‘Sasa
kilichotokea, baada ya mtundu kufungwa, wateja wote wa kampuni ya Mtundu, wakahamia
kwa huyu mtaalamu,kwahiyo mtaalamu akawa
juu sana kibiashara kipindi hicho, na ukumbuke kipindi cha nyuma kulikuwa hakuna ushindani mkubwa
wa kibiashara kwenye nyanja hii ya mitandao na komputa, kwahiyo alikuwa na
wateja wengi sana...’ akaendelea kuongea mpelelezi.
‘Hilo lipo
wazi endelea....’akasema mkuu wake akiangalia saa yake.
‘Utandawazi
na mambo haya ya mawasiliano yakaingiliwa na wawekezaji wengi njanja hii ikawa
inakuwa kwa kasi,....makampuni mengi yakajielekeza huko, kukaanza ushindani wa kibiashara, soko likawa
na bidhaa nyingi kuliko wanunuzi,...’ akasema
‘Na kama
ujuavyo, bidhaa zikiwa nyingi kuliko wateja, soko linapungua, bei
zinalazimishwa bei kushuka, bila kujali gharama za uendeshaji,...na hali kama
hii, ikaanza kuyumbusha makampuni mengi...bidhaa wanazo, utaalamu wanao, lakini
wateja hakuna, hilo likaanza kumyumbusha hata mtaalamu ,mwenyewe na biashara yake..
‘Ndio ni
kipindi hicho na ilikuwa ni tatizo la dunia nzima....au?’ akauliza mkuu
‘Ndio
lilikuwa janga la wengi, ...na kwa huyu jamaa aliyezoea kujiona yupo juu, ana
wateja wengi, alibweteka kwa kipindi hicho, ulipofika upinzani, akaanza kushuka
ki biashara mambo yakaanza kumuendea mrama, ikafika mahali sasa hana
wateja,...hana biashara, na kuanza kuandamwa na madeni,...mwanzoni kama
walivyo, waajiri wengi, ..., akaanza kupunguza wafanyakazi...
‘Wengi
hukimbilia kuunguza wafanyakazi kama njia ya kupunguza gharama, hivi hakuna
njia nyingine mbadala...’ akawa kama anauliza huyu mkuu
‘Ni kifo cha
mfa maji tu, kutapa tapa, zipo njia nyingine lakini hiyo hupewa
kipaumbele.....’akasema
‘Haya
endelea.....’akasema mkuu
‘Huku na
huku ndipo akamkumbuka rafiki yake aliyekuwa huko jela...’
‘Ndio ulisema
aliwahi kuonekena huko, ...lakini hilo la kumuendea rafiki yake mlijumuisha tu,
sizani kama mliongea na huyo rafiki yake akakubali kuwa aliendewa kwa ajili
hiyo, kutoa ushauri, je huo ushahidi una mshiko ...?’akasema
‘Tulifanya upelelezi
huo kwa huyo rafiki yake, lakini huyo rafiki yake hakukubali, yeye alisema
alitembelewa tu,..na huwa anatembelewa na wengi, lakini hawakuongelea maswala kama
hayo...’akasema
‘Ikawaje
sasa, maana huwezi kuniambia mtalaamu anayumba kibiashara, wakati sasa
anaonekana kuwa miongoni mwa watu wanaofanya vizuri, ..... sijauona huko
kuyumba kwake....hebu angalia sasa anavyofanya, anawasaidia vijana,kafungua
makampuni mengi sana, ushahidi gani wa kuweza kuonekana kuwa alikuwa hivyo, na
sasa yupo hivi..’akasema mkuu wake
‘Kwa mabadiliko
hayo ya ghafla, ndipo sisi kama watu wa usalama tuliweza kumtilia mashaka,
kwani kipindi cha miaka minne huko nyuma, alikuwa na hali mbaya kibiashara na
ghafla akainuka,na ghafla akawa na....’ mkuu akataka kumkatiza, lakini akasita
‘Wateja
hawakuongezeka kihivyo, kuonyesha kuwa biashara imeongezeka, lakini akaanza
kuinuka, tukashangaa anapanua hata makampuni...akaanza hata kujenga mahusiano
makubwa wa serikali, na watu mbali
mbali, akawa anapata zabuni serikalini...na utaona hata alianza kujiingiza
kwenye mambo ya kisiasa akitumia mitandao yake....’akasema
‘Mhh,yawezekana
alibuni mbinu zaidi za kitaalamu, na hizi zabuni si hab ukipata zabuni moja, ni
pesa nyingi, kama una akili ya kibiashara unaweza kupanua biashara zako, lakini
ni pale ukiwa na watendaji wazuri, wenye uzoefu, sasa huyu jamaa kama
mnavyomuona ana akili sana ya kibiashara, kwahiyo hio sio sababu ya msingi au....’akasema
mkuu
‘Mkuu
tulifanya uchunguzi wa kina kwa hilo...utaoa kwenye ushahidi ....’akasema
mpelelezi
‘Sawa naona muda
unakwenda mbio...’akasema mkuu akiangalia saa yake na mwendesha mashitaka akawa
anachukua kumbukumbu zake , na muda mwingi alimuachia mkuu huyo aulize maswali,
kwa vile alishaongea na mpelelezi.
‘Sasa
kukaanza hili wimbi,....ujambazi wa aina yake ukajitokeza, wizi wa benki kwa
aina yake, ufisadi wa hali ya juu, watu wanaiba hadi benki kuu, watu wana weka
pesa nchi za nje kwa wingi, hizi pesa zinapatikana wapi, wakati hali ya nchi
ndio kama unavyoiona....
‘Na
ukichunguza sana hawa watu wanaoweka pesa nje ni watu wa kisiasa, sio
wafanyabiashara, wafanyabiashara inajulikana kwako haina shaka, lakini hawa
watu wa kisiasa, inatia shaka,...tukahisi kuna jambo, tukahisi kuna mtu yupo
nyuma ya haya na lazima awe na utaalamu wa hali ya juu,....’akasema
‘Sawa hilo
tuliliongelea waati ninakua hii kazi, ....’akasema
‘Ndio mkuu,
na unakumbuka kulikuwa na swala la siri za serikali, zikawa zinavuja,
zinavujaje na kuwafikia watu wasiofaa..na zikifika kwa hawa watu wanazitumia
kama biashara....unalifahamu hilo,...tuliliongelea pia....’akasema
‘Kwanini
zivuje,..ni kwasababu siri hizo ziligeuka kuwa ni kuwa ni biashara, swali
likawa hizi siri zimewezaje kutoka na kuwafikia hawa watu,....hili ni swali
lilituumiza sana vichwa....’akaambiwa
‘Ndio maana
nikataka ulichunguze, lakini....lakini haya mauaji, na huku kuvunjika kwa
amani, watu wanalalamika sana, sikujua kuna mahusiano na hili...kwahiyo sasa
tunahitajia ushahidi wa hali ya juu, sio huu tu, mimi haujanitosheleza,..’akasema
‘Ushahidi
upo mkuu, nitakuja kukuelezea, hasa tukianza kuangalia ushahidi huo hatua kwa
hatua,kama utahitaji mkuu.....’akasema
‘Je na huu ufisaidi
wanaukuza hata kuleta sintofahamu kwa wananchi,.....haya ni mambo ya wanasiasa,...’akasema
akiangalia saa yake mara kwa mara
‘Mimi sizani
kama yana uhusiano na hii kesi, mimi naona kwa masilahi ya taifa, tusijiingize
sana hawa watu wa ...na mambo ya kisiasa, unajua tukianza kuwalenga wanasiasa
tunaweza kuanzisha uhasama usio na tija, vinginevyo, unionyeshe mahusiano yake
na hii kesi ...ninasema hivyo nikiwa na maana ,nina kikao na wakuu, na hili
ninaweza kuulizwa, ...’akasema
‘Mkuu, utakuja
kuona mahusiano yake ,....usiwe na shaka mkuu...’akaambiwa
‘Ni
muda...ok,..na , na wizi wa benki ok, huo ni ujambazi tu,..na unasema kuna
kuweka pesa nje , kwenye benki za nje, hawa ni wafayabiashara na kwa utashi wao
huwezi kuwazuia au sio, lakini inapokuja kwa wanasiasa inaleta walakini, sasa
kama wanasiasa wameguka kuwa wafanyabiashara, hii inaleta shida, hili
nitaliongelea na wakuu, ili tuone jinsi gani ya kufanya,......sasa niambie hilo
nalo linahusianaje na hii kesi,...’akatulia
Wakati
mpelelezi anafungua makabrasha yake mkuu akamgeukia muendesha mashitaka
aliyekuwa akiandika andika mambo yake...
‘Eti
muendesha mashitaka,....unajua mimi sijaelewa kitu, unaweza kuoanisha haya mambo
na hii kesi yenyewe, maana huu ni uwanja wako, kama mumeshaongea, ni vyema
ukanifafanulia hata wewe,... bado mnanichanganya....mimi naona tusichanganye
mambo, najua kunaweza kuwa na maingiliano....au mnasemaje?’ akasema na kuuliza
‘Ni sawa mkuu,
lakini kesi ya haya mauaji ina chanzo chake, na chanzo chake ndio hiki anachokuelezea
mpelelezi...., haya mambo yanayotokea, vurugu, migomo,kuchomwa majengo, wizi
sio bahati mbaya....ni mipango iliyosukwa,ni mambo yamepangwa na wajanja ili
ionekane kihivyo inavyoelezewa na hata ku-uwawa kwa huyu mtu, sio bahati mbaya,
mkuu...’akasema
‘Ukiangalia
mfuatano wa haya matukio, utaona ni mpangilio fulani,...na ilitakiwa ionekane
kihivyo, kuwa ni mambo ya kidini hayo, chuki za kidini hizo, au ni mambo ya kikabila, au ni mambo ya
kisiasa tu,.... lakini ndani kwa ndani kuna ajenda ya siri....’akaambiwa
‘Ajenda ya
siri! ni ajenda gani hiyo,....ya siri,...?’ akauliza mkuu akiangalia saa yake,
na mara simu yake ikalia, akaiangalia akaikata .., akasema;
‘Kabla
hujanijibu swali langu la hoja hiyo ya ajenda ya siri, kuna kitu nataka
kufahamu kwako mpelelezi, ...kuna kijana mmoja, sio kijana sana...ni rafiki
mkubwa wa kijana wangu....na wanafanya kazi pamoja..., nilikuambia pia ujaribu
kuangalia nyendo zake, je katika kesi yako anahusika...maana nimesikia kuwa na
yeye tumemshikilia, kwa vipi?’
‘Huyo ni
mmoja wa vijana wetu tuliowatumia,hata bila wao wenyewe kujijua,...na
tumemshikilia kwa madhumuni maalumu, ...’akaambiwa
‘Kuwatumia!....kwa
vipi...mbona hukuwahi kuniambia hilo kabla..’ akauliza kwa mshangao
‘Unajua huyu
jamaa, ni rafiki mkubwa wa kijana wangu, na sikupenda, ...walifikia hata
kugombea msichana..lakini nilimuambia kijana wangu aachane na hilo....wapo
wengi...lakini nikamtilia mashaka ndio maana nikataka umchunguze, ...’akasema
‘Tulifanya
hivyo mkuu, lakini kama nilivyokuambia yeye alikuwa kama chambo....’akatulia
‘Kwa
vipi,...maana mwanzoni ulisema ana uhusiano na huyu mshitakiwa mkuu, ni mlezi
wake,....lakini akaja kumkana, au sio, sasa je alikuwa akishirikiana na huyu
mlezi wake kwa siri kwanini amkane, ....au ilikuwaje mpaka na yeye
tukamshikilia, sipendi hii hali itaonekana imefanyika hivyo kwa vile alikuwa na
uhasama na kijana wangu....’akasema huku akiangalia saa
‘Naona muda
unakwenda, tuahirishe kikao mpaka baadaye, nina kikao na wakubwa au...?’
akauliza mkuu akiangalia saa yake.
NB: Naishia hapa kwa leo
WAZO LA LEO: Kwanini vurugu, kwanini migomo,
kwanini uhasama wa kidini au wa ukabila, haya na mengine yawezekana ikawa ni
mipango ya hali ya juu yenye malengo madhubuti, ya kurejesha ukoloni mambo leo, hayo ni maono yangu,
na mwenye akili ayatizame kwa uwoni wake,
kwanini hayo yatokee sana sehemu zenye maliasili, madini na utajiri wa asili....
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Soon narudi maeneo haya wangu. Acha nianze moja. Nimekumiss saaaaaana
Post a Comment