kitu kipo tayari, na sasa ...wote wanaohusika watafikishwa mbele ya sheria, tunasubiria maelezo yako tu, ili tuweze kuuanganisha haya mambo mawili...'akasema

'Mhh, mpaka sasa haya ya kwangu sijaona mahusiano yake na uchunguzi wenu...'akasema

'Mhh, umemuhoji vizuri,..?' akaulizwa.

‘Sijaingia kiundani, maana unajua ilipopotea ile taarifa yangu, nilipata shida sana,..lakini kwa vile sasa nimepata hiyo nakala yake,...naamini nilichogundua kipindi kile kinaweza kuleta picha halisi, mimi bado sijaamini kuwa hiyo ni ajali ya kawaida..'akasema

'Sasa jiulize kwanini hiyo ajali iaktengenezwa, na ni nani alianya hilo..'akasema


'Mhh, bado mimi sijaipata hiyo picha...'akasema

'Utaipata...hasa tukiwapata hao watu wawili...'akasema

'Na huyu...'akasema mpelelezi akigeuza kichwa kidogo, ni kama alikuwa akinionyeshea mimi.

'Wewe m-Mbane kivyako, na mimi nitakuja kumalizia kazi...'akambiwa

***************

Mimi kwa haraka nikageuka kumuangalia Dalali, naona na yeye alikuwa akihangaika kusikiliza hayo mazungumzo,..nahisi kuna kitu walikuwa wakiongea na wakili wake, halafu baadae ndio wakawa wanajaribu kusikiliza hicho wanachoongea hao wapelelezi, sikuwa n uhakika kama wamesikia...maana wapelelezi wale wawili walihakikisha Dalali na mwenzake hawasikii kitu,...

Nilipogeuka kumuangalia Dalali, macho yetu yakakutana na mimi nikatabasamu lile tabasamu lake la dharau, yeye hakutabasamu,…kilichoonekana sasa ni uso wenye mashaka,, …hapo nilitaka kumuongelesha, lakini nisingeliweza kufanya hivyo, kwani hawa jamaa walikuwa bado hawajatoka nje.

 Kabla sijaondoa macho yangu kwa Dalali, maana nilimuona akitikisa kichwa, kama kuna kitu kinamsumbua,.au kukubaliana na jambo fulani....sikuwa na muda wa kumkagua kwa kumuangalia vyema, kuna jambo waliongea hawa wapelelezi wawili likanifanya nimsahau Dalali kwanza;

‘Na huyo mwingine, ni nani…?’ sauti ikauliza

‘Huyo ni mshirika wa karibu sana wa yule mfanyakazi wa benki,..tumekuja kugundua kuwa, huyo jamaa ni rafiki mkubwa wa huyo jamaa wa benki..na tabia zao zinafanana-fanana, na wameamua kuwekeza pamoja, kitu cha kushangaza, uwekezaji wao, haujionyeshi wazi wazi, usoni mwa watu...kila mmoja ni kama anafanya shughuli zake kivyake, lakini kumbe ni washirika..’akasema.

‘Mhh, sasa kwanini wakafanya hivyo,..mmh…sasa naanza kuelewa..’sauti ikasema.

‘Hujaelewa bado…kwa hivi sasa yeye, huyu jamaa tuliyemkamata,  anadai, mwenzake kamtapeli, kaondoka na pesa nyingi, lakini hajui wapo huyo mwenzake alipo, zaidi kasema mwenzake alianza kama kuchanganyikiwa siku za hivi karibuni,,,,anadai mwenzake anaongea maneno yasiyoeleweka,..'akasema

'Mbona hadithi inakuwa kama inafanana na yule wa kwanza, madai madai..yana ukweli hayo..?' akauliza

'Haijajulikana wazi, yeye anadai hivyo, na yule wa awali anadai hivyo...sasa kama ni hadithi ya kutunga, tutalifahamu hilo, hawana ujanja tena…’sauti ikasema.

‘Mhh hapo nahisi maumivu ya dhuluma, mtu aliyezoea kudhulumu wengine, alidhulimuwa anaumia sana,… kwahiyo sasa ni mchezo wa kusalitiana au sio, hapo ni kumbana vyema atafunguka zaidi...'akasema

'Sawa nimewaacha vijana wakifanya kazi yao...nilitaka nije kidogo kuonana na Dalali, nihakiki jambo..unaelewa...'akasema.

Dalali, …Dalali, alikuwa katoa macho tu, akiniangalia mimi bila kutikisika,..angalia ile ilinifanya niingiwe na mashaka,.mtu anakuangalia hapepesi macho,…mimi kwa haraka nikaangalia pembeni…yale macho sio ya mtu wa kawaida, imekuwaje…

Na mara wapelelezi wale sasa wakawa wanafungua mlango.

‘Tumejaribu kumbana ili aongee zaidi, lakini hajafunguka bado, ila kwa kiasi alichoongea imetupa njia nyingine ya kulimaliza hili tatizo, hatua inayofuta ni huko benki, alipokuwa akifanyia kazi,…na wao wana kitu tumekiona..sio bure.., sijui kwanini hawakufungua mashitaka…’sauti ikasema

‘Ok..huyo mwenzake yupoje kwenye maisha yao ya kawaida...?' akauliza

'Yaani wawili hawa huwezi hata kuwadhania, wamekuwa kwenye maisha ya kawaida tu, wanavyojiweka kijamii, huwezi fahAmu wana mali hizo zote..sasa sijui ni  ...’ sauti ikasema na kufifia


‘Kwahiyo hapo swali muhimu wamezipatia wapi hizo mali, na kwanini wanazificha, hawataki kujuliana, au sio…?’ akauliza

‘Umejuaje hilo,…?’ akauliza

‘Hahaha…pua hunusa, na macho huona, lakini akili inafikiria zaidi..yule mtu nimeshamfahamu, sikujua kuwa mali hizo ni zao, kuna tukio nilifuatilia,  nilipoambiwa ni mali zake huyo jamaa sikuamini,...kumbe yupo shirika na huyo jamaa aliyekuwa mfanyakazi wa benki…’akasema

‘Wote waliwahi kufanyia kazi benk…’akasema mpelelezi

‘Unasema nini..oh..!?’ sauti ikauliza kwa mshangao

‘Ndio hivyo, ngoja nikamalizie kazi yangu kwanza..., najua nikirudi utakuwa umeshamalizana na Dalali, nilijua umemalizana naye, nimuhoji kidogo, kuna kitu nilitaka kuhakiki kutoka kwake, na huo ushahid nitakuja kuuhitajia baadae…’sauti

‘Kitu gani…?’ akauliza

‘Ok, wewe malizana naye kwanza, nitamuhoji baadae, …nataka hii kazi imalizike leo nakesho wafikishwe mahakamani…unasemaje kwa upande wako...’akasema mpelelezi, na wakawa wameshatoka nje.

Kabla hawajafunga mlango, nikasikia sauti ikisema

 ‘Ukimaliza naye, huyo  Dalali niambie...'sauti ikasema

‘Yah, nitakuambia, ...'akasema, sikuweza kusikia maneno hayo ya mwisho.

‘Yule aliyekaa naye ni wakili wake…?’ sauti ikauliza

‘Ndio…’sauti ikasema

‘Basi wamekutana...kesi ya udalali, imakuwa mtama uliorushwa kwenye kuku wengi, sijui ni nani atapata hapo.... hahaha, …’kikasikika kicheko, na mlango ukafungwa.

********

Kicheko kile kilinifanya nigeuke kumuangalia wakili, nikaona huyo wakili sasa akimuangalia Dalali, Dalali alikuwa vile vile kanikodolea mimi macho..na Dalali alipoona namuangalia sasa akajifanya kama kugeuka kidogo halafu akarejesha macho kuniangalia ..

‘Dalali umeyasikia hayo walikuwa wakiongea hao wapelelezi…?’ nikauliza

‘Hapana, na sina haja ya kuyasikia,...muhimu waje tumalizane , mimi siwezi kuendelea kuteseka hapa, wakati sina kosa, mizimu inaniuliza nimefikia wapo...wanataka kurudi…’akasema

'Kurudi wapi...?' akauliza mama mjane.

'Mimi niliwaambia nini...'akasema Dalali

‘Dalali mimi nakuusia, …sasa hivi, ni bora uwe mkweli, maana sasa ukweli umeshagundulikana,  wenzako wote wameshaongea ukweli wao..mimi nilikuambia tokea awali…’nikasema

Dalali akawa anakodoa macho ...ananiangalia, halafu anakuwa kama anapata shida fulani, anatamani hata kuvua lile koti.....

‘Ni-ni-mesha sema mimi ..si-sina ma-ma-kosa, sijafanya, mimi mnanionea bu-bure…’Dalali akawa anaongea hivyo,...lakini kwa shida mdomo ulionekana mnzito.

‘Shemeji mbona unaongea hivyo…kama umeingiliwa na mizimu yako?’ akauliza shemeji yake, akimuangalia Dalali kwa mashaka

‘Mhh..ni-nipo sawa-sawa…mizimu eeh, mmh, umejuaje shemeji, ..na-na jaribu kuisihi, wanataka kurudi, 'akasema, na mama mjane akamuangalia kwa uso wenye mashaka

'Watoto wangu, inabidi niondoke..'akasema mama mjane

'Usijali, shemu, mwenye mamlaka wa hiyo mizimu ni mtaalamu, ...yupo wapi sasa, na hana uwezi wa kuwasiliana na Dalali, simu ...ndio ilikuwa kiunganishi chao...'nikasema

'Hahaha....hahaha...ooh, kwenu ahsanteni waheshimiwa...'akasema Dalali, na mara akatulia kimia, baadae akahema kama ametokea usingizini, na aliyemuongelesha sasa alikuwa mama mjane.

‘Shemeji…samahani lakini, mimi nahisi wewe unaufahamu ukweli, na unawaafahamu waliofanya hivyo, ila wewe unaogopa kuwasema, au sio shemeji, unawaogopa,..maana wewe huwezi kufanya hivyo,...huwezi…’akasema mama mjane.

‘Shemeji, umeungana na huyo jamaa yako, niamini mimi shemeji, unaona mizimu imesema imefurahi, juhudi inafanyika sasa kuhakikisha hilo deni linalipwa, wanaendelea kutupatia muda,...sasa sijui kwa vipi..deni hilo linalipwa...'akasema

‘hemeji mimi siongelei hayo ya mizimu yako, ...mimi nataka kuufahamu ukweli je wewe hujui lolote kuhusu hilo deni,..kama unafahamu nakuomba tafadhali, jiweke wazi ili tuone tutafanyaje…’akasema mama mjane

‘Ukweli kuhusu deni,…hahahaha, shemeji yaani nilivyoongea hapa hukunielewa, kaam mzimu inatafuta deni lilipwe, hapo unataka kusema nini..deni lipo, na ...unajua ni hivi shemeji, kama ngelikuwa ni deni dogo tu, tungelisema hivyo, lakini hilo deni ni kubwa sana, sasa tutafanyaje hapo, .’akasema

‘Ina maana hadi sasa wewe unaongelea kuwa hilo deni ni la mume wangu..shemeji hilo deni sio la mume wangu…’akasema mama mjane

‘Hilo deni ni la Bro….unataka niseme mara ngapi, …mimi nimefuatilia kila kitu benki,na hawa mizimu wamenisisitizia hilo, kama unabisha shauri lako…’akasema

 ‘Sasa hivi mimi ninaanza kuogopa, kama ile ndoto iliyonielekeza hadi nikapata huo ushahidi je na hayo mengine niliyoyaona kwenye hiyo ndoto yakiwa ni kweli..hapana …shemeji tafadhali nakuomba uwe mkweli..ili haya mambo yaishe kwa amani…’akasema mama mjane

‘Nimeshakuambia mimi sina makosa, nijuavyo mimi hilo deni ni la Bro, …sijui lingine lolote,.unasikia shemeji, hivi mimi hadi nimefika hapa, kwanini niendelee kuwa mkaidi mimi nitapata nini hapo eeh, shemu hilo deni ni la Bro...'akasema Dalali

‘Hizo nyumba mumejanga kutokana na pesa gani…?’ akauliza mama mjane, hilo swali ni kama lilimshtua Dalali kutoka kwenye dunia nyingine.

‘Shemu....mmh...hayo sasa ni mengine…'akasema

'Je si kweli kuwa una majumba ya kifahari, matatu, au sio...kuacha hiyo ya...ni kweli si kweli...?' akulizwa

'Shemeji, hayo ya nyumba ..hayakuhusu,..kumbuka kitu kimoja shemeji, maisha yanatafutwa, kuna njia nyingi za kupata pesa, mimi ..nilihangaika kivyangu, tokea Bro yupo, na yeye alikuja kuligundua hilo, mbona hakusema zaidi...sikiliza shemeji mimi sijachukua hilo deni kwa kujengea nyumba zangu, nyumba hizi nimejenga kwa mbinu zangu nyingine..’akasema

‘Shemeji samahani sana..ila mimi siwezi kukuamini tena..’akasema mama mjane

‘Hiyo ni shauri lako,…kama huwezi kuniamini basi mungu wangu ni shahidi yangu, kuwa hizo nyumba ni kutokana na madili yangu mengine...inatosha kabisa kusema hivyo.. hata hao maaskari, wanaotaka kunichimba, kunidadisi kuhusu nyumba, watafikia sehemu watagonga ukuta..’akasema Dalali kwa kujiamini…sijui kitu gani kimemfanya ajiamini hivyo tena.

'Na huo ushahidi...'akauliza mama mjane.

'Ushahidi upo wapi...?' akauliza Dalali

‘Ushahid …unataka ushahidi gani tena…shemeji kwanini unaigeuka familia yako mwenyewe hizo barua je…?’ akauliza mama mjane.

‘Kama wewe umenigeuka , unatarajia mimi nifanye nini shemeji..hivi sasa,...utamuona yule Dalali mwingine, ...nakuambia hili wazi...na kwanza, ukisema eti mimi nimewageuka, ..kwanza..eh, mimi sijui unamaanisha nini, mimi sijaigeuka familia yangu, na wala sitakutaka kufanya hivyo, nahangaika kivyangu kuilisha familia zote mbili, ina maana kuwalisha nyie sasa inageuka kuulizwa napatia wapi pesa eeh..…’akasema Dalali.

‘Sijakaa hilo, unatusaidia sana, lakini huu ukweli wa deni, …nakuomba tafadhali shemeji kuwa mkweli, hilo deni sio la Bro, kiri hilo…’akasema mama mjane

‘Nini.. shemeji, unataka niseme nini sasa,..narudia tena , maana baada ya hii kauli yangu, sitapenda tena kulirudia hili kwko, shemeji, ku-ku-ku...mmh, kunishuku kwako huko, kutanifanya nianze kukuweka kundi jingine, nimeshasema ukweli wangu wote kuhusu hilo deni,..’akasema

‘Hapana shemeji kwa hilo ni bora unieweke huko tu,...mimi mwenyewe nashindwa kukuamini tena,....Dalali, hadi hatua hii, unadiriki kusema kuwa wewe hujui lolote kuhusu hilo deni, na ya kuwa hilo deni ni la kaka yako..?’ akasema mama mjane

‘Kiukweli mimi sijui,zaidi ya hivyo, wanavyodai benki...kuwa hilo deni ni la bro, sijapata ushahidi mwingine zaidi ya huo, nitasemaje,..haya tumefika huku polisi, wawasaidie basi, au watusaidie basi kuupata huo ukweli,..kipo wapi, wanazunguka na mambo mengina kabisa, ajali..ajali ..si ajali tu…’akasema


‘Sasa huo ushahidi uliotolewa hujauamini, eeh,..?’ nikamuuliza.

‘Ushahidi upi...hiyo barua… hiyo barua hatujasoma tukaona ni nini kimeandikwa,si ndio hivyo, tukiisoma na ikaonyesha hivyo, kuwa hilo deni sio la Bro, mimi nitaungana nanyi, vinginevyo, mimi bado nitakuwa na msimamo wangu..manjua ni kwanini nafanya hivyo....je hiyo barua inasemaje..huenda ilikuwa barua Bro aliandika ya kuomba mkopo, wa hilo deni,je ikiwa hivyo mtasemaje…?’ akauliza

‘Mimi nimeisoma,…sio barua ya kuomba mkopo, …’akasema mama mjane

‘Ni barua ya nini sasa sema ukweli wako, kama inasema hilo deni sio la bro, basi mimi nitakuwa pamoja na nyie,..ehe, sema ilihusu nini hiyo barua..?’ akauliza Dalali

‘Ni barua ya kulalamika,..kaka yako alikuwa analalamika kuwa kuna pesa zimetolewa bila ridhaa yake na sio mara moja, kaziorodhesha hizo pesa zilizochukuliwa kutoka kwenye akaunti yake,…kwa tarehe tofauti tofauti, na akaandika, kiasi ambacho kimebakia kwenye dhamana yake…’akasema

‘Kwahiyo haijagusia hilo deni. Au sio.?’ Akauliza Dalali

‘Haijagusia, itagusiaje wakati hilo deni halikuwepo..kwenye hiyo barua kaandika salio lake lilikuwa kiasi gani, kwa masahihisho yake aliyoyayafanya akaandika kiasi ambacho anatakiwa awe nacho kama salio lake halisi,lakini kwenye statement ya benk haionyeshi hivyo…’akasema

‘Je umeangalia barua hiyo iliandikwa tarehe gani…?’ akaulizwa Dalali

‘Mhh..ni tarehe za kabla hajaondoka hiyo safari yake aliyopatia ajali…’akasema mama mjane

‘Na je hilo deni lilichukuliwa lini…?’ akauliza Dalali

‘Sijui…’akasema mama mjane

‘Hilo deni lilichukuliwa awali kabisa, tarehe ..kabla ya safari, baada ya wiki moja akaongea kubwa lao..mimi mwenyewe sikuamini...na hiyo ya kulalamika,...kwanini hakuaniambia mimi...?' akauliza

'Mimi sijui ..maana sikuwahi kusikia akilalamika...'akasema mama mjane

'Unaonaeeh...hakuna kitu hapo...'akasema Dalali kwa kujiamini

'Dalali...'nikasema lakini hakunipatia muda

'Sikiliza wewe, wewe ndio umesababisha yote haya,..nikuambia sasa ilivyokuwa…ina maana kwamba, bro alitarajia kuwa ana salio la kutosha, ili akachukue mizigo, kwa jaili ya biashara zake...ndio akaja kugundua kuwa salio hilo halipo,..akaandika hiyo barua, na wakati huo umeshaagiza mizigo, unafikiri wangelimuelewa wenzake,... ndio akaamua kuchukua mkopo..’akasema Dalali

‘Lakini pesa iliyochukuliwa ni nyingi sana, haiji akilini kuwa alichukua kiasi hicho kikubwa kwa ajili ya biashara….’akasema mama mjane.

‘Labda yeye aliamua kuchukua nyingi ili afanyie kazi nyingine, kujenga, au kufanya jambo kubwa zaidi ni nana anajua hilo kusudio lake hapo, ni nani anajua kuwa aliandika hiyo barua, hakuna...sasa kwanini asichukue mkopo na nyie msifahamu.. ‘akasema Dalali

‘Una uhakika na unachokisema Dalali…’nikamuuliza Dalali, nilimuona kama anaongea tu, ..hata siamini kuwa huyu mtu, baada ya kusikia hayo yote bado angeendelea kuwa na msimamo huo

‘Mimi nawazia hivyo, kuwa labda alichukua hiyo pesa kwa madhumuni hayo, na ukumbuke kuwa gari liliungua, je..ni nani anajua, huenda kila kitu kilingua ikiwemo hizo pesa…’akasema Dalali

‘Ni kwanini basi hizo kumbukumbu za beni zipotee, ina maana alizibeba , ndio zikapotelea huko…?’ nikamuuliza

‘Hata mimi hapo ndio sielewi…kwanini hizo kumbukumbu zipotee, kwanini..hizo barua zichomwe moto..mimi kiukweli hilo sijui kabisa, …’akasema Dalali

‘Shemeji, mimi nakuuliza tena, je wewe unasema ukweli, kuwa kweli hujui lolote kuhusu hilo deni, na hujui lolote kuhusu hiyo ajali..?’ akauliza mama mjane

‘Shemeji unataka nifanye ili uniamini…?’ akauliza Dalali

‘Uape..’akasema mama mjane

‘Niape,…mimi nilijua utasema twende kisheria, ni kupata tu, mimi nitaapa kwa vile nina uhakika sina kosa, unataka niape vipi..?’ akauliza

‘Apa kwa mungu wako…’akasema shemeji yake

‘Haya mimi Dalali naapa kuwa..sijui lolote kuhus hilo deni,…’akasema Dalali, na mara akashikwa na kitu kama kwikwi…

‘Shemeji…shemeji…usijiapize utapata shida wewe, mali zitakupeleka kubaya…’akasema shemeji yake

Dalali akatulia kidogo, ile kwikwi ipite, halafu akachukua chupa ya maji na kunywa mafundo mawili…halafu akasema;

‘Leo kwikwi imeniandama kweli…tangia niamuke asubuhi…’akasema

‘Sio ishara hiyo…’akasema shemeji yake.

‘Ishara ya nini….?’ Akauliza

‘Mizimu yako..’akasema mama mjane,

‘Shemu…niamini mimi, nisingelifanya hivyo, unanijua nilivyo, kamaa nimekosea jambo ukiniambie niape, siwezi kuapata, nafahamu madhara yake,…’akasema Dalali, na hapo mama mjane  akisimama, akatembea hadi dirishani akawa anaangalia nje.

‘Dalali…kuapa ni wewe ni mungu wako, lakini sheria itakubana..ushahidi mbali mbali umeonyesha kuwa wewe unahusika…’nikasema

‘Acha huo ushahidi uje, twendeni mahakamani…mimi siogopi…maana sina kosa,..unajua awali nilikuwa naogopa, lakini ishara zimenionyesha hivyo, nisimamie kwenye haki, ukweli…na..hata huyo mtaalamu, najua mnamsingizia, yeye alinishauri sana, kuwa kama ni kweli sijui, nisije kuvunja kauli yangu…’akasema

‘Hahaha, kwahiyo yeye ndio alikudanganya kuwa usije kubadili kauli yako, hata kama ni kweli sio..?’ nikamuuliza

Mama mjane akaongea sasa, lakini akiwa badi kageukia dirishani, akasema;

‘Dalali, nakuita kwa jina lako la kikazi..kama kweli unayosema, kuwa hujui lolote, kama ni kweli, basi, mimi sioni ni kwanini tupoteze muda, …ndugu zanguni, mimi sioni haya ya kumshambulia huyu mtu, kama kweli kaapa, kwa jinsi nimjuavyo, hana hatia,…’akasema mama mjane.

‘Dada, hilo tuachie sisi,…hatua iliyofikia huyu mtu kama anaendelea kubisha, atawakilishiwa kila kitu, ushahidi …utakaombana na ikibidi ataingie mahakamani kama ndivyo anavyotaka,..wewe mwenyewe utaona..’nikasema

‘Wewe ulikuwa unategemea hiyo barua, si ndio hivyo, kama ushahidi wako, haya hiyo barua imesema nini kuhusu deni, hakuna kitu hapo…’akasema Dalali kwa kujiamini.

‘Wewe umeisoma hiyo barua…?’ nikamuuliza

‘Shemeji kaisoma, …na kaeleza ilivyoandikwa…’akasema

‘Dalali,…kwanini unataka kusumbua watu…?’ nikamuuliza

‘Sisumbui mtu hapa…mimi najitetea..na ukweli ndio huo,mimi sijui lolote kuhusu hilo deni na sijui lolote kuhusu kuchomwa moto kwa hivyo vitu, huo ndio ukweli, sasa kam mnataka kulazimisha haya,..na shemeji kasema niape,..nimesha-apa, mnataka nini zaidi kutoka kwa-kwa.ngu…’akasema Dalali, akjaribu kupambana na kwikwi.

Akatulia, lakini kwikwi ikaendelea …sasa Dalali akawa anashikilai kifua

‘Hii ni nini tena,....’dalali akawa anasema hivyo,..na wakili wake akasema.

‘Huyu mtu hayupo sawa, kaongea sana, anahitajia mapumziko,…’akasema wakili
Shemeji yake aliyekuwa kasimama sasa akageuka kuangalia upande ule alipokaa Dalali na wakili wake, kwa muda ule ..Dalali sasa kwikwi ikawa anampiga kwa mfululizo, mapaka anakosa hewa

‘Vipi Dalali, …’nikauliza sasa nikijiandaa kusimama, lakini kabla sijasimama, Dalali huyo akadondokea sakafuni. Kitendo kile cha kudondoka kilikwenda kwa haraka hata wakili wake hakuweza kuwahi kumzuia.

‘Vipi Dalali…’ wakili wake naye akasema hivyo.

‘Mungu wangu…’aliyesema hivyo ni shemeji yake akiwa kashika kichwa, sikuwa na muda wa kumuuliza kwanini kafanya vile,

‘Kwanini nimemuambia aape, na kwanini akaapa wakati anajua ana makosa…’akasema shemeji yake sasa, watu wa huduma za kwanza wakaitwa na kuanza kumuhudumia Dalali,
Ilionekana hali ya Dalali ni ya hospitalini, ..gari la wagonjwa likaitwa, …na wakati anawekwa kwenye kitanda cha wagonjwa, Dalali alijitahidi akasema ;

‘Mi-mi aah, si-na ko-sa…wa-na-nni-onea –bure..’akasema hivyo, na akapoteza fahamu
NB: Je ni kweli Dalali hana kosa,


WAZO LA LEO: Mola wetu ni mwingi wa rehema, mwenye kusamehe wakosaji, tukitubu kwake kwa dhati, lakini kuna makosa ambayo twahitajika kuwaomba wale tuliowakosea, wakati mwingine katika haya maisha, wengine hujiona wamefika, wakawa wanawakosea wengine  kwa makusudi tu, kwa kiburi tu, kwa vile ni watawala, au ni mabosi maofisini, tuliangalia hili,..maana makosa kama haya , toba yake ni kuwaomba  wale tuliowakosea msamaha, tuwapatie haki zao kwanza,..maana tukisubiria milango ya toba ikifungwa, tutakuwa hatuna pa kukimbilia.
Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

good job, endelea mkuu, ipo siku watakufahamu tu