‘Mungu
wangu’…nilijikuta na mimi nimesema hivyo
Kiukweli
matukio ya siku hiyo, yalikuw ni mtihani kwangu, maana pamoja na nia nzuri
niliyokuwa nayo kwa hii familia, lakini baada ya hayo matukio, …niliwaza mara
mbili tatu…maana jiulize litokee jambo baya kwa mtoto, mim nitajielezaje, hasa
jamaa akielezea kuwa mimi niliambiwa hayo mambo na mimi nikapuuzia,
Mama
ataulizwa je, ni kweli, akisema ni kweli nimekwiisha
Kiukweli
pale nilianza kujilaumu mimi mwenyewe..nikiona huenda nimefanya kosa,..mimi
ndiye nimesababisha kifo cha huyo mtoto,
maana mtoto nilivyomuangalia, hana dalili ya uhai,..sasa imegeukia kwa mama,
naye kwa hali kama hiyo kama ile hali ya kupooza mwili itamrejea, siji
itakuwaje
Wakati sasa mimi nahangaika na huyo mama,
awali nilimuona jamaa akihangaiak na simu yake, ni kama anaandika ujumbe kwenye
simu, kwa muda huo alijifanya kama hana wasiwasi, mimi kwa hasira nikasema;.
‘Hebu
fanya jambo wewe mtu mbona umesimama tu..huu sio muda wa kucheza na simu
unakuwa kama mtoto bwana, simu zipo kila siku …., hangaika na mtoto ili mimi
nimuhudumie huyu mama,…au … unajua kufanya huduma ya kwanza,..au basi hata ita usafiri, tuwawahishe hawa watu hospitalini…’nikasema
‘Niwapigie
hospitali gani, utaweza kuita gari la wagonjwa hapa nyumbani, mimi hapa nilipo
sina hata senti moja..najaribu kuomba chochote kwa jamaa yangu hapa,…unasema
nacheza na simu, ..hahaha, hivi unafikiri mimi sina uchungu na hii familia,
hapa natafuta pesa, bile pesa hapa, tutaumbuka…’jamaa akasema
‘Kwahiyo
sasa umenielewa, kuwa hawa watu ni wa hospitalini..?’ nikawa kama nauliza
‘Hospitalini,..wakipigwa
sindani hawa ndio basi tena..na huyo mtoto..hapana, …ngoja kwanza…’jamaa
akasema, na kuanza kupiga namba kwenye simu, kiukweli sikumuelewa kwa muda huo.
‘Unawapigia
watu wa usafiri, au…tuwahi hospitalini..?’ nikauliza
‘Huyu
jamaa namdai pesa yangu, ni tapeli mkubwa,, we acha tu….sasa oh…unajua wewe
haumini nilichokuambia, tatizo hata mtaalamu hapatikani kwenye simu sio kawaida
yake, ..na haya yote wewe ndiye sababu…’akasema sasa akifuta jasho usoni.
‘Huu sio
muda wake, muda huu ni wewe uwajibike kwanza, usilete visingizio vya kupoteza muda, na lolote likitokea baya, unafahamu sehemu yako..’nikasema
‘Ni
lazima nikuambie ukweli …maana mimi nitafanya nini sasa..huyo mtoto..mwili wote
umeshakuwa wa baridi..damu haifanyi kazi, hii ina maana gani ….nilikuambia
lakini, hana hata semu moja ina joto, na mapigo ya moyo, siyasikii kabisa, hii
ina maana gani…’akawa kamsogelea mtoto akamshika mwilini, kuanzia miguuni hadi
shingoni, halafu akaweka kiganya cha mkono usoni. Hapo akahema kwa nguvu.
‘Mama
yangu…’akasema hivyo…hapo sikuona dalili ya kuigiza, hapo niliona uso wa
wasiwasi kabisa, jamaa alikuwa kachanganyikiwa.
Mimi kwa
upande wangu nilikuwa nikijaribu kumuhudumia mama mjane, ili aweze kurejesha
fahamu zake, lakini ilikuwa kazi isiyo na mafanikio, hata baada ya kutumia kila
mbinu ninayoifahamu mimi, maana nilishajifunza hayo yote kupitia huduma za msalaba
mwekundu nilipoona nimeshindwa…huku najifuta jasho..
Kwa
haraka nikachukua simu yangu pale mezani nikampigia jamaa yangu;
‘Halooh,
sasa hali ni mbaya zaidi, fanya haraka, upo wapi kwani, sasa fanya hivi,
wapigie watu wa huduma ya kwanza, ndio kazini kwenu, mimi sina jinsi,…ni
hatari, ni …ukifika utajionea mwenyewe…’nikasema na kumsikiliza
‘Anahitajika
dakitari, na gari la wagonjwa, pia chakula,…ndio, hali zao ni mbaya sana,
hawajala, na zaidi…ndio ndio..jitahidi sana ndugu yangu, hili sio jambo la
kuongelea kwenye simu, haraka..,..’nikasema kwa sauti ndogo ndogo, hata jamaa
yangu hakunielewa nimeongea nini, ..ila pale niliposema;
‘Mje na
kila kitu …nahisi kuna uhalafu, kuna hujuma ndani yake, ni..sina…ila nahisi
hivyo, uje ,, ufanye kazi yako…u…’hapo nikasema kwa nguvu na jamaa akasikia, na
kunitupia jicho….huku akiendelea kulalamika.
‘Sasa unaona, haya yote umeyataka wewe…unaona
wewe mtu…sijui umetoka wapi wewe hukutaka kunielewi, wewe umeweka njaa yako
mbele…huyu mtoto tumeshampoteza, hii hali sio ya kawaida, kama ubaridi umeshaenea
mwili mnima,..ndio basi tena,..mungu wangu na isiwe hivyo, nitafanyaje mimi,…..
sasa na shemeji naye ndio hivyo, hilo ni janga jingine tena..’akasema
akimuangalia shemeji yake…
‘Hata
sijui..’nikasema hivyo, huku nikimpigia jamaa yangu mwingine simu, kujua ni nin
kinachoendelea kwenye kusitisha zoezi la mnada, lakini akawa hapatikani. Jamaa
sasa akamuacha mtoto na kusimama, akawa ananiangalia mimi na kusema;
‘Sikiliza
nikuambie sasa, …hali ya shemeji haikutakiwa kabisa apoteze fahamu, maana ikirudia
ile hali ndio basi tena,… hata sijui itakuwaje…huyu mtu hakutakiwa tena
kupoteza fahamu kwa mshtuko,..unajua ilivyokuwa tena hayo ni maagizo ya docta ,
bingwa wa magonjwa hayo, …unajua, huyo awali alikuwa kafanya nini,..ka-kaparalize,…si
unaelewa matatizo hayo yalivyo…?’ akawa kama ananiuliza na mimi nikabakia kimia
tu
‘Na
hayo,unasikia, ni wewe umeyasababisha, hapo huwezi kukwepa lawama, haya umeyataka wewe mwenyewe kwa ukaidi wako,
sijui wewe ni mtu wa wapi...’akasema sasa akihangaika na mtoto, na mimi sasa
nikamrudia shemeji yake…hapo nikasema;
‘Nimeyataka
mimi au wewe na huyo mtaalamu, wako…, ngoja polisi wafike hapa , utasema yote ,
nataka waje ili hili tatizo limalizike kabisa,…..’nikasema, na niliposema
hivyo, kwanza akanitupia jicho, halafu akasema.
‘Polisi…!!!
Hahaha, polisi watafanya nini kuhusu hili tatizo, haya ni maswala ua kifamilia,
hata wakija nikiwaelezea, watasema kama tulishasema ni maswala ya kifamilia,
basi yaishe kifamilia, maana ni maswala ya kimila..sasa haya umewaita polis
waje kufanya nini…?’ akauliza
‘Kumbe
unalijua hilo, kuwa sio swala la kipolisi ..lakini hata iweje lazima
uwajibike,..najua kabisa unafahamu ni nini kinachoendelea hapa..ndio maana unasema
hivyo, sasa ngoja tukuone ukipambana na hao watu..’nikasema
‘Tatizo
wewe unafikiri naogopa saana, hapana, kwani ni mara ya kwanza kukutana nao…ukweli
ni ukweli hata wakija, hata wakinifanya nini..mimi nitafanya nini, kama sina
uwezo na jambo sina, …waje tu…’akasema kama kujipa moyo.
‘Wewe unalifikiri
natania, nataka kwanza uje kunielewe kuwa mimi ni nani…’nikasema
‘Haijalishi…’jamaa
akasema hivyo
‘Haijalishi
sio…, ngoja hao jamaa waje ndio utaniamini kuwa mimi nipo hapa kwa madhumuni
gani, hatuwezi kuendelea kuendekeza haya mambo, haki ya wajane na mayatima
zinadhulumiwa na watu kama nyie, mnaojifanya wajanja…’nikasema
Jamaa akawa anahangaika na mtoto, huku
anasema;
‘Oh…haya
bwana…ngoja nijaribu tena, ila…mimi sijui huenda nazidi kuharibu zaidi, maana
mimi nafuata tu maagizo…’akasema hivyo, na wakati huo alikuwa kashikilia kile
kichpa chenye unga unga ndani yake,.
Akatoa
unga unga.. akawa anachezesha mkononi halafu akamweka mtoto puani….lakini mtoto
akawa kimia…alipoona hivyo, sasa nikamuona jasho likianza kumtoka…akwa
anampapasa mtoto kuanzia miguuni, hadi usoni…, uso wa jamaa sasa ukawa
umeashiria mashaka na wasiwasi, akafanya tena, alafu akasema;
‘Mungu
wangu..ina maana ni kweli…na hapa nimefanya kinyume na maagizo sikutakiwa
kufanya tena hivyo,…oh, sijui itakuwaje mungu wangu..’akasema sasa akihaha.
‘Ina
maana gani kusema ina maana ni ?…hahaha, sasa omba kusitokea tatizo, likitokea
taizo huyo mtoto akapoteza uhai, ujue wewe utahesabika kuwa ni muuaji,..hilo sasa
ni kosa la mauaji, umeua..mlifanya mkijua mnafanya mzaha..’nikasema.
‘Sikiliza
mimi nafuata alivyosema mtaalamu, yeye alisema hivyo, mimi sijui zaidi mbona
unanipakazia mambo ambayo mimi hayanihusu…’akasema
‘Hayo
utayesema mahakamani ukiwa umesimamishwa kwa kosa la kuua..’nikaema
‘Sikiliza,
ngoja nimpigie huyo mtaalamu mwenyewe,
maana hili sasa ni tatizo…, haiwezekani…uuuh…’akawa sasa kaonyesha
kuchanganyikiwa kiukweli, nashukuru mama mjane alikuwa bado hajazindukana, japokuwa na
kuendelea kuwa hivyo ni tatizo pia
Mimi pale
nikawa najitahidi tena kumpatia
huduma ya kwanza yule mama ili azindukane lakini ikawa …hazindukani, ila
nilihisi dalili ya joto, kuashiria bado uhai upo, nikahisi mapigo ma damu kwa
mbali sana, hapo nikapata matuamini,..ghafla nasikia jamaa akisema
‘Shemeji,
shemeji…..mtoto ame—ame---ku-ku…fa…’akawa anaongea huku kashika kichwa..
**************
‘Wewe mtu
vipi wewe...nani kasema mtoto kafa…’kwa haraka nikamuacha shemeji, na
kumsogelea jamaa, nikamsukuma pembeni.
Nilimsogelea
mtoto,…sasa kwa tahadhari kama vile unashika kitu cha kuogofya, binadamu akili
zetu ni dhoofu sana, hapo akili ilishahisi huyo mtoto hayupo tena duniani,
kwahiyo …..taratibu nikamshika yule mtoto mwilini, mtoto alikuwa baridi…nikahisi
mwili mnzima ukiniishia nguvu kabisa,..magoti sasa yanacheza cheza,…akilini
nasema
‘Mimi
ndiye nimeyasababisha haya…’ nikajikuta na mimi nimeduwaa..nimeshikwa na
bumbuwazi, siamini hicho ninachokiona. Kwa jinsi inavyoonekana mtoto hana
uhai,haiwezekani mwanadamu ukawa baridi hivyo.
‘Ina
maana imekuwa ni kweli…haiwezekani…’nikasema sasa nikizama kwenye ibada,
kumuomba muumba wa mbingu na ardhi, anikwepeshee na kikombe hicho,…kiukweli,
hata mimi ule uwezo wa kuhimili jambo, uliniishia hapo nikiwazia mbali.
Na hapo
hapo machozi yakaanza kunilenga lenga, maana hao watoto nilishawaweka kama ni
watoto wangu, na hali niliyowakuta nayo, haikutakiwa ije itokee jambo kama
holo, nilijikuta machozi yakianza kunilenga lenga. Lakini kwenye nafasi
nyingine ikaniambia; ‘sio kweli, na wala usilie, huo ni uchuro..’
‘Mimi
niliwaambia, mumeona sasa, ….’jamaa akawa anaongea huku sasa yeye analia..nilimuangalia
moja kwa moja usoni, niliyaona machozi yake, sizani kama hiyo ni ya kuigiza,..jamaa
kweli analia, kwahiyo ni kweli mtoto hatunaye duniani.
‘Haiwezekani…’nikasema
sasa nikimkodolea macho yule mtoto.
‘Sasa
mnaona..mimi niliwaambia nini.... wewe ndiye mbishi, wewe ndiye umemshawishi
shemeji akafanya mambo kinyume na miiko aliyopewa, mimi hapo sijui tena la
kufanya….’ Jamaa akasema sasa akigeuka
huku n akule, kawa kama kachanganyikiwa.
‘Sikiliza huyo mtoto hajafa…’mimi nikasema
‘Hajafa, hahaha, utafiki nacheka kumbe moyoni naumia...wewe..na uerevu wako, hujui mtu akifa anakuwaje..shika mapigo ya moyo,
utaniambia…angalia alivyo, mimi ndio nimemfunika macho..huyo mtoto hatunaye tena...mungu wangu sijui mama yake...oops...’jamaa akasema
‘Una uhakika na unachokisema, unajua hatari yake…’mimi nikasema hivyo
‘Niliwaambia
hatakiwi itokee zadi ya mara tatu, ni nani alinisikiliza eeh..mliniona mimi
mjinga, au sio, mimi naendekeza mambo ya..ya….mimi siliniwaambia hivyo jamani…
na miiko imenikataza kufanya lolote baada ya hapo..'akasema
'Mimi sijui ...'nikasema
'Ndug yangu hili ni janga, ...na...na..hebu
ngoja kwanza, nimpigie simu huyu mtu, sijui atawezaje kutusaidia..maana mtoto keshapoa, aliniambia ikifikia hiyo hali haiwezi kusaidia kitu...’jamaa
akasema huku akianza kupiga simu
'Sawa mpigie,...na umuambie kabisa, njama zenu zimeshagundulikana na ...yeye na wewe mtawajibika...'nikasema huku nikimtupia macho yule mtoto pale alipo,..nilihis mwili ukinisisimuka.
‘Jamaa
hayupo hewani,..mungu wangu sasa tutafanya nini..’akasema sasa kijaribu kupiga
simu tena na tena.
‘Hapokei,..simu
haipatikani…’akasema sasa akiwa kashusha mikono ile ya kukata tamaa
‘Polisi
wanakuja, watakuja kulimaliza hili tatizo, itabidi uongee kila kitu, na ufahamu
wapi mtaalamu huyo alipo vinginevyo haya yote yatakuangukia wewe mwenyewe, hizi
zote ni tamaa zenu, na usiposema yote, utaozea jela..’nikasema
‘Kwanini
unasema hivyo, mimi sikuwaambia hayo, ..haya ni mambo ya kimila yanawahusu nini
polisi,,… mimi nafuata alivyosema mtaalamu…’akasema sasa akijaribu kupiga simu
tena, lakini hakuna kitu
‘Kwa
usalama wako, huyo mtoto hali yake
ijirudie ili huyu mama akiinuka hapa amkute mtoto wake yupo salama, vinginevyo,
wewe ndiye umemuua, unasikia, mimi ni shahidi wa haya yote, nimekuja kugundua
kuwa nyie mna njama, sasa kazi kwako….’ Nikasema lakini kusema huko ni kwa
kujipa moyo tu, kama kweli huyo mtoto keshakata roho, jamaa atafanya nini.
Mara simu
yangu ikaita, kwa haraka nikaichukua na kuangalia ni nani mpigaji, …walikuwa
vijana wangu, nikaanza kuongea nao .
‘Vi-vipi
mumeshafika kituo cha polisi, …..sasa waambie waje hapa haraka,…na yeye
mumempata, bado kwanini, sasa sikilizeni,..sikilizeni kwanza..hapa eeh….kuna
tatizo kubwa sana hapa, nimemuambia huyo askari aje, yah..aje haraka..yule mpelelezi
ndio, …msiimcheleweshe tena, ..ndio tatizo kubwa sana…’nikasema na kusikiliza
‘Ok…wewe
unasema nini, ok, ok, nimekuelewa, sasa ….uje na huo ushahidi, ..fanya
haraka…’nikasema .
*************
Wakati
naongea na huyo jamaa yangu...huku kwa Dalali, pamoja alikuwa akihaha huku na kule lakini alipoona naongea kwa simu, na ...akasikia nikiaka polisi,...sasa akatulia na kuanza kusikiliza...na alipoona namtupia jicho, akaendelea kuhangaika na mttoto, mara asimame, mara afanye hiki na kile, ..alikuwa kiukweli
keshachanganyikiwa,.hasa aliposikia nikitaja polisi,
Baadaye akasimama, akiwa kashika kiuno, naona alichoka ile hali ya kuinama akiwa anahangaika na huyo mtoto, akafuta jasho...alisimama vile kwa muda, na baadae kama kakakumbuka jambo, akauendea ule mkoba wake, akatoa chupa,...ilikuwa chupa ya mafuta.
Akarudi pale kwa mtoto, ...
'Mungu wangu nakuomba hii dawa, haya mafuta, yafanikishe,..mimi sijui zaidi ya uwezo wako, huenda nilikosea kutumia hizo dawa zaidi ya mara tatu, mimi sikujua, natarajia uwezo wako tu ..ewe mungu wangu...'jamaa akawa anasema hivyo, halafu, ...
Akamvua yule mtoto nguo zote...
'Inabidi tufanye hivi, ili mafuta haya yapite sehemu zote za mwili, huenda joto litarudi..lakini lisiwe joto la ugonjwa tena...'akasema, na mimi hapo sikusema kitu.
Akampaka huyo mtoto mafuta mwili mnzima, akimgeuza huku na kule, mtoto alikuwa ni kama ...naogopa hata kusema...alipomaliza kazi hiyo ya mafuta, akachukua ule unga tena, akafanya alichofanya, akampaka mtoto tena mwili
mnzima ...halafu, akachukua na maji, akawa kama anayasomea hivi, akawa anamtupia mtoto , anayaweka kiganjani anamtupia mtoto yale maji....jamaa anahangaika
mpaka jasho linamtoka
Akachukua ule unga unga, akamwekea mtoto kwenye matundu ya pua…baadae sana tumeshakata tamaa,…mtoto akapiga chafya
Mimi wakati huo, nahangaika na mama mjane, lakini tena kimoyo moyo naomba huyo mama usizindukane kwanza..hebu fikiria awali
nilikuwa nafanya juhudi azindukane,..lakini kutokana na tukio la mtoto, moyoni nikawa naombea asizindukane mpaka tujue hatima ya huyo mtoto
‘Ndio
yeye kapiga chafya…?’ nikauliza sasa nikiwa nimesimama nikiwaangalia, nilimkuta
jamaa naye kasimama, kaduwaa, ni kama haamini vile.
‘Khuuuuuh,
hata siamini…’akasema huyu jamaa akimuangalia yule mtoto, yule mtoto sasa akawa
anajinyosha, kam vile mtoto akitoka usingizini anayofanya, akafungua macho, …halafu
akaanza kulia..akiita ;
‘Mama
mama….’
Yaani
pale nilipo, nilihisi kama…nimepata kitu gani,…nilihis kama naota, maana,
kiukweli yule mtoto alikuwa kama keshakara roho, sikuamini..hapo hapo mimi kwa
haraka nikamuendea mama mjane nikawa namfanyia huduma ya kwanza kwa haraka,
sasa naombea azindukane haraka, ili mtoto amuone mama yake akiwa na hali nzuri,
sio kama hivyo alivyolala
Nilifanya
juhudi zote....lakini mama akawa hazindukani. Nilimuashiria huyu jamaa amzuie
mtoto asije hapo kwa mama yake, isije ikaleta tatizo jingine tena kwa mtoto, jamaa
akanielewa. Akawa sasa anambembeleza mtoto kiaina, ili atulie.
Nilijaribu
tena na tena kutoa huduma kwa huyo mama, nikamuomba mungu, nikafanya kila
kilichowezekana, lakini mama akawa ..hatikisiki, hakuna dalili ya mapigo ya
moto,…mtihani mwingine!
****************
Jamaa
alipoona shemeji yake hazindukana akasema;
‘Mungu wangu kama ....ni ule sroke, imatokea tena, ya kumvunja mwili huyo mama, hilo sasa ni janga, naye tuliambiwa, na madocta wake, isije kutokea tena, ikitokea tena,..si unalewa mwenyewe, hayo sasa ni mambo ya kisasa, wala sio ya mizumu..'jamaa akasema
'Kwahiyo..?' nikawa kama nauliza
'Kwani..umemfanya nini..wewe si umesema unajua huduma ya kwanza, au...?' jamaa akauliza
'Nimeshamfanyia lakini bado hazindukani....'nikasema
'Mhh..ndio yale yale..mimi sijui kama nitaweza tena..niliangaika naye mwaka mnzima, watu wakakimbia, nikahangaika mimi mwenyewe...usione wanadamu, wanakuona mwema ukiwa an kitu, subiria uumwe, subiria uishiwe...'akasema
'Usiongee sana, fanya unaloweza ...muda..polis wanakuja...'nikasema
'Wewe na polis wako bwana...'akasema sasa akiondoka kwa mtoto na kusogea pale tulipo, akasema
'Anatakiwa apate hewa, hapa hakuna ujanja, ..hatufanyi makusudi...mfunue hivi, ili hewa ipite, kwenye mapafu...'akasema huku akijaribu kuondoa nguo ili hewa ipite kifuani kwa huyo mama.
'Hizi ni dalili zile zile...sasa kama itatokea vile itakuwaje, maana sio kazi ndogo ...?' akauliza
‘Nikuulize
wewe labda haya mumeyafanya kwa mama pia, ilikuwa kwa mtoto, sasa mumeelekeza
silaha zenu kwa mama, kwasababu ni mbishi au sio..mumevizia akiwa keshadoofika
kiimani, au sio…nawafahamu njama zenu nyie watu, ..’nikajikuta nasema hivyo,
sikuwa na uhakika na hicho ninachokisema, kilinitoka tu.
‘Mtoto
sasa hivi yupo safi..ooh, nashukuru sana mungu, … sijawahi, sijawahi kuogopa
hivi..….ila sijui kama itachukua muda, sijui, kama itafanya kazi….maana hii ni
mara ya ngapi sijui, na hii dawa sikuambiwa niitumie kwa mama yake ngoja
tujaribu tu, …’akasema
‘Mimi hayo
sijui hayo unayajua wewe…ngoja polisi afike utawaelezea wewe mwenyewe ni kwanini
ipo hivyo, si unajua walivyo, na huo hapo ni ushahidi tosha, umeharibu ushahidi
kwa mtoto, bado kwa mama sasa….na yule jamaa mpelelezi, unamafahamu sana alivyo…’nikasema
‘Mpelelezi,
..hahaha, wa nini sasa, wewe jamaa bwana,..hivi hujanielewa, kwanini huniamini,
mimi nafanya kujaribu tu, sina ujuzu wowote wa haya mambo…lakini tumuombe mungu
nijaribu huenda ikasaidia, lakini lolote
baya likitokea tusije kulaumiana…’jamaa akasema
‘Aaah,
mimi sijui lolote, ni wewe…kwa upande wangu nimeshalifikisha kwa wenyewe,
wakija wao watajua..mtajuana wewe na wao..’nikasema jamaa sasa akafika kwa
shemeji yake, kwanza akasita, akavuta nguo, na kuacha kifua wazi.
‘Mungu
nisamehe tu…..geuka huko, usiangalia..’jamaa akasema
‘Aaah,
wewe endelea tu, ..najua unajau ni nini unakifanya,…’nikasema
‘Mungu
nisaidie…’jamaa akasema akawa anawewesa maneno haya hayaeleweki akawa anampaak
shemeji yake hiyo dawa, kifuani, akaenda miguuni, akarudi kichwani, ….mama
kimia, hakuna hata dalili ya kuzindukana.
Mara tukasikia
mlango ukigongwa….mimi nikasema;
‘Polisi
hao….’ Kauli yangu ilimfanya jamaa aka chini, ile ya mtu umekamaa mkao kama
umechuchumaa, …na itokee jambo udondoke kwa nyuma, lakini uwahi kukaa, ndivyo
jamaa ilivyomtokea…,
WAZO LA LEO: Matukio mengine hutokea ili
kukuonyesha njia fulani, na ni wakati huo unatakiwa uwe na akili ya kutafakari
kuhusu hili tukio au jambo hilo.., laweza kuwa ni baya, lenye mtihani ndani
yake,..usikate tamaa, maana ubaya huo unaweza kuwa ni ishara ya kukuonya, au kukusaidia kuepukana
na jambo hilo au mengine yaliyopo mbele yako, kwahiyo uchukue tahadhari huku
ukimuomba mola wako akuonyeshe njia sahihi…
Lakini
pia laweza kuwa ni jambo jema, lenye heri na mafanikio kwako, hapo
usilemae,..fanya jitahada ulifanikishe kwa malengo yaliyo mema, na wala
usiingiwe na kiburi, ukajiona wewe umeweza kwa majaliwa yako.
MSHUKURU MOLA WAKO KWA KILA JAMBO
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment