Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 4, 2018

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-18


‘Nauliza swali tena, je hukuwahi kuingia tena, kwenye chumba ambacho kaka yalo alikuwa akihifadhia kumbukumbu zake, ukafungua hilo kabati, baada ya kaka yako kufariki…?’ nikamuuliza;

‘Sikuwahi, siku-wahi….’akasema

‘Una uhakika…?’ nikauliza

‘Ndio…’akasema

‘Wewe ni muongo…’nikasema na hapo ndio akahamaki

‘Kwanini, unasema mimi ni muongo…ina maana wewe ndio unafahamu zaidi yangu, wewe ulikuwepo eeh, niambie wewe ulikuwepo…?’ akanitolea macho, halafu akatabasamu ile ya kuigiza.

Mimi kwanza nilikaa kimia, ….na alipoona nimetulia hivyo, akasema;

‘Unajua mimi siwezi kukulaumu,…nafahamu bado huamini hilo..ila mimi nimejaribu kukuelezea ukweli wote ulivyokuwa..na…, hahaha….inasikitisha sana… , halafu wewe  unaniita mimi muongo, naweza kukuuliza wewe kama nani, lakini mmh, sawa, mimi sina hiana, nashukuru…’akasema hivyo na kutulia kidogo halafu akasema

Bado mimi nikaendelea kukaa kimia, nilitaka nimpe muda, wa kuongea….

‘Sasa eeh…kama wewe unaufahamu huo ukweli, zaidi yangu mimi, ina maana wewe ulikuwepo, eeh,… haya tuambie wewe ilikuwaje, na kama wewe unaufahamu huo ukweli, mimi najiuliza tu,…kwanini unapoteza muda kwa kuniuliza-uliza hayo maswali eeh…si unajua bwana eeh, mimi si muongo, kwanini sasa wanauliza hayo maswali…?’akawa anaongea, akigeuza kichwa kwa mpelelezi…na kwangu.

Tuendelee na kisa chetu

************

‘Wewe kwa kauli yako , ulisema, mlihangaika kutafuta nyaraka zote ndani kwa marahemu, na hamkuweza kuziona, ukiwa na maana  nyaraka za benki, kweli si kweli…je katika kutafuta huko mlitafutia wapi, kama sio huko-huko,… kwenye hicho chumba, au wewe utasema hukuingia huko ndani, haya, sema huo ukweli wako..?’ nikamuuliza

‘Hahahaha..yaani kumbe ndio maana yako hiyo....sasa ndio nimekuelewa, katika utaratibu huo, sikuwa peke yangu, tulikuwa tunatafuta watu wote, akiwemo wakili…kama ni hivyo, sawa, niliingia lakini sio mimi, ni ‘si-si’ tatizo la Kiswahili, uliza swali lieleweke vyema bwana…’akasema

‘Uwe mkweli…Dalali,….ujanja , ujanja wa kidalali, hapa hakuna….mpelelezi kakuambia, uwe mkweli, na nakuona unajaribu kuficha jambo…’nikasema.

‘Huo ndio ukweli sasa, ulitaka nisemeje, niambie wewe…’akasema

‘Kwa mtizamo huo, …wewe uliingia kabla, na ndio maana siku ile wewe uliwaelekeza wapi hizo kumbukumbu zilitakiwa ziwepo,  …ulisahau kuwa nyumba hiyo anaishi mama mwenye nyumba, na mama mwenye nyumba, aliwahi kuziona hizo kumbukumbu kabla mumewe hajafariki, sasa hizo kumbukumbu zilikwenda wapi…?’ nikamuulia

‘Sio kweli, mimi nimemuuliza shemeji mara nyingi, wakili naye halikadhalika,… hata huko mahakamani aliulizwa hilo swali, akasema yeye hakumbuki, kuziona ..maana  yeye mara nyingi alikuwa hana habari na maswala ya mumewe ya kibenki, hawakuwahi kufikia huko , hadi kuulizana maswala ya kibenki…..’akasema

‘Dalali, iweje mtu awe na akaunti benki, hata statement ya mwezi isiwepo, hata ile nakala ya kuchukua na kuweka isiwepo…hapo ina maana gani, huyo mtu aliyezichukua hizo kumbukumbu, alihakikisha kuwa hakuna nakala yoyote ya benki inayopatikana,sasa jiulize hapo ni  kwanini akafanya hivyo..?’ nikauliza

‘Mimi sijui… maana sisi tulijitahidi kuzitafuta hizo kumbukumbu na wakili, lakini hatukuwahi kuziona,..hakuna kumbukumbu yoyote ya benki, kamuulize hata huyo wakili…hata mimi nilishangaa…’akasema

‘Kwahiyo…’nikageuka kumuangalia mpelelezi, huku nikisema;

‘Nionavyo mimi washukiwa wa upotevu wa hizo kumbukumbu, hasa za kibenki…ni huyu Dalali,  na shemeji yake, nyie wawili mtuambie  ni nani alizichukua hizo kumbukumbu na zipo wapi, maana huo ni ushahidi muhimu sana,..je, utatusaidiaje kwa hilo…?’nikauliza.

‘Kuharibu..!!!, kwanini mtu aharibu kitu muhimu kama hicho, mbona haiingii akilini, hapo sizani kama upo sahihi….na mimi sijui, nitakuambia nini hapo…’akasema.

‘Nikuulize wewe….’nikasema

‘Mimi sijui…’akasema

‘Hujui sio…. Haya swali jingine,…, wakati marehemu yupo hai, wakati mpo naye hamukuwahi kufanya mambo ya kibenki pamoja, mkiwa hapo anapohifadhia kumbukumbu zake…?’ nikamuuliza

‘Tumefanya mara nyingi tu,..lakini kama nilivyowahi kukuambia..yeye kwenye maswala ya kibenki…kama ni kujaza fomu za kuchukua pesa anafanya yeye,…kama ni kuweka, anaweza akanihesabia pesa, nikaenda kujazia hizo fomu za kuweka huko huko benk,..’akatulia

‘Na baadae mimi ninamletea karatasi zile nilizowekea hizo pesa benki,…sasa wewe ukiniuliza wapi anazihifadhi hizo karatasi, nitasema ni hapo kwenye hilo kabati…ndivyo nijuavyo mimi, …sasa kwanini hazipo, mimi siwezi kulifahamu hilo…’akasema

‘Hukuwahi kuona sehemu nyingine anapohifadhia kumbukumbu zake…?’ nikauliza

‘Kiukweli sikuwahi…au mimi sijui…kama kuna sehemu nyingine mimi sijui, kama ipo sehemu nyingine labda wa kumuuliza ni shemeji, lakini mimi nilimuuliza na yeye akasema hajui,…hakuna…alisema,  hakuna sehemu nyingine, lakini siwezi nikawa na uhakika kwa asilimia mia, huenda ipo, lakini mimi siifahamu...niseme ukweli…’akasema

‘Lakini una uhakika kuwa kumbukumbu zake zote zilikuwa zinahifadhiwa kwenye hilo kabati…?’ nikamuuliza

‘Kwa jinsi nijuavyo mimi…ni hilo kabati, sasa siwezi nikafahamu zaidi, maana hii nyumba ni yake na dhamani hizo ni zake, siwezi nikajua zaidi….’akasema

‘Kwahiyo kwa namna nyingine mtu wa kumshuku ni shemeji yako, maana yeye ndio mwenye nyumba na yeye ndiye anayejua wapi mumewe anaweka kumbukumbu zake, kama ipo sehemu nyingine au sio…?... si ndivyo unataka kusema hivyo..?’ nikamuuliza

‘Hapana, mimi siwezi kumshuku shemeji yangu kihivyo,…asingeliweza kujua wapi zipo asiseme…maana hizo kumbukumbu ni kwa manufaa ya familia, yeye na watoto, sasa kwanini afiche…., ili iweje sasa…, haiji akilini, pili…alipofariki mumewe, shemeji yangu huyo alipoteza fahamu,..kwahiyo kama ni kupotea kwa hizo kumbukumbu, …kwa uoni wangu lakini,…ni kipindi hicho shemeji hajitambui, au kipindi marehemu yupo hai…’akasema

‘Kwahiyo zitakuwa zimetoweka, kipindi shemeji alipokuwa hajitambui, ..sizani kama ni kipindi marehemu yupo hai,…kwanini zipotee, na asiseme, au unataka kusema yeye mwenyewe labda aliamua kuziharibu, kwasababu gani sasa,..kuficha deni lisigunduliwe, au…?’ nikauliza

‘Ki uhakika, kiukweli wa mungu, mimi siwezi kujua…nitajuaje hapo,…hata wewe jaribu kulifikiria hilo,…bro, asingeliweza kufanya hivyo, kwa jinsi ninavyomfahamu, na shemeji asingeliweza kufanya hivyo, ili iweje…’akasema

‘Na wewe je, huwezi kufanya hivyo…?’ nikamuuliza

‘Ili iweje, inisaidie nini mimi…’akasema

‘Tutakuja kuliona hilo….ila ukweli ndio huo kuwa kumbukumbu hizo zilipotea kipindi shemeji hajitambui, na ilifanywa kwa makusudi ili asije kudai ukweli ..na waliofanya hivyo, wana dhamira ile ile ya deni,..kuwa hilo deni liendelee kutambulika hivyo kuwa ni la marehemu…’nikasema

‘Mimi siwezi kufahamu hilo, hizo ni hisia zako, ..labda tuzifanyie kazi, ili tuweze kuupata huo ukweli…’akasema

‘Na huo ukweli tutaipata kupitia kwako…au sio..?’nikauliza.

‘Kwa vipi…?’ akauliza

‘Wewe ndiye uliyekuwa mtu wa karibu wa kaka yako, wewe unajua wapi kumbukumbu za kaka yako zinahifadhiwa, wewe ndiye uliyekuwa ukitumwa benki, ..na wewe unaweza ukawa na masilahi ya chochote kwenye mali za marehemu..au sio….’nikasema na jamaa, akatulia.

Akatabasamu,….halafu akasema;

‘Ndugu mimi siogopi,..hisia zako maana kila mtu anaweza kujenga hisia zake ili kujirizisha, ila kiukweli, mimi sipendi kushutumiwa uwongo…nakuomba tafadhali , niamini, mimi siwezi kufanya ujinga kama huo kwenye familia yangu..unamuibia nani sasa..hawa ni familia yangu, …’akasema.

‘Kama sio wewe basi ni shemeji yako, au sio…nahisi unajaribu kusema hivyo, ila unaogopa, haya hebu niambie ukweli, ni nani mwingine angeliweza kuingia humo ndani na kuiba hizo kumbukumbu, na kwanini afanye hivyo…?’ nikamuuliza

‘Mimi siwezi kulijua hilo, hizo ni hisia zako umezijenga kichwani mwako, labda utuambie wewe…ni nani..lakini shutuma zako dhidi yangu ni uwongo…una taka kujenga chuki kwenye hii familia yangu, …kwa hilo nakuhakikishia, hutaweza kufanikiwa…kaulize kwingine, hapa hupati kitu…’akasema sasa akimtupia jicho mpelelezi.

‘Wewe unasema hujui, lakini wewe ndiye unayebeba dhamana ya hii familia na nia hapa sio kulete ushindani, unielewe, nia ni kuutafuta ukweli wa hilo deni…sasa tusipokuuliza wewe, tutamuuliza nani..?’ nikamuuliza

‘Mimi nimejaribu kukujibu maswali yako,…na kiukweli , lawama zako dhid yangu, ni kama vile mimi nilijua ..nikashindwa kuwajibika,..kama tungelijua,tungelichukua tahadhari hiyo…lakini yote yanatokea kwa mapenzi yake mungu, sisi kama wanadamu hatuna la kufanya…’ akasema.

Nikamuangalia huyu jamaa kwa makini, na alipoona namuangalia sana, akatabasamu, ….
‘Wewe umesema hufahamu lolote kulihusu hilo deni, na hukuwahi kufahamu ni kwanini kaka yako alichukua huo mkopo, na ni kwa jinsi gani angeliweza kuulipa huo mkopo,..umesema hufahamu…lakini unaamini kuwa kweli kaka yako alichukua huo mkopo, kutokana na nyaraka za kibenki, na pili kutokana na mizimu au sio..?’ nikamuuliza

‘Mimi sifahamu hilo,… huo ndio ukweli, …na…hebu niambie baada ya ushahid huo kutoka benki, wewe ulitaka mimi nifanyeje, ..wakati naona familia inaumia, hebu wewe tusaidie mawazo yako, kuwa mimi nilitakiwa nifanye hivi badala ya hicho nilichokifanya mimi…’akatulia kidogo akimtupia jicho mpelelezi.

‘Haya…nisaidie kwa hilo..tufanyaje sasa, ili ukweli wa hilo deni uwe bayana, mimi sijui zaidi..kiukweli nimehangaika vya kutosha…labda wewe utusaidie…’akasema

Aliposema hivyo, nikamgeukia mpelelezi,…na kusema;

‘Haya…natumai hilo limewekwa kwenye kumbukumbu,…sio kwamba naingilia kazi za watu, au sio…’nikasema na mpelelezi akatabasamu na kutikisa kichwa.

 Nikamgeukia Dalali….

‘Haya wewe umesema hakukuwa na namna nyingine ya kuona jinsi ya kulipa hilo deni, ndio maana mkakubaliana na benki kuwa wafanye kutokana na taratibu zao, ambao …kwa mujibu wa mkataba ni kupiga mnada hii nyumba..na kwa kukubali huko,… , mkawa tayari kukiuka ukweli, hulka na tabia ya kaka yako… na haki za marehemu, zikasahaulika, si ndio hivyo..?’ nikauliza

‘Baada ya mahakama kulipitisha hilo..ulitarajia sisi tufanye nini….maana shinikizo kubwa linatoka benki wanaodai…na sio swala la sisi kukubaliana, au kuona kuwa ni bora nyumba ipigwe mnada,..ndio deni lilipwe, kama ingelikuwa ni sisi, ..hata kama ni sisi, tungelifanya nini..hatuna la kufanya, kama bado wanataka deni lilipwe..tuliwambembeleza wakasema wao kama benki, wanafuata taratibu zao…’akasema


‘Lakini pia ni baada ya nyie kujirizisha kutokana na mizimu au sio..?’ nikauliza

‘Mizimu imekuja baadae…na tumefahamu hilo, baada ya kuhangaika sana, hilo la mizimu ..sijui kwanini unaliona lina umuhimu hapa…’akasema

‘Wewe ulisema, kuwa mlikuja kujirizisha, baada ya hiyo mizimu,..si ndio hivyo,…sasa kama mizimu iliwafanya muamini,..kwanini hiyo msiiulize,  jinsi gani ya kulipwa hilo deni,…?’nikauliza.

‘Hivi wewe una akili kweli, tuiulize mizimu, kwa vipi sasa…hiyo sio hoja kwangu…’akasema

‘Kama mizimu  imethibitisha kuwepo kwa  hilo deni, mka-amini,..na ikasema ni lazima hilo deni  lilipwe, hata kwa gharama za mali za marehemu,… si ndio hivyo..?’ nikauliza jamaa akabakia kimia.

‘Na wakati huo benki alishapitisha kuwa nyumba ipigwe mnada..si ndio hivyo…mizimu inamuwakilisha marehemu au sio? Na marehemu kwenye uhai wake alisema hii nyumba isiuzwe, kwanini sasa hiyo mzimu isiwaambia mbadala wake ni nini, kama kweli inamuwakilisha marehemu…?’ nikauliza

‘Mimi sijui…siwezi kulijibu hilo swali…’akasema

‘Mizimu ni nini…, ni marehemu au ni muwakilishi wa marehemu…?’ nikamuuliza na hapo kwanza akatabasamu , halafu akarejesha uso kwenye uwajibikaji.

‘Ni mizimu ya marehemu…’akasema
‘Kwahiyo ni marehemu ambedilika kuwa mzimu au...?’ nikauliza

‘Ni…aah, utakavyotaka wewe , ..tunaweza kusema hivyo, kuwa inamuwakilisha marehemu, maana marehemu keshfariki, huwezi kusema ni yeye tena…’akasema

‘Kwahiyo yenyewe inajua kila kitu kumuhusu marehemu…?’ nikauliza

‘Tunaweza kusema hivyo…’akasema

‘Kama ni hivyo,...eeh, huo mzimu si utakuwa unajua kila kitu kumuhusu marehemu…deni na jinsi gani ya kulilipa,.., basi kwanini isiseme, jinsi gani marehemu alipanga,kama ni mradi, kama kuna namna nyingine ya kulilipa hilo deni kuliko kuvunja ahadi yake ya kutokuiuza hii nyumba, umenielewa hapo…?’ nikamuuliza

‘Mimi hapo sijui …’akasema

‘Kwanini sasa hamukuiulizia hiyo mizimu…, kama kweli mlikuwa upande wa marehemu, upande wa kumtetea marehemu na haki zake na familia yake,…?’ nikauliza na jamaa akabakia kimia akitikisa kichwa kama kusikitika tu.

‘Kwa  namna nyingine basi ili itusaidie kwa hilo, fanya jambo , hiyo mizimu ije, tuweze kuiulizia, si inaweza kuja hata hapa…inaweza au…ni mambo ya kutisha,..mimi naona ufanye hivyo, ili na sisi tuamini, hiyo mizimu ije tuweze kuiuliza maswali, wewe si unalalamika kuwa tunakuuliza maswali yasiyokuhusu…unasemaje kwa hilo…’nikasema nikimgeukia mpelelezi, mpelelezi yeye alikuwa akiandika-andika, na alipoona namuangalia, akatikisa kichwa kuwa niendelee.

‘Mimi kwa hilo sina utaalamu nalo, na sina jibu la kukujibu,..ni mambo ambayo hata mimi siyajui, …’akasema

‘Mwenye utaalamu huo ni nani sasa, ambaye anaweza kutusaidia…?’ nikamuuliza

‘Ndugu,..hayo  maelezo tuliyapata kwa mtaalamu, sisi tusingelilifaham hilo, sasa ..mimi sijui, kama anaweza kuwauliza hao mizimu hilo swali,ujue mambo mengine tufanyie mzaha, kuna watu wanaumia kwasababu hiyo…’akasema

‘Ina maana mimi kuuliza hivyo nafanya mzaha…huu sio mzaha ndugu yangu, ni jambo la kuiondolea hii familia huu mzigo ambao mimi nahisi sio wao..ni mambo ya kubambikiwa vinginevyo, wewe kuna jambo unatuficha..’nikasema.


‘Mimi sijui,..mimi ..siwezi kujibu hilo swali lako…, labda tuje kumuuliza yeye huyo mtaalamu...’akasema.

‘Kwahiyo huyo Mtaalamu anaweza akatusaidia kwa hili, tukimuita akaja hapa , mimi ninataka tuwe na uhakika na hilo, je kweli anaweza kuifanya hiyo kazi, tukaongea na hiyo mizimu, au yeye akawa anaiuliza kwa niaba yetu….tuambie ili tusipoteze muda…?’ nikamuuliza

‘Kiukweli mimi sijui..naweza kusema anaweza, kumbe, haiwezekani, maana kitu kama hicho naona kama ni kuchezea hiyo mizimu, yenyewe imeshaleta taarifa ni kwanini familia hii inateseka, sasa tuanze kuidodosa,…mimi hapo sijui...’akasema

‘Kwa namna nyingine, huyo mtaalamu anaweza kuiita, kuelekeza, au kuipandikiza hiyo mizmu kwa watu wengine kwa jinsi nionavyo mimi, au sio…?’ nikauliza na jamaa akacheka, halafu akasema.

‘Hahaha…wewe mtu, usitake kumpandikizia mtu matatizo ambayo hayapo,…kama umeishiwa na maswali wewe useme tu…yeye kazi yake sio hiyo, yeye sio mchawi, eeh, ulizia utaambiwa, watu wengi wanamuamini sana…’akasema
‘Huko kwake ulisema ulielekezwa na nani …?’ nikauliza na hapo akasita kidogo baadae akasema

‘Kuna mzee mmoja anaitwa Mtupe…’akasema

‘Huyu mzee ni fundi, au sio..?’ nikauliza

‘Ndio…’akasema

‘Je katika kazi zake, alishawahi kuingi ndani, akapiga rangi hivi, au akakarabati ndani…?’ nikauliza

‘Ndani wapi,..kiujumla anafanya kazi sehemu yoyote, atakayoambiwa..’akasema

‘Kwahiyo naye pia tunaweza kumuweka kwenye kundi la kumshuku, kwa vile aliweza pia kuingia ndani,…hadi huko zinapowekwa kumbukumbu, kwa kumbukumbu zako, lini mara ya mwisho alifanya kazi kwenye hii nyumba…?’ nikauliza.

‘Ninavyokumbuka,…siku ile alipofariki bro, alikuwa akifanya kazi ya kupaka rangi nyumba nzima,…ninavyokumbuka mimi…lakini mimi siwezi kumdhania huyo mzee kwa lolote lile, namuheshimu sana…’akasema.

‘Na je huyo mzee, akisema yeye alikuona ukitoka na kumbukumbu hizo wakati anafanya hiyo kazi ya kupata rangi utasemaje…?’ nikamuuliza na hapo akashtuka,..halafu akasema

‘Huo ni uwongo…sijatoka na kumbukumbu zozote…aliniona wapi, na sikuwahi kuingia huko, hadi siku ile nilipoingia na wakili, huyo mzee atakuwa mnafiki, na ..kakaa kuchunguza chunguza…na…aje aseme hivyo mbele yangu, sio kweli kabisa….huyo mzee, hajui lolote, ….’akasema

‘Kwahiyo labda ni yeye aliziiba hizo kumbukumbu basi ndio maana anakushuku wewe,…?’ nikauliza nikimtega tu.

‘Ili azifanyie nini..mimi sioni hata haja ya kulifikiria hilo…kama kasema hivyo yeey ni muongo…na labda, mimi siwezi kujua, kama ni yeye alizichukua, mimi sio mwongo wa kusingizia watu kitu nisichokuwa na uhakika nacho…’akasema

‘Ukisema ili azifanyie nini, inanipa wasiwasi…’nikasema

‘Wasiwasi gani….niambie….Hahaha..unajua wewe maswali yako yamekaa kishari shari…sikiliza mimi siwezi kufanya hicho unachotaka kunipandikizia mimi,..kabisa kabisa, unapoteza muda wako, ..hilo deni lipo, na wanao ushahidi…kwanini usiende kuongea nao, kwanini unapoteza muda hapa….’ akasema

‘Kwa mtizamo huo, kwanza marehemu, hakupenda madeni, tena madeni yenye riba, hilo deni la benki lina riba, ni kweli si kweli…?’ nikauliza hilo swali

‘Ndio lina riba na kwa vile halijalipwa siku nyingi , riba yake ni kubwa sana…’akasema

‘Marehemu hakupenda deni , na tena deni lenye riba,…basi hilo deni sio la kwake, kama sio la kawake, ni nani mweney hilo deni, likaja kuhamishiwa kwa marehemu..?’ nikamuuliza.

‘Mimi siwesi kulijua hilo…hizi ni hisia zako…’akasema Dalali kwa kulalamika.

‘Katika mipangilio ya marehemu, yeye alitaka kujenga nyumba , nyumba yenyewe iwe imara, ili waje kuishi, wajukuu na vitukuu, kwa mantiki hiyo, hakutaka kabisa hii nyumba iachane na familia yake…iweje sasa aje kuiweka dhamana hii nyumba, kwa deni kubwa kiasi hicho, je alikuwa na miradi gani mikubwa…?’ nikamuuliza.

‘Mimi sijui, sijui, sijui…’akasema Dalali.

‘Iweje basi nyumba hii ije kupigwa mnada na nyie mkubaliane na hilo..?’ akaulizwa

‘Sasa sisi tungelifanyaje, na wakati nyumba hii ndio iliyowekwa dhamana na yeye mwenyewe…’akasema.

‘Ataiwekaje dhamana, nyumba hii, ya watoto wajukuu na vitukuu… wakati yeye kwanza hakupenda madeni, na tena madeni yenye riba, hakupenda nyumba hii ije kuachana na familia yake,…ina maana hakutaka kabisa hii nyumba ije kuuzwa, kwanini nyie mnakubaliana na hilo..?’ nikamuuliza

‘Nimeshakuambia mimi sijui…na hata hivyo, sisi tungelifanya nini, wakati hata mahakama imeshalipitisha hilo…’akasema.

‘Ndio maana sisi watu wa jamii, tukaona tuliingilie hili jambo, ili kulinda haki ya marehemu..haki ya wanafamilia, haki ya mjane na mayatima hawa, kama wewe ambaye uliyepewa dhamana hiyo umeshindwa, ma ,ajibu yako ni… hujui…hujui…..’nikasema

‘Mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu…’akasema

‘Umejitahidi wakati kila swali linalohusiana na ukweli huo, wewe kauli yak kubwa, ni ..’hajui,..’ je ni nani ataweza kulijua hilo, je ni nani ataweza kumtetea marehemu na haki zake…?’ nikamuuliza

‘Nimekuambia tumafanya kadri ya uwezo wetu, hatukuwahi kukaa kimia hadi ..tulipoona familia inateseka, ndio tukasalimu amri…’akasema

‘Au mseme ukweli, asiyekuwepo na lake halipo,marehemu akifa haki yake ndio imeshapotea au sio ndio maana mkakimbilia kuuza mashamba, kilichokuwa kimebakia cha thamani ni hii nyumba, je mtawezaje kuiuza pia…hakuna jinsi..au sio iliyobakia ni kuunda mizimu kweli si kweli...?’ nikamuuliza

‘Hahaha, hakuna kitu kama hicho, umeshindwa kukipata ulichokitaka, afande kauliza maswali yake yote,..hajapata alichokitaka,…sasa uamuzi ni wako, kumchukua ukamshughulikie kwa kuisumbua hii familia, na kupoteza gharama za serikali bure…’akasema

‘Swali je hadi hapo ulipofikia, mlipofikia mumekiri kuwa mumeshindwa kuutafuta ukweli, na mnahitajia msaada wa watu wengine..?’ nikamuuliza
‘Nimeshakujibu hilo swali, ..hata kama nyie mnaweza kutusaidia, basi karibuni…’akasema

‘Kwahiyo wewe umekiri kwa kinywa chako kuwa mumeshindwa, na pili, mnahitajia msaada si  ndio hivyo…?’ nikamuuliza

‘Khaaah, wewe vipi unataka niseme mara ngai, eti afande mimi nimesema nini…sisi hadi hapo tumeshindwa, ndio maana tukawaachia benki wafanye kazi yao,…ndio, msaada tunahitajia sana, kama yupo anaweza kulipa hilo deni, atusaidia, ili kuikoa hiyo nyumba…’akasema

‘Je kama yupo mwenye uweze wa kubaini ukweli wa hilo deni, kuwa sio sahihi na yeye mnamuhitajia…?’ nikauliza

‘Sawa..aje, lakini huyo itabidi apambane na watu wa benki…sio mimi, maana mimi sio niliyedai hilo deni, wanaodai ni benki…’akasema.

‘Na wewe umeshindwa kumtetea marehemu kuwa hahusiki na hilo deni, kweli si kweli..?’ nikauliza

‘Unarudia maswali yako unapoteza muda

‘Kweli si kweli..?’ nikauliza

‘Kweli…haya nimejibu , ni kweli , sisi kama familia kwa hatua tuliojitahidi…hatuwezi tena, kama yupo mtu wa kumtetea marehemu aje…tupo tayari, atusaidie…’akasema

Mimi pale nikageuka kumuangalia mpelelezi, nikasema

‘Umesikia….ukweli ndio huo, mimi sijafika hapa kuisumbua hii familia, nimefika hapa kusaidia, kuupata huo ukweli,..na hadi hapo, unaweza kubaini ukweli upo wapi..kilichobakia ni kuutafuta ushahidi…’nikasema

‘Hahaha, ….na kwanini ulituita sasa, ili iweje…?’ akauliza mpelelezi.

‘Ni kwasababu….nitakuonyesha, na sababu hizo pia zitasaidia kuifuchua ukweli mwingine uliojificha,..natumai baada ya hapo, wewe kama polis unaweza kuifanya kazi yako…’nikasema

‘Unataka kusema nini…?’ akauliza Dalali,

Mpelelezi akasimama, na akaniangalia….Dalali, akabakia kuduwaa…

NB: Msichoke, kuna kitu kinatafutwa hapo


WAZO LA LEO: Kuna watu wanafanya makosa, na makosa hayo huwasingizia wengine, pale wanapogundulikana, au wakiona watagundulikana....nia yao ni kujikosha ili wao waonekane sio wakosaji. Swali hapo, watu hao wanamdanganya nani…ukumbuke lolote ufanyalo, kuna yule usiyemuona, anayaona yote hayo, unayotenda kwa siri na dhahairi,…hata kama wanadamu wenzako hawataona, yeye anaona, na yeye kamwe hamuachi mja wake. Tuweni wakweli, ili ukweli uwe dira yetu ya maisha.
Ni mimi: emu-three

No comments :