‘Siamini
docta, una uhakika na hivyo vipimo kweli, kwani mimi nilishaambiwa kuwa ni
mgumba...sizai, toka lini mgumba akazaa, nahisi umekosea docta , una uhakika
kweli,’ yule mama akainuka huku akiangalia juu kama anamuangalia muumba wake,
docta akawa anamuangalia kwa mshangao, na kumuambia huyo mama.
‘Nina
uhakika ndio, vipimo vyako vyaonyesha hivyo, na ninani huyo alikuambia kuwa
wewe ni mgumba, je uliwahi kufika hapa ukapima, au ulikwenda hospitali yoyote
kupima ukathibitishiwa hivyo…?’ docta akamuuliza huyo mama, na huyo mama
alikuwa bado kazama kwenye mawazo akiwa kaangalia juu.
‘Mimi
nina mimba...mmh?’ akawa anaongea peke yake
‘Sikia
mpendwa, msipende sana kuamini waganga wa kinyesji au maneno ya mitaani, yasiyo
na vipimo vya uhakika, kutokana na vipimo vyetu, wewe una ujauzito na huenda
imeshapita miezi miwili kadhaa..hebu niambie toka lini ulikoma kuona siku
zako?’ akauliza docta.
Mama
hata hakuelewa docta anamuambia nini, alichomjibu ni kuwa hakumbuki , maana
siku zake zinaweza kukata hata miezi mwili akazipata tena mfulululizo, kwahiyo
hata hakumbuki lini alikosa siku zake.
Alitoka
hapo hospitalini akiwa na raha ya ajabu, mgumba kupata mtoto, na kwa jinsi
alivyotekwa na hiy raha, akawa kasahau kuwa kaja hapo hospitalini kwa
kujificha, moyoni akapanga akitoka hapo anakwenda kumpa mume wake habari nzuri,
na akapanga apitie sokoni kununua kile chakula mume wake anachokipenda...
Lifti
ya baiskeli ikamponza, kumbe watu walishamuambia mume wake kuwa mke wake
anatembea na rafiki yake mkuu, na kila huyo hupita hapo nyumbani kwake akiwa
keshaondoka,....na mkewe alipopewa lift ya baiskeli na huyo rafiki mtu,hadi
nyumbani, mumewe akawaona, mume wake akahisi kuwa huenda kauli za watu ni za
kweli...
Mara
mkewe anamwambia kuwa kaja na habari nzuri, habari gani hiyo, wakati kichwani
ana mawazo mengi, kuwa yeye hatazaa mpaka akamilishe mambo ya mizimu, na mimba ya kwanza ataipata kutoka kwa mke wake
mdogo, na mkewe mkubwa ugumba wake utakoma pale mkewe mdogo atakaposhika
mimba...., kwahiyo kama ni kuzaa kwanza atazaa na mke mdogo....
‘Mume
wangu hayo ni maneno ya watu, nakuhakikishia mimi siwezi kusaliti ndoa yangu
hata siku moja, sijui nani kakudanganya, ila nina habari nzuri nataka
kukuambia, ….’akasema na mume wake akageuka akiwa kakunja uso, akisubiri
Akatulia
kusikiliza hiyo habari nzuri...labda ndio hiyo kuwa akitembea na mkewe mdogo,
baada ya kukamilisha masharti, itakuwa ni nafasi ya kusafisha nuksi ya yeye
kuwa mgumba, kwani na yeye atashika mimba,...lakini hiyo ya kuwa tasa kama
masharti yatavunja ilimpa shida sana, hakutaka kumwambia hayo kabisa mkewe
kabla...alichokuwa kamsihi ni kuwa asije kwenda hospitalini
Lakini
dunia haina siri kama mke mdogo alikwenda kwa mganga na yeye akaambiwa hivyo,
ina maana kuna ukweli...lakini mkewe amekuja kwa habari gani anayoiita ni
nzuri..., akasubiria kuisikia hiyo habari nzuri..
Tuendelee na kisa
chetu....
***********
‘Mume wangu, nataka
kukufahamisha kuwa mimi ni mja mzito, nina mimba mume wangu, hatimaye mungu
katusikia duwa yetu nina mimba mume wangu, docta anakuta……’akasema kwa furaha.
‘Docta ina maana ulikwenda
hospitalini kupima...umeamua kwenda hospitalini , umevunja miiko ya mganga...?’
akauliza mume wangu kwa hasira
‘Mume wangu siku kadhaa
nimekuwa nikiumwa, na sioni tatizo ni nini, nimetumia dawa za miti shamba
nimeona hazisaidiii, ndio nikaona nipitie mata moja nipime, kumbe ni bahati
yetu, docta kagundua nina mimba, kama nisingeenda huenda, tungeiharibu kwa
madawa yasiyofaa...’akasema mama.
‘Madawa yasiyofaa,
unayaita madawa ya kimila yasiyofaa, wakati wazee na mababu zetu ndio walikuwa
wakitumia, dawa ambazo zingekusaidia kuondoa huo ugumba wako,...sasa unakuja na
uwongo...au ...kwanza, niambie hiyo mimba kakupa nani.....’akasema kwa hasira.
‘Mume wangu ni nani
wakunipa mimba zaidi yako wewe mume wangu, ni kauli gani hiyo , mimi simjui
mume mwingine zaidi yako, na siwezi kuvunja miiko ya ndoa yetu...’akasema mama
akionyesha mshangao usoni
Mume mtu hasira alikunja
uso kwa hasira, tofauti na alivyotarajia mama, taarifa ya furaha kwake iligeuka kuwa taarifa
ya kumpandisha baba hasira mama akabakia kaduwaa,
Baba mtu, alikuwa na mengi
kichwani, siku hiyo alipoamuka alijizuia kabisa kuongea, alikuwa na mambo yake
mengine, hakutaka kabisa kugombana na mtu, lakini kauli hiyo ya mke wake
ikabadili kila kitu, akarejeshewa hasira zake ,mwili ukaanza kutetemeka mikono
iliyokuwa inawasha kupiga ikatuna kama ya muinua vyuma...mama akaanza kuhisi
wasiwasi.
Akili yake ilikuwa
inashindana, kauli ya mganga wake na kauli hiyo mpya kutoka kwa mke wake, na
kauli za watu wa mitaani.
Alipokwenda kwa mganga wa kienyeji,
mganga anayemuamini sana, mganga huyo alimuambia kuwa kuzaa kwake kuna msharti,
kwanza mkewe asiende kuchanganya madawa yakwake na hospitalini ikiwa na pamoja
na kupigwa sindano kwake ni mwiko mpaka tambiko lipite
kupima, au kupigwa sindano
za hospitalini, pili,ugumba wa mkewe unatokana na mizimu, utaondoka tu pale mke
wake mdogo atakaposhika mimba, akajaribu kukumbuka mazungumzo yake na huyo
mganga....
‘Kwahiyo
mke wangu mkubwa sio mgumba kama ulivyosema awali?’ alimuuliza mganga wa
kienyeji.
‘Mke
wako mkubwa ana ugumba ndi-ndio.....lakini nilikuambia hili nitalifanyia kazi,
na nimeshalifanyia kazi, lakini ukumbuke kuwa ugumba wake unatokana na mizimu, na kwa vile ni kwa kimzimu, unaweza kuondoka kwa
matambiko, siku zila ulipoondoka nilifanya makafara mengi, ila kwa sasa msharti
yaliyobakia ndio hayo...
‘Sharti
muhimu ni tufanye matambiko ya kumwaga damu wa ngombe, na baada ya hapo,
ukutane na mkeo mdogo, ambaye atashika mimba, mimba hiyo itaondoa nuksi ya mkeo
mkubwa, ...na itaondoa nuksi mwilini mwako, kwahiyo ukienda kukutana na mkeo
mkubwa atashika mimba, na utakuwa mwisho wa ugumba wake.
‘Sijakuelewa
hapo,...ina maana mke wangu mkubwa sio mgumba wa kuwa hana kizazi, ndilo swali
langu ninalokuuliza mwanzoni ulisema kabisa ni mgumba, hana kizazi, au mimi
sikuelewa vyema?’ akauliza tena.
‘Ugumba
mwingine ni wa kimizumu, usipotimiza masharti unabakia hivyo hivyo..hatazaa
abadani mkiwa naye,yeye alikuja na nuski yake ambayo inafanya damu zenu
kukataana, ...’akaambiwa.
‘Unataka
kusema kuwa, mke wangu kama atakwenda nje ya ndoa akakutana na mwaname mwingine
anaweza kuzaa?’ akauliza
‘Anaweza
kama hiyo nuksi hataitamwingia huyo mwanaume mwingine, kutegemeana na nguvu za
mizimu ya huyo mwanaume mwingine..hayo ni mambo ya kimila zaidi, unajua kuna mambo
mengina hutokea nyie mkaona ni ya kawida tu kumbe kuna mazindiko,....mambo ya
kimila yanasababisha hayo..’ akaambiwa.
‘Kama
ni ya kwetu huyu mwanamke atahusikanaje na kusema kanipa nuksi..?’ akauliza
‘Nielewe
hapo, ulipomua huyo mwanamke kuna mambo ulitakiwa ufanye, uliambiwa na wazee
wako, hukuwahi kuambiwa hivyo, ukapuuza, sasa mizimu ikaona ikuonyeshe kwa
kupitia kwa huyo mwanamke....ni mambo ya ndani sana, cha muhimu sasa timiza
hili sharti la ng’ombe...’akaambiwa.
‘Kwa
hivi sasa, mkeo mkubwa akitembea na mtu mwingine, anaweza kushika mimba,
lakini sio kwako, njia yake
imeshasafishika, ilibakikia kwako,..kwako ni mpaka utoe tambiko,uzae na mke
mdogo, ukivunja hilo wewe unakuwa tasa...hutazaa tena...’
‘Mimi
nitakuwa tasa...ina maana huyu mwanamke kaniharibia maisha yangu....’akawa
anawaza
Na wakati anarudi kutoka
kwa mganga, mara akasikia uvumi kuwa mkewe anaonekana mara nyingi akiwa na rafiki yake, rafiki yake
ambaye wameshibana, aliyesimamia ndoa yake, na kuna watu wengine walimwambia
kuwa wameshaona na dalili zote kuwa hao watu ni wapenzi wa siri...
‘Mkeo anatafuta mimba ya
siri, ili aje akusingizie wewe....’akaambiwa
‘Kwani nani kawaambia kuwa
mimi sizai...mimi ni rijali ninaweza kuzaa, tatizo ni huyu mke...lakini
nitalimaliza,...huyu mke mkubwa ndiye ana mkosi...., ngoja nitachunguza kama ni
kweli, atanitambua kuwa mimi ni nani...’akasema aliposikia hayo maneno kutoka
kwa watu.
‘Kama unabisha muulize mke
wako mdogo, kwani yeye alipokwenda kwao yeye na wazazi wake walikwenda kwa
mganga wakaambiwa kikwazo ni mke wako mkubwa, mke wako mkubwa ana nuksi, ona
tangu umuoe, mali yako inavyopungua, huzai na sasa keshagundua kuwa akitembea
na mwanaume mwingine atazaa, wewe bado umelala tu....’akaambiwa na watu hao.
‘Hata mimi nalifahamu
hilo, ila, hilo la rafiki yangu kutembea naye, sijaliafiki mpaka nione
mwenyewe, nitachunguza na kama ni uongo na nyie nitawafanyizia ubaya ambao
hamjawahi kufanyiwa, msipende kuniingilia maisha yangu.....’akasema.
‘Utakuja kuliona wewe
mwenyewe kwa macho yako, wewe rudi mapema nyumbani utawafuma, utakuja
kutushukuru..’akaambiwa.
‘Nitampata wapi ng’ombe
mweusi asiye na doa...’akawa anajiuliza akilini kwani mganga wake alimwambia
atafute ng’ombe mweusi asiye na doa hata moja, hakutaka kukaribisha hasira
zake, kwani ana jukumu hilo la kufanya kama ni kweli atakuja kugundua mwenyewe,
lakini...akichelewa, ...ooh,
‘Ngombe mweusi....’akawa
akiuliza kwa watu wanaofuga ng’ombe lakini ikawa ngumu kumpata kwani kila ng’ombe
mweusi anayepatikana anakua na baka ama jeupe au la rangi nyingine,na ng’ombe
huyo hatakiwi kuwa na baka la rangi nyingine yoyote...
Katika kuhangaika ndipo
akakutana na mtu akamwambia ngombe kama hao wameonekana kijiji cha jirani...
‘Oho basi nitakwenda
kumtafuta kesho...’akasema, kwahiyo alishapanga kuwa kesho yake anakwenda huko
kijiji cha jirani, sasa huyu mkewe anakuja na taarifa hiyo kuwa ana mimba,...
‘Mke wangu ana mimba, kama
ni kweli, basi hiyo mimba sio yake, kama sio yake,kaipatia wapi,...ina maana ni
kweli kuwa anatembea na rafiki yake, ina kweli keshatembea na rafiki yake, na
kupata mimba, kwahiyo yeye sasa ni tasa, kwa vile keshaharibu tambiko hataweza
kuzaa tena, hata akipta huyo ng’ombe ni kazi bure...’ akili hapo ikazidi kuwaka
moto.
Akageuka huku na kule kwa
hasira kama anatafuta kifaa, kitu..lakini hakuona hicho kitu, akaanza
kumsogelea mkewe akiwa keshabadilika uso ukawa umejaa hasira za kuua, ‘Ina
maana mke wake keshamfanya yeye sasa awe tasa,....’ akawa anamsogelea mkewe
huku akinguruma kihasira
Kabla hajamkaribia mkewe
kwa kasi ya jabu akarusha makofi mawili ya haraka haraka vya nguvu.
Mkewe hakutarajia hiyo
hali na vibao vile vililenga usoni, mkewe akajiona anaona vinyota mbele yake,
akabaki kaduwaa, hakuweza hata kupiga ukelele wa kuomba msaada, hakutarajia
hayo...ina maana taarifa njema imegauka kuwa balaa....
‘Utaniambia kuwa hiyo
mimba ni ya nani…’ alisikia vibao vikiongezeka usoni, mara ngumi mateke
yakiingia mwilini na hakujua ni vipigo vingapii alivipata kwani giza
lilishaanza kutanda usoni....akaondoka chini.
‘Mimi niliambiwa na
mtaalamu siwezi kuzaa mpaka nimalize matambiko, na matambiko sijayafanya
umepata mimba,...kwahiyo umetaka mimi niwe tasa, kwa vile nimeoa mke mwingine,si
ndivyo unavyotaka ndio maana ukasema nioe hata mwingine ukijua umeshaniweza
mimi sitazaa tena, ndio lengo lako sio,sasa...utaniambia hiyo mimba ni ya nani...’hakujali
kuwa mkewe kadondoka chini akazidi kusindilia mateke
‘Hata ukifa sina
hasara,..ila kabla hujafa, nataka unieleze hiyo mimba niya nani, halafu ufe
ukazalie huko kuzimu....mchawi mkubwa wewe...hutaki kusema sio ngoja...’
akachukua rungu lilokuwa mle ndani akataka kumbamiza mkewe.
Kwa bahati nzuri mlango
ukagongwa na aliposikia hivyo akalirudisha like rungu lake ambalo hukaa humo
ndani kwa ajili ya usalama. Aliogopa kama ni mgeni wa heshima isije ikawa
dhahama na ukapatikana ushahidi kuwa kumbe kweli yeye ana mpiga mkewe mara kwa
mara,...na rungu, kitu alichokipinga kwa
wazee walipokaa kikao, akalitupa lile rungu pembeni .
Akageuka na kwenda
mlangoni kuangalia ni nani aliyegonga mlango, kutupa macho anamuona aliyegonga
mlango kumbe ni yule yule mbaya wake, aliyekuwa rafiki yake lakini sasa kawa ni
adui yake.
Kwanza alitabasamu, akatikisa
kichwa kama kukubali, akageuka kuangalia ukutani, alipolitupa lile rungu lake,
huku mwili ukisisimka kwa hasira, akijua kuwa mbaya wake kajileta mwenyewe, moyoni
akawa anasema huyu hyu ataniambia ukweli kuhusu hiyo mimba.
‘Eheee, naona umejileta
mwenyewe, kama ulijua vile, au ulifika ukijua nimeshaondoka, hahaha, karibu
sana rafiki ...hahaha rafiki, natamani nisitamke hilo neno...karibu....badi
nipo,sijaondoka....’akasema na rafiki yake bila kujua, akaingia ndani
Alipoingia ndani akahisi
hali sio shwari, akatupa macho, akamuona shemeji kalala sakafuni.
‘Mbo-mbona hivyo rafiki
yangu....?’ akawa anashangaa huyo rafiki yake.
‘Njoo, sogea huku nifunge
mlango, rafiki..rafikiiii rafiki eeh, hahaha, rafiki mpaka kwenye mke wangu,
kwa vile umesimamia ndoa yangu ndio unataka uhakikishe kuwa kweli mke wangu
hazai au sio...mitindo ya kupata mtoto wa kike, wa kiume yote unaifahamu wewe
au sio, sasa huyu....’akaonyeshea kule alipolala mkewe, kuna kitu kikamfanya
ashituke, mbona mkewe tangua adondeke pale chini hajajisogeza,..lakini akajipa
moyo kuwa anajifanyiza tu ili asiendelee kupata kipigi, akamgeukia rafiki yake
na kusema
‘Imemuona mwenzako, hebu
niambie hiyo mimba ni ya mtoto wa kike au wa kiume....?’ akauliza
‘Mbna sikuelewi rafiki
yangu, ulisema mke wako hawezi kubeba mimba mpaka umalize matambiko, na mimi
nimekuja kukuambia kuwa nimemuona huyo ng’ombe kwa jamaa mmoja,...’akasema
rafiki yake.
‘Ng’ombe, ng’ombe wa nini
tena wakati wewe mtaalamu umeshafanya vitu vyako...je huyu atakuwa wa kiume au
wa kike jibu swali langu...’akasema huku akiwa kamshikilia mkono kama vile
hataki amponyoke.
‘Hebu acha utani rafiki
yangu....hayo yanakutoka ukiwa umelewa au bado upo sawa sawa..ni mimi wa
kuniambia mambo hayo...?’ akauliza
‘Hahaha, hebu uniambie mke
wangu na wa kwako ni nani mnzuri zaidi, wewe si unajisifia kuwa mke wako ni
mnzuri kuliko wote hapa kijijini, sasa mke wangu kashinda nini mpaka umtake,
mpaka muwe wapenzi, na zaidi umeshampa mimba....’akasema
Rafiki yake akabakia na
mshangao.....akawa anashindwa hata kusema neno, akawa anatafuta mwanya wa
kujiondoa mikononi mwa huyo rafiki yake kwani anajua shari zake, na akianza
jambo lake haliishi mpaka utokee ugomvi.
‘Sikiliza ....rafiki
yangu...’akasema
‘Sasa ni hivi nimeshayajua
yote, kuwa wewe kuja kwako hapa si bure, unatumia mgongo wa urafiki wetu
kufanya mambo yako... sasa kwa vile umemuona mke wangu ni mzuri zaidi ya mke
wako, mchukue,....huyo hapo...anajifanya kazimia...na bado..mpaka sura
ichujuke...’akasema
‘Yaani ndio umempiga kiasi
hicho kwa maneno tu ya mitaani..., ...siamini..mimi nilijua labda huyo mganga
ndiye kakuambia hivyo...jaribu kuwa na subira utagundua kuwa sio kweli ni
uzushi tu...’akasema rafiki yake
‘Huamini, eeh, muda ule nilipokuona
umembeba mke wangu na baiskeli mlitoka wapi...si mpenzi wako, una cha
kutembelea, hivi ungelikuwa na gari si ungemaliza wanawake wote wa hapa
kijijini, baiskeli tu , una...kwanza tuache hayo,...mimi nataka tuyamalize haya
kimiya kimya,...wewe siumeona ni mzuri kwako, unakumbuka mahari nilitoa kiasi
gani..zilikuwa ng’ombe ngapi vile...?’ akawa kama anauliza
‘Sikiliza rafiki yangu,
tuliza munkari, hizo ni hasira na ibilisi keshakutawala, na kama unafanya
utani, ujue huo sio utani mzuri, usije ukafanya jambo ambalo utakuja
kujijutia...’akasema rafiki yake
‘Yah, zilikuwa ni ng’ombe
tisa, na yule wa kufunga uchumba wa kumi...unakumbuka wewe mwenyewe ulinisifia
kuwa ni mke mnzuri mweupe kwahiy ng’ombe hizo ni halali, eeh, kumbe na wewe
ulikuwa ukimmezea mate, sasa umewahi....hahaha kweli umewahi, maana
umaniweza...lakini hujaniweza...ulichofanya utakuja kukilipa...’akasema huku
akitikisa kichwa.
‘Unajua mimi sijakuelewa,
kilichonileta hapa ni kingine kabisa,nimekuja kwa habari nzuri, kuwa...’akasema
lakini mwenzake hakutaka kumpa nafasi.
‘Nataka ng’ombe zangu, mke
ni wako, huyo hapo, mimi sina haja naye,...nirejeshee mahari yangu yote...hapo
tutaelewana, vinginevyo tutaonana wabayaaaa...’akashika kichwa na kijikuna kama
nywele zinawasha na kwa kufanya vile akawa kamuachia mwenzake mikono, na
mwenzake akasogea mbali na yeye
Mwenzake akawa kasimama
akiwa ana mshangao wa ajabu , hakuamini hayo maneno yanatoka mdomoni kwa rafiki
yake ni ya kweli au anafanya mzaha, lakini sio mzaha, maana hali ya shemeji
pale chini sio nzuri.....
‘Unashangaa nini, ulijua
siwezi kuyatambua mambo yenueeh, unakuja hapa kwa tiketi ya urafiki, kuja
kumuonyesha mke wangu mitindo yako eeh, maana wewe unajiita docta wa mapenzi,
au sio…hahaha, basi mimi ni docta wa kuwatengeneza watu kama nyie...’ akawa anaongea
huku anatikisa kichwa chake huku na kule.
‘Rafiki yangu unajua mpaka
sasa hivi sijakuelewa, yale ni mazungumzo yetu tu...mitindo, sijui nini, ni
kawaiuda yetu kuongea tu....siwezi kuja kukufanyia hapo kwa ...hapana nahisi
unatania, ..wewe ni sawa na ndugu yangu, siwezi na shemeji namuheshimu
sana...yeye na mke wangu ni marafiki wakubwa....’akasema sasa kujitetea
‘Mhhh mke wako eeh, kama
yeye unaweza kumdanganya lakini sio mimi, ..kichwa hiki kimekwenda shule ya
asili, kinajua ya siri na ya dhahiri...’
Akasema sasa akiwa kashika
kiuno, hiyo ni ishara ya shari, anamfahamu sana huyo rafiki yake akishika
kiuno, kinachofuata hapa na vurugu, litarushwa teke au ngumi….
Rafiki mtu akabakiwa
kaduwaa, akishangaa, na kwa vile anamjua rafiki yake, akanyamaza kimya, akijua
leo kuna mambo, na huenda asiondoke hapo salama. Alikaa kimya kusikiliza
shutuma ambazo hakujua zimetokea wapi, akatulia kusikiliza, halafu alipoona
rafiki yake kanyamaza, akaanza kusalimia....
‘Habari yako rafiki yangu,
tuyaache hayo ya waosha vinywa mitaani kwanza pokea habari hiyo njema kuwa
nimeshapata ng’ombe uliyekuwa ukimtafuta, kwahiyo hata sasa hivi tunaweza kwenda kumchukua...!’akasalimia, lakini akaona
jamaa akiwa kama anawashwa, hatulii.
‘Rafiki yangu eeh, mimi ni
rafiki yako wewe...mnafiki mkubwa wewe...’hilo jibu likamfanya mwenzake abakiwa
mdomo wazi.
‘Kwanii vipi, ina maana
unachukulia vile nilivyomleta shemeji na baiskeli, kwani hiyo ni mara ya
kwanza, mara ngapi nafanya hivyo na wewe unaona, yote hayo ni maneno ya fitina
yametungwa kutuchonganisha, ....rafiki yangu kumbuka mimi na wewe ni kama
ndugu, tumeshibani usije kusikia majungu ukaharibu udugu wetu...’akasema
mwenzake.
‘Ni nani kakuambia
nimesikia majungu na kama sio kujihami huko.....je tumeshakubaliana, tunaondka
hapa mguu kwa mguu, unanihesabia ng’ombe mahari yangu nakuachia mke...vingnevyo
kijiji kizima kitajua kuwa umetembea na mke wangu,kabla hajazaa............’akasema
‘Hapo sasa naona unataka
kuharibu urafiki wetu kama kweli unaamini hayo, naona umefika mbali...’akasema
alipoona mwenzake hatanii.
‘Kama kweli wewe ni rafki
yangu, ...tuyamalize haya kimiya kimiya kama mlivyofanya na mke wangu kimiya
kimiya...tunakubaliana, nyie si mnataka mimi niwe tasa...na kama kweli nitakuwa
hivyo, na wewe nitamaliza nitahakikiahs huna uume,...’akasema
‘Eti nini....’rafiki yake
akasema
‘Hilo ni la baadaye,
kwanza tukubaliane hili, mke wako huyu hapo..nipe mahari yangu, sitaki
kashifa...tumeelewana...’akasema sasa akimsogea rafiki yake, na rafiki yake
akawa sasa anarudi kinyume nyume keshajua mwenzake kazamairia ubaya.
Rafiki yake huyo akajua huyu jamaa kayaamini
hayo na huenda keshampiga mkewe na hata kumuua, kwani tangu aiingie hapo hajaona
shemeji akitikisika, akajua huyo jamaa huenda ameshaua,, na sasa anatafuta
visingizio,akaona kwanza atumie busara yake ya mwisho.
‘Vipi rafiki yangu kwani
kuna jambo gani, naona shemeji anavuja damu yupo sakafuni, hatikisiki, anaonekana
hayupo salama, hebu tumuangalie kwanza , usije ukawa umemuumiza,....’akasema
akiendelea kumuangalia shemeji yake pale chini.
‘Kwa vile ni mpenzi wako
ndio unamuonea huruma au sio...unajifanya hujui chanzo ni nini au sio eeh,..sogea
pale kamuangalia vyema mpenzi wako, na hiyo ndio dawa ya wasaliti wa ndoa...na
wewe zamu yako bado, kwanza tunakubaliana hapa ngombe wangapi, tisa, huyo wa
kumi hakuhusu sana...’akasema rafki yake akasogea na kulichukua rungu lake, na
kumsogelea rafiki yake wakawa sasa wamesimama sambamba.
Jamaa kuona hivyo, akaona humo
hakukaliki, yeye alikuja kwa taarifa nzuri kuwa kaona ng’ombe mweusi kwa jamaa
yao mmoja, na hilo linaweza kumfurahisha rafiki yake, lakini anachokikuta hapo
ni tofauti, na alitamani atoke humo ndani haraka, kwani mkewe anamsubiria kuna
sehemu wanakwenda, lakini yeye aliona rafiki yake ni muhimu kwanza...
‘Ina maana mimi nimeacha
shughuli zangu kwa ajili ya kujali urafiki wetu, nimefanya makosa, ndio haya
yamekuwa hivi, kama ni hivyo,mimi naona hapa hakuna amani, ngoja nijiondokee
zangu tu , samahani naomba nitoke....’akasema akigeuka kuondoka, ikawa kosa.
Ilikuwa ni Bahati tu,kwani
aliinama kufungua kitasa cha mlango, na ndicho kilichomsadia, kwani rungu
lilikuwa lipasue kichwa likagonga kwenye bega upande wa nyuma.
‘Khaa, rafiki yangu
vipi...’akasema na kabla hajageuka vyema, alishitukia teke, na rungu la pili likimkosa
kosa tena, kwani kwa muda huo alishageuka kiaina kujihami, akaona sasa hana hiari ni mapambano
tu, kwani mwenzake inavyoonekana kadhamiria kumuua!
**********
NB Mafahali wawili
wanapambana, chanzo ni nini, na ni nini hatima yake,tuzidi kuwemo…
WAZO LA LEO:. Ushirikiana ni mpana sana, wenye
nia ya kuondoa imani halisi ya kumujua
mungu wa kweli, imani ya amani na upendo. Watu kutokana na shida zao hujikuta
wakihadaiwa na kusahau kabisa imani halisi yenye kumpwekesha mungu, imani ya
kujua kuwa watu wote ni kitu kimoja, wametokana na asili moja, imani hiyo
huondolewa nyoyoni.
Watu wanajikuta wakiingia kwenye imani nyingine ambazo zinawahadaa
watu kuwa kuna nguvu nyingine , nguvu za ziada,zenye kuponya , kuleta utajiri,
nk. Kutokana na shida, umasikini, na imani haba, elimu ndogo ya imani sahihi ya
mungu mmoja, watu wanakubali na kuukumbatia ushirikina, na huko hujengewa imani
za chuki, ubinafsi, na matokea yake, ndugu na ndugu, marafiki nk wanaanza kufarakana.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159
Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159
Post a Comment