Babu aliniambia, katika
maisha, tafuta mke mwenye sifa ya kujenga nyumba…
‘Mhh..babu…mimi kuoa bado.. .’nikaguna na kusema hivyo.
‘Unasikia mjukuu wangu…kuoa huanzia sasa kwa kuwaza ni nani mke
anayefaa kwako,…’akasema
‘Sawa babu…’nikasema
‘Mke kawaida yake..hubeba dhamana mbili,…mke sio mchezo, ndio
maana wao wana daraja kubwa sana…na heshima yao huanzia pale wanapokanyaga kwenye miliki ya mume wake.
Yeye huja kukamilisha familia, bila ya mke familia inakuwa haijakamilika.
Tofauti na mwanaume ambaye amekutwa hapo….’akasema babu
‘Mhh, kwanini babu…’nikajikuta nimesema hivyo tu. Babu huanzia
mbali kwenye hekima zake.
Mume yeye ana dhamana moja tu kwa vile yeye wajibu wake ndio
huo, hana jinsi, yeye anawajibika kujenga na kuongoza familia.lakini hata weza
bila ya kuwa na mke ..’akaendelea kuongea na mimi bado nilikuwa sijamuelewa.
‘Unajua mjukuu wangu, mwanamke ndiye anayeweza kujenga nyumba au
kuibomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe,..’aliposema hivyo hapo nikashtuka na
kumuuliza;
‘Kwa vipi babu…?’ akaniangalia kwa makini kama kunipima uelewa
wangu.
‘Unaifahamu nyumba ilivyo, hizi nyumba za kisasa kwa mfano…’akasema
‘Ndio babu , si hizi zinajengwa kwa matofali..’nikasema
‘Haswa…’akasema
‘Sasa mke akija kwenye familia, kaolewa na mume wake, tusema
kakuta nyumba, au hajakuta nyumba,sio tija sana..yeye anakuja na sifa hizo
mbili, kuwa yeye anaweza kuijenga nyumba au kuibomoa nyumba..’akasema na
kunikodolea macho, aakongeza kuniuliza
‘Huyo ni nani …?’ akaniuliza
‘Mke…’nikasema
‘Huyu mwanamke akifika hapo, anaweza kuijenga hiyo nyumba vyema
kabisa ikawa nyumba bora, ya kisasa zaidi ikawa na furaha, na maendeleo
yakapatikana, …na kizazi bora kikatokea hapo.
Lakini huyo huyo, anaweza akaja kubomoa nyumba, ikabomoka
kabisa, kukawa ni chanzo cha uhasama ndani ya familia na jamii kwa ujumla, ndio
maana mke anakuwa ni mtu muhimu sana kwenye maisha, bila ya kuwa na wake wema,
amani duniani inakuwa ni kitendawili …’akasema
‘Mhh..babu sijakuelewa…’nikasema.
‘Nimekuambia hivi mwanamke
akifika kwenye familia, anakuwa na sifa mbili, ana sifa ya kujenga au kubomoa…hapo
tupo sawa…’akasema
‘Sawa…’nikasema
‘Lakini kwa mwanamume kwa vile ni wajibu wake kuijenga familia,
ni wajibu wake kuwa msimamizi wa familia, ni wajibu wake kuwajibika na familia
hiyo,…, yeye sifa aliyo nayo ni kujenga sio kubomoa, kwanini abomoe, na wajibu
wake ndio huo kujenga, hilo ni jukumu lake, hana ujanja, na akilikwepa jukumu
hilo, atapelekwa wapi…?’ akauliza
‘Kwa mkuu wa mkoa…’nikasema….babu akacheka.
‘Sawa kabisa, kwa ustawi wa jamii,...na hapa ndio utaweza
kumpata hata kiongozi bora, sifa zake huanzia hapa…kwa mwanamke na mwanaume,
hili kwetu hatuliangalii sana, lakini kuna siri kubwa hapa,…’akasema.
‘Mhh…’nikaishia kuguna.
‘Sasa nikuambia kitu,…mwanamke mwenye sifa ya kuvunja nyumba ni
yule anayenyofoa zile tofari zilizojengewa nyumba kidogokidogo bila hata ya
yeye mwenyewe kufahamu, huku akilalamika kila siku, nyumba ina nyufa, nyumba
haifai, mume hanijali, ..na vitu kama hivyo..…’babu akasemana kutulia na mimi
haraka nikauliza
‘Babu mke huyu anayanyofoaje matofali ya nyumba, kwani hajui kuwa ni kuharibu hiyo
nyumba, na hayo matofali anapeleka wapi..??? ‘ nikauliza
‘Anaweza akajua au asijue kutokana na ufahamu wake ulivyo,..iwe
ni kutokana na ufahamu wa elimu au malezi, na muhimu sana hapa ni kutokana na
malezi, na malezi huanzia hapo kwa mke, mke ndio chanzo cha haya yote…’akasema.
‘Mhh, babu, mara nyumba, matofali, sijakuelewa babu…’nikasema.
‘Sasa ngoja nikufafanulie, mwanamke mbomoa nyumba, ni yule
anayetumia mbinu za ujanja ujanja kupata pato la mumewe, kwa ajenda za siri,…anaweza
kila siku akawa anatunga uwongo au ajenda za siri za kumchomoa mume wake pesa…siku
hizi kuna hii michezo..au anataka magauni ya harusi, vipodozi vya gharama, na
vitu kama hivyo,…na anayafanya haya yote bila kumshirikisha mumewe, kuwa anataka hizo
pesa kwa vitu kama hivyo,…’akatulia
‘Huyu mke,..anafanya hayo akifahamu fika pato la mume
wake,..hebu jiulize huyu mke ana jenga au anabomoa nyumba…?’ akaniuliza
‘Ana…ana..bomoa, sijui…’nikasema kwa kusita sita.
‘Huoni kuwa huyu anachomoa tofari za ujenzi wa nyumba yao,…tuchukulie
mfano katika harakati hizi mume akose kazi, hii familia itakuwajem mke si
atakimbia, jiulize ni kwanini kusiwe na makubaliano ya pamoja ya matumizi hayo….ili
waangalia umhimu wake.
‘Mhh,….lakini…’nikasema
‘Nakuambia hivi…mke huyo hana ufahamu wa mbali kuwa pato hilo ni kwa ajili
ya maendeleo ya familia, kusomeshea watoto, matibabu nk…yeye anachojali ni
ubinafsi wake, kwanini asimshirikishe mumewe, mume wangu nahitaji kiasi kadhaa
kwa ajili ya kufanya hiki, kwa ajili ya kuboresha , muonekano nak…
‘Kama
anayafanya haya kwa ajengda ya siri..basi mke kama huyu, ananyoa tofali moja
moja kwenye nyumba yao na,..mwisho wake nyumba itakuwaje..?’ akaniuliza babu
‘Itabomoka…’nikasema
hapo kwa sauti.
‘Mke
kama huyu, kwa vile ni mbinafsi….atatumia mbinu hizo hizo kwa mambo ya anasa,
nywele za gharama utafikiri hana nywele…anataka mpaka nywele za maiti…na
nimesikia siku hizi kuna asilimia sabini ya gharama hizo za kujirembesha..kukarabati
mwili, yatoke kwa mume ..mapambo nak, ni sawa, lakini …haya kwa mke mwema, alitakiwa
akubaliane na mume wake au sio, sio kutumia ujanja ujanja…’akasema babu.
‘Mhh,
babu kwani kuna wanawake wapo hivyo…?’ nikauliza
‘Wapo,
na wake hawa hawatajali afya za mume, au
hata za watoto wao, au kujali umuhimu wa elimu, yeye anachojali ni masilahi
yake…matokeo yake , mume atakuwa mdhaifu, watoto halikadhalika, matokeo yake ni
kuhatarisha maisha ya familia, ina maana matofali yanazidi kuchomolewa kwenye
nyumba.
Kwa namna hii uimara wa nyumba hiyo, utakuwaje..?’
akauliza na mimi sikumjibu.
‘Mjukuu
wangu kwa kawaida nyumba kama hiyo inakuwa haina maendeleo, zaidi ni ukosefu wa
maelewano, maana kila mtu hapo atakuwa na ajenda yake ya siri, magonjwa ya mara kwa mara yatakuwepo..,
mikopo mingi na maisha ni mashaka mashaka tu…matokeo yake ni nini….’ Akaniuliza
na mim nikakimbilia kuuliza hivi…
‘Na
sifa ya pili ya mke ni ipi.?’ Nikauliza
Sifa ya pili ya mke, ndio huyo mke mjengaji…
Mke mjengaji wa nyumba ni yule
anayefanya juhudi, kuongeza uimara wa kuta za nyumba…kama nyumba ipo kama haipo
atasaidiana na mume wake kuweka matofali, kuendeleza nyumba, na sio kuyaondoa matofali
yaliyopo…’akasema
‘Kwa vipi babu…?’ nikauliza.
.
‘Huyu mke, hata kama hana kazi ya kuajiriwa,..yeye atamsaidia mume wake
kuongeza kipato kwa mawazo, na wakati mwingine anafanya juhudi za halali kupata
kipato, kwa kubuni biashara ndogondogo. Akimshirikisha mumewe kwani hayo yote
ni kwa masilahi ya familia.
Mke kama huyu anakuwa na nidhamu ya pesa, hakuna kitu muhimu kwenye
maendeleo,kama kuwa na nidhamu ya pesa…pesa kawaida yake hazitoshi, kama pesa hazitoshi
ni lazima kuwe na utaratibu mnzuri wa matumizi yake, sio kutumia tu kwa vile
zipo, lazima muangalie umuhimu kwa kila tumizi…mke mjengaji, anayafahamu haya
kwa utaratibu walioyokubaliana na mumewe na akifanya zaidi, hatasita kumwambia
mumewe.
Mke mjengaji, hujitahidi hupunguza matumiz ya ndani yasiyo
ya lazima, hafanyi kwa ajili ya kujionyesha kwa watu wengine, kuwa na mimi
ninacho ..yeey hufanya kwa ajili ya wajibu wake na familia yake, kwa ajili ya
maendeleo ya familia yake....huyu ana nidhamu, ana maadili mema, mke mjengaji
Mke wa namna hii, huwa mstari wa
mbele kutetea kipato cha mumewe kisichukuliwe ovyo nje..kuna jamii, wanafamilia
hupenda kufuja mali ya ndugu yao, na sio wanafamilia tu, hata watu wan je, au
hata mume mwenyewe, anajitahidi kuongea na mumewe asiwe na tabia za ovyo,
kulewa, nak..…mke mwema, hujitahidi kuona mali ya familia inatumika kwa
utaratibu maalumu kutegemeana na bajeti yao.
Mke mjengaji, hujali sana afya ya
mume wake,..anajua hilo ndilo jembe lake katika kutafuta kipato, basi ni lazima
liwe imara,…liwe na afya…kwahiyo yeye atajitahidi kupika chakula bora, usafi wa
ndani, ucheshi, ujirani mwema…kujenga mahusiani mema, ndani na nje..hata
kimataifa.., ili kuongeza baraka , maana kipato ni pamoja na mahusiano na watu
wengine au sio,..sio lazima kila kitu utakuwa nacho, mke huyu huejenga jina
jema la mumewe….sio yule wa kutoa siri za ndani, kwa nia ya kumchafua mume
wake.
.
Mke kama huyu ndiye yule
anayeitwa mke mwema.
Kumpata mke kama huyu ni nadra,
na ukimpata shukuru sana mungu wako…na ukimpata tegemea maendeleo makubwa kwenye familia, na
jamii kwa ujumla, tegemea elimu bora na
makuzi mema ya watoto wa familia, maana mke huyu hujali sana familia yake.
Mke kama huyu ndiye chanzo cha amani duniani,…
Tumuombe mola wetu tuwapate wake
wa namna hii, na wanaume wa namna hii pia. Ili tusiishie kupelekwa kwa mkuu wa
mkoa….
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment