Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, December 22, 2014

NANI KAMA MAMA-11


‘Siamini docta, una uhakika na hivyo vipimo kweli, kwani mimi nilishaambiwa kuwa ni mgumba...sizai, toka lini mgumba akazaa, nahisi umekosea docta , una uhakika kweli,’ yule mama akainuka huku akiangalia juu kama anamuangalia muumba wake, docta akawa anamuangalia kwa mshangao, na kumuambia huyo mama.

‘Nina uhakika ndio, vipimo vyako vyaonyesha hivyo, na ninani huyo alikuambia kuwa wewe ni mgumba, je uliwahi kufika hapa ukapima, au ulikwenda hospitali yoyote kupima ukathibitishiwa hivyo…?’ docta akamuuliza huyo mama, na huyo mama alikuwa bado kazama kwenye mawazo akiwa kaangalia juu.

‘Mimi nina mimba...mmh?’ akawa anaongea peke yake

‘Sikia mpendwa, msipende sana kuamini waganga wa kinyesji au maneno ya mitaani, yasiyo na vipimo vya uhakika, kutokana na vipimo vyetu, wewe una ujauzito na huenda imeshapita miezi miwili kadhaa..hebu niambie toka lini ulikoma kuona siku zako?’ akauliza docta.

Mama hata hakuelewa docta anamuambia nini, alichomjibu ni kuwa hakumbuki , maana siku zake zinaweza kukata hata miezi mwili akazipata tena mfulululizo, kwahiyo hata hakumbuki lini alikosa siku zake.

Alitoka hapo hospitalini akiwa na raha ya ajabu, mgumba kupata mtoto, na kwa jinsi alivyotekwa na hiy raha, akawa kasahau kuwa kaja hapo hospitalini kwa kujificha, moyoni akapanga akitoka hapo anakwenda kumpa mume wake habari nzuri, na akapanga apitie sokoni kununua kile chakula mume wake anachokipenda...

Lifti ya baiskeli ikamponza, kumbe watu walishamuambia mume wake kuwa mke wake anatembea na rafiki yake mkuu, na kila huyo hupita hapo nyumbani kwake akiwa keshaondoka,....na mkewe alipopewa lift ya baiskeli na huyo rafiki mtu,hadi nyumbani, mumewe akawaona, mume wake akahisi kuwa huenda kauli za watu ni za kweli...

Mara mkewe anamwambia kuwa kaja na habari nzuri, habari gani hiyo, wakati kichwani ana mawazo mengi, kuwa yeye hatazaa mpaka akamilishe mambo ya mizimu, na  mimba ya kwanza ataipata kutoka kwa mke wake mdogo, na mkewe mkubwa ugumba wake utakoma pale mkewe mdogo atakaposhika mimba...., kwahiyo kama ni kuzaa kwanza atazaa na mke mdogo....


‘Mume wangu hayo ni maneno ya watu, nakuhakikishia mimi siwezi kusaliti ndoa yangu hata siku moja, sijui nani kakudanganya, ila nina habari nzuri nataka kukuambia, ….’akasema na mume wake akageuka akiwa kakunja uso, akisubiri


Akatulia kusikiliza hiyo habari nzuri...labda ndio hiyo kuwa akitembea na mkewe mdogo, baada ya kukamilisha masharti, itakuwa ni nafasi ya kusafisha nuksi ya yeye kuwa mgumba, kwani na yeye atashika mimba,...lakini hiyo ya kuwa tasa kama masharti yatavunja ilimpa shida sana, hakutaka kumwambia hayo kabisa mkewe kabla...alichokuwa kamsihi ni kuwa asije kwenda hospitalini

Lakini dunia haina siri kama mke mdogo alikwenda kwa mganga na yeye akaambiwa hivyo, ina maana kuna ukweli...lakini mkewe amekuja kwa habari gani anayoiita ni nzuri..., akasubiria kuisikia hiyo habari nzuri..

Tuendelee na kisa chetu....

***********
‘Mume wangu, nataka kukufahamisha kuwa mimi ni mja mzito, nina mimba mume wangu, hatimaye mungu katusikia duwa yetu nina mimba mume wangu, docta anakuta……’akasema kwa furaha.
‘Docta ina maana ulikwenda hospitalini kupima...umeamua kwenda hospitalini , umevunja miiko ya mganga...?’ akauliza mume wangu kwa hasira

‘Mume wangu siku kadhaa nimekuwa nikiumwa, na sioni tatizo ni nini, nimetumia dawa za miti shamba nimeona hazisaidiii, ndio nikaona nipitie mata moja nipime, kumbe ni bahati yetu, docta kagundua nina mimba, kama nisingeenda huenda, tungeiharibu kwa madawa yasiyofaa...’akasema mama.

‘Madawa yasiyofaa, unayaita madawa ya kimila yasiyofaa, wakati wazee na mababu zetu ndio walikuwa wakitumia, dawa ambazo zingekusaidia kuondoa huo ugumba wako,...sasa unakuja na uwongo...au ...kwanza, niambie hiyo mimba kakupa nani.....’akasema kwa hasira.

‘Mume wangu ni nani wakunipa mimba zaidi yako wewe mume wangu, ni kauli gani hiyo , mimi simjui mume mwingine zaidi yako, na siwezi kuvunja miiko ya ndoa yetu...’akasema mama akionyesha mshangao usoni


Mume mtu hasira alikunja uso kwa hasira, tofauti na alivyotarajia mama,  taarifa ya furaha kwake iligeuka kuwa taarifa ya kumpandisha baba hasira mama akabakia kaduwaa,

Baba mtu, alikuwa na mengi kichwani, siku hiyo alipoamuka alijizuia kabisa kuongea, alikuwa na mambo yake mengine, hakutaka kabisa kugombana na mtu, lakini kauli hiyo ya mke wake ikabadili kila kitu, akarejeshewa hasira zake ,mwili ukaanza kutetemeka mikono iliyokuwa inawasha kupiga ikatuna kama ya muinua vyuma...mama akaanza kuhisi wasiwasi.

Akili yake ilikuwa inashindana, kauli ya mganga wake na kauli hiyo mpya kutoka kwa mke wake, na kauli za watu wa mitaani.

Alipokwenda kwa mganga wa kienyeji, mganga anayemuamini sana, mganga huyo alimuambia kuwa kuzaa kwake kuna msharti, kwanza mkewe asiende kuchanganya madawa yakwake na hospitalini ikiwa na pamoja na kupigwa sindano kwake ni mwiko mpaka tambiko lipite

kupima, au kupigwa sindano za hospitalini, pili,ugumba wa mkewe unatokana na mizimu, utaondoka tu pale mke wake mdogo atakaposhika mimba, akajaribu kukumbuka mazungumzo yake na huyo mganga....

‘Kwahiyo mke wangu mkubwa sio mgumba kama ulivyosema awali?’ alimuuliza mganga wa kienyeji.

‘Mke wako mkubwa ana ugumba ndi-ndio.....lakini nilikuambia hili nitalifanyia kazi, na nimeshalifanyia kazi, lakini ukumbuke kuwa ugumba wake unatokana na mizimu,  na kwa vile ni kwa kimzimu, unaweza kuondoka kwa matambiko, siku zila ulipoondoka nilifanya makafara mengi, ila kwa sasa msharti yaliyobakia ndio hayo...

‘Sharti muhimu ni tufanye matambiko ya kumwaga damu wa ngombe, na baada ya hapo, ukutane na mkeo mdogo, ambaye atashika mimba, mimba hiyo itaondoa nuksi ya mkeo mkubwa, ...na itaondoa nuksi mwilini mwako, kwahiyo ukienda kukutana na mkeo mkubwa atashika mimba, na utakuwa mwisho wa ugumba wake.

‘Sijakuelewa hapo,...ina maana mke wangu mkubwa sio mgumba wa kuwa hana kizazi, ndilo swali langu ninalokuuliza mwanzoni ulisema kabisa ni mgumba, hana kizazi, au mimi sikuelewa vyema?’ akauliza tena.

‘Ugumba mwingine ni wa kimizumu, usipotimiza masharti unabakia hivyo hivyo..hatazaa abadani mkiwa naye,yeye alikuja na nuski yake ambayo inafanya damu zenu kukataana, ...’akaambiwa.

‘Unataka kusema kuwa, mke wangu kama atakwenda nje ya ndoa akakutana na mwaname mwingine anaweza kuzaa?’ akauliza

‘Anaweza kama hiyo nuksi hataitamwingia huyo mwanaume mwingine, kutegemeana na nguvu za mizimu ya huyo mwanaume mwingine..hayo ni mambo ya kimila zaidi, unajua kuna mambo mengina hutokea nyie mkaona ni ya kawida tu kumbe kuna mazindiko,....mambo ya kimila yanasababisha hayo..’ akaambiwa.

‘Kama ni ya kwetu huyu mwanamke atahusikanaje na kusema kanipa nuksi..?’ akauliza

‘Nielewe hapo, ulipomua huyo mwanamke kuna mambo ulitakiwa ufanye, uliambiwa na wazee wako, hukuwahi kuambiwa hivyo, ukapuuza, sasa mizimu ikaona ikuonyeshe kwa kupitia kwa huyo mwanamke....ni mambo ya ndani sana, cha muhimu sasa timiza hili sharti la ng’ombe...’akaambiwa.

‘Kwa hivi sasa, mkeo mkubwa akitembea na mtu mwingine, anaweza kushika mimba, lakini  sio kwako, njia yake imeshasafishika, ilibakikia kwako,..kwako ni mpaka utoe tambiko,uzae na mke mdogo, ukivunja hilo wewe unakuwa tasa...hutazaa tena...’

‘Mimi nitakuwa tasa...ina maana huyu mwanamke kaniharibia maisha yangu....’akawa anawaza

Na wakati anarudi kutoka kwa mganga, mara akasikia uvumi kuwa mkewe anaonekana  mara nyingi akiwa na rafiki yake, rafiki yake ambaye wameshibana, aliyesimamia ndoa yake, na kuna watu wengine walimwambia kuwa wameshaona na dalili zote kuwa hao watu ni wapenzi wa siri...

‘Mkeo anatafuta mimba ya siri, ili aje akusingizie wewe....’akaambiwa

‘Kwani nani kawaambia kuwa mimi sizai...mimi ni rijali ninaweza kuzaa, tatizo ni huyu mke...lakini nitalimaliza,...huyu mke mkubwa ndiye ana mkosi...., ngoja nitachunguza kama ni kweli, atanitambua kuwa mimi ni nani...’akasema aliposikia hayo maneno kutoka kwa watu.

‘Kama unabisha muulize mke wako mdogo, kwani yeye alipokwenda kwao yeye na wazazi wake walikwenda kwa mganga wakaambiwa kikwazo ni mke wako mkubwa, mke wako mkubwa ana nuksi, ona tangu umuoe, mali yako inavyopungua, huzai na sasa keshagundua kuwa akitembea na mwanaume mwingine atazaa, wewe bado umelala tu....’akaambiwa na watu hao.

‘Hata mimi nalifahamu hilo, ila, hilo la rafiki yangu kutembea naye, sijaliafiki mpaka nione mwenyewe, nitachunguza na kama ni uongo na nyie nitawafanyizia ubaya ambao hamjawahi kufanyiwa, msipende kuniingilia maisha yangu.....’akasema.

‘Utakuja kuliona wewe mwenyewe kwa macho yako, wewe rudi mapema nyumbani utawafuma, utakuja kutushukuru..’akaambiwa.

‘Nitampata wapi ng’ombe mweusi asiye na doa...’akawa anajiuliza akilini kwani mganga wake alimwambia atafute ng’ombe mweusi asiye na doa hata moja, hakutaka kukaribisha hasira zake, kwani ana jukumu hilo la kufanya kama ni kweli atakuja kugundua mwenyewe, lakini...akichelewa, ...ooh,

‘Ngombe mweusi....’akawa akiuliza kwa watu wanaofuga ng’ombe lakini ikawa ngumu kumpata kwani kila ng’ombe mweusi anayepatikana anakua na baka ama jeupe au la rangi nyingine,na ng’ombe huyo hatakiwi kuwa na baka la rangi nyingine yoyote...

Katika kuhangaika ndipo akakutana na mtu akamwambia ngombe kama hao wameonekana kijiji cha jirani...

‘Oho basi nitakwenda kumtafuta kesho...’akasema, kwahiyo alishapanga kuwa kesho yake anakwenda huko kijiji cha jirani, sasa huyu mkewe anakuja na taarifa hiyo kuwa ana mimba,...

‘Mke wangu ana mimba, kama ni kweli, basi hiyo mimba sio yake, kama sio yake,kaipatia wapi,...ina maana ni kweli kuwa anatembea na rafiki yake, ina kweli keshatembea na rafiki yake, na kupata mimba, kwahiyo yeye sasa ni tasa, kwa vile keshaharibu tambiko hataweza kuzaa tena, hata akipta huyo ng’ombe ni kazi bure...’ akili hapo ikazidi kuwaka moto.

Akageuka huku na kule kwa hasira kama anatafuta kifaa, kitu..lakini hakuona hicho kitu, akaanza kumsogelea mkewe akiwa keshabadilika uso ukawa umejaa hasira za kuua, ‘Ina maana mke wake keshamfanya yeye sasa awe tasa,....’ akawa anamsogelea mkewe huku akinguruma kihasira

Kabla hajamkaribia mkewe kwa kasi ya jabu akarusha makofi mawili ya haraka haraka vya nguvu.

Mkewe hakutarajia hiyo hali na vibao vile vililenga usoni, mkewe akajiona anaona vinyota mbele yake, akabaki kaduwaa, hakuweza hata kupiga ukelele wa kuomba msaada, hakutarajia hayo...ina maana taarifa njema imegauka kuwa balaa....

‘Utaniambia kuwa hiyo mimba ni ya nani…’ alisikia vibao vikiongezeka usoni, mara ngumi mateke yakiingia mwilini na hakujua ni vipigo vingapii alivipata kwani giza lilishaanza kutanda usoni....akaondoka chini.

‘Mimi niliambiwa na mtaalamu siwezi kuzaa mpaka nimalize matambiko, na matambiko sijayafanya umepata mimba,...kwahiyo umetaka mimi niwe tasa, kwa vile nimeoa mke mwingine,si ndivyo unavyotaka ndio maana ukasema nioe hata mwingine ukijua umeshaniweza mimi sitazaa tena, ndio lengo lako sio,sasa...utaniambia hiyo mimba ni ya nani...’hakujali kuwa mkewe kadondoka chini akazidi kusindilia mateke

‘Hata ukifa sina hasara,..ila kabla hujafa, nataka unieleze hiyo mimba niya nani, halafu ufe ukazalie huko kuzimu....mchawi mkubwa wewe...hutaki kusema sio ngoja...’ akachukua rungu lilokuwa mle ndani akataka kumbamiza mkewe.

Kwa bahati nzuri mlango ukagongwa na aliposikia hivyo akalirudisha like rungu lake ambalo hukaa humo ndani kwa ajili ya usalama. Aliogopa kama ni mgeni wa heshima isije ikawa dhahama na ukapatikana ushahidi kuwa kumbe kweli yeye ana mpiga mkewe mara kwa mara,...na rungu,  kitu alichokipinga kwa wazee walipokaa kikao, akalitupa lile rungu pembeni .

Akageuka na kwenda mlangoni kuangalia ni nani aliyegonga mlango, kutupa macho anamuona aliyegonga mlango kumbe ni yule yule mbaya wake, aliyekuwa rafiki yake lakini sasa kawa ni adui yake.

Kwanza alitabasamu, akatikisa kichwa kama kukubali, akageuka kuangalia ukutani, alipolitupa lile rungu lake, huku mwili ukisisimka kwa hasira, akijua kuwa mbaya wake kajileta mwenyewe, moyoni akawa anasema huyu hyu ataniambia ukweli kuhusu hiyo mimba.

‘Eheee, naona umejileta mwenyewe, kama ulijua vile, au ulifika ukijua nimeshaondoka, hahaha, karibu sana rafiki ...hahaha rafiki, natamani nisitamke hilo neno...karibu....badi nipo,sijaondoka....’akasema na rafiki yake bila kujua, akaingia ndani

Alipoingia ndani akahisi hali sio shwari, akatupa macho, akamuona shemeji kalala sakafuni.

‘Mbo-mbona hivyo rafiki yangu....?’ akawa anashangaa huyo rafiki yake.

‘Njoo, sogea huku nifunge mlango, rafiki..rafikiiii rafiki eeh, hahaha, rafiki mpaka kwenye mke wangu, kwa vile umesimamia ndoa yangu ndio unataka uhakikishe kuwa kweli mke wangu hazai au sio...mitindo ya kupata mtoto wa kike, wa kiume yote unaifahamu wewe au sio, sasa huyu....’akaonyeshea kule alipolala mkewe, kuna kitu kikamfanya ashituke, mbona mkewe tangua adondeke pale chini hajajisogeza,..lakini akajipa moyo kuwa anajifanyiza tu ili asiendelee kupata kipigi, akamgeukia rafiki yake na kusema

‘Imemuona mwenzako, hebu niambie hiyo mimba ni ya mtoto wa kike au wa kiume....?’ akauliza

‘Mbna sikuelewi rafiki yangu, ulisema mke wako hawezi kubeba mimba mpaka umalize matambiko, na mimi nimekuja kukuambia kuwa nimemuona huyo ng’ombe kwa jamaa mmoja,...’akasema rafiki yake.

‘Ng’ombe, ng’ombe wa nini tena wakati wewe mtaalamu umeshafanya vitu vyako...je huyu atakuwa wa kiume au wa kike jibu swali langu...’akasema huku akiwa kamshikilia mkono kama vile hataki amponyoke.

‘Hebu acha utani rafiki yangu....hayo yanakutoka ukiwa umelewa au bado upo sawa sawa..ni mimi wa kuniambia mambo hayo...?’ akauliza

‘Hahaha, hebu uniambie mke wangu na wa kwako ni nani mnzuri zaidi, wewe si unajisifia kuwa mke wako ni mnzuri kuliko wote hapa kijijini, sasa mke wangu kashinda nini mpaka umtake, mpaka muwe wapenzi, na zaidi umeshampa mimba....’akasema

Rafiki yake akabakia na mshangao.....akawa anashindwa hata kusema neno, akawa anatafuta mwanya wa kujiondoa mikononi mwa huyo rafiki yake kwani anajua shari zake, na akianza jambo lake haliishi mpaka utokee ugomvi.

‘Sikiliza ....rafiki yangu...’akasema

‘Sasa ni hivi nimeshayajua yote, kuwa wewe kuja kwako hapa si bure, unatumia mgongo wa urafiki wetu kufanya mambo yako... sasa kwa vile umemuona mke wangu ni mzuri zaidi ya mke wako, mchukue,....huyo hapo...anajifanya kazimia...na bado..mpaka sura ichujuke...’akasema

‘Yaani ndio umempiga kiasi hicho kwa maneno tu ya mitaani..., ...siamini..mimi nilijua labda huyo mganga ndiye kakuambia hivyo...jaribu kuwa na subira utagundua kuwa sio kweli ni uzushi tu...’akasema rafiki yake

‘Huamini, eeh, muda ule nilipokuona umembeba mke wangu na baiskeli mlitoka wapi...si mpenzi wako, una cha kutembelea, hivi ungelikuwa na gari si ungemaliza wanawake wote wa hapa kijijini, baiskeli tu , una...kwanza tuache hayo,...mimi nataka tuyamalize haya kimiya kimya,...wewe siumeona ni mzuri kwako, unakumbuka mahari nilitoa kiasi gani..zilikuwa ng’ombe ngapi vile...?’ akawa kama anauliza

‘Sikiliza rafiki yangu, tuliza munkari, hizo ni hasira na ibilisi keshakutawala, na kama unafanya utani, ujue huo sio utani mzuri, usije ukafanya jambo ambalo utakuja kujijutia...’akasema rafiki yake

‘Yah, zilikuwa ni ng’ombe tisa, na yule wa kufunga uchumba wa kumi...unakumbuka wewe mwenyewe ulinisifia kuwa ni mke mnzuri mweupe kwahiy ng’ombe hizo ni halali, eeh, kumbe na wewe ulikuwa ukimmezea mate, sasa umewahi....hahaha kweli umewahi, maana umaniweza...lakini hujaniweza...ulichofanya utakuja kukilipa...’akasema huku akitikisa kichwa.

‘Unajua mimi sijakuelewa, kilichonileta hapa ni kingine kabisa,nimekuja kwa habari nzuri, kuwa...’akasema lakini mwenzake hakutaka kumpa nafasi.

‘Nataka ng’ombe zangu, mke ni wako, huyo hapo, mimi sina haja naye,...nirejeshee mahari yangu yote...hapo tutaelewana, vinginevyo tutaonana wabayaaaa...’akashika kichwa na kijikuna kama nywele zinawasha na kwa kufanya vile akawa kamuachia mwenzake mikono, na mwenzake akasogea mbali na yeye

Mwenzake akawa kasimama akiwa ana mshangao wa ajabu , hakuamini hayo maneno yanatoka mdomoni kwa rafiki yake ni ya kweli au anafanya mzaha, lakini sio mzaha, maana hali ya shemeji pale chini sio nzuri.....

‘Unashangaa nini, ulijua siwezi kuyatambua mambo yenueeh, unakuja hapa kwa tiketi ya urafiki, kuja kumuonyesha mke wangu mitindo yako eeh, maana wewe unajiita docta wa mapenzi, au sio…hahaha, basi mimi ni docta wa kuwatengeneza watu kama nyie...’ akawa anaongea huku anatikisa kichwa chake huku na kule.

‘Rafiki yangu unajua mpaka sasa hivi sijakuelewa, yale ni mazungumzo yetu tu...mitindo, sijui nini, ni kawaiuda yetu kuongea tu....siwezi kuja kukufanyia hapo kwa ...hapana nahisi unatania, ..wewe ni sawa na ndugu yangu, siwezi na shemeji namuheshimu sana...yeye na mke wangu ni marafiki wakubwa....’akasema sasa kujitetea

‘Mhhh mke wako eeh, kama yeye unaweza kumdanganya lakini sio mimi, ..kichwa hiki kimekwenda shule ya asili, kinajua ya siri na ya dhahiri...’
Akasema sasa akiwa kashika kiuno, hiyo ni ishara ya shari, anamfahamu sana huyo rafiki yake akishika kiuno, kinachofuata hapa na vurugu, litarushwa teke au ngumi….

Rafiki mtu akabakiwa kaduwaa, akishangaa, na kwa vile anamjua rafiki yake, akanyamaza kimya, akijua leo kuna mambo, na huenda asiondoke hapo salama. Alikaa kimya kusikiliza shutuma ambazo hakujua zimetokea wapi, akatulia kusikiliza, halafu alipoona rafiki yake kanyamaza, akaanza kusalimia....

‘Habari yako rafiki yangu, tuyaache hayo ya waosha vinywa mitaani kwanza pokea habari hiyo njema kuwa nimeshapata ng’ombe uliyekuwa ukimtafuta, kwahiyo hata sasa hivi tunaweza  kwenda kumchukua...!’akasalimia, lakini akaona jamaa akiwa kama anawashwa, hatulii.

‘Rafiki yangu eeh, mimi ni rafiki yako wewe...mnafiki mkubwa wewe...’hilo jibu likamfanya mwenzake abakiwa mdomo wazi.

‘Kwanii vipi, ina maana unachukulia vile nilivyomleta shemeji na baiskeli, kwani hiyo ni mara ya kwanza, mara ngapi nafanya hivyo na wewe unaona, yote hayo ni maneno ya fitina yametungwa kutuchonganisha, ....rafiki yangu kumbuka mimi na wewe ni kama ndugu, tumeshibani usije kusikia majungu ukaharibu udugu wetu...’akasema mwenzake.

‘Ni nani kakuambia nimesikia majungu na kama sio kujihami huko.....je tumeshakubaliana, tunaondka hapa mguu kwa mguu, unanihesabia ng’ombe mahari yangu nakuachia mke...vingnevyo kijiji kizima kitajua kuwa umetembea na mke wangu,kabla hajazaa............’akasema

‘Hapo sasa naona unataka kuharibu urafiki wetu kama kweli unaamini hayo, naona umefika mbali...’akasema alipoona mwenzake hatanii.

‘Kama kweli wewe ni rafki yangu, ...tuyamalize haya kimiya kimiya kama mlivyofanya na mke wangu kimiya kimiya...tunakubaliana, nyie si mnataka mimi niwe tasa...na kama kweli nitakuwa hivyo, na wewe nitamaliza nitahakikiahs huna uume,...’akasema

‘Eti nini....’rafiki yake akasema
‘Hilo ni la baadaye, kwanza tukubaliane hili, mke wako huyu hapo..nipe mahari yangu, sitaki kashifa...tumeelewana...’akasema sasa akimsogea rafiki yake, na rafiki yake akawa sasa anarudi kinyume nyume keshajua mwenzake kazamairia ubaya.

 Rafiki yake huyo akajua huyu jamaa kayaamini hayo na huenda keshampiga mkewe na hata kumuua, kwani tangu aiingie hapo hajaona shemeji akitikisika, akajua huyo jamaa huenda ameshaua,, na sasa anatafuta visingizio,akaona kwanza atumie busara yake ya mwisho.

‘Vipi rafiki yangu kwani kuna jambo gani, naona shemeji anavuja damu yupo sakafuni, hatikisiki, anaonekana hayupo salama, hebu tumuangalie kwanza , usije ukawa umemuumiza,....’akasema akiendelea kumuangalia shemeji yake pale chini.

‘Kwa vile ni mpenzi wako ndio unamuonea huruma au sio...unajifanya hujui chanzo ni nini au sio eeh,..sogea pale kamuangalia vyema mpenzi wako, na hiyo ndio dawa ya wasaliti wa ndoa...na wewe zamu yako bado, kwanza tunakubaliana hapa ngombe wangapi, tisa, huyo wa kumi hakuhusu sana...’akasema rafki yake akasogea na kulichukua rungu lake, na kumsogelea rafiki yake wakawa sasa wamesimama sambamba.

Jamaa kuona hivyo, akaona humo hakukaliki, yeye alikuja kwa taarifa nzuri kuwa kaona ng’ombe mweusi kwa jamaa yao mmoja, na hilo linaweza kumfurahisha rafiki yake, lakini anachokikuta hapo ni tofauti, na alitamani atoke humo ndani haraka, kwani mkewe anamsubiria kuna sehemu wanakwenda, lakini yeye aliona rafiki yake ni muhimu kwanza...

‘Ina maana mimi nimeacha shughuli zangu kwa ajili ya kujali urafiki wetu, nimefanya makosa, ndio haya yamekuwa hivi, kama ni hivyo,mimi naona hapa hakuna amani, ngoja nijiondokee zangu tu , samahani naomba nitoke....’akasema akigeuka kuondoka, ikawa kosa.

Ilikuwa ni Bahati tu,kwani aliinama kufungua kitasa cha mlango, na ndicho kilichomsadia, kwani rungu lilikuwa lipasue kichwa likagonga kwenye bega upande wa nyuma.

‘Khaa, rafiki yangu vipi...’akasema na kabla hajageuka vyema, alishitukia teke, na rungu la pili likimkosa kosa tena, kwani kwa muda huo alishageuka kiaina  kujihami, akaona sasa hana hiari ni mapambano tu, kwani mwenzake inavyoonekana kadhamiria kumuua!

**********
NB Mafahali wawili wanapambana, chanzo ni nini, na ni nini hatima yake,tuzidi kuwemo…


WAZO LA LEO:. Ushirikiana ni mpana sana, wenye nia ya kuondoa  imani halisi ya kumujua mungu wa kweli, imani ya amani na upendo. Watu kutokana na shida zao hujikuta wakihadaiwa na kusahau kabisa imani halisi yenye kumpwekesha mungu, imani ya kujua kuwa watu wote ni kitu kimoja, wametokana na asili moja, imani hiyo huondolewa nyoyoni. 

Watu wanajikuta wakiingia kwenye imani nyingine ambazo zinawahadaa watu kuwa kuna nguvu nyingine , nguvu za ziada,zenye kuponya , kuleta utajiri, nk. Kutokana na shida, umasikini, na imani haba, elimu ndogo ya imani sahihi ya mungu mmoja, watu wanakubali na kuukumbatia ushirikina, na huko hujengewa imani za chuki, ubinafsi, na matokea yake, ndugu na ndugu, marafiki nk wanaanza kufarakana.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159

Anonymous said...

Nilisoma baadhi ya shuhuda kuhusu mtangazaji wa mapenzi anayeitwa DR DAWN kuhusu jinsi ambavyo amesaidia watu wengi kuwarudisha wapenzi wao wa zamani ndani ya masaa 48, kwa dhati nilikuwa nikifikiria kama hiyo ni kweli na ikiwa mwanaume huyu angeweza kusaidia kumrudisha mpenzi wangu ambaye Napenda sana. Niliamua kuwasiliana naye kwa sababu nampenda sana mpenzi wangu na tumetengana kwa miezi kadhaa. Kwa kweli nilimkumbuka sana, nimejaribu njia zingine zote kumrudisha lakini sikuweza. Niliwasiliana na DR DAWN na akaniambia kuwa ex wangu atanirudia baada ya saa 48 zijazo,
Kwa mshangao wangu Ex boyfriend wangu alirudi saa 48 haswa, shukrani kwa Dr DAWN,
Anaweza pia kukusaidia
*Tahajia ili kupata mimba.
*Tahajia ili kuungana tena.
*Tibu ugonjwa wowote.
*tahajia kwa bahati nzuri.
*Tahajia kwa ajili ya mali.
Na wengine.
Wasiliana naye kupitia: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159