‘Sasa ni ajenda ya mwisho, ajenda ya kusikia kauli na maamuzi ya
wanandoa ambao ndio waliotuweka hapa…
Kwa namna nyingine tunaweza kuiita ajenda hii kuwa ni ajenda ya
hukumu au hitimisho ya kile tuliyochokuwa tumeitiwa,.....na hapa mimi
sitaingilia sana, maana wanandoa waliosababisha hiki kikao wapo hapa, na
walishapata muda wa kukaa pamoja na kulijadili tatizo lao hili kwa mapana yake.....’akasema
mwenyekiti.
‘Japokuwa kwa nilivyolisikia…’hapo akageuka kumuangalia mume wa
familia, ambaye alikuwa kainamisha kichwa chini, halafu akageuka kuniangalia
mimi.
‘Sitaki niongee mimi,..japokuwa naona …kama bado kuna sintofahamu
kwa wanandoa hawa wawili..wengine kama docta na mwenzake wameshamalizana..
Sasa kwa vile tupo kwenye kikao cha wengi, na penye wengi
hapaharibiki neno, natumai tutalimaliza hili swala kwa amani na upendo,
ikishindikana mimi mwenyekiti nipo, itanibidi nitumie rungu langu la
uenyekiti...’ hapo akatabasamu akimuangalia mke wake.
‘Sio shida…kulimaliza hili tatizo,sio shida kabisa.lakini kwanini
tulazimishane, ..hapana, hili ni swala la wawili , waliopendana wenyewe, na
kama ni kulimaliza tatizo lao walimalize kwa amani…au sio...
Tuendelee na sehemu ya kwanza ya hitimisho la kisa hiki...........
**********
‘Kama mnakumbuka kikao
kilichopita ilibidi tuendeshe jambo hili la kifamilia kama kesi ili tuone haki
inatendeka, kwa vile mlalamikiwa hakukubali wala kukiri kosa lake, kwahiyo
tukaona ni vyema tukaliangalia hili jambo kwa undani zaidi…
Ilibidi tuliendesha kama kesi…kwa kutoa ushahidi, na maelezo yenye
ushahid ndani yake,.. hadi pale ukweli mnzima ulipobainika,..ukweli huo ulikuja
kufichua mambo mengine kabisa..lakini chanzo, ..ni familia husika,…sasa sijui
ni kwa bahati mbaya, au ilikusudiwa, yote hayo tuliyaona wenyewe.
Hayo mambo yaliyotokea, ambayo kwa ushahid, yalipangwa,
nisinelipenda kuyarajea hayo mambo, kila mtu kayasikia na kujionea..sasa leo kiko
chetu kinaendelea,.
‘Sasa basi mimi kama mwenyekiti, inabidi nilisimamie hili kwa
hekima zote ili mwisho wa siku tukimalize hiki kikao kwa kushikana mikono ..’
hapo akamuangalia mume wa familia ambaye bado alikuwa kainamisha kichwa chini.
‘Mimi bado natoa angalizo, kuwa hii ni familia yenye maadili yake,
kama kuna mtu anaona kuwa hataweza kuishi nasi, kwa kufuata sheria zetu za
kifamilia, basi awe huru kuondoka, hata kama ni mtoto wangu wa kumzaa,...ni
vyema tukafynza kutii amri na sheria kuanzia kwenye familia, na hili liwe wazi
kwa kila mtu,...
Hata hivyo, taratibu za familia ndogo, yaani za mke na mume
zitaendelea kutumika,..hatuwezi kuziingilia, labda wao wenyewe wasema kuwa
basi, hizo sheria kwa vile zimeleta mgongano, hatutazifuata tena, na kwa
minajil hiyo kwa vile waliusajili huo mkataba, itabidi wafuate taratibu zao.
Haya yote tunawaachia wao,..leo ukumbi ni wao, wawili, sisi kama
familia kuu hatustahili kuwaingilia,..hitimisho hili ni lao, kama kuna
kusameheana, ni heri sana kwetu, kama kuna kuwajibishana, hewala....
Naombeni muda wenu kidogo, nataka kuteta na mawakili…kabla
hatujaendelea…na mawakili wakasogea pale alipokuwa mwenyekiti wakawa wanaongea,
ilitakiwa iwe maongezi kidogo, lakini ikachukua muda..naona wakili wa mume wa
familia alikuwa akipinga jambo..
Lakini baadae wakakubaliana, na mwenyekiti akasema;
‘Unajua kama nilivyosema hapa kila kitu kimekamilika, pamoja na
hayo yaliyoamuliwa huko mahakamani,lakini sis bado tuna maamuzi yetu, au sio,
ndio maana pamoja na hukumu, bado sisi tuliambiwa turejee tukae kama familia
kulimaliza hili tatizo letu…
‘Sasa basi wazee walisema, yaliyopita ni ndwele tugange yajayo, au
sio jamani…’akasema mwenyekiti na wajumba wakasema
‘Sawa…’suti hafifu lakini.
‘Hayo yaliyotokea yawe ni fundisho kwetu, na tuape kuwa
hatutarudia tena,tusameheane na kukiri kuwa tulikosea, na hatutareeja ujinga
huo tena, kwani tumeshafinywa, mtu mzima ukifinywa, huona aibu,… eti jamani…leo
iwe siku ya kusameheana na iwe hitimisho na ukurasa mpya uanze..’akasema
mwenyekiti huku akimwangalia mume wa familia.
‘Hebu mwangalia mume wa familia alivyochongeka, ....ni taabu tupu,
kwanini tufanye haya, tukijua kuwa ni makosa, tunamkomoa nani, ...baba, sasa ni
wakati wako wa kurudisha mwili wako, ukae utulie ujipange vyema, muishi vyema wewe
na mkeo wako na familia yenu kwa ujumla,...au sio, lakini sasa…’akasema na
kutulia
‘Uamuzi wote upo mikononi mwa mke wako….’hapo akamgeukia mke wa
familia.
Na mume wa familia akainua kichwa kidogo, hakusema neno
‘Kama ulivyoona hata mahakamani walikunyoshea kidole wewe, na
kukupa onyo, na ulitakiwa ufungwe, lakini wakili wetu akafanya juhudi za ziada,
akirejea maadili na tabia za familia kuu, matendo yetu mema ya kifamilia
yakachukuliwa kukulinda wewe, ina maana kuachiwa kwako kunatokana na kumbukumbu
za matendo yetu mema, maadili yetu mema yamukusaidia, sasa mimi kama mwenyekiti
nikiwa hai sitakubali uadilifu wetu uporomoke tena, ...nawaomba kama
wanafamilia tuitunze hiyo kumbukumbu,...’akasema mwenyekiti.
‘Nimeona niongee haya kabla ya mke wa familia, sijui yeye ana
maamuzi gani, hatujui,…ila nina imani kuwa baada ya kipindi hicho kifupi
alichoweza kukaa, na kipindi hicho kifupi ambacho mume wake alishikiliwa…yeye
atakuwa ameweza kukaa na kutathimini, kama ulivyoomba yeye, na …’akatulia
kidogo.
‘Natumai hutatuangisha kwa hilo..
‘Baada ya mume wako kutoka huko aliposhikiliwa, uliomba wewe na
yeye make pamoja, myajadili maswala yenu..natumai mlifanya hivyo au sio, ...na
kwahiyo wewe kama mdhulumiwa, unayo haki yako ya upendeleo…, na hatutapenda wanafamilia
wengine waingilie kati hayo maamuzi yenu
Na maamuzi yenu yasije kuwadhulumu watu wengine, ...kama kuna mtu
atadhulumiwa kwa maamuzi yao..basi kila mmoja anayo haki ya kusema,na kikao
hiki ndicho halali cha kuyasikiliza hayo malalamiko ya mtu anayeona kadhulumiwa…msiogope
kusema jamani, sisi hapa tupo tutaangalia haki iko wapi.
‘Mke wa familia, tunakuomba uondoe jaziba, najua umeumia sana,
lakini yote ni maisha, kwenye wema, na wabaya wapo, na halikadhalika kwenye
wabaya na wema hawakosekani, na mitihani hii inakuwa ngazi ya kutuvusha daraja
fulani,…kwa wenye hekima watalielewa hilo, au sio…
Uliona pale mahakamani
walisema nini…hawakutaka kuamua moja kwa moja japokuwa haki ilikuwa
yako..mkataba wenu ulishahukumu..lakini bado wakasema tuwe na muda wa
kutafakari, tuwe na muda wa kukaa kikao cha kifamilia,…sasa wewe, unayo haki,
ya kuamua upendavyo..kwa vile wewe ndiye uliyedhulumiwa, na mkaaba wenu
unakulinda kwa hilo..
‘Tunatarajia wewe utatoa maamuzi yako yenye hekima na busara,…haki
ni yako, una haki ya kutumia mkataba wenu, au kutumia kauli yako mwenyewe, sisi
kama wazazi tumeliongelea hilo, tukaona kwanini misisameheane mkayasahau
yaliyopita na kuganga yajayo...’akasema mwenyekiti.
‘Nakumbuka kikao kilichopita tulimpa nafasi mlalamikiwa ajitetee,
na kuelezea hisia zake, leo hatuna nafasi naye tena, leo ni siku ya mke wa
familia kuongea yake na pia kutoa maamuzi yake, kwani imeonekana kweli kuwa mume
wa familia ana makosa na mke wa familia ulitendewa isivyo haki, kwahiyo kwa
upendeleo wewe mke wa familia una pewa nafasi mbili, ya kwanza ni
kumsamehe mume wako....
‘Upo tayari kumsamehe mume wako…?’ akasema mwenyekiti kama
ananiuliza, na mimi sikujibu kitu nikawa kimia tu, maana hakuna aliyejua nina
nini moyoni mwangu,…
‘Usinijibu kwa sasa utajibu muda wako ukifika…’akasema mwenyekiti
‘Ila napenda niseme hivi….kusameheana ni wajibu wa kila mwanadamu,
ni daraka kubwa ya ucha mungu…ukikosa na kukosewa hatuna budi kusameheana, ni
vyema tujifunze hilo...’akatulia
‘Lakini yote ni maamuzi yako wewe mke wa familia,…kama
utakubaliana nalo, basi sisi kama wanafamilia, tutawashikanisha mikono, na
tutamaliza haya mambo kwa amani na salama hilo ndilo kama wazee wenu
tunalihitajia na kulitarajia kutoka kwako wewe mke wa familia, ila sio kwamba
tunakulazimisha ufanye hivyo maana una nafasi nyingine ya pili...’akasema
mwenyekiti.
‘Nafasi yako ya pili, ambayo mimi kama mwenyekiti, sitaipendekeza
sana, japokuwa nyie mlikubaliana kwenye makataba wenu iwe hivyo, ...kuwa
atakayekiuka mambo fulani,…mambo mabaya yenye kuleta kashfa… ambayo wenzenu
waliamua kuyatumia kisiasa, na hata kidini hayakubaliki,..na kwene famila
kuu tumeyaanisha kama matendo yenye
kuleta kashifa
‘Mhh…basi moja kwa moja ndoa inakuwa haipo…swali likaja je ni nani
mwenye kuvunja ndoa…ni yoyote mke au mume…haya ni maswali manzito sana, na mume
wa familia kasimamia hapo kuwa yeye ndiye ana haki yakuvunja ndoa…
Sasa mkataba wenu ulikuwa na maana gani,…mlikubaliana mbele ya
wakili waliotambulikana, au sio na mola wenu ni shahidi…au sio…kwahiyo
yakitendeka ya kuvunja ndoa, ndooa hapo inakuwaje…
‘Lakini hapo hapo tunaweza kurejea nafsi ya kwanza ya kusameheana,…kama
mkoswaji, aliyekosewa, akaamua kusamehe..basi,…mambo yataendelea, na ndivyo
tunavyotegemea hapa kwenye kikao hiki.
‘Tukumbuke jambo moja, sisi wanadamu wote ni wakosaji…hakuna
mkamilifu, utamlaumu mwenzako kwa kosa hili kumbe na wewe una makosa mengne
makubwa zaidi ya hayo unayomlaumu mwenzako au sio..kuna makosa mengi, sisi kama
wanadamu tunayafanya kwa siri, sijui,…mimi sijui…mke wangu ananiamini sana kuwa
sifanyi hivyo..hahaha....’akatulia mwenyekiti na kumwangalia mke wa familia.
‘Unapoteza muda bwana…’mke wa mwenyekiti akasema;
‘Sawa sawa, msaidizi wangu lakini ni wajibu wangu kuyaongea haya
kama mzazi….maana hitimishi hili lisije kuwa ni mgogogo mwingine baadae…
Haya basi,..mimi naona nisipoteze muda, mke wa familia uwanja ni
wako, ...’mwenyekiti akamwangalia mke wa familia.
************
Hapo mimi kama mke wa familia, kwanza nikasimama,…nikainamisha
kichwa kidogo kutoa heshima kwa mwenyekiti..halafu nikageuka kumuangalia mume
wangu..huku nikitafakari maneno ya mwenyekiti kuwa nina nafasi mbili, ya kwanza
ni kusamehe, lakini ya pili ni kutumia mkataba wetu.
Kusamehe..yaha, yawezekana, moyoni sina
kinyongi tena…lakini mkataba ulikuwa na maana gani…nifanyeje sasa…nikamuomba
mola wangu anipe kauli yenye hekima na kulimaliza tatizo hili kabisa…
‘Naomba niongee nikiwa nimekaaa, ...mwenyekiti naomba kibali
chako....’nikasema na mwenyekiti akatabasamu na kusema;
‘Nyie vijana bwana, mbona mnachoka mapema, haya wewe kaa tu, hata
ukitaka lala, maana sote sasa hivi masikio na macho yetu ni kwako wewe….. sema
yale yaliyo moyoni mwako, uwanja ni wako....’akasema mwenyekiti.
‘Nilitaka nisimame, lakini kama wenzangu walivyofanya kwa leo,
nitaongea nikiwa hapa hapa, mtanisamehe kidogo, nipo kwenye wakati mgumu sana,
namuomba mola wangu aniongoze tu..…’nikasema
‘Kwanza nimshukuru mwenyekiti kwa kunipa nafasi hii, ambayo,
imekuwa kama vile mtu yupo kwenye chumba cha mtihani baada ya maandalizi ya
muda mrefu. Ni kweli nimekuwa nikijianda kwa siku kadhaa nyuma hasa baada ya
kikao kilichopita, ..ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu. Kama mke na kama mama
wa watoto wawili….
‘Ni wakati mgumu maana kuna mambo mengi yalikuwa yakiendelea
kichwani mwangu,..nikiwa sijui ya kesho yangu itakuwaje,
Je niamua nini, je hayo maamuzi yatakuwaje..
‘Haaah, …na leo ndio natakiwa kusema kile nilichokuwa nimejiandaa
nacho, kiukweli hadi tunafika hapa bado mimi sijaweza kuwa na maamuzi ambayo
ninaweza kusema ni sahihi kwangu…ndio ukweli wenyewe, utasemaje sasa, wakati …huna
msaidizi..
Nilimuomba mungu wangu sana, na …akilini nikawa nawaza, ni kwanini
najisumbua akili yangu wakati maamuzi tayari yalishajionyesha,…nilipoliwaza
hilo, nikapumua, ni kweli mola ni wetu sote na kila kwenye shida, kila kwenye
shinikizo la mawazo, mtegemee yeye, atakuongoza tu…
‘Nasema hilo kiukweli…maana maamuzi sio lazima mtu ayaongee,
vitendo vitasadikisha hilo…ila kama alivyosema mwenyekiti, tunaomba sote mungu
atupe hekima ili jambo hili liishe kwa amani na upendo, na mimi namuomba iwe
hivyo....’nikageuka kumwangalia mume wa familia.
‘Pamoja na yote hayo, mume wa familia alipotoka rumande, huko
alipokuwa ameshikiwa na polisi yeye na wenzake, maana imempita muda kidogo…,
nilijaribu kukaa naye ili nione jinsi gani tutasaidiana kulitatua hili,...
‘Hili jambo, ni jambo gumu sana kuliamua peke yako, unaweza
ukalitatua kwa jaziba, kwa hasira, mwisho wake ukaja kutulia ukaja kujijutia,
na ni rahisi kuliongea kwa maneno ya haraka, lakini madhara yake ni makubwa,
maana hili tatizo halinigusi mimi tu, linagusa kizazi changu ....ndio maana
nimekuwa nikiliwazia sana.
‘Tulipoweka makubaliano, yetu, kila mmoja aliyapokea makubaliano
yale ambayo yakaja kuwa mkataba wetu wa familia, …tuliyaweka kwa furaha tu..,
na mimi sikutarajia kuwa mwenzangu angelikuja kuyafanya hayo
aliyoyafanya,sikuamini..ndio maana wengine waliniona mimi kama mjinga….yanaonekana
wazi machafu, lakini mimi nikawa nimeyafumbia macho…sikuamini…hamjui tu siku
tunawekeana hayo makubaliano yetu ilikuwaje,
‘Kiukweli kwangu ilichukua muda sana kulikubali kichwani, inafikia
hatua unaona kama unaishi na watu wawili tofauti, na kwa ujumla nimekwazika sana
sana..sio siri, sijui nitakuja kumuamini nani katika dunia hii..
‘Wazazi wangu lazima niwaamini, nazungumzia, mume….’nikatulia
‘Kiukweli sikujua kuwa unaweza ukaishi na mtu, mkachangiana naye
kila kitu, ukampa moyo wako wote, kumbe mwenzako hayupo nawe kabisa, kumbe
mwenzako anaye anayempenda kwa dhati…, wewe upo kwa ajili ya kutumika tu...ni
dhuluma ya hali ya juu…’nikatulia huku nikionyesha uso wa huzuni.
‘Nimejaribu kuongea na mwenzangu ili nione vipi tutasaidiana kwa hili,
kama binadamu, sikutaka kuwe na unyonge, kuwa kwa vile mimi nina hali hii au
ile, ...kwahiyo nilimtaka ajitoe, aseme anataka nini, atoe ukweli wake ulio
moyoni mwake...lakini haikuwa kazi rahisi...’nikainama kama nasoma kwenye
karatasi.
‘Haikuwa kazi rahisi ndio maana nasema kwanini niumize kichwa
wakati …ukweli upo wazi…’ nikatulia.
‘Kwa ujumla kama mlivyoona, nia na malengo ya mwenzangu na
mwenzake, ilikuwa ni kupata maisha mazuri..hiy ndio ilikuwa ndoto yao…wenyewe
wamelibainisha hilo, kwa kauli yam dada, japokuwa mume wa familia, kwa nafasi
yake hakutaka kuliweka hilo bayana…kiukweli hawakuoa au kuolewa kwa mapenzi ya
dhati ...’nikatulia
‘Kwahiyo wakatumia hadaa, wakajipatia mume na mke, ambao wana kile
walichokitaka…, lakini nafsini mwao bado kulikuwa na mapenzi ya mwenza wao,
kama walivyoita wao, mpenzi wa asili. …unakuwa kama umelala na gogo au sio..
‘Nimeshasikia wengi wakisema waume au wake, wanaweza wakawa hivyo
katika mapito ya maisha,..moyoni wanaoa tu , lakini wanakuwa na wapenzi wao wa
asili, lakini siku zinavyokwenda, wanakuja kuyasahau hayo ya zamani, ya mapenzi
yao ya asili…na wangi wamefanikiwa hivyo na maisha yamesonga mbele…, hilo
lawezekana au sio…nikajiuliza kwanini sisi hilo lisifanikiwe...unaona eeh..’nikatulia
Sasa nilitarajia kwa mwenzangu kuwa huenda itakuwa hivyo,…ndio
maana baada ya yeye kutoka huko rumande, nilipoongea naye akasema anahitaji nafasi ya
pili,
‘Unahitajia nafasi ya pili kwa vipi…?’ nikamuuliza
‘Nahitajia kujirekebisha, …nimekosa basi, sasa unipe muda
mwingine..’akasema
‘Kwani uliyofanya ulikosea,..au..?’ nikamuuliza
‘ndivyo ilivyoonekana, au sio..basi kwa vile ndio hivyo, nimeshajifunza,
na mimi nipo tayari kuishi kama mume mwema. ..’ akaniambia hivyo.
‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza, kiukweli bado nilikuwa sina
uhakika na hilo, japokuwa wazazi wangu wamenithibitishia hivyo, kuwa kwa
mwanaume ikishatokea hivyo, basi hujifunza na hataweza kurudia makosa tena,
..mmh, ukishaumwa na nyoka kila ukiguswa na unyasi utashituka, huo ndio ukweli
halisi kutoka moyoni...’nikageuka kumwangalia mume wa familia.
‘Mimi tukizidi kuongea nikamtolea mfano wa mpenzi wake wa asili
ambaye kakiri makosa na kawa tayari kuchukua maamuazi magumu,...namsifu sana
huyo mdada, ni mdada wa pekee sana…yeye amekomaa kiutu uzima, hongera zake na
namuombea mola afanikiwa katika maisha yake..
Mimi nikamuuliza mwenzangu,
‘Unaona mwenzako alivyofanya, kaithibitishia dunia kuwa yeye
yupoje, na ya kuwa yeye yupo tayari kusamehe kila kitu, kwa ajili yako, je wewe
una msimamo gani,…?’ nikamuuliza
‘Msimamo gani…si nimeshakuambia, haya yote yamefanyika kwa chuki
tu, mimi bado nasema hivi ndoa yangu haitavunjika kwa lolote lile…’akasema
‘Sasa ndoa huvunjwa kwa kosa gani..?’ nikamuuliza
‘Kosa hata liweje, mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa ni mwanaume…’akasema
Unajua huyu mtu hadi hapo
hakuwa amenielewa…nini lengo langu la maswali hayo yote,nilimuuliza maswali
hayo kimtego kuona moyoni mwake yupoje..
Sawa anakiri kuwa kakosea, lakini kwanini aliyafanya hayo makosa,
kajibu vipi…
‘Mim niliyafanya hayo kama mume wa familia, nikiwa na lengo jema
la familia yangu…niliwajibika kama mume wa familia, kiukweli majibu haya yalinivunja
nguvu...’
Mke wa familia akatulia halafu akawaangalia wajumbe na kuendelea
kusema;
‘Hebu angalieni hilo jibu katikati ya mstari kwa hekima..kweli mtu
baada ya kukosea,angelitoa kauli hiyo, kuwa aliyafanya hayo japokuwa ni makosa,
lakini aliyafanya hayo kama mume wa familia, ..
Haaah.....nikaona bado kumbe mwenzangu anaona kuwa alichofanya ni
sahihi,na kwahiyo hali hiyo huenda inaweza ikatokea tena....’kama mume wa
familia..si ndio hivyo maana yake…au nimuulize tena hapa mbele yenu asema ni
kwanini aliyafanya hayo makosa..’nikasema
‘Hapana..huo sio muda wake tena, huu ni muda wako wa kutoa
maamuzi..’akasema mwenyekiti.
Najua na siwezi kumuuliza hayo maswali mbele yenu tena,maana
majibu yake yameshapigiwa mstari…..mwenye akili anaweza kuyatathimini, hata kwa
akili ndogo tu…
Kiukweli mkiishi sana, ndani ya ndoa, mnajenga udugu, ni zaidi ya
udugu, mnakuwa kitu kimoja, na swala la kuachana ni gumu sana, hata kama
itakuwa ni kwa jaziba…sio rahisi kuchukua hatua hiyo…
Na mimi nimeliwazia sana hilo…unajua unapokosewa nijuavyo mimi,
yule mkosaji ndiye anatakiwa kufanya juhudi za kulimalizia hilo tatizo,…ni
hekima au sio…sasa nyie kama wajumbe mngelipenda kuniuliza swali kama hilo
moyoni, je mume wangu tokea muda huo aliwahi kuifanya hiyo juhudi…
‘Huyu hapa muulizeni.’nikasema na hapo mume wa familia akataka
kuongea lakini mimi sikumpatia nafasi, nikaendelea kuongea…
Tutaendelea na sehemu hii ...kidogo tu, ili siku isiidhe bure, tutakuja kwenye hitimisho la isa chetu mola akipenda.
WAZO LA LEO: Maamuzi ya hekimakwenye matatizo,
huhitajia muda, huhitajia msaada wa yule aliyetuumba, sio kwa akili tu ya kibinadamu.
Wengi wetu hukimbilia kutoa maamuzi yao, kwa jaziba,…au kuwa ‘usomi’ walio nao…lakini
baadae wanakuja kukiri kuwa walifanya makosa.
Subira ni muhimu sana
kwenye matatizo,…
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment