‘Je nyie
mlijua vipi hilo…, kuwa hayo yanayotokea kwa mtoto,au kwa mama, ni mizimu ya
marehemu kaka yako…?’ nikamuuliza.
Tuendelee
na kisa chetu…
****************
Dalali
alipulizwa hilo swali, akageuka kumuangali mpelelezi, kabla hajanijibu,…halafu
akasema;
‘Tuliambiwa
na mtaalamu….’akasema huku akishika shika kichwa.
‘Mtaalamu
ukiwa na maana mganga wa kienyeji….au sio…?’ akaulizwa
‘Ndio…..’akasema
‘Wewe ni
mshirikina…?’ nikamuuliza hapo akanitolea macho, halafu akasema
‘Hapana..kwanini
unasema hivyo…?’ akauliza
‘Huyo
mtaalamu…alifanyaje mpaka akayafahamu hayo,…alifanya vitendo gani mpaka akaja
kukuambia hivyo…?’ nikamuuliza.
‘Yeye…?.....haah,
alifanya anavyojua yeye, mimi siwezi kufahamu mambo yake…’akasema.
‘Hukumuona
alivyofanya…?’ nikamuuliza.
‘Alifanya
mambo yake, ajuavyo yeye, mimi sikuwa na nia ya kumchunguza..’akasema
‘Hayo
mambo yake yanaitwaje..?’ nikamuuliza
‘Yanaitwaje…!!
…haah…Mimi sijui bwana…’akasema
‘Wewe ni
dalali, unajua sana mambo mengi, kwanini hili swali unashindwa kulijibu kwa
usahihi, wake, au hujiamini..au kwasaabbu labda, unaona ulivyofanya hivyo ni
makosa, au kuna kitu unaogopa..eeh?’ nikamuuliza.
‘Niogope
nini sasa…., mimi nimekuambia ukweli…’akasema
‘Nauliza
tena, mganga wako wa kienyeji, alifanya kitu gani, hadi akakuambia hayo
aliyokuambia, na wewe ukaja kuamini, kuwa ni kweli..?’ nikamuuliza
‘Mambo
yake,..mimi siwezi kuyafahamu,..ali…vuuuh, akatetemeka, akawa. Eeh, si ndio
unataka nisema hivyo, au niigize alivyokuwa akifanya, ilikuwa hivyo,….akatikisa
kichwa, akawa kama anaongea na watu, sisi hao watu hatuwaoni,baadae ndio
akatuambia hivyo…’akasema.
‘Hicho
kitendo, cha vuuuuuh, na kuongea na watu wake, msiowaona kinaitajwe…?’ nikamuuliza
‘Mimi
sijui bwana kamuulize yeye mwenywe…’akasema
‘Dalali,
dalali,… wewe ni mjanja, unajua mambo mengi sana..ni kwanini unaogopa kusema
ukweli, nauliza tena hilo swali, hicho kitendo cha vuuuuh..na kuongea na watu
wake, ambo unasema walikuwa hawaonekani, kinaitwaje..?’ nikauliza
‘Ramli….’akasema
kwa mkato.
‘Kwahiyo
wewe na huyo mtaalamu wako mlifanya kufuru , nyie wote ni washirikina,
unakubaliana na hilo…?’ nikamuuliza
‘Sasa
hizo ni kashfa…wewe…huna maana kazi yako ndio hiyo, umekosa la msingi, sasa
unakimbilia kukashfu wenzako, sio vyema kabisa…kama huna maswali ya msingi,
mwambie afande tumalize…’akasema kwa kulalamika
‘Wewe unaamini
dini,… una imani yoyote ya dini moyoni mwako…?’ nikamuuliza
‘Dini
yangu, na imani yangu haikuhusu wewe kabisa,…hilo ni swala la mtu
binafsi,..wewe unatakia nini kwenye imani yangu,..eeh,..na hilo swali linahusu
nini hapa…?’ akauliza.
‘Swali ni
hili, je dini yako, au imani yako binafsi kama ulivyotaka… inakuruhusu kupigiwa
ramli…?’ nikamuuliza.
‘Imani
yangu,…!?, umeshasema imani yangu,..nifanyavyo, haikuhusu, hilo sio swali, ama
kwa dini, najua ni kwanini unakwenda huko, ni vyema kama ilivyokuwa swali la
deni, eeh, ili upate majibu ya msingi, nenda kwa wahusika, na hili la dini, eeh…kawaulize
watu wa dini, mimi sio mtaalmu sana, wa mambo hayo, kwahiyo mimi sijui,…’akasema.
‘Wewe
hujui ukweli kuwa dini inaruhusu au hairuhusu kupiga ramli…, una uhakika na
jibu lako..?’ nikamuuliza
‘Mimi
nimeshakuambia, hivi…mimi sio mtaalamu sana wa dini, ..siwezi kulifahamu jibu
la swali lako, labda wewe unisaidie, unasikia, wewe si unajua sana, niambie
wewe…’akasema
‘Wewe
umesema sio mtaalamu wa dini, basi, hebu nikukumbushe kidogo…sitaki kuuliza
wewe ni dini gani, ila dini zote zinakubaliana na hilo nililokushutumu nalo,..kuwa
wewe umefanya shiriki, umekufuru… kwa mfano, kuna maandiko yanasema hivi…
Jamaa
akawa kimia, akiwa kainamisha kichwa huku akitikisa tikisa kichwa kama
kulalamika, lakini hasemi neno
‘Unaweza
kufahamu hayo maandiko yanatoka wapi…?’
nikamuuliza
‘Mimi
sijui….’akasema
‘Haya ni
maelezo kwenye kitabu cha Bibilia,….kuwa UASI, ni sawa na DHAMBI ya kupiga RAMLIi..kwa kufanya hivyo…, unakuwa
umeikataa amri ya mungu, kifupi umekufuru…na kumti mwenyezi mungu ni bora
kuliko matambiko, wewe umeyaendelea hayo kwa mtaalamu, hilo ni kosa…kweli si
kweli…?’ nikauliza
‘Hahaha….wewe
mtu bwana, kwanini unachanganya mada…unajua nikuambie ukweli..tukienda huko
sote tutakuwa wakosaji, sio wote wanaweza kuyatekeleza hayo, mitihani ikizidi
sana kwa wanadamu, tunashindwa kuvumilia, huo ndio ukweli halisi,
..tusidanganyane bwana,..hebu niambie kwenye hali kama ile, sisi tungelifanya nini,
eeh, ina maana wewe hujawahi kufanya dhambi yoyote, niambie ukweli…’akasema
kama ananiuliza
‘Mimi
nataka kukuonyesha kuwa, ulichofanya wewe nikufuru, umeingia kwenye
shriki..kuamini mizimu zaidi ya mungu wako,..kufanya hivyo ni makosa, na mimi
sijakukashfu…’nikasema
‘Sijakataa
eeh, kiimani eeh, ndio hivyo, ..unasikia sana mkuu, ..lakini zote ni …njia za
kutafuta kupona kwa mtoto na ..kwasababu hospitalini imeshindikana,
hatungeliweza kukaa kimia, hata wewe unalifahamu hilo,..hebu angalia duniani
ilivyo,…watu wanalewa, watu wanafanya madhambi mengi tu, kuua, kusengenya
nk..wakati mwingine sio kwamba wanapenda, inatokea tu…’akasema
‘Hebu
sikiliza na hapa, maana sitaki niongee tu, kuwa dini zote hazikubaliani na hilo
ulilolifanya, sasa wewe ukiwa dini hii au ile usije ukaweka kisingizio kuwa
dini fulani inaruhusu, hakuna dini inayoruhusu hayo,…na, kwasababu umetaja na
ulevi..basi ngoja nikupati ashahidi mwingine wa imani nyingine ya dini,
maandiko yanasema hivi;
“Enyi Mlioamini! Bila shaka ulevi, na
kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi za shetani.
Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa” (Sura ya 5: aya 90). Sura hii
inaitwa Al-ma’idah,
‘Unajua wewe hujanielewa…’akasema na baadae kumgeukia mpelelezi, huku
akionyesha ishara ya kulalamika.
‘Mimi nilitaka tu kukuonyesha kuwa nilipokuambia kuwa umemshirikisha
mwenyezimungu, nilikuwa na maana gani, sijakukashifu kama ulivyodai, ni
kukuonyesha kuwa vitendo ulivyofanya ni vya kufuru, ni shiriki, wewe uliingia kwenye
njia ya shetani, na kama umeingia huko…matokeo yake yatakuwa ni nini,…?’
nikamuuliza
‘Hahaha, unajua tusijifanye wanafiki, tukiangalia makosa ya watu wengine…’akasema
‘Nataka wewe uelewe…kuwa hayo yanayotokea kwa mtoto, na …unachoamini,
ni ushetani,..hakuna zaidi ya hapo, hata kama unasema wengi wanafanya hivyo,
lakini sio njia sahihi, au sio….’nikasema
‘Ngoja kwanza, …unajua tunapoteza muda, hayo maswala ya dini
yamekujaje hapa, ..mimi siyajui sana, ukinishinikiza huko unanionea tu bure…,
sema maswala ya kimahakama, ya kisheria za mahakama..ndio yaliyopitishwa na
kukubalika, na mimi…ni muathirika tu wa hukumu, kama walivyo hii familia, sisi
hatukuenda msikitini au kanisani, unielewe hapo…’akasema
‘Je Mahakama ilikushauri uende kwa mganga wa kienyeji…?’ nikamuuliza
‘Hapana bwana,..mbona hunielewi, huko nimekwenda baada ya kuhangaika
na mtoto, baada ya kuona kuwa,..eeh,..hospitalini hakuna tiba, sasa ulitaka
mimi nifanye nini,nikae tu..mtoto anateseka, kama mzazi unaangalia kote kote…’
akasema kwa ukali .
‘Haya twende kwenye sheria za mahakamani…wewe uliamini vipi kuwa deni
hilo ni sahihi, …maana kwenye dini huamini, ila kwenye mizimu unaamini,…au
sio..?’ nikamuuliza
‘Sijasema kuwa dini siamini, kama dini ingelinielekeza njia ya
kulilipa hilo deni, au ikanibainishia kuwa hilo deni ni sahihi au sio sahihi,
ningelifuata hivyo hivyo…tatizo wewe unaongeza mambo ambayo hayahusiani na hili
tatizo..na kwa vile wewe hayajakukuta…’akasema
‘Sio hivyo…mimi ninachotaka kufahamu ni kwa vipi uliamini kuwa deni
hilo ni sahihi, wewe awali ulisema nguvu za kuamini hilo deni kuwa ni sahihi
zilizidi zaidi kutokana na kutokewa na mizimu..kweli si kweli…?’ nikamuuliza na
hapo akakaa kimia.
‘Sasa mimi nimejaribu kukuonyesha kuwa mizimu,..vibwengo ,
vinyamkera..kupiga ramli,… ni njia za shetani, kwa maandiko…niambie wewe, ni
nguvu gani zaidi iliyokufanya uamini kuwa deni hilo ni sahihi, kama sio njia
hiyo ya kishetani…?’ nikamuuliza.
‘Ni ushahdi wa kibenki, ambao
una mahali pake kisheria, sema wengi bado tulikuwa hatujaliamini hilo..eeh,…hata
baada ya hukumu, bado nyoyo zetu zilikuwa zinalalamika, kuwa hatujatendewa haki…kwa
jinsi tunavyomfahamu bro……’akasema
‘Hulka na tabia ya kaka yako ilikuwaje,..hebu tuweke sawa, kwa
afande hapo…ili aweze kuweka kumbukumbu zake sawa, kaka yako alikuwaje kwenye
uso wa jamii..elezea tu, au ?’ nikamuuliza, na kumuona anatikisa kichwa kama
kutaka kulalamika.
‘Yeye kiukweli alikuwa mtu mkweli, mwaminifu, yeye, eeh akisimamia
kwenye haki na ukweli, huwezi kumbandua…na imani yake pia ilimsaidia sana,
hakuwa muongo, hakuwa mlaghai, hata kazi zake zilikuwa hivyo hivyo..akikuambia
jambo, sifanyi kweli hafanyi, hasa akisimamia kwenye ukweli na haki…’akasema.
‘Safi kabisa, umtusaidia sana, kumbe tunalolifanya ni sahihi,..haya …je
na kwenye madeni alikuwaje..?’ nikamuuliza
‘Hakupenda madeni, kiukweli marehemu kaka, eeh…hakutaka kukopa
katika maisha yake niliyoishi naye, mimi nilikuwa mtu wake wa karibu sana,
sijasikia akisema anadaiwa, sijasikia akisema naenda kukopa, yeye aliishi kadri
ya kipato chake, ..na hata sisi alituonya kuwa tusikope,..hasa madeni yenye
riba…’akasema
‘Hakupenda, madeni, na hasa hasa madeni yenye riba..hilo mna uhakika
nalo..sema ukweli wako..?’ nikamuuliza
‘Ndio…nilimsikia mimi mwenyewe, na alishakataa mara nyingi, hata akiwa
anataka kufanya jambo kubwa zaidi ya uwezo wa kipato chake,..yeye atasema ni
bora tuache au tufanye kadri ya kipato chetu,..wakati mwingine sisi tunaingilia
kati na kumshauri tukope yeye anakataa, kabisa kabisa hakubali…anasema tufanye
jamboo kadri ya kile tulichojaliwa nacho…’akasema Dalali.
‘Je maelezo hayo uliwahi kuyatoa mahakamani..?’ nikamuuliza
‘Tulitoa…eeh, ndio lakini kule si unaongozwa na wakili…tuliongea kwa
kadri ya maelekezo,..lakini, nikuambie kitu, sisi tulishindiwa kitu kimoja,
ushahidi..hatukuwa nao, ni manen tu….’akasema.
‘Kwahiyo mkakubali shingo upande, au sio…kuwa hilo deni ni la kaka
yako…lakini sasa wewe, na wenzako wenye imani hizo, mkaja kuamini kuwa eeh,
kumbe ni kweli, kumbe deni ni halali, pale mlipotokewa na hichop unachokiita mizimu
kwa mtizamo wako,..au sio..?’ akaulizwa.
‘Sio kwa mtizamo wangu…vitu vimejionyesha, mtoto anaumwa, anapelekwa
hospitalini, hana tatizo,,,akirejeshwa nyumbani, siku mbili tatu, anaanza
kuumwa tena…uone ajabu eeh, akifika eneo la hopitalini anapona kabisa…’akatikisa
kichwa
‘Hebu wewe niambie..hilo si jambo ambali sio la kawaida..ndio maana sisi tukashauriwa na watu,
unajua tena, mzazi kwa mtoto, ndio…ikabidi twende upande wapili, na huko ndio
tukaambiwa hivyo,..kuwa hilo ni tatizo la mizimu, mzimu wa marehemu umekuja
ukilalamika kuwa kuna deni, na deni hilo lilipwe…’akasema.
‘Je huo mzimu, ulisema hilo deni litalipwajwe, wakati hakuna pesa,
au marehemu aliacha namna yoyote ya kuweza kulipa hilo deni…?’ nikauliza
‘Kwa kauli ambayo, ilitokea hata kwa mtoto..unajua japokuwa ni
mtoto, awali kabisa, alipandisha, hutaamini, sauti ya marehmu ilisikika kwenye
kinywa cha mtoto,..hivi wewe ulishawahi kuona watu wakipandisha inavyokuwa…inashangaza
sana…sauti ilisema inataka hilo deni
lilipwe kwa njia yoyote ile…, hata kama ni kuuza mali zake…’akasema
‘Ilisema hivyo, hata kama ni mali zake..kwahiyo mali zake ni pamoja
na nyumba…sauti hiyo ilitaja hivyo, kuwa hata nyumba iuzwe..?’ akaulizwa
‘Hakutaja nyumba, ila alitaja mali zake,…na mali zake zilizokuwepo
kwa kipindi hicho ni nyumba..’akasema
‘Marehemu hakuwa na mali nyingine..?’ akaulizwa
‘Kulikuwa na mashamba, lakini mashamba hayo yalikuwa yakifamilia..ni
ushirika wa familia yetu,…ndugu zake na yeye, hata kwenye nyaraka za manunuzi
ya hayo maeneo , utaona hivyo, hakuna kitu cha siri…hayo maeneo hayakuwa ya
kwake, peke yake…unanielewa hapo…’akatulia akiniangalia.
‘Umenielewa…? Maeneo hayo yalikuwa yakwetu sote yeye, na sisi sote,
yaani ya kifamilia, sasa najua utaniuliza ni kwanini tuliuza..ni kutokana na
hali ngumu, kuumwa kwa shemeji na matatizo mbali mbali, tukikubaliana tuyauze
hayo mashamba,…na kwa bahati mbaya sana,…kipindi hicho, mke wa marehemu alikuwa
akiiumwa,…zile pesa zikatumika kumtibia….’akasema.
‘Je kipindi hicho, mnayauza hayo maeneo … wewe ulishajua kuhusu hilo
deni…?’ nikamuuliza.
‘Nilikuja kufahamu baadae..siwezi kulikataa hilo,…. lakini ni baada
ya kaka kufariki,…ndio tukaipta hiyo taarifa kutoka benki, wakilalamika kuwa…tumekaa
muda bila kulipa hilo deni,..ndio na mimi hapo nikaja kufahamu…’akasema
‘Kwahiyo hilo la kuuza nyumba ya marehemu ni nyie wenyewe iliwajia
kichwani, baada ya kukosa cha kuuza tena…si ndio hivyo…na ni baada ya kuliona
hilo deni kuwa ni kubwa sana, na mkaona hakuna jinsi nyingine, jinsi ni kuuza
hiyo nyumba, au sio…?’ akaulizwa.
‘Hapana sio sisi tulioamua hivyo, ni benki wanaomdai
marehemu..kwenye mikataba ya kibenki, marehemu aliweka nyumba yake kama
dhamana, na kwa maelezo ya benki wao wamefuatilia sana, na wameona hakuna
muendelezo wa kulipa hilo deni, na kutokana na mkataba, basi wao hawana njia
nyingine zaidi ni kushikilia mali za mdaiwa, ndio hapo wakageukia hiyo dhamana
ya nyumba…, kwahiyo sio sisi tulioamua hilo ni benki…’akasema.
‘Marehemu katika kauli yake, alisema nini kuhusu hii nyumba yake, ..?’ akaulizwa
‘Alisema mengi, na moja wapo ni kuwa nyumba hii ije kuishi hata
wajuu, na vitukuu, ndio maana aliijenga ikawa imara hivyo…’akasema
‘Kwahiyo yeye hakuwa na mawazo kabisa ya kuja kuiuza hii nyumba, kwa
vyovyote vile sio ndio hivyo au..?’ akaulizwa
‘Kwa jinsi tulivyomfahamu sisi,…hakuwa na mpango huo, sasa hatujui
ni kwanini akaja kuiweka hii nyumba yake dhamana,..lakini mimi nahisi yeye kama
angeliendelea kuwa hai, angelilipa hilo deni, kwa jinsi alivyojipangilia yeye
mwenyewe, asingeliweza kuchukua deni bila ya kuwa na mpangilio wa jinsi ya kulilipa
hilo deni au sio..sasa..tatizo hakuna anayefahamu huo mpango wake, hata mkewe
hajui…’akasema
‘Katika kutafuta ushahidii kwenye nyaraka za marehemu nyumbani
kwake, je mliwahi kuona ushahidi kama huo kuwa alikuwa na deni….hata nakala za
kibenki…?’ nikamuuliza
‘Hiyo ni mojawapo na ajabu… hatukuweza kuona kabisa, hata nakala
moja ya benki, hakuna, hakuna hata ile ya Ankara za benki, au kumbukumbu yoyote
ya kibenki, na alikuwa na akaunti benki..tulimuuliza hata shemeji, shemeji yeye
anasema maswala ya benki, hakuwa akiyafuatilia, kwahiyo hajui …,..ilitushangaza
sana…’akasema
‘Mkopo kama huo, ni lazima kuwe na nakala ya mdaiwa, ina maana yeye
alikuwa akiweka wpi kumbukumbu zake…maana wewe ni mtu wake wa karibu sana..?’
nikamuuliza
‘Kuna kabati lake huwa anahifadhi, mikataba,..na nyaraka mbali mbali
muhimu, tulipekua kote hakuna kabisa…’akasema
‘Ziliondolewa mapema na wajanja au sio…’nikasema
‘Wajanja gani sasa, maana kwenye hiyo nyumba alikuwa akiishi
mkewe,..na huko ndani kwake, hakuna mtu anayeingia ingia, ni mkewe tu….sasa ni
mjanja gania angelifanya hivyo, hakuna kitu kama hicho..’akasema
‘Wewe hujawahi kuingia huko..?’ nikamuuliza, na hapo akakunja sura
kabla ya kujibu,
‘Kuingia huko, wakati gani sasa…kama ni wakati marehemu yupo ndio,
nilikuwa naingia, kwa idhini yake, na nilikuwa naingia akiwepo, kama tunatafuta
kitu eeh maana kaka aliniamini sana.., au kama kuna jambo tunafanya, mimi na
yeye tulikuwa tunaingia pamoja…’akasema.
‘Kwahiyo wewe ulikuwa ukifahamu kila kitu,…na sehemu gani kumbukumbu
hizo zinawekwa, au sio…?’ nikauliza
‘Sikiliza kuingia kwangu sio kwa minajili ya kufahamu kila kitu…yeye
ndio anachukua tunachokitafuta, anakileta mezani, sio mimi napekua vitu vyake…nisingeliweza
kufanya hivyo wakati yeye yupo…sijui unanielewa hapo…’akasema.
‘Lakini macho yanaona..au sio, sizani kama ulikuwa unafunga macho,
na umesema kaka yako alikuwa akikuamini sana, kwahiyo hakuwa na shaka na wewe…si
ndio hivyo…’nikasema nahapo akakaa kimia.
‘Na alipofariki kaka yako, je wewe, hukuwahi kuingia tena huko ndani..?’
nikamuuliza
‘Nifuate nini tena huko, wakati mwenyewe hayupo au una maana gani…?’akasema
kama kuuliza
‘Si ulifuata hizo nyaraka za benki au sio…?’nikasema kumuuliza,
hakunielewa, yeye akasema;
‘Hapana, sikuwa na haja ya kuingia tena huko…’akasema
‘Una uhakika na hilo jibu lako…?’ nikamuuliza, hapo akainua uso
kumtizama mpelelezi, akajikuta anatizamana na sura ya polisi huyo, hapo kwa
haraka akasema;
‘Hivi, wewe unanishuku nini mimi, mimi na marehemu tulikuwa kitu
kimoja eeh….muulize hata shemeji, maswali yako yanaonyesha kama unanishuku
jambo,..mimi ninajali hii familia kuliko wewe unavyofikiria, ..nimemuuguza mimi huyo shemeji… kama ..mke
wangu, nime..sitaki hata kuongea, watu walifikia kukimbia,…shemeji alikuwa mtu
wa kugeuza, kumfanyia kila kitu, halafu unaleta fitina zako hapa…’akasema sasa
kwa ukali.
‘Nauliza swali tena una uhakika, hukuwahi kuingia tena, kutafuta
kitu kwenye hilo kabati…?’ nikamuuliza;
‘Jibu ni hapana, sijawahi…’akasema akinitolea macho.
‘Wewe ni muongo…’nikasema
‘Kwanini..?’ akauliza sasa akionyesha kakasirika…
NB: Maswali yanaendelea.
WAZO
LA LEO: Kamwe hatutakiwi kuwaamini
wapiga ramli, sio kuwaamini tu, bali hata kuwaendea, ili kutizamia mambo yetu,…au
kuuguliwa nk. Kwani wao wanachokifanya ni kinyume na maaandiko ya
mwenyezimungu, na nji za sheteni. Wao
huongea na mashetani ili kukidhi haja zao. Wataalamu hao, hawaachi
kuwagombanisha ndugu kwa ndugu, wanazikosanisha ndoa, na kuharibu upendo
nyoyoni mwa watu. Wao wanachokifanya ni kuganga njaa zao. Tuweni makini sana na
watu hao.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment