Jamaa kuona hivyo, akaona humo
hakukaliki, yeye alikuja kwa taarifa nzuri kuwa kaona ng’ombe mweusi kwa jamaa
yao mmoja, na hilo linaweza kumfurahisha rafiki yake, lakini anachokikuta hapo
ni tofauti, ..
‘Ina maana mimi nimeacha
shughuli zangu kwa ajili ya kujali urafiki wetu, nimefanya makosa, ndio haya
yamekuwa hivi, kama ni hivyo,mimi naona hapa hakuna amani, ngoja nijiondokee
zangu tu , samahani naomba nitoke....’akasema akigeuka kuondoka, ikawa kosa.
Ilikuwa ni Bahati tu,kwani
aliinama kufungua kitasa cha mlango, na ndicho kilichomsadia, kwani rungu
lilikuwa lipasue kichwa likagonga kwenye bega upande wa nyuma.
‘Khaa, rafiki yangu
vipi...’akasema na kabla hajageuka vyema, alishitukia teke, na rungu la pili likimkosa
kosa tena, kwani kwa muda huo alishageuka kiaina kujihami, akaona sasa hana hiari ni mapambano
tu, kwani mwenzake inavyoonekana kadhamiria kumuua!
Ilipita dikika kumi, ngumi zikurushwa, mateke, rungu, viti, ..na kila mmoja akijaribu kutumia ubavu wake, na kuhakikisha anamjeruhi mwenzake, ubinadamu ukatoka, ukabakia unyama, urafiki ukatoka ukabakia uadui...damu ikaanza kumwagika....
Tuendelee na kisa chetu...
Majirani walisikia ghasia
na baadhi wakafika hapo kuangalia kuna nini, wakasukuma mlango uliokuwa umeufungwa
kwa ndani, ukawa haufunguki, lakini watu wakiguna kuonyesha kuna mapigano
luliwaanya waamue kuuvunja huo mlango, walipoingia wakakuta jamaa wawili wakiwa
wanapambana mtu na rafiki yake. Damu zinawavuja
Hali waliyokutwa nayo
ilikuwa mbaya, wanaume walikuwa wakivuja damu, huku wakiwa hoi wamechoka, na
bado vita ilikuwa ikiendelea. Ilibidi vijana wenye nguvu waitwe kuwakamata na
walipokuja ilichukua muda sana kuwatenganisha.
Walishangaa kmuona mama
mwenye nyumba akiwa kalala sakafuni, walipomchunguza wakagundua hana fahamu,
ikabidi atolewe nje kwenye upepo na huduma ya kwanza ifanyike kwa haraka.
Mpaka muda huo hakuna
aliyeweza kugundua chanzo cha ugomvi huo ni nini,…wakati wengine wanahangaika
kumfanyia mke mtu huduma ya kwanza, wengine bado walikuwa na kibarua cha
kuwasuluhusha hao mafaili wawili,kwani japo wamechoka, wameumia, lakini kila
mmoja alikuwa na mori wa kupambana na mwenzake, kila mara walikuwa wakikurupuka
kutaka kupigana, ikaonekana dawa na kumuondoa kabisa huyo aliyekuja kwenye
nyumba ya mwenzake na kumpeleka mbali kabisa, ilikuwa mshike mshike hadi
anaondolewa hapo.
‘Niacheni huyu mtu hawezi
kuniumiza hivi bila kosa, nimemfanyia nini mimi , mangapi tunasaidia, leo hii
ananifania hivi sikubali…..’akawa anasema rafiki wa baba yako, na baba mtu
akisema;
‘Ni lazima ulipe, na bado
nitakuumiza sana, mpaka nihakikishe na wewe upo kama mimi, hamuwezi kunifanyia
hivi mimi na huu mzogo wako uuchukue…’wakawa wanajibishana kwa kauli za kukata hakuna aliyeweza kugundua
chanzo cha mapigano hayo ni nini kutokana na kauli hizi zisizokamlika….
Wazazi na mjumbe wakaitwa ili
kusuluhisha hayo mapigano, na hao mafaili wawili wakaitwa mbele ya mjumbe na
wazee wa kijiji, wakaanza kuulizwa, chanzo cha ugomvi wao, ikawa kila aliyeulizwa
anapandisha hasira, anataka kwenda kupambana na mwenzake hakuna aliyekuwa na
lakusema, ila kutizamana kwa hasira mbele ya mjumbe na wazee wa heshima.
Kule kwa mama aliyepoteza
fahamu, juhudi zilikuwa zinaendelea, Ilichukua muda mama kuzindukana, na alipozindukana, na kuonekana
kuwa anaweza kuongea, ikabidi aulizwe chano cha mapigani hayo nay eye kupoteza
ahamu ni nini, ikawa hakuna jinsi akaelezea ilivyokuwa.
‘Ukweli ukadhihiri, na
mafahali wawili wakaambiwa wajieleze, kila mmoja akaanza kujitetea kivyake, na
wazee wakasema;
‘Hili ni kosa na ni tatizo
kubwa, hatuwezi kuliacha hivi hivi kwani linaweza kuleta maafa baadaye, inabidi
kuitisha kesi ya kimila, ili kujua ukweli
na kama kuna ushahidi wowote wa hiyo shutuma unahitajika mbele ya baraza la
wazee…’ikatolewa hiyo taarifa.
Kesho yake, watu
wakakusanyika kwa mjumbe, wakiwemo wazee wa kimila ambao wanajua mambo hayo na
usuluhishi, ikabidi sasa kila mmoja apewe muda wa kujieleza na kutoa ushahidi
wake. Baba yako, akatoa taarifa yake kuwa alisikia tetesi za watu, na akaamua
kuuatilia akagundua kuwa kweli raiki yake ana mahusiano na mke wake.
‘Hizi taarifa au tetesi
ulipewa na nani?’ akaulizwa
‘Na marafiki zangu wa
kijiweni, na pia mke wangu mdogo ambaye hayupo mbali na nyumba ya mke wangu
mkubwa…’akasema
Ili kujua ukweli, Ikabidi
marafiki hao waitwe kuhojiwa, na wao wakasema walikuwa wakimona rafiki huyo akifika
mara kwa mara wakati mume wa familia hayupo.
‘Je kabla ya hapo huyu
rafiki alikuwa hafiki, kabla ya kuhisi hivyo, kuwa huenda wana mahusiano?’
wakaulizwa
‘Alikuwa anafika, lakini
hali iliyoendelea baadaye ilitutia mashaka ndio maana tukaona tumueleze rafiki
yetu achunguze mwenyewe…’wakasema.
‘Yeye ni rafiki yake, yeye
ndiye aliyesimamia harusi na mara nyingi mtu ambaye kakusimamia kwenye harusi
na ndoa yako anakuwa ndugu yako, kufika kwake hapo nyumbani ni jambo la kawaida
kuna ushahidi gani mwingine wa kuonyesha kuwa huyu mama alikuwa na mahusiano ya
karibu na huyo mke wa mtu?’ wakaulizwa
‘Hakuna…’wakasema.
‘Kuna mtu alifika kwake
akaona ushahidi wa kuonyesha kuwa hao watu wanamhusiano ya kimapenzi?’
wakaulizwa.
‘Hakuna aliyefika, ndio
maana tulimuambia achunguze kuhakikisha, hatukumwambia kuwa tuna ushahidi, …’wakajitetea.
‘Kwahiyo nyie mlihisi tu,
mkajenga fitina na umbea…’wakaambiwa, na baadaye akaitwa mke mdogo na kauli
yake ilikuwa hiyo hiyo kuwa huyu jamaa alikuwa akifika mara kwa mara na mara
nyingi mume wake anakuwa hayupo.
‘Wewe ni mke mwenza, je
uliwahi kufika ukashuhudia wakiwa na mahusiano kama hayo mnayodai, kuna dalili
gani zilizokuonyesha kuwa wana urafiki wa karibu?’ akaulizwa
‘Jinsi walivyokuwa
wakiongea na huyu mtu akifika hukaa sana ndani, akitoka anasindikizwa…’akasema
‘Ina maana wewe hajawahi
kufika mgeni kwako wa kiume, akakaa halafu alipotoka ukamsindikiza?’ akaulizwa
‘Wanakuwepo , lakini kwa
mwenzangu ilikuwa imezidi, ni huyo huyo tuu, inatia mashaka..’akasema.
‘Je uliwahi kufika
ukawafuma wakiwa katika hali ya mahusiano, maana wewe upo karibu, hukufanya
utafiti huo?’ akaulizwa.
‘Kwanini nisumbue kwenda
kuangalia wakati hali inajionyesha, sikutaka kupoteza muda wangu mimi
nilimwambia mume wangu ajaribu kuchunuza maana mimi nina wasiwasi na huyo
rafiki yake….’akasema.
‘Hivi kweli nyie mpo
majirani ulishindwaje kufanya utafiti, lakini ukaweza kwenda kutangaza mitaani
kuwa mwenzako ana mahusiano na huyo rafiki wa mume wako…huoni kuwa huo ni
uchonganishi, na wewe ndiye umesababisha yote hayo….’akaambiwa.
‘Kama hamuamini basi, ila
mimi nilitimiza wajibu wangu kusema kile nilichokiona, na nilimuambia mume
wangu achunguze, sasa yeye akachukulia hasira…’akasema mke mdogo.
‘Lakini hukuwahi
kuthibitisha hilo kuwa kweli watu hao wana mahusiano, umeona wakiongea, umeona
huyo mtu akiingia na kutoka , na ni kawaida yake kuja hapo, hata kabla yaw ewe hujaolewa,
hata akiwemo mume wake, kama alivyijieleza, je sio kweli kuwa anafika hapo hata
akiwemo mume wenu?’ akaulizwa.
‘Ni kweli huwa anafika,
lakini mara nyingia anafika mume wetu akiwa hayupo..ndio maana mimi nikatilia mashaka’akasema.
‘Hebu tumuulize muhusika
ni kwanini ulikuwa ukifika wakati mume wa nyumba hayupo?’ akaulizwa.
‘Mimi kazi zangu ni za
uvuvi, pamoja na uchungaji, nyumba ya rafiki yangu ipo njiani, napita hapo
nikiwa nimetokea kwenye kazi zangu, siwezi kupita tu bila kusalimia wakati huyo
ni rafiki yangu, na urafiki wetu ni kama udugu,kwa ukaribu tulio nao…’akasema.
‘Hebu tuambie siku ya
tukio ilikuwaje?’ akaulizwa.
‘Siki ya tukio mimmi
nilifika kutoa taarifa kwa rafiki yangu ambaye alikuwa akitafuta ng’ombe mweusi
kuwa nimempata huyo ng’ombe, nilipofika nikakuta mke wa rafiki yangu kalala
sakafuni, na kabla sijajua ni kitu gani kilichotokea rafki yangu akaanza
kuniandama kuwa kasikia kuwa mimi nina mahusiano na mke wake…ilikuwa ni
mshangao kwangu maana mimi na yeye tunaurafiki wa karibu, kama ndugu
haingeliwezekana mtu kama mimi kufanya uchafu wa namna hiyo…’akasema
‘Na kumpa lifti ya
baiskeli sio mara ya kwanza, kama nilimuona yupo sokoni na mimi naelekea njia
hiyo kuna ubaya ganni kumpa lifti, anafahamu sana, sema katekwa na ibilisi…’akasema.
‘Ibilisi umenipa wewe….acha
kujikweza hapa…..’akasema baba yako akanyamazishwa na wazee kuwa hajapewa nafasi
ya kuongea.
‘Lakini kwanini iwe kila
siku unafika nyumbani kwa mwenzako wakati hayupo, hilo ndilo linakuwa swali kwa
wengi, imeonakana kufika kwako kwa rafiki yako kumezidi sana,….’akaulizwa.
‘Kama nilivyosema mimi nikitoka
kwenye shughuli zangu napitia hapo, na muda huo rafiki yangu anakuwa hayupo, je
ingelikuwa ni busara mimi kupita bila kusalimia,..hivi kweli kwa mila zetu
inakubalika hivyo, je mimi hapo nimefanya kosa gani,mbona yeye akienda kijiweni
au kilabuni anapitia kwangu na kumsalimia mke wangu …’akasema.
‘Haya baba mwenye nyumba
tuje kwako, kuna ushahidi gani mwingine wa kuthibitisha hiyo kauli yako kuwa
rafiki yako anakuibia mke wako?’ akaulizwa
‘Mke wangu ni mja mnzito…’akasema
na watu wakacheka na wengine wakampa hongera.
‘Msicheke, huenda kauli
yake hiyo ina maana kwake, hebu tuambie mke wako kuwa mja mnzito inahusikanaje
na rafiki yako, maana huyo ni mke wako na kuwa na mimba ni jambo la kawaida..?’
akaulizwa na hapo ikabidi aelezee alivyoambiwa na mganga wa kienyeji.
‘Ndugu yetu, huyo mganga
yupo wapi, maana hilo linatushangaza sana,yeye anajuaje kuwa wewe hutazaa, ana
vipimo gani, vya kukuthibistishia hilo, au je uliwahi kwenda hospitalini
ukaambiwa kuwa hutazaa?’ akaulizwa.
‘Niende hospitali, ….nyie
wazee vipi, hivi hili nalo ni la kuwenda hospitalini kujitangaza, hapana, mimi
najua kuwa dawa za kienyeji na mambo ya wazee wetu yana uhalisia zaidi…’akasema
‘Kwahiyo wewe hivi sasa ni
tasa, unaamini kuwa hutazaa tena?’ akaulizwa
‘Nani tasa….sasa mnataka
kunitukana…’akasema na watu wakacheka.
‘Si ndivyo alivyokuelezea mganga
wako kuwa ukikiuka mashartii basi hutazaa tena, utakuwa tasa, si ndivyo
ulivyosema,je wewe unaamini hivyo. Kuwa wewe sasa ni tasa…ili wake waondoke,
maana sheria zinawaruhusu au?’ akaulizwa
‘Siiii-amini…kuwa mimi ni
tasa, mimi rijali bwana….kama itakuwa hivyo, hapana mimi sio tasa, nitahangaika
mpaka nilimalize hili tatizo na huyo rafiki yangu nitahakikisha na yeye anakuwa
kama mimi….’akasema akimuangalia rafiki yake kwa hasira.
‘Anakuwa kama wewe kivipi…?
kama wewe tasa au kama wewe nani?’ akaulizwa
‘Kama wameamua kuniharibia
yeye na mke wangu, basi na mimi nitawaharibia wao, nitahakikisha hakieleweki,
nitawafanya wao kama mimi…’akasema.
‘Kwahiyo wewe unaamini
kuwa sasa hivi umeshakuwa tasa?’ akaulizwa.
‘Nani kawaambia mimi ni
tasa bwana nyie wazee vipi, mimi tasa mimi tasa, mnafanya tangazo, je nikizaa
mtasemaje,….mabona hatuelewani…’akasema kwa jaziba.
‘Masharti ya tambiko, au
kama alivyokuagiza mganga wako yamevunjwa, mke kaenda kupimwa hospitalini na
ili apimwe damu inabidi achomwe sindano, je hajavunja hayo masharti…’akaambiwa
kama anaulizwa kabala hajasema neno mjumbe akasema;
‘Haya kwa kauli yako na
uvumi uliopewa wewe unaamini kuwa mke wako katembea na rafiki yako je hajavunja
hayo masharti, na kwa kauli ya mganga masharti ya kivunjwa wewe hutazaa tena,
umekuwa taa-saa, si ndio hivyo jamani alivyosema,…tunakuuliza tena je wewe
unaamini kuwa sasa hivi umeshakuwa tasa…?’ akaulizwa.
‘Siamini…nitahangaika,
japokuwa mganga kasema hivyo, lakini wanazidiana nitakwenda kwa mganga mwingine
atanitengeneza, na ole wao,nawaambia mbele yenu ole wao…’akasema.
‘Acha vitisho, kijana,
wewe bado mdogo sana, hujui maisha yalivyo, sikiliza tukuelemishe….’akaambiwa
na akatulia akiwa kainama chini.
‘Lengo letu la kukuhoji hivyo nikutaka
kukuonyesha kuwa hayo uliyoambiwa na mganga wako sio kweli,…mwenyewe unakiri
hapo kuwa huamini kuwa wewe ni tasa, kama ungelikuwa unamuamini basi
ungelikubali kuwa wewe ni tasa,au unaamini hivyo tukusaidie ..?’ akaulizwa tena
akawa kimia.
‘Jamani nyie vijana, nyie
watu, tusipende kuamini mambo hayo bila kuwa na vipimo halisia, na vipimo
halisia ni kwenda hospitalini je hawa waganga wana vipimo gani vya kukuonyesha
kuwa wewe hutazaa au utazaa, ni Bahati nasibu tu wanacheza, nikuulize tena wewe
bondia, je wewe uliwahi kwenda
hospitalini ukaambiwa huwezi kuzaa?’ akaulizwa.
‘Mimi siamini vipimo vyao
hivyo vya hospitalini huwa siendagi huko, wanaweza kukupiga sindani
wakakumaliza kabisa ukawa huzai kabisa, wajanja sana wazungu wanataka sisi
waafrika tusiwe na watoto wengi…’akasema na watu wakacheka.
‘Msicheke nyie hamjui tu…mimi
ni kichwa najua mengi, hayo madawa ya uzazi wa mipango, yote hiyo ni ujanja
wao, mara sindano za kinga, sijui madawa ya ….aaah, yote hayo ni mbinu zao za
kutaka kumaliza kizazi cha kiafrika, sasa mimi hawanipati ng’oooo,’akasema na
watu wakacheka.
‘Ndugu yetu kwa kauli zako
hizo inaonyesha jisni gani ulivyo nyuma ki-utalamu na elimu yako ina walakini,…inabidi
uende ukasome zaidi , ukaelemishwe vyema…fanya utafiti wewe bado mdogo,
jielimishe ndugu yetu….huoni watu wanakucheka, utajiri wako utakuwa hauna maana
kama huna elimu…’akaambiwa.
‘Ni kuambi ukweli, na huyo
mganga wako unayemuamini ni kwanini akuagize ng’ombe,…si unajua wewe ni tajiri
wa ng’ombe, kwani awe anaagiza nyama,
tena zilizonana, huoni kuwa ni mbinu yake ya kupata kitoweo…je huyo ng’ombe
akichinjwa nyama unarudi nazo..?’ akaulizwa
‘Hapana zinatolewa kafara…’akasema
kwa kujiamini
‘Kafara, kafara kafara…haya
wewe unalijua vyea hilo kafara, wazee
happ hapa watanisaidia nisije kukiuka utamaduni, ina maana hizo nyama
anapelekewa nani ili liwe kafara, ndi nataka kujua hapo au zinazikwa, au
zinapelekwa wapi?’ akaulizwa
‘Mimi sijui hiyo ni kazi
ya mganga aliyeniagiza….’akasema.
‘Hahaha, ndugu , kijana, umeliwa…’akasema
huyo mjumbe na watu wakacheka.
‘Jamani ndugu zanguni,
hatutaki kuzalilisha utamaduni wetu, tiba mbadala zipo, waganga wa kienyeji
wapo, kafara zipo na zinajulikana kuwa kama ni nyama zinapelekewa masiki
wasiojiweza, na nyingine tunagawana majirani hilo ndio kafara….’akasema
‘Lakini waganga wetu hawa,
wajanja, mafisadi, nia na malengo yao ni kuwahadaa wananchi, wanachotaka ni
kujali matumbo yao kwa udanganyifu wa ramli, hii inayoitwa ramli ni viini
macho, ujanja wa kukuhadaa wewe,kama wanaweza waniloge mimi, mimi siogopi
kwasababu hawawezi …’akasema
‘Hata kwenye vitabu
vitakatifu ramli ni haramu,…au nadanganya wataalmu wa dini, ramli ni haramu ,
ni haramu….huyo anayepiga ramli hamuamini mungu,maana mwenyezimungu kakataza
yeye anafanya, ni nani anayempinga mungu, ni rafiki wa shetani, na kama ni
rafiki wa shetani nay eye ni nani ….ni shetani, msiogope kusema waganga hao si
lolote, wezi wakubwa, hao wanapingana maandiko ….vijana, hata wazee hebu someni
dini zenu vyema someni elimu zote muijue duni ilivyo.
‘Pia hebu waangalieni maisha
ya hao wanaoitwa waganga, japokuwa siku hizi kuna ambao,wamekiuka miiko,
wanajijenga siku hizi, lakini swali ni hili, kama wao wanaweza kuleta utajiri,
watoto nk, mbona maisha ya ndio zaidi ya wewe unayekwenda kuomba msaada huo
‘Hahahaha,wengine hata
wake hawana, kama hana mke wewe unakuadanganya kuwa atakupa uzazi, kama yeye
anaweza kuleta utajiri kwanini wanadai muache pesa, muwalipe viingilio, mtoe
..mpaka wanatumia neno zuri ambalo hawastahili kulitumia, eti mtoe sadaka, sadaka
ni kitu kitakatifu hakistahiki kutumiwa na hawa watu, ….hebu jiulizeni hizo
pesa wanataka za nini kama wana uwezo wa kukupa wewe utajiri….msidanganyike,
chunguzeni kwanza…’akasema mjumbe.
‘Wanawadai pesa, wanawadai
eti sadaka, kwa vile wanajua kidogo kidogo, wewe umeika yula kaja, ikifika
jioni ana pesa,…ndio maana wengine wajanja sasa ni matajiri…kwa sababu ya
ujinga wenu…mimi hawanipati ng’oooo’ akasema mjumbe na watu wakacheka.
‘Sasa wewe uliyeamu
kuchukua sheria mikononi mwako una makosa, kwanza kusikiliza umbea, mwanaume
kama wewe hustahili,…unatuabisha, pili, kupiga, na kujeruhi, …halafu wewe
mwanaume unapigana na akina mama, kama una miguvu kajiunge na ngumi za kulipwa,
utatajirika, usipoteze nguvu zako bure kwa akina mama, hao akina mama,
hawatakiwi kutumia nguvu, eeh, au hujapitia jando wewe, kwakweli umetutia
aibu....’akaambiwa na wazee, na jamaa akainama chini.
‘Una makosa…kwahiyo
kama sheria za kimila zilivyo,
unastahiki kutoa faini, faini kwa mke wako, na faini kwa rafiki yako, kwanza umuombe
mke wako msamaha, pili unatakiwa umlipe ng’ombe mzima, na hilo pia ulianye kwa
rafiki yako,umuombe msamaha, na pia umlipe ngombe mzima…’akaambiwa
‘Nini, mimi niwaombe
msahamaha, nani mimi, labda sio mimi, eti nimpig make magoti nimuombe msamaha
wakati, wao ndio wana makosa, hapana wazee mimi hilo sikubali…’akatulia
alipoona wazee wanamkodolea macho.
‘Sisi kama wazee wako,
tumeliangalia hilo kwa makini tumelichunguza, na sio kwamba tunasema tu,tulishawahi
kusikia tetesi kama hizo, tukachunguza, kiukweli, hakuna kitu kama hicho,
umedanganywa, na kama ulitaka kupeleka
ng’ombe kwa huyo mganga, acha, utaliwa ng’ombe wako bure..huyo mganga ametafutwa
hajapatikana…kashakimbia kajua keshasababisha mapigano…’akaambiwa.
‘Sisi tunaona mbali,
tunatumia busara, hekima zetu zinaonyesha kuwa mkeo ana uja uzito wako,…unatakiwa
ufurahie, ndio maana unatakiwa upigia magoti, ili moyo wake ufurahi…’akaambiwa
akainua kichwa kuangalia upande ule aliokaa mke wake, kwa macho ya hasira.
‘Hivi mnanifanya mimi mtoto
mdogo au…?’ akauliza
‘Kwahiyo sisi tunaokuambia
haya ni watoto wadogo, hatuna akili, unatuzarau?’ akaulizwa
Baba yako hakuwa na
kufanya, akakubali shingo upande kwani wazee wa kimila wanaheshimiwa sana, na
hata hivyo akasema anasubiri mtoto akizaliwa kama ana sura ya huyo jamaa
atahakikisha anamletea huyo raiki yake kiwiliwili kisicho na kichwa na mke
atakuwa kiwete. Na rafiki yake akajibu;
`Na hata akizaliwa sura
kama yako, namchukua huyo mtoto kwangu, kwani hustahili kuwa na baba kama wewe
anayepinga uhalali wako, hivi utapata wapi mke kama huyo anayejiheshimu, na
kwanini mimi nitembee na mke wako, wakati mke wangu unamtambua kwa uzuri
wake...’akasema
‘Kama angekuwa mzuri
ungekuja kuzini na mke wangu….ipo siku nitakusana, na akizaliwa ushahidi
utabainika…’akasema
‘Kwa kauli yako sitaki
urafiki na mtu kama wewe, ole wako, ukanyage kwangu, na huyo mtoto akizaliwa sio
halali yako hata kama mnafanana naye, na kama atakusaidia, hatafanikiwa, maana
hustahili msaada wake, kwani umeshamkana…huyo ni mtoto wa mama,na hakuna mama
anayeweza kumkana mtoto wake, hakuna mzazi anayekana mtoto wake, wewe umemkana,
hata kabla hajazaliwa..…’ rafiki yake akasema.
`Tatizo lako unafikiri
mimi ninatania, we subiri uone, labda kama sio mimi…wewe unanionaje mimi, mimi siwezi
kulea mimba za watu, azaliwe mwanaharamu, utakuja kuchukua kinyago chako,
kikusaidie wewe…’ baba yako akasema na kuondoka hapo kwenye kikao.
NB: Mnaona eeh, weke akili
ni hapo
WAZO LA LEO: Chungeni sana kauli zenu, kauli
nyingine ni hatari zinaweza kusababisha maafa, na kauli nyingine huumba,..na
kwa wazazi msipende kuwaita watoto wenu majina mabaya,….majina hayo na matamshi
yenu yanaweza kuwaathiri watoto kisaikolojia, na watoto wakawa hivyo hivyo….tuwe
makini, maana ulezi ni ualimu, na elimu ya mtoto huanzia kwa wazazi wake.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment