Niliyoyakuta Dar, yalinikatisha tamaa, kwani sikutegemea kuwa kuna
watu wamefikia kiwango hicho cha uhalifu wa kimataifa, maana hayo yaliyofanyika
sio uhalifu wa kitoto, na hao watu
waliofanya hivyo, wamefanya kwa kujiamini,hawakujali kabisa kuwa kuna usalama,
kuna polisi,… sikuamini..
Kama nilivyoambiwa nisigusie huko, lakini nataka muone jinsi gani
tukio nzima lilivyotokea, hadi mimi nakaamua kukubali kuingia kwenye
makubaliano ambayo baadae nimekuja kulaumiwa na kuonekana kuwa mimi ni miongoni
mwao, huenda sitaweza kuthibitisha kwa mia kwa mia, lakini hivyo ndivyo
ilivyokuwa, mkiniamini sawa msiponiamini, mimi nimetimiza wajibu wangu…’akasema
na kutulia.
Mwenyekiti alikuwa katulia hakusema neno, nahisi mzungumzaji
alitarajia mwenyekiti atasema neno…
Niwaambie ukweli baada ya
uchunguzi wangu niligundua jambo, huenda halijagundulikana hilo, huenda
limeshagundulikana lakini nia na amdhumuni kwa sasa ni kuwajibishana, lakini
kuna mambo ambayo hamjayaweka kwenye mtizamo wa kihekima…samaahni kwa kusema
hivyo.
Hamjui kuwa, malengo na mbinu za hili, kwanza ilikuwa ni kuondoa
nguvu za ulinzi, akili na mawazo ya kikazo yaondolewe kisaikolojia, kuharibu ulinzi
na usalama wa familia, hilo hakuna aliyelifahamu, sijui naeleweka hapa, na…na pili kuondoa, mshikamano…familia iyumbe, ikose
udhibiti, ni nani kiongozi na ni nani wa kutiiwa, hilo lina umuhimu wake.
Lakini la tatu ambalo ndilo huja kuharibu kabisa, ni kujenga
chuki…ukiliangalia hili utaona mfano wake, ni nini kilifanyika kwenye familia
iliyolengwa,…na je hili halikufanikiwa, chuki ziliandaliwa kitalamu, kukajengwa
matabaka mawili ya mume upande wake na mke upande wake..je hili
halikufanyika…?’ akawa kama anauliza
Ilihakikishwa kwua hilo lawezekana, chuki ikasambazwa, kwa
marafiki, makundi, ..kundi mume n akundi mke, ushabiki ukajengwa, watu
hawalioni hili ubaya, wake, ushabiki wenye mlengo wa chuki ni mbaya
sana,…haujengi, familia ikawa sasa kila mtu na lake,…sijui naongea na watu
wanaolewa, au ndio bado makundi hayo yapo hapa.
Mzee mimi nayaongea haya kwa nia njema, sina nia ya kuwagawa hawa
watu sina nia ya kuingilia hii familia na sina nia mbaya ya kuchukua chochote
kwenye hii familia, mimi ni mtu wa kuja tu, wenye familia wapo, wenye mali
wapo, kwanini mimi nije kujiingiza humo,…sina fani yangu, na sio lengo langu,
lengo langu ni kujitegemea, kufanya kazi yangu kwa malengo mema.
Tuyaache hayo, nahisi mtaniona najitetea kwa vile nimeharibu, ni
kweli najuta sana kwa hiki lichotokea imeniuma sana,…lakini yameshatokea
nitafanya nini…’akaweka mikono kama anamuomba mungu wake.
‘Namuomba mungu sana anisaidie kwa hili….’akatulia kwa muda
‘Ndugu mwenyekiti, …haya yalipangwa kitaalamu sana, na kila tukio
lilikuja kutokea baadae lilichukuliwa kwa uzito wake, maana kashfa inaweza kuwa
ni ndogo tu, lakini jinsi itakavyokuzwa na vyombo vya habari, midomo ya watu,
inaweza ikawa kubwa kuliko kashfa yenyewe, ni kweli si kweli..hili lilipangwa
na maadui wa mzee, na kinara wa kulifanikisha hilo mnafahamu wenyewe…’akageuka
kushoto na kulia.
Sasa oneni hili, siku
nilipofika uwanja wa ndege kulitokea nini..na onenani ujanja wa mwenzetu,
ulivyo, yupo mbali kabisa na hili, na huwezi kabisa kumdhania, yeye anachofanya
ni kutia mafuta kwenye ule moto ulioanza kuwaka..kidogo kidogo…
Nasimulia hili nitajitahidi kutokuingilia kazi ya polisi…
*******a
Nilielezea kidogo yaliyotokea awali kwa ufupi, lakini
sivyo ilivyokuwa kwa undani wake, mimi nilitekwa nyara mapema tu, na nilikuwa
ndani ya mikono ya hao watu kwa siku mbili, hakuna anayelifahamu hilo…’akatulia
Nilipotoka uwanja wa ndege kaam nilivyosema awali mtoto wangu
nilimkabidhi mtu, nikijua huku huenda kukawa na jambo, na sikutaka kabisa mtoto
wangu aguswe, nilikuwa tayari kupigana hadi kufa, kama mtu atamgusa mtoto
wangu.
Nilijiamini kuwa mtoto wangu atakwua salama, nikatangulia kutoka,
na mtu niliyemuachia mtoto wangu alibakia nyuma, japokuwa hata nilipotoka macho
yangu kwa siri yalikuwa yakihakikisha kuwa mtoto wangu kaondoka uwanjani pale
salama, nikabakia mim, na yaliyonikuta
Baada ya ukaguzi wa mizigo yangu, sikuwa na mizigo mkubwa, ni
kiasi cha nguo za mtoto na zawadi kidogo,
sasa wakati natoka, nje, ..uon ilivypopangwa kumbe …hahaha maana huyu
mtu aliyekuwa nyuma yangu sikuwa na ..yaani hapo ndio nasema hawa watu sio wa
kawaida, huyu mtu sikuwahi kumuona kwenye ndege,..
Ukitoka pale uwanja wa ndege,unatembea kutoka, huku wapo watu
wanasubiria jamaa zao, wamejipanga, mstari, nyie mnapita ile sehemu ya
kutembea, huyu mtu alitokea wapi hadi kuwa nyuma yangu na mimi kwenye ndege
sikuweza kuiona sura hiyo.
Sasa namaliza ile sehemu ya
kutembea nataka kufika ile sehemu ya watu walijipanga mtu nyuma yangu ndio
akanigusa na kitu kikali, ina maana huyu mtu alikwua nyuma yangu wakati wote,
haiwezekani akatokea miongoni mwa watu na kuja kuniwahi kwa nyuma
..hapana…sijui naeleweka hapa…’akasema
Ilikuwa ni kisu kikali maana nilihis maumivi yake, sauti ikasema;
‘Fuata tutakavyokuelekeza, kuna taksi ile pale mbele yako, mlango
wake upo wazi, ingia, na mizigo yako tutakuchukulia, hatutaki
kukuumiza...’akaniambia, na baadaye akanipa bahasha, akaniambia
‘Fungua hiyo bahasha...’kwa mikono ya kutetemeka, nikaifungua,..nilitetemesha
ile mikono kwa makusudi, kumteka huyo mtu akili , ili ahisi kuwa mimi
nimeogopa, ni ujanja mdogo tu…nikafungua ile bahasha, na kwa mbali nikaona yule
mtu aliyekuwa an mtoto wangu akitoka, akawa anaendea gari, sikuona dalili ya
watu kuwa nyuma yake
Na kuwa muda huo ndio nimefungua ile bahasha na kuona zile picha mbaya, le nilizozoea kutumiwa, na huyo mtu akaniambia
‘Siku hizi hapa bongo kuna magazeti mengi yanazitafuta picha kama
hizo, hatutaki kukuharibia jina lako, na kukuharibia maisha yako ya baadaye, na
kumpoteza mtoto wako, yote hayo yanawezekana, au sio…ila sisi tunataka
kulijenga jina lako uwe karibu na wenye pesa, wewe unafaa kuwa kiongozi mwema,
tunataka kulifanikisha hilo…tunaweza…’nikaambiwa
‘Sasa ili uwe salama, ili mtoto wako awe salama, timiza masharti
yetu madogo tu, tutakuwa sambamba na wewe...’wakasema na mimi sikutaka
kubishana nao, nikaingia kwenye gari, na gari likaondoka, sasa linatoka, na
wakati huo niliona gari lililombeba yule mtu na mtoto wangu wakiondoka..
Kwa pale sikuona dalili kuwa na wao wametekwa, na hata wakati
tunatoka, wao walielekea njia ya kawaida ambayo nafahamu wanapokwenda, ila sisi
tukageuka upande wa kuelekea Pugu…unaona, na gari halikutembea mwendo mrafu
tukawa tumeshafika ahpo walipotaka kunipeleka mimi.
‘Tumefika mpendwa, tunachokuomba ni wewe kuwa mstaarabu, hatutaki
wewe uonane na mtu mwingine yoyote bila idhini yetu, kwahiyo tutakupeleka
mahali maalumu utakaa hapo, hadi lengo letu likamilike, mambo mengine utakuja
kuendelea nayo baadae..’wakasema
‘Ama hilo tataizo la kibali chako cha kwenda kusoma, usiwe na
wasiwasi nalo, limeshashughulikiwa, utapata muda mdogo tu wa kuweka sahihi yako
pamoja na mambo mengine,…utuelewe, sisi hatuna nia mbaya na wewe, ...’akasema huyo
mzungumzaji
Mimi sikuongea kitu adi hapo, sikutaka kwanza kuongea chochote,…na
wakati huo tulikuwa tunaingia kwenye jengo moja, ni jengo kwa nje linaonekana
kama halijakamilika , lakini kwa ndani limeshakamlika, sijui kwanini walifanya
hivyo.
Tuliingia ndani kama watu wa kawaida, na jamaa yule akaenda
kuongea na mlinzi, na mlinzi akatuelekeza wapi pa kwenda, kumbe pale kuna njia
mbili ya kwenda juu na nyingine ya kwenda chini…kuna jengo la chini ya ardhi,
humo humo lakini huwezi kuligudnua hilo .
Unajua mimi kule ilipangwa
niondoke baada ya siku mbili hivi, lakini kwa haraka nikaamua kuondoka mapema,
hawa watu walifahamu vipi, na mawazo hayo yalinijia usiku na usiku huo
nikawasiliana na watu w ndege, na kukubaliwa kuwa nafasi ipo naweza kubadili
tarehe,..yawezekana ndio, kama wana watu wao, lakini sio kwa haraka kihivyo.
Kwahiyo hapa Dar nilifika
siku mbili kabla ya ile tarehe iliyojulikana kuwa nitafika, ila hadi leo watu
wanafahamu nimefika siku ile ile ya tarehe iliyokuwa imepangwa, hadi leo hakuna
anayelifahamu hilo…’akasema
Tuliteremka ngazi chache
hadi chini..na kufika kwenye ghorofa ya chini ya ardhi,…tukatembea na kuingie kwenye
chumba chenye kila kitu, ...ni chumba cha kifahari, nikaambiwa hapo nitakaa
mimi hadi nitakapopewa maagizo mengine...’msemaji akasema na kuondoka zake.
Kitu cha kwanza nilitaka kujua ni nani yupo nyuma ya haya yote,
sikujua ni nani kwa muda ule,.japokuwa kwa mtizamo wa haraka, toka awali,
nilijua kuwa anayefanya haya yote huenda akawa ni Makabrasha, kutokana na
maaelezo ya watendaji wangu.
Nilipoingizwa mle na kuona hicho chumba nikawa na mashaka, huenda
sio makabrasha au kama ni yeye, basi kuna mtu anamtumiwa huyo Makabrasha,
…maana hicho chumba ni cha kifahari, kuna gharama kubwa imetumika kukiweka
vile.
Kwanza ikabidi nijimwagie
maji kidogo, na kutuliza akili, ...nikatulia na ukumbuke mtoto wangu alikuwa
mikononi mwa mtu niliyemuamini, na huyo mtu alinihakikishia kuwa atamfikisha
mtoto wangu kwa jamaa yangu mmoja, lakin je alimfikisha, ndio nilikuwa nawaza
jinsi gani nitawasiliana naye kulihakiki hilo..
Simu yangu hawakuichukua, nikasema basi ngoja nipige simu kwa mtu
mwingine yoyote kwanza nione kitakachotokea, kiukweli hakukuwa na mawasiliano
ya simu, mawasiliano ukiwa humo ndani hayafanyi kazi, wamezuia namna yoyote ya
kuwasiliana, kuna simu ya mezani…nikaiendea na nilipoinua tu, ujumbe ukasema
‘Kuna tatizo tunaweza kukusaidia…/’ nikaulizwa
‘Nataka kupiga simu nje…’nikasema
‘Unaweza kunitajia namba ya mtu unayempigia nikusaidia
tafadhali..?’ nikaulizwa na mimi nikakata simu.
Wasiwasi wangu kwa mtoto ukawa sasa umethilika, je ni kweli
kafikishwa hiyo sehemu salama, nikawa sina amani…nikaona ni lazima nifanye
jambo, ni lazima niweze kujua kama mtoto wangu yupo salama au la…
Ilipofika muda fulani, nikasikia mlango ukifunguliwa, na akaingia
dada mmoja akiwa kabeba vifaa ni vyakula na vifaa vingine vya kuongeza kwenye
jokofu.., alikuwa kafunga uso wote, haonekani sura, kaacha sehemu ya
macho tu, inaonekana ni muhudumu, aliwekea vyakula, hakuniangalia, alifanya hiyo kazi, na
alipomaliza, akanijia, na kuniuliza
‘Una shida yoyote?’ akaniuliza
‘Ndio , nataka kutoka nje...’nikasema
‘Mhh, fuata maagizo , kama ulivyoambiwa, ..’akasema na kuondoa
vyombo, akaacha kijiko, lakini ni kijiko cha plastiki, ni kama kakisahau,…mimi
sikuwa na mawazo yoyote nacho, akatembea hadi mlangoni , na kabla hajafungua
mlango akasema;
‘Ukweli wewe unaoufahamu,
nakushauri ufanye kama wao walivyotaka, na watakavyotaka…’akasema na
kuondoka. Kwa mpelelezi ujumbe huo ulinitosha kujua ni nini kinachoendelea
humo, lakini kwa muda huo, akili yangu haikuwepo, akili yangu ilikuwa kwa mtoto
wangu,..mama na mtoto wake sio kitu cha kubahatisha.
Nikawa nimetulia, kwanza niliangalia zile kamera juu, nikawa
nawaza jinsi gani ya kuharibu mawasiliano yao, ili wasijua kinachoendelea humo
ndani, …na mara macho yangu yakigundua kitu kwenye kile kijiko cha plastiki,
sikukichukua kwa haraka maana yoyote anayenichunguza juu, ataligundua hilo,
nikavua koto langu na kulirusha mezani kama najisikia joto, nikajinyosha,
nikatembea hatu kadhaa za mtu anayawaza.
Nikajivunga vunga na kujinyosha, halafu nikaliendea lile koti, kwa
haraka nikalizoa, na kuhakikisha kuwa kile kijiko kipo mikononi mwangu
Nilienda chooni, na baada ya kuhakikisha kuwa hakuna kamera,
nikachukua kile kijiko, kama nilivyohisi ilikuwa sio kijiko tu, bali kulikuwa
na zaidi ay hicho kijiko…
Kulikuwa na karatasi nyepesi imekunywa vyema na kunatishwa kwenye
kile kijiko, na nilipokitoa kile kikaratasi nikaona maandishi;
‘Tupo pamoja..’ nikakigeuza nyumba nikaona namba ya simu, nikaikariri halafu
nikakitafuna kile kikaratasi.
Nikarudi kule ndani, …kuna hali isiyo ya kawaida nilihis hali ya
hewa ni nzito, mwili ukanisihia nguvu, na kabla sijadondoka nikajirushia
kitandani, ..na hapo hapo nikazama kwenye usingizi mnzito
Nilianza kuhisi hali ..nahisi nililala sana, lakini hadi hapo
sikuweza hata kujiunua,ila nilihisi sipo peke yangu. Nikajipa moyo, kuwa nipo
salama, ni baada ya akili kutulia.
Nililala kwa muda wa nusu saa hivi, baadae sasa hali ikajidhihirisha kuwa kweli
kuna mtu mwingine humo ndani, hapo kitandani, lakini hadi hapo, mwili wangu
ulikuwa hauna nguvu hata kuinua mkono siwezi,…oh, wamenifanyia nini hawa watu
Hali hiyo ikanikumbusha siku ile nilipobakwa na ..na..mume wa
familia…’akatulia kuongea na kumuangalia mume wa familia.
‘Lakini hii ilikuwa zaidi, maana hata kuwaza kitu, inakuwa vigumu,
akili ni kama imefungwa hivi…’akaendelea kusimulia.
Kwa muda huo cumba kilikwua ni giza, na ni giza nene, …sijui taa
ilizimwa saa ngapi,.nio nikaanza kukumbuka, nikakumbuka wakati nataka
kujipumzisha chumba kilikuwa na mwanga, nikajisikia hewa ni nzito, ..na
nikajirusha kitandani, nikazama kwenye usingizi mnene, nikakumbuka yoet hayo
Kwa vile mwili ulikuwa bado hauna nguvu, sikuweza kuinuka, nikawa
nasubiria litakalokuja kutokea, nikasubiri, mara nikahisi kitanda kikitikisika,
kuwa huyo aliyekuwa karibu yangu, akajiandaa kufanya jambo, au kama alifanya
jambo anataka kuondoka,
Hapo nikawa najaribu kuvuta hisia za nguvu, nguvu ziweze kunirejea,
japokuwa siwezi kuinua hata mkono, au kukunja kidole, mwili umelegea, nikahisi
mkono ukinipapasa sehemu ya tumboni, nikatulia nione lengo la huyo mtu,..
Aliposogeza mkono chini zaidi, ule mkono ukasita, na mara nikaona
kitu kikiletwa mdomoni, ni kijiko, kina kitu kama dawa au maji, yakawekwa
mdomoni mwangu yakapenya, nikameza..nilihis mwili saa ukisimuka,. Na mara ule
mkono ukawa unashika tena tumbo langu, ukielekea chini zaidi.
Nilihisi sasa nguvu zimenirejea, hasira, zikanipanda, nilisubiri,
kabla mkono haujaenda mbali zaidi kwa haraka nikashusha mkono wangu ukaudaka
mkono huo ulioshiaka tumbo langu, nikajirusha,..ni mbinu zetu za mapigano,
nilichoskia baadae ni kilio cha maumivu, na jamaa alikuwa sakafuni akilalamika
maumivu.
‘Aaah, umeniumiza mkono, ooh,, ...nini unafanya wewe, sikuwa na
nia mbaya, nilikuwa nakusisimua ili damu ifanye kazi, aaah, watu wengine bwana...’sauti
ikaniuliza,. Ujue humo ndani kukizimwa taa ni giza kweli,
‘Kwani wewe nani na lengo lako ni nini?’ nikamuuliza
‘Usijali sikuja hapa kwa nia mbaya, kwanza sina muda wa kufanya
lolote na wewe, nimeshachoka, nilikuja kukusalimia tu, nikawa napendezewa
kushika mwili wako uliojengeka kimazoezi, una mwili mzuri sana, na nilitaka
kukusisimua, ili uondake na hiyo hali...’akasema
‘Wewe ni nani,…nijibu kwanza?’ nikamuuliza
‘Wala usijisumbue kutaka kufahamu mimi ni nani mimi ninachokuomba
ni wewe upumzike tu, usiwe na wasiwasi upo salama...’akasema.
‘Nipo salama, wakati mumeniteka nyara, na kupulizia madawa ya
kupoteza fahamu…’nikasema na kwa haraka nikawa naelekea sehemu ya kuwasha taa.
‘Wala usisumbuke kuwasha, nimekuja kukusalimia, tu, kesho asubuhi
nina kikao na wewe, ajenda ni moja, kukubaliana na hayo tuliyoyapanga, wewe
utatusaidia kutupa taarifa chache, na huenda tukakutuma mahali, ukimaliza kazi
yetu, utaenda kuendelea na madhumuni ya kuja huku kwa dharura, unasikia sasa
hii ni amri, vinginevyo....’akasema.
‘Hujanijibu swali langu, wewe ni nani…?’ nikamuuliza
‘Utanifahamu labda hiyo kesho, samahani kwa usumbufu, nashukuru
kwa kuwa mvumilivu, ukifanya hivyo, na kufuata masharti yetu, ukatii yote tunayohitajia,
hutapata taabu, na haya tunayafanya kwa ajili yako, na familia yako,...mwenyewe
utaona, kwa hivi sasa lala,..usijali..’akasema na kuondoka, sikutaka
kujishughulisha zaidi, nikarudi, na kulala huku bado nikimuwazia mtoto wangu.
‘Mtoto wangu yupo wapi…’nikawa naweweseka, maana nilihis kuzama
tena kwenye usingizi mnzito
Nakatiza kidogo, tutaendelea na sehemu hii, muhimu ambayo
inatupeleka kwenye mshukiwa wa mauaji
WAZO LA LEO: Maisha ya mtu yana thamani kubwa sana,
na ni lazima kila mtu atafikia umauti, lakini tujitahidi sana tusiwe sisi ni
sababu ya uamauti wa mwingine , dhambi yake ni kubwa sana, ni kama umeua dunia
nzima…je ni nani anaweza kubeba dhambi za dunia nzima…Tuwape pole wale wote
waliofikiwa na misiba, maana msiba uusikie tu kwa wengine, msiba unauma, hasa
akiwa ni ndugu yako wa karibu. Ila mwisho wa yote tusema tu, yote ni mapenzi ya
mungu, na mwenyezimungu anajua vipi atalilipizia hilo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment