‘Kama ni kweli, mtu umekosea ulitakiwa kukiri kosa na kuomba
msamaha jamani au sio…?’ nikawauliza wajumbe wengi wao wakatikisa kichwa
kukubaliana na mimi..
Mume wa familia akawa bado kainamisha kichwa chini...
‘Lakini hilo halikuwahi kutokea hadi tunafika hapa, ina maana kazi
yetu yot hapa hakiweza kufanikiwa…umeona hata hayo maswali niliyokuwa
nikimuuliza yalikuwa ni namna ya kumzindua, lakini yeye, aliona kama ninamkera,…’nikageuka
kumuangalia.
Bado alikuwa kainamisha kichwa chini...
‘Sasa..labda ni mimi ndiye niliyekosea, ni mimi ndiye natakiwa
kuhangaika, kumuomba msamaha…au wajumbe nimekosea, je ni nani anastahili
kumbembeleza mwanzake, kwa hali kama hii,…ni mkosaji au ni yule aliyekosewa...?’nikawa
nimeuliza hivyo, lakini sikutaka jibu la mtu nikasema
‘Mimi kwa uoni wangu naona bado kuna tatizo, na huenda hilo ni
tatizo sugu...nakiri kusema hivyo,…mungu anisamehe tu…’nikainama kidogo.
'Unamuuliza mtu swali kwanini ulifanya hivyo, makosa kama hayo... anakujibu nilifanya
hivyo kama mume wa familia katika kuhakikisha familia yangu inakuwa salama,…na nilifanya hivyo kama kuwajibika,....hivi hayo makosa yalikuwa na muenendo huo….sawa labda...yapo, ...mengine utasingizia kuwa alifanya hivyo kwa kulazimishwa, labda kwa vile…lakini yaangalie hayo makosa, na muda yaliyofanywa…
‘Sasa kiukweli kwa majibu hayo, ilinifanya nifikirie mara mbili je ni nini
mstakabali wa maisha bora ya mume na mke mwema...hivi nifanye nini mimi...unajua ni kazi kubwa sana kuchukua maamuzi hayo magumu!
‘Je…, ni, nini mstakabali wa watoto wangu...watakuwa wakiuliza baba yupo wapi...lakini je wataishije..watajifunza nini,, ili wawe na maisha
bora, tabia njema,..ili waje kuiga tabia ya wazazi wao..’hapo nikageuka kumuangalia mume wa
familia ambaye kwa muda huo alikuwa bado kainamisha kichwa chini, lakini sasa alikuwa akiniangalia kwa kujiiba.
‘Je maisha mema,…ndio hayo ya kutumia ubabe, uwongo, hadaa, ulevi... na ukikosa hutaki uambiwe umekosa, badili yake unatafuta visingizio...na zaidi hutaki kukiri kosa, …..hapana hatuendi
hivyo, mimi sikulelewa hivyo...’nikamwangalia mwenyekiti, na mwenyekiti alikuwa katulia akijifanya
anaandika andika.
‘Wazazi wangu nawashukuru sana kwa hekima zenu, kwakweli najisifia
kwa kuwa na wazazi kama nyie, kwani mnafahamu jinsi gani ya kuishi na
watu, kwani baada ya haya yote nilitarajia mungelikuwa na hasira na kuniambia
kuwa mimi nimejitakia,…’nikatulia tena nikiwaangalia wajumbe.
‘Ni kweli kwa haya nimejitakia, mwenyewe, wema wangu ndio
umeniponza…kwani mlishanikanya lakini sikuwasikia..nikajiona nimekuwa,
nikajiona naweza kujibea mimi mwenyewe..sasa muda umefikia .., nibebe mzigo
wangu mwenyewe, lakini baada ya yote haya mumekuwa mstari wa mbele, mkiniomba
haya tuyamalize kwa amani, tusameane....ikibidi turejeane...kama mke na mume...haya
nilikubaliana na hayo mawazo yenu, je ..mume yupo tayari kwa hilo…
‘Nimewaelewa sana, na mimi kama binadamu nahitajika kujirudi,
kusamehe na kuangalia kuwa kweli kuna kuteleza, kuna kukosea,..na mkijitambua
kama wazazi, kama mke na mume kama binadamu mwenye utashi, mnaweza
mkayasahihisha makosa yenu mkaendelea mbele..nimelikubali hilo, ...’nikatulia.
Wajumbe wakajikuta wakipiga makofi, sikuelewa wanapiga makosa kwa
lipi hasa, lakini sikuwajali kwa muda huo, …mwenyekiti alikuwa akiniangalia tu,
mama alikuwa kainamisha kichwa chini…
‘Kabla ya kutoa maamuzi yangu, mimi nimefikiri sana, nikaona kuna
haja ya kufanya yafuatayo..’nikasema hivyo na hapo mume wa familia akainua
kichwa kuniangalia…Nilitulia kwa muda,…mpaka watu wakafikiria nimeshindwa cha
kuongea..
‘Kwa vile mume wa familia
lengo lake kubwa ni mali, lengo lake kubwa ni kupata utajiri, lengo lake ni kubwa
ni kuwa na hali nzuri, basi, mimi kwa ridhaa yangu mimi mwenyewe nimekubali
kumuachia kampuni yake, kwa asilimia mia moja…’nikasema hivyo
‘Yeye ...achukue hisa zote, na amilikishiwe moja kwa moja kama
kampuni yake binafsi, …. Mimi sitakuwa na hisa tena kwenye kampuni hiyo, ina
maana ni mali yake moja kwa moja...hilo mimi nimeliamua kwa moyo wangu wote,
kuonyesha mapenzi yangu kwake..na hili wazazi wangu naomba mnisaidie hata kama
kuna madeni, myasamehe…’nikasema na kumuangalia mwenyekiti.
Mwenyekiti akatabasamu kidogo, akawaangalia mawakili, lakini
hakusema neno.
‘Kwa kufanya hivyo, sasa yeye ni tajiri, kwani ana kampuni ambayo
ni yake, ambayo itakuwa haina madeni, na madeni yake anayodaiwa mimi
nitajitolea kuyalipa, ina maana madeni ya kampuni hiyo yatahamia kwangu,
unataka nini tena wewe mwanaume...’nilimuona mwenyekiti akiniangalia kwa macho
makali hapo.
Nakumbuka wazo kama hilo niliwahi kuongea na wazazi wangu
wakanipinga sana, kuwa kwa kufanya hivyo namdekeza mume, lakini mimi nikaona
ndio njia pekee ya kumsaidia mume w familia, ili afikie malengo yake na huenda
akajirudi na kufanya zaidi ya hapo.
‘Mimi nitabakia na kampuni yangu na hisa za mume wangu
zitaondolewa kwa vile nimeshamkabidhi kampuni yake awe yeye ndiye mumiliki, na mimi
sitajihusisha na kampuni yake tena
‘Ila kama akitaka msaada kwangu,kwa ridhaa yake yake mwenyewe nipo
tayari kumsaidia…lakini sasa..
Katika hilo, wapo watu wa karibu yake, watu waliopigana naye bega
kwa bega, hao hawezi kuwaacha, lakini hayo ni kwa utashi wake..anaweza kuwauzia
wenzake hako hao hisa kama washirika wenza…
‘ni vizuri kufanya hivyo, ili kuonyesha wito wema, nakushauri
ufanye hivyo ili kuonyesha ukomavu, na ubinadamu, au sio…watu hao ni aliyekuwa
rafiki yangu,... na pia amuuzie, mpenzi wake wa asili baadhi ya hisa, hili ni
pendekezo langu ndio maana nikaamua kuyachukua mdeni yote ili muweze kuanza kwa
pamoja.
‘Nwaombe mfanya kazi hiyo kwa pamoja na kwa bidii kubwa,..nina
imani kuwa mtafanikiwa,…nawafahamu wote kuwa ni wachapakazi…hodari…, hii
itawasaidia wote, na ile ndoto yao ya kupata utajiri itakuwa
imekamilika,..natumai wakiwa pamoja wataweza kufanikisha hili jambo, na ndio
njia mojawapo ya kusaidiana..
‘Mimi nimeona tusaidiane kwa hilo, ili kila mwenye nacho amsaidie
na mwenzake, kwani huenda haya yote yasingelitokea kama watu tungelipendana,
wale walio nacho japo kuwa kidogo, wawasaidie wale wasio nacho, na
kupandishana, katika namna ya kupeana majukumu, sio kupeana tu kama zawadi...ingelikuwa
hivyo, nina imani dunia hii ingelikuwa
ya upendo na amani..
‘Lakini pamoja na yote hayo, nafahamu kuna watu hawatosheki,
nafahamu mtaka nyingi nasaba, anaweza akakosa yote, kama bado mume wa familia
hajatosheka na hilo…’ nikatulia kidogo
Mimi nilimuuliza swali kubwa, je yeye anataka nini…hakunielewa
nilikuwa na maana gani, nilitaka awe muwazi tu….hakuweza kunijibu, ila mimi
nimeona ni kitu gani anakitaka, sasa je hilo hajatisheka nalo…
‘Kama hajatosheka na hili sijui mimi nitamsaidiaje, mimi kwa
mtizamoo wangu, kama yeye hatariziki na hilo, itabidi twende mahakamani,…itapibidi
turudi mahakamani ili sasa sheria ichukue mkondo wake,.. ili haki yake
ipatikane, anayoitaka yeye,..
Na ikiwa hivyo basi mkataba wetu upo wazi utasimama hayo
yote,..mkataba wetu ni ushahidi tosha, mengi tuliyaficha ficha ili kesi ibakia
huko kwa wauaji watu, lakini haya yetu tuliona tuje tuyamalize hapa nyumbani..
Sasa kama mume wa familia hajarizika na hilo, basi mimi sitarudi
nyuma tena, ...mkataba utafanya kazi yake na yeye hatakuwa na haki ya kupata
kitu chochote, sasa ni uamuzi wake...’nikasema na kumwangalia mwenyekiti.
Mwenyekiti akatulia kwa muda halafu akaniuliza, ...’mbona
hatujakuelewa, hatujasikia maamuzi yako, au hayo ndio maamuzi yako ya mwisho...,
?’
**********
‘Nilisema kabla sijatoa maamuzi yangu,nilitaka niyaweke hayo wazi,
nilitoa hayo kama utangulizi, kabla sijatoa uamuzi wangu, ...nimefikiria sana…
Kwanza…nielewe wazi, moyoni nimeshasamehe yote yaliyotokea, na
walionikosea nimeshawasamehe, akiwemo mume wangu, rafiki yangu na wengineo
....kama binadamu yeye anastahili kusamehewa, natumai hatarejea makosa kama
hayo tena.
Niliposema hivyo mwenyekiti akatabasamu, mama ndiye aliinua kichwa
akaniangalia kwa macho ya mshangao…
‘Kama alivyosema mwenyekiti, kusamehe ni wajibu wangu, ni hilo
nimelitimiza, na nilishamwambia mwenzangu kuwa sina kinyongo nayeye tena..,
lakini nataka kuyasema haya kama binadamu wa kawaida..
‘Baada ya yote hayo na kuyapima yote kwa makini zaidi, mimi
nimegundua mengi, ambayo yatanifanya nitoe maamuzi yangu kama binadamu, natumai
mtanielewa, kwa hayo nitakayo yasema....’nikatulia na watu wakaguna, kukawa
kimiya.
‘Unajua kuna kitu kimoja nimekiwaza sana…ndoa ni ya mke na mume,
ni mafungamano yenye usawa, kila mmoja anawajibika kutegemeana na hali yake..na
nafsi ikubaliane na hilo..kama nafasi haitaki huwezi kulamisha, au sio..lakini
kama unaweza ukasema nitajitahidi basi, pambana na nafsi yako..mungu
atakusaidia,...
‘Nilishaongea na mwenzangu na kumtaka asome katiba yetu
vyema, ili sije akasema mimi nilikuja kubuni Katiba nyingine, lakini alikataa..hilo.
‘Yeye alikuwa kaninunia tu, na kubakia kuniangalia kwa macho ya
hasira na chuki,na alipoanza kuongea alikimbilia kunilaumu mimi na wazazi wangu
kuwa ndio tumesababisha haya yote, hadi akawekwa ndani, kwa kosa ambalo
hakulifanya, na aliyofanya yeye, alikuwa akiyafanya kwa minajili ya kuilinda
familia yake, alijitolea muhanga kwa ajili ya familia…ni sawa, kama
mlivyoona au sio kwa hilo namshukuru
sana.
‘Lakini hawezi kututupia sisi lawama mimi na wazazi wangu....jamani
hivi ni sisi tuliofanya hivyo, au ni matendo yao mabaya... je kwa hayo
aliyoyatenda ni nani angelistahili kumkasirikia mwenzake...hapo mimi sikumuelewa...’nikatikisa
kichwa.
‘Ina maana kweli mtu hajajifunza kwa hayo yaliyotokea, kuwa yeye
ndiye mkosaji, yeye ndiye aliyestahili kuomba msamaha, na kunyenyekea
kwangu, na kwa hawo walioathirika kutokana na matendo yake machafu.
Hivi kama mzazi, angelifurahia mtoto wake afanyiwe hivyo, au hata
hilo la kumbaka mtoto wa kazi ni mbinu za marehemu…, kamuharibia mtoto wa watu
mipangilio yake ya maisha...hilo halioni, na lo hilo ni kosa langu.
Haya labda..kama anavyodai labda, mimi sikuweza kumtosheleza…...yote
kwake anaona ni kuwa hay a aliyoyatenda kama mume wa familia,..yeye anaona
alivyotenda ni sawa tu kama anavyodai kuwa alifanya hayo akijua anawajibika
kama mwanaume,labda kwa vile alikuwa akitafuta mtoto wa kiume, lakini kawapata
wangapi, mbona alikuwa bado hajatosheka
‘Kwa mtizamo huo ninakuwa na mashaka, ,...msahamaha upo pale pale,
nimeshamsamehe…lakini…’nikatulia kidogo
‘Huenda mwenzangu bado haajtosheka, huenda mwenzangu bado
anahitaji muda wa kujirusha na kila mwanamke anayempenda, huenda nafsi yake
ilikuwa haijatulia, ndio hivyo tena, yeye alinioa tu kwasababu kuna kitu
alikitaka,…mali,
Lkini mali haiji hivi hivi, inabidi tufanyie kazi, ndivyo nilivyokuwa
nafanya mimi, nilijitahidi kumjenga afahamu hivyo, natumai atayakumbuka maadili
yangu kwenye kazi zake.., akiwa kama kiongozi mkuu, atajua kwanini nilikuwa
namfanyia hivyo, akiwa sasa hamtegemei mtu atakuja ni kwanini nilikuwa nafanya
hivyo....’nikamwangalia na yeye akawa ananiangalia kwa macho ya dharau hivi.
‘Sasa mimi nimeona nimpe kile alichokuwa akikitaka, natumai moyo
wake utarizika, na huenda akatulia, ..huenda, akawa mume mwema, na kuweza
kujenga familia yake kwa amani na upendo, maana watu wa namna hii hawatosheki
bwana, lakini sasa atafanya hivyo akiwa anataka nini tena,...’nikatikisa kichwa
kama kusikitika.
‘Mimi nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kutimiza wajibu
wangu,sikuwahi kuvunja masharti makubwa ya ndoa hata siku moja, ina maana mimi
nilikuwa mjinga, au sikuwa na vishwawishi vya hapa na pale…ina maana mimi
sikuwa na tamaa ya kimwili,..
Wapo watu walikuwa
wananikera, lakini mimi nilifahamu kabisa kuwa ni mwanandoa, na ndoa ina
masharti yake, ...nikayatimiza, ina maana mimi nilikuwa sina hisia za
kibinadamu kweli, ina maana mimi nimeumbwa kwa jiwe, hapana sio kweli hata mimi
kama binadamu hali kaam hiyo ilikuwa ikinishika, lakini niliweza kuitawala
nafasi yangu.
‘Kwakweli kila nikiliwazia hilo ninaumia sana, kwa ujumla
nimekwazika kupita kiasi, nimezalilika, hasa pale ninapoambiwa sikuweza
kutimiza wajibu wangu ndio maana mwenzangu akafanya hayo...
‘Jamani..hamfahamu jinsi gani mwanamke anavyojisikia pale mume
wake anapotembea na wanawake wengine wakati yeye ni mke wa ndoa, inaumiza mtu
kisaikolojia, unajiuliza mawali mengi, hivi mimi nina kasoro gani,
hivi..hivi...unaumia sana, lakini ni nani atalifahamu hilo...’nikasema kwa
machungu.
‘Lakini mungu ni mkubwa ukweli mara nyingi una nguvu, ukweli
ukadhihiri, ukweli ukajileta, na mambo sasa yapo hadharani, kumbe hayo
waliyapanga hata kabla hawajaingia kwenye ndoa, walichokuwa wanakitafuta ni
sababu tu,...na sababu ikapatikana,…tunabakia kumsingizia marehemu…
‘Sawa mimi nakubali nifanyeje sasa…au sio.. ndiooo, kama binadamu
hata mimi nilikuwa na madhaifu yangu, kama alivyodai, kuwa mimi mara nyingi
sikuwa karibu naye, kutimiza wajibu wangu wa kindoa
Lakini hilo lilikuwa swala la kuongea, mimi ningelimuelewa au sio....hakuniambia,
hakulalamika mbele yangu…mume na mke ni kuambizana, kubembelezana, ..ina leta
raha zake…, akafanya aliyoyafanya kwa wale wa chapu chapu, wasiohitajia hayo,
pesa ikaongea au sio.....lakini hicho ni kisingizio tu, walishayapanga hayo
kabla, wakishirikiana na mwalimu wao...wameshajieleza hayo, ushahidi upo…
‘Udhaifu wangu, haukuwa wa kuvunja masharti makubwa ya ndoa, ni
yale ya kibinadamu na kwenye mkataba tuliyaanisha hayo, yapo mapungufu ya
kibinadamu, yanasameheka,....sio hayo aliyoyafanya yeye, ya kukiuka miiko ya
ndoa, na kwenda kuzini nje, hadi kupata watoto, hawo watoto wanadai haki yao,
kwanini walizaliwa hivyo, na wengine wanatelekezwa
Haya mnayaona mitaani au sio..haya ni kwasababu ya tamaa ya watu
kama hawa wasio na maadili mema, hawa watu tutaishi nao mpaka lini, kwanini
kusiwe na njia ya kuwawajibisha, eti jamani mimi hapo nakosea, ni lazima wawaji-...’nikasema
na kumwangalia binti wa hiari wa wazee wangu, aliyekuwa mfanyakazi wangu wa
ndani, alikuwa bado hajaondoka. Alikuwa analia…
************
‘Na nimesahau jambo moja la muhimu sana, huyu binti wa hiari,
nimeamua kuwa nitamuajiri mimi kwenye kampuni yangu, nitaangalia jinsi gani ya
kumsaidia,kabla hajapata hiyo ajira.
‘Naamua kuchukua dhima hiyo, kwa vile mimi ndiye niliyekwenda
kumchukua kwa wazazi wake, yeye alikuwa katika mikono yangu na yote yalitokea
kwenye nyumba yangu, mimi ndiye nabeba dhamana hiyo, mimi mwenyewe nitamsomesha
na nina imani baada ya miaka mitatu atakuwa tofauti...namjenga rafiki mwingine
mpya
‘Mimi...sitachoka kusaidia watu pale inapowezekana, nina imani
baada ya muda huo, hatakuwa huyu binti tena....’nikasema.
‘Baada ya kusema hayo, ... ..., kama ilivyoanishwa kwenye
mkataba wetu wa hiari, na kutokana na ushahidi uliotolewa mimi nimeona ndoa
yetu ifikie kikomo na kila mmoja aangalie ustaarabu mwingine, kwani hata bila
kauli yangu hiyo ndoa ilishavunjika, au sio jamani…?’ akawa kama anauliza
‘Ndio hivyo hata kidini, kaulizeni mtaambiwa,..maana mkataba
tulisaini wenyewe kwa hiari zetu tukiwa na akili timamu,…tukakubaliana mtu akazini…na
ushahidi ukapatikana, adhabu yake ni nini… mungu ni shahidi yangu kwani
kanisaidia kutoa ushahidi…, ni dhahiri kuwa ndoa haipo tena...
‘Mwenyekiti alisema kama mtu hajatenda hiyo dhambi ajitokeze, haya
mimi hapa najitokeza sijawahi kuifanya dhambi,...mungu ni shahidi yangu, na
hata kama watu waliniona nikiwa na docta, tulikuwa naye tukiongea tu, mimi na
yeye hatukuwahi kuvunja amri hiyo kwenye mkataba wangu,...kwahiyo mimi nimetimiza
wajibu wangu,…
Hapo mimi nitasemaje nawaombeni mnisaidia hapo…ni kweli mimi
nilimpenda mume wangu lakini je kuna upendo wa sehemu moja….atasema ananipenda,
je ni kweli ananipenda, upendo wa kuigiza, hapana asema ukweli wake tu,..na
ukweli upi tena,...naombeni sheria ifuate mkondo wake....
Na naombeni mnielewe, Maamuzi
yangu ya kuachana na mume wangu, ni kuonyesha upendo wangu kwake, kuwa mimi
najali hisia zake,...kuwa yeye ana mpenzi wake wanayependana naye sana, ..mpenzi
wake wa asili…
Najua hata alipo anatamani awe naye, lakini kutokana na nakama za
kimaisha, walishindwa, sasa wanazo mali, sasa wao ni matajiri, wanaweza kuishi
kwa raha, nafiki ndoto yao sasa imetimia, au sio wenzangu...sasa wana mali,
...kwanini nisiwape nafasi hiyo,sitaweza kuwadhulumu kwa hilo, ndoa yangu na
mume wa familia imekwisha, na nashukuru mungu kwa yote hayo, na sio nasema
hivyo kuwa nina kinyongo tena, hapana nimeshawasamehe...
‘Ninachokifanya hapa ni kuwa sitaki kuwatendea dhuluma kwa vile
walikuwa na hali hii au ile, nimechukua maamuzi haya magumu, kwa vile nampenda
sana mume wangu, na nataka arikie na nafasi yake...’nikatulia kidogo.
‘Kama mlivyoona, mimi nilikuwa na mume ndani, nikijua kuwa
mwenzangu yupo na mimi kumbe alikuwa akinivunga, na kunipaka mafuta kwa mgongo
wa chupa....sasa muda umefika, yeye na mchumba wake wa asili wapo huru, baada
ya taratibu zote za kuvunja ndoa yangu, talaka na kila kitu, wao watakua huru
kuoana...hakuna kizuizi hapo,...’nikasema na kumwangalia aliyekuwa mke wa
docta.
‘Lile swala la kuwa eti kwasasa kajifunza, hatarudia tena, mimi
bado linanitia mashaka, na ninaona nisitumie mwanya huo kuwaharibia upendo wao
na mpenzi wake wa asili, nilishaongea na mpenzi wake huyo na tumekubaliana
mambo fulani fulani, ..
'Kwa ujumla mimi sioni kwanini wasioane, wanahitaji nini tena,
sioni kwanini mpenzi wake huyo aende akaanza maisha ya kipeke yake huko
kijijini, akae hapa, wafanye kazi, tumeshaliongea hilo na yeye japokuwa
hakukubali moja kwa moja, lakini natumai wakikaa na mwenzake, watakubaliana
kuhusu hilo..’nikasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia halafu aliyekuwa
mke wa docta.
Docta alikuwa kashika shavu
utafikiri hayupo kwenye kikao, naona alikuwa akiumia sana moyoni.
‘Sasa kazi ni kwenu wapendwa..ila cha muhimu, nawashauri tena na
tena, kazi kwanza, hayo mengine baadaye, ni muhimu sana hilo, muhangaike, ili
muweze kuuendeleza huo utajiri kwani haukuja kirahisi hivyo, unahitajika
kuwajibika, msilale, fanyeni kazi kwa bidii, nina imani mtafanikiwa, na kama
mkihitaji ushauri wangu mimi nipo, tutasaidiana pale mtakaponihitajia, lakini
kwa nia ya kutoa ushauri tu.
‘Ama kwa yule aliyeitwa rafiki yangu, mimi sina kazi naye tena ,
nilichofanya kwake ni kumsaidia, na kwa vile keshakuwa na anaweza
kujichukulia maamuzi yake mwenyewe, basi, ....naona nimuache, kama nilivyoshauri,
yeye apewe hisa kwenye hiyo kampuni,wanaweza kujiunga kwa pamoja wakajenga
kampuni yao ikawa yenye nguvu.
Mimi nina imani nguvu hizo zikukutana kwa pamoja, kutakuwa na
maendeleo makubwa sana..kwasababu nyote mnafahamiana, au sio...yeye sasa ana
uwezo huo , hata wa kujiajiri yeye mwenyewe...sina wasiwasi na yeye, ...na
nimemwambia kama atahitajia msaada kwangu mlango upo wazi
‘Hayo ndio maamuzi yangu, na sina zaidi naomba mawakili wetu
wayaweke hayo sawa, na taratibu zote za kutalikiana zifanyike kwa amani, nataka
hili zoezi lifanyike kwa amani ili baadaye tukikutana tukutane kama marafiki,
hakuna chuki wala kununiana, au sio jamani…
‘Hayo ndio maamuzi yangu na hakuna kurudi nyuma, nawaomba wazazi
wangu walipokee hilo , wakijua kuwa mimi sasa sio mtoto mdogo tena....’nikasema
nikiwaangalia mawakili wetu na wazazi wangu, nilimuona mama akipitisha mikon
usoni na kujifuta machozi....
‘Na kwa hivyo basi, ili kuweka mambo sawa, na kumhakikishia mume
wa familia kuwa mimi sina kinyongo na yeye tema, nawaomba mawakili, wafanye
taratibu za kisheria kuziondoa hisa zangu kwa kampuni ya mume wangu na
kumumilikisha yeye, ...na pia waziondoe hisa za mume wangu kwenye kampuni
yangu, na madeni ya kampuni y amume wangu yahamishiwe kwangu..
Na kwahiyo mimi nitamiliki kampuni yangu peke yangu, na yeye na
wasaidizi kama watakubaliana wataangalia ni nani apate kipi ...nafahamu mume wa
familia atakuwa na hisa kubwa kama mumiliki, ..wengine watakuwa na hisa zao
ndogo ndogo, lakini sitawasaidia kwa hilo, hilo wakubaliane wao wenyewe...
‘Na kwa vile mume wangu ndiye mkosaji, mali nyingine alizozikuta
zitabakia kama zilivyokuwa, kama alivyozikuta, ni mali yangu na watoto wangu
...ama kwa nyumba, ile nyumba,…nyumba aliyokuwa akikaa kwa sasa baada ya kutoka
kuumwa na kifungoni , ile ni mali ya kampuni yake, basi itakuwa ni mali yake,
sina haja nayo, ...’niliposema hivyo, mume wa familia akainua uso na niliona
ukikunjuka na zile hasira alizokuwa nazo usoni zikayeyuka..
Akatabasamu…
‘Mnaona wenyewe, ni nini kilichokuwa kikitafutwa, natumai
keshakipata, mimi namtakia maisha mema, na hili liwe fundisho kwake, na kwa wenzake,....mwenyekiti
mimi naona nimemaliza....’nikasema huku machozi yakinilenga lenga. Mume wa
familia alikuwa kavaa miwani, naona ni kwa ajili ya aibu ya hayo yaliyotokea.
*************
Ikawa kuna kuongea, kufurahi kucheka, baadae mwenyekiti akapiga makofi
na kusema;
‘Basi sisi kama wazazi, kama mumeriziana hivyo, natumai tulimalize
hivyo,… au mume wa familia una la kuongea, je hujarizika bado?....maana bado
wewe ni mume wa familia hadi hapo sheria itakapochukua mkondo wake...au
nimekosea?’ akauliza mwenyekiti akiwaangalia mawakili,..
Mume wa familia akawa kimiya kwa muda, lakini baadaye akasema;
‘Sina la kuongea ndugu mwenyekiti…, nitaongea nini wakati maamuzi
yameshapita....nimerizika…zaidi sina kwakweli..’akasema hivyo na kukaa kimiya
huku akiwa kainamisha kichwa na ile miwani aliyovaa huwezi hata kufahamu
anafikiria nini
Leo mume wa familia hakuvaa kama kawaida yake, .. leo alikuwa kava
kinyumbani zaidi, kawaida yake kwenye vikao kama hivyo huwa anavalia suti safi..na
tai shingni, huwa anajipenda sana…na hupenda kujionyesha kuwa yeye ni bosi
fulani hivi, lakini leo,…akafika na t-shirt,…na suruwali ya jeans..alivalia kinyumbani
zaidi. Nahisi alitarajia kuwa leo anakosa kila kitu.
‘Lakini ni vyema tukasikia kauli yako kama mume wa familia, hata
kama mwenzako ameshaamua hivyo, je umerizika, muhimu ni hapo.. ...upo tayari
kuendesha hiyo kampuni mwenyewe. Swala la talaka, mlishaongea wewe nay eye au
sio.., na hapa ni kama taarifa tu, ....sasa hebu tuambie na wewe una kauli
gani...’akasema mwenyekiti.
Hapo mume wa familia akainua uso na kusema….
‘Labda niongee tu, kwa vile mnataka kusikia kauli yangu..’akasema
hivyo.
‘Mimi…, nasema hivi kama binadamu nina mapungufu yangu, hayo
yaliyotokea ni kweli niliyafanya, lakini kipindi nayafanya nilijua natimiza
wajibu wangu, hilo siwezi kuliacha kulisema maana ndio ukweli wenyewe, ulivyo
kuwa..ndivyo nafsi yangu ilikuwa ikinituma hivyo…
‘Ndio wakati mwingine, nilizidiwa na kuyafanya hayo yasiyofaa, ni
kweli ni hulka, siwezi kuikataa. Wakati unafanya unaona ni sahihi, ila matokea
yake ndio yanakupa fundisho.....lakini nimejifunza, na nilikuwa tayari
kujirudi,…nilishaahidi iwe hivyo, lakini mwenzangu hataki,....nitafanya nini
sasa…
‘Sikuweza kujibishana naye, maana utasema nini, wakati mwenzako
kashika mpini,..ni haki yake aamue hivyo, huenda tangu mwanzo alitaka iwe
hivyo, lakini hakukuwa na mwanya huo,…aah, ndio mawazo yangu, si mumetaka
niongee…’akasema hivyo aliposikia watu wakiguna.
‘Ndio hivyo… sasa mwanya umepatikana, na katimiza dhamira yake,
sawa.....mimi nasema hivi kwa vile kaamua hivyo,…na kiukweli moyo wangu ulikuwa
haujarizika, mnafahamu ni kwanini..lakini nianyeje, .. na iwe hivyo tu…, kama
ningekuwa na njia nyingine ya kumshawishi kuwa sitarudia tena ningelifanya
hivyo, lakini sina,...sina..japokuwa mke bado nampenda…hamjui tu..
‘Ni kweli, ...nilikuwa na hasira sana, nikiona nasota jela,
...mimi sijaua, mimi nilijitolea muhanga kwa ajili ya watu wengine,..nilikuwa
sina jinsi, marehemu alishaniweka kati..nisamehewe tu, na yeye asamehewe huko
alipo…ilikuwa niamua familia yangu au mimi…nilikuwa sina jinsi, nikaona ni bora
nijitolee mhanga …sasa ni nani angeliamini hivyo, eeh..kiukweli inauma sana.....na
...sawa sitaki kulalamika sana na kwa vile yeye keshahitimisha, basi sina
jinsi..
‘Kwa vile keshamaliza, na maamuzi hayo ni hitimisho…, mimi
nimekubaliana na maamuzi yake, nitajitahidi kufanya yale yote yanayostahili
niyafanye, na kwa vile tuna mafungamano ya watoto, mimi na yeye bado tutakuwa
karibu, hadi hapo atakapoona yeye, au hali ikisema hivyo...natumai hatanifukuza
nikifika kuwaona watoto wetu...wale bado ni kuinganishi chetu…nawapenda sana
watoto wangu…
‘Nimekubaliana na yeye juu ya watoto kuwa waendelee kuwa kwenye
mamlaka yake, kwa vile kaona kuwa yeye anaweza kuwalea katika malezi bora, yeye
kaona wakikaa na mimi labda wataharibika , labda wataniiga mimi na tabia zangu
mbaya…mmh,...
‘Hilo kiukweli nalikana,..sio kweli kuwa mimi ni mbaya kiasi
hicho, inapofikia kwenye malezi ya watoto…mimi kama mzazi nitajitahidi kwa
kadri ya uwezo wangu kuwalea watoto kwenye maadili mema….hata hivyo, mimi sikutaka
kupingana naye sana juu ya hilo, kwa vile kwa kufanya hivyo tunaweza kuwaathiri
watoto wetu kisaikolojia,...nawaombea sana wapate malezi bora wawe kama mama
yao…
‘Sawa,mimi nimekubali, kwa vile nawapenda sana watoto wetu,
na nia yangu ni wao waishi maisha mema, yasiyokuwa na tabia mbaya kama za
kwangu..nimekubaliana na mawazo yake kuwa huenda nitaoa,..na hajui huyo mke
nitakaye muoa,…atakuwaje…anaweza asiwapende watoto…mimi sijui hilo kwa kweli…na
mimi nisingelikubali…hatahivyo sawa…hamna shida.
‘Ni kweli hata mimi nimeliona hilo, ...mimi kama mzazi nawapenda
sana watoto, nisingelikubali mtu awatese, lakini kwanini tugombane kwa hilo,
basi nimewaacha watoto wakae naye, sina kinyongo kwa hilo…kabisa kabisa…kwani
nitakwenda wapi, bado nipo kwenye jiji hili, tutazidi kuwa pamoja tu.
‘Ama kwa kampuni…nashukuru sana kwa uamuzi wake huo..mzigo mnzito
umeshaondolewa, madeni…kiukweli yalikuwa mzigo mnzito sana…
‘Hata hivyo, bado hata mimi,..nitajitahidi kuyalipa, sitaweza
kuwamtumpia mzigo weote yeye peke yake…ndio maana nasema., mimi nitajitahidi
kuiendesha hiyo kampuni kwa juhudi kubwa sana
‘Ni sawa…mimi nitakaa na wenzangu, kama alivyopendekeza yeye, mke
wa familia, kuwa nishirikiane nao,…nitashirikiana na rafiki yake, kwani hata
kabla , yeye alishakuwa msaada mkubwa kwangu… inabidi nifanye hivyo kwa vile
pia ana damu yangu, napia eeh, …mmh, nitamshirikisha,na,.. ..na....’hapo
akasita huku akimgeukia mpenzi wake wa asili kwa aibu, na mimi nikasema;
‘Mpenzi wako wa asili....mke mtarajiwa’nikasema na watu wakacheka,
na yeye akainama chini kwa kutahayari, lakini akaendelea kuongea kwa kusema;
‘Na yeye pia ataingizwa kwenye kampuni, kwani anaweza…yeye na
rafiki wa mke wa familia walikuwa wakifanya shughuli zao kwa pamoja…kwahiyo kwa
pamoja, sote tutasaidiana..sijakaa nao, ila baada ya hapa tutakaa pamoja na
kuona ni nini cha kufanya, natumai, hata wao wamejifunza mengi, na kwahiyo
hatutafanya makosa ..kampuni hiyo itaimarika na kuendelea kama kawaida...hilo
ninawaahidi.
‘Kiukweli mimi nimejifunza mengi , ni kweli namshukuru mke wa
familia kanisaidia sana,...tena sana,...na kwa hivi sasa ninaweza kuiendesha
hiyo kampuni bila ya kusaidiana na yeye, lakini kwa vile na wenzangu wana
uzoefu wa kikazi, na wana haki hiyo, ...sitawatupa, nitakuwa na wao bega kwa
bega...’akasema huku akiinua kichwa na kumwangalia mwenyekiti.
‘Na pia nawashukuruni sana wazazi, wakwe zangu kwa kunipigania na
kunijali,..nafahamu kama ingelifuatwa sheria basi ningelikuwa sina changu tena...
‘Kiukweli sikutegemea kabisa kuwa mngelinifikiria na kunitetea
hadi hatua hii ya mwisho, nilishawaona nyie ni maadui zangu, haah..kweli
nimeamini kuwa nyie ni wazazi wenye hekima, sitawatupa, na sitawasahahu katika
maisha yangu yote, nyie moyoni kwangu ni wazazi wa kweli...’akasema
akimwangalia mama na baba yangu.
‘Hata hivyo sina budi kukiri kuwa nimekosa, nimesikia kila
mmoja akitaka mimi nikiri hivyo,… ni kweli moyoni nakubali hivyo, lakini mara
nyingi kutoa kauli inakuwa na ugumu fulani kwa vile wakati mwingine unahisi
hivyo kuwa hujakosa..ndio hivyo, niseme huo ukweli.
‘Sasa….’hapo akatoka na kusimama mbele ya watu, akapiga magoti..
‘Hii naitoa kutoka moyoni, kuwa mimi ni mikosaji,nimewakosea sana..hasa
mke wangu, hasa wazazi wangu, na jamii kwa ujumla..naowaombeni sana mnisamehe
kwa makosa hayo…sijui nifanye nini ili mjue kuwa mimi nimekosa na nahitaji
msamaha wenu..nikifika hapa..aah, sijui nilitaka mke wangu,..lakini keshaamua
tena nifanyeje…’hapo akashika kichwa
‘Oh…, sitaweza kuongea zaidi ya hapa…, ahsanteni sana...’akasema
mume wa familia huku akionyesha huzuni fulani kama anataka kulia.
‘ Inatosha…kweli hapo nimeamini kuwa umekosa, na sisi , …mimi kwa
niaba ya wote tumekusamahe……kama hakuna muongeaji, labda tufunge
kikao,..’akasema mwenyekiti, wakati huo mume wa familia bado kapiga magoti.
***********
‘Mwenyekiti samahani kidogo naomba nifanye tendo hili kabla
hatujafunga hiki kikao...’nikasema na kwa haraka nikatoka pale nilipokuwa
nimekaa na kumsogelea mume wa familia,…nikamuinua maana alikuwa bado kapiga
magoti.
Na yeye akawa kama kashikwa na butwaa, nikamuashiria aliyekuwa mke
wa docta aje, na yeye bila kinyongo akasogea pale nilipokuwa, kwanza
nilichofanya ni kumkumbatia mume wa familia, na nikawambia;
‘Ahsante kwa yote, mimi kwa moyo mkunjufu.. nimekusamehe, na
nakutakia maisha mengine mema, ..’na yeye kwanza alisita kunishika na mikono
yake, ikawa inatetemeka hivi..baadaye akainua mikono na kunishika tukakumbatia
kwa muda, halafu tukaachana.
Baada ya tendo hilo,…mimi nikamsogelea aliyekuwa mke wa docta, na
kumshika mkono, nikasema;
‘Nakuomba tafadhali uje hapa…’nikasema, alipofika huyo, aliyekuwa
mke wa docta, nikamsogelea mume wangu na kusema;
‘Mume wangu kama nilivyokuomba…naomba utimize ile ahadi yenu,
mliyowekeana kule kijijini, wewe na mpenzi wako wa asili… mpange siku gani
mtafunga ndoa halali, ....sina shaka na uchumba wenu.., maana ilivyo, moyoni
siku zote mlikuwa wachumba, au sio, sasa wadhihirishieni uma kuwa kweli
mnapendana, kwa kukumbatiana...’nikasema
Kwanza iliwashika kama
butwaa…wakawa wamesimama huku wakiangaliana kwa hali ya kutahayari kidogo, na baadaye, wakasogeleana na kukumbatiana,
huku machozi yakiwatoka, kilichofuata hapo ni...vigelegele na shangwe
vikatanda.
Baadaye na mimi nikamkumbatia aliyekuwa mke wa docta, na
tukachekeana, nikampongeza, halafu ndio nikamgeukia mume wa familia,...nikamshika
mkono na kumkaribisha kifuani kwangu, tukakumbatiana, kumbatio la mwisho, kwa amani na kuagana, huku machozi
yakinitoka, ilikuwa kumbatio la kwaheri.
Ni heri iwe hivyo..
Kulikuwa hakuna njia nyingine, ilibidi hayo yafanyike kwa masilahi
ya wote, na namshukuru mungu, kuwa tulifikia muafaka, kwani baada ya kikao
hicho, na kumbatio hilo la mwisho kama mume na mke wa familia, mawakili
walifanya kazi yao vyema, ndoa ikavunjwa, talaka ikatayarishwa, na ikawa mwisho
wa ndoa yangu na mume wa familia, yeye akaanza maisha yake na mimi maisha
yangu.
MWISHO
NB: Mume wa familia kama ilivyotarajiwa baada ya miezi mitatu
walifunga ndoa na mpenzi wake wa asili, ndoa tuliyoisimamia mimi na docta na
wazazi wangu, na ilifana kwa kweli, ...mimi nikawa best woman wa
mke wake, na docta akawa best man wake...
Sio siri, yaliyopangwa na mungu hayapingiki, baada ya
mvutano, na ushawishi mwingi wa docta, nilikubali turejeane urafiki wetu, na
sisi mapenzi yetu ya asili yakarejea, nikakubali ombi lake kuwa tufunge ndoa,
ahadi ikatimia, lakini ni baada ya miaka kama miwili hivi ya mvutano…
Nikaona haina shida…kwanini tujivunge…tukafunga ndoa, na sisi
tukawa mke na mume.
Na aliyekuwa rafiki yangu, yeye aliendelea kumlea mtoto
wake, na alisema hataki kuolewa tena, sijui kwanini, ...
Pengine hajapata anayemtaka, yote maisha,..yeye anadai
alichokitaka keshakipata, yaani mtoto, na mdogo wake aliyekuwa mume wa familia
yangu, alihamia Kenya na kuanzisha maisha yake huko, na yule mfanyakazi wa
ndani sasa hivi ni mmoja wa mabosi ndani ya kampuni yangu..huwezi amini
ukiutana naye …anamiliki gari lake na nyumba yake mwenyewe..
‘Hicho ndicho kisa changu mpendwa...’ akamaliza mdada
WAZO LA LEO: Mkioana
na bahati mbaya ikafikia hatua ya kutalikiana na juhudi zote za kusuluhishwa
zikashiniakana, basi achaneni kwa amani, kuliko kuishi huku
mkiumia,fanyeni hivyo kwa amani na upendo, kwa masilahi ya watoto wenu, na
mahusiano mema, ili mje kutembeleana kama marafiki wa zamani kwa upendo na
furaha.
Natoa wazo hili sio kwamba napenda mawaza ya talaka, ila wakati
mwingine inabidi iwe hivyo, kwani kuna mengine hayavumiliki, na hatuwezi
kujidanganya kuwa tutaishi hivyo hivyo tu, ya mungu mengi, huwezi kujua ni nini
kakupangia badili yake,hatuwezi kulazimisha kitu ambacho hakitakuwa na amani
kwetu, tukaishi kwa maumivu na masononeko.
Japokuwa kiukweli,kuachana
si kuzuri, hasa mnapokuwa na watoto, mkifikia kuachana basi peaneni mikono na
muombeni mungu wenu, kila mtu aje kufanikiwa katika maisha mengine…mola anajua
zaidi.
NAWASHUKURU WOTE WALIKUWA NAMI TOKA MWANZO WA KISA HIKI, MUNGU
AWABARIKI SANA, NA MAONI YENU MAOMBI YENU, MUNGU AYAKUBALI, HUENDA SIKU MOJA NA
MIMI NITAWEZA.....kutengeneza kitabu, au hivi visa kuweza kuigizwa kwenye
runinga, halikadhalika kupata wadhamini, maana haya yote nayafanya kwa gharama
na muda,..lakini msijali ipo siko...
TUPO PAMOJA,....
Mwisho wa kisa hiki ndio mwanzo wa kisa kingine.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment