‘Kwanini
ulikimbia kwani hiyo video ilionyesha nini…?’ akaulizwa na hapo akatulia kama anawaza jambo, akaniangalia mimi, na alipoona namuangalia akageuza uso kuangalia kwingine, halafu akasema;
'Hiyo video, ilionyesha karibu kila kitu,
….’akasema na kutulia
Tuendelee na kisa chetu
***************
‘Kila kitu , ...hya tuambie vitu gani hivyo, mbona unakuwa kama unaogopa kuviongea hivyo vitu, ukumbuke kuwa haya tunayafanya kwasababu yako, sasa usitupotezee muda hapa…’akasema mke
'Unajua hapa natafakari mengi...sawa nitaongea tu, usiwe na shaka...'akasema
'Kwenye hiyo video, ilipoanza, ilikuwa inaonyesha kijana wangu, kakaa kashika shavu, kainamisha kichwa chini, baadae akainua kichwa, usoni kukaonekana machozi..kuashiria kuwa alikuwa analia..ndivyo ilivyoanza hivyo...baadae ikaonyesha anaongea, ...alikuwa anaongea mengi tu, lakini mimi nitaelezea yale yanayohusu hili tatizo.
'Ndugu walengwa, sikupenda kulifanya hili,...maana najua madhara yake, nawaheshimu sana wazazi wangu na kuwapenda sana, na najua baada ya kuuona huu ukweli, mtahakikisha kuwa video hii mumeiharibu, nisinelipenda hili likaenda zaidi ya nyie niliowalenga...'akalisema hivyo kwenye hiyo video.
'Mimi sina ubaya na mama, maana pamoja na ya kuwa awali nilihisi yeye ndiye mbaya kwa baba, lakini baada ya uchunguzi huu, nikagundua kuwa kumbe baba ndiye yupo nyumba ya haya mabaya yote kwa ushahidi wa haya mtakayoyaona...nampenda sana baba yangu, niliomba kila siku abadilike, niliomba kila siku ..ampende mama, niliomba kila siku hali yetu iwe kama zamani, lakini kila siku ilikuwa afadhali ya jana...
Basi hapo akaonyesha picha za wazazi wake, wakati wa ndoa, jinsi walivyokuwa wakipenda, na baadae akaonyesha kitu kama mpasuko...na kuweka ngurumo kwa radi, halafu akaanza kuongea...
‘Siku za baadaye hali ikaanza kubadilika, baba akawa kama hamjali mama, kukawa na mabishani hata kwa kitu kidogo, baadae nikahisi labda ni kutokana na hali za kiuchumi, maana kuna muda hali ilikuwa mbaya, maisha yalikuwa magumu, nikasikia mara kwa mara baba akisema ipo siku nitakuwa tajiri kama baba
yako na wewe na wazazi wako mtakuja kuniheshimu.
Kijana alielezea mengi kwa jinsi alivyoona yeye....'hapo akatulia kuongea na mama Ntilie akamuuliza
‘Sema
ukweli wako, ni nani chanzo cha mabadiliko ya ndoa yenu, ni kitu gani kiliwafanya
nyie wawili msielewane…?’ akaulizwa.
‘Ukiuliza
hivyo utanifanya nijitetee nafsi yangu, mimi niliona kama mke wangu hanijali,
kila nichomuambia hanisikilizi, anajiamulia anavyotaka yeye, vikao, shughuli, ..yaani hakuna kushirikishwa...na hilo
likanifanya nihisi ni kwa vile mimi sikuwa na mali kama wazazi wake, kwahiyo
uinabidi nitafute mali niwe kama wazazi wake …ndivyo nilivyoona hivyo…’akasema.
‘Ni
kweli kuwa mke wako alifanya hivyo, kwa vile wewe hukuwa na mali kama wazazi
wake..?’ akaulizwa.
‘Kwa
muda huo nilifikiria hivyo, lakini baada ya haya yote niligundua kitu, kuwa ni
udhaifu wangu tu, unajua tena sisi wanaume tulivyo,...ukiona huna kitu , mke ndiye mtendaji kuna hali ya...kujisikia vibaya fulani...kwahyo nikaona nitafuta namna ya kujionyesha kuwa mimi ni mwanaume...
Mara kwa mara kulikuwa na vikao vya watu fulani, unajua kwenye jami kuna makundi ya namna hivyo, wenye uwezo wanakutana kwenye mahoteli,..au vikao vya ..namna kwa namna, mimi ilifika sehemu siwezi kuhudhuria...sikuwa na kitu, na nikifika,..oh, labda michango , wenzangu wanatoa bila kusita, mimi, kwanza najiuliza..ni hali yangu ..lakini iliniuma sana..'akatulia
'Kwahiyo kwa hali hiyo, ikanivuta nifanye jambo...nikaanza kutafiti, wenzangu wamefanya nini..kwa bahati mbaya nikakutana na marafiki wa namna ambayo isingelinisaidia, na nikajikuta nimetekwa na mawazo yao zaidi, sikujali elimu yangu tena...'akatulia.
'Ni kwamba ilishafika mahali nahitajia mambo kwa haraka bila
kufikiria mbele, na hao niliowauliza ndio wakanisimulia utajiri wa kupitia huko kwa shetani ….…’akasema.
Haya tuache hayo tuelezee kuhusu hiyo video...'akaambiwa
‘Kwenye hiyo video alielezea kuwa ile hali ya
sisi wazazi kutokuelewana ilikuwa ikimkera sana , akawa anatafuta
jinsi gani ya kuwasuluhisha wazazi wake, jinsi gani hata yeye anaweza kuleta utajiri, ili wazazi wake wawe na raha.. lakini hakuweza, hakujua, kwani hata elimu yake aliyopata japokuwa alifaulu vyema, lakini alikuw ahajapata kazi, kazi zimekuwa ni adimu...
'Kuna muda akavutika na biashara haramu....'hapo akatulia
''Biashara gani...?' akaulizwa
'Hakusema, ila alisema hivyo, kuwa alitaka atafuta njia ya kupata utajiri, huenda ukawafanya wazazi wake wakajirudi na kuwa kitu kimoja...hapo akawa anaonyesha jinsi wazazi wake wanavyogombana, kumbe tukigombana , alikuwa akatuchukua kwenye video yake.
Alielezea mengi tu, na hata kuwatupia lawama babu na bibi kwa jinsi walivywatenga watoto wao, anasema kwamba kama babu na bibi wangeliwachukua watoto wao walivyo, wakawawezesha kuliko kuwatenga , eti kwa vile bint yao hakukubaliana na wao, huenda mengine yasingelitokea...
Sasa ndio akaja sehamu ya pili, sehemu hii akawa anaonyesha, mabadiliko ya baba...
Akaelezea
alivyoanza kuona mambo ya ajabu
‘Kiukweli
nimevumilia sana, na sijui hata nianzie wapi..ila ninachoweza kuwa na uhakika
nacho ni kuwa mambo yalianza kuwa mabaya pale baba aliporudi kutoka safari ya
mikoani…ninaweza kushuhudia hilo, maana mimi nipo karibu sana na baba yangu.
'Siku
hiyo aliporudi , usiku wake nilimuona akichimba shimbo upande wa mbele wa
nyumba, na nikajua labda kuna kitu kichafu anakifukia, lakini
kilichonishangaza, ni ile hali ya baba alikuwa hajavaa nguo, na ilikuwa ni
usiku sana, na kuna matukio kama hayo yaliendelea kutokea. hapo akaonyesha kwa mbali picha ya mimi nikifanya jambo..nikiwa sina nguo..
Akaendelea...
'Mara
nikaanza kuhisi kama kuna watu wanakuja usiku lakini siwaoni, na wakati
mwingine nahisi kama kukabwa, hali hii ilikuja hata kutokea kwa mabinti wa kazi
waliokuja hapo nyumbani, na kuna siku nilijaribu kumuuliza baba lakini hakutaka
kuliongelea hilo nikahisi kuna kitu ananificha, aliniambia ni mambo ya kawaida
ya watu wazima nisiwe na wasiwasi nayo…
Mimi
napenda kudadisi, nikavutika sana nikawa nachunguza kinachoendelea usiku, na kawaida
yangu nimejenga tabia hii ya kuhifadhi kumbukumbu nyingi kwenye video…basi nikaona
hili la baba nitalichukua kwenye kumbukumbu zangu, ili baadae nije kumuonyesha..
Uchunguzi huu ulinifanya nigundue mambo ya kutisha zaidi...maana usiku nilioweza kuamuka, na kufuatilia, niliweza kumuona baba akifanya mambo ya ajabu ajabu...na cha ajabu kuna usiku mwingine nilikuwa siwezi hata kualala, maana nikilala najikuta naota ndoto mbaya, au nahisi watu wanakuja
kunisumbua, japokuwa hata nikijitahidi kuna muda nazidiwa nguvu najiukuta
nimelala…hali hii ikwa inanipa mashaka, nikaogopa hata kulala humo ndani.
Hata
hivyo niliweza kuchukua baadhi ya video, zikimuonyesha baba akiamuka usiku, na
kilichonita mashaka ni jinsi baba alivyokuwa akitembea...anakuwa kaam sio yeye...ndio maana hata niliposikua habari kuwa baba ana ugonjwa wa kuota kwamatendo nikakubaliana na hilo.
Lakini baada ya kuchunuza sana nikagundua sivyo hivyo wanavyosema kutokana na matukio haya nitakayoyaonyesha hapa ...hapo akaanza kuonyesha baba yake anavyotoka usiku...na kuna muda kama anaongozwa na mtu , mtu aiyeonakena...
Ikawa inaonyesha video mbali mbali, nyingine baba yake akitioka usiku na kutembea
kama roboti akielekea chumba cha msichana wa ndani, baadae anatoka, ..na
vitendo kama hivyo vilikuwa vingi, lakini ambayo ilionyesha mambo ya ajabu
Baadae nikasikia kuwa mama katengeneza video ya kuchukua matukio humo ndani, nikachunguza mpaka nikaigundua ilipo, nikawa naifuatilia hiyo, na siku mama alipoipeleka kwa huyo mtu wake, mimi nikaifuatilia na kuiba, ...baada ya kukamlisha kazi aliyopewa,..huyo mtu namfahamu sana.
Na nilipoona hiyo video ndio nikaamini kuwa baba hakuwa na matatizo kama alivyosema docta kuwa baba anaota ndoto kwa vitendo, maana ….ndani ya video hiyo walioekana watu waliojificha kwenye kitu kama giza, na huyo mtaalamu akakuza, na kuwaonyesha watu wa ajabu,..wachawi waliokuwa wakimuongoza baba, na mambo ya ya ucafu waliyokuwa wakifanya...
Video hiyo ikaonyesha kila kitu...inatisha , hata mie ambaye sikuwa na ufahamu wa hayo, niliogopa, na kiukweli nilijuata kwanini niliuangana na hao watu..sitaki hata kuelezea zaidi ya hayo niliyoyaona kwenye hiyo video, kwani baada ya kuiona nilihsii vibaya sana,…’akasema
‘Ina maana ni kweli hizo taswira za hao wachawi ziliweza kuonekana kwenye hiyo video…?’ akaulizwa.
‘Unajua
kijana alichukua hiyo video akatoa nakala kama nne, hivi, moja akaniletea mimi,
nyingine kwa mama yake nyingine kwa babu yake, nyingine sijui alataka kumpa
nani, na ujumbe kuwa anakwenda na hatagemei kurudi, kurudi kwake labda apone,
lakini kaba hajafanya hivyo, anataka wanafamilia wajua kinachoendelea ndani ya
hiyo nyumba. Na alichogundua kuwa nyumba hiyo ilishatekwa na wachawi, na
aliyesababisha hayo ni baba yake, na video hiyo ndio ushahidi...kiukweli ilionyesha kila kitu, hakuna ubishi...'akasema
Jamani dunia hii , usiku wengine wamelala, wengine wanafanya mambo ya ajabu kabisa,..nilipoona video ile, nikahisi kichwa kinauma, nililia, nikalia…maana kweli kila
kitu kilionena kiu-wazi, jinsi gani hao wanga walivyokuwa wakiingia na kufanya
mambo, yao, ilikuwa kama unaangalia video ya kuigiza, kumbe ni matukio ya
kweli, na mimi ni muhusika…sijui huyo jamaa aliwezaje kuzifichua hizo taswira
za kichawi…’akasema.
‘Unasema
ulilia sana, kwanini sasa ulilia, wakati ulipenda wewe mwenyewe..?’ akaulizwa.
‘Nyie
hamjui jinsi gani nilivyokuwa nampenda huyo mtoto wangu, .jinsi gani nampenda mke wangu, hamjui ndani ya nafsi yangu kulivyo..lakini ningeliwezaje kulionyesha hilo, wakati akili imeshaona kuwa ili upendwe, ili uonekane ni bab bora ni mpaka uwe na mali...
Kiukweli kijana wangu
ambaye nilishibana naye sana alikuwa huru kunielezea matatizo yake na mimi yake
niliyoyaona anastahiki kuelezewa nilikuwa namuelezea, yeye alikuwa karibu na
mimi kuliko, alivyokuwa kwa mama yake, muulizeni hata mama yake hapa analijua
hilo…’akasema.
‘Sasa
kwanini ulimfanyia hayo uliyomfanyia..mbona sisi hapo hatukuelewi...?’ akaulizwa.
‘Kama
umenielewa vyema maelezo yangu tokea awali, mimi sikudhamiria kuyafanya hayo
mabaya kwa nia ya kuiumiza familia yangu.., lengo langu ilikuwa kutafuta hali nzuri ya maisha, kwa masilahi ya
familia yangu …na ujue shetani alivyo na nguvu nilijua hayo mambo ni ya muda
mfupi tu, nitapata nitafikia kileleni kama hao ninaowaona, na maisha
yataendelea, sikujua kuwa mambo hayo ni ya muda tu..yana mitihani yake…’akasema.
‘Sasa
ikawaje…?’ akaulizwa.
‘Nilitoka
kumtafuta, mtoto wangu, kwa marafiki zake, na sijui ilikuwaje siku kwa maana
kwa, kila rafiki yake niliyemuendea, nikifika kwake anasemaa ametoka sasa hivi,
ni kama alitaka kuwapitia marafiki zake kama anawaaga vile..mpaka usiku
sikuweza kumpata , na nilipochoka ndio nikakumbuka kuhusu hizo video nyingine
alizowatumia hao watu…
‘Ulijuaje
kuwa kawatumia hao watu wengine na ni akina nani..?’ akaulizwa.
‘Kwenye
hiyo video aliyonitumia mimi aliandika nakala kwa…mama, babu..na mtu mwingine
hakumtaja…
‘Sasa
ulikuwa una uhakika gani kuwa kweli kaituma kwa hao watu na kwa njia gani?’
akaulizwa
‘Hapo
sikujua, nikaanza kumtafuta mke wangu, nijue wapi alipo, nikajua kama kamtumia
mke wangu itakuwa humo humo ndani, nikatafuta sikuipata, nikamtafuta mtu wa
karibu na baba mkwe ajaribu kuona kama kutakuwa na mzigo wowote uliotumwa huko,
sikuweza kupata taarifa yoyote…kwani baba mkwe hakuwepo nyumbani.
‘Hayupo
nyumbani, nakuomba uhakikishe kama kuna mzigo utafika hapo unaupokea na mimi
nitakulipa pesa nyingi, si unanifahamu nilivyo,…sawa..’nikamwambia huyo mlinzi
wa hapo nyumbani kwa baba mkwe, mlinzi huyu niliahi kumfanyia jambo kubwa,
kiasi kwamba aliahidi kuwa hataniangusha.
‘Hamna
shida bro…’akaniambia, kwahiyo hapo nikawa sina shida napo sawa, lakini ni
swala la kubahatisha tu.
‘Mtu anayeweza kukusaidia ni yule bint…’nilipokumbuka
hilo ndio nikaanza kumtafuta huyo binti, nilijua wapi naweza kumpata, nikaenda
nyumbani hapo anapofanyia kazi, na nilipokutana naye hakutaka hata kuongea
name.
‘Umekuja
kufanya nini hapa, unataka kunigombanisha na mke wako au sio, kama ulivyofanya
huko nyumbani mapaka nikafukuzwa kazi…hayo uliyonifanyia hayatoshi, nakuheshimu
sana baba, nakuomba uondoke…’akasema
‘Nimekufanyia
nini, kwanini unasema hivyo, unajua nimekuja hapa kufanya nini,..…?’
nikamuuliza sasa kwa hasira na sauti hiyo ikamfanya anywee na kutulia.
‘Unafikiri
mimi sijui mlichonifanyia na huyo mchawi wako, nayajua yote, na najua
kilichokuleta hapa ni hicho, mnanitakia nini nyie watu, tumewakosea nini,…’akasema
kwa sauti ya huzuni.
‘Sijui
unaongea nini, wenyewe hawapo humu…?’nikajifanya sijui kitu, ni kama vile
nimekuja kukutana na wenye nyumba.
‘Wewe
na huyo mchawi mpo kitu kimoja japokuwa unajifanya wewe hujui kinachoendelea,
na unajua fika muda kam huu wenyewe wanakuwa kazini, …’akasema akiendelea na
shughuli za usafi.
‘Sikiliza
nikuambie kitu,…yule mzee mbaya wako amefariki, huna taarifa hiyo…’nikasema na
yeye akashtuka kidogo, halafu akasema, kama kuuliza
‘Mzee
gani…?’ akaniuliza, sasa akiwa kasimama na kuniangalia, uso wake ulijaa hamasa
au wasiwasi fulani.
‘Yule
mbaya wako wa kijini kwenu aliyetaka kukuoa…’nikamwambia
‘Nimesikia
hivyo, na kifo chake nasikia ni kibaya kweli, alikuwa kipiga kelele kama
anaumia,anaomba msamaha…mmmh, mpaka nikakufuru na kusema,..kumbe na yeye
anakufaga, au ndio huko kuigiza kwake, maana kuna kipindi walisema hivyo, kesho
yake tunaambiwa yupo hai…siwezi kuamini mpaka afikishwe kaburini, yule mzee
alikuwa tishio…lakini ndio hivyo hakuna atakaye ishi milele…’akasema
‘Ndio
keshafariki, usiwe na mashaka naye tena….’nikasema
‘Ndio
umekuja kutoa taarifa au…?’ akauliza.
‘Hapana,
najua watu wameshafahamu,..ila huu mguu ni wa kwako…nimekuja kwako unisaidie
jambo moja..’nikasema na hapo akageuka kuendelea na shughuli zake, akasema
‘Nilijua
tu…unajifanya umekuja kwa wenyeji hapa….haya niambie ni jambo gani, mimi sina
uhusiano na huyo mtu, zaidi ya kuwa alitaka kunioa,nikamkatalia…kama ni mambo
yenu ya kichawi, mimi sijui, na wala sijahusika kupambana na huyo mtu….’akasema
‘Sawa,…nisikilize
kwanza,…mbona unakuwa na maneno mengi,… wewe unajua huko anapotokea, ni nani
anaweza kunisaidia…unajua wewe unafahamu fika jinsi gani alivyopaharibu pale
ndani kwangu, na nilishaongea naye akasema atayaondoa mambo yake, sasa ndio
huyo ameshafariki, ninataka nyumba yangu
iwe safi, ni nani anaweza kunisaidia..?’ akaniuliza
‘Ni
yule yule adui yake, yeye alikuwa ni mwalimu wake, nenda ukaonane naye, huyo
ataweza kukusaidia…’akasema
‘Oh..mbona
hata yeye kafariki pia….’nikasema na hapo huyo binti akadondosha ufagio
aliokuwa kaushika kumbe alikuwa hajapata hiyo taarifa ya kifo cha huyo mzee
mwingine.
‘Hapana
..ina maana hata yeye kafariki, unajua wale watu, nasikia kipindi cha nyuma
walikuwa marafiki, mwalimu na mwanafunzi wake,..ghafla wakaja kukosana,
wakaanza kupigana vita ..niliposikia huyo marehemu kaja hapa Dar, nikajua na
huyo mwenzake atakuja tu, maana wanawindana kweli..oh, sasa, mimi sijui nikusaidieje…’akasema
‘Sasa
baada ya hao ni nani mwingine anayeweza kunisaidia,maana haya mambo yamekuwa
makubwa kwangu…’nikamuuliza
‘Mimi
sijui..huko kijijini kwenyewe nimekuja kupaelewa baada ya matatizo yaliyotokea
huko kwako…zaidi ya hayo mimi sitaki hata kurudi tena huko kijijini…, lakin
kama hao watu wawili wamekufa, nahisi kijiji sasa kitakuwa na amani…’akasema
‘Mhh…sasa
nitafanyaje…’nikabakia kushika kichwa
‘Sasa
umekuja kwangu ukijua mimi nitakusaidia, hahaha, sikiliza baba,..mambo kama hayo
ulitakiwa uende kuwauliza wazee wa huko huko, kijijini…na kuna watu wlifika
hapa karibu, niliwaona, wnatokea huko kijijini, wao ni watu wa dini, hao
wanaweza kukusaidia, kuliko njio hiyo ya kutafuta waganga wa kienyeji…’akasema
‘Nitawapataje
hao watu…?’ nikamuuliza.
‘Niliwaona
tu mara moja, sijui wapo wapi…jaribu kuulizia watuu…na jingine ni hilo la
kwenda kuwaona wazee wa huko kijijini…’, aliniambia,
‘Lakini
kuna mtu kasema wewe unaweza kunisaidia….’nikasema
‘Mimi
nitakusaidia kwa vipi sasa, na kwanini asema hivyo, anahusika na hao watu
nini,, anatokea huko kijijini au,..?….mimi kwa udadisi wangu niliwahi kuwauliza
wazee, waliniambia matatizo mengine kama hayo yako, ambayo yanaingiliana na
dhuluma,…wewe si umefanya mabaya, kwa watu , si ndio hivyo, kinachotakiwa ni
kuwaendea hao uliowakosea uwaombe msamaha, hakuna njia nyingine…’akaniambia
‘Oh,
basi mimi naanza kwako wewe…kukuomba msamaha….’nikasema
‘Kwani
mimi umenikosea nin…si unakumbuka nilikulilia hali kukupigia magoti wakati
nafukuzwa pale nyumbani kwenu.., ukasema wewe hujui lolote, ukanisaidi kuitoa
ile mimba, huku ukidai sio ya kwako…uliniambia kabisa wewe, huna makosa mimi
nakusingizia tu…’akasema
‘Kiukweli
mimi hata sijui kitu,..ila nahisi kuwa nimekukosea sana, nakuomba unisamehe…’nikasema
huku nikienda kumpigia magoti, yeye akabakia kushangaa tu.
‘Wewe
mbamba, mna nini leo, …mimi sijui kitu…kama ulinikosea ni haki yangu kufahamu
ulichonifanyia, niambie ulinifanyia nini, la sivyo sitaweza kukusamehe..nikuulize
tena je ni wewe ulinipa hiyo mimba..?’ akaniuliza
‘Sina
uhakika na hilo,…sio mimi…mi-mi-sijui…ndio maana nakuomba unisamehe, maana
yaliyokuwa yakifanyika mimi sina uhakika nayo, si unajua ilivyo kuwa…’nikasema
‘Kama
huna uhakika nayo, basi huna kosa, nenda kwa hao uliowakosea, hasa kijana wako,
mimi niache niendelee na kazi za watu, usije kunifukuzisha kazi..…’akasema
akiendelea na shughuli zake.
‘Kijana
wangu nitampata wapi sasa…?’ nikamuuliza
‘Alikuja
hapa akaniomba nimsamehe..na anaonekana kachanganyikiwa kabisa, nikamuuliza
kosa langu akasema hana uhakika, kama ulivyosema wewe, akanipigia magoti huku
analia, anataka nimsamehe, anadai kuwa kaambiwa ili apone awaombe msamaha wale
wote aliowakosea, kwahiyo kaja kwangu,.., nikamwambia mimi sijui kosa langu
kwake…akawa analia, hajijui,…mmh, nikamuonea sana huruma…’akasema
‘Oh,
jamani kijana wangu, sijui nitawezaje kumsaidia, sasa wewe utanisaidiaje mimi…?’
nikamuuliza
‘Unajua
nyie watu wawili mna nini sijui, hayo unayoniambia sasa hivi kijana wako
kaniambia hivyo hivyo…na nilipomuuliza ana matatizo gani akasema…, lakini
nikamuambia mimi siwezi kujua matatizo yake, wewe bab yake ndiye unaweza kuyafahamu…ndio
akasema, wewe yaonekana hutaki kumsaidia kwa hiyo atakachokifanya anakijua yeye
mwenyewe, ….’akatulia kama vile kasikia sauti
******************
‘Kuna
nini..?’ nikamuuliza.
‘Bosi
atakuwa kafika, nimesikia mngurumo wa gari lake…naomba tafadhali uondoke humu
ndani haraka, isije kulete picha mbaya, yaliyopita bado yapo kichwani mwa watu,
na mim sitaki kuzalilika tena…’akasema.
‘Usiwe
na wasiwasi nitaongea na huyo bosi wako, mimi sina matatizo na hii familia,
wananifahamu vyema…usijali kwa hilo…..’nikasema na haikupita muda, akaingia
mama mwenye hiyo nyumba, aliponiona akaonyesha uso wa kushangaa, nikasalimiana
naye na kumuambia nilikuja kuangalia kama mke wangu yupo hapa
‘Mke
wako!!!….hapana, hayupo hapa, japokuwa ndio nafika…’ akasema huku akimuangalia
mfanyakazi wake kwa mashaka, halafu akasema.
‘Nilihisi
yupo hapa napiga simu yake haipatikani…’nikadanganya hivyo.
‘Mhh….mke
wako aje hapa wewe usijue,… mke wako si yupo polisi…’akasema huku akimtupia
tena jicho huyo mfanyakazi wake , ambaye kwa muda huo alikuwa akipanga panga
vitu kwenye kabati.
‘Polisi…!!!?
Kufanya nini huko…?’ nikamuuliza na yeye akashikwa na butwa, akiniangalia kwa
mshangao.
‘Ok…yupo
huko, kuhusu maswala ya huyo marehemu, kuna mambo anahojiwa, sasa shemeji,
nikuulize tu, kwanini wewe hukufika siku ile hospitalini, wenzako wote
walikuja, kasoro wewe, hata hivyo tumemalizana, na keshazikwa..mmh, ndio hivyo
tena…yaani we yasikie tu…karibu shemeji mboana upo wima wima…’akasema
‘Kwanini
azikiwe hapa, si anatakiwa kupelekwa huko kijijini kwao au..?’ akaulizwa
‘Yaani
inatisha..japokuwa mwili uliwekwa kwenye majokofu, lakini umeoza, na kuanza
kujaa mafunza..inatisha huwezi hata kuangalia…kwa hali iliyopo, wakaona ni bora
tu kuzika hapa hapa kwenye makaburi ya city…’akasema
‘Mungu
wangu…’nikasema
‘Sasa
vipi kuhusu kijana wako, maana mke wako anasema kijana alikuwa akimitafuta
kwenye simu, na alipotaka kumpigia tena akawa hapatikani, kwenye simu alikuwa
akiongea huku kama analia, alivyosema mama yake, inaonekana hayupo vizuri,
….’akasema
‘Analia,
analia nini, mbona ….’akataka kusema jambo halafu akakatisha.
‘Zaidi
alisema ana mzigo muhimu sana kwa mama yake, alikuwa akitaka kumpatia mkono kwa
mkono kwani anasafiri, kwani anasafiri kwenda wapi..?’ akauliza
‘Sijui
kama anasafiri, lakini vijana wana shughuli zao nyingi, kama anasafiri
ataniambia,…hata hivyo, hata mimi namtafuta, nilijua mke wangu yupo hapa ,
maana simu ya kijana nilipompigia alikuwa hayupo hewani..’nikasema
‘Mhh..huyo
kijana mu8angalie sana, nahisi ana matataizo makubwa, …’akasema
‘Kwanini
unasema hivyo…kwani unamuonaje wewe?’ nikauliza
‘Mke
wako anadai kijana wake siku hizi hayupo sawa, na yeye anahisi huenda ni kunatokana
na nyie wenyewe wazazi, ..’akasema
‘Kasema
hivyo mke wangu, mmhh, siamini, kwanini asema hivyo…!?’nikaguna nikihisi huenda
wameongea mengi kuhusu familia yake, kitu ambacho siki-kipendelea.
‘Ni
katika kuongea tu, lakini mke wako hakutaka kusema zaidi, sasa kwa ushauri
wangu mtafuteni kijana wenu mkae naye pamoja, muone mtamsaidiaje, hilo linaweza
kuwa suluhisho, …kwani shemeji kuna tatizi gani, maana yule ni rafikiyangu
lakini sio kila kitu anakiongea, hasa kuhusu mambo ya familia yake, namuona
hana raha siku hizi…?’akaniuliza
‘Hamna
kitu shemeji ni mambo ya kawaida tu,…sawa shemeji,nashukuru, kama takuwa hewani
nitampigia simu, na kama ukimuona, basi mwambie namtafuta, au huenda sasa yupo
nyumbani..nikasema na kuanza kuondoka, na wakati nipo nje….simu yangu ikaita…,
alikuwa mke wangu.
‘Halloh..’nikasema
‘Sikiliza
wewe mwanaume, kama kuna kitu kitatokea kwa mtoto wangu, nitakachokufanyia
hutaamini, utakwenda kuozea jela..nakuhakikishia kwa hilo…’akasema
‘Kwanini
unasema hivyo, kwani kuna nini kimetokea, na wewe upo wapi..?’ nikamuuliza
‘Nipo
polisi, ndio naondoka huku, nikitoka hapa napitia kwa baba, nataka tuje naye huko nyumbani…’akasema, hapo nikahis labda ameshauona huo mkanda...na ukiona ilivyo, utahisi mimi ni mchawi...
‘Kuhusu
nini…ni kuhusu huyo marehemu kwanini nyie muende polisi..?’ nikamuuliza
‘Kuna
jingine ndilo limenichelewesha, askari wa kitengo cha madawa ya kulevya,
alitaka kuongea na mimi , anadai kuwa kijana wetu anatumia madawa ya kulevya, na wana wasiwasi
kuwa anafanya biashara hiyo,…’akasema
‘Kwa
ushahidi gani,…?’ akauliza.
‘Wanasema
kuna kipindi ghafla hali yake ilikuwa nzuri, maisha ya juu sana, hana shughuli
ya maana inayojulikana pesa alipatia wapi…na ameshaonekana akiwa kalewa hayo
madawa….’akasema
‘Sio
kweli, sasa umelimalizaje hilo, ngoja nitaongea na mume wa rafiki yako, tuone
atavyoweza kutusaidia au unasemaje mke wangu….?’ Nikauliza na kusema
‘Usitake
kusema hujui, hayo umeyasababisha wewe...'akasema hapo moyo ukanilipuka pwaah
'Kwanini unasema hivyo mke wangu, una ushaidi...'nikataka kusema hivyo bahato yeye akanikatiza kwa kusema
'Kwenye simu nilimuuliza ana matatizo
gani akasema nikuulize wewe, na kuna huo mzigo anataka kunipatia, una kila
kitu..nikamuuliza kitu gani, akakata simu, huku analia,…sasa nataka nikifika
nyumbani unieleze ni nini kinachoendelea, na hata baba anataka kuja kuongea na
wewe, na anaonekana kakasirika sana, mimi nimechoka..…’akasema na kukata simu.
‘Mungu
wangu….’nikasema hivyo huku nakimbia..nakimbia kuuwahi huo mzigo kabla
haujafika mikononi mwa mke wangu…na wakati nakimbia simu yangu ikaita tena
nilipoangalia, nikaona ni namba ya yule mlinzi wa kule kwa baba mkwe
‘Halloh..’
nikaita na mara simu ikazima, kuangalia imejizima, nikaiwasha, kumbe chaji
imekwisha, hapo hapo nikatafuta bajaji, sasa safari ikawa huko kwa baba mkwe,
nikakutane na huyo mlinzi, huenda ndio huo mzigo...yaani hiyo video haifai kabisa waione wakwe zangu, najua wakiiona itakuwa ni ushahid wa kile wakilichokuwa wakikisema, na sizani kama kutakuwa na mjadala hapo...
Bajaji ilienda kwa kasi, kama nilivyomuomba huyo muendeshaji, na nikakaribia hapo kwa baba mkwe, sikutaka nionekane kwa mbali
nikamuona huyo mlinzi kasimama mlangoni, na gari la baba mkwe linaingia…na nilimuona yule mlinzi kashika kitu...ni bahasha…nikajua ni huo mzigo wa video...
‘Hapa
nikumuwahi tu…’nikasema na kushuka kwenye bajaji mbio mbio kuelekea nyumbani kwa baba mkwe...
‘Pesa
yangu mzee….’mwenye najaji akaniuliza, na mimi sikuwa na muda wa kumsikiliza
mbio mbio kuelekea kumuwahi huyo mlinzi, nyuma yangu bajaji inakuja kwa kazi
'Mzee pesa yangu...
WAZO LA LEO: Tusione kuwa kuongea, kutumia ulimi,
kuandika mambo ya kiuzushi, ni jambo la kawaida tu, haya mambo ambayo yanaumiza
wengine, yanasababisha madhara kwa jamii, ni dhuluma, na madhambi yake ni
makubwa, maana hujui ukumbwa wa hayo madhara kwa wengine, hujui kiasi gani mtu
mwingine anaumia na huo uzushi…, na je kuumia huko kunaishia wapi…na je hayo
uliyoongea, au kuandika yana ukweli, yanasaidia jamii, tujiulize kwanza kabla
ya kuandika, au kuzua,..
Hala hala jamani...tuweni makini sana na ulimi, tuweni makini sana kalamu..tusione ni jambo rahisi tu,..Uzushi
waweza kusababisha vita, na vita havina macho, watu wanauwana, na wamakufa watu
wasio na hatia, watoto wadogo, wazee, akina mama,… je huoni kuwa wewe ulizua,
ukachonganisha ndio wewe uliyewaua, …kwanini twajifanya wacha mungu , lakini
matendo yetu ni ya kumcha shetani….
Tumuombe
mwenyezimungu azisafishe nyoyo zetu, tupendane, tusaidiane,…ili dunia iwe ya
amani na upendo.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment