Mlango
ulifunguliwa,…!
‘Aheri umefika shemeji …’ akasema mama mjane.
Akili
yangu ilikuwa kwa mtoto, lakini niliposikia kauli hiyo,…’shemeji..’ kwa haraka
akili yangu ikahamia kutaka kumuona huyo mtu….
Tuendelee
na kisa chetu
*********
Akaingia jamaa mmoja akiwa kavalia, kinamna
yake, suti kali na briefcase mkononi, na mawani ya jua usoni,…anatembea kama
muheshimiwa fulani hivi….au kama ofisa fulani
katokea safari ni Ulaya, ….;
Hakujali
jinsi tulivyo kuwa, akatembea taratibu hadi kwenye meza akawa briefcase yake,
na taratibu akavua mawani yake, na kutoa leso, akayafuta, halafu akapanidhs
mikono kuelegeza tai, ..halafu taratibu akageuka kutuangalia…hakusema neno,
aliyeongea ni mama mjane…
‘Oh karibu, nimeshindwa hata kukupokea,…maana kili
zimetingwa na hali ya mtoto, na nilipokuona nikashukuru mungu….’huyo mama akasema
akionyesha matumaini.
Sasa
shemeji mtu ndio akageuka upande ule nilipokuwa, bado nimesimama na
mtoto,…japokuwa akili ilishahamia kwa huyu jamaa, lakini akili nyingine kwa
kiasi kikubwa ipo kwa mtoto…naona tunachelewa…
Kwanza
nilishangaa, muda mchache nyuma, mama mjane alishaanza kunilaumu, kuwa ni mimi
nimesababisha yote haya, nilitegemea kabisa asingelipoteza muda, tuwahi
hospitalin, lakini sasa kamuona huyo jamaa ambaye kwa kauli yake ni shemeji
yake,..amekuwa kama hajali tena safari hiyo ya hopitalini.
Yule
jamaa kwanza aliniangalia..ile ya dharau …, halafu akaweka mawani yake vizuri
kuining’iniza kwenye mfuko wa suti yake,…taratibu akasogea hadi pale nilipokuwa
nimesimama,
Akawa
anaendelea kuniangalia mimi,..ni kama vile anakuja kwangu, sio kwa mtoto…na
aliponifikia, akanyosha mkono wake, ni kama anataka kunisalimia, lakini kwa
jinsi nilivyokuwa nimembeba mtoto nisingeliweza kuinua mkono..
Bado huku
akiniangalia, akanyosha mkono wake, na kushika shavu la mtoto kupima
joto….alivyokuwa akifanya utafikiri docta, akatikisa kichwa kama kukubali kitu,..sasa
akawa anamuangalia mtoto, akafunua sehemu ya migii yake, akawa anaipima joto,
na kwa haraka kamuachia kwa haraka, …akaguna tu kusema
`Oooh,…’
haraka akageuka kumuangalia shemeji yake, na kuuliza
‘Imepita
muda gani…?’ akauliza
‘Hata
robo saa haijapita…’akasema shemeji yake.
Akashikanisha
viganja vya mikono baada ya kuvipuliza, halafu akaviwekea viganja vyake
kichwani kwa huyo mtoto, akawa awewesa
maneno, sikuweza kuyasikia vyema, mdomo ulikuwa ukicheza cheza tu, alifanya
hivyo kwa muda, mtoto kimia, akamwangalia mama yake, akatikisa kichwa, akasema;
‘Shsmeji
mumefanya nini tena, umesahau maagizo uliyopewa, mbona hamna huruma na huyu
mtoto,..ni nini lengo lenu, kumuua huyu mtoto…’akasema na mama mjane akanitupia
jicho, hakusema neno, na shemeji mtu akaendelea kuongea
‘Unakumbuka
kipindi kile,…alizidiwa sana zaidi ya
hivi, eeh,…aah, mimi sijui nyie watu mpoke, haya basi tusipoze muda zaidi…nipe
ile dawa ya unga…..’akamwambia shemeji yake.
Shemeji mtu akawa kama anasita kidogo, lakini
baadae kwa haraka, akageuka na kuelekea kwenye vyumba, ..na kuingia kwenye
chumba kimojawapo, na wakati anaondoka,
huku nyuma simu yangu ikawa inaiita
lakini sikutaka hata kuipokea, ….
‘Pokea
simu yako….’akaniambia huyu mjamaa. Huyu jamaa anavyoigiza, sijui umweke fungu
gani, maan alisema hivyo akageuka kuangalia dirishani. Mimi nikamweka mtoto
vizuri, na kuipokea simu, ujue muda wote huo nimembeba mtoto.
Nikatoa
simu kutoka mfukoni, na kuiminya kitufe
cha kupokelea,..
Walikuwa
ni watu wangu niliwaomba taarifa mbali mbali, zinazomuhusu huyo mama, nikawa nasikiliza kwa muda,
…nilichosikia kilinifanya nianze kuwa na mashaka …nikawa najiiba kumtupia jamaa
jicho, hakuwa na wasiwasi na mimi alikuwa kanipa mgongo.
Mara
akageuka …akawa sasa anamuangalia mtoto, akawa anachezesha chezesha viganja
vyake vya mkono, akivisugua sugua na
badaye kuvipuliza, akawa anafanya hivyo kwa muda, ni kama mikono yake inasikia
baridi sasa anaipasha moto…nilimuangalia mtoto, yupo kimia…
Kwa muda
nilikuwa bado naendelea kusikiliza maelezo ya vijana wangu mmoja baada ya
mwingine, halafu nikasema;
‘Nyie endeleeni…tutaongea
baadaye,…nipo site…’nikasema na
kukata simu,
‘Site….’
Jamaa akasema hivyo, akitikisa kichwa huku akitabasamu ile ya dharau, mimi
nikamweka mtoto vizuri, sasa nikisogea kwenye sofa na kukaa,…niliona hakuna cha
kufanya, ngoja nisubirie wanachotaka kukifanya.
Nilitaka
kuurudidhs ile simu mfukoni , lakini nikakumbuka kitu, … sasa akili ilishaanza
kufanya kazi, nikajua sasa nipo kwenye mapambano, sitakiwi kupoteza kitu, nikaiminya simu sehemu ya kurekodia matukio,
bila jamaa kufahamu, nikaiweka ile simu kwenye meza.
‘Site..hizi
simu jamani, unaambia upo site, kumbe…hahaha..’akasema na kucheka, na mimi hapo
hapo nikasema;
‘Hizi
simu kwa sasa naziona hazina maana,..sitaki kuzipokea tena, unajua mimi hapa
nimechanganyikiwa kuhusu huyu mtoto, mimi nawashangaa, hamtaki tumpeleke
hospitalini….’nikasema huku nikiiweka ile simu pale mezani.
Akawa
anaangalia ninachokifanya, akasema;
‘Hiyo
simu ya bei mbaya, unaweka hapo mezani, …unaweza ukasaishau, na watu leo
wanaingia humu ndani na kutoka…’akasema huyo jamaa akiitizama pale nilipoiweka
ile simu
‘Ni za
kawaida tu…sitaweza kuisahau…nikisahau wewe si utanikumbusha au..’nikasema kama
nauliza
Mara
shemeji akaja na karatasi imekunjwa, kuonyesha kuwa dawa imekwisha,…
‘Shemu
mbona umechelewa hivyo,…muda, unajua kwa jinsi unavyochelewesha, damu
inaganda..unaelewa hivyo, tokea miguuni, mtoto anaweza kupooza,….dawa ..mbona
karatasi tupo, dawa ipo wapi…?’ akauliza.
‘Imekwisha,
…nilijua imebakia kidogo, kumbe hakuna kabisa…’akasema mama mjane.
‘Shemeji,
shemeji, ….nilikuambiaje,…hii iwe kama kinga yako, ikitokea tu, unaitumia, kama
nilivyokuelekeza,…sasa imeishaje, kwani alishawahi kuumwa tena na tena..au
imemwagika, shemeji hiyo dawa ni aghali
sana…?’ akawa anaongea kwa kituo, haionyeshi kukasiri, japokuwa maneno yake ni
kama kulalamika
‘Imetokea
mara kadha ..nikawa naitumia…wala haijamwagika..’akasema mama mjane.
‘Mhh..hata
sijui kama nina akiba, ngoja nione…’akasema akifungua ile briefcase yake,
akatoa kichupa, na akakitikisa,…
‘Bahati
nzuri, iiipoh, ngoja tuone,…, asante mungu…ipo…ok, sasa eeh….’akasema , huku
akimimina unga kwenye karasi, kiasi tu, ..halafu akamkabidhi shemeji
yake..halafu akajiwekea kidogo, kwenye kiganja cha mkono,…akawa kama anaisomea
maneno kwa kuwewesa, halafu, kwa kutumia
vidole viwili, akachota , na kuweka puani mwa huyo mtoto, na mara huyo mtoto
akapiga chafya, mara tatu…..
‘Tayari,…mmh,
naona keshaondoka huyo….’akasema sasa akitikisa kichwa kukubaliana na hilo
tendo.
‘Nani…?’
nikajikuta nimeuliza hivyo,na huyo jamaa akageuka kwa haraka akanitupi jicho
mara moja, halafu akageuza kichwa na kuendelea kumuangalia mtoto kwa sekunde
kadhaa, baadae akasema;
‘Huwezi
kuelewa haya…anajua shemeji, ….’akasema
Baadaye
akawa anasema maneno fulani huwezi kuyasikia vyema,…., akampaka Yule mtoto
usoni ile dawa, halafu taratibu bila wasi wasi akasogea hadi kwenye sofa, akakaa, na kukunja nne, yaani utafikiri docta
anayejua anachokifanya, inaonekana huyu
jamaa ana majigambo fulani hivi.
Mimi
nilikuwa bado nimempakata huyo mtoto, na Yule mtoto sasa akaanza kujitikisa na
baadaye akawa anajiinua kutaka kusimama, lakini akawa bado hana nguvu,
nikamsaidia kuinuka, akasimama…hapo nikapumua, eehuuuuh, …..
Mtoto
akasimama akitaka kuinua mguu, akawa anayumbayumba,
mimi kwa haraka nikajiinua kidogo ili
kuweza kumshikilia, asidondoke…
‘Haina
haja,..yupo safi, wala usiwe na wasiwasi…’jamaa akasema pale nilipojitahidi
kumshikilia huyo mtoto…Kiukweli mimi bado
nilikuwa sina imani, moyoni nataka tumpeleke huyo mtoto hospitalini. Nikasema;
‘Jamani
huyu mtoto tumpeleke hospitalini…hii hali sio ya kukaa nyumbani..muoneni alivyo
mdhaifu…’nikasema
‘Haina
haja,…yupo safi, nimeshakuambia, hayo eeh,..ni …mambo ya kimila basi…hata
ukimpeleka hospitalini, haitasaidia kitu, muulize mama yake…’akasema huyo jamaa,
sasa nikainua uso na kumuangalia vyema huyo jamaa usoni, nahisi niliwahi
kumuona mahali,…sikumbuki wapi, hata hivyo,kwa muda ule akili yangu ilikuwa
bado kwa mtoto..
Nikageuka
kumuangalia mtoto, sasa aliweza kutembea hatua kadhaa, akipiga miayo! Nikaona
bado niendelee kusisitiza mambo ya hospitalini..
‘Huyu mtoto
kwa hali hiyo inabidi tumpeleke kwa docta bingwa wa watoto, msiseme tu haina
haja, mlishawahi kumpeleka huyu mtoto kwa docta bingwa wa watoto, …kama tatizo kama
hili huwa linajirudiarudia ujue kuna kitu anatakiwa kuchunguzwa, kwenye kichwa,
msikimbilie mambo ya kimila, mlifanya hivyo….?.’nikauliza.
‘Hayo sio
maradhi ya kupelekwa hospitalini, hata hivyo,…ni kweli mtu akiumwa, hasa mtoto
inatakiwa kufanya hivyo, na sisi mwanzoni tulifanya hivyo, au sio shemeji….’akasema
akimgeukia shemeji yake, na sheemji yake hakujibu kitu, yeye akaendelea kuongea
‘Na kwa
vile tulikuwa hatujui kuwa tatizo ni nini,…tukahangaika hivyo
unavyosema..lakini haikusaidia kitu..na huko kwa docta bingwa, tena bingwa hasa wa watoto…yule
anaitwa nani vile shemu….hebu mwambia huyu mtu…’akasema akimuangalia shemeji
yake
‘Yeye
huyo docta akasemaje…?’ mimi nikamkatiza na kumuuliza hilo swali
‘Hana
tatizo, vipimo vyote hakuna tatizo, …unajua inashangaza sana, unamuona alivyo
kuwa na hiyo hali, ukimchukua mkafika hospitalini, atazindukana, pengine hata
kabla hujafika kwa docta, na…hapo hapo atachangamka, kwa furaha, akacheza na
wenzake,…, wakati tulimchukua hajiwezi…kama hivyo ulivyomuona…hata docta
ukimuambia anaumwa, inakuwa kama haamini…’akasema mama mjane
Yule
jamaa akawa anatikisa kichwa kukubaliana na hayo aliyoongea shemeji yake,
halafu akanionyeshea mikono, kama kusema, umesikia, baadae kukawa na ukimia,
mimi bado nikimuangalia yule mtoto, na mara jamaa akasema;
‘Ehe
niambieni…kulitokea nini…maana nilishikwa na majukumu…’akasema na tukawa kimia,
alipona hivyo akamgeukia shemeji yake na kuuliza;
‘Kuna nin
kinachoendelea, maana hii sio bure, umefanya nini tena shemeji….?’ Akamuuliza
shemeji yake
‘Kwahiyo …unasema
ni mambo ya kimila, au…?’ mimi nikadakia kabla shemeji hajaongea neno, huku
nikiendelea kumuangalia yule mtoto , kwa muda ule alikuwa akicheza na mwenzake
utafikiri sio yule aliyekuwa kazidiwa.
‘Shemeji
hebu muambie huyu. Eeeh, sijui ni nani….’akasema sasa akinikagua vyema kwa
kuniangalia usoni, na mimi sikumpa mdua huo nikawa nimegeuka kumuangalia mtoto.
Yule mtoto sasa akawa kachangamka, akamwendea
mama yake, na mama yake akamwinua na kumpakata miguuni mwake…., mama
alimuangalia mtoto wake kwa macho yenye huzuni, …na mara machozi yakaanza
kumtoka huyo mama, pale nilipo nilihisi hasira, sijui ni hasira za nini…nikageuka
kumuangalia huyo jamaa. Alikuwa sasa
kashika simu, anachat, au …huku akisema haya maneno;
‘Hawa
watu bwana, unaona wananilaumu mimi, kwani imekuwaje, mimi sijui kinachoendelea….walitaka
kuja kesho, eti kuna mtu kawazuia,…hata sijui ni nini kinachoendelea…’akawa
anaongea peke yake
‘Unajua
shemeji, kuna matajiri watatu, wanauhakika wa kulipa pesa nzuri, sasa…yupi ni
yupi, tutaangalia dau lao, watashindana, hadi kile kiwango kinachofaa, mwenye
kisu kikali ndiye atakula nyama, au sio shemeji….ngoja tuone.’akainua uso na
kumwangalia shemeji yake, akamuona shemeji yake machozi yakimtoka, alipoona hivyo akasimama na kumsogelea shemeji
yake, huku akisema;
‘Shemeji
lakini si nilikuambia, … usivunje miiko, unaona sasa, unamtesa huyo mtoto bure,…kuna
kitu ulitaka kukifanya, kweli si kweli…., ulitaka kufanya nini, au umefanya
nini,?’ akamuuliza shemeji yake lakini shemeji akawa anatoa machozi tu.
‘Shemeji,
wewe unajua kabisa,…. baba yake huyu mtoto hataki mambo hayo, …si unakumbuka
maagizo tuliyopewa…sasa haya ni matokeo yake, kwahiyo ukilia, haisaidii kitu kama
hutatimiza hayo uliyoambiwa,….kutokutii hayo maagizo…itaendelea kuwa hivi, na
sasa hali hiyo ilipofikia ni kubaya zaidi.’akasema jamaa
‘Samahan
kidogo, umesema baba yake hataki, baba yake yupi hataki mambo hayo, baba yake
si….., marehemu au ?’ nikauliza na kabla sijajibiwa nikauliza swali jingine…
‘Na hataki
mambo gani?’ sasa nikawa nimemkazia macho huyo jamaa na huyo jamaa akaniangalia
na kusema;
‘Shemeji
anajua,…mhh…haya, samahani kidogo, nikisema hayakuhusu…’akasema akionyesha
dalili za kunishangaa, alinitizama kwa muda halafu akageuka kumuangalia shemeji
yake.
‘Na mimi
nataka kujua pia, maana hii sio hali ya kawaida…mtoto anakuwa hivyo, halafu
….hapana, niambieni tatizo ni nini…’nikasema kama mtu mwenye mamlaka
‘Kwanza wewe
ni nani unayetaka kujua mambo ya nyumba hii?’ akaniuliza akigeuka kuniangalia,
ilikuwa sauti ya msisitizo kama mwenye nyumba.
‘Mimi pia
ni kaka wa mtoto, …’sasa nikajifanya ni
kaka wa mama mjane, ili niweze kuingiza miguu yangu
Akaniangalia
kwa uso wa kujiuliza, hakusema neno, na mimi nikaendelea kuongea
‘Kama mjomba
wa mtoto, ….nataka kujua kwanini imekuwa hivi, mtoto alikuwa mzima ghafla akaanza
kuumwa, na wewe umekuja, umemshika kichwani akapona,….na hutaki tumpele
hospitalini, kuna nini kinachoendelea
kwenye hii nyumba,… , hebu dada niambie, maana hili sio jambo la kawaida..’sasa
nikajifanya ni kaka, mjomba wa mtoto mwenye mamlaka, wajomba wana mamlaka yao.
‘Ndio
hivyo, kama ulivyoona, inaniuma kwa kweli,lakini nitafanya nini, ni hivyo kama
ulivyoona akianza kuumwa hapo ni …aah, inakatisha tamaa, sasa mimi sijui, wao
wanadai eti kuna mizimu…’akasema
‘Wao
akina nani…?’ nikauliza
‘Si hawa
baba zake,…sasa mimi sijui kwanini mambo kama hayo yanawafuta watoto wadogo
wasio kuwa na hatia…’akasema
‘Ni ajabu…basi
ni wachawi…’nikasema hivyo, na jamaa akatabasamu kwa dharau huku akitikisa
kichwa, huku mama mjane akiendelea kuongea;
‘Hawa
watoto masikini ya mungu wana makosa gani, …wangenifuata mimi basi, si mimi
mkosaji, basi iniandame mimi, sasa..sasa…kwanini wananitesea watoto
wangu….’akasema huyo mama kwa uchungu.
‘Anayewatesa
watoto ni wewe usiyetaka kuelewa shemeji, mimi nilishakuambia hilo, hiyo ni
mizimu, huyo ni baba yake, hataki maswala hayo unayoyataka kuyafanya wewe…..,
nilikuambia kabisa achana nayo, naona kama ulitaka kufanya kitu, unataka kufanya
nini wakati kesho hawa watu wanakuja kumalizia tatizo, yeye huko alipo hana
raha, yaonekana hivyo, ogopa sana deni, hata ukifa, utasumbuliwa tu…’akasema
‘Deni…?’
nikauliza kama vile sijui kitu
‘Hebu
shemeji……hivi nikuulize wewe unaona nyumba hii ina maana sana kwako, kuliko
afya ya mtoto, kuliko,..ina maana unataka mwenzako huko alipo aendelee
kuteseka, eeh…’akasema akionyeshea kidole kuzungusha hewani, kuonyesha nyumba
‘Bado
mimi sijaelewa…’nikasema na jamaa hakujali yeye akaendelea kuongea;
‘Shemeji,
hawa watoto wakipata shida watakuja kukulaumu wewe kwa kujali mali zaidi,..muhimu
ni afya yao, muhimu ni uhai wao,…hivi huyo mtoto akifa, hatuombei mabaya,
lakini kwa jinsi tulivyoambiwa, ukichelewa tu,….ukiendelea kufanya hivyo mara
tatu, ikamtokea mara zaidi ya tatu, mtoto utamkosa, sasa utakuwa na furaha
gani, hata ukiipata hii nyumba na mtoto keshakufa….hutakuwa na raha yoyote…’akasema
huyo jamaa.
‘Samahani
kidogo hapo…, ni nani atamuua huyo mtoto
ndio hiyo mizimu, au….mimi nijuavyo mtu akifa anakufa kwa mapenzi ya mungu au
sio,…’nikasema na huyo jamaa akanitupia jicho la dharau, halafu akasema;
‘Lakini ….eeh,
wewe mwenyewe si-umeshuhudia hapa, huyo mtoto alikuwa na
hali gani, , ….jinsi mtoto alivyobadilika, si uliona, sasa nikuambie kitu, sisi
hayo, tulihangaika nayo, mpaka basi, hebu jiulize, ….je sasa nisingelitoka kwa
muda muafaka ingekuwaje, hebu niambie unafikiri kingetokea nini hapo, walisema
ikitokea hivyo, mtoto akaachwa saa moja,…basi…tunakwenda kuzika’akatikisa kicha
kusikitika
‘Kweli…..ni
nani huyo ana mamlaka ya mungu..!!’ nikasema kwa mshangao
‘Ndio..hivyo..sio
mamlaka ya mungu.., akiwa katika hiyo hali, damu imesimama,…akaachwa zaidi ya
saa moja akiwa kapoteza fahamu, wewe unafikiri itakuwaje, hata kitaalamu
tu,wewe si umesoma kidogo..damu ikiwa haitembei mtu anakuwaje…?’ akaniuliza
‘Sijakuelewa…’nikasema
‘Tatizo
labda shule haikupanda..ila hali hiyo ya kupoteza fahamu ni dalili mbaya,
mwanzoni alikuwa hapotezi fahamu , ni joto tu kuwa kali, sasa hii,…ya kupoteza
fahamu kutokana huyo mtaalamu alivyosema hiyo ni dalili mbaya shemeji …achana
na hiyo tamaa, nyumba, nyumba ….nyumba kitu gani mbele ya uhai wa mtoto ,….’akasema
akimuonyeshea kidole shemeji yake.
‘Lakini
sijafanya kitu shemeji….huyu ….huyu , she-, eeh,… kaka yangu, alikuwa
akiniulizie jinsi gani tulivyofuatilia, nikataka kumuonyesha jinsi
tulivyohangaika, sasa…..’shemeji akamkatiza kwa kusema.
‘Shemeji
hao jamaa hawadanganyiki,..unajidanganya mwenyewe…huyu sijui nani, au yoyote
yule hataweza kukusaidia kwa hili, vinginevyo, walipe deni, au sio…’akasema ,
halafu akanigeukia na kusema.
‘Kwani
wewe unasemaje, una…taka nini …?’ akaniuliza na mimi badala ya kumjibu
nikauliza swali
‘Jamaa
gani hawadanganyiki..?’ nikauliza
‘Mizimu….’akasema
na kabla sijamuuliza swali jingine akasema;
‘Unajua
ndugu, Sisi tumemuhangaikia sana huyu mtoto na ndio tukaambiwa ni baba yake
hataki maswala ya kesi, …na baya ni kuwa kaondoka duniani akiwa kaacha deni,
hilo deni linamtesa, kwahiyo anataka hilo deni lilipwe kwa gharama yoyote
ile,….ili yeye aweze kupumzika huko alipo, kauli ya marehemu ni muhimu sana,
maana hatujui huko anapata shida gani….., sasa huyu shemeji yangu sijui haelewi…’akasema
‘Kauli ya
marehemu, alitamka lini…sijakuelewa hapo, yeye, keshafariki, au sio, sasa hiyo
kauli aliitoa lini, kabla hajafariki au baada ya kufariki..?’ nikauliza na
jamaa akanitupia jicho la haraka, ilionyesha kama mshtuko, au …
‘Haijalishi….muhimu
ni deni….’akasema
‘Ohooo
kwahiyo kumbe, nilikuwa sijaelewa, ….kwahiyo kumbe mtoto alipoanza kuumwa ndio mkaenda
kwa mganga,au sio? Si ndio hivyo au? Na huko mkaambiwa kuwa tatizo lake sio la hospitalini,
ni maswala ya kimila, au sio…?’ nikauliza na kujifanya nipo pamoja na yeye
‘Haswa,…..lakini
hatukuanzia kwa mganga, hapana…..wewe, usininakili vibaya,…sisi sio watu wa
namna hiyo…kwanza tulihangaika na mambo ya hospitalini, kila akipimwa hana
tatizo, mtoto anazidi kuteseka, homa haishuki….mtoto anaweweseka, wengine wakasema
ni degedege, wengine UTI, naimonia na nini sijui ..lakini kwenye vipimo hakuna
kitu kama hicho, akifika hospitalini mzima hajambo,, sasa ana tatizo gani, ni
shidaa..’akasema
‘Mlikwenda
hospitali gani…?’ nikauliza na hakunijibu akasema
‘Ni kama
ulivyoona leo, ….je nikuulize wewe , ulipokuja hapa ulikuta huyu mtoto anaumwa….?’
Akaniuliza
‘Hapana
alikuwa mzima kabisa…sikumuona na dalili yoyote ya kuumwa,japokuwa anaonekana
mdhaifu tu, hiyo ni dalili kuwa anaumwa umwa, au sio…..’nikasema
‘Sasa
umeona, kuna mambo yakifanyika mambo amabyo yanakwenda kinyume na matakwa,
maagizo tuliyopewa, miiko….mtoto huyo huanza kuumwa,…’akawa anachezesha mkono
kama anaongea jambo, lakini sasa akawa hatamki neno kwa sekunde kadhaa, baadaye
akasema;
‘Ujue na sisi awali tulikuwa hatujui
hilo….tunahangaika huku na kule, hospitalini ,dawa hizi na zile…wakati tunafuatilia, maswala ya mkopo, maswala ya
deni, kumbe hayo ndio tatizo,hatujui masikini,, twauliza huyu mtoto ana nini,
mbona hivi, mtoto anaumwa haponi….homa inageuka sasa kama anapandisha mashetani,
mtoto mdogo apandishe mashetani, wapi na wapi, ….tuliona ajabu
sana….hospitalini akipimwa, hana ugonjwa,…’akatulia
‘Mara kwa
bahati akatokea mzee mmoja, akasema nyie huyu mtoto mpelekeni kwa mtaalamu,…kwa
mtaalamu!, ….’akasema akitamka neno hilo la mwisho kwa mshangao.
‘Ndio….tukabakia
kuulizana ni nani huyo mtaalamu…. Unajua tena sisi wa siku hizi mambo ya waganga wapi na wapi….lakini sasa
tufanyeje, na mimi ndiye baba yao, nikamwambia shemeji hilo…shemeji naye ndio
mambo hayo hayajui kabisa, …nikaona na yeye anasita sita, Mimi nikaona hakuna
jinsi, mimi ni baba yake…nikaanza kazi ya kuulizia,maana hao watu wapo wengi,
na wengine hawaaminiki…nikampata anayestahiki….’akaonyesha mkono wa kishujaa
akiwa kakunja ngumi.
‘Na kwa bahati
nzuri kipindi hicho hapa nyumbani kulikuwa na ndugu yake shemeji, yeye
alikuwepo hapa kumsaidia dada yake…yeye ni mkubwa kwa shemeji, ana akili za utu
uzima akajitolea kwenda na mimi, ….tukaondoka naye…kama angelikuwepo mungemuuliza
vyema yeye, ….maana mimi nikisema mtaona labda aah...lakini ujue mimi ni baba
yake mdogo, mimi ni mzazi wa mtoto pia, nina
uchungu zaidi….’akatulia
‘Ni sawa
nakuelewa, hebu nieleze mlipokwenda huko kwa huyo, umesema nani..….?’nikasema na
kuuliza
‘Mtaalamu…’akasema
‘Ndio
nani, mtaalamu wa nini, sijakuelewa hapo…?’ nikauliza
‘Wewe wa
wapi eeh...au ndio nyie mnajifanya hamuamini hayo mambo,…shemeji mwenyewe
alikuwa haamini, sasa kipo wapi, amekuja kuamini, huwezi kuamini haya mambo
mpaka yakukute…na hasa kwa mtoto, mzazi lazima utaaumua, labda uwe huna watoto….wewe
una watoto…?’akasema na kuuliza mimi sikujibu swali lake, nikamuuliza hivi;
‘Sawa,
ulipokwenda huko, ukaambiwaje…?’ nikamuuliza, hapo akasimama, akajinyosha
kidogo, na baadae akamuangalia mama mjane, …baadae akaanza kusimulia…
NB: Alisema
nini huyu jamaa…ngoja niishie kwanza hapa, kabla hatujaenda huko kwa mtaalamu.
WAZO LA LEO: Utu wema ni pamoja na kujali,…kujali
wenzako, kuwajali watoto wa wenzako, sio kuwajali watoto wako tu, kumbuka
ukijali watoto wa wenzako na wa kwako pia watajaliwa,..wema huzaa mema, na kamwe wema hauozi.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment