Ushahidi
ulianza kuonyeshwa hatua kwa hatua....na ikafikia sehemu ya ufafanuzi
‘Kwahiyo kilichoweza
kumfichua huyu mtu ni pale alipoonekana gerezani akimtemtembelea huyu Mtundu....
‘Ndio,....hilo
lilitufanya turejee kesi ya huyu Mtundu, tukajua kuwa huko kwenda kwake
magerezani, kulikuwa na jambo,.. .tukawa tunalichunguza hilo...
‘Je mliweza
kuthibitisha hilo, maana katika maelezo yako ya awali ulisema hawa watu wawili,
yaani mtaalamu na mtundu, walikuja
kukosana na sababu kubwa ni tabia za mtundu ambayo ilikuwa sio sahihi kwa mtaalamu.
Mtaalamu hakupenda mambo yanayokwenda kinyume na elimu yake, sasa ikawaje na
yeye akaelekea hukohuko,...?’ akaulizwa.
‘Mkuu,
hakuna kitu kibaya kama njaa,...mtu ulizoea raha, biashara inaingiza pesa
nyingi, ...halafu unashuka hadi kufikia hatua ya kukosa hata mishahara ya
mwezi,ukumbuke huyu mtu alikuwa na wafanyakazi, wanahitajia mishahara yao,
anatakiwa kulipa kodi nk.....ikafika hawezi kuyamudu hayo yote tena, unafikiri
angelifanya nini
‘Kugundua
utaalamu zaidi, kugundua biashara nyingine, huoni alivyoanzisha miradi mingine
japokuwa hakuwa anaisimamia yeye, lakini yeye ndiye chanzo...’akasema mkuu.
‘Kutokana na
pesa gani, alipatia wapi hiyo mitaji,...hakuna ushahidi kuwa alikopa
mahali....’akasema mpelelezi.
‘Ina maana ndio
....
‘Baada ya yeye
kuonekana gerezani, tulianza kufuatilia kazi zake, watu anaoshirikiana naye...,
tukaanza kuunganisha moja baada ya jingine...ndio tukagundua kuwa yale yale ya
mtundu ndio anayoyafanya huyu jamaa....ila ni kitaalamu zaidi...’akasema
mpelelezi
Tuendelee na
kisa chetu....
**********
‘Jana
nilikuuliza kuhusu huyu kijana , rafiki wa mtoto wangu, ...’akaanza mkuu,
‘Ndio
mkuu...kijana yule anatokea Afrika Mashariki,...historia yake ilikuwa wazi ilionekana
hadi kwenye vyombo vya habari,....kilichowashangaza wengi ni yeye kumkana huyo mlezi wake baadaye....’akasema
‘Kwanini
sasa amkane wakati huyo mlezi ndiye aliyefanya juhudu zote hadi akapata
wadhamini,....na hao wadhamini kuja kumsomesha huku Ulaya...?’ akauliza
‘Hilo pia ni
moja ya jambo lililotufanya liweze kutusaidia kwenye uchunguzi wetu,....na
kiukweli kijana alifanya hivyo, sio ni kutokana na tabia mbaya za mlezi wake,
....bali kulikuwa na sababu nyingine ambayo haikuwa wazi sana....’akasema
‘Huyu,
kijana alikuwa na mahusiano na binti wa yule mama mtemi,na kipindi hicho huyo
mama mtemi alikuwa na uhasama na mshitakiwa mkuu....uhasama wao haukuwa wazi
kwani unahusishwa na mambo ya mlungula,..katika upelelezi wangi ikabidi nimvae
huyu mama, ....huyo mama akaja kuniambia kuwa huyu mshitakiwa mkuu, alijaribu
kumfanyia visa vya mlungula alipomuajiri nyumbani kwake....’akasema
‘Huyu mama
aliweza kuyasema hayo! Kuwa alifanyiwa visa vya mlungula, na je aliweza kusema
ni kitu gani alichomuhusisha nacho ili kumdai pesa za mlungula...?’ akauliza
‘Huyu mama
hakutaka kusema undani wa hilo,...ila sisi kama wapelelezi tulichunguza,
tukagundua hilo,..unajua huyu mama kwa kumbukumbu alipokuwa mmoja wa wahalifu,alikuwa
na machafu mengi, ndio akafikiwa kufungwa...’akasema
‘Hilo
linajulikana,...sawa...tusiende mbali sana kupoteza muda....’akasema mkuu
‘Huyu mama
katika athari za kufungwa alipoteza kizazi,...alipoolewa na huyo mume wake, ...wakataka
kupata mtoto, na mwanzoni huyu mama hakumuambia mumewe kuwa hana kizazi,
ikabidi wahangaike sana, na mume alipogundua hilo, kuwa mkewe hana kizazi, hakutaka
waachane, wakapanga kupata mtoto kwa njia nyingine yoyote ...’akasema
‘Walitumia
mbinu , lakini hizo mbinu hazikuwa wazi,sio halali ..... wakapata huyo binti
walie naye,....’akasema
‘Hazikuwa
wazi kwa vipi?’ akauliza
‘Hakuna
sehemu yoyote inayooyesha kuwa walifuata taratibu sahihi kisheria, ...ina maana
walifanya hayo kwa kificha na isivyo halali,...’akasema
‘Ndio
wakampata huyo binti, ni kiukweli wanampenda sana huyo binti yao, na..hawataki
kabisa huyo binti afahamu kuwa kupatikana kwake sio kwa njia halali...na
hawataki kabisa yeye ajua kuwa huyo baba yake sio baba wa kumzaa.....’akasema
‘Lakini
...’akataka kusema kitu mkuu
‘Wamejitahidi
kulificha hilo, na binti anaamini kabisa hao ni wazazi wake halali, hadi huyu
mshitakiwa alipoweza kugundua nyaraka zinazoonyesha tukio hilo, na kama
anavyofahamika huyu mshitakiwa akipata kisababu kidogo hukitumia kuingiza
pesa,..yeye alipolipata hilo, akaanza kulifanyia kazi, akaweza kwenda hadi kwa
dakitari aliyefanikisha hilo tendo, akapata ushahidi wake,.....’ akasema mpelelezi.
***********
‘Sasa
tukirejea kwa huyu kijana, ...kijana
kampenda binti wa huyu mama, na wakawa marafiki ,na mama mkwe ni adui wa
mshitakiwa, je itakuwaje kwa huyu kijana kupata huyu binti ikiwa yeye ana
mahusian na adui wa mama mkwe.
Kijana
ikabidi aukane ulezi wa huyu baba yake, kuwa hamtambui, kuwa huyo baba
alimtumia tu kama daraja ,lakini jana uhusiano kabisa na huyo baba.
Mama akaona
ndio mwanya wa kumfundisha adabu huyu mshitakiwa...akampa kijana mashartim kama
kweli hana mahusiano na huyo baba mlezi..’akasema
‘Masharti
gani....?’ akauliza
‘Kama kweli
huyu mshitakiwa sio mlezi wake kama alivyodai, basi atafute kila mbinu,...za kufanya
huyo mlezi wake, afungwe....’akasema
‘Kwanini....?’
akauliza kijana
‘Ina maana
hujui, kuwa huyu mtu ni mhalfu...’akaambiwa
‘Kama ni
mhalifu mimi nipo tayari kutoa ushahidi ili afungwe...’akasema kijana
‘Ina maana
hujui kuwa anauza madawa yasiyofaa, kuwa anajishughulisha na biashara ya
mlungula...’akaambiwa na kijana japokuwa alikuwa anafahamu hayo,hakujua kuwa
huyo mama anayafahamu kijana ikabidi akiri kuwa alifahamu lakini hakutaka
kuingilia mambo yasiyomuhusu.
‘Kwasababu
hanihusu mimi sikutaka kumuingilia mambo yake...’akasema
‘Sasa kama
sio mlezi wako, kama huna uchungu naye, kama unataka kujitakasa kuwa wewe ni
msafi , unaweza kuishi na binti yangu nataka utimize masharti
yangu....’akaambiwa
‘Kijana
akakubali....kutoa ushahidi ikiwemo kuwa mlezi huyo alikuwa akiuza madawa
yasiyo halali, na pia anajishughulisha na biashara la mlungula,...
‘Hiyo
haitoshi...ili umuoe binti yangu, nataka huyo mtu ashitakiwa...wewe mwenyewe
uutafute ushahidi halisi, huyu mtu akamatwe kwani hafai katika jamii....’akaambiwa
na mama mkwe.
‘Kwahiyo
kijana akawa akitafuta kila mbinu kumnasa huyu mlezi wake, na kwa vile alikuwa
akifanyia kazi kampuni ya mtaalamu, ....siku moja akamuona baba mlezi akifika
maeneo hayo, kuona hivyo akahisi kuna jambo akatoa taarifa kwa mama mkwe....kuwa
mlezi wake kaonekana akikutana mara kwa mara na mtaalamu
‘Kuna kitu
gani wanajadili, amekuja kuomba kazi...?’ akauliza mama mkwe
‘Sizani kama
nikuomba kazi, na sina uhakika wana jambo gani na huyoo bosi...’kijana akasema
‘Una hisi
bosi wako ana jambo analofanya lisilo halali ?’ akauliza
‘Huwa kuna
mambo yake anayofanya hataki watu wayafahamu, sasa nilimpomuona huyu mtu hapo,
nahisi kuna jambo, nahisi bosi ana mambo ya siyo halali,...’akasema kijana
‘Huwezi
kufahamu ni kazi gani kwa kuchunguza kwenye komputa zake...? akaulizwa
‘Nimechunguzwa
nimeshindwa kujua..lakini nina uhakika kama huyu mtu kaja kwa
mtaalamu kuna
jambo linafanyika...’akasema.
‘Ngoja
nitalifanyia kazi mwenyewe.....’akasema mama mkwe.
‘Sisi
tulishalinasa hilo mapema,...hata wakati kijana anamuambia mama mkwe wake,
Mama mkwe
akamuendea mtaalamu akiwa na lengo lake kichwani...ujue hawa watu hawa
wahaivani, yaani mtaalamu na huyo mama, mama alipofika kwa huyu jamaa, jamaa
akatambua kuna jambo...
‘Nikusaidie
nini mama yangu.....’akamwambia kwa unyenyekevu, na huyo mama hakupoteza muda
akamwambia anachokihisi..
‘Wewe mama
nakuheshimu sana, kwanini unanishutumua kwa mambo hayo machafu.....’akang’aka
mtaalamu
‘Sikushutumu
ila kweli unashirikiana na wahalafu, mimi siwezi kuja kukuambia kitu kama hicho
kama sina ushahidi,....sasa kama unataka nije kulifikisha kwa mbele za sheria,
nikatalie...’akasema huyu mama, mtaalamu ikabidi ampooze huyo mama ...’akasema
‘Kwa
vipi....?’ akauliza
‘Huyu mama
anapenda sana pesa....mtaalamu analifahamu hilo, akamuahidi pesa nyingi pindi
mipango yale ikifanikiwa, hakuambiwa ni mipango gani,.....
‘Huyu mama
hakutaka aonekane kwa watu, kwahiyo alikwena kwa huyo jamaa mara moja, na mambo
mengine yaliyofuata hakuwa anafika yeye kwa mtaalamu......akijua kuwa mtaalamu
ni mjanja, na anajulikana na wakubwa,...na pia hakutaka kuonekana bado yupo na
tabia ile ile ya kudai pesa kwa njia ya milungula, ....’akatulia
‘Sasa
alifanyaje.....?’ akaulizwa
‘Akawa
anamtumia kijana wetu...’akasema
‘Kijana
yupi?’ mkuu akauliza kwa sauti kama ya kushituka
‘Rafiki wa
kijana wako...yaani huyu mtoto aliyemkana mlezi wake...’akasema
‘Kwa vipi,
nakumbuka ulisema kijana huyu pia mlikuwa mkimtumia kwa upelelezi, bila ya yeye
kufahamu....?’ akaulizwa
‘Ndio..tulikuwa
tukimtumia, ....lakini sio moja kwa moja, kuwa anasaidiana na
polisi,...kulikuwa na watu wetu wakimfuatilia, na kupata taarifa kutoka
kwake,....’akasema
‘Ehe,
ikawaje...?’ akaulizwa
‘Na kijana
keshapenda ....kwahiyo akawa tayari kufanya kila kitu atakachotuma na mama mkwe
wake...akawa anatoa taarifa za bosi wake kwa huyu mama, na huyu mama akawa
anadai pesa kwa mtaalamu, ..japo hakutaka ionekana ni njia ile ile ya mlungula....’akasema
‘Mhh, huyu
mama hajaacha tabia yake....’akasema mkuu
‘Mtaalamu
akaona sasa kazungukwa pesa aliyokuwa akiipata kwa njia zisizo halali
imeshaingiwa na mdudu, kuna mtu keshafahamu mipango yake, inabidi afanye mbinu
za kuhakikisha kuwa huyo mama hafahamu dili zake, au amnyamazishe kwa lolote
lile...akaona amtumie huyu huyu mshitakiwa.
‘Kitu
kilichomshangaza ni kwa jinsi gani mambo yake yamegundulikana, na taarifa zake
kufika kwa huyu mama, akawahisi watu wawili, kijana wa huyu mshitakiwa, na
mshitakiwa mwenyewe, ndio akamuhamisha huyo kijana kwenye kitengo kingine,
hakutaka kumfukuza kwani angelifanya hivyo angeonakena ana jamabo,...jamaa ni
mjanja sana....
Hata hivyo huyu
mama naye hakuwa mjinga, akawa
anafuatilia kujua ni dili gani ambayo huyu mtaalamu anaifanya akishirikiana na
marehemu akaja kuigundua, na akampigia simu moja kwa moja mtaalamu na kumwambia
mtaalamu kuwa keshagundua kuwa kuna dili ambayo yeye mtaalamu anashirikiana na
mshitakiwa...’akamwambia
‘Dili gani
wewe mama, unajua mimi nitakushitaki kwa kuniharibia jina langu...’akamwambia.
‘Nitaliharibu keli jina lako, natumai unanitambua nilivyo.....’akasema huyo mama na kukata simu
‘Mtaalamu
anamfahamu huyu mama kuwa anaweza kufanya hivyo, ikabidi afanya mipango ya
kuongea naye, na kumuahidi kuwa atajitahidi ampatie chochote, japokuwa huyu
mtaalamu hakukubali kuwa anashirikiani kwa lolote na mshitakiwa, ila akasema;
‘Mama kama
huyu jamaa ana dilii ni lazima nitaigundua, na nikigundua nitahakikisha unapata
chochote,....mimi siwezi kufanya mambo kama hayo nina kazi zangu za maana, naaminika na
serikali...’akasema
‘Usinifanye
mimi mjinga....najua,...na ole wako, ..unidanganye nitafuatilia hatua kwa
hatua....’akasema huyo mama, na mtaalamu akafahamu huyo mama anaweza kufanya
kweli, ikabidi akili ianze kufanya kazi.
Kama
nilivyosema huyu mama japokuwa litoa vitisho hivyo, lakini hakuwa na malengo ya
kumshitakia mtaalamu, mtaalamu sio adui yake japokuwa hawaelewani sana , adui
yake ni huyu mshitakiwa, lakini kwa vile ana tamaa ya pesa, akaona ni sehemu
nzuri ya kupata pesa huku na huku, ..kutoka kwa mtaalamu na kutoka kwa
mshitakiwa.....’akasema mpelelezi.
‘Ukumbuke
kuwa pamoja na kuwa huyu jamaa ana makampuni, na ni mkurugenzi, lakini makamuni
mengi hayapo kwa jina lake, yeye ni kama muwekezaji wa hisa tu....na kama mpiga
debe wa kuwezesha ajira kwa vijana....lakini kuna hiki kipato kingi alichokuwa
akikipata kwa njia isiyo halali, kutoka kwa watu mbali mbali kwa njia ya
mlungula, lakini sio kwa kupitia yeye, bali kwa kupitia kwa mawakala mbali
mbali,...’akasema mpelelezi.
‘Ina maana
kwa kazi hiyo alikuwa akipata pesa nyingi.....mimi sioni ni pesa nyingi kiasi
cha kumfanya aitegemee.....’akauliza
‘Mkuu, huyu
mtu alishawaweka wakubwa wengi, matajiri wengi, mikononi, anajua shughuli zao
zisizo halali,...na ili zisijulikane ...inabidi watu hao wadaiwe pesa
nyingi....sio kwa moja kwa moja, .. hao watu ilibidi watoe pesa nyingi kuziba
mambo yao,...inategemea ni mtu gani, na anashughuli gani...wengine wana
shughuli kubwa, ...na malipo yake yatakuwa makubwa zaidi.....’akasema
mpelelezi.
‘Huyu mtu
alishaweza kuingiza mambo yake kwenye mitandao ya kibenki, ....anajau jinsi gani
ya kuwaibia watu, kwa kupitia kwenye akaunti zao...akiwatumia mawakala wake,....’akasema
‘Kwa
vipi...?’ akauliza
‘Wewe
unapokea taarifa kwa mtu kuwa yeye ana shughuli, anamtaji, anataka kuwekeza na
wewe,.... umpatia habari hizi na hizi,ili akutimie pesa...wewe usiyejua
unampatia,..hizo hizo taarifa wanazitumia, wanakuibia kwenye akauntii zako za
benki...huu ni mfani mdogo tu,...lakini kwa wakubwa, anatuma ujumbe kuwa
nimegundua kuwa una shughuli hizi na hizi zinakuingizia mabilioni ya pesa...ili
usifikishwe kwa sheria, toa asilimia kumi....
‘Kirahisi tu
hivyo...?’ akauliza
‘Wanatumia
mawakala wao, wanakwenda moja kwa moja kuonana na hawa wakuu, wakiwa na
vielelezo, mkuu, huyu anaona sasa nitaumbuka, anakubali, anatoa pesa....’akasema
‘Haiwezekani,
kirahisi hivyo....’akasema
‘Hujakutana
na hawa watu, wanahakikisha wakimuendea huyo mtu wanakuwa na vielelezo vyote na
ni sahihi kabisa....kama unafanya hivyo, utasemaje....wengine wanajaribu
kupambana, lakini kila wakifanya hivyo, wanagundua ndio wanajiweka hatarini
zaidi, inabidi watoa.....’akasema
‘Ok, lakini
tunazunguka tu...hatujajenga hoja ya kwabana hawa watu, hatujajenga hoja ya
washitakiwa hawa na hasa ukiunganisha na haya mauaji nataka kuwe na hoja ambayo
itawashika hawa watu, maana kama wamefikia kuua, unafikiri itakuwaje, jamii
itatuelewaje,....’akasema mkuu
‘Ndio
tunaelekea huko mkuu, nakuhakikishia hili kundi tutalimaliza, na tatizo hili
litakwisha kabisa hapa maeneo yetu...utaona mwenye mkuu, kwenye ushahidi wetu kila
kitu kipo tayari, .....’akasema mpelelezi, na mkuu akawa kama anawaza jambo,
akasema;
‘Una majina
ya wakubwa waliowahi kupatikana na hizi shutuma.....na ...na hawa vijana
mliwatumia vipi, watasimama mahakamani kutoa ushahidi ?... je ni huyu peke yake
au ni nani mwingine anahusika....?’ akauliza akionekana na mashaka fulani. Na mara simu ya
muendesha mashitaka ikalia, anaipokea na akawa anasikiliza,
Alipomaliza
kusikiliza simu akawageukia wenzake akasema;
‘Mimi naona
mengi tutayaona huko mahakamani....mnaonaje, hii kesi ipo kamili, hakuna
utata...nimeshajitosheleza na huu ushahidi, na kesho kesi inaanza,...kwahiyo
mimi nawasikiliza nyie tu....’akasema muendesha
‘Haiwezekani
kesho kesi ianze, na kama ni lazima ianze nataka uvute muda...usianze moja kwa
moja, uahirishe kuwa bado hatujajitosheleza, kuna mambo bado sijarizika nayo,
kwa masilahi ya taifa..’akasema mkuu.
Muendesha
mashitaka akatabasamu.....
Kesi ikaanza
kesho yake.....
*******
‘Bro mimi....nashindwa kabisa kuamini kuwa
kijana wetu alitumiwa kuniangamiza mimi, na alisimama mahakami kutoa ushahdi
dhidi yangu mimi,...hakuwa na huruma kabisa na mimi....
Hakujali kabisa kuwa mimi ni mzazi
wake, ...hata kama sio baba yake wa kumzaa, lakini mimi ni jamaa yake, mimi
ndiye niliyemtoa hatarini, mimi ndiye....hata hata....’ alisema profesa kwa
uchungu, akimuangalia kaka yake ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini...
Kaka yake akatabasamu.....
NB: Haya
kijana wetu anaanza kuonekana tuone anahusikanaje ni hili janga je ilikuwaje mpaka
baba mlezi amuone huyo mtoto hafai na hataki hata kumsikia.
WAZO LA LEO: Kuwafanyia wenzako ubaya kwa vile tu
hawakuhusu,...ya kuwa sio ndugu zako, sio wenzako, hata wao wakiingia matatani,
hayakuhusu, ilimradi tu,wewe unaneemeka,
unapata masilahi yako, wewe ukijinadi kwa maneno ya kejeli...., ‘mjini
hapa’...utambue kabisa hiyo sio neema, ...huo sio ujanja , hiyo ni dhuluma,
hata kama utapata leo, utashiba, utajijenga, utakuwa kiongozi, lakini ukumbuke hiyo ni dhuluma, na dhambi
hiyo itakuandama maishani mwako hadi kaburini, na hapa duniani ipo siku
utadhalilika tu...
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment